Serikali yaunda Kamati kuchunguza chanzo cha moto Soko Kuu Kariakoo. Waziri Mkuu asema hatua zitachukuliwa moja kwa moja ikijulikana kuna mkono wa mtu

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,802
Habari wakuu,

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akiwa Soko Kuu la Kariakoo, amesema serikali imeunda tume ya watu kumi kuchunguza na kupata ukweli wa chanzo cha moto na athari zilizopatikana ikiwemo mali zilizoteketea, pia amesema Waziri mkuu yuko njiani kuja kukagua na kuongea na wafanyabiashara na umma kwa ujumla.

Makalla amesema kamati itakuja na mapendekezo ya namna bora ya kufanya ili kuendelea kukabiliana na majanga ya aina hiyo.

Mkuu wa Mkoa amewaomba waathirika kuwa watulivu wakati Serikali inachukua hatua za kubaini chanzo na athari. Pia amewakaribisha Bima kuja kuona wateja wao(Ambao walikuwa wamekata bima).

=========

Amos Makalla: Mheshimiwa Waziri mkuu, sisi tuko hapa toka jana, tumelala hapa baada ya janga hili la moto.

Athari ya janga hili ni kubwa na tumechukua hatua mbalimbali kuhakikisha usalama wa watu isitkee vifo au ajali za watu lakini mali nyingi zimeharibika.

Waziri Mkuu: Ndugu wafanyabiashara, nimekuja kuleta salam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Samia Suluhu. Kuja kwangu leo asubuhi ilikuwa ni moja ya maelekezo yake bna kuja kuona hali halisi ya kuungua kwa bidhaa mbalimbali ambazo ndizo zilizokuwa zinaipa hadhi ya eneo hili la Kariakoo.

Nimeona hali halisi na kwa namna ninavyojua soko la Kariakoo, hasara kubwa inatarajiwa kupatikana, kama ambavyo nimetangulia kuwapa pole, nirudie tena kuwapa pole kwa kupoteza mali, fedha lakini pia hata muelekeo wa kufanya shughuli zenu za kibiashara hapo baadae.

Eneo hilo kwa sasa ni hatarishi kwasababu bado moto unafuka mwingi, hatujajua bado kuna maeneo yana milipuko kama vile mitungi ya gesi ambao wanatumia gesi lakini kuna nyaya nyingi sana za umeme, kuna mitambo mingi iliyokuwa inauzwa lakini pia ilikuwa inatumika ndio maana eneo hili sio salama.

Tumeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi viendelee kuwa hapa kwa ajili ya kulinda usalama eneo zima lakini pia kuhakikisha moto huo hauendelei tena na watakuwa hapa mpaka utakapotulia kabisa.

Nawasihi sana wafanyabiashara wote muwe watulivu, kwasasa Serikali ipo na itaendelea kuwepo hapa mpaka tutakapojua nini chanzo cha moto huu, nani kisababishi cha moto huo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa

Mkuu wa mkoa ameunda timu ya uchunguzi lakini bado haitoshi, hili soko ni la kimataifa. Itakuja timu ya kitaifa ambayo itaungana na timu ya mkuu wa mkoa.

Timu ya mkuu wa mkoa ni wale ambao walikuwa hapa kuanzia jana wakafanya kazi ya uokoaji na kusikia hiki na kile na kupata taarifa

Timu hii ya kitaifa kuchunguza moto itajumuisha wafuatao
  1. Ofisi ya RAS
  2. Ofisi ya Rais Ikulu na TAMISEMI
  3. Ofisi ya waziri mkuu-Mkurugenzi wa Maafa
  4. Vyombo vya ulinzi na usalama vinne(JWTZ, Polisi)
  5. TBA(Mhandisi wa majengo na Mhandisi wa umeme kwenye majengo)
  6. TANESCO
  7. Mwanasheria Mkuu
  8. Mkurugenzi wa Mashtaka
Kama nilivyosema awali, tubaini chanzo cha moto. Nini kimesababisha au nani kasababisha moto huu. Pili tunataka tujue angalau kutabiri tu kiwango cha mali zilizopotea.

Tatu tunataka tujue usalama wa jengo lenyewe baada ya moto, Je jengo bado linaweza kutumika?

Endapo itagundulika kuna mtu alihusika kwa namna moja au nyingine, ndio maana huko ndani kuna Mwanasheria Mkuu, mkurugenzi wa mashtaka, Polisi. Hatua zitachukuliwa moja kwa moja.

Ndugu wafanyabiashara, tunatambua mheshimiwa Rais alipotembelea hapa aliunda tume ya kufanya mapitia ya tuhuma mbalimbali ziliibuliwa, inawezekana pia sijui, labda tume hiyo ilianza kuwagusa. Kama kulikuwa na njama zozote zilizowahusu tume ile na hao waliokuwa wanaguswaguswa na wakigundulika, hatua kali zitachukuliwa
 
Kamati ya nini mabata kweli haya majamaa.
Shoti ya umeme unaenda kamati.

Undeni kamati kuangalia kwa nini zimamoto ni taka taka
Kuna yule Kamishna Mkuu wa Zimamoto aliwahi kutumbuliwa enzi za JPM kwa tuhuma za kusaini mkataba aghali wa vifaa vya Zimamoto saa hizi atakuwa anachekelea tumboni. Alidhalilishwa sana kama mnakumbuka japo kwa sasa nadhani ana kau- RC sijui wapi huko.

Matokeo ya siasa kuingilia professionalism tena mbele ya kamera ndio kama hayo. Kwenye hili la Kariakoo hao Zimamoto wana la kujitetea; HATUNA VIFAA sawa kabisa na ukosefu wa PPE kwa madaktari kwenye issue ya COVID19.
 
Tunatakiwa kujiandaa kuzuia majanga sio kuunda kamati kuwapa posho kuchunguza tukio ambalo limeshatokea.

Yaani pesa ya kuwapa zimamoto wakawa na magari mengi yenye Maji kila eneo hatarishi kiusalama wa moto tunawapa watu kama posho.

Hatujifunzi ya MV Bukoba ilianguka karibu kabisa na bandari ya Mwanza, kivuko cha ukelewe kilikuwa karibu na mwalo, Mabomu ya Mbagala yakaja Gongolamboto na Tetemeko Kagera.

Kote huko hatujawai kuokoa watu na mali ipasavyo.

Hii nchi in viongozi vilaza sana.
 
Majanga yatakuwepo tuu hata chanzo kikijulikana na ndio maana kuna kitengo cha Zimamoto

Sasa tunahitaji zimamoto watueleze huwa wanakwama wapi!?
Kamishna Mkuu wa Zimamoto aliwahi kutumbuliwa enzi za JPM kwa tuhuma za kusaini mkataba aghali wa vifaa vya Zimamoto
 
Kuna yule Kamishna Mkuu wa Zimamoto aliwahi kutumbuliwa enzi za JPM kwa tuhuma za kusaini mkataba aghali wa vifaa vya Zimamoto saa hizi atakuwa anachekelea tumboni. Alidhalilishwa sana kama mnakumbuka japo kwa sasa nadhani ana kau- RC sijui wapi huko.
Ule mkataba ulikuwa unaleta Dron hapo sokon ingefanyaje kazi? Lakini ata hivo huwezi kufanya mipango ya kusaini mkono wa takriban Trilion 1 huku baraza la waziri halijui chochote
 
Back
Top Bottom