Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,445
- 7,816
Naibu Spika akiongea katika hafla ya kuwaapisha mawaziri, manaibu na viongozi wengine, amewapongeza wote walioteuliwa na kuwashauri wameteuliwa kufanya kazi za Rais nao wao wanamsaidia hivyo wazifanye kama wasaidizi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano na si vinginevyo. Kuhusu Bunge, amesema kuna watu wanahisi kazi ya Bunge kila wakati ni kukosoa pekee. Amesema uko wakati Bunge linaishauri Serikali, kuna wakati linatunga sheria pia uko wakati Bunge linaisimamia Serikali.
Tulia amesema katika kipindi cha awamu ya sita imekuwa ikiwasikiliza ushauri wa wabunge na imekuwa ikizifanyia kazi.
Kwa muktadha huo, Tulia amesema Bunge liko tayari kushirikiana na awamu ya sita kwa mambo yote ambayo itayaleta bungeni ili wasimamie Serikali.
Naibu Spika amesema pale ambapo wanahitaji kukosoa Serikali wataikosoa kwa heshma na kwa muktadha ambao katiba inaruhusu kufanya hivyo, kwenye kushauri watashauri na si lazima Serikali kufata ushauri wa Bunge lakini katiba imetoa nafasi ya Bunge kuisimamia Serikali na kupata fursa ya kuiuliza Serikali walifanyia ushauri gani.
''Mihimili yote ina kazi zake na hapo mheshimiwa Rais nisisitize jambo moja maana kunakuwa na upotoshaji, Rais ni mkuu wa nchi, wapo watu wanachukua hiyo sehemu inayosema Rais ni kiongozi wa Serikali lakini Rais ana mambo yote, ni mkuu wa nchi, ni kiongozi wa Serikali, ni amiri Jeshi mkuu wa nchi hii.
Naamini kwa ufafanuzi huu watu watafahamu kwamba Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan sio tu kiongozi wa Serikali lakini ni mkuu wa nchi kwa hiyo yeye uongozi wake hauko sawasawa yeyote wa mhimili wowote ulioko hapa nchini"
Alisema Naibu spika, Tulia Ackson