Ramadhan Special Thread
Maswali: Bid'ah - Uzushi


Kusoma Halal Badiri au Albadiri (Ahlul-Badr) Kwa

Ajili Ya Kinga Na Kuapiza Ni Shirki Na Dhambi Kuu!



Alhidaaya.com





SWALI:



Assalama Alaykum Warahmatullah T'aalaa Wabarakatu.



Napenda kuanza kwa kumshukuru Rabb mlezi wa ulimwengu kwa kuwapa nguvu, afya na uwezo ndugu zetu wa alhidaaya kwa kutuelimisha sisi ndugu zenu Waislam katika musuala mengi yanayohusu dini yetu ya haki. Rabb awape kheir, baraka na pepo In Shaa Allaah. Ameen.



Na suali langu ni kutaka kujua kama kusoma halal badr ni sawa au si sawa katika uislam? Kuwa kama kinga na kuomba Allaah akuhukumie kwa anetaka kukudhuru au kukufania ubaya.

Asanteni....assalam aleykum.





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Awali twataka kurekebisha ibara hiyo kwani sivyo inavyokusudiwa au inavyotamkwa au kuandikwa. Ibara hiyo imetoka katika lugha ya Kiarabu lakini kupotolewa au kuandikwa na kusomwa makosa katika Kiswahili. Wapo wanaosema Alibadiri lakini makusudio ni Ahlul-Badr, yenye maana watu wa Badr (wale waliopigana vita vya Badr). Badr ni sehemu iliyo karibu na Madiynah na ndio iliyokuwa sehemu ambayo Waislamu wakiongozwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walipambana na mushirikina wa Makkah katika vita vya kwanza baina ya pande hizo mbili. Waislamu waliohudhuria walikuwa baina ya 313 – 317, lakini pamoja na idadi yao ndogo hiyo waliweza kuwashinda washirikina waliokuwa na idadi kubwa ipatayo mara sita yao.





Kisomo cha Ahlul Badri inakuwa ni kutaja majina ya Swahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) mmoja baada ya mwingine. Katika kutaja huko ni Imani ya mwenye kusoma hao Maswahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) wanamsaidia kwa njia moja au nyingine. Ima kupata kitu alichopoteza au kilichoibiwa au kulaaniwa aliyefanya. Na hii katika Uislamu ni njia moja ya shirki ambayo Allaah Aliyetukuka na Nabiy Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameikema na kuipiga vita sana. Allaah Aliyetukuka Anasema:



إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾

Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu. [An-Nisaa: 48].





Ingia Katika Kiungo Kifuatacho pia upate maelezo yam as-ala haya:





Wazazi Wangu Wako Kwenye Maasi,Ushirikina Wa Waganga Na Albadiri (Ahlul-Badr)





Ikiwa unataka kinga basi kinga ni nyingi sana tulizopatiwa na Uislamu ni nyingi. Qur-aan yenyewe ni ponyo na kinga ya mambo mengi na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye hakutuacha hivi hivi ila ametupatia kinga nyingi katika Surah na Aayah za Qur-aan na du’aa alizotuachia. Miongoni mwa kinga ni Muislamu kusoma Surah 112, 113 na 114 mara tatu tatu asubuhi, jioni na wakati wa kulala. Hiswnul Muslim ni kijitabu kizuri cha du’aa na adhkaar katika mas-ala haya.





Utakipata kitabu hicho ndani ya Alhidaaya kwenye kiungo hiki:



Hiswnul Muslim





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kusoma Majina Ya Allaah Kwa Idadi Maalum



Alhidaaya.com





SWALI:



Nimeona kitabu kimeandikwa majina ya Allaah na maana yake kwa kiswahili, na baadhi ya majina yameelezwa kwamba kama ukiyataja mara kadhaa 70 au 100-nk, basi unaweza kupata jambo fulani, jee nikweli mambo haya?





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Vitabu kama hivyo vipo vingi vinavyoelezea mambo haya ya kutaja majina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa idadi maalumu nawe utapata thawabu kadhaa. Kwa hakika ukiangalia vitabu hivyo hutapata kukuta maelezo hayo ni Hadiyth na ikiwa imesemekana kuwa ni Hadiyth basi aghalu za ni Hadiyth zisizotegemewa. Kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kutumia Majina Yake au aina yoyote ya Tasbiyh kwa kutaja idadi ma'aluum bila kuweko dalili katika Qur-aa au Sunnah ni jambo la uzushi (Bid'ah) na linapaswa kuachwa kwani mtu atahangaika bure na kitendo hakitokubaliwa kutokana na dalili za Hadiyth nyingine kuhusu mambo ya Bid'ah, mojawapo wapo ni hii:

((من عمل عملا ليس عليه أمرنا فهو رد ((خرجه مسلم في صحيحه

"Atakayefanya kitendo kisichokuwa katika amri yetu basi kitarudishwa (hakitokubaliwa)" [Imesimuliwa na Muslim]





Jambo ambalo lipo wazi kuhusu majina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni kama inavyotueleza Qur-aan kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ana majina mazuri hivyo tumuombe kupitia majina hayo yake. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. [Al-A'araaf: 180]



Na Amesema tena:

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ

Sema; Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. [Israa: 110]





Kwa hiyo unaweza kuomba mfano unataka Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akughufurie dhambi zako, ukamwita kwa Jina Lake Tukufu 'Yaa Ghaffaaru' au 'Ya 'Afuwwu' kama mfano unataka Akuruzuku kitu ukamwita 'Ya Razzaaq' au mfano unamuomba kitu na unataka Akutakabalie dua yako, ukamwita 'Ya Sami'u', 'Ya Qariybu', 'Ya Mujiybu' na kadhalika. Hivi unaweza kumwita kwa mara unazotaka bila ya kuweka idadi ma'aluum.





Katika vitu vyenye idadi maalumu ni dhikri (kumtaja Allah) kwa kusema: Subhanallah, Alhamdullillah, Allahu Akbar na adhkari nyingine za baada ya Swalaah, au za mchana na usiku. Tazama Kitabu cha




Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)



kilichokuweko Alhidaaya humo utapata dalili ya Tasbiyh na Adhkaara ambazo zimetajwa idadi ma'aluum kuzisoma.





Kiungo kifuatacho kumetajwa idadi maaulumu zilizothibiti.



Fadhila za Tasbiih, Tahmiid, Tahliil, na Takbii





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kusoma Tawassul Inafaa Katika Hedhi?



Alhidaaya.com





SWALI:



Is one allowed to recite (read) "Tawasul" when they are on their periods? Some people read it every thursday night and usually even at "taaziya's". Mtu akifa, jamaa husoma tawassul alafu wakamtiliya maiti fatha. Also, for example, I have it on tape and I would usually play it in the car and my children and I will follow along.





JIBU:




AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.




Bila ya shaka hiyo tawassul ni ile inayojulikana kama Wasiylatush-Shaafiy au Wasiylatun-Nabaahaniy ambayo ‘Ulamaa wamefutu kuwa haifai na ni bid’ah.



Bonyeza kiungo kifutacho upate maelezo bayana:



29-Tawassul Za Shirki Kufru Na Bid’ah: Kutawassal Kwa Wasiylatush-Shaafiy



Haifai kabisa na unapaswa kuachana nayo na badala yake ushikilie kusoma Qur-aan na nyiradi au du’aa zilizothibiti katika Qur-aan na Sunnah,, na badala ya kuwasikilizisha watoto wako hiyo du'aa ya bid'ah, wasikilizishe watoto wako Qur-aan, kwa sababu Qur-aan ni khayr na ni bora na ni muhimu na yenye faida zaidi na manufaa kwako na kwa Aakhirah yako.

Fanya na fuata mambo yaliyothibiti kishariy'ah na usifuate mazoea au kuona watu wanafanya au kutenda kama ada na mazoea.



Jizoeshe na wanao kusoma Qur-aan sana na kuisikiliza sana na kusoma du'aa na adhkaar zilizothibiti za asubuhi na jioni na za minaasabah mbalimbali.

Hayo yana faida kwako na khayr na ndiyo yenye kuchumwa thawabu, na hayo ya bid’ah ni kinyume chake kutokupata thawabu zozote zile na juu ya hivyo kuchuma dhambi.



Inakupasa kuwalea watoto katika mafunzo sahihi ili waokoke na bid’ah ili wabakie katika mwenendo wa Salafus-Swaalih (Wema waliotangulia) na ili waokoke na makundi potofu.



Suala la kusomwa Al-Faatihah katika shughuli mbali mbali kama za misiba n.k pia halikuthibiti katika Shariy’ah, hivyo nalo ni bid’ah.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Kusoma Uradi Kwa Pamoja Kila Mwezi Kwa Kukusanyika Inafaa?



Alhidaaya.com







SWALI:



Assalaam alaykum

Sisi huwa tunakusanyika pamoja kwa kila mwezi mara moja kwa ajili ya kuswali, kuleta adhkar na kuomba dua ya pamoja. Dua ambazo huwa tunatumia ni zile zilizomo kwenye Quran na mapokezi sahihi ya Nabiy (s.w). Je kufanya hivi inakubalika katika uislam?





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Nabiy, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta'aalaa) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea au kivivu. Pia hiyo ni ‘ibaadah na ‘ibaadah inatakiwa ifanywe kwa namna iliyofundishwa na haifai kugeuza, kuongeza au kupunguza. Hali kadhalika Swahaba walikuwa wakiandikiana barua na hakuna aliyekuwa akikatisha Salaam, wala kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwenye barua zao. Tuige na tufuate nyendo zao tusalimike.





Tumekuwa tukisema mara nyingi kuwa katika Uislamu kila kitu ambacho kinamridhisha Allaah (‘Azza wa Jalla) ni 'Ibaadah pamoja na kufuata Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hakuna utata kuhusu kuswali Swalaah ya Sunnah kwa Jama'ah na kufanya I’tikaaf katika Msikiti kwa siku moja.





Hata hivyo, haijakuwa kukutana huko ni fursa kwenu nyinyi kufanya mengine kama kuleta Adhkaar na du'aa kwa pamoja. Hilo halijapokewa katika Qur-aan, Sunnah wala Wema Waliotangulia (Salaf Swaalih). Ikiwa ni Adhkaar za asubuhi au usiku kila mmoja anapaswa awe ni mwenye kuleta pekee yake isipokuwa ikiwa ni kufunzwa ili aweze kuzisoma yeye peke yake baada ya hapo.





AlhamduliLlaah, siku hizi suala hilo limekuwa sahali kupatikana vijitabu vidogo kama vile Hiswnul Muslim, ambacho kina du'aa takriban zote ambazo tunazihitajia. Pia kuna kitabu kinachoitwa “Hiswnul-Muumin”. Hizi Adhkaar za pamoja ndio zimeleta matatizo mpaka watu wakawa wanalichezea jina la Allaah (‘Azza wa Jalla) kwa kufanya katika kiza na kuwa ni wenye kutoa maneno hata yasioeleweka au kufanya Adhkaar kwa kukohoa.





Na du'aa nayo ni hivyo hivyo mbali na kuwa kuna wakati ambao Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amefundisha kuwa iletwe kwa sauti kama wakati wa kuomba mvua, Swalaah ya kupatwa kwa jua au mwezi. Ama wakati mwengine inabidi kila mmoja wetu alete kivyake kwani kila mmoja wetu ana tatizo tofauti na mwenziwe. Katika hili utapata Maimaam kwa kutojua au kwa kujua huwa wanajiombea wenyewe na Maamuma wanaitikia “Aamiyn”.





Tunapata makatazo hayo na madhara yake katika usimulizi ufuatao:



Kutoka kwa ‘Amru bin Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tulikuwa tumeketi mlangoni mwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd kabla ya Swalaah ya Alfajiri, akatoka nje. Tukaenda naye Msikitini. Kisha Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akatujia na kusema: “Je, Abuu ‘Abdir-Rahmaan ameshakuja kwenu?” Tukasema: “Hapana!” Akaketi hadi akatoka nje na alipotoka nje tukasimama. Abuu Muwsaa akamwambia: “Ee Abaa ‘Abdir-Rahmaan! Sasa hivi nimeona jambo Msikitini sijapatapo kuliona kabla, lakini sidhanii baya ila ni jambo jema”. Akasema: “Jambo gani?” Akasema. “Ukiendelea kuishi utaliona”. Akasema: “Nimeona Msikitini watu wameketi kwa mkusanyiko wa duara wakisubiri Swalaah. Katika kila duara alikuweko mtu na mikononi mwao mna changarawe. Mmoja wao akisema: “Semeni Allaahu Akbar mara mia!” nao wakisema “Allaahu Akbar!” mara mia. Kisha husema: “Semeni laa ilaaha illa-Allaah mara mia”! Nao husema “laa ilaaha illa-Allaah!” mara mia. Kisha husema: “Semeni Subhaana-Allaah mara mia!” Nao husema “Subhaana-Allaah!” mara mia. Akasema: “Je umewaambia nini?” Nikasema: “Sikusema lolote, nilikuwa nasubiri nione utaonaje na nikisubiri amri yako”. Akasema: “Kwa nini usiwaambie wahesabu vitendo vyao viovu na kuwahakikishia kwamba vitendo vyao vyema havitopotezwa?”





Kisha akasogea nasi tukaenda hadi alipofikia moja kati ya maduara hayo akasimama na kusema: “Mnafanya nini?” Wakasema. “Ee Abaa ‘Abdir-Rahmaan, hivi ni vijiwe tunavyohesabia takbiyr, tahliyl na tasbiyh”. Akasema: “Hesabuni vitendo vyenu viovu, kwani nakuhakikisheni kwamba vitendo vyenu vyema havitopotea hata kimoja! Ole wenu Ee Ummah wa Muhammad! Ni kwa haraka gani mnakimbilia kwenye uharibifu! Hawa ni Maswahaba wa Nabiy wenu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao wameenea. Hizi ndizo nguo zake ambazo bado hazijachakaa, na bakuli lake ambalo halijavunjika! Naapa kwa Yule Ambaye roho yangu ipo mikononi Mwake! Aidha mpo kwenye dini iliyoongoka zaidi kuliko Dini ya Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ama mnafungua milango ya upotofu!”





Wakasema: “Ee Abaa ‘Abdir-Rahmaan, hatukukusudia lolote ila khayr tu”. Akasema: “Wangapi waliokusudia khayr hawakuzipata?” Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia: ((Watu wataisoma Qur-aan, lakini haitovuka zaidi ya koo zao)) “Naapa kwa Allaah! Mimi sijui, lakini pengine mengi kati ya hayo yanatoka kwenu!” Baadaye akaondoka. ‘Amr bin Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Tumewaona wengi kati ya watu hao wakipigana dhidi yetu katika siku ya Nahrawaan, wakiwa pamoja na Khawaarij [Sunan Ad-Darimy 206 – Ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (5/11)]





Kila mmoja wetu ajifunze katika Adhkaar na du'aa ambazo anaweza kuleta katika hali ya upweke. Tukumbuke kuwa Allaah (‘Azza wa Jalla) si kiziwi bali Anasikia hata minong'ono yetu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ ﴿٥٥﴾

Muombeni Rabb wenu kwa unyenyekevu na kwa siri, hakika Yeye Hapendi wenye kupindukia mipaka. [Al-A’raaf: 55]



Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aala):



وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦﴾

Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah: 186]





Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aala):

وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ﴿١٦﴾

Na Sisi Tuko karibu naye kuliko mshipa wa koo. [Qaaf: 16]





Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aala):



وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُبْصِرُونَ ﴿٨٥﴾

Nasi Tuko karibu naye zaidi kuliko nyinyi, lakini hamuoni. [Al-Waaqi’ah: 85]







Hizi ni sifa za Allaah (Subhaanahuu wa Ta’aalaa), hivyo tumuombe Yeye kwa unyenyekevu na taadhima ya hali ya juu, na si kumuomba mpaka watu wengine wasikie na mikusanyiko ambayo huenda ikaingia riyaa (kujionyesha).







Na Allaah Anajua zaidi
 
Kutumia Tasbihi (Kuhesabia Shanga) Katika Kumdhukuru Allaah Inafaa?



Alhidaaya.com







SWALI LA KWANZA:



Asalam alaykum,

Naomba kuliza suali hili. kuna mtu aliniambia kuwa kusoma uradi kwa kushika mtasbihi ni ktk uzushi, na mwengine ameniambia kuwa sio kweli kwani swahaba Abuu Hurayrah alikuwa akivuta uradi kwa utumia kokwa za tende, kwa hiyo hakuna tofauti na mtasbihi. Sasa hapa nilikuwa naomba jibu la sawa kutoka kwenu wenye elimu, inafaa au haifai? Na kweli huyu sahaba alifanya hivi?





SWALI LA PILI:



A allakum. ningependa kuuliza kuhusu utumiaji wa tasbih ni bidaah na vipi tutawaeleza wazazi kuhusu kutotumia. mimi mzee wangu amenipa yake nitumie jee niifanyeje.





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Jibu La Kwanza:



Ni wazi kwa kila Muislamu kuwa jambo lake lolote analolifanya lazima liafikiane na sheria ya Kiislamu; Qur-aan na Sunnah. Hilo ni kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametuhimiza sana kufuata mwenendo wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyo bayana katika Suwrah Al-Hashri Aayah ya 7:



وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ

Na lolote analokupeni Rasuli ((صلى الله عليه وآله وسلم basi lichukueni, na analokukatazeni, basi acheni. [Al-Hashr: 7].





Kwetu sisi kumfuata Nabiy(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inafaa tujue alilotenda au kusema. Pia kipenzi chetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia:



"Nawausia kumcha Allaah, na kusikiliza muambiwayo na kutii hata akiwa Kiongozi wenu ni mtumwa wa Kihabashi. Kwani hakika atakayeishi katika nyinyi ataona khitilafu nyingi, basi jilazimisheni na kufuata mwendo wangu na mwendo wa Makhalifa wangu waongofu, yashikilieni kwa magego yenu mambo yao. Na nawatahadharisha nyinyi na uzushi katika mambo" [Abu Daawuud na at-Tirmidhiy].



