Ramadhan Special Thread

Historia Fupi Ya Palestina​

Jamii

Historia Fupi Ya Palestina

Muhammad Al-Ma’awy

Alhidaaya.com


Ulimwengu wetu wa sasa umekuwa ni wa utandawazi (ulimwengushi) kwa kiasi ambacho yaliyo ndiyo yamekuwa siyo na ya makosa yamechukuliwa kuwa ni ya makosa. Ulimwengu umekuwa ukipigwa makombora na vyombo vya habari kwa njia moja au nyingine.

Mwenye kumiliki chombo cha habari cha kilimwengu anaweza kupeperusha au kuandika ya kwake na yakaweza kuchukuliwa kama ukweli mtupu. Ulimwengu umekuwa ni wenye kuchukua yote na wenye sauti kubwa kwa kuwa na vyombo hivyo wameweza kusikika mbali japokuwa hawana haki wa kupata wanayopata.

Kadhiya moja ambayo imeeleweka sivyo ni kadhiya ya historia ya Palestina. Waliojizatiti kuiweka katika hali hiyo iwe hivyo ni Wazeyuni bila kuwa na pingamizi kwa kuwa na sauti kubwa. Juhudi dhidi yao zimekuwa zikifanywa bila ufanisi wowote kwa sababu ya sauti kubwa waliyonayo wao. Taasisi kubwa na maarufu za vyombo vya habari zinamilikiwa nao kwa namna moja au nyingine. Mbali na hiyo hatufai kufa moyo kuhusu juhudi hizo kwani nusura hutokea baada tawfiki ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Aliyetukuka, kisha juhudi zetu kwa kutumia njia tofauti.

Kwa sababu ya sifa zake Palestina, kama hali ya hewa, rutuba ya ardhi na upatikanaji wa maji safi ndio wavamizi wengi wamejaribu kuiteka ardhi hii na kuitawala kimabavu.

Makao ya awali yalianzishwa Palestina katika miaka ya 14000 hadi 8000 KI (Kabla ya kuzaliwa kwa ‘Nabiy ‘Iysa) kwa utawala wa Tatwafi. Na katika mwaka 8000 KI, mji wa Ariha (Jericho) ulianzishwa huko Palestina. Mji huo ulijengwa na wenyeji ukajengeka kwa njia ya mipango kama ilivyo miji ya kisasa.

Makabila ya mwanzo kuja kuweka makazi yao katika nchi ya Palestina ni yale makabila ya Wayebusi, Waamori, Wahiti, Wakanaani, Waamalika na Wafiniki. Makabila haya yalikaa katika maeneo tofauti ya nchi hiyo: Wakanaani waliweka makazi yao katika eneo la Gaza ilhali Wayebusi walibuni mji wa Yebus, ambao kwa sasa unajulikana kama mji wa al-Quds. Makabila haya yalihamia huko kutoka kusini mwa Bara Arabu takriban mwaka 3000 KI.

Katika mwaka wa 1900 KI, Nabii Ibraahim ('Alayhis-salaam) alihamia kutoka Iraq na kuja kuweka makazi yake katika mji wa Khalil. Hapo ndipo alipomzaa Nabiy Ismaa‘iyl na Ishaaq ('Alayhim-salaam) na baadaye kuzaliwa Nabii Ya‘quub ('Alayhis-salaam).

Katika kipindi 1800 – 1600 KI, Palestina ilitawaliwa na Waheksosi. Ni katika kipindi hiki katika mwaka wa 1750 KI ndio Nabii Ya‘quub ('Alayhis-salaam) alizaliwa.

Katika karne ya 16 KI (yaani mwaka wa 1580 KI), Bani Israili waliokuwa Misri walitiwa utumwani na Firauni wa wakati huo kuvamia na kuitawala Palestina kwa muda kabla ya sehemu hiyo kuingia katika utawala wa Kiislamu.

