Ramadhan Special Thread

10-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Alikuwa Na Mwili Mlaini Kabisa Na Wenye Kutoa Harufu Nzuri Mno Ya Manukato​

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

10-Alikuwa Na Mwili Mlaini Kabisa Na Wenye Kutoa Harufu Nzuri Mno Ya Manukato

www.alhidaaya.com



عن أَنَسٌ رضي الله عنه قال: مَا شَمِمْتُ عَنْبَرًا قَطُّ وَلاَ مِسْكًا وَلاَ شَيْئًا أَطْيَبَ مِنْ رِيحِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَلاَ مَسِسْتُ شَيْئًا قَطُّ دِيبَاجًا وَلاَ حَرِيرًا أَلْيَنَ مَسًّا مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم
Kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Sijapatapo kusikia ‘ambar au misk wala harufu yoyote nyengine yenye harufu nzuri kama harufu ya mwili wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Na sijapatapo kugusa makhmeli wala hariri iliyo laini kabisa kulikono mwili wa Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)) [Muslim]


‘Ambar = Aina ya mafuta mazito yenye manukato mazuri kabisa.

Misk = Aina ya mafuta mazito yenye manukato mazuri. Miski ziko rangi mbili: nyeupe na nyeusi. Hii ndio iliyotajwa katika Sunnah kwa ajili ya wanawake kujitwaharisha hedhi zao.


Na pia:

عن جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ، قَالَ صَلَّيْتُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم صَلاَةَ الأُولَى ثُمَّ خَرَجَ إِلَى أَهْلِهِ وَخَرَجْتُ مَعَهُ فَاسْتَقْبَلَهُ وِلْدَانٌ فَجَعَلَ يَمْسَحُ خَدَّىْ أَحَدِهِمْ وَاحِدًا وَاحِدًا - قَالَ - وَأَمَّا أَنَا فَمَسَحَ خَدِّي - قَالَ - فَوَجَدْتُ لِيَدِهِ بَرْدًا أَوْ رِيحًا كَأَنَّمَا أَخْرَجَهَا مِنْ جُؤْنَةِ عَطَّارٍ ‏.‏
Kutoka kwa Jaabir Bin Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah ya mwanzo kisha akatoka kwenda kwa ahli zake nami nikatoka kwenda naye. Akakutana na watoto (njiani). Akawagusa mashavu yao mmmoja mmoja. Akanigusa mimi pia shavu langu nikahisi ubaridi au harufu ya mkono wake kama vile umetolewa kutoka mfuko wa mafuta ya manukato mazuri.” [Muslim
 

11-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Mifano Ya Ukarimu Wake: Akitoa Swadaqah Hadi Kwamba Alipofariki Hakuacha Dirham Wala Dinari​


Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

11-Mifano Ya Ukarimu Wake:

Akitoa Swadaqah Hadi Kwamba Alipofariki Hakuacha Dirham Wala Dinari

www.alhidaaya.com


Kutoa kwake swadaqah Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kulikuwa hadi alipofariki hakuwa na chochote cha kumiliki wala dirham wala dinari kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

عَنْ عَمْرِو بْنِ الْحَارِثِ، خَتَنِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَخِي جُوَيْرِيَةَ بِنْتِ الْحَارِثِ قَالَ مَا تَرَكَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عِنْدَ مَوْتِهِ دِرْهَمًا وَلاَ دِينَارًا وَلاَ عَبْدًا وَلاَ أَمَةً وَلاَ شَيْئًا، إِلاَّ بَغْلَتَهُ الْبَيْضَاءَ وَسِلاَحَهُ وَأَرْضًا جَعَلَهَا صَدَقَةً‏.‏

Imepokelewa kutoka kwa ‘Amruw bin Al-Haarith, kaka yake mke wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Alipofariki Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuacha dirham wala dinari, wala mtumwa wala kijakazi, isipokuwa baghala wake mweupe (aliyekuwa akimpanda), na silaha na kipande cha ardhi alichokitolea swadaqah.” [Al-Bukhaariy]
 
slogan_mobile.png

Ukurasa Wa Kwanza




12-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Mifano Ya Ukarimu Wake: Akitoa Bila Kukhofia Umasikini​

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

12-Mifano Ya Ukarimu Wake: Akitoa Bila Kukhofia Umasikini

www.alhidaaya.com



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitoa swadaqah kila mara bila ya kukhofu umasikini:



عَنْ مُوسَى بْنِ أَنَسٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: مَا سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى الإِسْلاَمِ شَيْئًا إِلاَّ أَعْطَاهُ. قَالَ: فَجَاءَهُ رَجُلٌ فَأَعْطَاهُ غَنَمًا بَيْنَ جَبَلَيْنِ فَرَجَعَ إِلَى قَوْمِهِ فَقَالَ: "يَا قَوْمِ أَسْلِمُوا فَإِنَّ مُحَمَّدًا يُعْطِي عَطَاءً لاَ يَخْشَى الْفَاقَةَ"
Imepokelewa kutoka kwa Muwsaa bin Anas kutoka kwa baba yake kwamba: Hakupata kuombwa kitu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ajili ya Uislamu isipokuwa alitoa.” Akasema: “Alimjia mtu akampa kundi la mifugo ya (kondoo na mbuzi). Akarudi kwa watu wake na kusema: “Enyi watu wangu! Silimuni katika Uislamu kwani Muhammad anatoa swadaqah bila ya kukhofia ufukara.” [Muslim]
 
Kumuabisha nduguyo kwa dhambi kwa kudai una ghera ya Dini.


Atakayemuaibisha ndugu yake kwa Dhambi (fulani) hatokufa hadi (na yeye) aifanye : Shaykh Al Fawzan Hafidhahullah:

Katika aliyosema:

Waislamu wanayo madhambi na sio Maa'sumiin (Waliokingwa na Makosa)

Kukingwa na Makosa ni kwa Manabii pekee

Wewe usifanye aibu za watu kuwa ndio njia ya kuwatia kasoro/aibu/upungufu na ukataja aibu zao na ukawaaibisha (ukawa unasema): "Ewe uliyefanya kadhaa ewe uliyefanya kadhaa!"

Ukimuaibisha (ndugu yako) kwa dhambi (fulani) basi Allah Atakuadhibu, kuwa hutakufa ila utafanya hii dhambi.

Jiweke mbali na kuziingilia aibu za watu

Zisitiri aibu zao

Nasaha haijakatazwa, nasaha inatakiwa lakini Kuaibisha?!

Mwenye kunasihi haaibishi bali ananasihi kwa: Kumsikitikia na kumhurumia, na kwa kumsitiri na kwa ulaini

Kuna tofauti kati ya Nasaha na Kuaibisha.

Anasema eti "Hii ni katika ghera (kuwa na ghera na Dini) la! hakuna cha ghera hii haijuzu!

Ghera ni kuwa: Umnasihi na Umsikitikie na kumuhurumia hii ndio Ghera sio Fedheha (Kumfedhehesha)

Kufedhehesha haijuzu

Ni wajibu kwako umsitiri ndugu yako.


Chanzo:

View: https://t.me/thereligionisadvice/29173
════ ❁✿❁ ════
Salafi Da'wah East Africa (Salafi Da'wah Afrika Mashariki)
 
Sifa za kupata mke mwema kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu na hekima za maisha ni kama zifuatazo:

1. Dini: Mtume Muhammad (s.a.w) alisema:
“Mwanamke huolewa kwa sababu nne: kwa mali yake, uzuri wake, nasaba yake, na dini yake. Basi chagua mwenye dini, utabarikiwa mikono yako.” (Bukhari na Muslim)

2. Tabia njema: Awe na adabu, heshima, si mjeuri, mwenye haya na mwenye kujali.

3. Utiifu kwa Allah: Mwenye kumuogopa Allah, anaeswali, na anayejiepusha na maasi.

4. Mlezi mzuri: Mwenye uwezo wa kulea familia, watoto, na kutunza nyumba.

5. Heshima kwa mume: Mwenye moyo wa kuheshimu, kusikiliza na kushirikiana na mume katika kila hali.

6. Uvumilivu: Awe mvumilivu katika changamoto za ndoa na maisha kwa ujumla.

7. Amani na utulivu: Mwanamke mwema huleta amani moyoni na utulivu katika familia.
 
Sifa za mume mwema katika Uislamu na maadili ya kijamii ni kama zifuatazo:

1. Mcha Mungu (taqwa) – Anamwogopa Allah, huswali, na hufuata maamrisho ya Dini.
2. Mwaminifu – Huwa muadilifu kwa mke wake, si mzinifu, hana hila wala hadaa.
3. Mvumilivu – Huvumilia makosa madogo ya mke wake na hujenga badala ya kubomoa.
4. Mwenye upendo – Humpenda mke wake, humsikiliza, humjali na kumthamini.
5. Mlezi na mlinzi – Huwajibika kumtunza mke wake kwa mali, usalama, na heshima.
6. Anajua mawasiliano – Huongea kwa hekima na si kwa ukali au matusi.
7. Mkarimu – Huwapa familia yake matumizi ya halali kwa moyo wa kutoa.
8. Mshauri mwema – Husaidia familia kufanya maamuzi kwa busara na kwa mashauriano.
9. Mfano wa kuigwa – Katika tabia, ibada, na uongozi wa familia.
10. Hana kiburi – Hathamaki wala kudharau mkewe au watu wake.

Mtume Muhammad (s.a.w) alisema:
"Bora wenu ni yule aliye bora kwa wake zake." (Tirmidhiy).
 
HUTBA YA IJUMAA: UMUHIMU WA KUOA

Khutba ya Kwanza:

Alhamdulillah! Tunamshukuru Allah Subhaanahu wa Ta’ala kwa neema ya uhai, Imani na Uislamu. Tunamwomba rehema na amani zimshukie Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wasallam), familia yake, Maswahaba wake na Waislamu wote waliomfuata kwa wema hadi Siku ya Qiyaamah.

Enyi ndugu Waislamu! Leo tutazungumzia juu ya Umuhimu wa Kuoa katika Uislamu.

Kuoa ni moja ya Sunnah tukufu za Mtume Muhammad (Swalla Allahu ‘alayhi wasallam), na ni jambo lililosisitizwa sana katika Qur'an na Hadith. Allah Subhaanahu wa Ta'ala anasema:

"Naowaeni wajane miongoni mwenu, na wale walio wema miongoni mwa watumwa wenu wanaume na wanawake. Wakiwa mafakiri, Allah atawatajirisha kwa fadhila Zake."
(Surat An-Nuur: 32)

Ndugu zangu, ndoa ni njia halali ya kutuliza matamanio ya kimaumbile, kupata utulivu wa moyo, kujiepusha na zinaa na kujenga familia ya Kiislamu.

Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wasallam) amesema:
"Enyi vijana, anayemiliki uwezo wa kuoa, na aoe. Hakika ndoa humsaidia kuangusha macho (na kuzuia uzinzi)..."
(Bukhari & Muslim)

Khutba ya Pili:

Enyi Waislamu! Uislamu umeweka ndoa kuwa ni ibada, siyo anasa. Kupitia ndoa, Muislamu hujijengea tabia ya kuwajibika, kushirikiana, kusamehe na kuendeleza kizazi chenye maadili mema.
Wazazi, tuwahimize vijana kuoa kwa wakati. Tuwape mwongozo, si vikwazo. Na nyinyi vijana, msitafute mahitaji ya dunia kupita kiasi kabla ya ndoa, kwani riziki ni ya Allah, na neema iko ndani ya ndoa.

Mwisho, tuombe:
"Rabbanaa hab lanaa min azwaajinaa wa dhurriyyaatinaa qurrata a’yunin waj’alnaa lil-muttaqiina imaamaa."
(Aayah: Al-Furqan: 74)

Ewe Mola! Tujalie wake zetu na watoto wetu wawe faraja ya macho yetu, na utufanye kuwa kiongozi wa wachamungu. Ameen.

Wasalaamu Alaykum Warahmatullah.
 
slogan_mobile.png

Ukurasa Wa Kwanza




Amali Za Kuwatendea Wazazi Waliofariki Waendelee Kupokea Thawabu​

Jamii

‘Amali Za Kuwatendea Wazazi Waliofariki Waendelee Kupokea Thawabu

Alhidaaya.com


‘Amali za mwana Aadam zinakatika baada ya kufariki kwake isipokuwa matatu kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((إذا مات إبن آدم إنقطع عمله إلا من ثلاث: صدقة جارية أو علم ينتفع به أو ولدٌ صالح يدعوا له)) مسلم
((Anapokufa mja, hukatika amali zake zote isipokuwa mambo matatu, swadaqah inayoendelea, au elimu yenye kunufaikiwa, au mtoto mwema anayemuombea)) [Muslim]

Lakini Muislamu anaweza kuendelea kuwatendea wema wazazi wake wawili kwa ‘amali nyenginezo ambazo zimethibiti kuwa thawabu zake zinawafikia kama ifuatavyo:


1-Kuwaombea du’aa na kuwaombea maghfirah:

عن أبي أسيد مالك بن ربيعة رضي الله عنه قال: بينا نحن جلوس عند رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا جاءه رجل من بني سلمة فقال يا رسول الله هل بقي من بر أبوي شيء أبرهما به بعد موتهما ؟ قال: ((نعم! الصلاة عليهما والاستغفار لهما وإنفاذ عهدهما من بعدهما وصلة الرحم التي لا توصل إلا بهما وإكرام صديقهما)) رواه ابن حبان في صحيحه أبو داود وابن ماجه
Kutoka kwa Abuu Asyad Maalik bin Rabiy’ah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Tulipokuwa tumekaa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja mtu kutoka [kabila la] Bani Salamah akasema: Ee Rasuli Allaah, je, kuna kilichobakia katika wema ninaoweza kuwafanyia wazazi wangu baada ya kifo chao? Akasema: ((Naam! Kuwaombea du’aa, kuwaombea maghfirah, kuwalipa deni zao, na kuunga ukoo ambao hauungiki ila kutokana nao, na kuwakirimu rafiki zao)) [Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake, Abu Daawuwd na Ibn Maajah]


Kuwaombea Maghfirah Ni Kupandishwa Kwao Daraja Ya Jannah (Peponi):

عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : قال رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْه ِ وَ سَلَّمَ: ((إِنَّ الرَّجُلَ لَتُرْفَعُ دَرَجَتُهُ فِي الْجَنَّةِ فَيَقُولُ : أَنَّى هَذَا ؟ فَيُقَالُ :باسْتِغْفَارِ وَلَدِكَ لَكَ)) لإمام أحمد و في سنن ابن ماجة أيضاً بإسنادٍ صحيح
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mtu hupandishwa daraja yake Jannah (Peponi). Kisha huuliza: Kwa ajili ya nini? [huku kupandishwa kwangu daraja?] Huambiwa: Kwa ajili ya kuombewa maghfirah na mtoto wako)) [Ahmad, na katika Sunan Ibn Maajah ikiwa na isnaad Swahiyh]

Miongoni mwa du’aa za kuwaombea ni zilizotajwa katika kauli za Allaah ('Azza wa Jalla)

رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾
Rabb wangu! Warehemu kama walivyonilea udogoni. [Al-Israa: 24]


رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾
Rabb wetu! Nighufurie na wazazi wangu wawili na Waumini Siku itakayosimama hesabu. [Ibraahiym: 41]

Katika Sunnah wanaposaliwa Swalaah ya Janaazah:

Maiti mwanamume:

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُ وَارْحَمْـه، وَعافِهِ وَاعْفُ عَنْـه، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـه، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَه، وَاغْسِلْـهُ بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِ مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُ داراً خَـيْراً مِنْ دارِه، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـه، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِه، وَأَدْخِـلْهُ الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُ مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار
Eee Allaah, Mghufurie na Mrehemu, na Muafu na Msamehe na Mtukuze kushuka kwake (kaburini) na Mpanulie kuingia kwake, na Muoshe na maji na kwa theluji na barafu na Mtakase na makosa kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na Muingize Jannah (Peponi) na Mkinge na adhabu ya kaburi na adhabu ya moto.

Maiti mwanamke:

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُا وَارْحَمْـها، وَعافِهاِ وَاعْفُ عَنْـها، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـها، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَها، وَاغْسِلْـهُا بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِا مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُا داراً خَـيْراً مِنْ دارِها، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـها، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِها، وَأَدْخِـلْهُا الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُا مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار

Kuwaombea Wazazi Wawili:

اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُما وَارْحَمْـهما، وَعافِهِما وَاعْفُ عَنْـهما، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـهما، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَهما، وَاغْسِلْـهُما بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِما مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُما داراً خَـيْراً مِنْ دارِهما، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـهما، وأَزَوْاجَـاً خَـيْراً مِنْ اَزْوَاجِهِما وَأَدْخِـلْهُما الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُما مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار



2. Kuwalipia Deni La Swawm:

Kuwalipia deni la Swawm ikiwa ni la fardhi (Ramadhwaan) au Swawm ya nadhiri au ya kafara. Ama ikiwa amefariki kabla ya kumalizika Ramadhwaan na amewahi kufunga siku za nyuma, hakuna haja kumlipia:

عن ابن عباس رضي الله عنهما ، قال :جاء رجل إلى النبي صلى الله عليه و سلم فقال : يا رسول الله إن أمي ماتت، و عليها صوم شهر أفأقضيه عنها ؟ قال : (( لو كان على أمك دين أكنت قاضيه عنها ؟)) قال : نعم. قال: (( فدين الله أحق أن يُقضى)) البخاري و مسلم
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Ee Rasuli wa Allaah, Mama yangu amefariki naye ameacha deni la mwezi la Swawm, je nimlipie? Akasema: ((Je angelikuwa mama yako ana deni [la fedha] ungelimlipia?)) Akajibu: Ndio. Akasema ((Basi deni la Allaah lina haki zaidi ya kulipwa)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na pia:

عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قال رسول الله صلى الله عليه و سلّم: ((من مات و عليه صيامٌ صام عنه وليُّه)) البخاري و مسلم
Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Aliyefariki akiwa na [deni la] Swawm, walii wake amfungie)) [Al-Bukhaariy na Muslim]


3-Kuwafanyia Hajj Ikiwa Hawakufanya Au Kuwafanyia ‘Umrah:

عن ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما أَنَّ امْرَأَةً جَاءَتْ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ، فَقَالَتْ : إِنَّ أُمِّي نَذَرَتْ أَنْ تَحُجَّ ، فَمَاتَتْ قَبْلَ أَنْ تَحُجَّ ، أَفَأَحُجُّ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ ، حُجِّي عَنْهَا أَرَأَيْتِ لَوْ كَانَ عَلَى أُمِّكِ دَيْنٌ أَكُنْتِ قَاضِيَتَهُ ؟ )) قَالَتْ : نَعَمْ . فَقَالَ : ((اقْضُوا اللَّهَ الَّذِي لَهُ ، فَإِنَّ اللَّهَ أَحَقُّ بِالْوَفَاءِ )) رواه البخاري
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Alikuja mwanamke kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Nina mama ambaye aliweka nadhiri kuwa atahiji, akafariki kabla ya kuhiji, je nimhijie? Akasema: ((Ndio, mhijie je ingelikuwa mama yako ana deni ungelimlipia?)) Akasema: Ndio. Akasema: ((Mkidhieni Allaah (deni) Lake, kwani Allaah Ana Haki zaidi kutimiziwa)) [Al-Bukhaariy]

Pia:

عن عَبْد اللَّهِ بْن بُرَيْدَةَ عَنْ أَبِيهِ رَضِي اللَّه عَنْهما ، قَالَ : بَيْنَما أَنَا جَالِسٌ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ، إِذْ أَتَتْهُ امْرَأَةٌ ، فَقَالَتْ: إِنِّي تَصَدَّقْتُ عَلَى أُمِّي بِجَارِيَةٍ ، وَ إِنَّهَا مَاتَتْ . فَقَالَ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : (( وَجَبَ أَجْرُكِ وَ رَدَّهَا عَلَيْكِ الْمِيرَاثُ)) قَالَتْ : يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ كَانَ عَلَيْهَا صَوْمُ شَهْرٍ أفأصُومُ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((صُومِي عَنْهَا)) قَالَتْ : إِنَّهَا لَمْ تَحُجَّ قَطُّ ، أَفَأَحُجُّ عَنْهَا؟ قَالَ: ((حُجِّي عَنْهَا)) مسلم
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah kutoka kwa baba yake (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Nilipokuwa nimekaa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja mwanamke akasema: Nimemtolea mama yangu swadaqah ya kijakazi. Naye amefariki. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Umewajibika kupata ujira na mirathi itakurudia)). Akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, alikuwa ana deni la mwezi la Swawm, je nimfungie?” Akasema: ((Mfungie)). Akasema: “Yeye hakuwahi kuhiji, je nimhijie?” Akasema: ((Mhijie)) [Muslim]


4-Kuwatolea Swadaqah:

عن أمّ المؤمنين عَائِشَةَ رَضِي اللَّه عَنْهَا ، أَنَّ رَجُلاً قَالَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ أُمِّي افْتُلِتَتْ نَفْسُهَا ( أي ماتت فجأةً ) وَ أَظُنُّهَا لَوْ تَكَلَّمَتْ تَصَدَّقَتْ ، فَهَلْ لَهَا أَجْرٌ إِنْ تَصَدَّقْتُ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ)) البخاري
Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Mtu mmoja alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Mama yangu imesokoteka nafsi yake [kwa maana amefariki ghafla] na nadhani kama alizungumza kutaka kutoa swadaqah. Je, atapata ujira nikimtolea swadaqah?” Akasema: ((Ndio)) [Al-Bukhaariy]