Hebu tumsikilize tena kipenzi chetu anatueleza nini kuhusu haya mambo yanayozuliwa katika Dini:



"Mwenye kuzua katika hili jambo letu lisilokuwamo humo litakataliwa" [al-Bukhaariy na Muslim].



Katika riwaya ya Muslim:



"Mwenye kufanya amali isiyokuwa na hukumu yetu, itakataliwa".





Suala ambalo tunafaa sisi kama Ummah bora, Waislamu kujiuliza ni kuwa: Je, Nabiy alitumia tasbihi ili kuleta uradi au alitumia kifaa gani? Je, Makhalifa waongofu walifanya hivyo? Je, Swahaba wengine nao walifuata mwendo huo?



Awali ya yote hebu tutazame mas-ala ya kutumia vijiwe au shanga, au kokwa za tende n.k. katika kuleta tasbihi na nyuradi.



Hadiyth ifuatayo ndio wanayoitumia wengi wa wanaotumia tasbiyh:

"Bora ya chenye kukumbusha ni Tasbiyh" Hii ni Hadiyth dhaifu.



Vilevile tunaona dalili nyingi za kuonyesha kinyume na hivyo wanavyofanya hao wenye kutumia Tasbiyh. Tutazame Hadiyth zifuatazo:





Imepokewa kwa Sa'd bin Abi Waqqaas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Wakati mmoja Sa'ad, akiwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walimzuru mwanamke ambaye mbele yake kulikuwa na vijiwe au kokwa za tende ambazo alikuwa akitumia kumsabihi Allaah. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Nakuambia kitu ambacho kitakuwa sahali na bora zaidi kwako kuliko unavyofanya. Akasema: Msabihi (SubhaanaLlaah) mara nyingi kama vile Alivyoviumba mbinguni, mara nyingi kama Alivyoviumba ardhini.. Mkabiri idadi kama hiyo, pia Mhimidi idadi kama hiyo na Mhalili .." [Abu Daawuud].





Sasa huyu mwanamke alikuwa atumie mbinu gani ya kuweza kuhesabu nyuradi hizo baada ya kuambiwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa njia hiyo si bora kufanywa na Muislamu. Katika mwenendo wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tunapata kuwa yeye alikuwa akitumia vidole vyake vya mkono wa kulia ili kuhesabu Tasbihi, Takbiri, Tahmidi na Tahlili alizokuwa akifanya. Hii imepokewa na mtu kwa Banu Sulaym:





Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alizihesabu mkononi mwangu au mkononi mwake kwa kusema: Tasbiyh (SubhaanaLlaah) inajaza nusu ya mizani, Tahmiyd (AlhamduliLlaah) inajaza kamili. Takbiyr (Allaahu Akbar) inajaza baina ya mbingu na ardhi, Funga ni nusu ya subira na twahara ni nusu ya Imani [at-Tirmidhiy].





Pia Yusayrah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) anasimulia kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), aliwaamuru (wanawake wa Muhajirina) wawe ni wenye kushikilia sana katika kumdhukuru Allaah kwa kusema: Allaahu Akbar, SubhaanaLlaah, Laa ilaaha illa Llaah, na wasimsahau Allaah na rehma Yake. Wahesabu hizo kwa vidole vyao kwani vidole vitaulizwa na vitazungumza [Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa'iy, Ibn Maajah na al-Haakim kwa Isnadi iliyo sahihi].





Naye 'Abdullaah bin 'Amr bin al-'Aasw (Radhwiya Allaahu anhuma) anasimulia, "Nilimuona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akihesabu kumsabihi Allaah na vidole vya mkono wake wa kuume" [Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa'iy na Ibn Maajah].





Na kutoka kwa Asswalt bin Bahraam amesema, Ibn Mas'uud alimpitia mwanamke mmoja aliyekuwa na Tasbiyh akimsabihi Allaah kwa Tasbiyh hiyo akaikata na akaitupa, kisha akampitia mwanamume aliyekuwa akimsabihi Allaah kwa vijiwe akampiga kwa mguu wake kisha akasema;





"Mumetangulia, mumefanya uzushi kwa dhulma, na mumewashinda Swahaba wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa elimu" [Sanad yake ni sahiyh mpaka kwa Asswalti, naye ni "thiqah" (mkweli mwenye kutegemewa) katika wanaowafuatia Taabi'iyn (wenye kufuatia Maswahaba).]





Hivyo, badala ya kutumia tasbihi tuwe ni wenye kutumia mkono kwani hajapatikana hata Swahaba mmoja aliyefanya hivyo. Ni salama kwetu zaidi kutumia vidole vyetu na ndio Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye tumeamriwa kumfuata.



Tufahamu kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anatuambia:



الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ

Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu. [Al-Maaidah: 3]





Imaam Maalik aliielezea Aayah hii kwa kusema: "Lolote ambalo halikuwa Dini wakati wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) haliwezi kuwa Dini sasa". Hii ina maana Dini imekamilika hatuwezi kuikamilisha zaidi ya hapo wala sisi hatuna daraja ya kuja kumkosoa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa yeye alifanya khiyana hakufikisha mengine ambayo alikuwa afaa atufikishie hivyo sisi Waislamu wa sasa tumekuja tukakamilisha hayo.





Tujiepushe na vizushi vyote nasi tutasalimika kabisa.





Jibu La Pili:



Ukitazama hapo juu kwa jibu la swali la kwanza utakuta kuwa utumiaji wa Tasbihi ni Bid'ah na inafaa kwetu sisi wafuasi wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tuache kuzitumia. Na badala yake tutumie vidole vyetu vya mikono ambavyo navyo tunapata baraka kwa kufanya hivyo.





Inafaa kwetu sisi tutumie hekima katika kuwaelimisha wazazi wetu kuhusu hilo na mengineyo kwani bila ya hivyo kutakuwa na fitna na mzozo mkubwa zaidi. Wapo wazee ambao wanaelewa wanapoambiwa na kurekebishwa kwa njia nzuri na wapo walio wakaidi. Ni vigumu kwa mtu ambaye huenda kwa miaka 50 anafanya jambo fulani kisha ukaja ukamuarifu na utegemee aache hayo mara moja na akufuate! Lakini pia wapo wenye uoni na kutaka haki, ambao hawatazami haki inatoka wapi au kwa nani; wao ni wenye kujisalimisha na kufuata mara moja. Allaah Aliyetukuka Anasema kuhusu kutumia hekima na busara na mawaidha mazuri:



ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ

Lingania katika njia ya Rabb wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. Na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi. [An-Nahl: 125].





Ikiwa mzazi wako ni mkaidi tumia upole na njia ya taratibu wala usikate uhusiano naye kabisa. Usimsahau katika Swalaah na du'aa zako kwani kwa kufanya hivyo pia utakuwa unamsaidia kwa kiasi kikubwa. Wema ni kitu muhimu sana kuwafanyia wazazi kama alivyotuamuru Aliyetukuka:



وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا ﴿٢٣﴾وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾

Na Rabb wako Amehukumu kwamba: Msiabudu isipokuwa Yeye Pekee na (Ameamrisha) kuwafanyia ihsaan wazazi wawili. Kama mmoja wao akifikia uzee naye yuko pamoja nawe, au wote wawili basi usiwaambie, Uff! Na wala usiwakemee; na waambie maneno ya heshima. Na wainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma, na useme: Rabb wangu! Warehemu kama walivyonilea udogoni. [ Al-Israa: 23-24].





Ama tasbihi aliyokupa unaweza kuiweka ikiwa bado ana ukaidi na kutochukua hadiya kutoka kwake inaweza kuleta zogo zaidi na kukatika kwa mahusiano, lakini usiitumie. Ikiwa ameelewa kuwa haifai basi yeye mwenyewe ataitupa na wala hatakupatia wewe.





Njia nzuri ya kutumia vidole kama tulivyopata kutoka kwa Wanachuoni walioelewa masuala hayo ya kutumia vidole, wanasema ni kutumia matumbo ya vidole karibu na kucha kuhesabia na si ile mistari mitatu ya kila kidole kama ilivyozoeleka na wengi. Lakini atakayefanya kwa njia zote hizo maadam anatumia vidole vyake, basi katimiza Sunnah na ana ujira mkubwa kwa hilo.





Na Allaah Anajua zaidi
 
00-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Suwrah Al-Faatihah

Aayah Na Mafunzo



Al-Faatihah



Fadhila Za Suwrah Al-Faatihah





Hii ni Suwrah iliyokuwa Adhimu na bora, kuliko Suwrah zote za Qur-aan, nayo ni miongoni mwa Suwrah zenye majina mengi na miongoni mwa majina yake ni: Al-Faatihah, Ummul-Qur-aan, AlhamduliLLaah, Asw-Swalaah, Ash-Shifaa, Ar-Ruqyah, Sab‘ul-Mathaaniy, Ummul-Kitaab. Haijateremka katika Tawraat wala katika Injiyl wala katika Zaburi mfano wake.

Utukufu na Fadhila za Suwratul-Faatihah unaelezewa katika Hadiyth nyingi, baadhi yake ni hizi zifuatazo:



Hadiyth Ya Kwanza:

Abuu Sa’iyd bin Al-Mu’allaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Nilikuwa nikiswali, akaniita Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikawa sikumuitikia mpaka nilipomaliza kuswali. Kisha nikamwendea akaniambia: “Kimekuzuia nini usinijie?” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, nilikuwa naswali. Akasema: “Kwani Allaah Hakusema: “Enyi walioamini! Muitikieni Allaah na Rasuli Anapokuiteni kwenye yale yenye kukuhuisheni.” [Al-Anfaal (8: 24)]. Kisha akasema: “Nitakufundisha Suwrah tukufu kabisa katika Qur-aan kabla hukutoka Msikitini.” Akanikamata mkono, alipotaka kutoka Msikitini, nikamwambia: ee Rasuli wa Allaah, ulisema utanifundisha Suwrah tukufu kabisa katika Qur-aan. Akasema: “Naam, AlhamduliLLaahi Rabbil-‘Alaamiyn, hizo ni (Aayaat) Saba zinazokaririwa (kusomwa) na Qur-aan Adhimu niliyopewa.” [Al-Hijr (15: 87) Al-Bukhaariy]



Hadiyth Ya Pili:

Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Baadhi ya Swahaaba (wakiwa safarini) walifika karibu na kabila fulani la Waarabu, wakakataa kuwapokea. Walipobakia katika hali hiyo, huku mkuu wao alitafunwa na nyoka (au nge). Wakasema: Je, mna dawa yoyote au tabibu? Wakajibu: Nyinyi mmekataa kutupokea kwa hiyo hatutamtibu mgonjwa wenu hadi mtulipe! Wakakubali kuwapa kundi la kondoo. Mmoja wa Swahaaba akaanza kumsomea Suwratul-Faatihah huku akikusanya mate na kumtemea (mahali alipotafunwa). Mgonjwa akapona kisha watu wake wakawaletea kondoo lakini wakasema. Tusiwachukue mpaka tumuulize Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Walipomuuliza alicheka akasema: “Mmejuaje kuwa Suwratul-Faatihah ni ruqya? Chukueni na nigaieni sehemu yangu.” [Al-Bukhaariy]



Hadiyth Ya Tatu:

Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amehadithia kwamba: Jibriyl ('Alayhis-Salaam) alipokuwa na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisikia sauti kutoka juu. Jibriyl ('Alayhis-Salaam) akatazama juu akasema: “Huu mlango wa mbinguni umefunguliwa na haujapatapo kufunguliwa isipokuwa leo.” Malaika akateremka humo akasema: “Huyu Malaika ameteremka ardhini, hajapatapo kuteremka kamwe isipokuwa leo.” Akasalimia kisha akasema: “Pokea bishara ya nuru mbili ulizopewa ambazo hakuna Nabiy aliyepewa kabla yako; Ufunguo wa Kitabu (Al-Faatihah), na Aayah (mbili) za mwisho wa Suwratul-Baqarah. Hutosoma herufi humo ila utapewa barakah zake ziliomo.” [Muslim]



Hadiyth Ya Nne:

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayeswali Swalaah bila ya kusoma humo mama wa Qur-aan (Suwratu Al-Faatihah) huwa haikutimia (ina kasoro).” Alikariri mara tatu: “Haikutimia.” Mtu mmoja alimwambia Abuu Hurayrah: (Hata) tukiwa nyuma ya Imaam? Akasema: Isome mwenyewe (kimya kimya) kwani nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Allaah (تعالى) Amesema: Nimeigawa Swalaah baina Yangu na mja Wangu nusu mbili, mja Wangu atapata yale aliyoyaomba. Mja anaposema: Himidi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu, Allaah (Ta’aalaa) Husema: Mja Wangu kanihimidi. Na anaposema: Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu, Allaah (Ta’aalaa) Husema: Mja wangu kanisifu na kunitukuza kwa wingi, na anaposema: Mfalme wa siku ya malipo, Allaah (Ta’aalaa) Husema: Mja wangu kaniadhimisha. Na mara moja alisema: Mja wangu ameniaminisha. Na anaposema: Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada, Husema: Hii ni baina Yangu na mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba. Na anaposema: Tuongoze njia iliyonyooka, njia ya wale Uliowaneemesha, si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea, Husema: Hii ni ya mja Wangu na mja Wangu atapata kile alichokiomba.” [Muslim, Maalik, At-Tirmidhiy, Abu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah]



Hadiyth Ya Tano:

‘Ubaadah bin Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakuna Swalaah kwa asiyesoma (ndani yake) Ufunguo wa Kitabu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
03-Aayah Na Mafunzo: Maana Ya Ar-Rahmaan Na Mwenye Kurehemu
Aayah Na Mafunzo



Al-Faatihah



Maana Ya Ar-Rahmaan, Mwenye Kurehemu





Al-Faatihah Aayah 3:



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿١﴾

Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.



الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu.



الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٣﴾

Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.





Mafunzo:



Ar-Rahmaan ni katika Jina la Allaah tukufu na Sifa ya Rahmaan ni ambayo inawaenea viumbe Vyake vyote duniani; wana Aadam na majini, makafiri na Waumini na makafiri, wenye taqwa na wenye kumuasi, wanyama, mimea na kadhaalika. Hakuna kiumbe chochote isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amekiteremshia rahmah Yake. Amejiita Mwenyewe (Tabaaraka wa Ta’aalaa):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

Ar-Rahmaan; Mwingi wa Rahmah juu ya ‘Arshi Istawaa (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah) [Twaahaa 5]

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

رَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ

Na rahmah Yangu imeenea kila kitu [Al-A’raaf: 156]



Na hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



عَنْ عَطَاءٍ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إِنَّ لِلَّهِ مِائَةَ رَحْمَةٍ أَنْزَلَ مِنْهَا رَحْمَةً وَاحِدَةً بَيْنَ الْجِنِّ وَالإِنْسِ وَالْبَهَائِمِ وَالْهَوَامِّ فَبِهَا يَتَعَاطَفُونَ وَبِهَا يَتَرَاحَمُونَ وَبِهَا تَعْطِفُ الْوَحْشُ عَلَى وَلَدِهَا وَأَخَّرَ اللَّهُ تِسْعًا وَتِسْعِينَ رَحْمَةً يَرْحَمُ بِهَا عِبَادَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ))

Na pia imepokelewa kutoka kwa ‘Atwaa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Ana rahmah mia, Ameiteresha moja kati ya majini na wana Aadam na wanyama na wadudu, ambao wanaoneana huruma na wanarehemeana, na hiyo hiyo mpaka mnyama mwitu anamhurumia mwanawe. Akazuia Allaah rahmah tisini na tisa Atawarehemu kwazo waja Wake Siku ya Qiyaamah)) [Muslim (6/98), Ahmad (2/434), Ibn Maajah (4293)]



Ama Rahiym ni Sifa inayowastahiki Waumini pekee. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا ﴿٤٣﴾

Naye kwa Waumini daima ni Mwenye kurehemu. [Al-Ahzaab: 43]



Na waja Wake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) watakapoingia Jannah:



إِنَّ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ الْيَوْمَ فِي شُغُلٍ فَاكِهُونَ ﴿٥٥﴾

Hakika watu wa Jannah leo wamo katika kushughulika wakifurahi.



هُمْ وَأَزْوَاجُهُمْ فِي ظِلَالٍ عَلَى الْأَرَائِكِ مُتَّكِئُونَ ﴿٥٦﴾

Wao na wake zao, wakiwa katika vivuli, juu ya makochi ya fakhari wakiegemea.



لَهُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ ﴿٥٧﴾

Watapata humo kila aina ya matunda, na watapata wanavyoomba.



سَلَامٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ ﴿٥٨﴾

“Salaamun”; kauli kutoka kwa Rabb Mwenye kurehemu. [Yaasiyn: 55-58]



Rejea viungo viufatavyo upate faida zaidi:



004-Majina Ya Allaah Na Sifa Zake: AR-RAHMAAN



005-Majina Ya Allaah Na Sifa Zake: AR-RAHIYM
 
05-Aayah Na Mafunzo: Haki Ya Allaah Kwa Waja Na Haki Ya Waja Kwa Allaah

Aayah Na Mafunzo



Al-Faatihah



Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada





Al-Faatihah Aayah 5:



إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

5. Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.





Mafunzo:



Haki Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni kumwabudu bila ya kumshirikisha na chochote.



عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: كُنْتُ رَدِيفَ اَلنَّبِيِّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) عَلَى حِمَارٍ فَقَالَ لِي: ((يَا مُعَاذُ؟ أَتَدْرِي مَا حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ، وَمَا حَقُّ الْعِبَادِ عَلَى اَللَّهِ؟)) قُلْتُ اَللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: ((حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ أَنْ يَعْبُدُوهُ، وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَحَقُّ الْعِبَادِ عَلَى اَللَّهِ أَنْ لاَ يُعَذِّبَ مَنْ لاَ يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا)) قُلْتُ يَا رَسُولَ اَللَّهِ أَفَلاَ أُبَشِّرُ اَلنَّاسَ؟ قَالَ: ((لاَ تُبَشِّرْهُمْ فَيَتَّكِلُوا)) أَخْرَجَاهُ فِي اَلصَّحِيحَيْنِ

Imepokelewa kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilikuwa nyuma ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya punda akasema: ((Ee Mu’aadh! Unajua nini haki ya Allaah kwa waja Wake, na nini haki ya waja kwa Allaah?)) Nikajibu: Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi: Akasema: ((Haki ya Allaah kwa waja wake ni kwamba wamwabudu na wasimshirikishe na chochote. Na haki ya waja kwa Allaah ni kwamba Hatomwadhibu yeyote ambaye hamshirikishi na chochote)). Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Niwabashirie watu? Akasema: ((Usiwabashirie wasije kuitegemea)) [wakaacha kufanya juhudi katika ‘ibaadah])) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Isti’aanah ni kuomba kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee katika ambayo hakuna mwenye uwezo nayo:



كُنْتُ خَلْفَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يًوْماً، فقال: ((يا غُلامُ، إنِّي أُعَلِّمُكَ كلِماتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجاهَك، إذا سأَلْتَ فاسْأَلِ اللهَ، وإذا اسْتَعنْتَ فاسْتَعِنْ باللهِ، واعْلَمْ أنَّ الأُمَّة لَوِ اجْتَمَعَتْ على أَنْ يَنْفَعُـوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيْءٍ قدْ كَتَبَهُ اللهُ لَكَ، وإن اجْتَمَعُوا على أن يَضُرَّوكَ بِشيءٍ لَمْ يَضُروكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأقْلامُ وَجَفَّتِ الصُّحُفُ))

Siku moja nilikuwa nyuma ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: “Ee kijana! nitakufundisha maneno (ya kufaa); Mhifadhi Allaah (fuata maamrisho Yake na chunga mipaka Yake) Atakuhifadhi. Muhifadhi Allaah utamkuta mbele yako. Ukiomba, muombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), ukitafuta msaada tafuta kwa Allaah. Tambua kwamba ikiwa ummah mzima utaungana kukunufaisha wewe kwa kitu, basi hutonufaika ila tu kwa kile Alichokwishakuandikia Allaah. Na wakikusanyika kukudhuru kwa chochote, hutodhurika ila tu kwa kile Allaah Alichokwishakukuandikia (kuwa kitakudhuru), kwani kalamu zimeshanyanyuliwa (kila kitu kishaandikwa) na swahifa zimeshakauka.” [At-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]



Bonyeza kiungo upate faida zaidi:



18-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aanah (Kuomba Msaada) Kwa Asiyekuwa Allaah
 
06-Aayah Na Mafunzo: Maana Ya Njia Iliyonyooka

Aayah Na Mafunzo

Al-Faatihah

Maana Ya Njia Iliyonyooka







اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿٦﴾

6. Tuongoze njia iliyonyooka.





Mafunzo:



Hadiyth Ya Kwanza:



An-Nawaas bin Sam’aan (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Allaah (Ta’aalaa) Amepiga mfano; Swiraatw (njia) iliyonyooka, imezungukwa pande zote na kuta mbili na kila ukuta una milango iliyo wazi na imefunikwa na mapazia. Na katika lango la swiraatw kuna mlinganiaji akiita: “Enyi watu! Ingieni nyote katika swiraatw na msipite pembeni.” Na juu ya swiraatw, mlinganiaji mwengine anamuonya mtu yeyote anayetaka kufungua hiyo milango akiwaambia: Masikitiko kwenu! Msiufungue! Kwani mkifungua mtapita ndani! Kwani Asw-Swiraatw ni Uislaam, na kuta mbili ni mipaka Aliyoiweka Allaah. Na milango iliyofunguliwa ni yaliyoharamishwa na Allaah. Na huyo Daa’iy (mlinganiaji) juu ya lango la Swiraatw ni Kitaabu cha Allaah, na Daa’iy juu ya swiraatw ni maonyo ya Allaah yaliyo ndani ya kila nafsi ya Muislaam.” [Ahmad, ameisahihisha Al-Albaaniy; Swahiyh Al-Jaami’ (3887)]





Hadiyth Ya Pili:

Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba: Tulikuwa tumekaa pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akachora mstari mbele yake, akachora mistari miwili kuliani, na mistari miwili kushotoni kisha akaweka mkono wake katika njia ya katikati akasema: “Hii njia ya Allaah” Kisha akasoma: “Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni, na wala msifuate njia (nyinginezo) zitakufarikisheni na njia Yake.” [Ahmad, Swahiyh Ibn Maajah (11)]
 
07-Aayah Na Mafunzo: Walioghadhibikiwa Na Waliopotea

Aayah Na Mafunzo

Al-Faatihah

Walioghadhibikiwa Na Waliopotea







صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ ﴿٧﴾

7. Njia ya wale Uliowaneemesha, si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.





Mafunzo:



‘Adiy bin Haatim (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Walioghadhibikiwa ni Mayahudi, na waliopotea ni Manaswara.” [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Ghariyb na taz. Silsilah Asw-Swahiyhah (363)]
 
Fadhila Na Sifa Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام)



Alhidaaya.com





Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):



إِنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِّلَّـهِ حَنِيفًا وَلَمْ يَكُ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٢٠﴾

Hakika Ibraahiym alikuwa mwenye akhlaaq na maadili yote mema, mtiifu kwa Allaah, aliyeelemea haki, na hakuwa miongoni mwa washirikina.





شَاكِرًا لِّأَنْعُمِهِ ۚ اجْتَبَاهُ وَهَدَاهُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿١٢١﴾

Mwenye kushukuru Neema Zake, (Naye Allaah) Akamteua na Akamuongoza kuelekea njia iliyonyooka.





وَآتَيْنَاهُ فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَإِنَّهُ فِي الْآخِرَةِ لَمِنَ الصَّالِحِينَ﴿١٢٢﴾

Na Tukampa duniani mazuri. Na hakika yeye Aakhirah bila shaka ni miongoni mwa Swalihina.





ثُمَّ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ أَنِ اتَّبِعْ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٢٣﴾

Kisha Tukakufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba fuata mila ya Ibraahiym aliyeelemea haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.



[An-Nahl: 16:120-123]





Katika Aayah (120-123) za Suwrah hii An-Nahl, Allaah (سبحانه وتعالى) Amemsifia Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kwa sifa zifuatazo: Mwenye akhlaaq na maadili yote mema, mtiifu, Haniyfah (ameelemea katika haki), hakuwa katika washirikina, mwenye kushukuru Neema za Allaah (سبحانه وتعالى), mwongofu na miongoni mwa Swalihina.



Na katika Suwrah nyenginezo, Allaah (سبحانه وتعالى) Amemsifia pia kwa sifa nyenginezo mbalimbali na Akamjaalia kuwa na fadhila tele.





Miongoni Mwa Fadhila Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام):



-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemteua yeye Nabiy Ibraahiym na mwanawe Nabiy Ismaa’iyl (عليهما السّلام) waijenge Al-Ka’bah. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akamteua Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) awatangazie watu kwenda kutekeleza Hajj. Hivyo basi, akawa yeye (عليه السّلام) na ahli wake ni mwongozo kwa watu katika utekelezaji wa manaasik (ibaada na taratibu) za Hajj na ‘Umrah. Rejea Al-Hajj (22:26-37). Na miongoni mwa manaasik hizo, ni kuswali katika Maqaam Ibraahiym baada ya kutufu Al-Ka’bah. Rejea Al-Baqarah (2:125). Pia, kusai baina ya Swafaa na Marwah, rejea Al-Baqarah (2:158) kama ni kigezo cha mkewe Haajar alipokuwa akihangaika kumtafutia maji mwanawe Ismaa’iyl (عليه السّلام). Na huko ndiko palipotokea mbubujiko wa maji ya Zamzam ambayo watu wanakunywa kwa niya tofauti kama alivyogusia hilo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Pia kuchinja mnyama baada ya yeye kupewa mtihani au majaribio makubwa, pindi alipoona njozini kuwa anamchinja mwanawe, naye kutokana na utiifu wake, akataka kutekeleza njozi hiyo akiamini kuwa ni Amri ya Allaah (سبحانه وتعالى). Lakini kumbe ilikuwa ni mtihani na jaribio, hivyo akafaulu katika hili, na hapo Allaah (سبحانه وتعالى) Akambadilishia kwa kumteremshia kondoo kutoka mbinguni ili amchinje badala ya mwanawe. Rejea Asw-Swaaffaat (37:101-107). Pia kutupia vijiwe Jamaraat ambayo ni katika waajibaat za Hajji na Sunnah zake nyenginezo.







-Ni kipenzi cha Allaah. Rejea An-Nisaa (4:125).





-Ameitwa Baba wa Manabii: Kama ilivyokuwa hali ya Nabiy Nuwh (عليه السّلام): Al-‘Ankabuwt (29:27). Na katika Al-Hadiyd (57:26), ametajwa yeye Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) pekee kuwa amejaaliwa kuwa na Unabii na kupewa Kitabu.



Imaam Ibn Kathiyr amesema kuhusu Aayah ya Suwrah Al-‘Ankabuwt: “Hii ni fadhila na baraka kubwa sana. Sio tu kwamba Allaah Alimfanya (Nabiy Ibraahiym) kuwa ni kipenzi Chake na kumfanya Imaam wa watu, bali pia Alijaalia Unabii na Kitabu kuwa katika dhuriya zake. Baada ya zama za Ibraahiym, hapakuwa na Nabii ambaye hakutokana na kizazi chake. Manabii wote wa Wana wa Israaiyl (Ya’quwb) walikuwa katika kizazi chake, kuanzia Ya’quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym hadi wa mwisho wao, `Iysa bin Maryam, ambaye alisimama kuwatangazia kaumu yake, bishara ya kuja kwa Nabii Mwarabu, Al-Qurashiy, Al-Haashimiy, Nabii wa mwisho wa Manabii wote, bwana wa wana wa Aadam katika dunia hii na Aakhirah, ambaye Allaah Alimteua kutoka kwa Waarabu safi wa asili kutoka kwa kizazi cha Ismaa’iyl bin Ibraahiym (عليهما السلام). Hakuna Nabii yeyote katika ukoo wa Ismaa’iyl isipokuwa yeye Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). [Tafsiyr Ibn Kathiyr]





-Ameomba duaa kizazi chake kitoe Nabii wa mwisho; Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baada ya kujenga Al-Ka’bah. Rejea (2:129).





-Ibraahiym (عليه السّلام) ni Imaam wa Tawhiyd:

Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfanya kuwa ni Imaam wa watu wa kufuatwa katika Tawhiyd. Rejea Al-Baqarah (2:124). Na pia Ummah umeusiwa kufuata mila yake. Rejea Al-Baqarah (2:135), Aal-‘Imraan (3:95), An-Nisaa (4:125), Al-An’aam (6:161), na An-Nahl (16:123). Na pia, Amewausia wanawe na kizazi chake Uislamu. Rejea Al-Baqarah (2:130-132). Na pia Amefanya neno la Tawhiyd (laa ilaaha illa-Allaah) lenye kubakia katika kizazi chake. Rejea Az-Zukhruf (43:28). Ingawa Rusuli wengineo wote wamekuja pia katika kulingania Tawhiyd, ila Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) amekuwa ni makhsusi kwa Tawhiyd. Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (رحمه الله) amesema alipoulizwa:



Kwa nini Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) amehusishwa zaidi na Tawhiyd, ilhali Manabii wote wengineo wamelingania Tawhiyd?



Akajibu: Manabii wote wamekuja na (kulingania) Tawhiyd. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):



وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾

“Na Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rasuli yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: Hakika hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, basi Niabuduni.” [Al-Anbiyaa (21:25)]





Lakini Ibraahiym ni baba wa Waarabu, na baba wa Waisrael, naye amelingania Tawhiyd khalisi, na Mayahudi na Manaswara wamedai kuwa ni wafuasi wake, na Waislamu ndio wafuasi wake. Kwa hiyo yeye (عليه السّلام) akahusishwa kuwa ni baba wa Manabii, na kwamba yeye ndiye mwenye Haniyfiyyah (sifa ya kuelemea haki na kujiweka kando na shirki). Na sisi tumeamrishwa kumfuata, kwa sababu sisi ndio tulio karibu zaidi Ibraahiym kama Anavyosema Allaah (عزّ وجلّ):



إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا ۗ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٦٨﴾

“Hakika watu walio karibu zaidi kwa Ibraahiym ni wale waliomfuata na huyu Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini. Na Allaah Ni Mlinzi wa Waumini.” [Aal-‘Imraan (3:68)]





Na Akasema kuwaradi Mayahudi na Manaswaara:



مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٦٧﴾

“Ibraahiym hakuwa Yahudi wala Naswara, lakini alikuwa mwenye kujiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki, Muislamu na hakuwa miongoni mwa washirikina.” [Aal-‘Imraan (3:67)]

[Liqaa-a Al-Baab Al-Maftuwh Swali namba (7/189).







-Anatajwa katika kila Swalaah, kwenye Tashahhud, kwa Swalaah inayojulikana kama Swalaatul-Ibraahiymiyyah.



Na fadhila hii tukufu ni kutokana na sababu zilizotangulia kutajwa juu na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn. Pia kutokana na sababu zifuatazo kama walivyosema ‘Ulamaa: Kwamba (عليه السّلام) Ibraahiym ni babu (kizazi kilichoanzia kwa Ismaaiyl) wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)



Na ‘Allaamah Badr Ad-Diyn Al-Hanafiy (رحمه الله) ana maelezo mengineyo katika kubainisha sababu ya hili. Amesema: “Ikiwa mtu atauliza: Kwa nini Ibraahiym (عليه السّلام) ameteuliwa yeye pekee kutajwa katika Swalaah badala ya Manabii wengine (عليهم السّلام)?



Nitajibu: Kwa sababu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaona katika usiku wa Mi’iraaj, Manabii na Rusuli wote, na akamtolea Salaam kila Nabii, na hakuna hata mmoja wao aliyesalimia ummah wake isipokuwa Ibraahiym (عليه السّلام) . Hivyo basi, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ametuamrisha tumswalie kila mwisho wa Swalaah mpaka Siku ya Qiyaamah, kama malipo ya wema wake. Na imesemwa: Ibraahiym (عليه السّلام) alipomaliza kuijenga Al-Ka’bah, aliuombea Ummah wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: Ee Allaah! Atakayehiji Nyumba hii miongoni mwa Ummah wa Muhammad, basi Mpe amani kutoka kwangu. Pia akawaombea ahli zake na watoto wake kwa duaa hii. Hivyo basi tukaamrishwa tuwakumbuke katika Swalaah kama malipo ya wema wao.” Mwisho. Ufafanuzi wa Sunan Abi Daawuwd cha Al-‘Ayniy (4/260). Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.





-Kizazi chake kimepewa ufalme mkubwa: An-Nisaa (4:54).





-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimkuta mbingu ya saba akielemea Bayt Al-Ma’muwr inayozungukwa na Malaika elfu sabiini. (Haya yapo katika Hadiyth ndefu iliyopokelewa na Imaam Muslim katika Kitaab Al-Iymaan, na wengineo).



-Alijaaliwa Ar-Rushd (Uongofu) na Allaah (سبحانه وتعالى) Alimjua vyema: Al-Anbiyaa (21:51).





-Ni Nabii ambaye amemshabihi Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم): Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) [Al-Bukhaariy, Muslim]



-Ni miongoni mwa Rusuli watano wa Ulul-‘Azmi: Al-Ahzaab (33:7).





-Amewaombea Waislamu wawe wenye kuelekeza nyoyo zao kuipenda Makkah na Al-Ka’bah. Ibraahiym (14:37).





-Amewaombea duaa kizazi chake wasimamishe Swalaah, na Amewaombea Waumini maghfirah Siku ya Hesabu. Ibraahiym (14:40-41).





-Atakuwa wa kwanza kuvalishwa nguo baada ya kufufuliwa kutokana na vile washirikina katika kaumu yake walivyomuingiza motoni akiwa uchi baada ya kuvunja masanamu yao. Yapo haya kwenye Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما):



Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Enyi watu, hakika mtafufuliwa na Allaah hali ya kuwa hamna viatu, mpo uchi na bila kutahiriwa (na magovi). ”Kisha akasoma:



كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ ۚ

Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena. [Al-Anbiyaa (21:104)]







Tanabahini! Hakika mtu wa kwanza atakayevishwa nguo ni Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام). [Al-Bukhaariy na Muslim]



Na ‘Ulamaa wameeleza pia kuwa sababu ya kutangulizwa Ibraahiym kuvishwa nguo Siku ya Qiyaamah kabla ya wengine ni kuwa hapakuweko miongoni mwa watu wa mwanzo na wa baadae, waliomkhofu zaidi Allaah kuliko yeye. Hivyo basi, nguo zitamharakia ili kumhifadhi, na moyo wake upate kutulia.



Na sababu nyingine -kama ilivyoeleza Hadiyth- ni kuwa, inawezekana kwamba yeye alikuwa ni wa kwanza kuvaa suruali wakati anaposwali ili kupata sitara ya ziada isiyo na shaka na kulinda tupu yake isigusane na sehemu yake ya kuswalia, naye akafanya kama alivyoamrishwa, na akalipwa hilo kuwa wa kwanza kusitiriwa Siku ya Qiyaamah.



