Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,575
- 13,261
Salaam Wakuu,
Hapa chini ni Muhtasari wa ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mwaka wa Fedha 2019/2020
===
Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PAC; Mhe. Grace Tendega (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya LAAC; Mhe. Daniel Sillo (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti; Mhe. Japhet Hasunga (Mb), Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PAC; Mhe. Suleman Zedy (Mb), Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya LAAC; Mhe. Omary Kigua (Mb), Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti; Ndugu Wanahabari; Watumishi Wenzangu wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi;
NAWASALIMU KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Hivyo hii ni ofisi inayozingatia weledi, miongozo, kanuni za ukaguzi pamoja na viwango vya kimataifa vya ukaguzi katika kuikagua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mujibu wa Katiba na Sheria pamoja na ukaguzi wa Taasisi za Kimataifa ambazo tunapata fursa ya kuzikagua.
2.0 RIPOTI ZILIZOWASILISHWA
Ripoti zilizowasilishwa leo bungeni ni 21 zinazojumuisha masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika Ukaguzi nilioufanya kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2020 kwa Taasisi nilizozikagua ambazo ni kama ifuatavyo:
3.0 MWENENDO WA HATI ZA UKAGUZI
Kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 nimetoa jumla ya Hati 900 za Ukaguzi; ikiwa ni hati 243 za Serikali Kuu, 185 Mamlaka za Serikali za Mitaa, 165 Mashirika ya Umma, 290 Miradi ya Maendeleo na 17 Vyama vya siasa. Kati ya hizo, Hati zinazoridhisha ni 800 (sawa na asilimia 89); Hati zenye shaka ni 81 (sawa na asilimia 9); Hati mbaya ni 10 (sawa na asilimia moja); na nilitoa hati tisa za kushindwa kutoa maoni (sawa na asilimia moja). Jedwali hapa chini linaonesha mchanganuo wa hati hizo.
MCHANGANUO WA HATI ZA UKAGUZI WA HESABU KWA MWAKA 2019/20
Nitoe wito kwa Menejimenti, Bodi za Wakurugenzi na Maafsa Masuuli wa Taasisi hizo hapo juu kuhakikisha wanatimiza matakwa ya Kikatiba na Kisheria kwa kuhakikisha kwamba wanawasilisha hesabu kila mwaka kwa ajili ya kutolewa maoni ya kikaguzi. Pia wale ambao hutakiwa kufanya marekebisho ya hesabu ili kuhakikisha wanazingatia viwango vya kimataifa vya kutengeneza hesabu, warekebishe kisha wazilete ndani ya muda ili niweze kutoa hati na kutimiza matakwa ya Ibara 143(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2005) badala ya kutoziwalisha kwa kuona kwamba watapata hati wasiyoipenda.
Kwa Mwaka huu nimetoa Hati Mbaya kwa taasisi zifuatazo:
4.0 TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO YALIYOTOLEWA MIAKA ILIYOPITA
Katika ukaguzi wangu wa mwaka huu, nilifanya tathmini ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa miaka iliyopita; kati ya mapendekezo 8,740 yaliyotolewa miaka iliyopita, mapendekezo 2,610 sawa na asilimia 30 yametekelezwa kikamilifu. Mapendekezo 2,662 sawa na asilimia 30 utekelezaji wake unaendelea. Aidha, mapendekezo 2,292 sawa na asilimia 26 utekelezaji wake haujaanza; mapendekezo 751 sawa na asilimia 9 yamerudiwa; na mapendekezo 426 sawa na asilimia 5 yamepitwa na wakati. Jedwali hapa chini linafafanua mchanganuo wa utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi.
HALI YA UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO YALIYOTOLEWA KWENYE KAGUZI ZA UFANISI
Kwa ujumla, utekelezaji wa mapendekezo niliyotoa hauridhishi ikizingatiwa kuwa ni asilimia 14 tu ya mapendekezo yote yaliyotolewa yametekelezwa kikamilifu; hivyo, jitihada zaidi zinahitajika kukamilisha utekelezaji wa mapendekezo yote.
5.0 MATOKEO YA UKAGUZI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
Hadi tarehe 30 Juni 2020 deni la serikali lilikuwa linahimilika.
Lita milioni 2.47 za mafuta zenye makadirio ya ushuru wa forodha wa Sh. bilioni 1.97 yalibaki nchini bila kusafirishwa kwenda nchi zilizokusudiwa kwa muda uliopangwa wa siku 30.
Lita milioni 14.08 za mafuta zenye ushuru wa forodha unaokadiriwa kufikia Sh. bilioni 10.43 zilizoshushwa Tanzania Bara kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Zanzibar tangu Julai 2019 hazijaondoshwa kwa muda uliopangwa wa siku 21. Kwa mujibu wa sheria ya forodha, mafuta yanayokaa nchini kwa zaidi ya muda uliopangwa yanapaswa kurasimishwa kwa matumizi ya ndani na hivyo kutozwa ushuru unaotakiwa.
Pia, nilibaini bidhaa (mitambo) zenye thamani ya Sh. bilioni 20.25 na ushuru wa forodha Sh. bilioni 1.24 zilizoingizwa kwa muda nchini kupitia mipaka ya Namanga, KIA, Holili na Bandari kavu hazijaondolewa baada ya kumalizika kwa muda ulioruhusiwa kuwapo nchini, wala hazijarasimishwa kwa matumizi ya ndani kama sheria ya forodha inavyoelekeza.
5.1.3 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Pia, nilibaini kuwa, Kiasi hicho cha fedha kilichukuliwa na Mtunza Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka katika akaunti hiyo kwa vipindi tofauti kwa kutumia nyaraka za fedha za kughushi.
Aidha, nilibaini kuwa, usuluhishi wa taarifa za benki kwenye akaunti ya masurufu haukufanywa kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai 2019 hadi tarehe ya kukamilisha ukaguzi. Hii ni kinyume na Kanuni Na. 162 (1) ya Kanuni ya Fedha za Umma ya mwaka 2001 ambayo inahitaji taarifa za fedha za benki zifanyiwe usuluhisho angalau kila mwezi.
Hali Hii inaashiria udhibiti dhaifu wa mifumo ya ndani kwenye usimamizi wa fedha katika akaunti za benki za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Hata hivyo, ninaona uamuzi wa kuwekeza fedha za walipa kodi zenye thamani ya Sh. bilioni 3.92 kufanya ukarabati mkubwa wa ndege bila kufanya tathmini ya kina ya gharama na faida haukuwa sahihi, na hivyo, kusababisha hasara kwa taifa.