Pia

عن ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِي اللَّه عَنْهمَا ، أَنَّ سَعدَ بْنَ عُبَادَةَ رَضِي اللَّه عَنْهما تُوُفِّيَتْ أُمُّهُ وَ هُوَ غَائِبٌ عَنْهَا فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ أُمِّي تُوُفِّيَتْ وَ أَنَا غَائِبٌ عَنْهَا أَيَنْفَعُهَا شَيْءٌ إِنْ تَصَدَّقْتُ بِهِ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ )) قَالَ: فَإِنِّي أُشْهِدُكَ أَنَّ حَائِطِيَ الْمِخْرَافَ ( اسم لبستان كان له) صَدَقَة ٌ عَلَيْهَا .- البخاري
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Sa’ad bin ‘Ubaadah (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) alifiwa na mama yake naye alikuwa hayupo akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, Mama yangu amefariki nami sikuweko. Je, itamfaa lolote nikimtolea swadaqah?” Akasema: ((Ndio)) Akasema: “Basi nashuhudia kwako kwamba ukuta wangu wa al-Mikhraaf [jina la bustani yake] ni swadaqah kwa ajili yake.” [Al-Bukhaariy]

Pia,

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَجُلاً قَالَ لِلنَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ أَبِي مَاتَ ، وَ تَرَكَ مَالاً وَ لَمْ يُوصِ ، فَهَلْ يُكَفِّرُ عَنْهُ أَنْ أَتَصَدَّقَ عَنْهُ ؟ قَالَ : (( نَعَمْ)) روى مسلم و ابن ماجة و النسائي
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtu mmoja alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Baba yangu amefariki na ameacha mali wala hakuiusia. Je, itakuwa kafara yake (atapata ujira na malipo) nikimtolea swadaqah kwayo?” Akasema: ((Ndio)) [Muslim, Ibn Maajah na an-Nasaaiy


5-Kuunga Ukoo Ambao Hauungiki Ila Kutokana Na Wao:

Dalili ni Hadiyth iliyotangulia katika nukta ya kwanza ambayo imetaja:
((na kuunga ukoo ambao hauungiki ila kutokana nao))

Ni kuwasiliana na ndugu, jamaa wenye uhusiano wa damu, wa karibu na wa mbali, mfano ‘ammu (kaka wa baba) ‘ammat (shangazi), khaal (kaka wa mama), khaalat (mama mdogo au mkubwa), watoto wao wote, bibi wa baba, bibi wa mama na wanaouhusiana wote kwa damu kwa kila upande.

Tutamube kwamba kuunga undugu wa uhusiano wa damu ni kitendo ambacho kimesisitizwa sana. Dalili zake zinapatikana katika Qur-aan na Sunnah kwamba mwenye kukataa kuunga undugu amelaaniwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), rizki yake itadhikika, umri wake utapunguka, Allaah ('Azza wa Jalla) Atamkatilia mbali na hatoingia Jannah (Peponi).



6-Kuwakirimu Rafiki Zao

عن عبد الله بن دينار عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما أن رجلا من الأعراب لقيه بطريق مكة فسلم عليه عبد الله بن عمر وحمله على حمار كان يركبه وأعطاه عمامة كانت على رأسه . قال ابن دينار : فقلنا أصلحك الله إنهم الأعراب وهم يرضون باليسير , فقال عبد الله بن عمر إن أبا هذا كان ودا لعمر بن الخطاب وإني سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: (( وإن أبر البر صلة الولد أهل ود أبيه )) مسلم
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Diynaar na kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba bedui mmoja alikutana naye njiani akielekea Makkah, akamsalimia ‘Abdullaah bin ‘Umar kisha akampakia juu ya punda aliyekuwa amempanda akavua kilemba chake na kumpa. Akasema Ibn Diynaar: Tukasema: “Allaah Akuwekee vizuri. Hao ni mabedui nao wanaridhika na kichache.” ‘Abdullaah bin ‘Umar akasema: “Baba yake huyu alikuwa mpenzi wa ‘Umar ibnul Khattwwaab [Baba yangu] nami nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Kitendo chema kabisa ni mtoto kumpenda (kuungana na) rafiki wa baba)) [Muslim]

Na pia:

عن أبي بردة قال: قدمت المدينة فأتاني عبد الله بن عمر فقال أتدري لم أتيتك ؟ قال قلت لا . قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((من أحب أن يصل أباه في قبره فليصل إخوان أبيه)) وأنه كان بين أبي عمر وبين أبيك إخاء وود فأحببت أن أصل ذاك - ابن حبان في صحيحه
Pia kutoka kwa Abuu Bardah ambaye amesema: Nilikuwa naelekea Madiynah akanijia ‘Abdullaah bin ‘Umar akasema: “Je, unajua kwa nini nimekujia?” Akasema: Nikasema: “Hapana!” Akasema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Anayependa kuungana na baba yake katika kaburi lake basi awasiliane na ndugu zake (rafiki zake) baba yake)) Na baina ya baba yangu ‘Umar na baba yako walikuwa na undugu wa mapenzi, basi nimependa kuwaunga.” [Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake]
 
Jamii
Amana Katika Uislamu

www.alhidaaya.com


Baada ya kumhimidi na kumshukuru Allaah Aliyetukuka Ambaye Ametuneemesha na fursa hii ya kukutana ili kunasihiana na kukumbushana. Swalah na salamu zimfikiye hashimu, Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam), Maswahaba zake, ahli zake na Waumini wote mpaka Siku ya Qiyaamah.

Maudhui yetu ya leo ni muhimu sana katika zama zetu za leo na matatizo mengi tunakumbana nayo kwa sababu ya kukosekana. Hiyo ni maudhui ya amana.

Huenda mmoja wetu akauliza: Amana ina maana gani katika Dini yetu ya kweli? Suala hilo limejibiwa na Imaam al-Qurtwubiy (Allaah Amrehemu) pale aliposema: Amana inajumlisha shughuli zote za Kidini. Amana ndio faradhi ambazo kwayo Allaah Aliyetukuka Amewapatia waja Wake.
Na wametofautiana katika tafsili, hivyo kukawa na kauli nyingi. Baadhi yake ni:

Pakasemwa: Hiyo ni kuweka amana ya mali na nyengineyo.

Na pakasemwa: Katika kila faradhi, na iliyo nzito ni amana ya mali.

Na pakasemwa: Ni katika amana, kwa alichoaminiwa mwanamke kwa utupu wake, asiitumie katika uzinifu.

Na wakasema wengineo: Kuoga josho la janaba ni katika amana.

Na pakasemwa: Amana ni Swalah, pia Swawm na kuoga josho la janaba.

Na pakasemwa: Hana Imani asiye muaminifu.

Na pakasemwa: Hii ni amana ambayo Allaah Aliyetukuka Aliipatia mbingu, ardhi, majabali na viumbe katika dalili za Uungu Wake.

Na ametaja Ibn al-Jawziy amenukuu kutoka kwa baadhi ya Wafasiri wa Qur-aan kuhusu amana katika Qur-aani Tukufu imegawanyika sehemu tatu:


Ya kwanza: Ni Faradhi, na miongoni mwayo ni kauli ya Aliyetukuka:

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَخُونُواْ اللّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُواْ أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ﴾ (الأنفال 27).

“Enyi walioamini! Msimfanyie khiyana Allaah na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua” (8: 27).


Ya pili: Kurudisha, na miongoni mwayo ni kauli ya Aliyetukuka:

﴿إِنَّ اللّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤدُّواْ الأَمَانَاتِ إِلَى أَهْلِهَا﴾ (النساء 58).

“Hakika Allaah Anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe” (4: 58).



Ya tatu:
Ni utwahara na usafi, na miongoni ni kauli ya Aliyetukuka:

﴿إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ ﴾ (القصص 26).

“Hakika mbora wa kumuajiri ni mwenye nguvu na muaminifu” (28: 26).


Ndugu zangu katika Imani, jueni kuwa amana ni sifa miongoni mwa sifa za Manabii na Waumini wema kama Alivyotuambia Allaah Aliyetukuka katika Kitabu Chake.

Amesema Aliyetukuka kuhusu Nuwh (‘Alayhis Salaam):

﴿كَذَّبَتْ قَوْمُ نُوحٍ الْمُرْسَلِينَ. إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ. إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ. فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ﴾ (الشعراء 105 – 108).

“Kaumu ya Nuwh waliwakadhibisha Mitume. Alipowaambia ndugu yao, Nuwh: Je, Hamuwi wachaji? Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. Basi Mcheni Allaah, na nitiini mimi” (26: 105 – 108).

Na kuhusu Nabii Huwd (‘Alayhis Salaam) Anatuambia Aliyetukuka:

﴿كَذَّبَتْ عَادٌ الْمُرْسَلِينَ. إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ. إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ. فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ﴾ (الشعراء 123 – 126).

“Kaumu ya Huwd waliwakadhibisha Mitume. Alipowaambia ndugu yao, Huwd: Je, Hamuwi wachaji? Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. Basi Mcheni Allaah, na nitiini mimi” (26: 123 – 126).

Na kuhusu Muwsaa (‘Alayhis Salaam), Anasema Aliyetukuka:

﴿قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ﴾ (القصص 26).

“Akasema mmoja katika wale wanawake: Ee baba yetu! Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumuajiri ni mwenye nguvu na muaminifu” (28: 26).

Na kuhusu Yuwsuf (‘Alayhis Salaam), Anasema Aliyetukuka:

﴿وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ أَسْتَخْلِصْهُ لِنَفْسِي فَلَمَّا كَلَّمَهُ قَالَ إِنَّكَ الْيَوْمَ لَدَيْنَا مِكِينٌ أَمِينٌ﴾ (يوسف 54).

“Na mfalme akasema: “Nileteeni (Yuwsuf) nimteue mahsusi kwangu.” Basi aliposema naye, akasema: “Hakika wewe leo kwetu umetamakani kwa cheo na umekuwa muaminiwa.” (12: 54).

Ama Waumini watendao mema, Allaah Aliyetukuka Anatuambia:

﴿وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ﴾ (المؤمنون 8).

“Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao” (23: 8).


Allaah Aliyetukuka Ametuamuru kuwa waaminifu na kutekeleza amana kama Alivyotuambia:

﴿وَإِن كُنتُمْ عَلَى سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُواْ كَاتِبًا فَرِهَانٌ مَّقْبُوضَةٌ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللّهَ رَبَّهُ وَلاَ تَكْتُمُواْ الشَّهَادَةَ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ وَاللّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ﴾ (البقرة 283).

“Na mkiwa safarini na hamkumpata mwandishi, basi (mdai) akabidhiwe rahani. Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah, Rabb wake; na wala msifiche ushahidi; na mwenye kuuficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allaah kwa mnayoyatenda ni Mjuzi.” (2: 283).

