Wafanyabiashara takribani 90% wana maisha magumu. Kijana usidanganyike na mafanikio ya wachache, Business is not for everyone!

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,455
Hii ni tahadhari kwa vijana kuhusu uhalisia wa biashara, si kuwakatisha tamaa wala kuwaambia waajiriwe. Biashara ni njia nzuri, imetajirisha watu lakini si hadithi ya kupendeza kama inavyochorwa mitandaoni. Biashara ni vita, inahitaji akili, mikakati madhubuti, uwezo wa kujifunza kila siku, uvumilivu wa hali ya juu na nidhamu isiyotetereka.

Wakati kijana anapofikiria kuingia kwenye biashara, mara nyingi picha anayojenga akilini ni hii:
  • Kwenda ofisini siku yoyote apendayo, muda anaoamua mwenyewe
  • Kuwa bosi / ceo wa biashara yake.
  • Kusafiri kwenda vacations
  • Kuendesha gari la kifahari
  • Kuishi kwenye nyumba nzuri ya ndoto

Lakini kwa uhalisia wa Tanzania, Wafanyabiashara wanaoishi maisha hayo ni asilimia ndogo mno na hata ndani ya aina za biashara wanazofanya, wao ni kundi dogo (cartel)

Wafanyabiashara wakubwa katika maeneo mengi ni walafi wa kiwango cha juu, Hawatosheki kamwe ! kila siku ni mipango ya kuzoa wateja wengi hata wa yule mdogo asiye na uwezo wa kujitetea iwe rushwa, ushawishi wa connections, discounts, n.k. Kwao, mfanyabiashara mdogo anaewakaribia ni adui wa lazima kuangamizwa mapema lasivyo anaweza kuwaibia wateja wao. Kwa nchi zilizoendelea wafanyabiashara wakubwa wamedhibitiwa kucheza rafu kwa pesa na connections walizonazo.

Takribani 90% ya wafanyabiashara kwa kipindi cha miaka 20 wamepitia au wanapitia changamoto hizi:
  • Kuishi na msongo wa mawazo kutokana na madeni yasiyokwisha
  • Kuamka kila siku alfajiri na kurudi usiku.
  • Kufilisika na kufunga biashara
  • kuambulia patupu siku nzima
  • Kukimbizana na kodi na tozo zisizotabirika wala zenye miongozo ya kueleweka
  • Kukosa uhakika wa mapato, faida au hata wateja wa kudumu
  • Kukosa muda wa kupumzika, maisha ya familia au kujitunza kiafya
  • Kwenda kwa waganga mambo yakiwa magumu (mtashangaa lakini ndio wateja wakubwa)
Maisha ya wafanyabiashara wengi ni one man army, yeye atahusika na kila kitu.
  • Sheria
  • Masoko
  • Mikopo
  • Uendeshaji
  • Teknolojia
  • Mauzo
  • Uhasibu
  • Ubora nk
 
Huu uzi mzuri sana. Ni kweli wafanyabiashara wengi ni kama wanazifanyia kazi taasisi za mikopo, TRA, serikali za mitaa na taasisi zingine za tozo. Wengine naweza sema huwafanyia kazi wafanyakazi wao. Yaani wafanyakazi wanakula maisha kuliko mmiliki wa biashara. Biashara ina mambo mengi sana. Wazazi badala ya kuwapeleka watoto shule za mamilioni ni bora muwapeleke shule za bei nafuu au hata Kayumba ili polepole muwekeze kwenye biashara na assets ili watoto waje kuendeleza biashara ambayo tayari ina mizizi. Mzee LIKUD anaweza elezea zaidi.
 
Wakati kijana anapofikiria kuingia kwenye biashara, mara nyingi picha anayojenga akilini ni hii:
  • Kwenda ofisini siku yoyote apendayo, muda anaoamua mwenyewe
  • Kuwa bosi / ceo wa biashara yake.
  • Kusafiri kwenda vacations
  • Kuendesha gari la kifahari
  • Kuishi kwenye nyumba nzuri ya ndoto

Lakini kwa uhalisia wa Tanzania, hiyo ni hali ya wachache sana.
Wafanyabiashara wanaoishi maisha hayo ni asilimia ndogo mno na hata ndani ya sekta wanazofanya, wao ni kundi dogo lililofanikiwa kukamata sehemu kubwa ya soko, huku wengi wengine wakibaki wakigawana mabaki yanayobaki sokoni.

Takribani 90% ya wafanyabiashara kwa kipindi cha miaka 20 wamepitia au wanapitia changamoto hizi:
  • Kuishi na msongo wa mawazo kutokana na madeni yasiyokwisha
  • Kuamka kila siku alfajiri na kurudi usiku.
  • Kufilisika na kufunga biashara mara kwa mara
  • Kukimbizana na kodi na tozo zisizotabirika wala zenye miongozo ya kueleweka
  • Kukosa uhakika wa mapato, faida au hata wateja wa kudumu
  • Kukosa muda wa kupumzika, maisha ya familia au kujitunza kiafya
  • Kwenda kwa waganga mambo yakiwa magumu (mtashangaa lakini ndio wateja wakubwa)
Biashara si ndoto tamu kama inavyopakwa sukari mitandaoni. Ni vita ya akili, mikakati, kujifunza, uvumilivu, na nidhamu kali.
ambayo hawafanyi biashara wanamaisha marahisi?
 