Mwaka 1250 KI, Nabiy Muwsaa ('Alayhis Salaam) aliagiziwa na Allaah Aliyetukuka atoke Misri ambako wana wa Israili walikuwa ni watumwa waende wakaishi katika ardhi tukufu. Kwa ajili ya ukaidi wao (Qur-aan 5: 21 – 26), walipigwa marufuku kuingia katika ardhi hiyo. Mbali na hilo walipigwa adhabu kali ya kutangatanga katika jangwa kwa muda wa miaka arobaini (40). Katika kipindi hicho, wale wote waliokuwa wamebaleghe walikufa katika jangwa kikabakia kizazi ambacho kililelekea katika maadili ya Kiislamu, Imani na uchaji Allaah kuingia katika ardhi hiyo tukufu. Kizazi hicho kilipata darsa ya ukakamavu, utii, kujitolea mhanga na malezi bora, hivyo kwa tawfiki ya Allaah Aliyetukuka kuweza kuingia ardhi hiyo mwaka 1190 KI wakiongozwa na Yusha bin Nuwh ('Alayhis-salaam). Wakati huo tayari Nabiy Muwsaa ('Alayhis-salaam) alikuwa ameaga dunia hivyo kutoweza kuingia katika ardhi hiyo.

Yusha bin Nuwh ('Alayhis-salaam) ndiye mwana Israili wa kwanza aliyeanzisha dola katika maeneo ya Palestina. Hata hivyo, wana wa Israili chini ya uongozi wa Yusha bin Nuhw ('Alayhis -salaam) hawakuweza kuliteka eneo lote la Palestina katika mipaka yake ya sasa na hata mji wa al-Quds haukuingia mikononi mwake. Ifahamike kuwa dola hiyo haikuwa katika misingi ya Kiyahudi kwani dini ya Kiyahudi ilikuwa haijabuniwa kamwe wakati huo bali ilikuwa ikipekeshwa katika misingi ya Kiislamu.

Dola hii haikukaa kwa muda kwani vurugu liliingia kati baada ya kuaga dunia Yusha bin Nuwh ('Alayhis-salaam), hivyo kushikiliwa na Ma-Qaadhi kabla ya kusambaratika kabisa kabisa. Kufikiwa na hayo, Bani Israili waliingia katika utawala wa Wapalestina ambayo asili yao ni Wakanaani. Kudhalilishwa kwao huko kuliwafanya watake msaada kutoka kwa Allaah Aliyetukuka ili warudi katika enzi zao (Qur-aan, 2: 246). Allaah Aliyetukuka Aliwateulia Twaaluut kuwa mfalme wao wa kuwaongoza wao kwenda kupambana na Wapalestina wakiongozwa na Jaaluut (Qur-aan, 2: 247). Bani Israili waligomba sana kuhusu uchaguzi huo, hata hivyo wapo waliokuwa na Imani ambao walisalimu amri na kujizatiti kwenda kupambana na Wapalestina. Wakati huo, Nabii Daawuud ('Alayhis-salaam) alikuwa kijana mdogo aliyejiunga na jeshi hilo ambalo kwa tawfiki ya Allaah Aliyetukuka liliweza kulishinda jeshi la Jaaluwt (Qur-aan, 2: 248-251). Ushindi huo ulipatikana mwaka wa 1025 KI. Twaaluut aliweza kuanzisha tena dola ya Kiislamu Palestina ikiwa inaongozwa na Bani Israili mpaka kufa kwake mnamo 1004 KI.

Baada ya kuaga dunia tu, hatamu za uongozi zilishikwa na Nabiy Daawuud (‘Alayhis-salaam) ambaye aliipanua dola hiyo kwa kasi kubwa sana. Ni wakati wake ndio mji wa al-Quds uliweza kutekwa. Nabiy Daawuud ('Alayhis-salaam) aliaga dunia mwaka wa 960 KI na kumuacha mtoto wake, Nabiy Sulaymaan ('Alayhis-salaam) katika utawala. Kwa upande wake naye, Nabiy Sulaymaan ('Alayhis-salaam) aliipanua dola hiyo lakini haikufika katika mipaka yake ya sasa. Nabiy Sulaymaan ('Alayhis-salaam) aliimarisha sana dola hiyo, akiwa yeye na babake wameitawala kwa misingi ya Kiislamu. Ilibaki hivyo hadi mwaka wa 922 KI pale naye alipoaga dunia.

Kufariki kwake kuliifanya dola hiyo igawanywe sehemu mbili: Dola ya Yuda (kusini) na Kizeyuni (kaskazini). Bani Israili waligawanyika katika koo zao kwa kiasi ambacho walianza kupigana wao kwa wao (baina dola mbili hizo) na ufisadi ukakithiri kwa kiasi kikubwa sana. Wakati huo ndio alitokea mtu kwa jina la Yuda aliyekiuka mipaka ya Dini na kuasi. Alipata wafuasi wengi na hapo kukazaliwa Dini ya Uyahudi.

