Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 876
- 4,101
Tanzania kwa miaka kama saba hivi spika na Jaji Mkuu ni sehemu ya msafara wa Rais. Kila anapokuwa Rais lazima spika awepo pembeni na Jaji Mkuu. Utatu huu mtakatifu unawezaje kutekeleza dhana ya separation of power?
Ukimsikiliza Spika na Jaji Mkuu wakiwa wanaongea ni kama wapo sehemu ya serikali. Yaani wao wanaongea kama vile ndio wakuu wa Muhimili wa serikali. Wanajadili sana performance ya serikali kuliko Mahakama na Bunge. Hakuna Sehemu mbele ya Rais wanaoshauri bali wanapongeza.
Huu mfumo unatumiwa na nchi gani Duniani ya kidemokrasia au kidikteta? Je, kuna sheria inalazimishwa wakuu wa Mihimili kuambatana kila wakati? Wao wanafanya kazi zao za kibunge na mahakama wakati gani kama ratiba yao ipo subject kubadilika kuendana na ratiba ya president?
Wanapokuwepo kwenye mikutano na vikao vya mhe Rais huwa wanaongeza tija gani? Hawaoni kama wanamzuia Rais kuwakosoa kwa kuwaonea aibu? Uhuru wa Mihimili upo kweli nchini?