Tarime: Polisi watumia mabomu ya machozi kutawanya wananchi waliotaka kumshushia kipigo ajuza

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime-Rorya limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wakitaka kumshushia kipigo ajuza ambaye jina lake halijafahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 60, wakimtuhumu kuhusika na kupotea kwa watoto watatu kwa njia za kishirikina.

Tukio hilo limetokea wakati Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Chikoka akiwa kwenye mkutano na wananchi hao, wakijadili tukio la watoto hao ambao wamefanyiwa ukatili ikiwamo kupigwa, kuchomwa moto na kufungiwa ndani kwa muda usiojulikana, ndipo mwanamke huyo aliposikika akiongea na wachawi wenzake juu ya watoto hao, kwa lugha ya kijaluo.

Chanzo: ITV

===============

Bibi awachoma moto watoto wa mwanamke aliyemuoa

Watoto watatu wa familia moja wilayani Rorya mkoani Mara, wamelazwa katika hospital ya wilaya ya Shirati wakipatiwa matibabu kwenye majeraha mbalimbali ya moto waliyochomwa na mwanamke anayedaiwa kuwa ni bibi yao aitwaye Eliza Odira (68).

Taarifa zimeeleza kuwa bibi huyo amemuoa kimila mama wa watoto hao (Nyumba ntobhu)ili amzalie watoto na kwamba chanzo cha ukatili huo bado hakijajulikana na bibi huyo yupo kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.

Akizungumza baada ya kutembelea watoto hao, Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka, amesema kuwa bibi huyo anadaiwa kuwafanyia watoto hao vitendo vya kikatili kwa muda mrefu na kwamba baada ya taarifa hizo kupatikana polisi walifika nyumbani kwake na kuwakuta watoto hao wakiwa katika hali mbaya na kulazimika kuwawahisha hospitalini huku bibi huyo akipelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano.


=========

DC: Wananchi walitaka niwakabidhi mtuhumiwa wamuue


Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka amefafanua kilichotokea akisema "Kuna mama wa miaka 68 aliwaficha hao watoto, akiwanyanyasa na kuwafanyia ukatili wa kiwango cha juu sana, alifikia hatua akawa anawachoma, ndio maana wakawa na hasira.

"Wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikina, walikuwa wakiniambia wanataka niwakabidhi huyo mtuhumiwa wamuue, lakini tayari tumeshamkamata na sheria itaenda kuchukua mkondo wake.

"Kweli Mkuu wa Wilaya naweza kutoa mtu akauliwe, hasira za tukio lao zilienda mbele zaidi na baadhi ya Wananchi wakaanza kushambulia wanawake wengine wenye umri mkubwa waliokuwa eneo la tukio.

"Kwa kuwa Wananchi walikuwa wengi ikabidi nguvu itumike kuwadhibiti, baadaye nikazungumza nao wakiwa wametulia.

"Watoto wapo hospitali wanaendelea na matibabu napo hospitali.

"Huku nilikuta wana mila potofu, mfano wanamke akiwa na uwezo na kifedha na hana uwezo wa kupata matoto, anamtolea mahari binti mdogo, anamlea kisha akipata watoto wanakuwa wa huyo bibi ambaye hajazaa.

"Ndivyo ilivyokuwa, huyo bibi alimtolea mahari ya ng’ombe wawili akawa anawamiliki hao watoto.
Hiyo mila huku wanaita ‘Nyumba ntobhu’, kibaya zaidi mama mzazi wa watoto yupo na tulipomuuliza ulienda lini kuwaona watoto, hakuwa na jibu."
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime-Rorya limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliokuwa wakitaka kumshushia kipigo, Ajuza ambaye jina lake halijafahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 60, wakimtuhumu kuhusika na kupotea kwa watoto watatu kwa njia za kishirikina.

Tukio hilo limetokea wakati Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Chikoka akiwa kwenye mkutano na wananchi hao, wakijadili tukio la watoto hao ambao wamefanyiwa ukatili ikiwamo kupigwa, kuchomwa moto na kufungiwa ndani kwa muda usiojulikana, ndipo mwanamke huyo aliposikika akiongea na wachawi wenzake juu ya watoto hao, kwa lugha ya kijaluo.

Chanzo: ITV

IMG_9819.png
 
02 February 2023
Shirati, Rorya

Juma Chikoka DC wa Rorya awatuliza wananchi




DC Chikoka awatuliza wananchi waliotaka kumpiga mama aliyeoa kimila nyumba "tobo" kisha kuwafungia na kuwanyanyasa watoto wa "mke" wake.

Watoto hao wana alama za kupigwa, zafungwa kamba, kunyimwa chakula pia kuchomwa moto na DC Chikoka anasema mateso hayo yanaonesha ni ya muda mrefu.

Watoto hao sasa wapo chini ya uangalizi wa vyombo husika vya serikali.
 
Huu upuuzi wa kupiga na kuua wazee bongo utaisha lini??? nchi imejaa wapumbavu wengi ndio maana rahisi sana kuongoza Tz. Yaani rais aliekua makamu linasimama mbele za wananchi linasema kuna pesa ziliibwa na zingine zikawekwa bank China.Sasa wananchi wafanye nini>??? Mwenyewe si ndio kiongozi mkuu chukua hatua.
 
Back
Top Bottom