Mkuu hazina maana yeyoteUle mwezi kwneye misikiti huwakilisha nn?
Mkuu ukipata mda, endelea kutuletea zaidi hizi mada za swala
masharti ya swalah
Masharti ya swalah ni tisa:
Sharti ya kwanza: Uislamu.
Sharti ya pili: Mtu kuwa na akili.
Sharti ya tatu: Uwezo wa kupambanua.
Sharti ya nne: Kuondosha hadathi.
Sharti ya tano: Kuondosha najisi.
Sharti ya sita: Kufunika zile sehemu zisizotakiwa kuonekana (´Awrah).
Sharti ya saba: Kuingia kwa wakati.
Sharti ya nane: Kuelekea Qiblah.
Sharti ya tisa: Kunuia.
Mwandishi: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Chanzo: Duruus-ul-Muhimmah li ´Aammah al-Ummah, uk. 12
Tarjama: Wanachuoni.com
nguzo za swalah
Nguzo za swalah ni kumi na nne:
Nguzo ya kwanza: Kusimama kwa mwenye kuweza.
Nguzo ya pili: Kusema "Allaahu Akabr".
Nguzo ya tatu: Kusoma Suurah "al-Faatihah."
Nguzo ya nne: Kurukuu.
Nguzo ya tano: Kuinuka kwenye Rukuu´.
Nguzo ya sita: Kusujudu juu ya viungo saba.
Nguzo ya saba: Kutoka hapo.
Nguzo ya nane: Kukaa baina ya Sajdah mbili.
Nguzo ya tisa: Kuwa na utulivu katika nguzo zote.
Nguzo ya kumi: Kuzipangilia.
Nguzo ya kumi na moja: Tashahhud ya mwisho.
Nguzo ya kumi na mbili: Kukaa katika [Tashahhud] hiyo.
Nguzo ya kumi na tatu: Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Nguzo ya kumi na nne: Kuleta Tasliym mbili.
Mwandishi: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Chanzo: Duruus-ul-Muhimmah li ´Aammah al-Ummah, uk. 13
Tarjama: Wanachuoni.com
mambo ya wajibu ya swalah
Mambo ya wajibu ya swalah ya ni manane:
La kwanza: Kusema "Allaahu Akbar" mbali na ile ya kwanza.
La pili: Kusema "Sami´ Allaahu li man hamidah" kwa imamu na anayeswali peke yake.
La tatu: Kusema "Rabbanaa wa lak al-Hamd". Inasemwa na wote.
La nne: Kusema "Subhaana Rabbiy al-´Adhwiym" katika Rukuu´.
La tano: Kusema "Subhaana Rabbiy´ al-A´laa" katika Sujuud.
La sita: Kusema "Rabb Ighfir liy" kati ya Sajdah mbili.
La saba na la nane: Tashahhud ya kwanza na kukaa kwayo.
Mwandishi: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Chanzo: Duruus-ul-Muhimmah li ´Aammah al-Ummah, uk. 13-14
Tarjama: Wanachuoni.com
vumilia sheikh kasome Qur-an muda utaenda haraka tuwakuu swaumu mie pamoja na kwamba tunaanza, ila imenikamata maghrib naona mbali aisee
NdioEbwana waungwana kwenye hii thread kuna anayefuturisha??
Masha Allah. Ukumbusho mzuri sana huu na wenye manufaa.allahuma inna kaafuuu tuhibbul afwaaa faafwannaaa yaaa karyyym alfuww. haya ni maneno mtume saw alikuwa akiyataja sana ramadhan. tupunguze soga,story za vijiweni,instagram,magroup yasio na msingi, tukithirishe kuskiliza mawaidha na kujua mambo ya dini. Na pia quraaan kusoma kwa wengi wakat ndio huuu kuziba mashimp dunia si chchte akina ivan walikuwa wanacheza na madola kwenye mitandao sasa yuko maiti lets wake up brothers and sisters fill imaaan
Ameen. Ameennafikiri kama mda mwingi tutakuwa tunautumia hapa kwa ajili ya kuelimishana na kupeana nasaha ramadhan tutaiendea haki, na InshaAllah tutakuwa hapa ramadhani yote ili tupate radhi za M/Mungu (s.w)