5.1.5 Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Makusanyo ya kivuko ambayo hayajapelekwa benki na hayapo kituoni Sh. 81,194,650
Nilibaini kuwa Kituo cha Kivuko cha Magogoni kilikusanya jumla ya Sh. bilioni 5,757,041,950 ikiwa ni tozo za kivuko kwa kipindi kilichoanzia tarehe 1 Julai 2019 hadi 30 Juni 2020. Hata hivyo, kati ya pesa zilizokusanywa, ni Sh. 5,675,847,300 ndizo zilizowekwa kwenye akaunti ya Benki inayosimamiwa na Makao Makuu ya TEMESA, ikiacha jumla ya kiasi cha Sh. 81,194,650 kikiwa bado hakijawekwa benki hadi muda wa ukaguzi, tarehe 31 Julai 2020. Aidha, nilibaini kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho hakikuwekwa benki pia hakikuwa kwenye himaya ya kituo. Kwa maoni yangu, fedha hizi ambazo hazijawekwa benki kuna uwezekano kwamba zimetumiwa vibaya au kutumiwa katika shughuli zingine.
Ni maoni yangu kuwa, tiketi hizo zinaweza kutumika tena na kusababisha serikali kupoteza mapato.
5.1.6 Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Ukaguzi wangu wa mkataba huu umebaini kuwa kulikuwa na makubaliano ya kusambaza kadi 25,000,000 mpaka kipindi cha Ukaguzi, Novemba 2020, nilibaini kwamba msambazaji aliwasilisha kadi 13,735,728 tu. Aidha, uchambuzi wangu ulibaini kwamba, kati ya kadi zilizowasilishwa, NIDA imetumia kadi 6,180,015 kutengeneza vitambulisho vya taifa na kubakiza kadi 5,084,257 zikiwa hazijatumika.
Hata hivyo, nimebaini kuwa kati ya kadi 5,084,257 zilizobakia, ni kadi 4,657,500 tu ndizo zilikuwa zimehifadhiwa kwenye bohari, huku kadi 426,757 zenye thamani ya Sh. 3,399,973,019[1] zikiwa zimeharibika na hazifai kwenye matumizi ya kutengeneza vitambulisho vya taifa. Licha ya menejimenti ya NIDA kueleza kuwa imetuma barua kwenda kwa mkandarasi (IRIS) ili afanye usuluhisho wa kadi zilizoonekana na matatizo na kubadilisha na kadi mpya ni maoni yangu kuwa kuna hatari ya NIDA kupata hasara ikiwa IRIS atashindwa kubadilisha kadi hizo ambazo hazifai kutokana na kukosekana kwa mkataba halali kati ya NIDA na M/s IRIS Corporation Berhad.
5.1.7 Wakala wa Umeme Vijijini (REA)
Kwenye ukaguzi wa mkataba huu, nilibaini kuwa mkandarasi aliweka nguzo za umeme 6,541 zenye thamani ya Sh. 2,965,562,433.33 katika mkoa wa
Lindi. Hata hivyo, wakati wa kutembelea mradi mnamo Oktoba 2020 niliona
kwamba kati ya nguzo zilizowekwa, nguzo za umeme 2,612 (40%) zenye thamani ya Sh. 1,065,696,000 zilikuwa na nyufa. Mbali na hivyo, mkandarasi hakuwa amebadilisha nguzo hizo zenye kasoro. Hii ni kinyume na Kifungu 23.6 cha GCC kinachomtaka mkandarasi kusahihisha au kubadilisha bidhaa au sehemu ya vifaa ikiwa bidhaa hizo au vifaa vimeshindwa kufaulu jaribio au ukaguzi.
5.1.8 Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali
Chanzo: Taarifa za Benki
Kutotumiwa kwa bakaa ya fedha katika akaunti kunasababishwa na kutokuwapo kwa sheria na kanuni za kudhibiti matumizi ya fedha itokanayo na mali zilizotaifishwa na kurejeshwa serikalini.
Ni maoni yangu kuwa, kuwapo wa fedha zisizotumiwa kwa sababu ya kukosekana kwa Muongozo au mfumo wa kisheria kunaweza kusababisha matumizi mabaya ya Fedha za umma na ucheleweshaji wa maendeleo ya umma.
5.1.9 Masuala Mtambuka
Chanzo: Barua ya mapungufu kwa menejimenti
Ni maoni yangu kwamba, kutokurudishwa kwa fedha zilizokopwa na Wizara kunaathiri utekelezaji wa shughuli za Mifuko Maalumu, hivyo fedha hizo zirejeshwe ili kutekeleza shughuli zilizopangiwa.
Chanzo: Barua ya mapungufu kwa menejimenti
Ni maoni yangu kuwa chanzo cha kuwa na matumizi yenye nyaraka pungufu ni kuwa na mfumo dhaifu wa udhibiti na Maafisa Masuuli kushindwa kuchukua hatua stahiki kwa maafisa wanaosababisha udhaifu huu. Ninaamini kuwa hii inaweza kuwa ishara ya kufanyika kwa matumizi ya udanganyifu na mabaya. Mawanda yangu ya Ukaguzi yalizuiwa hivyo sikuweza kuthibitisha uhalali wa malipo yaliyofanyika.
[1] Gharama ya kila kadi ni Dola za Marekani 3.452 sawa na Sh. 7,967 kwa kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni cha BOT mnamo tarehe 30 June 2020; hivyobasi, kadi 426,757 mara Sh. 7,967 ni sawasawa na Sh. 3,399,973,019
Hapa chini ni Muhtasari wa ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mwaka wa Fedha 2019/2020
===
Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PAC; Mhe. Grace Tendega (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya LAAC; Mhe. Daniel Sillo (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti; Mhe. Japhet Hasunga (Mb), Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PAC; Mhe. Suleman Zedy (Mb), Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya LAAC; Mhe. Omary Kigua (Mb), Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti; Ndugu Wanahabari; Watumishi Wenzangu wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi;
NAWASALIMU KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
1.0 UTANGULIZI
Ndugu Wanahabari,
Awali ya yote napenda kutanguliza shukurani kwa Mwenyezi Mungu aliyetupa uzima na afya njema kuweza kuiona siku hii ya leo. Pia, ninawashukuru kwa kuitikia wito wa kuja kusikiliza muhtasari wa masuala yaliyojitokeza kwenye kaguzi zangu za Mwaka wa Fedha 2019/20.Ndugu Wanahabari,
Mnamo tarehe 28 Machi 2021 nilitimiza jukumu langu la kikatiba kwa mujibu wa Ibara ya 143 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 (iliyorekebishwa mwaka 2005), inayonitaka kuwasilisha ripoti za ukaguzi za kila mwaka kwa Mhe. Rais kabla au ifikapo tarehe 31 Machi kila mwaka.Ndugu Wanahabari,
Kwa mujibu sheria ya ukaguzi, ripoti hizi zinakuwa tayari kwa matumizi ya umma zinapowasilishwa bungeni ambapo tukio hilo limefanyika leo kwa Mawaziri husika kuwasilisha ripoti hizi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, natumia fursa hii kuujulisha umma kwa ufupi mambo mbalimbali yaliyojitokeza kwenye ukaguzi nilioufanya kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.Ndugu Wanahabari,
