Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Polisi Nyamongo wameshambulia msafara wetu kwa mabomu ya machozi wakizuia njia kuelekea kwenye mkutano wetu wa kampeni

Mbepo yamba

JF-Expert Member
Aug 5, 2012
751
1,000
Kupitia akaunti ya Twitter ya Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu ameandika

Polisi Nyamongo wameshambulia msafara wetu kwa mabomu ya machozi wakizuia njia kuelekea kwenye mkutano wetu wa kampeni. Wamepiga na kuumiza wananchi waliotupokea. Nawaambia Jeshi la Polisi mfanye kazi yenu kwa weledi, hakuna mabomu wala risasi za kutuzuia!! Hatutishwi!

For English Audience
Our convoy has been subjected to a massive teargas attack by the Police in Nyamongo, in attempt to block our route heading to our campaign meeting. Our supporters have equally been brutally caned and hurt. Let them bomb us and shoot us, but we shall never back down!!


Lissu.JPGTARIME: POLISI WAKANUSHA KUSHAMBULIA MSAFARA WA LISSU BALI WALIKUWA WAKIWADHIBITI WALIOKUWA WAKIWARUSHIA MAWE ASKARI

Kamanda wa Polisi, ACP William Mkonda amesema msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA haujashambuliwa

Amesema wao wamewapiga mabomu ya machozi watu waliokuwa wanawarushia mawe Askari wa Jeshi la Polisi na hadi sasa Msafara wa Tundu Lissu upo njiani kuelekea Serengeti na unaongozwa na Polisi

Kuhusu usalama wa Mgombea amesema kuwa tangu jana Mgombea huyo alipofika Tarime amekuwa salama na anaondoka salama

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Tarime Rorya, William Mkonda amesema wamelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao walikuwa wakishambulia Askari Polisi kwa mawe baada ya kukatazwa kufanya mkutano katika eneo ambalo halipo kwenye ratiba ya Chama hicho kwa leo.

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom