Masoko yaanza kuchomwa tena? Angalia Soko la Mbuyuni Moshi likiteketea

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,718
218,265
Taarifa ya Azam inaeleza kwamba soko la Mbuyuni huko Moshi linateketea usiku huu.

Moto umeanza usiku wa saa 7 tarehe 06/02/2024

Hivi kwanini masoko hayaungui mchana?

============

Kufuatia ajali ya Moto iliyoteketeza Soko la Mbuyuni, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema moja ya changamoto zilizosababisha moto huo kutodhibitiwa kwa wakati ni Ubovu wa gari la Zimamoto la Manispaa hiyo, uliosababisha kuomba msaada wa gari kutoka TPC ambalo lilichukua takriban Dakika 30 kufika eneo la tukio

Amesema Serikali inafanya tathmini ya kujua chanzo na hasara za moto huo ulioanza majira ya Saa 7 usiku wa Februari 6, 2024

Ikumbukwe, Mnamo Februari 29, 2016 Soko hilo liliungua baada ya moto mkali kuzuka majira ya Saa 2 usiku, pia Februari 1, 2022 Soko hilo liliteketea upande wa Matunda na Mbogamboga kwa moto ambao chanzo chake hakikujulikana mara moja


Screenshot_2024-02-06-02-26-06-1.png
 
Soko Hilo Ni Muhimu Sana Moshi Mjini Na Kwa Namna Palivyokaa Oops
Nimepata Huduma Sana Sokoni Hapo
 
Back
Top Bottom