Ramadhan Special Thread

183, Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.

184. (Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua.
 
SWALI :

Asalaam alaykum.

Napenda kuuliza suala langu kuhusu Ramadhan "Nimeamka usiku na kula daku mapema, lakini nikaamka usiku na kuendelea na ibada, nilipokuwa nikiendelea na ibada, mara kiu ikanishika na nikanywa maji, lakini kwa bahati nikasikia adhana ya pili ya sala ya alfajiri, wakati huu, yale maji nusu yamekwenda na nusu yamo mdomoni, nikaendelea kuyanywa yale yaliyo mdomoni wakati huu adhana hiyo ya pili inaendelea kusomwa. JEE HUKUMU YANGU NINI KUHUSU USAHIHI WA FUNGA YANGU

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

“…Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku...” Al-Baqarah: 187

Ni waajib kwa mwenye kufunga ajizuie kula au kunywa pale panapoingia Alfajiri ya kweli, kwa hali ya leo hii wengi wanajua alfajiri ya kweli kwa sauti ya Adhaan ya pili japo hiyo inaweza isiwe ni kipimo sahihi mia kwa mia kwani Misikiti mingi huadhiniwa kwa kutazamwa saa na si kwa kutazamwa weupe wa alfajiri ya kweli kama ushadhihirika au la.

Swawm yako inaweza kuwa ni sahihi kutokana na kutokujua kwako hukumu ya jambo hilo.

Hadiyth ifuatayo inatuonyesha kuwa mtu anaruhusiwa kumaliza tonge au chakula chake alichoonza kula wakati Adhaan inapoadhiniwa:

Imesimuliwa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):“Atakaposikia mmoja wenu Adhaan na hali ana chombo cha chakula mkononi mwake, asikishushe chini hadi amalize kilichomo”[Ahmad, Abu Daawuud, na Shaykh Al-Albaaniy kaitaja katika Swahiyh ya Abu Daawuud].

Hata hivyo, Hadiyth hii isichukuliwe moja kwa moja kuwa mtu anaweza kuendelea kula na hali ishaingia Alfajiri ya kweli. Kwani kuna makatazo ya wazi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:

“Msisimamishe daku yenu mnaposikia Adhaan ya Bilaal, kwani yeye anaadhini usiku, kwa hiyo kuleni na kunyweni mpaka Ibn Umm Maktuum aadhini.” Al-Bukhaariy

Kwa hali yako muulizaji, ni bora uwe makini kutokula tena baada ya Adhaan ya pili ambayo huwa ndio kipimo cha Alfajiri ya kweli, na kwa sababu ulikuwa hujui hukumu hapo mwanzo, basi tunataraji Swawm yako itakuwa sahihi inshaAllaah.

Lakini ni vizuri Muislamu kuchukua tahadhari ya kujua muda gani khaswa Adhaan ya kwanza na muda gani ni Adhaan ya pili ili asalimike na matukio kama haya. Hakika ni dakika chache tu mtu unaweza kujiweka katika usalama wa kula daku
 
Mwezi wa Ramadan unaagiza watu kufanya mema mambo mazuri yanayo mpendeza Mungu ivyo kwa kuwa Mungu wetu ni Baba wa mambo mema basi hata sisi wa kristo tuna heshimu mwezi huu wa Ramadhan kwa kutenda mambo mema
Mfano mm mwezi huu wote natulia kwa kutenda mambo mema na kuacha mambo maovu kama zinaa na mengine
By Pastor Askari Muoga
 
☪ ((1⃣))

MAFUNZO MAALUM
*RAMADHANI KARIM*

☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆
MAANA YA
*RAMADHAN*
{{1 }}
☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆☆

Ramadhani *(رَمَضَانُ)*
ni neno la kiarabu latokana na neno la asli lenye harfu 3 za asili ( mujarrad), nalo ni ramadha
(َرَمَض) .

✍Neno *Ramadhan* limetajwa katika Qur-ani; Surat Baqarah; Aya 185 aliposema Allah Taalaa:~

*" شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ "*

" Mwezi wa Ramadhan ambao umeteremshwa ndani yake (katika laylatu qadri) Qur'an."

Na hakuna mwezi uliotajwa kwa jina lake ila mwezi huu kwa utukufu mkubwa uliopo ndani yake na fadhila zake.