Hali hiyo halisi ya mapambano baina ya Bani Israili iliwapelekea dola zao mbili hizo kudhoofika na mwisho katika mwaka wa 722 KI, dola ya Israili ilianguka na eneo hilo kutawaliwa na Wa-Asiria. Nayo dola ya Yuda ilivamiwa na mfalme Nubukadneza wa Babeli (Iraq) mwaka 586 KI, na dola hiyo kuingia katika utawala wa Kibabeli. Wana wa Israili wote walipelekwa uhamishoni huko Iraq kama watumwa. Hapo wengine wao walipata kukimbia na kuingia Ufursi (Iran) ambapo walijaribu kufanya mahusiano ya karibu na utawala wa huko hadi wakamtoa msichana wao kwa ajili ya kuolewa na mfalme wa Iran. Mafungamano hayo yalimfanya mfalme Cyrus wa Iran aunde jeshi kwa usaidizi wa Mayahudi ili kuivamia Palestina na kuwang’oa Wababeli. Cyrus alifanikiwa kuwashinda Wababeli kutoka Palestina na kuwapatia ruhusa Mayahudi kurudi katika nchi hiyo lakini hata hivyo waliorudi hawakuwa wengi, walikuwa wachache sana. Wengi miongoni mwao walibakia katika nchi ya uhamisho wao. Kushinda kwao kulitokea mwaka wa 538 KI. Hata hivyo, Mayahudi wakati wa utawala wa Kifursi hawakuwa na mamlaka wala madaraka yoyote lakini walipatiwa uhuru wa kufanya Ibadah zao bila kufuatiliwa, kuingiliwa wala kubughudhiwa na Wafursi.

Na katika mwaka 332 KI, Palestina ilivamiwa na kutekwa na Warumi wakiongozwa na Alexander kutoka Macedonia. Hata hivyo, Warumi hawakuweza kukaa huko kwa muda mrefu pale wafalme wa kutoka Syria walipovamia sehemu hiyo na kuitia katika utawala wao mwaka 198 KI.

Wayunani nao waliiteka ardhi hiyo mwaka wa 175 Ki na kuitawala. Mayahudi waliweza kujizatiti na kuiteka sehemu hiyo ya ardhi mwaka wa 166 KI na ikabaki mikononi mwao kwa kipindi cha miaka 4. Wasyria walirudi tena kwa kishindo na kuwashinda Mayahudi mwaka wa 162 KI. Hata hivyo, nao Mayahudi walijizatiti kwa mara nyingine tena wakaja wakawang’oa Wasyria kutoka sehemu hiyo mwaka 143 KI. Hapo waliweza kuibakisha ardhi hiyo katika utawala wao hadi mwaka 70 KI.

Kwa miaka saba baada ya huo mwaka wa 70 kukawepo vurugu kubwa hadi mwishowe Warumi wakaweza kuwashinda Mayahudi mnamo 63 KI. Kuanzia mwaka huo hadi mwaka wa 616 BI (Baada ya kuzaliwa kwa Nabii ‘Iysa) Palestina ilibaki katika utawala wa Warumi isipokuwa kile kipindi cha mapinduzi ya Mayahudi cha mwaka 66 BI na 132 – 135 BI. Hata hivyo, katika kipindi cha mapinduzi hayo ya Mayahudi serikali ya Roma ilituma wanajeshi wake wengi ili kuyasagasaga hayo mapinduzi. Ni wakati huo ndio serikali ya Kirumi ilipitisha sheria kuwa mji wa al-Quds haufai kukaliwa na Mayahudi.

Utawala wa Kirumi ulisitishwa kidogo na ule wa Wafursi mwaka wa 616 BI. Lakini utawala wa Wafursi haukukaa kwa muda mrefu kwani katika mwaka wa 624 BI walishindwa na Warumi katika vita ambavyo Allaah Amevizungumzia katika Suwrah Ruwm (30): Aayah 1 – 5. Warumi waliweza kusonga mbele hadi kuuteka mji wa al-Quds katika kipindi cha muda miaka 3 hadi 4.