Kabla ya kuwajulisha muhtasari wa mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye ukaguzi nilioufanya kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 naomba niongelee kwa kifupi Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na mchakato wa ukaguzi wenyewe kwa manufaa yenu na manufaa ya wananchi kwa ujumla.Ndugu Wanahabari,
Ofisi ya Taifa ya ukaguzi ni miongoni wa ofisi katika nchi hii ambazo zina mifumo madhubuti ya utendaji kazi. Ofisi hii inafanya kazi kwa kuzingatia misingi ambayo imekuwa ikijengwa tangia kuanzishwa kwa ofisi ya CAG Mnamo tarehe 1 Julai 1961 hadi sasa. Misingi na Mifumo hii inafanya kazi kwa usahihi kabisa, hivyo si rahisi mtu yeyote awe CAG ama msaidizi wake kuivuruga misingi hii. Ukaguzi ni mchakato unaohusisha watu wengi sana hadi kuona ripoti zinatoka na hakuna mtu mmoja anayeweza kufanya maamuzi kuhusu nini kiandikwe kwenye ripoti; kazi hii hufanywa na watu wengi sana kwenye mnyororo wa ukaguzi.Ndugu Wanahabari,
Ofisi hii ni mwanachama wa Shirikisho la Taasisi Kuu za Ukaguzi Duniani yaani INTOSAI. Pia ofisi hii ni mwanachama wa umoja wa Taasisi Kuu za Ukaguzi kwa Afrika kwa Nchi zinazozungumza Kiingereza yaani AFROSAI E. Hizi Taasisi zote hufanya ufuatiliaji wa jinsi ofisi hii inavyofanya kazi kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa na miongozo tuliojiwekea.Ndugu Wanahabari,
Kwa misingi, umakini pamoja na miongozo, imeifanya ofisi hii kuwa Mkaguzi wa Umoja wa Mataifa kwa miaka 6 na sasa ni Mkaguzi wa Nje wa Kamisheni ya Usafiri wa Anga Afrika (AFCAC) kuanzia Mwaka huu hadi Mwaka 2022/23. Pia imekuwa miongoni mwa Wakaguzi wa Nje wa Kamisheni ya Afrika (Umoja wa Afrika – AU) kuanzia mwaka huu. Pia ni Mkaguzi wa EAC na SADC; na kazi hizi zinafanyika kwa umahiri na weledi mkubwa.Hivyo hii ni ofisi inayozingatia weledi, miongozo, kanuni za ukaguzi pamoja na viwango vya kimataifa vya ukaguzi katika kuikagua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mujibu wa Katiba na Sheria pamoja na ukaguzi wa Taasisi za Kimataifa ambazo tunapata fursa ya kuzikagua.
Ndugu Wanahabari,
Mchakato wa kukagua Taasisi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huanza mnamo mwezi Mei ya kila mwaka kwa mujibu wa kalenda yetu ya ukaguzi. Inapofika mwezi Januari mwaka unaofuata huwa tunakamilisha zoezi la ukaguzi kwenye field na kuanza kuandaa ripoti za ukaguzi. Kwa maana hiyo taarifa hii ambayo leo nawapa muhtasari wake, ukaguzi wake ulianza mnamo mwezi Mei 2020 na kazi za field zilimalizika mwezi Januari 2021 na kuanza kuandaa ripoti hizi. Mapema mwezi wa Machi ripoti hizi zilienda kwa mchapishaji kwa ajili ya kuchapishwa na kuwa tayari ambapo tarehe 28 Machi 2021 niliziwasilisha kwa Mh Rais.Ndugu Wanahabari,
Mtakumbuka kwamba niliteuliwa kuingia ofisi hii mnamo Mwezi Novemba 2019, hivyo hii ni taarifa yangu ya kwanza ambayo nimeisimamia kuanzia planning hadi kumalizika kwa ripoti na kuwasilishwa kwa Mh Rais na kisha leo kuwasilishwa Bungeni.2.0 RIPOTI ZILIZOWASILISHWA
Ndugu Wanahabari,
Baada ya utangulizi huo, sasa niingie kwenye taarifa yenyewe.Ripoti zilizowasilishwa leo bungeni ni 21 zinazojumuisha masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika Ukaguzi nilioufanya kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2020 kwa Taasisi nilizozikagua ambazo ni kama ifuatavyo:
- Ripoti ya Ukaguzi ya Serikali Kuu;
- Ripoti ya Ukaguzi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Ripoti ya Ukaguzi ya Mashirika ya Umma;
- Ripoti ya Ukaguzi ya Miradi ya Maendeleo;
- Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi;
- Ripoti ya Ukaguzi wa Mifumo ya TEHAMA;
- Ripoti ya ufuatiliaji wa mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti za Ukaguzi wa ufanisi kwa miaka iliyopita; na
- Ripoti 14 za ukaguzi ufanisi zinazohusu sekta mbalimbali.
Ndugu Wanahabari,
Ripoti 14 za Ukaguzi wa Ufanisi (Performance Audit) katika maeneo mbalimbali ni kama ifuatavyo:- Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Usafi wa Masoko ya Vyakula;
- Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa udhibiti wa Mafuriko;
- Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Uandikishaji na Utoaji wa Vitambulisho vya Taifa;
- Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Matengenezo ya Magari na Mitambo ya Serikali;
- Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Ununuzi wa Pamoja wa
- Magari ya Serikali na Usambazaji wa Mafuta; vi. Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Mifumo ya Kudhibiti Ubora wa Vyakula Vinavyosindikwa Nchini;
- Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Ujenzi wa Majengo ya Vituo vya Huduma za Afya Nchini;
- Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Mali zilizotelekezwa;
- Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Utekelezaji wa Udhibiti wa Uhamishaji wa Bei ya Mauziano ya Bidhaa au Huduma Baina ya Makampuni yenye Mahusiano;
- Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Ufuatiliaji na Usimamizi Wa Miradi ya Ujenzi Kwenye Sekta ya Elimu Inayotekelezwa kwa Njia ya ‘Force Account’;
- Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Udhibiti wa Uchafuzi Unaotokana na Taka za Plastiki kwenye Bahari na Maziwa;
- Ukaguzi wa Ufanisi Kuhusu Utekelezaji wa Mradi wa Awamu ya Pili ya Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam;
- Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Misamaha ya Kodi ya kwenye Miradi Ya Uwekezaji; na
- Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Utekelezaji wa Mradi wa Uzalishaji Sukari wa Mbigiri.
