Ripoti ya Ukaguzi wa CAG kwa Mwaka 2022/23 kutua kwa Rais wiki hii

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
161
619
MKUTANO wa Bunge la Bajeti umepangwa kufanyika kuanzia Jumanne ya juma lijalo. Pamoja na mambo mengine, ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka 2022/23 itawasilishwa kwa mujibu wa sheria.

Ibara ya 143 ya Katiba ya nchi (1977), inaelekeza CAG kuwasilisha kwa Rais taarifa yake ya ukaguzi.

Katiba hiyo inaelekeza pia kitika kifungu hicho kuwa, baada ya kupokea taarifa hiyo Rais atawaagiza watu wanaohusika wawasilishe taarifa hiyo kwenye kikao cha kwanza cha Bunge kitakachofanyika baada ya Rais kupokea taarifa hiyo na itabidi iwasilishwe katika kikao hicho kabla ya kupita siku saba tangu siku ile kilipoanza kikao hicho.

Kwa kuzingatia, Ijumaa itakuwa sikukuu, ripoti ya CAG itawasilishwa kwa Rais kati ya leo na Alhamisi ya juma hili ili kukidhi maelekezo ya kikatiba.

CAG amekuwa akiandaa ripoti za ukaguzi wa mwaka zikijumuisha Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Kuu; Ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa; Ukaguzi wa Hesabu za Mashirika ya Umma, Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo na Ukaguzi wa Ufanisi. Pia amekuwa akiandaa ripoti za Ukaguzi Maalum.

Ripoti ya mwaka 2022/23, kama ilivyokuwa katika ripoti zilizopita, inatarajiwa kugusia ukusanyaji wa kodi kutoka vyanzo mbalimbali, uandaaji na utekelezaji bajeti ya serikali, hali ya Deni la Serikali, usimamizi wa rasilimali watu, usimamizi wa mali na madeni ya serikali pamoja na usimamizi na uendeshaji wa taasisi za umma.

Baada ya kuwasilishwa bungeni na mawaziri husika, Ripoti ya CAG itakabidhiwa kwa kamati za Bunge zenye mamlaka ya kuifanyia uchambuzi.

Miongoni mwa yanayotarajiwa kuwa gumzo katika ripoti ya CAG ni madai ya kuwapo ufujaji wa fedha za umma unaodaiwa kufanywa na maofisa wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI wakishirikiana na watendaji wa serikali, pia upigaji wa fedha miradi inayosimamiwa na taasisi na mashirika ya umma na 'mchwa' wa fedha za maendeleo katika halmashauri mbalimbali hasa mikoa yenye miradi mikubwa.

Hoja nyingine ni kukua kwa kasi kwa Deni la Serikali na utendaji usioridhisha wa kujiendesha kwa hasara ya mabilioni, hali ya miundombinu ya sekta za elimu na maji, pia majibu ya serikali kuhusu hoja zilizopita, zikiwamo malipo ya mamilioni ya shilingi kutunza vyura Marekani na hujuma katika ghala la pembe za ndovu jijini Dar es Salaam.

Vilevile, Ripoti ya CAG inatarajiwa kuangazia hali ya mifuko ya hifadhi ya jamii na uwiano wa kazi na watumishi waliopo, hasa katika sekta za elimu na afya.

Nipashe
 
Hazina tija kwasabb Sa100 hana maamuzi...ataishia tu kusema 'stupid, watupishe'...halafu baasi, itaishia hapo!.
 
Back
Top Bottom