Wanaume acheni kudhalilisha miili ya wanawake

Wanaume acheni kudhalilisha miili ya wanawake

I wonder kama wanawake mngekuwa na maumbile ya kiume, ndio tuseme dunia ingekuwa salama zaidi?

▪ Anyway sitetei ubakaji.

Najaribu kufikiria kama mtu mwenye maumbile ya tofauti anaweza kuwaza nje ya box, akajiweka kwenye position ya hao anaowaponda.

Sio unawaponda hao kwa kujifikiria wewe kwenye nafasi uliyopo, that's easy; kwasababu naamini kama nyege wote tunazo kwa kiwango sawa tu...

Sasa tofauti yetu inakuja wapi?!

Binafsi sijawahi kusikia mwanaune kabakwa na mwanamke, why.. sababu ya kimaumbile.
Maumbile yapi unayoyasema, mwanaume na mwanamke wana kichwa kimoja kilichojaa nywele, wana macho, masikio, pua, mdomo, shingo, kifua, matiti, tumbo, mbavu, mikono, kitovu, vikojoleo, makalio, miguu, unataka twende na viungo vya ndani!!?
Haya niambie tofauti yenu ya kimaumbile ni ipi hadi umshangae mwengine na kufikia hatua ya kumbaka au kumdhalilisha?
 
Kwa mwanamke mtu mzima hakuna mwanaume anaweza kukubaka kama wewe mwenyewe haujajiweka kwenye mazingira yanayoruhusu kubakwa. Kuna sheria nyingi zimewekwa kuwalinda wanawake, lakini ulinzi mnaopewa na jamii na sheria haimaanishi kwamba ndio mmpewa ruhusa ya kujipeleka kwenye hatari. Ukivaa nguo zisizo za heshima utabakwa tu. Ukijiweka kwenye mazingira yanayoruhusu kubakwa utabakwa tu
Nipo kanda ya ziwa huku kuna project nafanya matukio ya ubakaji wamama na watoto ni mengi na hawavai visketi vifupi wala manyonyo wazi, kwa hiyo shida ni mwanamke kuvaa kiguo kifupi ndio abakwe na yule mtoto nae kavaa nini hadi anabakwa?
Wanaume wenye mitazamo kama yako mlipaswa mkaishi maporini huko na mababu zenu manyani, hamfai kuishi kwenye jamii iliyostaarabika.
 
Serikali iingilie kati tu,
Unao watetea nao Tatizo wanapenda hayo mambo sana na wanatengeneza Mazingira wenyewe,

Pima pande zote kabla ya kukasilika then suggest solution.
Hakuna mwanamke anayetaka kubakwa au kudhalilishwa, shida ipo kwenu mnatakiwa mbadili mitazamo yenu, miili yote ni sawa, mwili wa mwanamke sio chombo cha starehe, mwanamke ana haki ya kua mwanamke na sio kuishi kwa hofu kuhofia usalama wake dhidi ya mwanaume, swali kwako mbona jamii za zamani watu waliishi uchi uchi na hawakubakana?
 
Ok kumbe, sasa tujiulize, kama licha ya maumbile yao kutokuwa wezeshi sana kama ya wanaume lakini bado wanabaka pia, hata kama kwa kiasi kidogo ..

Vipi kama nao wangekuwa na maumbile kama ya wanaume, naamini hali ingekuwa hii hii iliyopo sasa, wanaume ndio tungekuwa tunawalaani wanawake kwa ubakaji.
Mwanamke hata kama maumbile yake yangekua wezeshi bado asingembaka mwanaume, why? Mwanamke anajielewa na kujitambua amestaarabika pia,, hivi mbona wamasai wanavaa nusu uchi na hawabakani? kuna jamii moja niliiona sijui ni Wasandawe wanaitwa sina hakika sana wanawake wanatembea matiti wazi, wamejifunga vikaniki kiunoni tu, na walaaa hakuna anayeshtuka wala sikupata taarifa yoyote ya ubakaji, jitafakari na uchukue hatua
 
This is what we call internalized misogyny effects.

Somehow somewhere unaamini mwanamke akivaa vibaya inahalalisha kufanyiwa vitendo vya uzalilishaji, bado hamjafahamu tatizo ninini na tatizo linaanzia wapi, unadhani katika jamii wanazovaa stara hakuna ubakaji? Kama upo unauelezeaje?

Ukiachana na wanawake kuvaa hovyo, watoto wadogo wa kike na wakiume wanabakwa kwasababu zipi? Vikongwe je? wanabakwa kwanini na wanabakwa nani?

Naelewa unakotokea, sio mara moja mtu kureport kufanyiwa udhalilishaji, mwingine tena mwanamke anauliza kwani alivaaje 😏 Normalize kudeal na tatizo na sio kumlaumu victim. Wabakaji watatafuta justification za kubaka kila leo hata kama jamii nzima tutakuwa tunavaa majuba.
Amenisikitisha sana huyo binti,
Kama jamii tunapaswa kutoa elimu zaidi na kutilia mkazo kuhusu mipaka ya kimwili na heshima kwa mtoto wa kike, hii ukiiangalia ipo kwenye malezi zaidi, wote wakike na wakiume wanapaswa kupewa elimu ya kiwango cha juu ili kutokomeza hii mitazamo isiyofaa.
 