Kadhalika, inawezekana kuwa wale waliomtupa motoni, walimwacha uchi na wakamvua nguo zote mbele ya watu kama anavyofanywa mtu anayetekelezewa adhabu ya kifo. Hivyo atalipwa nguo zake Siku ya Qiyaamah, na atakuwa mtu wa kwanza kuvaa mbele ya halaiki, na haya ni malipo mazuri zaidi. [Al-Qurtwubiy katika At-Tadhkirah]





-Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema kwamba yeye ni kiumbe bora kabisa: Amesimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه): Alikuja mtu mmoja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: “Ee kiumbe bora kabisa!” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamjibu: “Huyo ni Ibraahiym (عليه السّلام). [Muslim]





Sifa Za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام):



-Hakuwa mshirikina kabisa. Ametajwa kwa sifa hii katika Suwrah kadhaa kwenye Qur-aan ikiwemo Suwrah hii An-Nahl (16:120). Pia, kisa chake katika Al-An’aam (6:74-81) cha kutokuabudu nyota wala mwezi wala jua kinathibitisha sifa hii. Kadhalika, alimuomba Allaah Amuepusha yeye na wanawe wasiwe washirikina: Ibraahiym (14:35). Isitoshe, alimnasihi baba yake pia asiwe mshirikina lakini hakumsikiliza bali alimfukuzilia mbali: Maryam (19:41-48) na Ash-Shu’araa (26:69-89).





-Alikuwa ni mtimizaji ahadi: An-Najm (53:37).





-Ni mwenye huruma mno na mvumilivu: At-Tawbah (9:114).





-Ni mvumilivu sana, mnyenyekevu mno kwa Allaah, na mwingi wa kurejea Kwake. Huwd (11:75).





-Mkarimu mno: Huwd (11:69), na Adh-Dhaariyaat (51:24-26).





-Mwenye utukufu: Rejea Tanbihi namba 1 ya Aayah namba (4) katika Suwrah Yuwsuf.





-Mnyeyekevu, kwani aliomba duaa baada ya kujenga Al-Ka’bah: Al-Baqarah (2:128). Al-Ka’bah ni Nyumba Tukufu kabisa katika Vitukufu vya Allaah katika Mji Mtukufu kabisa. Lakini juu ya utukufu huu, alikuwa na wasiwasi juu ya kutaqabaliwa kitendo hiki, kwa maana hakuwa na kibri kuwa madamu amejenga kitu kitukufu kabisa cha Allaah, basi awe amesifika au ni mtu bora kabisa.







-Ana kisa muhimu cha uthibitisho wa Tawhiyd iliyojikita moyoni mwake wakati alipoingizwa motoni na watu wake kwa sababu aliyavunja masanamu waliyokuwa wakiyaabudu: Al-Anbiyaa (21:51-70), na Asw-Swaaffaat (37:83-99).





-Mwenye moyo uliosalimika: Asw-Swaaffaat (37:84).





-Swiddiyq (mkweli wa kidhati): Maryam (19:41).





-Mwenye akhlaaq na mfano wa maadili mema: Al-Mumtahinah (60:4).





-Amekhitariwa duniani, na Aakhirah ni miongoni mwa Swalihina: Al-Baqarah (2:130).





-Mwenye nguvu na busara: Swaad (38:45). Na katika busara zake, alimwambia mwanawe Ismaa’iyl abadilishe kizingiti chake badala ya kumwambia moja kwa moja “mwache mkeo.” Hii ni kutokana na malalamiko ya mke huyo kuhusu maisha yao na shida zao. Kisha akamtaka athibitishe kizingiti chake, akimaanisha aendeleze ndoa yake na mkewe mwengine (asimtaliki), mke wa pili ambaye hakulalamika shida zao za kimaisha. Maelezo ya hili yapo katika Hadiyth ndefu ya Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) iliyopokelewa na Al-Bukhaariy, Kitaab Ahaadiyth Al-Anbiyaa.







Pia katika busara zake ni kumtaka mfalme Namruwd aliyejifanya kuwa yeye ni Mola na mwabudiwa, alichomoze jua kutoka Magharibi badala ya Mashariki, lakini mfalme huyo akabakia kinywa wazi ameduwaa. Rejea Al-Baqarah (2:258) kwenye maelezo bayana katika faida ya Aayah hiyo.





Pia katika busara yake nyengineyo ni vile alivyovunja masanamu kisha akatundika shoka ya sanamu lilokuwa kubwa lao. Kaumu yake walipomuuliza nani aliyevunja masanamu yetu, alijibu: “Waulizeni wakiwa wanaweza kunena!” Akikusudia pia kama kweli wanastahiki kuabudiwa ikiwa hawawezi kujihami wenyewe kusingiziwa uvunjaji wa masanamu yao. Rejea Al-Anbiyaa (21:57-63), na Asw-Swaafaat (37:88-96)





-Alikhofia familia yake wasije kuabudu masanamu. Naye mwenyewe tokea utotoni alichukia ibaada ya shirki na masanamu. Na alikhiari Dini kuliko dunia, napo ni pale alipowaacha familia yake katika bonde la Makkah ambako hapakuwa na chochote, na alitaja sababu yake kuwa ili wasimamishe Swalaah: Ibraahiym (14:35-37).



Hizo ni baadhi ya fadhila na sifa za Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) , na bila shaka zinapatikana nyenginezo katika Kitabu na Sunnah.
 
Kisa Cha Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) – 2



Alhidaaya.com









Da'wah Kwa Baba Yake:





Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alikuwa akiumia kupita kiasi kumuona baba yake (Au ‘ammi yake aliyemlea kama walivyonukuu baadhi ya Mufassiriyn) kuwa anaabudu masanamu. Bali akiumia zaidi kwani yeye huyo baba yake ndiye aliyekuwa akichonga hayo masanamu. Hii ni tabia ya mwenye kufanya da'wah anapoona jamaa zake wenyewe wako katika upotofu na khaswa inapokuwa jamaa aliye karibu zaidi kama baba, mama, ndugu, watoto na kadhalika. Kwa hiyo, lilikuwa tamanio lake kubwa kumtoa baba yake kutoka katika upotofu na kumuingiza katika Tawhiyd. Akamuita kwa maneno ya upole kabisa na kumpa kila hoja ili atambue upotofu huo:





إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنكَ شَيْئًا ﴿٤٢﴾ يَا أَبَتِ إِنِّي قَدْ جَاءَنِي مِنَ الْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَاتَّبِعْنِي أَهْدِكَ صِرَاطًا سَوِيًّا ﴿٤٣﴾ يَا أَبَتِ لَا تَعْبُدِ الشَّيْطَانَ ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ عَصِيًّا ﴿٤٤﴾ يَا أَبَتِ إِنِّي أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ فَتَكُونَ لِلشَّيْطَانِ وَلِيًّا ﴿٤٥﴾

42. Pindi alipomwambia baba yake: Ee baba yangu! Kwa nini unaabudu vile visivyosikia na visivyoona na visivyokufaa kitu chochote? 43. Ee baba yangu! Hakika mimi imekwishanijia elimu isiyokufikia wewe; basi nifuate nikuongoze njia iliyonyooka. 44. Ee baba yangu! Usimwabudu shaytwaan. Hakika shaytwaan daima ni mwenye kumuasi Ar-Rahmaan. 45. Ee baba yangu! Hakika mimi nakhofu isikushike adhabu kutoka kwa Ar-Rahmaan, ukaja kuwa rafiki kwa shaytwaan. [Maryam: 42-45]



Lakini baba yake Ibraahiym (‘alayhis- salaam) hakutaka kuacha ibada yake na hakupendezewa na wito wa mwanawe, na ingawa Ibraahiym (‘alayhis- salaam) alimuita kila mara kwa upole na adabu kabisa kama aya hizo za juu "Ee baba yangu", baba yake hakumjibu kwa upole wala hakuonyesha adabu baina ya baba na mtoto, bali alimtisha kuwa akiendelea kumwita katika ibada yake atamfukuza na kumpiga mawe kama ilivyotajwa katika Kauli Zake Allaah (‘Azza wa Jalla):



قَالَ أَرَاغِبٌ أَنتَ عَنْ آلِهَتِي يَا إِبْرَاهِيمُ ۖ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ لَأَرْجُمَنَّكَ ۖ وَاهْجُرْنِي مَلِيًّا ﴿٤٦﴾

(Baba yake) Akasema: Unachukia waabudiwa wangu ee Ibraahiym? Usipokoma, bila shaka nitakupiga mawe; na niondokelee mbali kwa muda mrefu! [Maryam:46]



Hata hivyo Ibraahiym (‘alayhis-salaam) anatupa mafunzo makubwa hapa kuwa juu ya kwamba alimuita baba yake kwa upole na adabu kisha baba yake akamjibu kwa kumkemea, majibu ya Ibraahiym (‘alayhis-salaam) yalikuwa ni ya uzuri zaidi kwa kumtakia amani iwe juu yake na kumuombea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amghufurie.



قَالَ سَلَامٌ عَلَيْكَ ۖ سَأَسْتَغْفِرُ لَكَ رَبِّي ۖ إِنَّهُ كَانَ بِي حَفِيًّا ﴿٤٧﴾وَأَعْتَزِلُكُمْ وَمَا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَأَدْعُو رَبِّي عَسَىٰ أَلَّا أَكُونَ بِدُعَاءِ رَبِّي شَقِيًّا ﴿٤٨﴾

47. (Ibraahiym) Akasema: Salaamun ‘Alayka. (Amani iwe juu yako). Nitakuombea maghfirah kwa Rabb wangu. Hakika Yeye daima ni Mwenye kunihurumia sana. 48. Na natengana nanyi na mnavyoviomba badala ya Allaah; na namuomba Rabb wangu asaa nisijekuwa mwenye kunyimwa du’aa yangu kwa kumwomba Rabb wangu. [Maryam:47- 48]





Baba Yake Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) Atageuzwa Kuwa Fisi Siku Ya Qiyaamah Na Kutupwa Motoni:





Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alijiombea Du'aa mwenyewe na kumuombea baba yake:



رَبِّ هَبْ لِي حُكْمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ ﴿٨٣﴾وَاجْعَل لِّي لِسَانَ صِدْقٍ فِي الْآخِرِينَ ﴿٨٤﴾وَاجْعَلْنِي مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ النَّعِيمِ ﴿٨٥﴾وَاغْفِرْ لِأَبِي إِنَّهُ كَانَ مِنَ الضَّالِّينَ ﴿٨٦﴾وَلَا تُخْزِنِي يَوْمَ يُبْعَثُونَ ﴿٨٧﴾يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ ﴿٨٨﴾إِلَّا مَنْ أَتَى اللَّـهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ ﴿٨٩﴾

83. Rabb wangu! Nitunukie hikmah; elimu ya Dini na Unikutanishe na Swalihina. 84. Na Nijaalie kusifika kwa heshima kwa vizazi watakaokuja baadaye. 85. Na Nijaalie miongoni mwa warithi wa Jannah ya neema. 86. Na Mghufurie baba yangu, hakika yeye amekuwa miongoni mwa waliopotea. 87. Na wala Usinihizi Siku watakayofufuliwa. 88. Siku hayatofaa mali wa watoto. 89. Isipokuwa yule atakayemfikia Allaah na moyo uliosalimika. [Ash-Shu'araa: 83-89]



Tunaona kwamba katika Du'aa hizo Ibraahiym (‘alayhis-salaam) amemuombea baba yake maghfira kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:



وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ ۚ إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَأَوَّاهٌ حَلِيمٌ ﴿١١٤﴾

Na haikuwa Ibraahiym kumuombea maghfirah baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyoahidiana naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Allaah, alijiepusha naye. Hakika Ibraahiym ni mwenye huruma mno na mvumilivu. [At-Tawbah:114]



Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: "Ibraahiym (‘alayhis-salaam) aliendelea kumuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amghufurie baba yake mpaka alipokufa. Baada ya hapo alipotambua kwamba baba yake amekufa akiwa ni adui ya Allaah, akajitenga naye". [At-Twabariy 14.519]





Katika kauli ya

وَلَا تُخْزِنِي يَوْمَ يُبْعَثُونَ ﴿٨٧﴾

Na wala Usinihizi Siku watakayofufuliwa. [Ash-Shu'araa 87]



Imaam Al-Bukhaariy amesimulia Hadiyth ifuatayo:



عن أبي هريرة، رضي الله عنه، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((إن إبراهيم رأى أباه يوم القيامة عليه الغَبَرَةُ والقَتَرَةُ)) البخاري 4768

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasul wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Ibraahiym atamuona baba yake siku ya Qiyaamah akiwa amefunikwa na vumbi na kiza” [Al-Bukhaariy 4768].



Usimulizi mwingine kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:





يلقى إبراهيم أباه، فيقول: يا رب، إنك وعدتني أنك لا تخزيني يوم يبعثون. فيقول الله: إني حرمت الجنة على الكافرين

Ibraahiym atakutana na baba yake na atasema: "Ee Rabb, Umeniahidi kwamba Hutonihizi siku watakaofufuliwa viumbe vyote". Allaah Atasema: "Nimeiharamisha Jannah (Pepo) kwa makafiri" [Fat-h Al-Baariy 8:357]



Usimulizi mwingine vile vile:



((يلقى إبراهيم أباه آزر يوم القيامة، وعلى وجه آزر قَتَرَةٌ وغَبَرة، فيقول له إبراهيم: ألم أقل لك: لا تعصني فيقول أبوه: فاليوم لا أعصيك. فيقول إبراهيم: يا رب، إنك وعدتني ألا تخزيني يوم يبعثون، فأي خزي أخزى من أبي الأبعد؟ فيقول الله تعالى: إني حرمت الجنة على الكافرين. ثم يُقال: يا إبراهيم، ما تحت رجليك؟ فينظر فإذا هو بذبح متلطخ، فيؤخذ بقوائمه فيلقى في النار)) البخاري

Ibraahiym atakutana na baba yake Aazar siku ya Qiyaamah na kutakuweko na vumbi na kiza usoni mwa Aazar. Ibraahiym atamuambia: "Sikukuambia kwamba usiniasi?". Baba yake atasema: "Leo sikuasi". Ibraahiym atasema: "Ee Rabb, Umeniahidi kwamba hutonihizi siku watakaofufuliwa, lakini hizaa gani itakuwa kubwa zaidi ya kumuona baba yangu katika hali hii?". Allaah Atamuambia: "Nimeharamisha Jannah (Pepo) kwa makafiri". Kisha itasemwa: "Ee Ibraahiym! Tazama chini ya miguu yako". Atatazama na ataona (kwamba baba yake amebadilishwa kuwa) fisi amefunikwa katika samadi/kinyesi, atachukuliwa kwa miguu yake na kutupwa motoni. [Al-Bukhaariy 3350 katika kunukuliwa na Fat-h Al-Baariy 6:445]



Kugeuzwa baba yake Ibraahiym (‘alayhis-salaam) kuwa fisi ni Rahma kutoka kwa Allaah ili Ibraahiym (‘alayhis-salaam) asimuone baba yake katika sura yake akiwa anatupwa motoni.





Kuvunja Masanamu:



Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anatuambia kuhusu Khaliyl Wake Ibraahiym (‘alayhis-salaam) na vipi Alivyomjaalia uongofu tokea zamani yaani tokea udogoni mwake. Alimpa moyo kwa kumuonyesha haki na dalili dhidi ya watu wake kwa yale waliokuwa wakiabudu kama Anavyosema:



وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ .. ﴿٨٣﴾

Na hiyo ndio hoja Yetu Tuliyompa Ibraahiym juu ya watu wake... [Al-An'aam:83]



Na kumpa uongofu tokea alipokuwa mdogo Anasema Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa

وَلَقَدْ آتَيْنَا إِبْرَاهِيمَ رُشْدَهُ مِن قَبْلُ وَكُنَّا بِهِ عَالِمِينَ ﴿٥١﴾

Na kwa yakini Tulimpa Ibraahiym uongofu wake kabla, na Tulikuwa Wenye kumjua vizuri. [A-Anbiyaa:51]



Na ndio maana alipokuwa mdogo alikuwa anashangazwa na ibada yao ya masanamu, akiyaendea masanamu hayo kuyatazama na kuona jinsi walivyokuwa wapumbavu watu wake kuabudu mawe yaliyochongwa ambayo akiona kuwa hayawezi kuwafaa kitu wala kuwadhuru kitu.



Akaapa Ibraahiym (‘alayhis-salaam) kuwa atayavunja haya masanamu, na alipoapa kiapo hicho mmoja wa watu wake alimsikia. Walikuwa wana sikukuu ambayo walikuwa wakienda wote kusherehekea. Yeye akabakia, na walipomuuliza sababu ya kutokwenda aliwajibu kuwa anaumwa.

