Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Polisi Nyamongo wameshambulia msafara wetu kwa mabomu ya machozi wakizuia njia kuelekea kwenye mkutano wetu wa kampeni

JIWE hapo kakakaa anachekelea, yeey hata vumbi haruhusiwi kupigwa, okay kama MUNGU yupo kweli na naamini yupo ATENDE MUUJIZA AMPENDE ZAIDI HUYU ANAYEFANYA HAYA, ampende tu zaidi.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya ametoa ufafanuzi juu ya msafara wa mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Antiphas Lissu kusambaratishwa na polisi eneo la Nyamongo akiwa njiani kuelekea Serengeti
 

Attachments

  • TAARIFA YA JESHI LA POLISI TARIMERORYA KWA VYOMBO VYA HABARI 28 SEPT 2020.pdf
    169.8 KB · Views: 9
Mabomu ya machozi ni silaha kama zilivyo silaha nyingine, kuyaelekeza kwa wananchi wasio na hatia kunaudhi na kuumiza sio tu walengwa bali moshi unasambaa na kuwafikia hata wasiohusika.

Bei ya bomu moja la machozi linagharimu pesa ngapi za walipakodi? Ni lazima yawepo kama nchi, lakini ulazima wa kuyaelekeza kwa walipakodi walioyanunua ni vema utizamwe mara mbilimbili.

Mtu aliyetupiwa moshi wa mabomu haya hawezi kusahau kamwe kwenye maisha yake yote.
 
Kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji!

Wametoka kusifiwa juzi tu Hapa kwa kusimamia usalama wa raia na mali zao vizuri tangu kipindi cha Campaign kianze Eti baada ya siku 2-3 tangu wasifiwe wanaanza kupiga mabomu?!
 
Hao pilisi wana roho ya shetani, hata akilala na njaa, asubuhi akiamka anafikia kupiga saruti, hawezi kudai haki yake ya kupatiwa chakula
Nadhani wanarogwa kabla ya kuajiriwa hivi unapata wapi ujasiri wa kutetea mtu aliyekunyima nyongeza za mishahara na kukuletea kikotoo, huku ukistaafu unakosa mafao yako.
 
Ocd Ni kilaza Sana ajui hata sheria za uchaguzi zinasemaje, ilitakiwa Kama ana malalamiko ayapeleke tume
 
Polisi wengi ni weupe Sana kwenye Sheria utumia nguvu zaidi ukiwazidi hoja ukiambiwa usinifundishe kazi, takuweka lockup, chek mfano ishu ya nyamongo unapiga mabomu na mkutano unafanyika nini hii Sasa.
Tuliwaambia polisi mnawajengea watu tabia mbaya za kuzoea kukamatwa kupigwa mabomu watu sio wanyama nyie mpo wachache watu wakiamua hamtoweza wadhibiti.
 
IGP RPC OCD wote wanaoshiriki vitendo vya kuwaonea wapinzani kuhatarisha Amani watambue kuwa mara baada ya uchaguzi watafikishwa ICC The Hague kujibu tuhuma zao
Hilo liko wazi mkuu na wanajua....Umemsahau mkurugenzi wa tume yeye ndo kawa wa kwanza kujiwekea ushahidi wa wazi wa kupelekwa the Hague maana kasema wameamua chadema wapigwe mabomu
 
Back
Top Bottom