Hapa tunapata kuwa hata katika safari ambapo hakuna shahidi, Muislamu anatakiwa awe muaminifu na asimkhini yeyote kwa chochote kile. Na shahidi naye ikiwa atakuwepo anafaa asifiche ushahidi kwani kuficha ni utovu wa amana. Na Muislamu anafaa afahamu kuwa yote anayofanya yanafahamika kwa Allaah Aliyetukuka, hivyo kufanya khiyana kutamweka mahali pabaya. Na Amesema Aliyetukuka:

﴿إِنَّ اللّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤدُّواْ الأَمَانَاتِ إِلَى أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُواْ بِالْعَدْلِ إِنَّ اللّهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ إِنَّ اللّهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا﴾ (النساء 58).

“Hakika Allaah Anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayo kuwaidhini Allaah ni mazuri sana. Hakika Allaah ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona” (4: 58).

Pia Mtume (صلى الله عليه وسلم) ametuamuru kutekeleza amana katika hali zote na hilo lilifahamika hata kwa wasikuwa Waislamu wa zama zake hata wa sasa pia. Imepokewa na ‘Ubaydullaah bin ‘Abdillaah kuwa ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) alimpasha habari:
أخبرني أبو سفيان أن هرقل قال له سألتك ماذا يأمركم؟ فزعمت أنه أمركم بالصلاة والصدق والعفاف والوفاء بالعهد وأداء الأمانة. قال: وهذه صفة نبي.

Alinieleza Abu Sufyaan (رضي الله عنه) kuwa Heraclius (Hiraql) alimwambia nilikuuliza (huyu Mtume) anawaamuru nini? Ukadai kuwa anawaamuru msimamishe Swalah, muwe wakweli, muwe safi (siozini), kutekeleza ahadi na amana. Akasema: Hizo ni sifa za Nabii (Al-Bukhaariy).

Enyi ndugu zangu watukufu, khiyana ya amana ni miongoni mwa alama za unafiki. Ametufahamisha hayo mkweli, mwenye kusadikiwa katika Hadith ya ‘Abdullaah bin ‘Amr bin al-‘Aasw (رضي الله عنهما) kuwa Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

}أربع من كن فيه كان منافقا خالصا ومن كانت فيه خصلة منهن كانت فيه خصلة من النفاق حتى يدعها: إذا اؤتمن خان وإذا حدث كذب وإذا عاهد غدر وإذا خاصم فجر{ متفق عليه.

“Mtu yeyote akiwa na mambo manne atakuwa mnafiki hasa (kamili), na kama atakuwa na moja katika hayo manne atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aliache. Akiaminiwa hufanya hiyana; na akizungumza anaongopa; na apotoa ahadi huvunja na anapogombana anaiacha haki na kuwa jeuri” (Al-Bukhaariy na Muslim).

Na amesema Abu Hurayrah (رضي الله عنه):

بينما النبي صلى الله عليه وسلم في مجلس يحدث القوم جاءه أعرابي فقال: متى الساعة؟ فمضى رسول الله صلى الله عليه وسلم يحدث فقال بعض القوم سمع ما قال فكره ما قال وقال بعضهم بل لم يسمع حتى إذا قضى حديثه قال: }أين السائل عن الساعة؟{ قال: ها أنا يا رسول الله قال: }إذا ضيعت الأمانة فانتظر الساعة{ قال: كيف إضاعتها؟ قال: }إذا وسد الأمر إلى غير أهله فانتظر الساعة{

Alipokuwa Mtume (صلى الله عليه وسلم) alipokuwa anakhutubia kikao cha watu, mara akaja Mbedui na kuuliza: “Qiyaamah kitakuwa lini?” Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akaendelea na mazungumzo yake. Hapo wakasema baadhi ya watu: “Amesikia alichoulizwa, lakini akachukia kukatizwa”. Na wengine wakasema: “Bali hajasikia”, mpaka alipomaliza mazungumzo yake, akasema: “Yuwapi muulizaji kuhusu Qiyaamah?” Akajibu: “Nipo hapa, ewe Mtume wa Allaah”. Akasema: “Inapopotezwa amana (kukawa na khiyana) basi ngojeeni Qiyaamah”. Akaulizwa: “Na itapotea vipi?” Akasema: “Pindi uongozi unapopatiwa watu wasiostahiki basi ngojeeni Qiyaamah” (Al-Bukhaariy).

Mvurugiko na machafuko mengi yanayotokea na yanayoendelea kutokea hivi sasa ni kwa sababu ya khiyana na kuchaguliwa kwa wasiofaa katika madaraka tofauti ya uongozi. Inabidi kama Waislamu tushikane barabara na muongozo wa Dini yetu Tukufu, miongoni mwayo ikiwa ni kutekeleza amana na kuwarudishia wanaostahiki.

Na kupotea kwa amana pia kumetabiriwa na Mtume (صلى الله عليه وسلم) kwa kiasi ambacho katika kijiji au mji hakutakuwa na waaminifu wenye kuchunga na kudhibiti amana ila wachache. Allaah Aliyetukuka Atujaalie tuwe wenye kuichunga amana.

Pia tufahamu kuwa yule mwenye sifa hiyo ya khiyana hatokuwa ni mwenye kutazamwa Siku ya Qiyaamah na Allaah Aliyetukuka. Kila mmoja ajiulize, Ikiwa Hutotazamwa na Allaah Aliyetukuka Utakuwa Wapi? Kila mmoja wetu atajijibu mwenyewe. Imepokewa na Abu Hurayrah (رضي الله عنه) kuwa Mtume (صلى الله عليه وسلم) amesema:

(قال الله ثلاثة أنا خصمهم يوم القيامة رجل أعطى بي ثم غدر ورجل باع حرا فأكل ثمنه ورجل استأجر أجيرا فاستوفى منه ولم يعطه أجره) رواه البخاري.

“Allaah Anasema: Nitakuwa dhidi ya (watu) watatu Siku Ya Qiyaamah; mtu anayefunga fungamano kwa jina langu kisha akafanya usaliti, na anayemuuza mtu huru (kama mtumwa) na kula thamani yake, na anayemuajiri mtu akafanyiwa kazi zake kwa ukamilifu lakini hamlipi ujira wake.” (Al-Bukhaariy).
 

Ardhi Iliyosahaulika​

Jamii

Ardhi Iliyosahaulika

Muhammad Al-Ma'awy

Alhidaaya.com

Utangulizi

Ardhi hii iliyosahaulika ilikuwa na migongano mingi sana baina ya staarabu tofauti, baina ya Uislamu na Ukafiri, baina ya haki na batili na baina ya Tawhiyd na Shirki. Migongano hii ilikuwa ya kutumia silaha au baridi kwa kuelezea, kujadiliana na kulingania. Mgongano wa mwisho ni ule ulioletwa na maandishi ya Mkataba wa Sykes – Picot ulioandikwa 1916 baina ya Uingereza na Ufaransa.Ardhi hii inatajwa ana lakini haipo kwenye ramani na imesahaulika sana na hususan sisi Waislamu. Allaah, Nabiy Wake na historia imetupatia sifa tofauti ya ardhi hii. Sifa hizi zimefanya kila taifa kuigombea.

Itikadi Ya Muislamu Juu Ya Ardhi Hii

1. Ardhi Tukufu:

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

يَا قَوْمِ ادْخُلُوا الْأَرْضَ الْمُقَدَّسَةَ الَّتِي كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ وَلَا تَرْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ ﴿٢١﴾
Enyi kaumu yangu! Ingieni ardhi iliyotakaswa ambayo Amekuandikieni Allaah kwenu, na wala msirudi kugeuka nyuma kukimbia (kupigana) hapo mtageuka kuwa wenye kukhasirika.
[Al-Maaidah:21]

Je, hii aya imewapatia Mayahudi urithi wa moja kwa moja kwenye ardhi ya Palestina? Je, huu ni urithi wa majukumu au wa dam?
Allaah Anasema yafuatayo kuhusu Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam):

وَإِذِ ابْتَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ ۖ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ ﴿١٢٤﴾
Na pindi Alipojaribiwa Ibraahiym na Rabb wake kwa amri nyingi, naye akazitimiza. Akasema: Hakika Mimi Nakufanya uwe Imaam kwa watu. (Ibraahiym) Akasema: Na katika kizazi changu? (Allaah) Akasema: Haiwafikii ahadi Yangu madhalimu. [Al-Baqarah:124]

Kuna dhulma gani kuliko ya Mayahudi kuwafanyia ndugu zetu Palestina. Hususan angazia yaliyotokea kuanzia tarehe 29 Machi 2002 mpaka wakati wetu huu wa sasa.

2. Ardhi Iliyobarikiwa:

Ardhi hii imebarikiwa kiroho na kirutba. Ni jambo hili ndilo lililowafanya watu na staarabu tofauti kuigombania. Agano la Kale inatuhadithia ya kuwa ardhi hii ilibubujika asali na maziwa. (Hesabu, 13:27) Na katika kitabu cha Hesabu Sura ya 13 inatueleza kuwa majasusi wa Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam) walipata humo matunda ya makudhumani, tini na zaituni ambayo yalikuwa makubwa na kila tunda kubebwa na watu wawili. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ ... ﴿١﴾
"...mpaka Al-Masjid Al-Aqswaa ambao Tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake;...."
[Al-Israa:1].

Lakini ardhi yote ya Palestina imebarikiwa. Allaah Anasema:

وَنَجَّيْنَاهُ وَلُوطًا إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا لِلْعَالَمِينَ ﴿٧١﴾
Na Tukamuokoa na Luutw kuelekea ardhi ambayo Tumeibariki humo kwa walimwengu.[Al-Anbiyaa: 71]

3. Ardhi ya Rusuli:

Katika ardhi hii Mitume tofauti ima walihamia au walizaliwa na kuishi utotoni mwao au walifanya Da’wah na kuzikwa katika sehemu hii au walizuru japokuwa kwa muda mfupi. Miongoni mwao ni Manabii kama Ibraahiym, Ismaa’iyl, Is-haaq, Ya’quub, Luut, Daawuud, Sulaymaan, Zakariyyaa, Yahyaa, ‘Iysaa na Muhammad.

4. Ardhi ya Wahyi:

Wahyi ndio uliokuwa na mpaka sasa unajenga ustaarabu na utamaduni za watu tofauti. Miongoni mwa Vitabu vilivyoteremshwa kutoka kwa Allaah katika ardhi hii ni Suhuf za Nabiy Ibraahiym, Zaburi ya Nabii Daawuud, Injiyl ya Nabiy ‘Iysa na pia baadhi ya aya katika Suwrah Al- Zukhruf katika Qur-aan.

5. Ardhi ya Israa Wal Mi’iraaj:

Hii ni safari ya usiku aliyopelekwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Israa ni safari ya kutoka Msikiti Mtukufu wa Makkah mpaka Baytul Maqdis. Mi’iraaj ni ngazi ya kutoka Baytul Maqdis mpaka wingu wa saba. Natija mzuri kabisa ya safari hii ni kufaridhiwa Ummah huu Swalaah tano, mchana na usiku. Swalaah ya kwanza ya jama’a h ilifanyika katika Msikiti Mtukufu wa ‘Aqswaaa ambapo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwasalisha Rusuli wote (‘Alayhim-salaam). hii inatukumbusha kila tunaposwali mahusiano yetu ya karibu sana na ardhi hii.