فَنَظَرَ نَظْرَةً فِي النُّجُومِ ﴿٨٨﴾فَقَالَ إِنِّي سَقِيمٌ ﴿٨٩﴾

Akatazama mtazamo katika nyota. 89. Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa. [As-Swaaffaat: 88-89]



Ilikuwa siku moja baada ya kuapa kuwa atayavunja masanamu. Watu wake wakatoka kwenda kwenye sherehe zao, huku nyuma Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akayavunja masanamu yote isipokuwa sanamu kubwa kabisa, akachukua shoka alilotumia kuwavunjia na kuliweka katika mikono ya hilo sanamu kubwa ili watu wafikiri kuwa hilo sanamu ndilo lililovunja masanamu mingine. Akaanza kwa kuapa kuwa atayafanyia hila masanamu yao:

وَتَاللَّـهِ لَأَكِيدَنَّ أَصْنَامَكُم بَعْدَ أَن تُوَلُّوا مُدْبِرِينَ ﴿٥٧﴾فَجَعَلَهُمْ جُذَاذًا إِلَّا كَبِيرًا لَّهُمْ لَعَلَّهُمْ إِلَيْهِ يَرْجِعُونَ ﴿٥٨﴾

57. Na naapa kwa Allaah, bila shaka nitafanyia hila masanamu yenu baada ya mkishageuka kwenda zenu. 58. Basi akayavunja vipande vipande isipokuwa kubwa lao ili wapate kulirejea. [Al-Anbiyaa: 57-58]



Walikuwa wanawaekea chakula masanamu yao na alipokwenda kuyavunja masanamu Ibraahiym (‘alayhis-salaam) aliyasemesha na kuyauliza masanamu kwa kejeli:



فَتَوَلَّوْا عَنْهُ مُدْبِرِينَ ﴿٩٠﴾ فَرَاغَ إِلَىٰ آلِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ ﴿٩١﴾مَا لَكُمْ لَا تَنطِقُونَ ﴿٩٢﴾ فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًا بِالْيَمِينِ ﴿٩٣﴾

90. Wakaachana naye wakimgeukilia mbali kwenda zao. 91. Akaenda kwa siri kwa waabudiwa wao; akasema: Mbona hamli? 92. Mna nini! Mbona hamsemi?
93. Akayakabili (masanamu) kwa siri akawapiga kwa mkono wa kulia. [As-Swaaffaat: 90-93]



Waliporudi wakapatwa na mshangao mkubwa kuona masanamu yao wanayoyaabudu yamevunjwa!



قَالُوا مَن فَعَلَ هَـٰذَا بِآلِهَتِنَا إِنَّهُ لَمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٩﴾ قَالُوا سَمِعْنَا فَتًى يَذْكُرُهُمْ يُقَالُ لَهُ إِبْرَاهِيمُ ﴿٦٠﴾قَالُوا فَأْتُوا بِهِ عَلَىٰ أَعْيُنِ النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَشْهَدُونَ ﴿٦١﴾قَالُوا أَأَنتَ فَعَلْتَ هَـٰذَا بِآلِهَتِنَا يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿٦٢﴾قَالَ بَلْ فَعَلَهُ كَبِيرُهُمْ هَـٰذَا فَاسْأَلُوهُمْ إِن كَانُوا يَنطِقُونَ ﴿٦٣﴾


59. Wakasema: Nani amefanya hivi kwa waabudiwa wetu? Hakika yeye ni miongoni mwa madhalimu. 60. Wakasema: Tulimsikia kijana akiwataja anaitwa Ibraahiym. 61. Wakasema: Mleteni mbele ya macho ya watu ili wapate kushuhudia. 62. Wakasema: Je, ni wewe uliyefanya hivi kwa waabudiwa wetu, ee Ibraahiym? 63. Akasema: Hapana, bali amefanya hayo hili kubwa lao. Hivyo waulizeni wakiwa wanaweza kunena! [Al-Anbiyaa:59-63]



Wakajirudi kidogo kuwaza kwamba kweli walikuwa wanaabudu miungu isioweza hata kujikinga na madhara, lakini kuwaza kwao kulikuwa kwa muda mdogo, kisha wakarudi katika upotofu ule ule:



فَرَجَعُوا إِلَىٰ أَنفُسِهِمْ فَقَالُوا إِنَّكُمْ أَنتُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٦٤﴾ثُمَّ نُكِسُوا عَلَىٰ رُءُوسِهِمْ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا هَـٰؤُلَاءِ يَنطِقُونَ ﴿٦٥﴾قَالَ أَفَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكُمْ شَيْئًا وَلَا يَضُرُّكُمْ ﴿٦٦﴾أُفٍّ لَّكُمْ وَلِمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٧﴾

64. Basi wakajirudia nafsi zao, wakasema: Hakika nyinyi ndio madhalimu. 65. Kisha wakarudia hali yao ya mwanzo ya upotofu: (Wakasema): Umekwishajua kwamba hawa hawasemi. 66. (Ibraahiym) Akasema: Je, basi mnaabudu badala ya Allaah isiyokunufaisheni kitu chochote na wala kukudhuruni? 67. Aibu yenu nyinyi na vile mnavyoviabudu badala ya Allaah. Je, hamtii akilini? [Al-Anbiyaa: 64-67]



Hii ndio ilikuwa sababu khaswa ya Ibraahiym (‘alayhis-salaam) ya kuyavunja hayo masanamu ili wajiulize na watambue ujinga wao wa kuabudu vitu visivyosema na wala visivyoweza kujihifadhi na madhara.



Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) Anaingizwa Katika Moto:



Hapo tena ndipo walipotaka kumchoma moto:



قَالُوا حَرِّقُوهُ وَانصُرُوا آلِهَتَكُمْ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ ﴿٦٨﴾

Wakasema: Muunguzeni na mnusuru waabudiwa wenu, mkiwa ni wafanyao (kunusuru). [Al-Anbiyaa:68]



Wakakusanya kuni nyingi kabisa za kuandaa moto mkubwa. Wakachimba shimo na ukawashwa moto uliowaka kwa cheche kubwa, moto ambao haujapata kuwashwa moto kama huo kabla wakamtia Ibraahiym (‘alayhis- salaam).



Yafuatayao ni maelezo mbali mbali kuhusu tukio hilo:



-Bwana mmoja Mkurdi aliyekuwa ni mhamajihamaji, ambaye ametokea Persia, alitoa rai kuwa Ibraahiym (‘alayhis-salaam) atiwe katika manati kubwa (chombo cha kurushia mawe) [Al-Qurtwubiy 11:303]



-Shu'ayb Al-Jabaa'i kasema: (Bwana huyo) "Jina lake alikuwa ni Hayzan na kwa sababu ya rai yake hiyo aliyotoa, Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Kamjaalia kumezwa na ardhi na ataendelea kudidimia hadi siku ya Qiyaamah.



-Alipotumbukizwa Ibraahiym (‘alayhis-salaam) katika moto alisema:

حَسْبُنا اللَّه وَ نِعْم الْوَكِيل

Ananitosheleza Allaah na Yeye Ndiye Mbora wa kupanga mambo yangu [At-Twabariy 18:465]



-Inavyosemekana kuwa zilikusanywa kuni kwa muda wa mwezi na alipotupwa kwenye moto huo alikuja Jibriyl (‘alayhis-salaam) akasema: Ee Ibraahiym, una haja yoyote? Akajibu: Ama kwako la!



حَسْبِيَ اللَّه وَنِعْمَ الْوَكِيِل

Hasbiya-Allaah Wa Ni'mal-Wakiyl [Aysarut-Tafaasiyr – Abu-Bakkar Al-Jazaairiy 3:426]



-Kutokana na wingi wa kuni zilizokusanywa ilifika hadi watu kuweka nadhiri, ya kupeleka kuni.



-As-Sudi kasema: "Mwanamke alipokuwa akiumwa akiweka nadhiri kuwa akipona ataleta kuni za kumuunguza Ibraahiym (‘alayhis-salaam). [Al-Qurtubiy 11:303]



-Kutokana na Hadiyth ifuatayo, baadhi ya Mufassiriyn wamesema kwamba fadhila hii ya kuwa Ibraahiym (‘alayhi-salaam) atakuwa ni mtu wa kwanza kuvishwa nguo, ni kwa sababu yakutiwa motoni bila ya sababu yoyote ya haki bali kwa kushikilia Tawhiyd na kukanusha shirk:



عن ‏ ‏ابن عباس ‏ ‏رضي الله عنهما ‏ عن النبي ‏ ‏صلى الله عليه وسلم ‏قال: ((إنكم محشورون حفاة عراة غرلا ثم قرأ ((كما بدأنا أول خلق نعيده)) وأول من يكسى يوم القيامة إبراهيم)) البخاري ومسلم

Imetoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)

amesema: “Mtafufuliwa bila ya viatu, uchi nabila ya kutahiriwa (khitaan) kisha akasoma”: ((Kama Tulivyoanza umbo la awali tutalirudisha tena)) na wa kwanza kuvalishwa nguo siku ya Qiyaamah ni Ibraahiym)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



-Sa'iyd bin Jubayr karipoti kwamba Ibn 'Abbaas kasema: "Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alipotupwa katika moto, Malaika wa mvua alisema: Lini nitaruhusiwa kuteremsha mvua? Lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Alijibu haraka kama aya inavyosema:



قُلْنَا يَا نَارُ كُونِي بَرْدًا وَسَلَامًا عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ ﴿٦٩﴾

Tukasema: Ee moto! Kuwa baridi, na salama juu ya Ibraahiym! [Al-Anbiyaa: 69]



-Na kwa maneno hayo ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) hakuna moto uliokuwa ukiwaka duniani wakati huo ila ulizimwa [At-Twabariy 18:466]



-Ibn 'Abbaas na Abu Al-Aliyah kasema: "Ingelikuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Hakusema (Hakuuambia moto):

.. وَسَلَامًا …﴿٦٩﴾

Na salama



Basi Ibraahiym (‘alayhis-salaam) angelidhurika kwa ubaridi wake [At-Twabariy 18:466, 465]



-Qataadah amesema: "Siku hiyo hakikuweko kiumbe kisichojaribu kuuzima moto wa Ibraahiym (‘alayhi wa sallam) ila mjusi" [At-Twabariy 18:467].



-Az-Zuhriy kasema: "Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamrisha kuwa (mjusi) auliwe na akaitwa 'mnyama mharibifu' [At-Twabariy 18:467 na pia imesimuliwa katika Muslim Namba 2238]



Mbinu zao za kutaka kumuunguza Ibraahiym (‘alayhis-salaam) katika moto hazikufaulu kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa).



وَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَخْسَرِينَ ﴿٧٠﴾

Na wakamkusudia njama; lakini Tukawajaalia wao ndio wenye kukhasirika. [Al-Anbiyaa:70]



Moto ukamalizika kuwaka, watu wakiwa wanasubiri kwa hamu kubwa waone majivu tu, lakini dhana yao iliwashtua, na walitahayarika walipomuona Ibraahiym (‘alayhis-salaam) anatoka salama mbele ya macho yao akitembea mzima bila ya kudhurika popote. Ni muujiza mkubwa hakika!



Lakini kama kawaida ya hali ya watu wa zamani walivyokuwa na ukaidi wao hawakumuamini Ibraahiym (‘alayhis-salaam) na wito wake wa ibada ya Tawhiyd kwamba kuna Ilaah Apasaye kuabudiwa Pekee, Ambaye Alifanya maajabu haya ya Moto kutokumuunguza Ibraahiym (‘alayhis- salaam).





Ibraahiym (‘Alayhis-salaam) Anahama Iraq Kuelekea Shaam:



Hakuamini mtu isipokuwa Luutw (‘alayhis-salaam) ambaye alikuwa ni binamu (cousin) wake, na mke wake Saarah.



فَآمَنَ لَهُ لُوطٌ ۘ وَقَالَ إِنِّي مُهَاجِرٌ إِلَىٰ رَبِّي ۖ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٦﴾

Basi Luutw akamwamini; na (Ibraahiym) akasema: Hakika mimi nahajiri kwa Rabb wangu; hakika Yeye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al'Ankabuut: 26]



Vile vile akasema Ibraahiym (‘alayhis-salaam):



وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهْدِينِ ﴿٩٩﴾رَبِّ هَبْ لِي مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٠٠﴾

99. Akasema: Hakika mimi ni mwenye kwenda kwa Rabb wangu Ataniongoza. 100. Rabb wangu! Nitunukie miongoni mwa Swalihina. [As-Swaaffaat: 99-100]

Hapo tena Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akamhamisha na kumpeleka Shaam nchi ambayo ndio iliyokusudiwa kuwa 'nchi Tulioibariki'.



وَنَجَّيْنَاهُ وَلُوطًا إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا لِلْعَالَمِينَ ﴿٧١﴾

Na Tukamuokoa na Luutw kuelekea ardhi ambayo Tumeibariki humo kwa walimwengu. [Al-Anbiyaa:71]



Na kutokana na Du'aa yake hiyo ya:

رَبِّ هَبْ لِي مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٠٠﴾

Rabb wangu! Nitunukie miongoni mwa Swalihin. [As-Swaaffaat:100]



Allaah (Subhaanahu Allaahu wa Ta’aalaa) Akamjaaliya kupata watoto kama aya zifuatazo zinavyotuelezea:

فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ ﴿١٠١﴾

Basi Tukambashiria ghulamu mvumilivu. [As-Swaaffaat:101]



Aayah hii imekusudiwa ni Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam)



Na katika Aayah nyingine Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)

وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ نَافِلَةً ۖ وَكُلًّا جَعَلْنَا صَالِحِينَ ﴿٧٢﴾

Na Tukamtunukia Is-haaq na (mjukuu) Ya’quwb kuwa ni ziada. Na wote Tumewajaalia kuwa Swalihina. [Al-Anbiyaa:72]



'Atwaa' na Mujaahid wamesema: "Naafilatan (Na ziada) ina maana kwamba zawadi" [At-Twabariy 18:471]



Ibn 'Abbaas na Qataadah wamesema: "Zawadi ya mtoto mwenye mtoto, maana kwamba Ya'quwb alikuwa mtoto wa Is-haaq kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa)

.. فَبَشَّرْنَاهَا بِإِسْحَاقَ وَمِن وَرَاءِ إِسْحَاقَ يَعْقُوبَ﴿٧١﴾

..Tukambashiria Is-haaq na baada ya Is-haaq ni Ya’quwb. [Huwd:71]





.../3
 
Kisa Cha Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) - 3



Alhidaaya.com





Kuhama Iraq:



وَنَجَّيْنَاهُ وَلُوطًا إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا لِلْعَالَمِينَ ﴿٧١﴾

Na Tukamuokoa na Luutw kuelekea ardhi ambayo Tumeibariki humo kwa walimwengu. [Al-Anbiyaa:71]



Ibraahiym (‘alayhis-salaam) aliondoka Iraq pamoja na Luutw (‘alayhis-salaam) na wakaelekea kwanza katika mji unaoitwa 'Aur, kisha Haraan, kisha tena Falastina (Palestine).



Alivyompata Haajar (Mama wa Nabiy Ismaa’iyl (‘alayhis-salaam):



Akaelekea Misri na wakati wote alipokuwa safarini ilikuwa hima yake ni kuwaita watu katika Tawhiyd, kuwaongoza katika haki na katika mambo mema. Alipokuwa anaelekea Misri alipita mji wa dhalimu mmoja, akapiga kambi hapo. Matukio yote hapo yameelezwa katika Hadiyth ifuatayo:



عن أبي هريرة رضي الله عنه؛ أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((إن إبراهيم، عليه السلام، لم يكذب غير ثلاث: ثنتين في ذات الله ، قوله: ( بَلْ فَعَلَهُ كَبِيرُهُمْ هَذَا ) وقوله (إِنِّي سَقِيمٌ ) قال: "وبينا هو يسير في أرض جبار من الجبابرة ومعه سارة، إذ نـزل منـزلا فأتى الجبار رجل، فقال: إنه قد نـزل بأرضك رجل معه امرأة أحسن الناس، فأرسل إليه فجاء، فقال: ما هذه المرأة منك؟ قال: هي أختي. قال: فاذهب فأرسل بها إليّ، فانطلق إلى سارة فقال: إن هذا الجبار سألني عنك فأخبرته أنك أختي فلا تكذبيني عنده، فإنك أختي في كتاب الله، وأنه ليس في الأرض مسلم غيري وغيرك، فانطلق بها إبراهيم ثم قام يصلي. فلما أن دخلت عليه فرآها أهوى إليها، فتناولها، فأخذ أخذًا شديدًا، فقال: ادعي الله لي ولا أضرك، فدعت له فأرسل، فأهوى إليها، فتناولها فأخذ بمثلها أو أشد. ففعل ذلك الثالثة فأخذ، [فذكر] مثل المرتين الأوليين فقال ادعي الله فلا أضرك. فدعت، له فأرسل، ثم دعا أدنى حجابه، فقال: إنك لم تأتني بإنسان، وإنما أتيتني بشيطان، أخرجها وأعطها هاجر، فأخرجت وأعطيت هاجر، فأقبلت، فلما أحس إبراهيم بمجيئها انفتل من صلاته، قال: مَهْيَم؟ قالت: كفى الله كيد الكافر الفاجر، وأخدمني هاجر)



قال محمد بن سيرين وكان: أبو هريرة إذا حدث بهذا الحديث قال: فتلك أمكم يا بني ماء السماء



Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya-Allaahu ‘anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “ Ibraahiym (‘alayhis-salaam) hakuongopa ila mara tatu tu; mara mbili kwa ajili ya Allaah aliposema:

( بَلْ فَعَلَهُ كَبِيرُهُمْ هَذَا )

((Bali amefanya hayo huyu mkubwa wao))



na aliposema:

(إِنِّي سَقِيمٌ )

((Hakika mimi ni mgonjwa!)). Na alipokuwa akisafiri katika mji wa dhalimu mmoja na (mkewe) Sarah alikuwa naye. Alipopiga kambi, mtu mmoja alikwenda kwa dhalimu na kumwambia, "Kuna mtu amepiga kambi katika ardhi yako na anaye mwanamke mzuri kupita wote". Dhalimu akamuita Ibraahiym (‘alayhis-salaam) kwake, na akamuuliza, "Nini uhusiano wa mwanamke huyu na wewe?". Akasema, "Yeye ni dada yangu". Dhalimu akasema, "Nenda kamlete kwangu". Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akaenda kwa Sarah na akasema, "Dhalimu huyu ameniuliza kuhusu wewe, na nimemwambia kwamba wewe ni dada yangu, kwa hiyo usimfanye akajua kwamba nimeongopa, kwani hakika ni dada yangu kufuatana na kitabu cha Allaah, na hakuna Waislamu katika ardhi hii ila mimi na wewe". Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akampeleka (Sarah) kwake, kisha akasimama na kuswali. Alipoingia kwa dhalimu na (dhalimu) alipomuona (Sarah), akataka kumshika kwa matamanio, lakini akagandishiwa (mkono) Akasema, "Niombee kwa Allaah na sitokudhuru". Sarah akamuombea, na akaachiliwa. Kisha akamfikia kwa matamanio, lakini akapatwa tena (kuganda mkono) kama mwanzo au zaidi. Ikaendelea hivyo mara tatu, na kila mara alisema kama alivyosema mara ya mwanzo. Kisha akamwita mlinzi wake wa karibu naye kabisa na akasema, "Hukuniletea binaadamu bali umenilitea shaytwaan! Muondoshe na mpe Haajar". Akaondoshwa (Sarah) na kupewa Haajar, akarudi. Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alipotambua kuwa (Sarah) amerudi, alimaliza kuswali na kugeuka akasema, "Imekuwaje?". Akasema, "Allaah Ametosheleza njama za kafiri dhalimu, na amenipa Haajar kama mtumwa")) [Al-Bukhaariy na Muslim].



