Ramadhan Special Thread

Asalam aleykum ..hakika ndug zang nawakumbusha juu ya vitu vidogo vitakavyoweza sababishia kuptea kwa swaumu zetu na tuzichunge sana...simu..huku kwe mitandao facebook.whatssap.instragram nk..tujaribu kupunga matumizi inawez kupunguza ubora wa swaume zetu...
Television...nazo tuziepuka maana kuna mavipind ya ajabu ajabu km miziki,tamthilia zingne mbaya watu wanashinda uchi hii pia itapunguza ubora.wa swaumu zetu..pia la mwisho...swaumu bila swala ni bure tufunge na tuswal vipind vyote vitano..inshaallah..mwenyez mung atufanyie wepec kwa haya
 
Asalam aleykum ..hakika ndug zang nawakumbusha juu ya vitu vidogo vitakavyoweza sababishia kuptea kwa swaumu zetu na tuzichunge sana...simu..huku kwe mitandao facebook.whatssap.instragram nk..tujaribu kupunga matumizi inawez kupunguza ubora wa swaume zetu...
Television...nazo tuziepuka maana kuna mavipind ya ajabu ajabu km miziki,tamthilia zingne mbaya watu wanashinda uchi hii pia itapunguza ubora.wa swaumu zetu..pia la mwisho...swaumu bila swala ni bure tufunge na tuswal vipind vyote vitano..inshaallah..mwenyez mung atufanyie wepec kwa haya
Shukraan
 
Na mimi naungana na wewe punyeto imenitawala hadi sina hamu tena ya wanawake mie na baby care yangu usiku kabla sijalala sasa mwezi wa toba huu vichupa vyote natupa na video zote chafu nimezifuta leo
 
*﴿ ﺑِﺴْﻢِ ﺍﻟﻠﻪِ ﺍﻟﺮَّﺣْﻤﻦِ ﺍﻟﺮَّﺣِﻴﻢِ ﴾*

_*MIONGONI MWA NASAHA MUHIMU KABLA YA RAMADHANI*



*♡ ﻓﻲ ﺭﻣﻀــــﺎﻥ:*
*Katika Ramadhani:*

*♡ ﻧﺤﻦ ﻣﻘﺒﻠﻮﻥ ﻋﻠﻰ ﺷﻬﺮ ﻋﻈﻴﻢ ﺃﻻ ﻭﻫﻮ ﺷﻬﺮ ﺭﻣﻀﺎﻥ.*
_Sisi umetukaribia mwezi wenye ubora. Enyi fahamuni nao ni mwezi wa ramadhan._

*♡ ﻭﻣﺎ ﺃﺩﺭﻙ ﻣﺎ ﺷﻬﺮ ﺭﻣﻀﺎﻥ ...؟*
_Kipi cha kukujuza ni nini mwezi wa ramadhani?_

*♡ ﺷﻬﺮ ﺍﻟﺒﺮ واﻹحسان.*
_Nimwezi wa kufanyiana wema na ihsani._

*Allah ﷻ Anasema:*

{لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنْفِقُوا مِنْ شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّهَ بِهِ عَلِيمٌ}
```KABISA HAMTAFIKIA wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda. Na kitu chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua.``` (3:92)

*♡ ﺷﻬﺮ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﺷﻬﺮ ﺍﻟﺘﺴﺎﻣﺢ..*
_Mwezi wa ramadhan ni mwezi wa kusameheana (kwa waliyo kosana)_

*♡ ينبغى على المسلم أن ﻳﺘﺤﻠّﻰ ﺑﺎﻷﺧﻼﻕ الكريمة.*
_Yatakikana kwa muisilamu ajipambe na tabia nzuri._

*♡ ﻭﻳﻌﺎﻣﻞ ﺍﻟﻨﺎﺱ ﻣﻌﺎﻣﻠﺔ ﺣﺴﻨﺔ، ﻭﺇﺫﺍ ﺃﺧﻄﺄ ﺍﻟﻤﺴﻠﻢ ﻓﻲ ﺣﻖ ﺃﺧﻴﻪ ﻧﺪﻡ ﻋﻠﻰ ﺫﻟﻚ ﻭﺳﺎﺭﻉ ﺑﺎﻻﻋﺘﺬﺍﺭ ﺇﻟﻴﻪ.*
_Na awafanyiye watu muamala ulo mzuri kabisa, Na pindi akoseapo katika haqqi ya nduguye ajute juu ya hilo na akimbiliye kumtaka udhuru na (msamaha)_

*♡ ﻻ ﺗﻨﺴﻰ ﺍﻟﻔﻘﺮﺍﺀ واليتامى والمساكين واﻷرامل فى رمضان.*
_Usiwasahau mafuqara, mayatima, masikini, wajane (kuwasaidia) zaidi katika mwezi wa ramadhani._

*Allah ﷻ Anasema:*

*{إِنْ تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ ۖ وَإِنْ تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنْكُمْ مِنْ سَيِّئَاتِكُمْ ۗ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ}*
```Mkizidhihirisha sadaka ni vizuri; na mkizificha mkawapa mafakiri kwa siri basi hivyo ni kheri kwenu, na yatakuondoleeni baadhi ya maovu yenu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.``` (2:272)

*♡ ﺍﺣﺬﺭ ﻣﻦ ﺍﻹﺳﺮﺍﻑ ﻓﻲ ﺍﻟﻤﺎﻝ والطعام ﻭﻏﻴﺮهما، ﻓﺎﻹﺳﺮﺍﻑ ﻣﺤﺮﻡ.*
_Tahadhari kufanya israfu katika mali na chakula pia vitu vinginevyo, kwani israfu imeharamishwa._