6. Ardhi ya Msikiti wa ‘Aqswaa:

Msikiti huu ulikuwa kibla cha kwanza kwa Waislamu. Kwa miezi 16 au 18 baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake kuhamia Madiynah walikuwa wakielekeza nyuso zao kwa upande wa Baytul Maqdis mpaka Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Alipokibadilisha kwa kuteremsha aya ya 144 na 150 ya Suwrah Al-Baqarah. Msikiti huu ni wa tatu kwa utukufu baada ya Msikiti Mtukufu wa Makkah na Msikiti wa Nabiy Muhammad Madiynah. Swalaah moja katika Msikiti huu ina thawabu mara 500 kuliko Misikiti mingine ila Msikiti wa Makkah na Madiynah. (At-Twabaraaniy)
Kwa hivyo kila Muislamu ulimwenguni ana hamu sana ya kwenda kuuzuru na kuswali ndani yake. Lakini je, tunaujua Msikiti huu ni upi? Wengi wetu tunaujua ule Msikiti ambao unachapishwa katika magazeti na majarida, kuonyeshwa katika televisheni, kuwepo kwenye makalenda, picha zinazotundikwa majumbani, n.k. Huu Msikiti ninaouzungumzia una sifa ya kipekee na unajulikana kwa kuwa na Qubba rangi ya njano au ya dhahabu. Lakini ndugu zangu wapendwa, Masjidul ‘Aqswaa ni eneo lote ambalo lipo katika kuta nne ikiwemo Masjid Qubbatus Swakhraa (Msikiti wa Qubba ya Jabali au Dome of the Rock), Masjidul ‘Aqswaa (huu ulijengwa baada ya ule wa Qubbatus Swakhraa), Masjid Marwani, miti ambayo imo ndani, shule na kuta zenyewe. Sehemu hii yote ni tukufu na ndio Msikiti wa ‘Aqswaa bila ya tofauti yoyote baina ya wanavyuoni wote wa Kiislamu.

7. Ardhi ya Maswahaba:

Swahaba watukufu waliipigania ardhi hii na kuweza baada ya taufiki ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kuitawala. Swahaba 200 walioshiriki katika Vita vya Badr walikuwa katika msitari wa mbele wa kuuteka mji wa al-Quds. Takribani makaburi 18,000 ya Swahaba yanapatikana katika ardhi hii.

8. Ardhi ya Jihadi, Ribati na Vita vya Mwisho:

Vita vitagavyopiganwa baina ya Waislamu upande mmoja na Mayahudi upande mwengine. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatueleza:
"Qiyaama hakitofika mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi. Mayahudi watakuwa wanauliwa na kuwafanya wajifiche nyuma ya miti na mawe ambayo itasema: ‘Ee Muislamu! Ee mja wa Allaah! Njoo nyuma yangu yupo Yahudi umuue …" [Al-Bukhaariy na Muslim]

Hitimisho
Ndugu zetu wanauliwa kila saa na dakika. Je, tufanyeje ili kuwasaidia ndugu zetu katika ardhi hii yetu?
1. Tumjue Allaah vilivyo na tuongeze Iymaan yetu kwa kufuata mafundisho ya Uislamu na kuacha makatazo yake. Tujipinde na 'Ibaadah.

2. Tuanze kususia bidhaa za Israeli na Marekani ambaye ni rafiki yake wa chanda na pete na wa hali na mali. Kwa mfano tusinunue soda za kampuni ya coca-cola na pepsi cola, rangi ya kiwi na bidhaa nyenginezo. Kampuni za coca-cola na pepsi zinamsaidia vilivyo Israeli, pamoja na maduka ya Sainsbury, Debenham, Marks & Spenser na kula kwenye kwenye migahawa ya McDonald, Kentucky na zingine nyingi ambazo ni nyingi sana kuziorodhesha hapa.

3. Tusiwasahau ndugu zetu katika Du’aa hata baada ya kujiombea nafsi zetu hususan tunapokuwa katika sijdah, tunaposafiri, tunapofunga, tunapoinuka usiku kwa Swalaah ya Tahajjud, n.k.

Kumbukeni Ni Jihadi Pekee Inayoweza Kuikomboa Ardhi Hii
 
Hutuba ya Ijumaa: Kuepukana na Riya (Kujionyesha katika Ibada)

Khutba ya Kwanza:

Alhamdulillahi rabbil ‘aalamin. Tunamshukuru Allah (S.W) kwa kutujaalia kuwa hai na kutuwezesha kufika siku hii tukufu ya Ijumaa. Tunamswalia Mtume Muhammad (S.A.W), maswahaba wake, familia yake na wote waliomfuata kwa wema mpaka siku ya Qiyama.

Enyi Waumini! Leo tuzungumzie jambo muhimu sana katika maisha ya Muumini – kujiepusha na Riya.

Riya ni kufanya ibada au matendo mema kwa ajili ya kuonekana na kusifiwa na watu, si kwa ajili ya Allah. Hii ni miongoni mwa shirki ndogo lakini madhara yake ni makubwa mno.

Allah anasema katika Qur’an (Surat Al-Baqarah, 2:264):
“Enyi mlioamini! Msivue thawabu zenu kwa kutoa sadaka kwa ajili ya kujionyesha kwa watu…”

Mtume Muhammad (S.A.W) amesema:
“Hakika jambo ninalowaogopa sana kwa ajili yenu ni shirki ndogo.” Wakasema: Ewe Mtume wa Allah, shirki ndogo ni ipi? Akasema: Riya.” (Ahmad)

Muumini wa kweli anatakiwa kuficha ibada zake iwezekanavyo, au kuifanya kwa namna ya unyenyekevu bila kutafuta sifa, kama alivyokuwa Mtume na maswahaba zake.

Khutba ya Pili:

Enyi Waumini! Kumbukeni kuwa matendo hayatakubalika kwa Allah isipokuwa yafanywe kwa ikhlas (unyofu wa nia). Mtume (S.A.W) amesema:
“Hakika matendo yote yanategemea nia, na kila mtu atalipwa kulingana na nia yake.” (Bukhari & Muslim)

Tujiepushe na matendo ya kutafuta sifa mitandaoni, misikitini, au kwenye jamii, tukumbuke kuwa Allah anaona nia ya kila mmoja.

Tusome dua ya kujikinga na Riya kama alivyofundisha Mtume:
"Allahumma inni a’udhu bika an ushrika bika wa ana a’lamu, wa astaghfiruka lima la a’lamu."

Hitimisho:
Tuombe kwa Allah atujaalie tufanye ibada zetu kwa ajili Yake pekee. Atulinde na shirki ndogo ya riya, na atupokelee matendo yetu mema. Ameen.

Wasalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh.
 
TAREHE YA KIISLAMU

ASALAM ALEYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH

LEO NI SIKU YA JUMAMOSI.

Saudia 24 Muharram Mfungo Nne 1447H

Zanzibar/Oman 23 Muharram Mfungo Nne 1446H

Milladiyya 19/07/2025

UJUMBE WA LEO

TUCHUNGE ATHARI ZA MATENDO YETU

Athari Za Matendo Yetu Ni Zenye Kurekodiwa Allah Mtukufu anatujulisha Zingatia

إنا نحن نحيي الموت ونكتب ما قدموا وآثارهم وكل شيء أحصيناه في إمام مبين

Hakika Sisi tutahuisha Wafu, Na Tutaandika Yale Waliyo Yatanguliza Na Athari Zao, Na Kila Kitu Kitarekodiwa barabara Katika daftari Waziwazi

Wapo Waandishi Juu Yetu Wenye Kuyajua Yote tunayoyatenda Zingatia:---

وإن عليكم لحافظين

Na hakika Juu Yenu bila Shaka Kuna Wenye Kuhifadhi Na (Kuchunga)

كراما كاتبين

Malaika Wawili Wanaoandika Amali Zenu

يتعلمون ما تفعلون

Wanajua Yale Myafanyayo

Tunapaswa Kuchunga Sana Yale tunayoyatenda Ikiwemo Kuwazuria Watu, Kuwasingizia Kwa ambayo hawajayatenda, Kwani Yote Yanarekodiwa Kesho tutayakuta Katika Madaftari Yetu

Swalaa Swalaa Swalaa Aswalatu Khayrun Minannaum, Allah tunakuomba tujaalie Mema Katika Dunia Na Mema Katika Akhera Utulinde Na adhabu

¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥¥
 

Fadhila Za Kumtembelea Mgonjwa​

Jamii

Fadhila Za Kumtembelea Mgonjwa


Alhidaaya.com



1. Kwanza Kabisa Ni Miongoni Mwa Haki Ya Muislamu Kwa Nduguye Muislamu

عن أبي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ خَمْسٌ: رَدُّ السَّلَامِ وَعِيَادَةُ الْمَرِيضِ وَاتِّبَاعُ الْجَنَائِزِ وَإِجَابَةُ الدَّعْوَةِ وَتَشْمِيتُ الْعَاطِسِ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Haki ya Muislamu kwa nduguye Muislamu ni tano: Kujibu Salaam, kumtembelea mgonjwa, kulisindikiza jeneza, kuitikia mwito na kumuombea mwenye kupiga chafya)) [Al-Bukhaariy Muslim]


2. Siku Ya Qiyaamah Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atakuuliza

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يَقُولُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ: يَا ابْنَ آدَمَ مَرِضْتُ فَلَمْ تَعُدْنِي، قَالَ: يَا رَبِّ كَيْفَ أَعُودُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ: أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ عَبْدِي فُلَانًا مَرِضَ فَلَمْ تَعُدْهُ؟ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ لَوْ عُدْتَهُ لَوَجَدْتَنِي عِنْدَهُ؟ يَا ابْنَ آدَمَ، اسْتَطْعَمْتُكَ فَلَمْ تُطْعِمْنِي ، قَالَ: يَا رَبِّ وَكَيْفَ أُطْعِمُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ: أَمَا عَلِمْتَ أَنَّهُ اسْتَطْعَمَكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تُطْعِمْهُ؟ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ لَوْ أَطْعَمْتَهُ لَوَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟ يَا ابْنَ آدَمَ اسْتَسْقَيْتُكَ فَلَمْ تَسْقِنِي، قَالَ: يَا رَبِّ كَيْفَ أَسْقِيكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ اسْتَسْقَاكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تَسْقِهِ، أَمَا إِنَّكَ لَوْ سَقَيْتَهُ وَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟)) مسلم
Kutoka Kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: ((Hakika Allaah ‘Aliyetukuka na Jalali Atasema siku ya Qiyaamah: Ee mwana wa Aadam, Niliumwa na usije kunitembelea? Atasema: Ee Rabb (Mola), vipi nije kukutembelea nawe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Kwani ulijua kuwa mja wangu fulani alikuwa mgonjwa na hukwenda kumtembelea! Hukujua kuwa ungekwenda ungalinikuta Niko pamoja naye? Ee mwana wa Aadam, Nilikuomba chakula na hukunipa. Atasema: Ee Rabb, vipi nitakupa chakula na Wewe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Kwani hukujua kuwa mja wangu fulani alikuomba chakula na hukumpa? Hukujua kuwa ungalimpa chakula ungalikuta hayo (jazaa) kwangu mimi? Ee mwana wa Aadam, nilikuomba maji na hukunipa. Atasema: Ee Rabb, vipi nitakupa maji na Wewe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Mja wangu fulani alikuomba maji na hukumpa. Hukujua kwamba ungalimpa maji ungalikuta hayo (jazaa) Kwangu Mimi)) [Muslim]