✍ wametofautiana maulamaa neno la (Ramadhan) nini hassa maana yake

Ufupisho wake ni kama hivi::-

1⃣ - Amesema *Alkhalili* kuwa maana yake ni mvua; Huja kusafisha katika ardhi na mavumbi.., yaani mwezi huu ukija husafisha miili ya binaadamu na maovu

2⃣- Na wako waliosema kuwa Ramadha ni jiwe lilokuwa moto sanaa baada ya kupigwa na juwa kisawa sawa

3⃣ - Na wako waliosema kuwa Ramadha ni unguzaji uliomkali .. Yaani kumainisha kuwa mwezi huu unaunguza madhambi ya waja wake Allah

4⃣ - *Amesema Mujaahid*kuwa Ramadha ni jina katika
Majina yake Allah

☪ Kwa ufupi Ramadhani inamainisha kuwa:~

*kusafisha,*
*kufuta*
*kuunguza*
*kutoharisha kila*
kichafu kiovu katika
mwili na roho

وَاللّٰهُ أَعْلَمُ

*"RAMADHANI KARIM* "

____________________

((1⃣))
 
السؤال Swali

ما حكم الصوم مع ترك الصلاة في رمضان؟
Nini hukumu ya funga ya mtu asiyeswali?

فأجاب الشيخ بن عثيمين رحمه الله:
Akajibu Shekh Bin Uthaimin Allah amrehem

إن الذي يصوم ولا يصلي لا ينفعه صيامه Hakika yule ambaye anafunga na wala haswali hainufaishi funga
yake

ولا يُقْبَل منه ولا تبرَأ به ذمَّته.
Wala haikubaliki kwake hiyo funga na wala haimuondoi yeye kwenye dhima ya kutekeleza hiyo funga(anahesabika kuwa hajafunga)

بل إنه ليس مطالباً به مادام لا يصلي؛
Bali hakika ya hiyo funga yake haihitajiki maadam haswai

لأن الذي لا يصلي مثل اليهودي والنصراني،
Kwasababu asiyeswali ni mfano wa Myahudi na Mnaswara

فما رأيكم أن يهوديًّا أو نصرانيًّا صام وهو على دينه، فهل يقبل منه؟
Mnaonaje iwapo Myahudi au Mnaswara akifunga na hali yuko kwenye dini yake, Je atakubaliwa funga yake?

لا. إذن نقول لهذا الشخص:
Hapana, haiwezi kukubaliwa, kwahiyo tunasema kumwambia huyu mtu:

تب إلى الله بالصلاة وصم،
Tubia kwa Allah, kwa kuswali na kufunga.

ومَن تاب تاب الله عليه.
Na atakayetubu, Allaah atamkubalia toba yake

والله{سبحنه وتعلا} اعلم.
 
SWALI :

Asalaam alaykum.

Napenda kuuliza suala langu kuhusu Ramadhan "Nimeamka usiku na kula daku mapema, lakini nikaamka usiku na kuendelea na ibada, nilipokuwa nikiendelea na ibada, mara kiu ikanishika na nikanywa maji, lakini kwa bahati nikasikia adhana ya pili ya sala ya alfajiri, wakati huu, yale maji nusu yamekwenda na nusu yamo mdomoni, nikaendelea kuyanywa yale yaliyo mdomoni wakati huu adhana hiyo ya pili inaendelea kusomwa. JEE HUKUMU YANGU NINI KUHUSU USAHIHI WA FUNGA YANGU

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

“…Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku...” Al-Baqarah: 187

Ni waajib kwa mwenye kufunga ajizuie kula au kunywa pale panapoingia Alfajiri ya kweli, kwa hali ya leo hii wengi wanajua alfajiri ya kweli kwa sauti ya Adhaan ya pili japo hiyo inaweza isiwe ni kipimo sahihi mia kwa mia kwani Misikiti mingi huadhiniwa kwa kutazamwa saa na si kwa kutazamwa weupe wa alfajiri ya kweli kama ushadhihirika au la.

Swawm yako inaweza kuwa ni sahihi kutokana na kutokujua kwako hukumu ya jambo hilo.

Hadiyth ifuatayo inatuonyesha kuwa mtu anaruhusiwa kumaliza tonge au chakula chake alichoonza kula wakati Adhaan inapoadhiniwa:

Imesimuliwa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):“Atakaposikia mmoja wenu Adhaan na hali ana chombo cha chakula mkononi mwake, asikishushe chini hadi amalize kilichomo”[Ahmad, Abu Daawuud, na Shaykh Al-Albaaniy kaitaja katika Swahiyh ya Abu Daawuud].