Mwanaume mwenye afya iliyokamilika, akiona maungo au kuwekewa ishara ya kuona maungo, mwili wake bila hiari hutuma taarifa kwenye ubongo na kiungo husika kusisimka.
Kwa hiyo, kuvaa nguo za kutaka kutuonyesha maungo yenu, ni kutaka kuwasisimua wanaume ili wawape 'credit'.
Kujiheshimu ni kuvaa nguo za heshima ili usimkwaze mwingine.​
Kama matukio ya ubakaji sababu ni nguo basi jamii za kimasai, kimang'ati, kisandawe, Asia, Ulaya na America wangekua wanabakana hovyo kama kuku, na vipi wale wanaobakwa wakiwa wamevaa magauni na masketi ya kuburuza?
mwanaume mwenye afya njema iliyokamilika na akili timamu unapataje wazo au nguvu ya kumbaka mwanamke au mtoto? wewe una tatizo na tatizo hilo sio dogo unapaswa ufungiwe jela tutokomeze kizazi kisichojielewa
 
Jaribu kujichunguza vizuri kwenye uumbaji utakuja kugundua mwanamke alivyoumbwa nikama chombo cha starehe.
Pia Inasikitisha sana kuhusianisha namna mnavyo vaa na ubakaji mwanamke vaa unavyo vaa ukiwa mzuri lazima utavutia tu wanaume hata ujifunike kila mahali.

Mimi nadhani ubakaji ni tatizo kubwa zaidi ya uliyoandika hapo maana unaweza kuta mtu anamwanamke mzuri tu lakini kafumwa analawiti mtoto wa kindagaten. Au mzee wa miaka 78 amebaka mtoto wa miaka 7 .Au unakuta mtu kabaka mtoto wa miezi 2
Sahihi kwa maana una amini ni tatizo la akili mtu alilokua nalo japo wachangiaji wengi wamekimbilia kwenye mavazi, mavazi, kwa hoja yako hii imehusisha watu ni wagonjwa na hawajijui kama ni wagonjwa, kuna mmoja kasema ana afya njema hivyo akiona titi atabaka, hii inadhihirisha kua mtu anakua mgonjwa wa akili lakini hajijui kama anaumwa
 
Wanawake ndo mmekosa maadili ndo maana mnaishia kubakwa na kufanyia mambo ya ajabu.

Mwanamke anayejiheshimu hata wanaume huona haya kumwendea.. Ni nyie ndo mmekosa tabia nzuri, mnavaa nguo za uxhi mnategemea kuleta picha gani kwa jamii?
Na watoto nao wamefanya yapi hadi wanabakwa?
 
Mwanamke hata kama maumbile yake yangekua wezeshi bado asingembaka mwanaume, why? Mwanamke anajielewa na kujitambua amestaarabika pia,, hivi mbona wamasai wanavaa nusu uchi na hawabakani? kuna jamii moja niliiona sijui ni Wasandawe wanaitwa sina hakika sana wanawake wanatembea matiti wazi, wamejifunga vikaniki kiunoni tu, na walaaa hakuna anayeshtuka wala sikupata taarifa yoyote ya ubakaji, jitafakari na uchukue hatua
Unazungumzia jambo la kufikirika lisilo na uhalisia, kusema wanawake wanajielewa ni sawa, but sio wote ndio maana mdau pale juu kanipa kesi ya Zimbabwe mdada alimbaka mtoto wa kiume, hii ni fact sio issue ya kusadikika kama unavyojibu hapa.

So, still i believe, sababu kuu ya ubakaji ni ya kibiolojia inayochangiwa zaidi na maumbile, sasa kama nyie hamna maumbile kama yetu huwezi kujibu hii issue kwa ufasaha, utajipendelea tu.
 
Guys, wallah leo nimechafukwa sana ukija hapa uje na akili timamu, nina kirungu changu ukileta uzwazwa nakubwenga cha utosi akili ikukae sawa,

Matukio ya ubakaji wanawake na watoto wa kike ni mengi hadi natetemeka lakini haya yote yanaletwa na wanaume wapumbavu wanaoangalia mwili wa mwanamke kama chombo cha starehe,

Hivi nyie wanaume miili ya wanawake ina tofauti gani na yenu? ile kujazia jazia hata nyie mmejazia, wembamba hata nyie kuna wembamba, manyonyo hata nyie kuna wenye nayo, nini shida jamani mbona mnatukosesha amani wanawake?

