Mbunge Joseph Mhagama: Sera ya Mambo ya Nje imesaidia ushindi wa Dkt. Tulia kuwa Rais wa IPU

Kayugumis

Member
Jun 6, 2022
85
63
Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama amesema sera ya Mambo ya Nje na Diplomasia ya Nchi ni bora pamoja na uhusiano wa Kidiplomasia umechangia ushindi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Tulia Ackson kuwa Mshindi wa nafasi ya Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Hoja hiyo pia ilizungumzwa na Dr Tulia aliyesema kuwa ushindi alioupata umetokana na Nchi nyingi Duniani kufurahishwa na misingi mbalimbali iliyowekwa na Tanzania katika masuala mengi ikiwemo Demokrasia.

Akizungumzia kuhusu mchakato wa Kampeni ulivyokuwa , Mbunge Mhagama amesema "Kifupi tumeanza Kampeni za Mhe. Dr kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani mwezi Machi 2023. Katika kipindi hiki chote hadi tulipo fanya uchaguzi tarehe 27.10. 2023.

"Timu ya Kampeni imehusisha Wabunge 6 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Wabunge watano wa vyama mbalimbali vya kibunge kikanda na Kimataifa, Mabalozi Watatu, Wajumbe wa Sekretarieti ya Bunge."

Dr Tulia alipokelewa Oktoba 30, 2023 wakati akipokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi.

Upande wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwa niaba ya Serikali amesema “Moja ya majukumu ni kuhudhuria vikao vya Umoja wa Mataifa, tunajua kuwa Serikali yetu ina mikataba mingi katika Umoja wa Mataifa, tutakutumia wewe utakapokuwa unaenda kwenye vikao vya UN kuwa utatupigania.”

Tulia alishinda nafasi hiyo Oktoba 27, 2023 baada ya kupata Kura 172 kati ya 303 zilizopigwa.

Matokeo ya jumla katika kinyang’anyiro hicho yalikuwa hivi:

Adji Diarra Mergane Kanouté (Senegal) - 52
Catherine Gotani Hara (Malawi) - 61
Marwa Abdibashir Hagi (Somalia) - 11
Dkt. Tulia Ackson (Tanzania) - 172

Dkt. Tulia amechukua nafasi ya Duarte Pacheco kutoka Ureno aliyechaguliwa Mwaka 2020 baada ya kufanyika uchaguzi wa kwanza kupitia mtandao kutokana na maambukizi ya COVID-19.
 
Back
Top Bottom