Hata hivyo, Hadiyth hii isichukuliwe moja kwa moja kuwa mtu anaweza kuendelea kula na hali ishaingia Alfajiri ya kweli. Kwani kuna makatazo ya wazi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:

“Msisimamishe daku yenu mnaposikia Adhaan ya Bilaal, kwani yeye anaadhini usiku, kwa hiyo kuleni na kunyweni mpaka Ibn Umm Maktuum aadhini.” Al-Bukhaariy

Kwa hali yako muulizaji, ni bora uwe makini kutokula tena baada ya Adhaan ya pili ambayo huwa ndio kipimo cha Alfajiri ya kweli, na kwa sababu ulikuwa hujui hukumu hapo mwanzo, basi tunataraji Swawm yako itakuwa sahihi inshaAllaah.

Lakini ni vizuri Muislamu kuchukua tahadhari ya kujua muda gani khaswa Adhaan ya kwanza na muda gani ni Adhaan ya pili ili asalimike na matukio kama haya. Hakika ni dakika chache tu mtu unaweza kujiweka katika usalama wa kula daku
JazakAllah khayr
 
Mwezi wa Ramadan unaagiza watu kufanya mema mambo mazuri yanayo mpendeza Mungu ivyo kwa kuwa Mungu wetu ni Baba wa mambo mema basi hata sisi wa kristo tuna heshimu mwezi huu wa Ramadhan kwa kutenda mambo mema
Mfano mm mwezi huu wote natulia kwa kutenda mambo mema na kuacha mambo maovu kama zinaa na mengine
By Pastor Askari Muoga
shukrani mkuu
Mungu akujalie hayo mema uendelee nayo kwani dunia tunapita
Tunakutakia amani upendo na baraka tele wewe na familia yako!
.
 
السؤال Swali

ما حكم الصوم مع ترك الصلاة في رمضان؟
Nini hukumu ya funga ya mtu asiyeswali?

فأجاب الشيخ بن عثيمين رحمه الله:
Akajibu Shekh Bin Uthaimin Allah amrehem

إن الذي يصوم ولا يصلي لا ينفعه صيامه Hakika yule ambaye anafunga na wala haswali hainufaishi funga
yake

ولا يُقْبَل منه ولا تبرَأ به ذمَّته.
Wala haikubaliki kwake hiyo funga na wala haimuondoi yeye kwenye dhima ya kutekeleza hiyo funga(anahesabika kuwa hajafunga)

بل إنه ليس مطالباً به مادام لا يصلي؛
Bali hakika ya hiyo funga yake haihitajiki maadam haswai

لأن الذي لا يصلي مثل اليهودي والنصراني،
Kwasababu asiyeswali ni mfano wa Myahudi na Mnaswara

فما رأيكم أن يهوديًّا أو نصرانيًّا صام وهو على دينه، فهل يقبل منه؟
Mnaonaje iwapo Myahudi au Mnaswara akifunga na hali yuko kwenye dini yake, Je atakubaliwa funga yake?

لا. إذن نقول لهذا الشخص:
Hapana, haiwezi kukubaliwa, kwahiyo tunasema kumwambia huyu mtu:

تب إلى الله بالصلاة وصم،
Tubia kwa Allah, kwa kuswali na kufunga.

ومَن تاب تاب الله عليه.
Na atakayetubu, Allaah atamkubalia toba yake

والله{سبحنه وتعلا} اعلم.
Swadakta mkuu
Ibada ya swala imekuwa mtihani mkubwa katika familia zetu
Waislamu tuna dhima kubwa mbele ya M/Mungu (s.w) kuziangalia na kuwasaidia ndugu zetu
Tushikamane na swala 5 ndugu zangu na tusichoke kukumbushana juu hili
 
emoji287.png
emoji294.png
emoji287.png
emoji294.png

masharti ya swalah

Masharti ya swalah ni tisa:

Sharti ya kwanza: Uislamu.

Sharti ya pili: Mtu kuwa na akili.

Sharti ya tatu: Uwezo wa kupambanua.

Sharti ya nne: Kuondosha hadathi.

Sharti ya tano: Kuondosha najisi.

Sharti ya sita: Kufunika zile sehemu zisizotakiwa kuonekana (´Awrah).