Muhammad bin Siriyn amesema, "Abu Huraryah amesimulia Hadiyth hii akasema: "Huyu ni mama yenu enyi wana wa maji ya mbinguni" (yaani Waarabu kizazi cha Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam), mwana wa Haajar ambaye ndiye aliyesababisha maji ya Zamzam). [Fat-h Al-Baariy 6:447, Muslim 4:1840]



Mke wa Ibraahiym (‘alayhis-salaam) Sarah, alikuwa tasa. Na Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alikuwa anazeeka na nywele zake zikatawaliwa na mvi baada ya kuita watu miaka mingi katika dini ya Allaah. Sarah akafikiria kwamba yeye na Ibraahiym (‘alayhis-salaam) wako katika upweke kwa vile hawakupata mtoto. Kwa hiyo akampa mumewe mtumwa wake Haajar amuoe. Haajar akamzaa Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) ambaye ndiye mtoto wa mwanzo wa Ibraahiym (‘alayhis-salaam).



Siku zikapita na Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akawa na furaha ya kupata mtoto, lakini Sarah akawa na wivu sasa na Haajar, ingawa yeye mwenyewe ndiye aliyempa Ibraahiym (‘alayhis-salaam) Haajar amuoe. Wivu huo ukamfanya Haajar awe anajificha ili Sarah asimuone anapokwenda kwa mumewe. Akawa ni mwanamke wa kwanza kufunga mkanda kuficha alama zake kama ilivyotajwa katika Hadiyth ndefu kutoka kwa Al-Bukhaariy iliyopokelewa na Ibn 'Abbaas kwamba "Haajar ni mwanamke wa mwanzo kutumia mkanda".



Makusudio hapo ni mkanda kiunoni kuzuia nguo yake ndefu inayoburuza ardhini isiache alama apitapo (ikaja ikajulikana na Sarah kuwa kapita). Inasemekana kuwa wakati huo wanawake walikuwa wakivaa nguo ndefu zinazoburuza. Na hii inaonyesha jinsi stara ilivyokuwa kwa wanawake tangu wakati huo.



Pia katika masimulizi kwenye Al-Bukhaariy anasema, ''Wakati Nabii Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alipomuoa Haajar na akamzalia Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam), mkewe wa mwanzo, Sarah, akapata wivu na akaapa kuwa atamkata mwili wake vipande vitatu, hivyo Haajar akajifunga mkanda kiunoni mwake na kukimbia huku akiburuza vazi lake nyuma yake ili kufuta alama za nyayo zake ili Sarah asiweze kujua alipoelekea. [Al Bukhaariy - Kitabu cha Visa Vya Manabiim, Hadiyth namba 3364]



Na Allaah Anajua zaidi.





Safari ya Makkah:



Siku moja Ibraahiym (‘alayhis-salaam) aliamka na kumwambia mke wake Haajar ajitayarishe kwa safari ndefu. Baada ya siku chache, Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akaanza safari yake pamoja na mkewe na mwanawe Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) ambaye alikuwa bado ananyonya.

Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akatembea na kupitia ardhi zilizolimwa, majangwa na milima hadi akafika katika jangwa la kisiwa cha Uarabu (Arabian Peninsula) na akafika katika bonde lisilolimwa ambalo halikuwa na miti wala matunda wala chakula wala maji. Bonde hilo halikuwa na athari yoyote ya maisha. Baada ya kumsaidia mkewe kuteremka kipando cha safari, akawaacha hapo wakiwa na chakula na maji kidogo tu ya kuwatosheleza kama siku mbili tu.



Aligeuka nyuma na kuondoka. Nyuma yake mkewe akamkimbilia na kumuuliza: "Unakwenda wapi ee Ibraahiym na kutuacha sisi katika bonde hili tupu?" Ibraahiym (‘alayhis-salaam) hakumjibu kitu bali aliendelea kuondoka. Haajar alirudia kumuuliza tena, lakini alinyamaza kimya bila ya kumjibu. Mwishowe alifahamu kuwa hafanyi hivyo kwa matamanio au amri yake, na akatambua kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amemuamrisha kufanya hivyo. Akamuuliza: "Je, Allaah Amekuamrisha ufanye hivyo?". Akamjibu: "Naam". Haajar akasema: "Basi hatutapotea kwani Allaah Aliyekuamrisha Atakuwa nasi". Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akaondoka na alipokuwa mbali kiasi ya kutowaona akaomba:



رَّبَّنَا إِنِّي أَسْكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِندَ بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا الصَّلَاةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِّنَ النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُم مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ ﴿٣٧﴾

Rabb wetu! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria wangu katika bonde lisilokuwa na mmea wowote, kwenye Nyumba Yako Tukufu. Rabb wetu, ili wasimamishe Swalaah na Ujaalie nyoyo za watu zielekee kwao na Uwaruzuku mazao ili wapate kushukuru. [Ibraahiym :37]





Kupatikana Maji Ya Zamzam:





Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akamuacha mkewe na mwanawe katika jangwa na akarudi alikotoka kuendelea kufanya daawah ya kuwalingania watu katika katika Tawhiyd. Haajar akabakia kumlea mwanawe hapo alipoachwa. Chakula kiliwaishia, maziwa yakamkauka, jua lilikua kali mno, maji waliyokuwa nayo yalikwisha na kiu kikawashika, hali ikawa mbaya ya njaa ya kiu kikubwa.



Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) akaanza kulia kwa kiu. Mama yake akamuacha kwenda kutafuta maji. Akatembea kwa haraka hadi akafikia kilima cha Swafaa. Akapanda kilima na kuangaza kama ataona kisima au aone kama kuna msafara au chochote ili apate maji, lakini hakuona lolote. Akateremka kilima na akawa anahangaika kwenda baina ya kilima cha Swafaa na kilima cha Marwah, akipanda vilima vyote kila anapofikia kuangaza kama ataona lolote, lakini hakufanikiwa, na huku mwanawe anagaragara na kulia kwa kiu. Akawa anatembea na huku akikimbia mara nyingine baina ya Swafaa na Marwah kwa mara saba. Na ndio maana wenye kutekeleza ‘Umrah au Hajj, huwa wanatembea baina ya vilima viwili hivyo kama ni taratibu mojawapo ya ‘Umrah na Hajj.



Hakika hii taadhima kubwa aliyojaaliwa nayo Haajar, na ni fakhari kwa wanawake wote wa Kiislamu kuwa taratibu hiyo ya kutembelea baina ya vilima vya Swafaa na Marwah, imekuwa ni ibaada tukufu na inatekelezwa na milioni ya watu tokea zama za Hajj na itaendelea hadi siku ya Qiyaamah.



Alipofika Marwah kwa mara ya saba, alisikia sauti, mara akamuona Malaika anachimba ardhini kwa mbawa zake na mara maji yakamwagika kwa nguvu kabisa, akawa anayateka na kuyazuia yasimwagike zaidi.



عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: ((يرحم الله أم إسماعيل لو تركت زمزم)) أو قال: ((لو لم تغرف من الماء لكانت زمزم عينًا معينًا )) البخاري



Imetoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) kwamba Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “(Allaah Amrehemu mama yake Ismaa'iyl angeliacha (maji ya Zamzam)) (yamwagike bila ya kuyazuia) au kasema ((asingelichota kutoka katika maji hayo, Zamzam ingelikuwa chemchemu inayoendelea kumwagika katika ardhi))” [Al-Bukhaariy]



Akanywa maji na kumnywesha mwanawe. Kulikuwa na misafara ya watu kutoka Yemen na walipoona kuna ndege wanazunguka wakatambua kuwa ni sehemu yenye maji. Walikuwa watu wa kabila la Jurhum kutoka Yemen wakaja kuishi hapo. Wakamuuliza Haajar: "Je, unaturuhusu tuishi hapa?" Akajibu: "Naam, lakini hamtakua na haki kumiliki maji haya ya Zamzam". Wakakubali na Haajar akaridhika na akafurahi kupata watu kuishi nao. Wakaleta familia zao na wakazidi kuwa wengi hapo.



Mtihani Mkubwa Aliopewa Nabiy Ibraahiym (‘alayhis-salaam) Wa Ndoto Ya Kumchinja Mwanawe Ismaa’iyl:





Miaka ikapita na Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akawa anamtembelea mkewe Haajar na mwanawe mara kwa mara. Kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akamtahini kuhusu mapenzi ya mwanawe Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam). Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema hayo katika Aayah zifuatazo:





وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهْدِينِ ﴿٩٩﴾رَبِّ هَبْ لِي مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١٠٠﴾فَبَشَّرْنَاهُ بِغُلَامٍ حَلِيمٍ ﴿١٠١﴾فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ السَّعْيَ قَالَ يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّابِرِينَ ﴿١٠٢﴾فَلَمَّا أَسْلَمَا وَتَلَّهُ لِلْجَبِينِ ﴿١٠٣﴾وَنَادَيْنَاهُ أَن يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿١٠٤﴾قَدْ صَدَّقْتَ الرُّؤْيَا ۚإِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿١٠٥﴾إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْبَلَاءُ الْمُبِينُ ﴿١٠٦﴾وَفَدَيْنَاهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ ﴿١٠٧﴾وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ ﴿١٠٨﴾سَلَامٌ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ ﴿١٠٩﴾كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ ﴿١١٠﴾إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ ﴿١١١﴾

99. Akasema: Hakika mimi ni mwenye kwenda kwa Rabb wangu Ataniongoza. 100. Rabb wangu! Nitunukie miongoni mwa Swalihina. 101. Basi Tukambashiria ghulamu mvumilivu. 102. Alipofikia makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye; akasema: Ee mwanangu! Hakika mimi nimeona ndoto usingizini kwamba mimi nakunchinja, basi tazama unaonaje? (Ismaa’iyl) Akasema: Ee baba yangu! Fanya yale uliyoamrishwa, utanikuta In Shaa Allaah miongoni mwa wanaosubiri. 103. Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza kifudifudi juu ya kipaji. 104. Na tukamwita: Ee Ibraahiym. 105. Kwa yakini umesadikisha ndoto. Hakika Sisi hivyo ndivyo Tunavyolipa wafanyao ihsaan. 106. Hakika hili bila shaka ni jaribio bayana. 107. Na Tukamtolea fidia kwa dhabihu adhimu. 108. Na Tukamuachia (sifa nzuri) kwa karne za baadaye. 109. Salaamun! Amani iwe juu ya Ibraahiym. 110. Hakika hivyo ndivyo Tunavyolipa wafanyao ihsaan. 111. Hakika yeye ni miongoni mwa waja Wetu Waumini. [As-Swaaffaat: 99-111]



Hakika huu ulikuwa ni mtihani mkubwa kwa Ibraahiym (‘alayhis-salaam) wa kuoteshwa amchinje mwanawe kwa kuwa ni mwana mmoja tu aliyejaaliwa na ambaye aliyempenda sana, na aliyeruzukiwa baada ya kufika uzee.



Ibraahiym (‘alayhis-salaam) anatupa fundisho ya adabu baina ya mzazi na mtoto, pindi alipomtajia Nabiy Ismaa’iyl kuwa ameoteshwa amchinje. Alimuuliza anaonaje? Basi Nabiy Ibraahiym (‘alayhis-saalaam) ameonyesha upole na huruma kwa mwanawe na adabu njema, kwa sababu, angelimchinja bila ya kumtaka ushauri wake maadamu ni amri ya kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Na hivyo kwa kuwa ndoto za Manabii ni Wahyi kutoka kwa Allaah:



.. يَا بُنَيَّ إِنِّي أَرَىٰ فِي الْمَنَامِ أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ مَاذَا تَرَىٰ ۚ.. ﴿١٠٢﴾

Ee mwanangu! Hakika mimi nimeona ndoto usingizini kwamba mimi nakunchinja, basi tazama unaonaje? [As-Swaafaat: 102]



Na mtoto naye anatupa mafunzo kwa kuheshimu wito wa baba yake ambao anajua haukuja kwa matamanio yake bali ni kutimiza amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), amri ambayo baba yake alijua ni muhimu kuliko mapenzi ya mwanawe. Naye Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) alimjibu:



.. ۚ قَالَ يَا أَبَتِ افْعَلْ مَا تُؤْمَرُ ۖ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللَّـهُ مِنَ الصَّابِرِينَ ﴿١٠٢﴾

Ee baba yangu! Fanya yale uliyoamrishwa, utanikuta In Shaa Allaah miongoni mwa wanaosubiri. [As-Swaaffaat:102]



Basi Nabiy Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alitambua mapenzi na utiifu wa mwanawe kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwani hakujali kuchinjwa bali aliona kutekeleza amri ya Mola wake ni muhimu kuliko maisha yake.



Nabiy Ibraahiym (alayhis-salaam) alimlaza Ismaa’iyl kifudifudi ili asimuone wakati anapomchinja, bila shaka kutokana na huruma. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:



فَلَمَّا أَسْلَمَا وَتَلَّهُ لِلْجَبِينِ ﴿١٠٣﴾

Basi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza kifudifudi juu ya kipaji. [As-Swaaffaat:103]



Yaani: Wote wawili walitamka Shahaada na kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwani alikuwa Ibraahiym (‘alayhis-salaam) anakaribia kumchinja Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam), hivyo ingelikuwa ni mauti yake. Au 'walipojisalimisha' ina maana kwamba walipofuata amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alimtii Mola wake na Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) pia alimtii baba yake. Hii ni rai ya Mujaahid, Ikrimah, Qataadah, As-Sudi na Ibn Is-haaq na wengineo. [At-Twabariy 21:77]



Maana ya:



.. وَتَلَّهُ لِلْجَبِينِ ﴿١٠٣﴾

na akamlaza kifudifudi juu ya kipaji.



ni kwamba, alimuelekeza uso wake kifudifudi ili amchinje kutoka kwa nyuma ili iwe wepesi kwake kufanya hivyo (asipate kuuona uso wake akashikwa na huruma na kushindwa kutekeleza amri ya Mola wake). Ibn 'Abbaas, Mujaahid, Sa'iyd bin Jubayr, Adhw-Dhwahaak na Qataadah wamesema ina maana kwamba, "Alimgeuza kifudifudi". [At-Twabariy 21:77, 78]





Shaytwaan Anamshawishi Ibraahiym Asimchinje Mwanawe Ismaa’iyl:



Imaam Ahmad amerekodi kwamba Ibn 'Abbaas amesema: "Wakati alipokuwa anataka kutekeleza Ibraahiym (‘alayhis-salaam) amri ya kumchinja 'Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam), shaytwaan alimjia katika Mas'aa na akakimbia naye, lakini Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alifika mwanzo. Kisha Jibriyl (‘alayhis-salaam) akamchukua katika Jamratul-'Aqabah na shaytwaan akamjia tena huko, kwa hiyo akamtupia vijiwe saba mpaka akatokomea. Kisha akamjia tena katika Jamratul-Wustwaa, akamtupia vijiwe saba. Kisha akamlaza kifudifudi. Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) alikuwa amevaa shati jeupe akasema: "Ee baba yangu, sina nguo yoyote ambayo nitakafiniwa, kwa hiyo nivue ili iwe nikafiniwe nayo.” Alianza kuivua ndipo alipoitwa nyuma:



وَنَادَيْنَاهُ أَن يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿١٠٤﴾قَدْ صَدَّقْتَ الرُّؤْيَا ۚإِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ﴿١٠٥﴾

104. Na tukamwita: Ee Ibraahiym. 105. Kwa yakini umesadikisha ndoto. Hakika Sisi hivyo ndivyo Tunavyolipa wafanyao ihsaan. [As-Swaaffaat:104-105]



Ibraahiym (‘alayhis-salaam) aligeuka, tahamaki akamuona kondoo mweupe mzuri mwenye pembe.



Ibn 'Abbaas kasema: "Tulikuwa tukitafuta aina kama ya huyo kondoo" (yaani wakati wa kuchinja katika 'Iydul-Adhwhaa) [Ahmad: 1:297]



As-Suddiy na wengineo wamesema kwamba alikipitisha kisu shingoni mwa Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) lakini hakikumkata kwa sababu aliwekewa bamba la shaba.



Na ndipo Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alipoitwa:



قَدْ صَدَّقْتَ الرُّؤْيَا ۚ…﴿١٠٥﴾

Kwa yakini umesadikisha ndoto [As-Swaaffaat:105]

[At-Twabariy 21:74]



Ibn 'Abbaas amesema kuwa: "Kondoo huyo alikuzwa Peponi kwa muda wa miaka arubaini". [At-Twabariy 21:90]



Kitendo hiki cha kuchinja ndicho kinachofanyika katika taratibu za Hajj, kufuata Sunnah ya baba yetu Ibraahiym (‘alayhis-salaam), ya kurusha vijiwe katika milingoti mitatu.





