Hahhahah sasa wewe mie mkali wa hizi kazi tokea nipo chuo kitamboo nimeivuruga sana hiyo Kariakoo hahah hadi leo nipo yaani na sibanduki ng'ooo inabidi tuwasaidie wenzetu bana maana haya maisha mtu akikuongezea jero kwenye product ni kubwa sanaaaa.Na hivi vyuma vimekaza acha tu na wenyewe wale. Ila si unajua mjini wasioujua bado wengi utawapata tu maana hawapo humu JF.


Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000, 8000, 12000 lipo maeneo ya Nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee Msimbazi Kota, karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa Congo na Aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka Aongo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k, 25k, 28k, 30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo Mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro. Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh, pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau? Danhappy
Mkuu tuwasiliane nimejaribu kuku pm imegoma.
 
Original crocs bei Elfu 25,000 tuu
Tupo Kariakoo
Mtaa ; Makutano ya Kongo na Aggrei
Jengo la Capetown Underground
Frem/Duka namba 5

IMG-20221120-WA0016.jpg
IMG_20221201_095100_573.jpg
IMG-20221130-WA0023.jpg
IMG-20221130-WA0018.jpg
IMG20220921130119.jpg
IMG_20220902_131118.jpg
750ca3d7dc9ca852db125d92e469433a.jpg
1515948838_00.g_800-w-st-pj_g.jpg
mmexport1654534562519.jpg
 
Habari wakuu. Natafuta nguo za shule hasa shati za tomato, sweta na viatu. Msaada wa chimbo jamani, asante
 
Hahahah nitakupa mtu akusindikize maana kwa nature ya job yangu sitoki nje weekdays na weekdays shop nyingi ndo zinakua wazi jmos nusu siku possibilty ya kufanikiwa inakua kidogo na jumapili ndo kabsaa.
Mkuu habari Naona pm yako umefunga nipo mkoani nilikuwa naomba mawasiliano ya hayo machimbo wanayouza vitenge,pochi na sandles kama hutojali unaweza nitumia inbox .

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Jaman nataka kufanya biashara ya hardware mini shop ila chimbo la vitu bei poa sijui kwa kariakoo au popote pale ndani ya dar mfano bomba za ips ,fittings,na machepe nyundo sululu na vingine msaada jamn
 
Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah!
Hi na maduka ya vifaa vya watoto kwa Bei ya jumla ni mitaa gan?
 
Back
Top Bottom