3. Malaika Sabini Elfu Wanakuombea Rahmah

Kumtembelea mgonjwa kuna fadhila nyingi tukufu kama zilivyothibiti katika Hadiyth kadhaa mojawapo ni kwamba mwenye kumtembelea mgonjwa huswaliwa na Malaika elfu sabini. Hadiyth ya ‘Aliy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu):

قَالَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِذَا عَادَ الرَّجُلُ أَخَاهُ المُسْلِمَ مَشَى فِي خِرَافَةِ الجَنَّةِ حَتَّى يَجْلِسَ فَإِذَا جَلَسَ غَمَرَتْهُ الرَّحْمَةُ، فَإِنْ كَانَ غُدْوَةً صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُوْنَ أَلْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُمْسِيَ، وَإِنْ كَانَ مَسَاءً صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُوْنَ أَلْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُصْبِحَ)).
Amesema (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mtu anapomtembelea ndugu yake Muislamu mgonjwa, basi hutembelea katika bustani ya Jannah mpaka atakapoketi, na anapoketi hufunikwa na Rahmah ikiwa ni asubuhi wanamtakia Rahmah Malaika sabini elfu mpaka jioni. Na ikiwa ni jioni wanamtakia Rahmah Malaika sabini elfu mpaka asubuhi)) [Swahiyh Ibn Maajah (1/244), Swahiyh At-Tirmidhiy (1/286)]


4. Du’aa Kutakabaliwa

Juu ya hivyo ni fursa kwa Muislamu kuomba du’aa yake itakabaliwe. Aanze kwanza kumwombea mgonjwa du’aa zilizothibiti katika Sunnah kisha ajiombee nafsi yake:

عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ (رضي الله عنها) قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِذَا حَضَرْتُمْ الْمَرِيضَ أَوْ الْمَيِّتَ فَقُولُوا خَيْرًا فَإِنَّ الْملآئِكَةَ يُؤَمِّنُونَ عَلَى مَا تَقُولُونَ)) قَالَتْ: فَلَمَّا مَاتَ أَبُو سَلَمَةَ أَتَيْتُ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ أَبَا سَلَمَةَ قَدْ مَاتَ قَالَ: ((قُولِي: اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي وَلَهُ وَأَعْقِبْنِي مِنْهُ عُقْبَى حَسَنَةً)) قَالَتْ: فَقُلْتُ فَأَعْقَبَنِي اللَّهُ مَنْ هُوَ خَيْرٌ لِي مِنْهُ مُحَمَّدًا (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)
Imepokelewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mnapohudhuria mgonjwa au maiti basi semeni yaliyo mema kwani Malaika wanaitikia ‘Aamiyn’ msemayo)). Akasema: Alipofariki Abuu Salamah nilimwendea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Abuu Salamah amefariki. Akasema: ((Sema: ‘Allaahumma-ghfir-liy wa lahu wa 'a-qibniy minhu ‘uqba hasanah’ [Ee Allaah, nighufurie pamoja naye na nilipie baada yake badali iliyo njema])). Akasema: Akanilipa Allaah aliye mbora zaidi kuliko yeye; (ambaye ni) Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam))). [Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]
 

Fadhila Za Kusuluhisha Waliokhasimiana -1​

Jamii

Fadhila Za Kusuluhisha Waliokhasimiana

Alhidaaya.com


Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

لَّا خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١١٤﴾
Hakuna khayr katika minong’ono yao mingi isipokuwa anayeamrisha swadaqah, au mema, au kusuluhisha baina ya watu. Na atakayefanya hivyo kutaka radhi za Allaah, basi Tutampa ujira adhimu. [An-Nisaa: 114]

Na kasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam):
((ألا أخبركم بأفضل من درجة الصيام والصلاة والصدقة ؟ إصلاح ذات البين وفساد ذات البين هي الحالقة)) رواه أحمد وأبو داود والترمذي صحيح الجامع
"Je, nikujulisheni lililo na daraja bora kuliko Swawm na Swalah na Sadaqah? Ni kusuluhisha baina ya watu. Na ama kuharibu uhusiano (baina ya watu) ni uharibifu" [Ahmad na Abu Daawuud na At-Tirmidhy katika Swahiyhul-Jaami'i]

Katika mambo ya kheri Aliyoyataja Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) watu wanapozungumza kwa siri ni kuamrishana kutoa sadaka au kutenda mema. Kisha Ametaja kuhusu kupatanisha watu, jambo ambalo mara kwa mara hutokea katika jamii na khaswa jamii yetu. Na bila ya shaka ugomvi na ikhtilaaf ni katika silaha ya hatari kabisa anayopenda kuitumia Shaytwaan kufarikisha watu watengane na kuchukiana baada ya kuwa ni ndugu au marafiki au majirani au baina ya mume na mke. Lakini Uislamu haukuacha kutilia hima jambo la kusuluhisha ugomvi kwa kutukumbusha fadhila zake kubwa katika Qur-aan na Sunnah kama tunavyoona katika Aayah na Hadiyth hapo juu.

Lakini inasikitisha kuona kwamba jambo hili la kusuluhisha halikutiliwa mkazo sana katika jamii yetu, kwani wangapi tunasikia miongoni mwetu kuwa 'fulani kagombana na fulani na hawasemeshani', kisha zikapita siku na miezi na miaka hawa watu wako katika hali hii jambo ambalo Nabiy Swalla Allaahu amekataza kabisa zisipite zaidi ya siku tatu ndugu wa Kiislamu kuwa katika hali kama hiyo:
عن أبي أيوب الأنصاري رضي الله عنه قال : قال النبي صلى الله عليه وسلم : (( لا يَحِلُّ لِمُسْلِمٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلَاثِ لَيَالٍ ، يَلْتَقِيَانِ فَيُعْرِضُ هَذَا وَيُعْرِضُ هَذَا ، وَخَيْرُهُمَا الَّذِي يَبْدَأُ بِالسَّلامِ .(( رواه البخاري ومسلم و في رواية أبو داود بإسناد على شرط البخاري ومسلم
((فَمَنْ هَجَرَ فَوْقَ ثَلاَثٍ فَمَاتَ دَخَلَ النَارَ ))
Imetoka kwa Abu Ayyuub Al-Answariy (Radhwiya 'anhu) ambaye alisema: Kasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Haimpasi Muislamu amhame ndugu yake kwa zaidi ya siku tatu hata wanapokutana huyu anamgeuzia (uso) huyu na huyu anamgeuzia (uso) huyu. Na aliye mbora wao ni yule anayeanza kutoa salaam". [Al-Bukhariy na Muslim na katika Riwayaah ya Abu Daawuud]
((Atakayemhama (mwenzake) kwa zaidi ya siku tatu akafariki basi ataingia motoni))

Na huenda ikawa kila mmoja anataka kupatana na mwenziwe lakini Shaytwaan amewatia ari kuwa vipi aanze yeye? Na pia pengine huenda wakawa ni ndugu, au jamaa au jirani lakini hakuna mmoja wetu anayekimbilia kusuluhisha, sababu ni kwamba kila mmoja ameshughulika na kazi zake na maisha yake. Kwa hiyo tulichukulie hima jambo hili bila ya kuchelewesha kila inapotokea ugomvi baina ya ndugu wa Kiislamu na kufanya hivyo ni kumcha Allaah na kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na ndio sifa ya Waumini kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
فَاتَّقُواْ اللّهَ وَأَصْلِحُواْ ذَاتَ بِيْنِكُمْ وَأَطِيعُواْ اللّهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴿١﴾
Basi mcheni Allaah na tengenezeni yaliyo baina yenu. Na mtiini Allaah na Rasuli Wake mkiwa ni Waumini.. [Al-Anfaal: 1]

Itaendelea sehemu ya pili In Shaa Allaah...


************
 

Fadhila Za Kusuluhisha Waliokhasimiana -2​

Jamii

Fadhila Za Kusuluhisha Waliokhasimiana - 2

Alhidaaya.com


Tukiendelea na fadhila za kusuluhisha waliogombana wakakhasimiana, na iwapo baada ya kusoma mada hii tutazithamini fadhila hizi, basi kila mmoja wetu atakimbilia kufanya hima ya kupatanisha ndugu zetu wa Kiislamu waliokhasimiana. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amelichukia jambo hili kwani linavunja asili ya undugu wa Kiislamu kama Anavyosema :
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ ..﴿١٠﴾
Hakika Waumini ni ndugu, basi suluhisheni baina ya ndugu zenu. [Al-Hujuraat: 10]

Na kwa jinsi jambo hili lilivyochukiza hadi kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anakataa kupokea amali za watu waliokhasimiana mpaka wapatane, na hawasamehe watu hao:
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((تُعرض الأعمال في كل أثنين وخميس فيغفر الله لكل أمريء لايشرك بالله شيئاً، إلا إمرءاً بينه وبين أخيه شحناء فيقول: اتركوا هذين حتى يصطلحا)) رواه مسلم
Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba kasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Amali njema (vitendo vyema) hutandazwa kila Jumatatu na Alkhamiys, kisha Allaah Humghufuria kila mtu asiyemshiriki kitu Allaah, isipokuwa mtu aliyekuwa baina yake na baina ya ndugu yake uhasama, Husema: Waacheni hawa wawili mpaka wapatane)) [Muslim]

Kwa hiyo ni hatari kubwa kwa waliogombana kuwa wanapoteza umri wao bure kutenda mema na hali kumbe havipokelewi vitendo hivyo hadi wapatane.


Njia za kupatanisha Watu

1-Kwanza tia nia kuwa unafanya kupata Radhi na ujira mkubwa kutoka kwa Allaah na muombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akuwafikie jambo hili.

2-Msikilize kila mmoja malalamiko yake.

3-Ukishajua sababu ya ugomvi, watajie hatari ya kuhasimikiana kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

4-Tafuta wakati na sehemu munaasib kwa wote wawili.