3.0 MWENENDO WA HATI ZA UKAGUZI
Ndugu Wanahabari,
Aina ya Ripoti | Jumla ya Hati | Hati zinazoridhisha | Hati zenye shaka | Hati mbaya | Kushindwa kutoa maoni |
Mamlaka ya Serikali za Mitaa | 185 | 124 | 53 | 8 | 0 |
Mashirika ya Umma | 165 | 162 | 3 | 0 | 0 |
Serikali Kuu | 243 | 235 | 6 | 2 | 0 |
Vyama vya siasa | 17 | 4 | 4 | 0 | 9 |
Miradi ya Maendeleo | 290 | 275 | 15 | 0 | 0 |
Jumla | 900 | 800 | 81 | 10 | 9 |
Asilimia | 100 | 89 | 9 | 1 | 1 |
Kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 nimetoa jumla ya Hati 900 za Ukaguzi; ikiwa ni hati 243 za Serikali Kuu, 185 Mamlaka za Serikali za Mitaa, 165 Mashirika ya Umma, 290 Miradi ya Maendeleo na 17 Vyama vya siasa. Kati ya hizo, Hati zinazoridhisha ni 800 (sawa na asilimia 89); Hati zenye shaka ni 81 (sawa na asilimia 9); Hati mbaya ni 10 (sawa na asilimia moja); na nilitoa hati tisa za kushindwa kutoa maoni (sawa na asilimia moja). Jedwali hapa chini linaonesha mchanganuo wa hati hizo.
MCHANGANUO WA HATI ZA UKAGUZI WA HESABU KWA MWAKA 2019/20
Ndugu Wanahabari,
Katika mwaka wa fedha 2019/20 nilishindwa kukagua Balozi/Misheni 43 kutokana na kushindwa kusafiri kwa sababu ya ugonjwa wa Covid-19. Aidha, sikukamilisha ukaguzi wa mashirika ya umma 11 kwa sababu hayakuwasilisha taarifa za hesabu wakati wa ukaguzi. Mashirika ambayo sikuweza kuyatolea maoni ya ukaguzi ni haya yafuatayo:Na | Shirika |
1 | Hospitali ya Taifa ya Muhimbili |
2 | Kampuni ya Mbolea Tanzania |
3 | Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya |
4 | Mfuko wa UTT AMIS/PID |
5 | Kampuni ya Magazeti ya Serikali |
6 | Shirika la Posta Tanzania |
7 | Shirika la Reli la Tanzania |
8 | Kampuni ya Simu Tanzania |
9 | Shirika la Umeme Tanzania |
10 | Soko la Bidhaa Tanzania |
11 | Taasisi ya Mifupa Muhimbili |
Nitoe wito kwa Menejimenti, Bodi za Wakurugenzi na Maafsa Masuuli wa Taasisi hizo hapo juu kuhakikisha wanatimiza matakwa ya Kikatiba na Kisheria kwa kuhakikisha kwamba wanawasilisha hesabu kila mwaka kwa ajili ya kutolewa maoni ya kikaguzi. Pia wale ambao hutakiwa kufanya marekebisho ya hesabu ili kuhakikisha wanazingatia viwango vya kimataifa vya kutengeneza hesabu, warekebishe kisha wazilete ndani ya muda ili niweze kutoa hati na kutimiza matakwa ya Ibara 143(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2005) badala ya kutoziwalisha kwa kuona kwamba watapata hati wasiyoipenda.
Ndugu Wanhaabari,
Kwa Mwaka huu nimetoa Hati Mbaya kwa taasisi zifuatazo:
- Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
- Halmashauri ya Wilaya ya Singida
- Halmashauri ya Wilaya ya Itigi
- Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
- Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge
- Halmashauri ya Wilaya ya Urambo
- Halmashauri ya Wilaya ya Momba
- Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
- Tume ya UNESCO.
- Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Morogoro.
Ndugu Wanahabari,
Hati zenye shaka zimetolewa kwa taasisi zifuatazo: MCHANGANUO WA TAASISI ZILIZOPATA HATI ZENYE SHAKA
NA. | JINA LA TAASISI | KUNDI |
1. | Wakala wa Usimamizi wa Maendeleo ya Elimu (ADEM) | Serikali Kuu |
2. | Wakala wa Huduma za Manunuzi Serikalini (GPSA) | Serikali Kuu |
3. | Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) | Serikali Kuu |
4. | Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Shinyanga | Serikali Kuu |
5. | Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Sumbawanga Rukwa | Serikali Kuu |
6. | Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Temeke | Serikali Kuu |
7. | Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam | Mashirikay ya Umma |
8. | Chuo cha Diplomasia (CFR) | Mashirika ya Umma |
9. | Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) | Mashirika ya Umma |
10. | Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
11. | Halmashauri ya Wilaya ya Butiama | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
12. | Halmashauri ya Wilaya ya Songea | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
13. | Halmashauri ya Manispa ya Kigoma/Ujiji | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
14. | Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
15. | Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
16. | Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
17. | Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
18. | Halmashauri ya Wilaya ya Siha | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
19. | Halmashauri ya Jiji la Arusha | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
20. | Halmashauri ya Wilaya ya Bahi | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
21. | Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
22. | Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
23. | Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
24. | Halmashauri ya Wilaya ya Bunda | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
25. | Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
26. | Halmashauri ya Wilaya ya Chemba | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
27. | Halmashauri ya Wilaya ya Chunya | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
28. | Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
29. | Halmashauri ya Wilaya ya Geita | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
30. | Halmashauri ya Wilaya ya Hanang | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
31. | Halmashauri ya Wilaya ya Iramba | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
32. | Halmashauri ya Wilaya ya Iringa | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
33. | Halmashauri ya Manispaa ya Iringa | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
34. | Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
35. | Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
36. | Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
37. | Halmashauri ya Mji wa Kasulu | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
38. | Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
39. | Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
40. | Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
41. | Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
42. | Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
43. | Halmashauri ya Mji wa Kondoa | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
44. | Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
45. | Halmashauri ya Mji wa Korogwe | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
46. | Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
47. | Halmashauri ya Wilaya ya Liwale | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
48. | Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
49. | Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
50. | Halmashauri ya Wilaya ya Msalala | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
51. | Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
52. | Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
53. | Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
54. | Halmashauri ya Wilaya ya Nzega | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
55. | Halmashauri ya Mji wa Nzega | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
56. | Halmashauri ya Wilaya ya Rorya | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
57. | Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
58. | Halmashauri ya Manispaa ya Singida | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
59. | Halmashauri ya Manispaa ya Temeke | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
60. | Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
61. | Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
62. | Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza | Mamlaka za Serikali Za Mitaa |
63. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Monduli | Miradi ya Maendeleo |
64. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Mji wa Mafinga | Miradi ya Maendeleo |
65. | Miradi ya Maendeleo | |
66. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe | Miradi ya Maendeleo |
67. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Wilaya ya Itigi | Miradi ya Maendeleo |
68. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Wilaya ya Urambo | Miradi ya Maendeleo |
69. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Wilaya ya Nzega | Miradi ya Maendeleo |
70. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Wilaya ya Bunda | Miradi ya Maendeleo |
71. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Wilaya ya Butiama | Miradi ya Maendeleo |
72. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu | Miradi ya Maendeleo |
73. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Wilaya ya Magu | Miradi ya Maendeleo |
74. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga | Miradi ya Maendeleo |
75. | Mfuko wa Afya-Halmahsuri ya Wilaya ya Kakonko | Miradi ya Maendeleo |
76. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Wilaya ya Longido | Miradi ya Maendeleo |
77. | Mfuko wa Afya-Halmashauri ya Wilaya ya Musoma | Miradi ya Maendeleo |
78. | United Democratic Party (UDP) | Chama Cha Siasa |
79. | Chama Cha Kijamii (CCK) | Chama Cha Siasa |
80. | Civic United Front (CUF) | Chama Cha Siasa |
81. | National League for Democracy (NLD) | Chama Cha Siasa |
4.0 TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO YALIYOTOLEWA MIAKA ILIYOPITA
Ndugu Wanahabari,
Katika ripoti za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa miaka iliyopita, nilitoa mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuimarisha usimamizi wa rasilimali za umma pamoja na kuboresha ukusanyaji wa mapato.Katika ukaguzi wangu wa mwaka huu, nilifanya tathmini ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa miaka iliyopita; kati ya mapendekezo 8,740 yaliyotolewa miaka iliyopita, mapendekezo 2,610 sawa na asilimia 30 yametekelezwa kikamilifu. Mapendekezo 2,662 sawa na asilimia 30 utekelezaji wake unaendelea. Aidha, mapendekezo 2,292 sawa na asilimia 26 utekelezaji wake haujaanza; mapendekezo 751 sawa na asilimia 9 yamerudiwa; na mapendekezo 426 sawa na asilimia 5 yamepitwa na wakati. Jedwali hapa chini linafafanua mchanganuo wa utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi.
TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO YA UKAGUZI
Aina ya Ripoti | Jumla Kuu | Yaliyo tekelezwa Kikamilifu | Utekelezaji unaendelea | Yasiyo tekelezwa | Mapendekezo yaliyorudiwa | Yaliyopitwa na wakati |
Mamlaka ya Serikali za Mitaa | 15 | 6 | 0 | 5 | 4 | 0 |
Mashirika ya Umma | 116 | 25 | 36 | 52 | 0 | 3 |
Serikali Kuu | 5,483 | 1,508 | 2,003 | 1,211 | 502 | 259 |
Miradi ya Maendeleo | 3,126 | 1,071 | 623 | 1,024 | 245 | 164 |
Jumla | 8,740 | 2,610 | 2,662 | 2,292 | 751 | 426 |
Asilimia | 100 | 30 | 30 | 26 | 9 | 5 |
Ndugu Wanahabari,
Pia, niwape tathmini ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa kwenye kaguzi tano za ufanisi katika kipindi cha mwaka 2016 kama inavyoainishwa kwenye Jedwali hapa chini.HALI YA UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO YALIYOTOLEWA KWENYE KAGUZI ZA UFANISI
Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi | Mapendekezo | ||||
Jumla Kuu | Yaliyo tekelezwa Kikamilifu | Yaliyo tekelezwa Kiasi | Yasiyo tekelezwa | Yaliyopitwa na wakati | |
Utekelezaji wa Masharti ya Mahitaji ya Ndani na Uhakiki wa Gharama Rejeshi Unaotokana na Makubaliano ya Mgawanyo wa Uzalishaji | 10 | 0 | 6 | 3 | 1 |
Usimamizi wa Takwimu za Jiofizikia na Jiolojia ya Mafuta na Gesi nchini Tanzania | 16 | 8 | 5 | 3 | 0 |
Usimamizi wa Mchakato wa Utoaji wa Mikataba ya Utafutaji, Uendelezaji na Leseni za Gesi Asilia | 12 | 0 | 9 | 3 | 0 |
Ufuatiliaji wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni zinazohusu Shughuli za Utafutaji wa Petroli nchini Tanzania | 15 | 13 | 1 | 0 | |
Usimamizi wa Uendelezaji wa Rasilimali Watu katika Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia | 10 | 0 | 5 | 5 | 0 |
Jumla | 63 | 9 | 38 | 15 | 1 |
Asilimia | 100 | 14 | 60 | 24 | 2 |
Kwa ujumla, utekelezaji wa mapendekezo niliyotoa hauridhishi ikizingatiwa kuwa ni asilimia 14 tu ya mapendekezo yote yaliyotolewa yametekelezwa kikamilifu; hivyo, jitihada zaidi zinahitajika kukamilisha utekelezaji wa mapendekezo yote.
Ndugu Wanahabari,
Napenda nichukue nafasi hii kumshukuru sana Mh. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maelekezo yake aliyoitoa siku nakabidhi hizi ripoti kwamba wahusika watekeleze mapendekezo ambayo nimekuwa nikiyatoa. Utekelezaji wa mapendekezo na ushauri ninaoutoa utasaidia kuimarisha mifumo ya udhibiti wa ndani na hivyo kuongeza mapato na kupunguza matumizi ya Serikali kwani hoja zingine zimekuwa zikijirudia kwa kuwa wahusika wanaacha tu kutekeleza mapendekezo na ushauri ninaoutoa.5.0 MATOKEO YA UKAGUZI KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020
Ndugu Wanahabari,
Naomba sasa niwape matokeo ya ukaguzi nilioufanya mwaka unaoishia tarehe 30 Juni 2020.5.1 MATOKEO YA UKAGUZI WA SERIKALI KUU
5.1.1 Mwenendo wa Deni la Serikali
Deni la Serikali hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2020 lilikuwa Sh. trilioni 56.76 ambapo deni la ndani lilikuwa Sh.trilioni 15.52 na deni la nje ni Sh. trilioni 41.24 ikiwa ni ongezeko la Sh. trilioni 3.65 sawa na asilimia saba ikilinganishwa na deni la Sh. trilioni 53.11 lililoripotiwa Mwaka wa Fedha 2018/19. Ongezeko hilo linajumuisha Sh. bilioni 652 za deni la ndani na Sh. trilioni 3 za deni la nje.Hadi tarehe 30 Juni 2020 deni la serikali lilikuwa linahimilika.
5.1.2 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Kwa mwaka 2019/20, Mamlaka ya Mapato Tanzania ilikusanya Sh. trilioni 17.92 dhidi ya makisio yaliyowekwa ya Sh. trilioni 19.41, hivyo kuwa na upungufu wa makusanyo kwa Sh. trilioni 1.49 sawa na asilimia nane ya jumla ya makisio ya makusanyo.Ndugu Wanahabari,
Mamlaka ya Mapato ilikuwa na changamoto mbalimbali katika ukusanyaji mapato kama ifuatavyo:Bidhaa zinazopita kwenda nchi jirani zenye ushuru wa forodha wenye thamani ya Sh. bilioni 5.14 hazikuthibitishwa kutoka nchini
Katika ukaguzi wangu wa bidhaa zinazopita nchini kuelekea nchi jirani kupitia mipaka ya forodha ya Tunduma, Kasumulu, Rusumo, Kabanga, Mutukula, Namanga, Holili na Kigoma kwa kuangalia mfumo wa TANCIS na nyaraka za kusafirishia sikuthibitisha kuwa bidhaa zenye makadirio ya kodi ya forodha Sh. bilioni 5.14 zilitoka nchini.Mafuta yaliyopitiliza muda wa kukaa nchini ambayo yalipaswa kwenda nchi jirani yenye ushuru wa forodha Sh. bilioni 12.14
Katika mapitio ya mafuta yanayopita nchini kwenda nchi jirani nilibaini yafuatayo:Lita milioni 2.47 za mafuta zenye makadirio ya ushuru wa forodha wa Sh. bilioni 1.97 yalibaki nchini bila kusafirishwa kwenda nchi zilizokusudiwa kwa muda uliopangwa wa siku 30.