Kipindi baada ya Sulhu ya Hudaybiyah ndicho kile ambacho Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alianza kupeleka barua kwa mataifa mbali na ndio barua hiyo ikamfikia mfalme wa Warumi, Hiraql (Heraclius) akiwa al-Quds mwaka wa 628 BI. Hapo ndio yalianza mapambano baina ya Waislamu wakiongozwa na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Warumi. Mji wa al-Quds uliingia mikononi mwa Waislamu wakati wa ukhalifa wa 'Umar bin al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye alifunga safari kwenda kuchukua funguo za mji kutoka kwa kasisi Sophronius mwaka wa 638 BI na hapo miji mingi ya Palestina ikaingia katika Dola ya Kiislamu. Nchi hiyo pamoja na nchi za Shaam zote zilibakia katika utawala wa Kiislamu hadi mwaka wa 1099 BI wakati ambapo Wakristo walikuja kuzivamia ardhi hizo katika vita vya Msalaba.

Watu wa Msalaba kutoka bara Ulaya waliweza kuwaua Waislamu 70,000 ndani ya eneo la Msikiti wa Aqswa. Wakristo waliweza kuitawala ardhi hiyo kwa muda wa miaka 88 ambapo harakati za kuikomboa zilipamba moto. Harakati hizo zilianzishwa na Nuurud-Diyn Zinkiy, mwanae Nuurud-Diyn Mahmuud na baadaye Swalaahud-Diyn Hasan al-Ayyuubiy ambaye aliweza kwa tawfiki ya Allaah kuirudisha Palestina kuwa katika Dola ya Kiislamu mwaka 1187 BI.

Kuanzia mwaka huo wa 1187 BI, Palestina ilibakia kuwa katika Dola ya Kiislamu hadi baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia (1917) ndio Palestina iliingia katika utawala wa Uingereza. Wenyeji wa al-Quds hawakusadiki masikio yao pale walipokusanyika kumsikiliza jemadari Allenby katika uwanja wa al-Quds. Allenby alisema kwa uwazi kabisa: "Leo ndio vita vya Msalaba vimekwisha". Kabla hata ya kuiteka na kuitawala ardhi hiyo, serikali ya Uingereza tayari ilikuwa imewaahidi Wazeyuni kuwa wakiondoka watawazawadia wao kipande hicho cha ardhi. Hayo yanapatikana katika ahadi au tangazo la Waziri wa Nje, Arthur James Balfour ya tarehe 2 Novemba 1917.

Na kweli kwa ahadi yao, Uingereza ilipoondoka Mei 1948 waliwaachia ardhi hiyo Wazeyuni wasiokuwa na mafungamano na ardhi hiyo. Hakika ni kuwa Mayahudi wakati huo na kabla ya hapo hawakuwa na kitambulisho cha aina yoyote ile. Hii ni kwa mujibu wa barua aliyoiandika Dkt Chaim Weizman ya 18 Aprili 1918 kwa mkewe: “Ni masikitiko makubwa kuona kuwa hapa hatuna chochote. Hapa hakuna hata taasisi moja ya Kiyahudi, lakini kumejaa minara (kumaanisha wingi wa Misikiti)”.

Ndugu zetu walianzisha harakati ya kutaka kujikomboa na minyororo ya ukoloni. Harakati ya kwanza ni ile iliyoongozwa na Sh. Abdul-Qaadir al-Qassaam, kutoka Syria mwaka 1925. Mwaka wa 1929 kulikuwa na Intifadha ya al-Buraaq, naye Sh. Al-Qassaam akauliwa mwaka wa 1935 alipokuwa anapambana na jeshi la Muingereza katika maeneo hayo matakatifu.

Kuanzia mwaka wa 1948, kumekuwa na vita baina ya Waarabu na Wazeyuni, lakini Waarabu wakashindwa sana kwa kutokuwa na kuwa wamoja na kauli moja, kutokuwa na mipango mizuri na wakati mwengine kushirikiana na dola haramu ya Kizeyuni. Hata hivyo, sababu kubwa ya kushindwa ni kule Waarabu kuichukulia kuwa hiyo ni kadhiya ya Waarabu tu na kutowajumuisha Waislamu wengineo.