Wakati kijana anapofikiria kuingia kwenye biashara, mara nyingi picha anayojenga akilini ni hii:
  • Kwenda ofisini siku yoyote apendayo, muda anaoamua mwenyewe
  • Kuwa bosi / ceo wa biashara yake.
  • Kusafiri kwenda vacations
  • Kuendesha gari la kifahari
  • Kuishi kwenye nyumba nzuri ya ndoto

Lakini kwa uhalisia wa Tanzania, hiyo ni hali ya wachache sana.
Wafanyabiashara wanaoishi maisha hayo ni asilimia ndogo mno na hata ndani ya sekta wanazofanya, wao ni kundi dogo lililofanikiwa kukamata sehemu kubwa ya soko, huku wengi wengine wakibaki wakigawana mabaki yanayobaki sokoni.

Takribani 90% ya wafanyabiashara kwa kipindi cha miaka 20 wamepitia au wanapitia changamoto hizi:
  • Kuishi na msongo wa mawazo kutokana na madeni yasiyokwisha
  • Kuamka kila siku alfajiri na kurudi usiku.
  • Kufilisika na kufunga biashara mara kwa mara
  • Kukimbizana na kodi na tozo zisizotabirika wala zenye miongozo ya kueleweka
  • Kukosa uhakika wa mapato, faida au hata wateja wa kudumu
  • Kukosa muda wa kupumzika, maisha ya familia au kujitunza kiafya
  • Kwenda kwa waganga mambo yakiwa magumu (mtashangaa lakini ndio wateja wakubwa)
Maisha ya wafanyabiashara wengi ni one man army, yeye atahusika na kila kitu.
  • Sheria
  • Masoko
  • Mikopo
  • Uendeshaji
  • Teknolojia
  • Mauzo
  • Uhasibu
  • Ubora nk
Biashara si ndoto tamu kama inavyopakwa sukari mitandaoni. Ni vita ya akili, mikakati, kujifunza, uvumilivu, na nidhamu kali.
Wafanya biashara ndio wenye maisha mazuri ndio wenye magari mengi ndio wanao endesha mzunguko wa hela Tanzania. Ndio walio jenga majengo mazuri tena mapema. Ndio wanaolipa kodi za mishahara yote wanayolipwa wafanyakazi. Ndio wenye ndoa zilizo tulia. Ndio wenye mali nyingi. Ndio wenye pesa nyingi bank. Bila wafanya biashara sijui tungekuwaje. Tusingekua na maendeleo. Na mara nyingi maeneo mengi yenye wafanyakazi wengi huwa yanakua hayana maendeleo.

Mfanyakazi:
1. When you increase speed of working at your employment, money remains constant.

2. When you increase time of working at your employment, money remains constant.

3. When you increase intelligence in working at your employment, money remains constant.

4. When you increase energy of working at your employment, money remains constant.

Mfanyabiashara:

1. When you increase speed of working at your business, money increases.

2. When you increase time of working at your business, money increases.

3. When you increase intelligence in working at your business, money increases.

4. When you increase energy of working at your business, money increases.
 
Kwa kifupi,biashara isikie tu Kwa mwenzio !!! Hali ni mbaya asikwambie mtu!!! Watu wakiacha kazi serikalini wakaenda kwenye biashara wanajuta !!!huwezi amini!!!.
Imagine mtu aliacha kazi Sasa wanalia!! Wanasiasa wameharibu baadhi ya biashara Hasa za usafirishaji
 
Wafanya biashara ndio wenye maisha mazuri ndio wenye magari mengi ndio wanao endesha mzunguko wa hela Tanzania. Ndio wanaolipa kodi za mishahara yote wanayolipwa wafanyakazi. Ndio wenye ndoa zilizo tulia. Ndio wenye mali nyingi. Ndio wenye pesa nyingi bank.
Imeisha iyo
 
Wafanya biashara ndio wenye maisha mazuri ndio wenye magari mengi ndio wanao endesha mzunguko wa hela Tanzania. Ndio wanaolipa kodi za mishahara yote wanayolipwa wafanyakazi. Ndio wenye ndoa zilizo tulia. Ndio wenye mali nyingi. Ndio wenye pesa nyingi bank. Bila wafanya biashara sijui tungekuwaje. Tusingekua na maendeleo. Na mara nyingi maeneo mengi yenye wafanyakazi wengi huwa yanakua hayana maendeleo.
Hao ndio wahache waliobaki wenye maisha mazuri na ndio hutazamwa zaidi, hawana huruma na hawatosheki, hutafuta mbinu kila siku kupata wateja wengi iwezekanavyo hadi wale wa wenzao wenye mitaji midogo.
 
Imeisha iyo
Pole Sana !!! Mfanyakazi ndio Wana maisha braza!!! Haza kwenye taasisi Fulani Fulani!! Fikiria mtu analipwa labda million nane8,000,000 Kila tar 25 ya mwezi hata akiamua kuto.........m....Bea yote nyingine itakuja next month!! Sasa mfanyabiashara atumie faida hovyo aone! .
Pia watumishi Sasa ndio wamehamia kwenye biashara Hasa za mabasi na magest!! .watu walikuwa serikalini wakaacha kazi Sasa wanalia
 
Back
Top Bottom