Lita milioni 14.08 za mafuta zenye ushuru wa forodha unaokadiriwa kufikia Sh. bilioni 10.43 zilizoshushwa Tanzania Bara kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Zanzibar tangu Julai 2019 hazijaondoshwa kwa muda uliopangwa wa siku 21. Kwa mujibu wa sheria ya forodha, mafuta yanayokaa nchini kwa zaidi ya muda uliopangwa yanapaswa kurasimishwa kwa matumizi ya ndani na hivyo kutozwa ushuru unaotakiwa.
Kodi zilizoshikiliwa na kesi zilizopo katika mamlaka za rufaa za kodi Sh. Trilioni 360 na Dola za marekani milioni 181
Nimebaini kuwa Mamlaka ya mapato imekuwa na kesi 1,097 za muda mrefu katika Mamlaka za Rufaa za Kodi zenye thamani ya Sh. trilioni 360 na dola za Kimarekani milioni 181 kama inavyoonekana katika jedwali hapa chiniKESI ZILIZOKUWEPO KATIKA MAMLAKA ZA RUFAA ZA KODI HADI TAREHE 30 JUNI 2020
Mamlaka za Rufaa za Kodi | Idadi ya Kesi | Kodi zilizoshikiliwa kwenye Mapingamizi | |
| | (Sh.) | (Dola za Marekani) |
Mahakama ya Rufaa | 20 | 176,832,218,835 | 150,137,310 |
Baraza la Rufaa za Kodi | 94 | 2,681,308,049,509 | 23,451,738 |
Bodi ya Rufaa za Kodi | 983 | 357,223,517,421,771 | 7,841,204 |
Jumla | 1097 | 360,081,657,690,120 | 181,430,252 |
Chanzo: Taarifa ya mapato ya Mamlaka 2019/20 na bodi za rufaa 2019/20
Ucheleweshaji wa Utatuzi wa Mapingamizi ya Kodi Sh. Bilioni 38.78
Nilibaini uwepo wa mapingamizi 44 yenye kodi ya thamani ya Sh. bilioni 38.78 katika Idara ya Walipakodi Wakubwa, Idara ya Upelelezi wa kodi na Idara ya kodi za Ndani ambayo hayajatatuliwa kwa muda unaotakiwa kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa huduma na mlipa kodi ya mwaka 2017. Kucheleweshwa kwa utatuzi wa mapingamizi ya kodi kunaathiri malengo ya ukusanyaji wa kodi kwani mapingamizi haya yanafunga kiasi kikubwa cha kodi.Kutokusanywa kwa Ushuru wa Forodha kwa Magari na Bidhaa (mitambo) Zilizoingizwa Nchini kwa Muda ambazo Hazijaondolewa Baada ya Muda Kuisha
Nilibaini magari 936 yaliyoingizwa nchini kwa muda kupitia mipaka ya forodha ya Namanga, Holili, Tarakea, Mtambaswala na Sirari yamebaki nchini kwa zaidi ya muda ulioruhusiwa bila uthibitisho wa maombi ya waingizaji kuongezewa muda.Pia, nilibaini bidhaa (mitambo) zenye thamani ya Sh. bilioni 20.25 na ushuru wa forodha Sh. bilioni 1.24 zilizoingizwa kwa muda nchini kupitia mipaka ya Namanga, KIA, Holili na Bandari kavu hazijaondolewa baada ya kumalizika kwa muda ulioruhusiwa kuwapo nchini, wala hazijarasimishwa kwa matumizi ya ndani kama sheria ya forodha inavyoelekeza.
5.1.3 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Akaunti ya masurufu ya Jeshi la Zimamoto ilitumika kupitishia malipo batili ya Sh. milioni 261.35
Nilibaini Sh. milioni 261.35 ziliwekwa kwenye akaunti ya masurufu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika mojawapo ya benki za biashara kwa vipindi tofauti. Hata hivyo, Menejimenti ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji haikutambua vyanzo vya fedha hizo na hakukuwa na mawasiliano yoyote yaliyofanywa na benki kuhusuiana na mapokezi ya fedha hizo.Pia, nilibaini kuwa, Kiasi hicho cha fedha kilichukuliwa na Mtunza Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka katika akaunti hiyo kwa vipindi tofauti kwa kutumia nyaraka za fedha za kughushi.
Aidha, nilibaini kuwa, usuluhishi wa taarifa za benki kwenye akaunti ya masurufu haukufanywa kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai 2019 hadi tarehe ya kukamilisha ukaguzi. Hii ni kinyume na Kanuni Na. 162 (1) ya Kanuni ya Fedha za Umma ya mwaka 2001 ambayo inahitaji taarifa za fedha za benki zifanyiwe usuluhisho angalau kila mwezi.
Hali Hii inaashiria udhibiti dhaifu wa mifumo ya ndani kwenye usimamizi wa fedha katika akaunti za benki za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
5.1.4 Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA)
Nilibaini kuwa, TGFA ililipa jumla ya Sh. bilioni 3.92 mnamo tarehe 14 Februari na 26 Aprili 2018 ikiwa ni gharama za huduma ya matengenezo makubwa ya ndege aina ya Fokker 28-5H-CCM ya mwaka 1978. Hata hivyo, wakati wa ziara yangu kwenye hifadhi ya ndege za Serikali Dar es Salaam mnamo 19 Agosti 2020, nilibaini kuwa ndege hiyo ilikuwa haifanyi kazi na ilikuwa imetelekezwa tangu mwaka 2015. Aidha, niligundua kuwa, TGFA iliwasilisha suala hili Wizara ya Fedha na Mipango ikiomba ifanyike tathmini ya kina juu ya ndege hiyo ili kuweza kuishauri Serikali juu ya uamuzi sahihi wa hatua za kuchukua.Hata hivyo, ninaona uamuzi wa kuwekeza fedha za walipa kodi zenye thamani ya Sh. bilioni 3.92 kufanya ukarabati mkubwa wa ndege bila kufanya tathmini ya kina ya gharama na faida haukuwa sahihi, na hivyo, kusababisha hasara kwa taifa.