Uthibitisho Kwama Aliyetaka Kuchinjwa Ni Ismaa’iyl Na Sio Is-haaq Kama Wanavyodai Watu Wa Kitabu:



Imaam Ahmad amerekodi kwamba Swafiyyah bin Shaybah alisema: "Mwanamke kutoka Bani Sulaym ambaye alikuwa mkunga wa wengi katika jamii yetu, kaniambia kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma 'Uthmaan bin Twalhah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akazifunike pembe katika Ka'bah ili zisiwashawishi watu wanaposwali: Akasema Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:



))إني كنتُ رأيت قرني الكبش، حين دخلت البيت، فنسيت أن آمرك أن تخمرهما، فَخَمَّرْهما، فإنه لا ينبغي أن يكون في البيت شيء يشغل المصلي". قال سفيان: لم يزل قرنا الكبش معلقين في البيت حتى احترق البيت، فاحترقا)) أحمد.

“Niliziona pembe za kondoo nilipoingia katika Nyumba (yaani Ka’bah) nikasahau kukuambia uzifunike, zifunike kwani kusiweko na kitu katika nyumba (Ka'bah) cha kuwashawishi watu wanaofanya ibada”. [Ahmad 4:68]



Wasimulizi waliosimulia kuhusu pembe hizo za kondoo:



-Sufyan kasema: "Pembe za kondoo zilibakia zikining'inia katika Nyumba (Ka'bah) hadi zilipoungua wakati Nyumba ilipoungua".



-Sa'iyd bin Jubayr, 'Aamir Ash-Sha'abiy, Yuusuf bin Mihraan, Mujaahid, 'Atwaa' na wengineo wameripoti kutoka Ibn 'Abbaas kwamba alikuwa ni 'Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam).



-Ibn Jariyr amesimulia kwamba Ibn 'Abbaas amesema: "Aliyefidiwa alikuwa ni Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam). Mayahudi wamedai kuwa ni Is-haaq, lakini Mayahudi wameongopa". [At-Twabariy 21:83]



-Ibn Is-haaq amesema, "Nimemsikia Muhammad bin Ka'ab Al-Quraazi anasema, "Ambaye Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ameamuamrisha Ibraahiym (‘alayhis-salaam) kumchinja miongoni mwa wanawe wawili alikuwa ni Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam).



Tunapata dalili hii kutoka kitabu cha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anapomalizia kisa cha mmoja wa wana wawili wa Ibraahiym (‘alayhis-salaam) ambaye alitakiwa kuchinjwa Anasema:



وَبَشَّرْنَاهُ بِإِسْحَاقَ نَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٢﴾

Na Tukambashiria Is-haaq; Nabiy miongoni mwa Swalihina. [As-Swaaffaat:112]



Vile vile,

وَامْرَأَتُهُ قَائِمَةٌ فَضَحِكَتْ فَبَشَّرْنَاهَا بِإِسْحَاقَ وَمِن وَرَاءِ إِسْحَاقَ يَعْقُوبَ﴿٧١﴾



Na mkewe amesimama wima, akacheka; Tukambashiria Is-haaq na baada ya Is-haaq ni Ya’quwb. [Huud:71]



Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amemtaja mtoto na mwanawe (Ya’quwb), lakini Asingelimuamrisha kumchinja Is-haaq wakati Aliahidi kuwa mwanawe (Is-haaq) atazaa mtoto. Kwa hiyo ni dhahiri kuwa yule aliyeamrishwa amchinje ni Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam). [At-Twabariy 21:84].



Hadiyth nyingi zimenukuliwa kuhusu mas-ala haya [Tafsiyr Ibn Kathiyr 8:277-279]





Ziara Ya Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam) Kwa Wake Zake Ismaa’iyl:



Maelezo haya yamenukuliwa kutoka Hadiyth ndefu ya Ibn 'Abbaas iliyosimuliwa na Al-Bukhaariy:



Baada ya kufa mama yake Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam), Ibraahiym alikuja kumtembelea Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) nyumbani kwake (ambaye alikuwa amekwishaoa). Alipofika hakumkuta Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) bali alimkuta mkewe peke yake. Akamuuliza: "Yuko wapi Ismaa'iyl?" Akajibu: "Amekwenda kutafuta rizki". Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akamuuliza kuhusu hali ya maisha yao, akajibu: "Tunaishi katika shida, dhiki na karaha". Akamwambia: "Atakaporudi mumeo mpe salam zangu na mwambie abadilishe kizingiti chake".



Aliporudi Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) alihisi hali sio ya kawaida yaani kama kumetokea kitu, akamuuliza mkewe: "Je, amekuja mtu yeyote kukutembelea?" Akajibu: "Naam! Ni Bwana mmoja mtu mzima mwenye sifa kadha na kadha amekuja na ameniuliza kuhusu wewe nikamjulisha, kisha akaniuliza kuhusu hali ya maisha, nikamuambia kuwa tunaishi katika shida, dhiki na umasikini". Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) hapo akamuuliza: "Je, amekupa maagizo yangu yoyote?". Akajibu: "Naam! Amenipa salaam zako, kisha amesema nikuambie kuwa ubadilishe kizingiti chako". Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) akasema: "Huyo ni baba yangu, na ameniamrisha nikutaliki, hivyo basi rudi kwenu". Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) akampa talaka, kisha akaoa mwanamke mwingine miongoni mwao (yaani kutoka kabila la Jurhumu).



Mara ya pili alipokuja Ibraahiym (‘alayhis-salaam) kumtembelea Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) alimkuta mke wake Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) wa pili, alipoumuuliza kuhusu Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) alisema: "Amekwenda kutafuta rizki". Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akamuuliza kuhusu maisha yao, akajibu: "Tuko katika neema na tumebahatika (yaani tuna kila kitu cha kututosheleza)". Akamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akamuuliza: "Aina gani ya chakula mnakula?" Akasema: "Nyama". Akasema: "Mnakunywa nini?", Akasema: "Maji". Akasema: "Ya Allaah Wabarikie nyama yao na maji yao". (Mke huyo wa Ismaa’iyl amesema hivyo ingawa hali yao ilikuwa ni ya shida).



Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akamwambia mke wa Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam): "Atakaporudi mumeo mpe salaam zangu na mwambie ashikilie kizingiti chake". Aliporudi Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) alimuuliza mkewe: "Je, amekuja mtu yeyote?". Akajibu: "Naam! Amekuja bwana mmoja mtu mzima mwenye sura nzuri". Akamsifia kisha akaendelea: "Ameniuliza kuhusu wewe nikamjulisha, kisha akauliza kuhusu hali ya maisha yetu, nikamuambia kuwa tunaishi katika hali nzuri". Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) akamuuliza: "Je, alikupa nasiha yoyote?" Akajibu: "Naam! Amekupa salaam zake kisha anakuamrisha ushikilie kizingiti chako".



Kwa maneno haya, Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) akasema: "Huyo alikuwa ni baba yangu na wewe ndio kizingiti, na ameniamrisha nibakie na wewe".







.../4
 
Kisa Cha Nabiy Ibraahiym (‘Alayhi-Salaam) – 4



Alhidaaya.com





Kujenga Al-Ka’bah:



Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akamuamrisha Ibraahiym (‘alayhis-salaam) ajenge Al-Ka'bah. Ibraahiym (‘alayhis-salaam) na Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) wakapandisha msingi wa nyumba (yaani Ka'bah). Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) akawa analeta mawe huku Ibraahiym (‘alayhis-salaam) anajenga. Kuta za nyumba ziliponyanyuka juu, Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) alileta jiwe na kumpa Ibraahiym (‘alayhis-salaam) ili asimamie kuendelea kujenga huku Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) anamletea mawe.



Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alikuwa akisimama juu ya jiwe hilo, na kila alipomaliza kujenga upande mmoja, alisogea upande mwingine kumalizia kujenga Ka’bah.



Jiwe hilo liliweka alama ya miguu yake Ibraahiym (‘alayhis-salaam). Alipomaliza kujenga, aliliweka jiwe karibu na ukuta wa Ka’bah na hapo ndipo mahali lilipokuwa miaka yote hiyo hadi ilipofika zama za ukhalifa wa 'Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye alilisogeza kutoka kuta za Ka’bah. 'Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ni mmoja wa wawili ambao Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa salaam) amesema:



اقتدوا باللَّذَين من بعدي أبي بكر وعمر

“Wafuateni watakaokuwa baada yangu, Abu Bakar na 'Umar” [Tuhfat Al-Ahwadhiy: 569]



Na hapo ndipo mahali panapoitwa Maqaam Ibraahiym (Kisimamo cha Ibraahiym) ambako mwenye kufanya Hajj au 'Umrah, anapaswa kuswali Raka'ah mbili baada ya kufanya twawaaf.



Na amri ya kuswali Raka'ah mbili ilikuwa ni kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), kama ilivyo katika Hadiyth ifuatayo:



عَنْ أَنَسٍ، قَالَ قَالَ عُمَرُ: وَافَقْتُ رَبِّي فِي ثَلاَثٍ، فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ لَوِ اتَّخَذْنَا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى فَنَزَلَتْ: ((‏وَاتَّخِذُوا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى))‏ وَآيَةُ الْحِجَابِ، قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، لَوْ أَمَرْتَ نِسَاءَكَ أَنْ يَحْتَجِبْنَ، فَإِنَّهُ يُكَلِّمُهُنَّ الْبَرُّ وَالْفَاجِرُ‏.‏ فَنَزَلَتْ آيَةُ الْحِجَابِ، وَاجْتَمَعَ نِسَاءُ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي الْغَيْرَةِ عَلَيْهِ فَقُلْتُ لَهُنَّ عَسَى رَبُّهُ إِنْ طَلَّقَكُنَّ أَنْ يُبَدِّلَهُ أَزْوَاجًا خَيْرًا مِنْكُنَّ‏.‏ فَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ‏

Kutoka kwa ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rabb Wangu Ameniwafikia mambo matatu: Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Lau tungefanya sehemu aliyosimamia Ibraahiym kuwa sehemu ya kuswali. Ikateremka:



.. وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ ...﴿١٢٥﴾

“na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia.” (2: 125) Na Aayah ya hijaab nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Ungewaamrisha wake zako kujiwekea hijaab (kizuizi) kutokana na wanaume kwa sababu watu wema na waovu wanaongea nao. Basi ikateremka Aayah ya hijaab kwa wanawake. Na wakeze Nabiy walijiunga dhidi ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na wivu wao baina yao. Nikawaambia: Huenda akutalikini kisha Rabb wake Ambadilishie wake walio bora zaidi kuliko nyinyi” ikateremka Aayah (At-Tahriym 5) [Al-Bukhaariy]



Utukufu Wa Ka’bah:





a-Mahali Pa Salama Na Amani:



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kuhusu utukufu wa Ka’bah:



وَإِذْ جَعَلْنَا الْبَيْتَ مَثَابَةً لِّلنَّاسِ وَأَمْنًا وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ وَعَهِدْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ ﴿١٢٥﴾



Na Tulipoifanya Nyumba (Al-Ka’bah) kuwa ni mahali pa kurejewa na watu na pa amani, na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia. Na Tulichukua ahadi kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl kwamba: Itakaseni Nyumba Yangu kwa wanaotufu na wanaokaa i’tikaaf, na wanaorukuu na kusujudu. [Al-Baqarah:125].





Mahali pa amani: Yaani: amani kutokana na maadui. Na ikaendelea Ka’bah kuwa mahali patukufu na amani tokea zama hizo na itaendelea mpaka Siku ya Qiyaamah. Hata zama za ujaahiliyyah watu mara nyingi walikuwa ni waathirika wa uvamizi na watekwa nyara, ila waliokuwa katika eneo la Ka’bah (Al-Masjidul-Haraam) ndio walikuwa katika usalama wa kutekwa nyara. [At-Twabariy 3:29]





Vile vile Mujaahid, 'Atwaa' As-Suddiy, Qataadah na Ar-Rabi' bin Anas wameripotiwa wakisema kwamba: Aayah hiyo ina maana: "Yeyote atakayeingia humo atakuwa salama". [Ibn-Abi Haatim 1:370].





Aayah hii ina inaonyesha kwamba, Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ameitukuza nyumba hii tukufu ambayo Ameifanya iwe kimbilio na bandari ya salama. Kwa hiyo nafsi za watu huwa zina hamu kubwa ya kuweko hapo, na hawachoshwi kutembelea kila mara au kila mwaka. Hii ni kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Aliikubali Duaa ya Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alipomuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), Ajaaliye nyoyo za watu zipende kuelekea huko, wakati alipomuacha mkewe Haajar na mwanawe Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) mwanzo kabisa pindi alipofika hapo. [Al-Bukhaariy 3364]



Aliomba:



رَّبَّنَا إِنِّي أَسْكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِندَ بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا الصَّلَاةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِّنَ النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُم مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ ﴿٣٧﴾

Rabb wetu! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria wangu katika bonde lisilokuwa na mmea wowote, kwenye Nyumba Yako Tukufu. Rabb wetu, ili wasimamishe Swalaah na Ujaalie nyoyo za watu zielekee kwao na Uwaruzuku mazao ili wapate kushukuru. [Ibraahiym :37]





b-Mahali Patukufu Pa Kuswaliwa:



Heshima ya mwanzo inamfikia Ibraahiym (‘alayhis-salaam) kwa kufanywa sehemu aliyosimama kujenga Ka’bah kuwa mahali patukufu pa kuswaliwa.



.. وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى ۖ ...﴿١٢٥﴾



Na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia. [Al-Baqarah:125]





c-Nyumba Iliyotakaswa:



Vile vile ilikuwa ni amri kwa Ibraahiym (‘alayhis-salaam) na mwanawe Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) kwamba waitakase Ka’bah.



ۖ وَعَهِدْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ أَن طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ ﴿١٢٥﴾



Na Tulichukua ahadi kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl kwamba: Itakaseni Nyumba Yangu kwa wanaotufu na wanaokaa i’tikaaf, na wanaorukuu na kusujudu [Al-Baqarah:125]



Hali kadhalika ilikuwa ni amri ya kuitakasa na shirki:



وَإِذْ بَوَّأْنَا لِإِبْرَاهِيمَ مَكَانَ الْبَيْتِ أَن لَّا تُشْرِكْ بِي شَيْئًا وَطَهِّرْ بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْقَائِمِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ ﴿٢٦﴾



Na (taja) Tulipomwonyesha Ibraahiym mahali pa Nyumba; Al-Ka’bah, (Tukamwambia): Usinishirikishe na chochote; na twaharisha Nyumba Yangu kwa wafanyao Twawaaf, na wanaosimama kuswali na wanaorukuu na kusujudu. [Al-Hajj:26]





Maana: Ifanye iwe safi kwa wale wanaomuabudu Allaah Pekee bila ya kumshikirikisha na mtu au msaidizi.





d-Nyumba Ya Pekee Inayozungukwa Kama Ibaada:



Ni nyumba pekee katika ulimwengu wa Waislamu inayozungukwa, kuwa ni ibaada. Twawaaf na Swalaah zimetajwa pamoja katika Aayah hiyo, kwa sababu hakuna mahali popote kwengine kulikofaradhishwa ibaada hizi mbili kwa pamoja, isipokuwa hapa katika Ka’bah.





e-Ni Msikiti Wa Mwanzo Ulimwenguni Na Ni Msikiti Wenye Baraka Na Mwongozo:





Nayo ni nyumba ya mwanzo kabisa duniani iliyofanywa kuwa ya ibaada, yenye baraka, uongofu kwa watu wote, na ndipo Waislamu huenda kutekeleza Hajj:



إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾

Hakika nyumba ya awali iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibaada) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah), yenye barakah na mwongozo kwa walimwengu. [Aal-‘Imraan:96]



عن أبي ذَر، رضي الله عنه، قال قلتُ: يا رسولَ الله، أيُّ مَسجِد وُضِع في الأرض أوَّلُ؟ قال: الْمسْجِدُ الْحَرَام .قلت: ثم أَيُّ؟ قال: الْمسجِدُ الأقْصَى. قلت: كم بينهما؟ قال: أرْبَعُونَ سَنَةً .قلتُ: ثم أَيُّ؟ قال: ثُم حَيْثُ أدْرَكْت الصَلاةَ فَصَلِّ، فَكُلُّهَا مَسْجِدٌ. أخرجه البخاري، ومسلم، وأحمد

Imetoka kwa Abu Dharr amesema: "Nilisema Ee Rasuli wa Allaah! Ni Msikiti gani ulikuwa wa mwanzo kabisa kujengwa duniani?" Akasema: ((Al-Masjidul-Haraam)) (Ulioko Makkah). Nikasema: Kisha upi? Akasema: ((Al-Masjidul-Aqswaa)) (Palestina). Nikasema: Ilikuwa muda gani kujengwa baina yao? Akasema: ((Miaka arubaini)) Akaongeza: ((Popote (mtakapokuwa) na Swalaah ikawakuta, Swalini humo, kwani ardhi yote imefanywa kuwa ni mahali pa kusujudu)) [Al-Bukhaariy, Muslim na Imaam Ahmad]



Usemi mwingine kutoka kwa wataalamu wanaofasiri, wamesema kuwa kwa vile Adam (‘alayhis-salaam) ni kiumbe cha mwanzo katika ardhi, alipewa heshima kujenga nyumba ya mwanzo ya ibaada. Aliijenga kisha akaizunguka kama Malaika wanvyozunguka juu katika Baytul-Ma'amuur huko juu katika 'Arshi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) iliyoko katika mbingu ya saba. Na inasemekana alijenga hema akawa anafanya ibaada yake hapo, lakini baada ya kufariki na karne nyingi kupia, ikapotea alama ya sehemu hiyo.





f-Nguzo Ya Tano Ya Kiislamu Inatimizwa Hapo:





فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ ۖ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا ۗ وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾

Ndani yake kuna Aayaat (Ishara, Dalili) zilizo wazi; mahali pa kisimamo cha Ibraahiym. Na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru, basi hakika Allaah ni Mkwasi kwa walimwengu. [Al-'Imraan: 97]





Du’aa Za Ibraahiym ‘Alayhis -Salaam Baada Ya Kujenga Ka’bah:



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):



وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿١٢٧﴾

Na aliponyanyua Ibraahiym na Ismaa’iyl msingi wa Nyumba (Al-Ka’bah): Rabb wetu, Tutakabalie, hakika Wewe ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote. [Al-Baqarah:127]



Hapa tunapata fundisho kubwa kutoka kwa baba yetu Nabiy Ibraahiym (‘alayhis-salaam) kwamba ingawa yeye na Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) wamejenga Ka’bah, ambayo inayozungukwa na Waislamu kama ni ibaada tukufu, lakini hawakutegemea kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Atawapokelea amali hii moja kwa moja, bali walimuomba Allaah Awatakabalie. Hivi ni katika sifa za Waumini kuwa baina ya khofu na matumaini wanapotekeleza amali njema. Na sisi tunatakiwa tuwe tunaiomba Duaa hii kila mara tunapomaliza matendo mema, kwani nasi hatujui kama matendo yetu yatakubaliwa na Allaah.