Rejea:

  1. Quds Qadhwiyah Kull Muslim.
  2. Mustwafa Muhammad atw-Twahhaan, Filistwiyn wal Muaamaratul Qubraa.
  3. Al-Islaam wal Qadhwiyatul Filistwiyniyah.
  4. Dkt. Muhsin Muhammad Swaalih, atw-Twariyq ilal Quds.
  5. Dkt. Muhammad Siddiq Qureishi, Zionism and Racism.
  6. Dkt. Mohsen M. Saleh, The Palestinian Issue.
  7. Mawlana Mawdudi, Tafhiymul Qur-aan.
  8. Raymond Caroll, The Palestine Question.
  9. Maryam Jamiylah, Islam versus Ahl al Kitab: Past and Present.
  10. Dkt. Bhatt, Zionism and Internal Security.
  11. Dkt. Muhsin Muhammad Swaalih, al-Haqaaiq al-Arba'una fil Qadhwiyatil Filistwiyniyah.
  12. Tovuti:
 
Hutuba ya Ijumaa: Faida ya Kuwahi Msikitini

Khutba ya Kwanza:

Alhamdulillahi Rabbil 'Alamin. Tunamshukuru Allah (S.W) kwa kutufikisha tena katika siku tukufu ya Ijumaa. Tunamswalia na kumtakia amani Mtume wetu Muhammad (S.A.W), familia yake, Maswahaba wake na wote wanaomfuata kwa wema hadi Siku ya Qiyama.

Enyi waumini!

Kuwahi msikitini siku ya Ijumaa ni jambo la kheri kubwa. Allah (S.W) amesema katika Surat Al-Jumu'ah (62:9):

"Enyi mlioamini! Iwapo mtaitwa kwa ajili ya swala siku ya Ijumaa, nendeni kwa dhikri ya Allah na acheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau mngalijua."

Kuwahi msikitini huonyesha mapenzi ya mja kwa swala, kwa Allah na kwa Mtume wake. Katika Hadith sahihi kutoka kwa Abu Huraira (R.A), Mtume (S.A.W) amesema:

"Atakayeoga siku ya Ijumaa kisha akawahi, ni kama mtu aliyetoa sadaka ya ngamia. Atakayekwenda katika saa ya pili, ni kama aliyetoa sadaka ya ng’ombe. Saa ya tatu ni kama mbuzi, saa ya nne ni kama kuku, na saa ya tano ni kama yai. Na anapomtokea Imamu, malaika hufunga vitabu vyao na kumsikiliza khutba." (Bukhari & Muslim)

Faida za kuwahi msikitini ni pamoja na:

1. Kupata thawabu kubwa – mapema zaidi, thawabu kubwa zaidi.
2. Kukaa karibu na Imamu – na kusikiliza khutba
3. Kuwa miongoni mwa wale ambao malaika huwaandikia kwa jina.
4. Kujiepusha na usumbufu wa kuchelewa, mfano wa kutofahamu khutba au kuikosa kabisa.

Khutba ya Pili:

Enyi ndugu waislamu!

Tujitahidi kuwahi Ijumaa kila wiki, kwa ajili ya radhi za Allah. Tuwe watu wa kuonyesha mfano kwa familia zetu na watoto wetu.

Tujue pia kuwa kuchelewa bila sababu ni hasara na kupunguza thawabu. Mtume amesema, "Mtu anayeacha Ijumaa mara tatu mfululizo bila udhuru, Allah huweka muhuri katika moyo wake."

Ewe Muislamu! Usikose kheri hizi. Wahi msikitini, osha mwili, vaa nguo safi, tumia manukato, soma Qur’an, fanya dua – ujikurubishe kwa Allah.

Tunamaliza kwa dua:
Ewe Mola, tufanye miongoni mwa wanaowahi Ijumaa, wanaosikiliza kwa makini na wanaonufaika na khutba. Ameen.

Wasalamu Aleykum warahmatullah wabarakatuh.
 
Hutuba ya Ijumaa: Umuhimu wa Kumtaja Allah kwa Wingi (Dhikr)

Khatibu anaanza kwa Hamdu:


Alhamdulillahi Rabbil 'aalamiin. Namsifu Allah kwa neema Zake zisizo na idadi. Namuomba rehema na amani zimshukie Mtume Muhammad (SAW), familia yake, maswahaba zake na wote wanaomfuata kwa wema hadi siku ya mwisho.

Ama baad:

Enyi Waumini!
Ninawanasihi, nafsi yangu kwanza, tumche Allah kwa kumuogopa kwa haki ya kumuogopa. Mcheni Mola wenu kwa dhati, na msife ila mkiwa Waislamu.

Enyi Waja wa Allah,

Leo hutuba yetu inahusu: Kumtaja Allah kwa wingi — Dhikrullah.