Sharti ya saba: Kuingia kwa wakati.

Sharti ya nane: Kuelekea Qiblah.

Sharti ya tisa: Kunuia.

Mwandishi: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Chanzo: Duruus-ul-Muhimmah li ´Aammah al-Ummah, uk. 12
Tarjama: Wanachuoni.com

nguzo za swalah

Nguzo za swalah ni kumi na nne:

Nguzo ya kwanza: Kusimama kwa mwenye kuweza.

Nguzo ya pili: Kusema "Allaahu Akabr".

Nguzo ya tatu: Kusoma Suurah "al-Faatihah."

Nguzo ya nne: Kurukuu.

Nguzo ya tano: Kuinuka kwenye Rukuu´.

Nguzo ya sita: Kusujudu juu ya viungo saba.

Nguzo ya saba: Kutoka hapo.

Nguzo ya nane: Kukaa baina ya Sajdah mbili.

Nguzo ya tisa: Kuwa na utulivu katika nguzo zote.

Nguzo ya kumi: Kuzipangilia.

Nguzo ya kumi na moja: Tashahhud ya mwisho.

Nguzo ya kumi na mbili: Kukaa katika [Tashahhud] hiyo.

Nguzo ya kumi na tatu: Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Nguzo ya kumi na nne: Kuleta Tasliym mbili.

Mwandishi: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Chanzo: Duruus-ul-Muhimmah li ´Aammah al-Ummah, uk. 13
Tarjama: Wanachuoni.com

mambo ya wajibu ya swalah

Mambo ya wajibu ya swalah ya ni manane:

La kwanza: Kusema "Allaahu Akbar" mbali na ile ya kwanza.

La pili: Kusema "Sami´ Allaahu li man hamidah" kwa imamu na anayeswali peke yake.

La tatu: Kusema "Rabbanaa wa lak al-Hamd". Inasemwa na wote.

La nne: Kusema "Subhaana Rabbiy al-´Adhwiym" katika Rukuu´.

La tano: Kusema "Subhaana Rabbiy´ al-A´laa" katika Sujuud.

La sita: Kusema "Rabb Ighfir liy" kati ya Sajdah mbili.

La saba na la nane: Tashahhud ya kwanza na kukaa kwayo.

Mwandishi: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Chanzo: Duruus-ul-Muhimmah li ´Aammah al-Ummah, uk. 13-14

Tarjama: Wanachuoni.com
 
Asalaam Aleykum Ndugu zangu!

Napenda kuwakumbusha hasa dada zangu kuhusu suala la mavazi, kwa kweli walinena kweli walionena kuwa''ukimuelimisha mwanamke umeelimisha jamii''

Mungu anawataka mjihifadhi
''Na waambie waislamu wanawake wainamishe macho yao,wazilinde tupu zao.wala wasidhihirishe viungo vyao ila vile vinavyodhirika.Na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao,na wasionyeshe mapambo yao ila kwa waume zao……….(Q.24:31)

''Ewe Mtume waambie wake zako,na binti zako na wanawake wa kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao.Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane (ni watu wa heshima) wasiudhiwe. Na M/Mungu ni mwingi wa kusamehe mwingi wa kurehemu. (Q,33:59)

Jamii imeharibika kwenye video za muziki, mabararani maofisini vyuoni kwa kweli dada zetu mavazi mengine wanavaa hadi unajiuliza kama kweli wana wazazi!!Hawana aibu
Mtume (sa.w) anasema ''aibu ni katika mafungu ya imani"

Na sisi wanaume ambao tunaziona familia zetu, wake zetu na watoto wanaharibika yatakiwa tuwe wakali na tujaribu kuwaelimisha ama tutakuja kuulizw siku ya kiyama

DADA ZANGU AMKENI HATA KAMA NI UFUKARA JITAHIDINI MJIHIFADHI NA MUNGU ATALETA REHEMA ZAKE,HAKUNA BINADAMU ALIEMTEGEMEA MUNGU KWA DHATI MWISHO AKAJUTA. SIO KATIKA RAMADHANI TU MJITAHIDI MIEZI YOTE KUVAA KWA STAHA
hijab-4-1.gif
2018987676.jpg
8f9feb0f3f7f16e12a4cb2637c62e907.jpg
08f2422b6796056f36e18ef114b4af6f.jpg

