Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa IPU kwa kishindo, apata kura 172 kati ya 303

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,715
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameshinda Urais wa umoja wa mabunge duniani(IPU) leo Octoba 27, 2023. Kura 303 zilipigwa huku mshindi akihitaji angalau nusu ya kura hizo(kura 152)

Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
Ms. Adji Diarra Mergane Kanouté(Senegal) kura 52
Ms. Catherine Gotani Hara(Malawi) kura 61
Ms. Marwa Abdibashir Hagi(Somalia) kura 11
Ms. Tulia Ackson(United Republic of Tanzania) kura 172

Dkt. Tulia Ackson anachukua nafasi Duarte Pacheco kutoka Portugal aliyechaguliwa mwaka 2020 baada ya kufanyika uchaguzi wa kwanza kupitia mtandao kutokana na janga la COVID-19 lililokuwa linaikabili dunia.

Kwa miaka 25 sasa urais wa IPU umetawaliwa na wabunge kutoka Misri, Hispania, India, Italia, Namibia, Morocco, Bangaladesh, Mexico na Portugal.

Dr. Tulia Ackson anakuwa Rais wa 31 wa IPU na amechaguliwa kwenye bunge la 147 la IPU lililofanyika mjini Luanda, Angola kutoka Oktoba 23 mpaka Oktoba 27.

Rais wa IPU ni kiongozi wa kisiasa wa taasisi hiyo, anaongoza vikao vyote vya taasisi hiyo na anaiwakilisha kwenye matukio ya kimataifa. Rais wa IPU anaongoza muhula wa miaka mitatu. Rais lazima awe mbunge kipindi chake chote cha miaka mitatu ya Urais.

IPU ilianzishwa mwaka 1889 kama kundi dogo la mabunge na kukua kwa kasi kama taasisi ya kimataifa ikijishughulisha na kukuza demokrasia, usawa, haki za kibinadamu, maendeleo na amani.

IPU ina wanachama 180 kati ya nchi 193 zilizopo duniani. Mabunge yote yaliyoanzishwa kisheria na nchi zao au mataifa yanayotambulika na umoja wa mataifa yanarusiwa kuwa mwanachama wa IPU.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, akiwasili katika Ukumbi wa Bunge la Angola leo tarehe 27 Oktoba, 2023 wakati wa Mkutano wa 147 unaoendelea Jijini Luanda, Angola.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 Jijini Luanda nchini Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa Umoja huo.
Ni Tulia Ackson Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Tanzania ambaye ni Mgombea wa IPU akiomba kura.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mungu ni mwema, asanteeee sana kwa maombi yenu watanzania wenzangu kwa dada yetu na speaker wetu Dkt. Tulia Ackson.

Habari njema ni kuwa tayari ameibuka kidedea na yupo kuzungumza, ngoja nimsikilize nakuja kuandika zaidi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Kila la heri, uzalendo kwanza!
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mungu ni mwema, asanteeee sana kwa maombi yenu watanzania wenzangu kwa dada yetu na speaker wetu Dkt. Tulia Ackson.

Habari njema ni kuwa tayari ameibuka kidedea na yupo kuzungumza, ngoja nimsikilize nakuja kuandika zaidi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Bro utafika umechoka sana. Hivi hata hiyo IPU unaijua kweli?
…..….you have one of the most difficult jobs in our republic.
 
Duh.. nimepita kwenye website yao.. si kitoto.. good for her and for the coutry
 
Back
Top Bottom