*Allah ﷻ Anasema:*

*{وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِين..}*
```Na kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye(Allah) hapendi wanao fanya israfu.```
(Al aarafu 31)


*WEKA MKAKATI WA KUFANYA KILA YALO MAZURI UFIKAPO MWEZI WENYE KHERI FADHILA NYINGI.

NAWATAKIENI RAMADHANI KARIIM
 
*KUFUNGA RAMADHANI BILA KUSWALI SWALA TANO*

HAKUNA 'Amaal yoyote inayopokelewa kwa Allaah ikiwa mtu hafanyi ibada ya Swala, iwe Funga, Zakah, Hajj au Sadaka au chochote kile katika ibada

Kuacha kusali unaingia katika Kufru

Mtume (Swalla Allaahu 'aleyhi wasalam) alisema:

*"Kati ya mwanadamu na kuingia kwake kwenye shirki na kufru ni kuacha Kuswali".*

[Imaam Muslim ]

ALLAAH Aliyetukuka Amesema katika Qur-aan:

*"Na tutayaendea yale waliyo yatenda katika vitendo vyao, tuvifanye kama mavumbi yaliyo tawanyika".*

[Suratil Furqaan : 23 ]

Imekuja Hadiyth kutoka kwa Imaam Bukhaary kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'aleyhi wasalam) alisema:

*"Mwenye kuacha sala ya 'Asr matendo yake yameharibika".*
[Imaam Bukhaary ]

Maana yake matendo ya mtu huyo hayapokelewi na Allaah.

Mtu asiyeswali Allaah hapokei vitendo vyake na matendo yake mema hayamsaidii chochote ikiwa hatimizi Swala Tano.

Katika swala la kuacha Swala kuna watu wa aina mbili ;

Kuacha kabisa siku zote Yaani *"Taariq Swalaa"* maarufu

Na kuacha sala baadhi ya vipindi, nyakati na siku.

*KAULI ZA WANAZUONI*

1. Wa mwanzo ambaye haswali kabisa kaacha hakuna anachofanya katika Swala huyu kaingia katika KUFRU/UKAFIRI kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'aleyhi wasalam)

2. Na huyu wa pili anayeacha baadhi ya Swala na nyakati, siku ambayo ameacha Swala zake matendo ya siku hiyo hayapokelewi.

Ibn Qayyim Al jawziyyah (Allaah Amrehem) alisema:

_"Wale wanaoacha Swala baadhi ya masiku, matendo yao masiku hayo hayakubaliki, hakuna jambo linalopokelewa kwa Allaah ikiwa mtu kaacha Swalaa"_

[Kitab Al salaa ukurasa wa 65 ]

KUACHA KUSWALI NA MTU ANAFUNGA anajishindisha NJAA MCHANA wa RAMADHANI

Sheiykh Swaaleh Al 'Uthaymeen (Allaah Amrehem) alisema:

_"Ikiwa mtu anafunga na hali ya kuwa haswali, Funga haipokelewi na haikubaliki kwani mwenye kuacha kuswali ni kaafir na murtadi kwani ALLAAH (Aliyetukuka) Anasema:_

*"Basi wakitubu na wakashika Swala na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini"....*

[Suratul Tawbah : 11]

Pia Mtume (Swalla Allaahu 'aleyhi wasalam) alisema:

*"Tofauti yetu na wao (mushrik) ni kuacha swala na atakaewachau sala ni kaafir".*

[Imaam Tirmidh ] na imesahihishwa na Sheikh Albaani (Allaah Amrehem).

[FATAWA AL SWIYAAM ukurasa 87 ]

*UZINDUSHI*

Tunaishi na jamii ya watu ambao wao wanajua Swawm (Funga) maana yake ni kuacha kula na kinywa mchana tu, KUWSALI HAKUMUUSU na tunao majumbani au hata wewe unaesoma ujumbe huu kama una tabia hii iache na badilika, fahamu kuwa Funga yako haipokelewi bila ya kuswali.

Kwa kifupi hakuna kinachopokelewa mbele ya Allaah ikiwa mja hafanyi ibada ya swala hili lieleweke vizuri.

Allaah Alete hidaaya mioyoni mwao na mioyoni mwetu.

Allaahumma Aamiyn!!

Na ALLAAH Anajua zaidi.
 
Asalam aleykum ..hakika ndug zang nawakumbusha juu ya vitu vidogo vitakavyoweza sababishia kuptea kwa swaumu zetu na tuzichunge sana...simu..huku kwe mitandao facebook.whatssap.instragram nk..tujaribu kupunga matumizi inawez kupunguza ubora wa swaume zetu...
Television...nazo tuziepuka maana kuna mavipind ya ajabu ajabu km miziki,tamthilia zingne mbaya watu wanashinda uchi hii pia itapunguza ubora.wa swaumu zetu..pia la mwisho...swaumu bila swala ni bure tufunge na tuswal vipind vyote vitano..inshaallah..mwenyez mung atufanyie wepec kwa haya
Ni kweli asee, hasahasa Facebook na instagram, Mimi hiyo nishaisahau hata kama nimitandao ya kijamii, natumiaga whatsap pekee
 
Nawatakia waislam wote kheri katika kisomo chema cha Qur'an tukufu,

Kwakuanzia na suratu- l baqqara ( juzuu 1),

Karibuni ndugu zangu wapendwa akiwemo

1. Mughalimat bi. Faizafoxy

2. Ukhuty

3.emmtya

4. Byong

Nawengineo.

Ramadhani makbul.
 
Nashauri,kila siku litolewe darsa kuwalingania
1.Waislam
2.Watu wote
Kwa kuwa katika mafundisho ya Kiislam,kuna aya zinazozungumzia watu wote na zipo zinazowataja Waislam tu. Kwa mfano kuzuia binadam kuua binadam mwenzako,tumekatazwa watu wote.
 
Back
Top Bottom