5-Ikibidi kusema uongo, inafaa katika jambo hili kwa kutaka kumridhisha mmojawao ili kuleta suluhisho kama alivyoruhusu Nabiy(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth:

((لَيْسَ الْكَذابُ الَّذِي يُصْلِحُ بَيْنَ النَّاسِ فَيَنْمِي خيرا أو يقول خيرا)) رواه البخاري ومسلم
"Si muongo yule anayesuluhusha watu kwa kusema uongo, kwani anaarifu mema au anasema mema [kwa lengo la kusuluhisha]" [Al-Bukhariy na Muslim]

6-Fanya uadilifu, usipendelee hata kama mmoja ni jamaa yako wa karibu au unampenda zaidi. Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
.فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ
Basi suluhisheni baina yao kwa uadilifu, na timizeni haki. Hakika Allaah Anapenda wanaotimiza haki. [Al-Hujuraat: 9]

Na Anasema tena Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa :
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّـهِ وَلَوْ عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ ۚ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقِيرًا فَاللَّـهُ أَوْلَىٰ بِهِمَا ۖ فَلَا تَتَّبِعُوا الْهَوَىٰ أَن تَعْدِلُوا ۚ وَإِن تَلْوُوا أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٣٥﴾
Enyi walioamini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu mtoapo ushahidi kwa ajili ya Allaah japokuwa ni dhidi ya nafsi zenu au wazazi wawili, au jamaa wa karibu. Akiwa tajiri au maskini Allaah Anawastahikia zaidi. Basi msifuate hawaa mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkikanusha basi hakika Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [An-Nisaa: 135]


7-Wakishapatana In shaa Allaah omba du'aa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Awaendeleze masikilizano na mapenzi baina yao na muombe pia Akutakabalie juhudi yako.


Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atunufaishe kwa yale tunayojifunza na Atuajaalie miongoni mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo njema. Aamiyn.
 

Fiqh Ya Kuwaita Majina Watoto​

Jamii

Fiqh Ya Majina Ya Watoto

Alhidaaya.com


Ni Sunnah kutunza jina zuri, na katika majina mazuri ni:

'Abdullaah (Mja wa Allaah Subhanahu wa Ta'aala)
na
'Abdur-Rahmaan (Mja wa Mwingi wa Rahmah);

na majina ya ki kweli hasa ni:

Al- Haarith (Anayezaa)
na
Humaam (Hodari);

na majina mabaya zaidi ni:

Harb (Vita)
na
Murrah (Chungu)


Hadiyth ifuatayo imethibitisha:

((Majina yanayopendezewa kwa Allaah (Subhaana wa Ta'aalaa) ni 'Abdullaah na Abdur-Rahmaan.)) [imeripotiwa na Muslim.


Kwa Abu Daawuud kuna nyongeza ((Na majina ya ki kweli hasa ni Al-Haarith na Humaam, na mabaya zaidi ni Harb na Murrah)).


Na majina mabaya, na yale ambayo yanamaanisha vitu vibaya katika kutokuwepo kwao, ni makuruhu (Yasiyopendeza), kama vile:

Nujayh (fanikiwa),

Barakah (baraka),

Kulayb (kijimbwa),

Harb (vita),

Murrah (chungu),

Shihaab (kimondo),

Himaar (punda),

Aflah (fanikiwa sana),

Yasaar (wepesi),

Rabaah (faida), na

Naafi` (kunufaika)

na majina kama:

Sittun-nisaa (mwanamke wa wanawake wote) ni yanayogombezewa sana.

Na Mfalme wa Wafalme limekatazwa, kama ilivyokuwa:

'Shahenshaah',

na

Aqdhwaal-Qudhwaat (hakimu wa mahakimu).


Na inapendelewa kubadilisha majina mabaya na ambayo yanamaanisha vitu vibaya katika kutokuwepo kwao.


Na inapendelewa kwa mtoto wa kiume, mwanafunzi au mfanyakazi kutomwita kwa jina lake, na kwamba watu wazuri (wanaume na wanawake) wawe wana kun-yah, hata ikiwa hawana watoto wa kiume, na kun-yah huhusiana na mtoto wa kiume wa mwanzo.


Na imekatazwa kuwa na Kun-yah ya 'Abul-Qaasim kwa mtu ambaye jina lake ni Muhammad na vile vile kwa watu wengine, katika kipindi cha Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na vile vile baadae ya hapo.


Tanbihi:

Kuna khitilafu baina ya madhehebu juu katika nukta hii- wengine wameshika kwamba katazo lake (kutumia kun-yah ya Abul-Qaasim) liliwekwa katika kipindi cha uhai wa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tu na si baada ya kufariki.


Na aliyeruka mipaka (faasiq) au mzushi asipewe kun-yah mpaka kukiwepo hofu ya fitnah, au ikiwa kwa sababu ya utambulishi, (kama vile Abu Lahab).


Na inapendelewa kwamba mtu asitumie kun-yah yake pekee (yaani bila ya kutimiza jina lake pia), isipokuwa akiwa anajulikana kwa kun-yah yake na sio kwa jina lolote isipokuwa hilo.


Na pia imekatazwa (Haraam) kumtania mtu kwa jina ambalo halipendi. Kama ikiwa anajulikana kwa jina jengine (ambalo halimchukizi) na hata kama jina hilo lina dhamiria kitu ambacho kinamhusu yeye ambacho ni cha kweli.


Kun-yah (Lakabu au Jina la kupachika)
Ushahidi uliombwa wa kuchukuliwa kun-yah kuwa ni Sunnah. Kuna vidokezo mbali mbali juu ya hili katika Hadiyth.


Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na kun-yah, na hakuna ushahidi wowote wa kuonyesha kwamba kuwa na kun-yah ilikuwa kwa yeye pekee, na hii ndio inayoamua ni Sunnah (kumfuata mtu katika kitu ambacho hakikua kwa ajili yake pekee (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).



Zaidi, kuna Hadiyth iliyoripotiwa na At-Tirmidhiy katika "Ash-Shamaail"


Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwita mvulana mdogo kwa kun-yah, kuonyesha kwamba si muhimu kuwa na mtoto kabla ya kutumia kun-yah.


Mazungumzo zaidi ya Hadiyth hizi yanapatikana katika Fat-h al-Baariy (maelezo ya Swahiyh Al-Bukhaariy).


 

Haki Za Wazazi Kuwatendea Ihsaan​

Jamii

Haki Za Wazazi Kuwatendea Ihsaan

'Khutbah ya Ijumaa

Alhidaaya.com


Allaah Aliyetukuka Anatuambia yafuatayo:

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا ﴿٢٣﴾وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾
Na Rabb wako Amehukumu kwamba: Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee na (Ameamrisha) kuwafanyia ihsaan wazazi wawili. Kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe, au wote wawili basi usiwaambie, Uff! Na wala usiwakemee; na waambie maneno ya heshima.Na wainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma, na useme: Rabb wangu! Warehemu kama walivyonilea udogoni. [17: 23 – 24]

Allaah Aliyetukuka Amekariri katika surah saba tofauti kuhusu haki za wazazi kwa aina tofauti. Hata hivyo, kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa Qur-aan huwezi kupata maelezo yoyote kuhusu majukumu ya mzazi kwa watoto wake. Je, kuna hekima gani kwa Allaah Aliyetukuka kuwahimiza watoto kuwatendea wema wazazi na kutowahimiza wazazi juu ya majukumu yao kwa watoto wao? Ni jambo linalojulikana kuwa hata kwa wanyama, wanakuwa ni wenye kuwalinda na kutekeleza majukumu yao kwa watoto wao. Kwa ajili hiyo kuku anakuwa karibu na vijifaranga vyake ili kuvilinda wakati wa hatari.

Ni maumbile ya mwanadamu anapokuwa ni mzazi kutekeleza majukumu kwa watoto wake – majukumu ya msingi. Hata hivyo, watoto mara nyingi hujitazama wao wenyewe bila kujali kama mzazi anacho au hana. Mwanaadamu kimaumbile anapopata watoto hamu yake kubwa ni watoto wake na sio wazazi ambao ndio sababu ya kuja kwao. Kwa ajili hii Allaah Aliyetukuka Akatoa ufafanuzi mrefu kuhusu majukumu ya watoto kwa wazazi wao. Ukumbusho huu umekaririwa mara kadhaa ili kumpatia hisia mtoto atekeleza majukumu yake kwa mzazi wake.

Aayah ambayo imefafanua kwa kina suala hilo ni Aayah ya Suwrah 'Al-Israa' ambayo tumeitaja hapo juu. Amri ya kwanza iliyokuja katika Aayah hizo mbili zilizofuatana ni kumuabudu Allaah pekee bila ya kumshirikisha na yeyote wala chochote. Baada ya agizo hilo ni amri ya kuwatendea wema wazazi wawili. Kwa ile bahati ambayo anapata mtoto ni pindi wazazi wanapokuwa ni wakongwe na wako kwako wakiwa wanakutegemea wewe peke yako. Wakati huo utiifu wa kweli unajitokeza kwa kiasi kikubwa sana. Je, utawatazama kwa njia gani? Hakika huo ni mtihani mkubwa sana kwa mtoto au watoto wenye kulea wazazi wakongwe, ndio Allaah Aliyetukuka Akatoa maagizo Yake kuhusu wema na ihsani wanaofaa kufanyiwa. Katika walio kwako anaweza kuwa ni mzazi mmoja au wawili. Katika hali hiyo yao ya uzee wakiwa wanakutegemea wewe sio kinyume chake ndio utiifu wa kihakika unajulikana na ndio hapo pia hufai kuwaambia hata Ah au Uff au Uh na kadhalika.

Ibara iliyotumika hapa inamaanisha kuwa wewe pia si mtoto hivyo japokuwa mzazi wako bila shaka atakuwa ni mkubwa kuliko wewe. Ikiwa mzazi wako ni miaka themanini wewe huenda ukawa arobaini. Katika hali ya kuwa wapo kwako Allaah Aliyetukuka Anasema: "Usiwaambie Ah!" Wanazuoni wasema kuwa lau kuna neno dogo zaidi kuliko Uff basi Allaah Angelitumia lakini hakuna dogo zaidi. Katika Kiswahili chetu husema kuwapigia kitunu (kuguna). Hii ni alama ya kuonyesha kutoridhika kwako, hali hiyo isiwe ni yenye kutokea kabisa kwani sio sifa nzuri.

Pia usiwatolee ukali wala kuwakemea. Hii ni tabia ya utoto ambaye anakuwa hana hisia na jambo lolote linaweza kumkasirisha na hayo ndio maumbile ya mwanadamu anapozeeka. Wazazi wako walikuwa hawakukaripii ulipokuwa mdogo, nawe pia inatakiwa ufanye hivyo. Mbali na hayo unatakiwa useme nao maneno yaliyo mazuri, kauli za kuwafurahisha na sio kinyume chake. Bado Allaah Anaendelea kutupatia maagizo kuhusu kuwatendea wema wazazi wakati huo. Na baada kuwafanyia yote hayo basi pia kuwa mnyenyekevu kwao kwa kiwango cha juu. Bado hata baada ya kuwafanyia yote hayo utakuwa hujalipa ihsani na wema waliokufanyia. Ulipokuwa mdogo walisumbuka, walikopa, walikosa kula na mengineyo kwa ajili yako. Ihsani usiyoifahamu utailipa namna gani?