Allah Subhaanahu wa Ta’ala anasema katika Qur’an:

"Enyi mlioamini! Mtajeni Allah kwa wingi wa dhikri, na mtukuse asubuhi na jioni."
(Suratul Ahzaab: 41-42)

Kumtaja Allah ni ibada nyepesi kwa ulimi, lakini ni nzito mizani ya thawabu. Ni ngao ya moyo, ni utulivu wa nafsi, ni kinga dhidi ya shetani.

Mtume (SAW) amesema:

"Mfano wa yule anayemtaja Mola wake na yule asiyemtaja, ni kama aliye hai na aliyekufa."
(Hadith – Bukhari)

Faida za Dhikr:
1. Hujenga uhusiano wa karibu na Allah
2. Hutoa utulivu wa moyo: “Hakika kwa kumkumbuka Allah, mioyo hutulia.” (Surah Ra’d: 28)
3. Ni sababu ya msamaha na rehema
4. Humsukuma mja kujiepusha na maasi

Aina za Dhikr:
  • Subhanallah
  • Alhamdulillah
- Allahu Akbar
  • Laa ilaaha illa Allah
  • Astaghfirullah
  • Kusoma Qur’an
  • Swala na sala ya usiku
  • Kumtaja Allah kwa moyo na kwa ulimi

Kumbuka:
Sio kila mwenye ulimi anamkumbuka Allah. Dhikr ya kweli huanzia moyoni. Mtu hujua thamani ya Allah, huelewa ukuu wake, na maisha yake yote hujawa na utii na kumtaja.

Hitimisho:
Enyi ndugu zangu katika imani, tujifunze kujaza muda wetu kwa kumtaja Mola wetu. Tusisubiri matatizo ndiyo tumkumbuke. Acheni ulimi wenu uwe na unyevunyevu wa dhikr kila siku.

Tumalizie kwa dua:

Allahumma ja'alnaa minadhaakira lakathiran wa dhaakiraat.
(Ya Allah tufanye tuwe miongoni mwa wanaokukumbuka kwa wingi, wanaume kwa wanawake.)

Ameen.

Wassalaamu alaikum wa Rahmatullah.
 
Assalaam alaikum warahmatullah wabarakatuh

Naam ndugu zangu katika imani, tuhangaike tunavyohangaika na maisha,tuwe busy Kadri itakavyo kuwa lakini kikubwa tusimsahau Allah subhaanahu wataala

Hakika amesema Rasulullah swalla aalahu alaih wassalaam mfano wa watu wanao mkumbuka Allah huesabiwa wako hai na wale wasio mkumbuka Allah hata kama angali wahai ila wanahesabiwa kuwa ni Maiti

Hii inaonyesha umuhimu mkubwa wa swala Zima la kumkumbuka Allah,waeza mkumbuka kwa kusoma qur'an,kuswali,kumtaja katika dhikri mbali mbali ambazo tunazojua

Pamoja na kutafuta mkate wetu wa kila siku hapa duni lakini katu tusimsahau Allah subhaanahu wataala
 
🕌 Hutuba ya Ijumaa

Kichwa: Kuwahurumia Wasiojiweza

Alhamdu lillahi rabbil-‘ālamīn, na shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema na mwenye kurehemu. Tunamshukuru Yeye, tunamuomba msaada na msamaha Wake. Tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari za nafsi zetu na matendo yetu mabaya. Yeyote atakayeongozwa na Mwenyezi Mungu hakuna wa kumpoteza, na atakayepotezwa na Mwenyezi Mungu hakuna wa kumuongoza.

Ama ba‘du:

Enyi ndugu Waislamu, ninawasii nafsi yangu na nafsi zenu tumche Mwenyezi Mungu kwa ucha-Mungu wa kweli, kwani ucha-Mungu ndiyo kinga bora ya mja.

Sehemu ya Kwanza

Ndugu zangu katika imani, leo hotuba yetu ni kuhusu kuwahurumia wasiojiweza.
Huruma ni alama ya imani. Mtume (ﷺ) amesema:

“Mwenye huruma kwa wengine, Mwenyezi Mungu atamhurumia; rehemeni waliomo ardhini, atakuhurumieni aliye mbinguni.”
(Imepokewa na Abu Dawud, Tirmidhi)



Watu wasiojiweza — maskini, mayatima, wajane, wagonjwa, na wahitaji — ni ndugu zetu katika ubinadamu na dini. Kuwasaidia si hisani tu, bali ni jukumu la kiimani.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema katika Qur’an:

“Na wanawalisha chakula, ingawa wanakipenda, masikini na yatima na mfungwa. Wanasema: Hakika tunakulisheni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukrani.”
(Surat Al-Insaan: 8-9)



Aya hii inatufundisha kuwa sadaka na msaada tunayotoa kwa wasiojiweza ni ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, si kwa kujionyesha.