5.1.5 Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Makusanyo ya kivuko ambayo hayajapelekwa benki na hayapo kituoni Sh. 81,194,650
Nilibaini kuwa Kituo cha Kivuko cha Magogoni kilikusanya jumla ya Sh. bilioni 5,757,041,950 ikiwa ni tozo za kivuko kwa kipindi kilichoanzia tarehe 1 Julai 2019 hadi 30 Juni 2020. Hata hivyo, kati ya pesa zilizokusanywa, ni Sh. 5,675,847,300 ndizo zilizowekwa kwenye akaunti ya Benki inayosimamiwa na Makao Makuu ya TEMESA, ikiacha jumla ya kiasi cha Sh. 81,194,650 kikiwa bado hakijawekwa benki hadi muda wa ukaguzi, tarehe 31 Julai 2020. Aidha, nilibaini kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho hakikuwekwa benki pia hakikuwa kwenye himaya ya kituo. Kwa maoni yangu, fedha hizi ambazo hazijawekwa benki kuna uwezekano kwamba zimetumiwa vibaya au kutumiwa katika shughuli zingine.
Mfumo Usio Madhubuti wa Tiketi za Kielektroniki Katika Kituo cha Feri cha Magogoni – Sh. Bilioni 2.594
Nilibaini kuwa TEMESA iliuza jumla ya tiketi 21,447,004 zenye thamani ya Sh. bilioni 5.76. Hata hivyo, ni tiketi 9,122,690 tu zenye thamani ya Sh. bilioni 3.16 ndizo zilizothibitishwa na mashine (scanned) na kuacha jumla ya tiketi 12,324,314 zenye thamani ya Sh. bilioni 2.60 zikitumika bila ya kuthibitishwa na mashine (not scanned).Ni maoni yangu kuwa, tiketi hizo zinaweza kutumika tena na kusababisha serikali kupoteza mapato.
5.1.6 Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Usimamizi Usioridhisha wa Kadi za Kutengenezea Vitambulisho vya Taifa Sh. Bilioni 3.399
Mnamo tarehe 21 Aprili 2011, NIDA iliingia kwenye Mkataba na M/s IRIS Corporation Berhad ya Malaysia (Supplier) kwa ununuzi wa bidhaa na vifaa vya utekelezaji wa mfumo wa Kadi za Taifa kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa gharama ya Dola 149,956,303. Muda wa mkataba uliisha tokea tarehe 14 Machi 2018 (miaka mitatu nyuma) bila ya kuongezwa kwa muda.Ukaguzi wangu wa mkataba huu umebaini kuwa kulikuwa na makubaliano ya kusambaza kadi 25,000,000 mpaka kipindi cha Ukaguzi, Novemba 2020, nilibaini kwamba msambazaji aliwasilisha kadi 13,735,728 tu. Aidha, uchambuzi wangu ulibaini kwamba, kati ya kadi zilizowasilishwa, NIDA imetumia kadi 6,180,015 kutengeneza vitambulisho vya taifa na kubakiza kadi 5,084,257 zikiwa hazijatumika.
Hata hivyo, nimebaini kuwa kati ya kadi 5,084,257 zilizobakia, ni kadi 4,657,500 tu ndizo zilikuwa zimehifadhiwa kwenye bohari, huku kadi 426,757 zenye thamani ya Sh. 3,399,973,019[1] zikiwa zimeharibika na hazifai kwenye matumizi ya kutengeneza vitambulisho vya taifa. Licha ya menejimenti ya NIDA kueleza kuwa imetuma barua kwenda kwa mkandarasi (IRIS) ili afanye usuluhisho wa kadi zilizoonekana na matatizo na kubadilisha na kadi mpya ni maoni yangu kuwa kuna hatari ya NIDA kupata hasara ikiwa IRIS atashindwa kubadilisha kadi hizo ambazo hazifai kutokana na kukosekana kwa mkataba halali kati ya NIDA na M/s IRIS Corporation Berhad.
5.1.7 Wakala wa Umeme Vijijini (REA)
Nguzo za Umeme Zenye Kasoro Zilizowekwa Mkoani Lindi Sh. Bilioni 1.07
Mnamo tarehe 17 Julai 2017, REA iliingia mkataba wenye namba: AE/008/2016-17/HQ/G/09-Lot 4 na M/s State Grid Electrical & Technical Work Ltd kwa ajili ya kuweka umeme vijijini katika mkoa wa Lindi (awamu ya III) kwa bei ya kandarasi ya Sh. 20,878,061,665.12 na Dola za marekani 4,794,467.15 (ikijumuisha kodi ya ongezeko la Thamani). Muda wa kuisha kwa mkataba ulikuwa tarehe 25 Juni 2020 lakini uliongezwa mpaka tarehe 31 Desemba 2020.Kwenye ukaguzi wa mkataba huu, nilibaini kuwa mkandarasi aliweka nguzo za umeme 6,541 zenye thamani ya Sh. 2,965,562,433.33 katika mkoa wa
Lindi. Hata hivyo, wakati wa kutembelea mradi mnamo Oktoba 2020 niliona
kwamba kati ya nguzo zilizowekwa, nguzo za umeme 2,612 (40%) zenye thamani ya Sh. 1,065,696,000 zilikuwa na nyufa. Mbali na hivyo, mkandarasi hakuwa amebadilisha nguzo hizo zenye kasoro. Hii ni kinyume na Kifungu 23.6 cha GCC kinachomtaka mkandarasi kusahihisha au kubadilisha bidhaa au sehemu ya vifaa ikiwa bidhaa hizo au vifaa vimeshindwa kufaulu jaribio au ukaguzi.
5.1.8 Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali
Kutokutumiwa kwa Fedha Zinazotokana na Mali Zilizotaifishwa na Kurejeshwa Serikalini - Sh. Bilioni 51.521
Nilipitia uendeshwaji wa Akaunti ya fedha zinazotokana na mali zilizotaifishwa na kurejeshwa Serikalini zilizo chini ya Mkurugenzi wa Mashtaka hadi kufikia tarehe 30 Juni 2020. Nilibaini kuwapo kwa bakaa ya fedha Sh. bilioni 51.521 kutokana na kesi zilizomalizika katika mahakama mbalimbali kwa kipindi cha miaka 6 na zaidi kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini.BAKAA YA FEDHA ZILIZO KATIKA AKAUNTI YA FEDHA ZA MALI ZILIZOTAIFISHWA NA KUREJESHWA SERIKALINI
Namba ya Akaunti | Jina la Akaunti | Bakaa hadi kufikia tarehe 30 Juni 2020 |
9921161271 | Akaunti ya Fedha za Mali zilizo taifishwa na kurejeshwa serikalini | 15,264,026,469.22 |
9921169817 | Mkurugenzi wa Mashtaka | 18,567,255,515.53 |
9931209531 | Akaunti ya Fedha za Mali zilizo taifishwa na kurejeshwa serikalini Dola za Marekani 7,741,633.92 @Sh 2,285.0891 kwa kiwango cha kubadilisha fedha tarehe 30 Juni 2020 | 17,690,323,286.78 |
Jumla | 51,521,605,271.53 |
Kutotumiwa kwa bakaa ya fedha katika akaunti kunasababishwa na kutokuwapo kwa sheria na kanuni za kudhibiti matumizi ya fedha itokanayo na mali zilizotaifishwa na kurejeshwa serikalini.
