Serikali yaunda Kamati kuchunguza chanzo cha moto Soko Kuu Kariakoo. Waziri Mkuu asema hatua zitachukuliwa moja kwa moja ikijulikana kuna mkono wa mtu

Kwenye sehemu za umma ambazo serikali ndio muwajikabi hizo sheria hazifuatwi, lakini taasisi za binafsi utakuta watu wa fire brigade wanashinda hapo kufanya ukaguzi...
Halafu ukute hata insurance ya jengo hamna, na kama ilikuwepo iliexpire. Sasa muziki wa fidia kwa hao wafanyibiashara. Very Sad. Lazima serikali ibadilike aisee.
 
Halafu ni kwanini zile Ghorofa za Wafanyabiashara wadogo wadogo ( Wamachinga ) wengi na kule chini ( shimoni ) kabisa kwenyewe kupo tu Salama, ila huku ( kule ) kwa Wafanyabiashara Wakubwa ( Matajiri ) ndiyo Kumeathirika ( Kumeungua ) sana?

Nawaamini sana JF Members kwa kujua mambo mengi ( yaani Wajuvi ) hivyo hapa mtanisaidia nami Mzito wa Kuelewa na nisiyejua mambo mazito mazito Kuelewa na kuwa kama nyie na 'Great Thinker' wa uhakika.
 
Ukijiuliza sana kupita maelezo unaweza kukimbilia kwenye ujinga.

Kwa sababu lazima tujue chanzo cha moto kimetokea wapi ?

Kama chanzo kimeanzia juu maana yake kule kwenye chanzo ndo kutaathirika zaidi kuliko huku chini.

Lakini pia huku chininpengine kuna bidhaa ambazo haziwezi kusapoti combustion kwa uharaka.

Na kwa inavyoonesha moto umeanzia huku huku juu,jiulize baina ya juu na chini pale kariakoo kupo sawa kwa material ambayo yanaweza kusapoti moto kuwaka.

Soo unaanza kujiuliza maswali mengi mkuu ukaichosha akili yako nzuri.
 
Umeona tayari wale machinga wanaopanga vitu barabarani wameambiwa wahamie machinga complex, na wale waliokua kwenye jengo lililoathirika wahamie soko la kisutu, hoja hapo ni kua jiji la Dar halihitaji machinga barabarani so hiyo ni sababu na maelekezo yametolewa na hutosikia wanaruhusiwa kurudi barabarani
 
Na wanasema huu sio moto wa mwisho mingine mikubwa kwa mikubwa kama ule ulioiunguza bank kuu ya Tz iko kwa barabara
 
Zua tatizo, solve tatizo.

Chanzo cha moto hakifahamiki ndio maana watu wanabuni vitu vyao. Tunasuri tume hata wewe hukutakiwa kusema ivo kwasababu chanzo hujui.

Usishangae tume ikaja na majibu kuwa serikali imehusika😂😂, zama nyingine hii mkuu ni ukweli na uwazi.
 
Nmeulizwa hilo swali. Nikatataa kabisa kuwa hakuna uhusiano na wala tusiwaze hivyo.

Kuwa serikali iliona kuwaondoa wafanyabiashara kwa njia ya kawaida ni ngumu na kuwa soko la Kisutu limefunguliwa ila liwazi tu hamna watu.

Hivyo inabidi wadau waondolewe kariakoo. Kwa style hiyo. Wengi wakisema hata inapotakiwa kuliondoa soko hutumika njia hii au kuhamisha watu.

Mimi sioni kama haya ni mawazo sahihi. Huu ni moto tu wa bahati mbaya na utachunguzwa. Period.
 
Kamati ya Tanzania zilizowahi kufanikiwa ni za harusi tu....nyingine ni maigizo tu....hivi kweli kesi ya moto possibly arson inachunguzwa na waziri mkuu wakati Fire wapo...haya mambo wawaachie wataalamu ..PM akaendelea na mambo ya msingi
 
Mi nawaza coincidence ya Raisi kwenda kkoo kuongea na watu, then rehearsal ya Askari pale airport eti mazoezi ya kuokoa watu ikitokea janga..... Mara kkoo pamewaka, hapo hakuna maflekechee kweli???
 
'
JamiiForums1120482783.jpg


Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
mama Samia anasukumwa kuwa mkatili!
Unapohujumu soko kuu nchini kama la kariakoo ni wazi unatenda tendo la kigaidi kwani mfumuko wa bei kariakoo ni mfumuko wa bei Tanzania.

iwapo ikithibitika kuna uhujumu lazima wahisika wachukuliwe hatua Kali
 
Back
Top Bottom