Enyi ndugu zangu, Mtume (ﷺ) pia amesema:

“Si muumini yule anayelala akiwa ameshiba ilhali jirani yake ana njaa.”
(Imepokewa na Tabarani)



Hivyo basi, huruma inaanza na majirani zetu, ndugu zetu, jamii yetu.

Sehemu ya Pili

Ndugu Waislamu, faida za kuwahurumia wasiojiweza ni nyingi:

1. Huchangia mshikamano wa kijamii.


2. Hupunguza wivu na chuki miongoni mwa watu.


3. Huletea baraka katika mali na riziki.


4. Huvuta huruma ya Mwenyezi Mungu kwa mtoa msaada.



Tusisahau kuwa tunapowasaidia maskini, mayatima, na wahitaji, si kwamba tunawasaidia wao tu, bali tunajisaidia nafsi zetu kwa kujitayarishia thawabu za Akhera.

Hitimisho

Nawasii ndugu zangu tuiishi kauli ya Qur’an:

“Mwenye kufanya wema wa chembe ya haradali ataona, na mwenye kufanya uovu wa chembe ya haradali ataona.”
(Surat Az-Zalzalah: 7-8)



Tuwahurumie wasiojiweza, tuwasaidie kwa mali zetu, kwa muda wetu, na kwa dua zetu. Huu ndio ucha-Mungu wa kweli.

Wa aqimus-salah.
 
 
Hutba ya Ijumaa: Kuwapenda Majirani

Khutba ya Kwanza

Alhamdulillahi Rabbil-‘Aalameen, tunamsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu, tunamuomba msaada na msamaha, na tunajikinga kwake na shari za nafsi zetu na madhambi yetu. Yule anayeongozwa na Mwenyezi Mungu hakuna wa kumpoteza, na yule anayepotezwa na Mwenyezi Mungu hakuna wa kumuongoza. Nashuhudia kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allah pekee, hana mshirika, na Muhammad (rehema na amani zimshukie) ni mtumwa na Mtume wake.

Amma ba’ad:

Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, nawanasihi mimi na nyinyi tumche Allah kwa kumtii katika siri na dhahiri, kwani kumcha Allah ndilo nguzo la kufanikisha maisha hapa duniani na kesho Akhera.

Leo khutba yetu itahusu kuwapenda na kuwatendea wema majirani.

Islam imehimiza sana kuwatendea mema majirani, bila kujali dini zao au asili zao. Mtume ﷺ amesema:

“Jibril aliendelea kuniusia kuhusu jirani mpaka nikadhani atamfanya kuwa mrithi (wa mali yangu).”
(Bukhari na Muslim)



Hadith hii inaonyesha nafasi kubwa aliyopewa jirani katika Uislamu. Jirani ni mtu wa karibu zaidi nawe, anakushuhudia katika maisha yako ya kila siku. Ikiwa jirani ni mwema na mwenye mapenzi, maisha yanakuwa mazuri. Ikiwa jirani ni mwenye kudhulumu na kuchukia, maisha yanakuwa magumu.

Waislamu tunapaswa kuwa mfano bora kwa majirani zetu. Tuwatembelee wanapougua, tuwashirikishe furaha zao, tuwasaidie wanapopatwa na matatizo, na tusile kile kizuri nyumbani mwetu bila kuwafikiria. Mtume ﷺ amesema:

“Hayuko muumini yule ambaye analala akiwa ameshiba, hali jirani yake yuko njaa.”
(Tabarani)



Enyi Waislamu, jirani ana haki tatu ikiwa ni Muislamu wa ukoo wako: haki ya Uislamu, haki ya ujirani na haki ya undugu. Na ikiwa si Muislamu ana haki mbili: haki ya ujirani na haki ya ubinadamu.

Kwa hiyo tusichague kuchagua, bali tuwapende wote, kwa kuwa kufanya hivyo ni kujijengea jamii ya upendo, mshikamano na heshima.

Khutba ya Pili

Alhamdulillahi Rabbil-‘Aalameen, tunaendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema nyingi alizotupa.