Na miongoni mwa masharti ya hijaab ni kuwa vazi lisiwe lenye kujifadhirisha na kubana
Dada yang usivae hijaab kama pambo, vaa hijaab kwa ajili ya kujistiri na kumuogopa Mungu (s.w)
kwa baraka ya Ramadhani hii Mungu atuongoze katika kheri InshaAllah
 
Wajamvi habarini
Kifupi nmejitahid kupigana na hii hali kwa muda mrefu sasa lakini kwa neema za mungu nauona huu mwezi nataka niache kabisa uzinzi na punyeto
Mungu nisaidie
Allah haibadilishi nafsi ya mja mpaka wewe mwenyewe uibadilishe nafsi yako..
Na njia ilio bora ya kuacha uzinzi ni kuoa.
Tafuta mke upate pa kukatia matamanio yako.
Allah akufanyie wepesi ndugu yangu.
 
Hakika Allah ni mjuzi sana, katufanyia wepesi hadi Qur'an tunatembea nayo mfukoni ama mkononi, hata ukiwa ofisini kwako umetulia waweza isoma Qur'an kiwepesi kabisa, high level of science and technology.

Ramadhan Kareem.
 
SADAKA

A.aleykum

Alhamdulillah natanguliza shukrani kwa ALLAH mtukufu wa daraja na kumtakia ziada ya Rehma Mtume wetu Muhammad (S.A.W) pamoja na maswahaba zake. Naam tumeingia kwenye masiku yenye kuhesabika tunatarajia kuwa na siku 29 au 30. Ni vyema kuyatumia masiku haya machache kwa kukithirisha ibada mbali mbali. jambo lisilo shaka ni kwamba tumetenda maovu mengi katika kipindi cha miezi 11 iliyopita M/Mungu ametupa fursa ambayo wenzetu hawakupewa japokuwa waliitaka kwa hamu kubwa.

Ni muda wa kutubia madhambi yetu na kuweka mkataba kwa-kuto kuyarejea yale maovu tuliyo yatenda huko nyuma. Hii ni fursa adhiim kuendelea kuwa hai ndani ya mwezi mtukufu wa [HASHTAG]#Ramadhan[/HASHTAG]. Wakti tulio nao ni wakati mbaya kutokana na wingi wa vichocheo vitokanavyo na utandawazi. Basi kwa kulitambua hilo ni vyema tukaongeza bidii ya kupambana na bilisi alie laaniwa.

Kwa hakika itakuwa khasara kubwa ikiwa Ramadhan itapita bila ya kupata faida hizi
RAHMA
MAGHFIRA
KUACHWA HURU NA MOTO.

Si ajabu kuanzia leo tukaanza kuitwa waja wema hata kama huko nyuma tulitenda makosa In sha ALLAH tuitumie Ramadhani hii kuwa ndio ufunguo wa kutupeleka Peponi.

Kina mama na dada wenzangu sisi ni nguzo ya maadili mema katika jamii

Kumekuwa na kawaida kwa dada wenzangu kupost picha zao katika hali tofauti bila kisisi na ndipo hapo panapo anza vishawishi. Wengi wao huweka picha zao hali ya kwamba wapo UCHI. Bahati mbaya sana 'baadhi yao' wamekuwa wakiweka picha hizo huku zikiambatana na ujumbe wenye viashiria vya KIBRI, baadhi ya Jumbe hizo "picha ni zangu kwa raha zangu wewe zinakuhusu nini?" "Mimi sio mwanao wewe kinakuuma nini?" Na mengi mengine maneno ya jeuri ambayo huonesha kuwa mimi sina khofu.

Ukumbusho wangu kwenu enyi mama,ndugu na watoto wetu ni kwamba kama tujuwavyo kuwa kuna SADAKA/THAWABU zenye kuendelea pia tusisahau kuna DHAMBI zenye kuendelea. Chukulia mfano moja katika mapicha yako ambao umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii upo nywele wazi, kifua wazi na kwapa nje endapo Allah ameichukua amana yake umeenda mbele ya haki huku nyuma picha hizi ndio utambulisho wako kwa wale wasio kujua utakuwa upo katika hali gani? Hii ni dhambi yenye kuendelea tuiepuke.

Allah tuoneshe HAKI tuifate na tuikamate. Allah tuoneshe BATILI tuiwache na tuiepuke.

[HASHTAG]#RamadhanKareem[/HASHTAG]
 
Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    32.5 KB · Views: 61
Back
Top Bottom