Hivyo ndio Allaah Aliyetukuka bado Anatuusia tuwe ni wenye kuwaombea du’aa kwa kusema: "Ee Rabb wangu! Warehemu wao kama walivyonilea nikiwa mdogo". Hii ina maana kuwa Ee Allaah! kwa kuwa mimi siwezi kuwalipa kwa waliyonifanyia basi warehemu wazazi wangu. Hii ni Aayah moja miongoni mwa Aayah nyingi inayotufundisha kuwaamili wazazi wanapokuwa wazee wakiwa kwetu.

Suala ni kuwa wengi wetu tuna wazazi, je muamala wetu kwao ni vipi? Utakuta kuwa wengi wetu huondosha kero (udhia na usumbufu) nyumbani huwa tunawapeleka wazazi wetu katika nyumba za wazee. Kufanya hivyo sio kwa sababu ya kuwa hakuna nafasi nyumbani wala hakuna cha kuwapa bali sababu kuu ni kuwa mke haridhiki kwa hilo. Huo sio ubinadamu kabisa. Allaah Anauliza: "Je, malipo ya wema yapo mengine ila wema?" Gari mara nyingi huwa tunalitazama likiwa ni jipya, lipo kazini na laleta pesa kwa mwenyewe lakini pindi linapozeeka anakwenda kulitupa mahali likimalizika kidogo kidogo. Hivyo ndivyo tunavyowafanya wazazi wetu wakati huu wetu wa leo.

Hakika ni kuwa haifai kuwepo majumba ya wazee katika jamii ya Kiislamu ikiwa tutakuwa tunafuata Uislamu inavyotakiwa. Lakini ni sikitiko kubwa sana kuona kuwa majumba hayo yanakithiri kila uchao. Huu si Uislamu. Kiislamu familia ni pana zikiwajumlisha wazazi wako, wazazi wa mke, mkeo, watoto wako na wajukuu na kadhalika. Lakini kwa kuwa fikra za kimagharibi zimetuvaa na kututawala tumejaalia kuwa familia ni wewe, mkeo na watoto wako basi. Leo katika nchi za kimagharibi wazee wamekuwa ni kero na kuna njia inayoitwa kuua kwa huruma inayotumika kuwamaliza na hivyo kuwapumzisha na mateso na udhia kwako.

Kiislamu sio hivyo bali kila wazazi wanapokuwa wazee ni nafuu kwetu kwa kiasi kikubwa. Imepokewa kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: “Mwana pua yake kusuguliwa na mchanga (amekhasirika)[1], kisha mwana pua yake kusuguliwa na mchanga, kisha mwana pua yake kusuguliwa na mchanga yule ambaye atawakuta wazazi wake wawili wakiwa wazee, mmoja au wote kisha asiingie Peponi?” [Muslim].

Hakika kwetu sisi wazazi kuwa wazee ni neema na ni mlango wa mtu kuingia (Jannah) Peponi. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema: "Pindi mtu anapokuwa na wazazi wake wakiwa kwake basi milango miwili ya Peponi yanafunguliwa kwake". Uamuzi wa kuingia au kutoingia ni wake. Na kinyume chake pia ni sahihi, hivyo ukiwafanyia ubaya milango miwili ya Motoni itafunguliwa kwa ajili yake.

Wazazi tulipokuwa wadogo walikuwa wakitutazama kwa hali na mali mbali na kutufurahikia lakini wanapokuwa wazee huwa tunawakodishia wafanyakazi wa kuwatazama. Wewe uliyetoka katika tumbo lake huona huwezi kushika uchafu wa mzee wako. Je, unadhania kuwa hisia zako na za mfanyakazi itakuwa sawa? Tunadhania kuwa kumuwekea mtumishi inatosha lakini hilo halitoshi kabisa na ipo haja ya sisi kuzingatia hilo na kujirekebisha kwa njia iliyo nzuri. Kwa ajili ya umuhimu wa suala hili kwa kukaririwa mara nyingi na Allaah Aliyetukuka ipo haja kwetu kukumbushana kila mara tunapopata nafasi na fursa.

Utiifu kwa wazazi unakuja baada ya utiifu kwa Allaah Aliyetukuka lakini utiifu kwa wazazi una mipaka. Ipo hali moja ambayo mtoto hafai kumtii mzazi wake nayo tumefahamishwa na Allaah katika Qur-aan. Allaah Anasema:

وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ
Lakini wakikushikilia kuwa Unishirikishe na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii. Na suhubiana nao kwa wema duniani. [Luqmaan: 15]

Hii ni hali ambayo hufai kuwatii kwani Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: "Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba". Hata hivyo, katika hali yoyote ile ni lazima uwatii na hata wakikuamrisha mabaya wewe hufai kuwatii tu lakini unatakiwa usuhubiane nao kwa wema hapa duniani. Sababu ni kuwa haki yao ya uzazi haipomoki (haiondoki) kwa wao kufanya ubaya au kuamrisha mabaya.

Kila mmoja wetu ana wazazi wawili na huenda tukawa tunauliza ni nani katika wao mwenye haki zaidi kuliko mwengine. Jawabu la hilo tunapatiwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam).

Imepokewa na Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu.) ambaye amesema: "Alikuja mtu kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akasema: “Ewe Mjumbe wa Allah! Ni nani mwenye haki zaidi miongoni mwa watu kwa mimi kusuhubiana naye kwa wema?” Akasema: “Mamako”. Akasema: “Kisha nani?” Akasema: “Mamako”. Akasema: “Kisha nani?” Akasema: “Mamako”. Akasema: “Kisha nani?” Akasema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): “Babako” [al-Bukhaariy na Muslim].
Na katika riwaya nyengine: “Ee Rasuli wa Allah! Nani ana haki zaidi kwa mimi kusuhubiana naye kwa wema?” Akasema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): “Mamako, kisha mamako, kisha mamako, kisha babako, kisha wale waliokaribu, wale walio karibu nawe kijamaa”.

Hadiyth hii inatuonyesha kuwa mama ana sehemu tatu ziada za kufanyia wema na watoto kuliko baba. Na hii ni sababu ya shida na uzito anaopata wa kubeba mimba, kisha kuzaa na baadaye kunyonyesha.

Al-Qurtubiy amesema: “Mama anastahiki wema na ihsani zaidi kuliko baba, na amemtangulia baba katika mashindano hayo”.

Haya yalizungumzwa wakati ulimwengu hauna masuala ya gender (jinsia). Bila shaka, masuala hayo ni katika nadharia za kimagharibi lakini katika Uislamu kila mmoja anapatiwa haki yake anayostahiki na Allaah Aliyetukuka. Hapa mama hakupendelewa kabisa bali alipatiwa haki yake anayostahiki kulingana na wajibu wake aliopewa. Majukumu ya mama ni makubwa zaidi. Yeye ndiye aliyekubeba wewe kwa udhaifu juu ya udhaifu na mimba hiyo ikamletea matatizo na pia akaonja mauti akiwa hai. Na kuna msemo kwetu unaosema: "Kuzaa ni kuonja mauti". Mbali na maendeleo katika utabibu bado wapo wanawake wengi wanaoaga dunia wakati wa kuzaa. Na mama kwa kumpenda mtoto wake lau ataulizwa achukuliwe nani baina yake na mwanae basi atajibu achukuliwe naye, abaki mwanae katika uhai. Hii ni ruhuma (huruma) ya mwisho aliyonayo mama kwa mtoto wake. Baba akiwa na ruhuma nyingi atakuwa na wasiwasi wakati mkewe anajifungua lakini si zaidi ya hapo. Hata hivyo, ni masikitiko makubwa sana kuona leo vijana wanawachukulia akina mama kama kitambaa cha mkono, hatuwajali kabisa.

Tumenyonya maziwa ya mama kwa miaka miwili, hiyo ni kunyonya nguvu zake. Maziwa hayo hayakutoka katika mfereji. Allaah Aliyetukuka Anasema:

وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ ۖ لِمَنْ أَرَادَ أَن يُتِمَّ الرَّضَاعَةَ ۚ
Na wazazi wa kike wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa mwenye kutaka kutimiza kunyonyesha. [Al-Baqarah: 233].

Baba hata akitaka vipi hawezi kukunyonyesha labda akusaidie kukushikia chupa ya maziwa.

Allaah Aliyetukuka Anasema:

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ إِحْسَانًا ۖ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ كُرْهًا وَوَضَعَتْهُ كُرْهًا ۖ وَحَمْلُهُ وَفِصَالُهُ ثَلَاثُونَ شَهْرًا ۚ
Na Tumemuusia insani kuwafanyia wema wazazi wake wawili. Mama yake amebeba mimba yake kwa tabu na akamzaa kwa tabu, na kuibeba mimba na kuachishwa kwake kunyonya ni miezi thelathini. [Al-Ahqaaf: 15].

Hapa Allaah Anataja haki za wazazi wawili na kisha anabainisha uzito Aliopata mama hivyo kustahiki haki zaidi. Hakika shida na unyonge wa mama katika kubeba mimba yako ni mkubwa na kila miezi ilipokuwa inapita ndio udhaifu zaidi aliokuwa akipata. Si hayo tu bali mtoto si kama kifaranga ambapo anapoanguliwa tu anaanza kula bali mwanadamu ananyonya kwa miaka miwili kutoka kwa mamake.

Ama kuhusu fadhila nyengine za haki kwa wazazi ni Hadithi zifuatazo:

Imepokewa kwa Ibn Mas‘uud (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nilimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam): “Ni amali gani inampendeza Allah Aliyetukuka?” Akasema: “Ni Swalaah kwa wakati wake”. Nikasema: “Kisha ni ipi?” Akasema: “Kuwatendea wema wazazi wawili”. Nikasema: “Kisha ipi?” Akasema: “Jihadi katika Njia ya Allah” [al-Bukhaariy na Muslim].

Na imepokewa kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: “Mtoto hawezi kumlipa babake (kwa yale aliyomfanyia) isipokuwa anapomkuta kuwa ni mtumwa, akamnunua kisha kumwacha huru” [Muslim, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy].

Pia kama ilivyo haki za wazazi na hasa ya mama, kuna kuwaasi wazazi. Kufanya hivyo ni katika madhambi makubwa kama alivyotuelezea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), yaani kumshirikisha Allaah Aliyetukuka na kuwaasi wazazi. Kumuasi mzazi si lazima umtusi au kumweka na njaa kama tulivyoona hata kuwaambia Uff.

Khasara ngapi mtu anapata kwa kukasirikiwa na mzazi wake. Hakika hii ni hasara kubwa ambayo Muislamu atapata ikiwa hataweza au atashindwa kuwajibika ipasavyo kwa kuwapatia wazazi wake. Allaah Aliyetukuka Atuepushe mbali na hilo.


[1] Hii ni kinaya ya mtu kudhalilishwa.
 
Back
Top Bottom