Kinachoendelea Mkutano wa Waziri Mkuu Majaliwa na Wafanyabiashara Kariakoo leo Mei 17, 2023

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,462
FwTzv8wXgAAQwqr.jpg

Wakati baadhi ya maduka katika eneo la Kariakoo yakiendelea kufungwa kwa siku ya tatu sasa, wafanyabiashara wa soko hilo tayari wamewasili ukumbi wa Arnaoutoglou jijini hapa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa ajili ya kutatua changamoto zao leo.

Baadhi ya wafanyabiashara hao wa soko hilo maarufu nchini na Afrika Mashariki wamegoma kufungua maduka yao kuishinikiza Serikali kutatua kero wanazoita za kikodi zinazowakabili.

Miongoni mwa kero hizo wanazozidai ni sheria wasiyokubaliana nayo ya usajili wa stoo, kamatakamata ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kubambikiwa kodi kubwa.

Juzi Mei 16, 2023 Majaliwa alifika sokoni hapo kutuliza hali ya hewa baada ya wafanyabiashara hao kugomea kauli ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ya kuwaomba waende naye Dodoma kufanya kikao na Waziri Mkuu huku wao wakishinikiza kiongozi huyo ndio afike sokoni hapo.

Sakata hilo likiwa linaingia siku ya tatu, leo Jumatano Mei 17, 2023 nje ya ukumbi wa Arnaoutoglou baadhi ya wafanyabiashara wamejitokeza wakisubiri mkutano na Waziri Mkuu kwa ajili ya kujadili hatma yao

Wakati majadiliano ya wafanyabiashara hao yakiendelea nao askari wapo katika wapo eneo hilo wakilinda amani.

Chanzo: Mwananchi

FwTzwSoWwAI2KsB.jpg

UPDATES...
Leo ndiyo siku ya mkutano kati ya Waziri Mkuu na wafanyabiashara Kariakoo.Kumekua na kutoelewana miongoni mwa wafanyabiashara kuhusu hasa ni nani atayefanya mazungumzo na Waziri Mkuu.

Wengi wa wafanyabiashara hawaridhii viongozi wao kwenda peke yao, wakisisitiza mgomo sio wa viongozi ni wa wote, hivyo wote washiriki.

Chanzo: The Chanzo
 
Serikali isikubali kuyumbishwa iweke utaratibu unao faaa.

Baadhi ya wafanyabiashara waliinyesha utovu wa nidhamu kwa kupuuza ombi la waziri Mkuu la kuwaomba wagungue maduka.
 
Duka langu, bidhaa iliyo dukani ni yangu na nililipia ushuru. Inakuwaje utovu wa nidhamu nikiamua kufunga?
 
View attachment 2624899
Wakati baadhi ya maduka katika eneo la Kariakoo yakiendelea kufungwa kwa siku ya tatu sasa, wafanyabiashara wa soko hilo tayari wamewasili ukumbi wa Arnaoutoglou jijini hapa kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa ajili ya kutatua changamoto zao leo.

Baadhi ya wafanyabiashara hao wa soko hilo maarufu nchini na Afrika Mashariki wamegoma kufungua maduka yao kuishinikiza Serikali kutatua kero wanazoita za kikodi zinazowakabili.

Miongoni mwa kero hizo wanazozidai ni sheria wasiyokubaliana nayo ya usajili wa stoo, kamatakamata ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kubambikiwa kodi kubwa.

Juzi Mei 16, 2023 Majaliwa alifika sokoni hapo kutuliza hali ya hewa baada ya wafanyabiashara hao kugomea kauli ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ya kuwaomba waende naye Dodoma kufanya kikao na Waziri Mkuu huku wao wakishinikiza kiongozi huyo ndio afike sokoni hapo.

Sakata hilo likiwa linaingia siku ya tatu, leo Jumatano Mei 17, 2023 nje ya ukumbi wa Arnaoutoglou baadhi ya wafanyabiashara wamejitokeza wakisubiri mkutano na Waziri Mkuu kwa ajili ya kujadili hatma yao

Wakati majadiliano ya wafanyabiashara hao yakiendelea nao askari wapo katika wapo eneo hilo wakilinda amani.

Chanzo: Mwananchi

View attachment 2624900

UPDATES...
Leo ndiyo siku ya mkutano kati ya Waziri Mkuu na wafanyabiashara Kariakoo.Kumekua na kutoelewana miongoni mwa wafanyabiashara kuhusu hasa ni nani atayefanya mazungumzo na Waziri Mkuu.

Wengi wa wafanyabiashara hawaridhii viongozi wao kwenda peke yao, wakisisitiza mgomo sio wa viongozi ni wa wote, hivyo wote washiriki.

Chanzo: The Chanzo
tunataka tujue kwanza kwa nini hawataki stoo zisisajiliwe?kuna nini ndani ya stoo hizo?naishauri serikali kuwa makini na wafanyabiashara hao.hakuna mfanyabishara duniani ambaye anapenda kulipa kodi kwa hiari sababu wao huwa wanataka super profit.ni lazima sheria za kodi na forodha zifanye kazi yake vinginevyo serikali itaonekana imefeli ktk ukusanyaji kodi na hiyo serikali itakuwa mfilisi.
 
USAJILI WA STOO NI LAZIMA

Baadhi ya wafanyabiashara wanakwepa KODI kwa kuingiza mizigo yao BANDARI BUBU USIKU WA MANANE.....hapa asilaumiwe mh.Mwigulu Nchemba......

#SiempreJMT
 
Back
Top Bottom