Mwanamke akivaa kiguo chake kifupi atembee kwa raha zake inakua gumzo lakini mwanaume akivaa kiguo kifupi husikii kabakwa au kadhalilishwa, miili mbona ni ile ile tu,

Mbona watu wa zamani walikua wanaishi uchi na hakukua na matukio ya ubakaji wala udhalilishwaji, hiki nini mnafanya nahisi hadi kichefu chefu,

Ifike mahala sasa tutaichukua heshima yetu kwa nguvu, haiwezekani kila siku nyinyi tu, kuna wengine humu humu hizo tabia chafu mnazo, unajisikiaje kushika titi la mwanamke bila ridhaa yake au kushika tako la mwanamke ambaye huna mahusiano nae?,

Hakuna mwili unaohalalisha ubakaji,
Hakuna vazi linalohalalisha ubakaji,
Hakuna tabia inayompa mtu haki ya kuvuka mipaka ya mwingine,

Tujenge jamii inayohehimu wanawake bila kufanya miili yao kua sababu ya lawama au udhalilishaji,

Nikisema hii gender ifutwe naitwa feminist.
Are you married?
 
Watoto wadogo wanakuwa wamekula vya nani?

Nataka ufikirie ubakaji ina bigger picture.
Na wewe fikiria dysfunction kwa bigger picture... Inaanzia kwenu wanawake... Msio na heshima kwa waume zenu...

Unampa trauma mwanaume anaenda kubaka mtoto mdogo.

Yaani nyie huwa hamjui ya kuwa nyie ndo nurturing gender?

Umeshawahi kusikia msemo unasema mwanamke akisoma jamii imesoma? Mzizi wa fitna na mbomoko unaanza kwenu nyie wanawake wabishi wabishi mlio tumia elimu zenu kuuza ego uchwara..

Nyie ndo mnaosababisha jamii iteseke.
 
Nimetumia kizaramo hapo, enzi hizo watoto ndio tulikua tunasema kukubwenga,😆😆

Umeelezea kitu kikubwa sana, malezi malezi malezi, kuna jamii haimfunzi mtoto wa kiume kuheshimu mtoto wa kike na inaanzia kwa dada zake anakua nayo hadi huku nje
Anayepaswa kumfunza mtoto wa kiume namna ya kum treat mwanamke ni jukumu la nani? Na ni nani anaye kuwa na mtoto katika developmental years?
 
Kuna tatizo gani mtu kuvaa anavyojisikia yeye kuvaa? yaani yeye akivaa sketi fupi wewe unapungukiwa na nini kama sio tatizo la akili ulilonalo
Sasa kama wewe ni daktari professional yako haikufundishi kuhusu animalistic instincts? Kuna mmoja kule juu alisema tume gundua mavazi ili usiwe kama wanyama, ambao wanakimbiana kufanya mapenzi bila hiyana,

Sasa wewe na udaktari wako hata akili ya kujiongeza huna kweli Kujua ya kuwa mwanaume akiona huo upaja ana dindisha?
 
This is what we call internalized misogyny effects.

Somehow somewhere unaamini mwanamke akivaa vibaya inahalalisha kufanyiwa vitendo vya uzalilishaji, bado hamjafahamu tatizo ninini na tatizo linaanzia wapi, unadhani katika jamii wanazovaa stara hakuna ubakaji? Kama upo unauelezeaje?

Ukiachana na wanawake kuvaa hovyo, watoto wadogo wa kike na wakiume wanabakwa kwasababu zipi? Vikongwe je? wanabakwa kwanini na wanabakwa nani?

Naelewa unakotokea, sio mara moja mtu kureport kufanyiwa udhalilishaji, mwingine tena mwanamke anauliza kwani alivaaje 😏 Normalize kudeal na tatizo na sio kumlaumu victim. Wabakaji watatafuta justification za kubaka kila leo hata kama jamii nzima tutakuwa tunavaa majuba.
Sometime muwe mnaacha kutumia psychology kwenye human animalistic instincts... Hamuoni waarabu walivyo na misingi ya uvaaji na namna maisha yao yame nyooka... Angalia walivyo successful hata nchini tu hapa.

Sio kila kitu mnachofunzwa kwa logic kina apply kwenye kila angle..

Utakuwa ni mtu usiye na reasoning kuja kuanza kusema eti, mwanaume anatafuta justification umemvalia nusu uchi.

We are controlled much by our environmental sio free will kama formal education unavyosema.. Ndo maana hata maofisini kuna dressing codes kuondoa distractions and temptations.

Msiwe mnabisha mambo without reasoning
 
Sometime muwe mnaacha kutumia psychology kwenye human animalistic instincts... Hamuoni waarabu walivyo na misingi ya uvaaji na namna maisha yao yame nyooka... Angalia walivyo successful hata nchini tu hapa.

Sio kila kitu mnachofunzwa kwa logic kina apply kwenye kila angle..

Utakuwa ni mtu usiye na reasoning kuja kuanza kusema eti, mwanaume anatafuta justification umemvalia nusu uchi.

We are controlled much by our environmental sio free will kama formal education unavyosema.. Ndo maana hata maofisini kuna dressing codes kuondoa distractions and temptations.

Msiwe mnabisha mambo without reasoning
Upo sahii kwa maelezo yako.,what about wanaobaka wanyama??..Kuna watu wakiona mbuzi tu gari linawaka,tatizo inakua nini pale?tako la mbuzi,upaja au manyonyo??..
 
Back
Top Bottom