Enyi Waislamu, kumbukeni kuwa kuwapenda majirani ni ibada na njia ya kufikia radhi za Allah. Tukiwapenda majirani zetu, tunaimarisha umoja wa kijamii, tunapunguza uhasama na tunakuwa jamii yenye mshikamano.

Tumuombe Mwenyezi Mungu atujalie tuwe miongoni mwa waja wake wanaowapenda na kuwatendea mema majirani zao.

Allahumma, tujaalie tuwe watu wa upendo, heshima na mshikamano. Allahumma tujaalie tuwe mfano bora katika jamii zetu. Allahumma tusamehe madhambi yetu, na utuongoze kwenye njia iliyo nyoofu.

Hakika Allah na Malaika wake humtakia rehema Mtume, basi enyi mlioamini msalieni na mumsalimie kwa wingi.

Wasalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.
 
🌙 Hutba ya Ijumaa Kuhusu Malezi Bora ya Watoto


---

Khutba ya Kwanza

Alhamdulillahi Rabbil-‘aalamiin. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu. Tunamwomba msaada na msamaha, na tunajikinga kwake na shari za nafsi zetu na mabaya ya matendo yetu. Rehema na amani zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad ﷺ, Ahlul-Bayt wake na Maswahaba zake wote.

Enyi Waislamu wenzangu, nasaha ya leo inahusu malezi bora ya watoto wetu.

Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani Tukufu:

“Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe...” (Qur’an 66:6).



Aya hii inatufundisha kuwa ni wajibu kwa wazazi kuwalea watoto wao katika njia ya uislamu, kuwafundisha tofauti kati ya halali na haramu, na kuwalinda na shari za dunia na Akhera.

Mtume ﷺ amesema:

“Kila mmoja wenu ni mchungaji, na kila mmoja ataulizwa juu ya wale aliowachunga.” (Bukhari na Muslim).



Hii ni dalili kuwa mzazi ana jukumu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuhusu watoto wake. Malezi siyo tu chakula na mavazi, bali ni pamoja na kuwafundisha sala, heshima, maadili, na elimu.


---

Khutba ya Pili

Enyi waumini, malezi bora ya watoto yanajumuisha mambo kadhaa:

1. Upendo na huruma – Mtume ﷺ alikuwa mfano bora. Alikuwa akiwapenda watoto na wajukuu wake, na kusema “Si miongoni mwetu yule asiyeonyesha huruma kwa wadogo.”


2. Kuwafundisha dini – Sala, Qur’an, na adabu za Kiislamu ni nguzo ya malezi bora. Mtoto akilelewa na misingi ya dini, atakuwa nguzo ya umma kesho.


3. Elimu ya dunia na Akhera – Mtume ﷺ amesema: “Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila Muislamu.”


4. Kuwa mfano bora – Watoto hujifunza zaidi kwa yale wanayoona. Ikiwa mzazi ataswali, atasema kweli, na ataheshimu, basi mtoto atafuata mfano huo.


5. Kuwalinda na maovu ya zama – Teknolojia, marafiki wabaya, na mitindo isiyo ya Kiislamu vinaweza kuharibu watoto. Wazazi ni walinzi wa heshima na mustakabali wa watoto wao.



Enyi Waislamu, tukumbuke kuwa watoto ni amana. Mtume ﷺ amesema:

“Hakuna zawadi bora ambayo mzazi humpa mtoto wake kuliko malezi mema.” (Tirmidhiy).




---

Hitimisho na Dua

Ewe Mwenyezi Mungu, tujaalie tuwe wazazi wema wanaolea watoto kwa malezi bora.
Ewe Mwenyezi Mungu, waongoze watoto wetu katika njia ya haki.
Ewe Mwenyezi Mungu, walinde na maovu ya dunia na fitna za zama hizi.
Ewe Mwenyezi Mungu, wafanye watoto wetu kuwa chemchemi ya kheri, na si maumivu kwetu wala jamii.

Wa Aqimisswalaah.
 
Assalaam alaikumu warahmatullah wabarakatu

Naam ndugu zangu katika imani natumaini mnaendelea vizuri,ni mda kidogo sasa nimekuwa slow slow humu ndani lakini inshaAllah kwa uwezo wa Allah tutaendelea kukumbushana na kuzinduana masuala mbali mbali ya dini yetu
 
Back
Top Bottom