Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Wakubwa! Hivi mmeangalia ratiba ya kampeni? Mpaka mnakuja ajenda, kila mgombea ana muda wa kupumzika hata TL alipumzika siku 2 tarehe 8&9 hii ni kutokana na muongozo wa ratiba ya NEC.
 

Attachments

  • ratiba ya kampeni.pdf
    367.5 KB · Views: 4
Katika hali inayoashiri mikikimiki ya Campaign, Mgombea urais kupitia chama cha Mapinduzi amepumzika kufanya kampeni.

Wachambuzi wa mambo wanatafsiri kuwa kampeni za Mwaka huu zimekuwa siyo nyepesi kama zilivyodhaniwa.

Magufuli ambaye mwaka 2015 alizunguuka kwa barabara nchi nzima, inaonekana dhahiri kuwa safari hii hawezi kuifikia rekodi ya mwaka huo. Safari hii inaonekana ameweka nguvu zaidi katika mikoa ya ukanda wa ziwa huku Wapiga kampeni wengine wakienda kanda nyingine.

Hata hivyo wapiga kampeni wake yaani Mama Samia na Kassim Majaliwa hawana mvuto mkubwa wa kisiasa wa kuweza kuchangia kura za maana kwa Magufuli.

Wakati huohuo mgombea wa Chadema Tundu Lissu ambaye ana faida ya kujinadi mapema makhsusi kwa ajili ya uchaguzi huu kwa kisingizio cha "kutafuta wadhamini" ameendelea kuchanja mbuga kwenye ngazi ya jimbo kwa jimbo baada ya kumaliza kupiga show kwenye ngazi ya kanda kwa kanda.

Sambamba na ngazi ya Jimbo kwa jimbo, Chadema watafanya mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha wanamng'oa Magufuli madarakani.

Bado haijajulikana kama kupumzika huku kwa mgombea wa CCM ni routine ya kawaida tu au uchovu au afya, tunangoja chama cha mapinduzi kitujuze zaidi.

View attachment 1567050
Atuletee umeme ,maji , barabara vijiji vya hapa geita vijijini, vijiji vya Nyamikoma,lwenge,Kamwanga na bugurura mkuyuni. Huko hali ni mbaya .
 
Au inawezekana afya haimruhusu kuendelea na mikikimikiki ya kampeni. Tungoje CCM watujuze zaidi

Lakini kikubwa zaidi, wana CCM wengi hawana shauku ya kumpigania Magufuli kwenye kampeni za mwaka huu isipokuwa kwa unafiki na hofu tu ya kushughulikiwa.
Akishinda ni kwa mbinu zile, siyo kwa kura maana hata ma-ccm wengi hawatompa kura
 
ccm ndio chama pekee kinachofanya kampeni zake kisayansi na kujaribu kuwafikia wapiga kura
Ni jimbo kwa jimbo,kata kwa kata
Tundu lissu anatoka anaenda bagamoyo kwa helicopter!kilometa 60 tu,hapo kati kawaacha wapiga kura kibao
 
Nashindwa kuelewa weredi wa wachangiaji wa hii post, hivi ni kweli kwamba nyote hamjapitia ratiba ya kampeni ya wagombea wa kiti cha urais?

Tarehe 9 anafanya kampeni Chato, baada ya hapo anapumzika siku tano, kisha ataendelea tarehe 15 huko Bukoba.
 
Hakuna watu wabaya kama mabepari,kwa nilichokisikia jana hapa Morogoro kutoka kwa Tundu Lisu balaa la CCM,maana Tundu Lisu amekuwa mwiba ulioingiza taharuki ndani ya CCM na kuwafanya wamuone ni balaa kubwa ambalo halijawahi kuishukia CCM tokea iasisiwe na vyama vyetu vya Tanu na ASP.

Yaani kila Mabepari weusi wanapojificha Tundu Lisu anawafichuwa na kuwakurupusha ,utawaona hao tokea walikuwa wakiwagaia waongeza vichwa sare za CCM bure sasa jana wameonekana wakigawa maji ya kunywa kwenye viwanja bure ,mara hii CCM mtagawa mpaka lakini mnapigwa na chini.

CCM mnaonekana wazi mnajitahidi kuwarubuni wananchi kwa kuwapa sare za CCM bure ,mi hapa mtaani nimewambia wananchi wenzangu wasiziache wazichuwe kwa wingi tu,wasiziache ni hela zao hizo,watazitumia kwenye maisha baada ya uchaguzi.

CCM sababu ya kutaka kushinda kwa hali yeyote sababu zinazidi kujizihirisha ,ni mali walizojinafsishia na kujikusanyia mali na maeneo makubwa sana ,inaonyesha ndani ya CCM kumejaa wanyang'anganyi Malibaba kibao.

Mabepari mwaka huu wakitoboa wanaingilia migodi,lakini asilimia ya ushindi wa CCM imeonyesa kushuka hadi kufikia asilimia 35 hadi jana,hivyo ushindi mwaka huu watausikia tu ukitangazwa kwa wengine.
 
Sasa mna yote hayo kwa nini mmeshindwa uwepo wa tume huru ili muwashinde kiroho safi wasiwe hata na kisingizio?

Kwa nini muwabanie vyombo vya habari?

Kwa nini kuwa engua engua?

Kwa nini mafigisu yasiyokwisha dhidi yao?
Tume huru ikija bado litatafutwa lingine la kulalamikia.
 
Back
Top Bottom