Ni maoni yangu kuwa, kuwapo wa fedha zisizotumiwa kwa sababu ya kukosekana kwa Muongozo au mfumo wa kisheria kunaweza kusababisha matumizi mabaya ya Fedha za umma na ucheleweshaji wa maendeleo ya umma.
5.1.9 Masuala Mtambuka
Kutorejeshwa kwa Fedha Zilizokopwa na Wizara Sh. Bilioni 4.083
Nilibaini kuwa wizara mbali mbali zilikopa jumla ya Sh. bilioni 4.083 kutoka mifuko maalumu mitatu bila ya kurudisha kiasi hicho kama ilivyoelezewa kwenye Jedwali hapa chini.FEDHA ZILIZOKOPWA NA WIZARA
Na. | Jina la Mfuko | Kiasi kilichokopwa (Sh.) | Taasisi iliyokopeshwa |
1 | Mfuko wa Uwezeshaji wa Maendeleo ya Madini (EMDF) | 521,831,816.56 | Wizara ya Madini |
2 | Akaunti ya Mfuko wa Barabara-TAMISEMI | 3,442,788,003.52 | OR - TAMISEMI |
3 | Mfuko wa Maji Taifa Wizara ya Maji | 119,293,355.00 | Wizara ya Maji |
Jumla | 4,083,913,175.08 |
Ni maoni yangu kwamba, kutokurudishwa kwa fedha zilizokopwa na Wizara kunaathiri utekelezaji wa shughuli za Mifuko Maalumu, hivyo fedha hizo zirejeshwe ili kutekeleza shughuli zilizopangiwa.
Malipo Yenye Nyaraka Pungufu – Sh Bilioni 13.061
Katika ukaguzi wa mwaka huu, nimebaini malipo yenye thamani ya Sh. bilioni 13.061 ambayo hayakuwa na nyaraka za kujitosheleza kinyume na Kanuni 95 (4) ya Kanuni za Fedha za Umma, 2001 kama inavyoonyeshwa kwenye Jedwali hapa chini.Taasisi zenye malipo yenye nyaraka pungufu
Na. | Taasisi | Kiasi (Sh.) |
1. | Wakala Wa Huduma Za Misitu Tanzania (TFS) | 200,061,021 |
2. | Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) | 451,457,684 |
3. | Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza | 530,446,323 |
4. | Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) | 87,738,385 |
5. | Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) | 46,083,900 |
6. | Shirika la Mzinga | 3,584,216,021 |
7. | Hospitali ya Rufaa ya MkoaTemeke | 172,156,483 |
8. | Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) | 101,242,748 |
9. | Wakala Wa Barabara Za Vijijini Na Mijini (TARURA) | 72,860,000 |
10. | Kituo cha Mafunzo ya Takwimu cha Afrika Mashariki (EASTC) | 98,097,349 |
11. | Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma | 257,424,600 |
Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora | 139,210,000 | |
12. | Jeshi la Zimamoto na Uokozi – Fungu Na. 14 | 1,766,605,227 |
13. | Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali – Fungu Na. 16 | 74,719,150 |
14. | Tume ya Taifa katika Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) – Fungu Na. 18 | 138,003,604 |
15. | Jeshi la Wananchi wa Tanzania – Fungu Na. 38 | 605,695,511 |
16. | Wizara ya Mambo ya Ndani – Fungu Na. 51 | 36,495,728 |
17. | Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Fungu Na. 53 | 143,564,642 |
18. | Idara ya Huduma za Uhamiaji – Fungu Na. 93 | 11,200,000 |
19. | Ikulu - Fungu Na. 20 | 46,548,534 |
20. | Msajili wa Vyama vya Siasa – Fungu Na. 27 | 7,823,000 |
21. | Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki – Fungu Na. 34 | 97,087,278 |
22. | Wizara ya Katiba na Sheria – Fungu Na. 41 | 61,050,292 |
23. | Tume ya Taifa ya Uchaguzi – Fungu Na. 61 | 1,545,034,285 |
24. | Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu – Fungu Na. 65 | 6,735,600 |
25. | Sekretarieti ya Mkoa Geita | 15,323,383 |
26. | Sekretarieti ya Mkoa Kagera | 36,903,658 |
27. | Sekretarieti ya Mkoa Mara | 18,650,000 |
28. | Sekretarieti ya Mkoa Simiyu | 20,000,000 |
29. | Sekretarieti ya Mkoa Iringa | 5,315,441 |
30. | Sekretarieti ya Mkoa Katavi | 5,651,088 |
31. | Sekretarieti ya Mkoa Rukwa | 21,756,360 |
32. | Sekretarieti ya Mkoa Ruvuma | 5,327,000 |
33. | Sekretarieti ya Mkoa Mbeya | 32,487,500 |
34. | Sekretarieti ya Mkoa Geita | 1,652,898,617 |
35. | Ofisi ya Rais ya Usimamizi wa Nyaraka na Utunzaji wa Kumbukumbu – Fungu Na. 04 | 6,000,000 |
36. | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia - Fungu Na. 46 | 29,175,569 |
37. | Tume ya Kuzuia UKIMWI - Fungu Na. 92 | 15,538,680 |
38. | Sekretarieti ya Mkoa Mara | 18,650,000 |
39. | Sekretarieti ya Mkoa Mwanza | 22,062,858 |
40. | Sekretarieti ya Mkoa Dar es Salaam | 213,011,595 |
41. | Sekretarieti ya Mkoa Mtwara | 15,000,000 |
42. | Sekretarieti ya Mkoa Lindi | 5,580,000 |
43. | Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – Fungu Na. 48 | 424,757,390 |
44. | Sekretarieti ya Mkoa Tanga | 4,737,000 |
45. | Sekretarieti ya Mkoa Shinyanga | 86,362,063 |
46. | Tume ya Taifa ya mipango na matumizi ya Ardhi – Fungu Na. 3 | 5,110,000 |
47. | Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – Fungu Na. 56 | 119,275,653 |
Jumla | 13,061,131,220 |
Chanzo: Barua ya mapungufu kwa menejimenti
Ni maoni yangu kuwa chanzo cha kuwa na matumizi yenye nyaraka pungufu ni kuwa na mfumo dhaifu wa udhibiti na Maafisa Masuuli kushindwa kuchukua hatua stahiki kwa maafisa wanaosababisha udhaifu huu. Ninaamini kuwa hii inaweza kuwa ishara ya kufanyika kwa matumizi ya udanganyifu na mabaya. Mawanda yangu ya Ukaguzi yalizuiwa hivyo sikuweza kuthibitisha uhalali wa malipo yaliyofanyika.
[1] Gharama ya kila kadi ni Dola za Marekani 3.452 sawa na Sh. 7,967 kwa kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni cha BOT mnamo tarehe 30 June 2020; hivyobasi, kadi 426,757 mara Sh. 7,967 ni sawasawa na Sh. 3,399,973,019