Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 12,132
- 20,295
Ikiwa wakiteuliwa wanaachwa wapumzike tu then wanarudishwa tena.
Wakichoka wanapumzishwa uchovu ikiisha wanarudishwa tena. Je, sisi Chawa wa Mama ma Chawa wa Chama ni lini tutaingiamo? Au nafasi hizi ni za kwao tu?
Sitasema mengi oneni mwenyewe.
==========
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amewatoa wasiwasi Mawaziri waliopumzishwa kwenye nafasi zao ambapo amesema nafasi hizo huwa ni kwa zamu kama vile Kocha wa mpira ambavyo anaweza kumpumzisha Mchezaji kwa ajili ya mechi ijayo.
Spika Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo Bungeni Dodoma leo September 04, 2023 wakati akimkaribisha Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Dotto Biteko na akitoa salamu za pongezi kwake na kwa Baraza zima la Mawaziri.
“Wale ambao mmepumzika kidogo msiwe na wasiwasi, hili Baraza linao ambao waliwahi kupumzika, wakarejea, wakapumzika tena, wakarejea, kwahiyo msiwe na wasiwasi mnafasi hizi huwa ni kwa zamu ”
“Mtu zamu yake inapofika basi anapewa hiyo kazi, zamu yake inapopungua kidogo ni kama kocha anaweka huyu si kwamba wewe uliyetoka ni mbaya ama namna gani, Kocha anataka akupumzishe kwa ajili ya maandalizi ya shughuli nyingine hapo baadaye”
AYO