Akaendelea Ibraahiym (‘alayhis-salaam) kuomba pamoja na mwanawe Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam)



رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ ﴿١٢٨﴾

Rabb wetu, Tujaalie tuwe wenye kujisalimisha Kwako pamoja na kizazi chetu wawe ummah wenye kujisalimisha Kwako na Tuonyeshe taratibu za ibaada zetu na Pokea tawbah zetu, hakika Wewe ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu. [Al-Baqarah: 128]

.. وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا .. ﴿١٢٨﴾

na Tuonyeshe taratibu za ibaada zetu



Ina maana ni Taratibu za Hajj na 'Umrah ambazo Waislamu wanazifuata kutekelea nguzo hii ya Kiislamu.



رَبَّنَا وَابْعَثْ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِكَ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَيُزَكِّيهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٢٩﴾

Rabb wetu, wapelekee Rasuli miongoni mwao atakayewasomea Aayaat Zako na atakayewafunza Kitabu na Hikmah na atakayewatakasa. Hakika Wewe ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Baqarah:129]



Duaa hii: ((Waletee Rasuli anayetokana na wao)), ndio sababu ya kutoka Nabiy wa mwisho kutoka kizazi cha Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam), ambaye ni Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa salaam).



Vile vile maana ya ((awasomee Aayah Zako, na awafundishe Kitabu na hikma)), ni Kitabu cha mwisho kuteremshwa kutoka mbinguni; Qur-aan aliyoteremshiwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa salaam) kwa ajili ya walimwengu wote.



Duaa nyingine alizoomba Ibraahiym (‘alayhis-salaam):

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّ اجْعَلْ هَـٰذَا الْبَلَدَ آمِنًا وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ ﴿٣٥﴾ رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ ۖ فَمَن تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي ۖ وَمَنْ عَصَانِي فَإِنَّكَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣٦﴾ رَّبَّنَا إِنِّي أَسْكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيْرِ ذِي زَرْعٍ عِندَ بَيْتِكَ الْمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُوا الصَّلَاةَ فَاجْعَلْ أَفْئِدَةً مِّنَ النَّاسِ تَهْوِي إِلَيْهِمْ وَارْزُقْهُم مِّنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَشْكُرُونَ ﴿٣٧﴾ رَبَّنَا إِنَّكَ تَعْلَمُ مَا نُخْفِي وَمَا نُعْلِنُ ۗ وَمَا يَخْفَىٰ عَلَى اللَّـهِ مِن شَيْءٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ﴿٣٨﴾الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي وَهَبَ لِي عَلَى الْكِبَرِ إِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبِّي لَسَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٩﴾رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلَاةِ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَاءِ﴿٤٠﴾رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾


35. Na pindi Ibraahiym aliposema: Ee Rabb wangu! Ujaalie mji huu (Makkah) uwe wa amani; na Uniepushe na wanangu kuabudu masanamu. Rabb wangu! Hakika hao (masanamu) wamepoteza wengi kati ya watu. Basi atakayenifuata, huyo ni katika mimi, na atakayeniasi, basi hakika Wewe ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. Rabb wetu! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya dhuria wangu katika bonde lisilokuwa na mmea wowote, kwenye Nyumba Yako Tukufu. Rabb wetu, ili wasimamishe Swalaah na Ujaalie nyoyo za watu zielekee kwao na Uwaruzuku mazao ili wapate kushukuru. Rabb wetu! Hakika Wewe Unajua tunayoyaficha na tunayoyadhihirisha. Na hakifichiki kitu chochote kwa Allaah katika ardhi wala katika mbingu. AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Ambaye Amenitunukia juu ya umri mkubwa wangu Ismaa’iyl na Is-haaq. Hakika Rabb wangu bila shaka ni Mwenye kusikia duaa yangu. Rabb wangu! Nijaalie niwe mwenye kusimamisha Swalaah na dhuria wangu. Rabb wetu! Nitakabalie duaa yangu. Rabb wetu! Nighufurie na wazazi wangu wawili na Waumini Siku itakayosimama hesabu. [Ibraahiym: 35-41]





Kuwaadhinia Watu Waitikie Kwenda Hajj:



Alipomaliza Nabiy Ibraahiym (‘alayhis-salaam) kujenga Ka’bah, Allaah Alimtaka awatangazie watu wafike Makkah kuhiji:



وَأَذِّن فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالًا وَعَلَىٰ كُلِّ ضَامِرٍ يَأْتِينَ مِن كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٍ ﴿٢٧﴾

Na tangaza kwa watu Hajj; watakufikia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, watakuja kutoka katika kila njia pana za milima zilioko mbali kabisa. [Al-Hajj:27]



Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alisema: "Rabb wangu, vipi niwatangazie watu hivyo na hali sauti yangu haitawafikia?" Akaambiwa: "Waite (waadhinie) na Sisi Tutawafikishia". Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akasimama na kusema: "Enyi watu! Rabb wenu Ameanzisha Nyumba ili mje kuhiji".



Imesemekana kuwa milima ilijiinamisha ili sauti ifikie pande zote za dunia, na ikawafikia watu wote mpaka waliokuwa matumboni mwa mama zao na migongo ya baba zao (yaani waliokuwa bado hawakuzaliwa).



Majibu yakawa ni:

"لبيك اللهم لبيك"





"Labbayka Allaahumma Labbayk"



Nimekuitika Ee Allaah nimekuitika,





Na hao ni ambao wamejaaliwa kutekeleza Hajj. Na kauli hiyo anaitamka mwenye kufanya Hajj au Umrah anapoingia katika Ihraam.





Kuondoka Makkah Baada Ya Kujenga Ka’bah:



Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akaondoka na mkewa Sarah kurudi Palestina. Lakini alumuacha Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) pamoja na familia yake Makkah.



Siku moja, Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alikuwa amekaa katika kambi yake akimfikiria mwanawe Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) kuhusu ndoto ya kumchinja na fidia Aliyomteremshia Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Moyo wake ukazidi kujaa mapenzi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa neema Zake zisizohesabika. Chozi kubwa likamdondoka alivyokuwa akimfikiria Ismaa'iyl (‘alayhis-salaam) na umbali alioko, jinsi alivyokuwa akimkosa na hamu ya kuwa naye.





Mara Malaika watatu wakateremka; Jibriyl, Israafiyl na Miykaaiyl. Walimjia kwa maumbo ya binaadamu wenye sura nzuri kabisa. Ibraahiym (‘alayhis-salaam) aliinuka na kuwakaribisha. Aliwaita ndani ya kambi huku akiwaza kuwa ni wageni asiowajua. Akawakaribisha vizuri na kuhakikisha kuwa wamestarehe, kisha akaomba idhini kwao ili aende kwa ahli yake. (kuagiza waletewe chakula).



Sarah wakati huo ameshakuwa mzee, mvi zimemjaa kichwani. Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akamuambia: "Tumepata wageni watatu".



Akamuuliza: "Ni nani hao?" Akamjibu: "Simjui hata mmoja wao". Akauliza Ibraahiym (‘alayhis-salaam): "Tuna chakula gani?". Akajibu Sarah: "Tuna nusu kondoo". Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akasema: "Nusu kondoo? Wachinjie nusu ndama, kwani wao ni wageni tusiowajua na hatujui pengine wana njaa".



Watumishi wakachinja nusu ndama na kumchoma vizuri. Kikaletwa chakula mbele ya hao wageni, Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akawakaribisha wasogee kula. Akaona hawasogei kula, basi akaanza kula yeye ili awatie moyo nao watake kula lakini aliona kuwa hakuna hata mmoja wao aliyegusa chakula. Akawauliza: "Kwa nini hamli?". Akaendelea yeye kula, lakini wao walibakia vile vile bila ya kukaribisha mikono yao katika chakula. Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akaanza kuogopa.



Khofu ya Ibraahiym (‘alayhis-salaam) ikazidi na Malaika wakawa wanamsoma mawazo yake, kisha mmoja wao akasema: "Usikhofu". Ibraahiym (‘alayhis-salaam) akasema: "Hakika nina khofu, kwani nimekukaribisheni mle lakini naona hamjanyoosha mikono yenu kutaka kula. Je, mmekusudia uovu?"



Malaika mmoja akatabasamu na kusema: "Sisi hatuli, kwani sisi ni Malaika wa Allaah". Mmoja wao akageuka kwa mkewe Ibraahiym (‘alayhis-salaam) na kumbashiria bishara njema ya mwana Is-haaq.

Ibraahiym (‘alayhis-salaam) na Sarah walishtuka kubashiriwa mtoto katika umri huo walionao. Lakini juu ya mshtuko huo, Sarah aliingiwa na furaha kubwa kuwa atapata mtoto ambaye alimtamani miaka mingi sana! Na furaha ilizidi alipoambiwa kuwa mtoto huyo atakuwa ni mtoto mwenye ujuzi.



Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anatuelezea matukio haya kwa kirefu katika Aayah zifuatazo:



وَنَبِّئْهُمْ عَن ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ﴿٥١﴾إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا قَالَ إِنَّا مِنكُمْ وَجِلُونَ﴿٥٢﴾قَالُوا لَا تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ﴿٥٣﴾ قَالَ أَبَشَّرْتُمُونِي عَلَىٰ أَن مَّسَّنِيَ الْكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ﴿٥٤﴾قَالُوا بَشَّرْنَاكَ بِالْحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ الْقَانِطِينَ﴿٥٥﴾قَالَ وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ﴿٥٦﴾قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ﴿٥٧﴾قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ﴿٥٨﴾إِلَّا آلَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ﴿٥٩﴾إِلَّا امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَا ۙ إِنَّهَا لَمِنَ الْغَابِرِينَ﴿٦٠﴾

Na wajulishe kuhusu wageni wa Ibraahiym. Pale walipoingia kwake, wakasema: Salaama! (Ibraahiym) Akasema: Hakika sisi tunakuogopeni. (Malaika) Wakasema: Usiogope! Hakika sisi tunakubashiria ghulamu mjuzi. (Ibraahiym) Akasema: Je, mnanibashiria (mwana) na hali uzee umeshanishika, basi kwa njia gani mnanibashiria? Wakasema: Tunakubashiria kwa haki, basi usiwe miongoni mwa wakatao tamaa. Akasema: Na nani anayekata tamaa na rahmah ya Rabb wake isipokuwa wapotofu. Akasema: Basi nini jambo lenu muhimu enyi Wajumbe. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakhalifu. Isipokuwa familia ya Luutw, hakika Sisi Tutawaokoa wote. Isipokuwa mkewe Tumehukumu kwamba yeye bila shaka ni miongoni mwa watakaobakia nyuma (kuangamizwa). [Al-Hijr: 51-60]



Waliposema kuwa wanakwenda kuangamiza mji wa Luutw (‘alayhis-salaam) Ibraahiym (‘alayhis-salaam) alikhofu kuwa vipi wataangamiza mji huo na hali yumo Luutw (‘alayhis-salaam)? Majibu yao Malaika yamo katika aayah zifuatazo:



وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ قَالُوا إِنَّا مُهْلِكُو أَهْلِ هَـٰذِهِ الْقَرْيَةِ ۖ إِنَّ أَهْلَهَا كَانُوا ظَالِمِينَ ﴿٣١﴾ قَالَ إِنَّ فِيهَا لُوطًا ۚ قَالُوا نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَن فِيهَا ۖ لَنُنَجِّيَنَّهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ ﴿٣٢﴾

Na Wajumbe Wetu walipomjia Ibraahiym kwa bishara walisema: Hakika sisi tutawahiliki watu wa mji huu. Hakika watu wake wamekuwa madhalimu. (Ibraahiym) Akasema: Hakika humo yumo Luutw. (Malaika) Wakasema: Sisi tunajua zaidi waliokuwemo humo; tutamuokoa na ahli zake isipokuwa mke wake amekuwa miongoni mwa watakaobakia nyuma. [Al-'Ankabuwt: 31-32]



هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ﴿٢٤﴾إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ﴿٢٥﴾فَرَاغَ إِلَىٰ أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ﴿٢٦﴾فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ﴿٢٧﴾فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۖ قَالُوا لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ﴿٢٨﴾فَأَقْبَلَتِ امْرَأَتُهُ فِي صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ﴿٢٩﴾قَالُوا كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ﴿٣٠﴾قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ ﴿٣١﴾قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ ﴿٣٢﴾لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن طِينٍ ﴿٣٣﴾مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ ﴿٣٤﴾

Je, imekufikia hadithi ya wageni wahishimiwao wa Ibraahiym? Walipoingia kwake wakasema: Salaam! Akasema: Salaam watu wasiotambulikana. Akaondoka bila kuhisiwa kuelekea kwa ahli yake akaleta ndama aliyenona. Akawakurubishia; akasema: Mbona hamli? Akawaogopa ndani ya nafsi yake. Wakasema: Usikhofu! na wakambashiria ghulamu mjuzi. Mkewe akawakabili kwa hoihoi na vifujo (kushtuka), akijipiga usoni na akasema: Kikongwe, tasa! Wakasema: Hivyo ndivyo Alivyosema Rabb wako, hakika Yeye Ndiye Mwenye hikmah wa yote, Mjuzi wa yote. (Ibraahiym) Akasema: Basi nini shughuli yenu mloikusudia enyi Wajumbe? Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wahalifu. Ili Tuwapelekee mawe ya udongo. Yaliyotiwa alama kutoka kwa Rabb wako kwa wapindukao mipaka. [Adh-Dhaariyaat: 24-34]



Malaika hao walikuwa wanakwenda katika mji wa Nabiy Luutw (‘alayhis-salaam) kuwaangamiza watu wake ambao walikuwa katika maasi.

Baada ya hapo, na kutokana na kubashiriwa mtoto, Sarah akashika mimba na akamzaa Is-haaq (‘alayhis-salaam).



Naye Is-haaq (‘alayhis-salaam) akamzaa Ya'aquwb (‘alayhis-salaam) ambaye amemzaa Yuwsuf (‘alayhis-salaam) pamoja na ndugu zake wengine kumi na mojo. Mmoja wa ndugu yake Yuwsuf (‘alayhis-salaam) akiitwa Binyaamiyn ndiye aliyekuwa ni ndugu yake khalisa (ndugu kwa baba na mama).



Ibraahiym (‘alayhis-salaam) amefariki katika umri wa miaka mia na sabini na tano. [Qwisasul-Anbiyaa- Ibn Kathiyr] na amezikwa Falastina katika mji ulioitwa Khaliyl.



Na Allaah Anajua zaidi.



Mwisho wa Kisa Cha Nabiy Ibraahiym (‘Alayhis-Salaam)





Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anatujulisha kuhusu visa vya Manabii kwamba:





قَدْ كَانَ فِي قَصَصِهِمْ عِبْرَةٌ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ۗ مَا كَانَ حَدِيثًا يُفْتَرَىٰ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ كُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿١١١﴾

Kwa yakini katika visa vyao kuna mazingatio (na mafunzo) kwa wenye akili. Haikuwa (Qur-aan) hadithi zinazotungwa, lakini ni sadikisho la (Vitabu) vya kabla yake na tafsili ya waziwazi ya kila kitu, na ni mwongozo na rehma kwa watu wanaoamini. [Yuwsuf (12:111)]
 
Ajali ya Ndege India 2025: Fundisho kwa Waislamu

Mnamo Juni 12, 2025, ndege ya Air India Flight 171, aina ya Boeing 787 Dreamliner, ilipata ajali mbaya muda mfupi baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Ahmedabad kuelekea London. Ndege hiyo ilianguka kwenye jengo la hosteli ya Chuo cha Tiba cha B. J., na kusababisha vifo vya watu 279, wakiwemo abiria 241 na zaidi ya watu 38 waliokuwa ardhini. Kati ya abiria wote, mtu mmoja tu alinusurika, akitoka kwenye kifusi akiwa na majeraha madogo.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ndege ilikumbwa na hitilafu ya injini zote mbili, na kusababisha kushindwa kupata urefu wa kutosha kabla ya kuanguka. Marubani walijitahidi kuiepusha ndege isiangukie makazi ya watu, lakini iligonga jengo la kijeshi na hosteli ya chuo, na kusababisha vifo vya wanafunzi na wafanyakazi.

Fundisho kwa Waislamu:
Ajali hii inatufundisha kuwa maisha ni mafupi na hayana uhakika. Waislamu wanapaswa kuishi kwa kumcha Allah kila wakati, kwani hatujui lini maisha yetu yatakatika. Tunapaswa kuwa tayari kwa mauti kila wakati, kwa kutubu dhambi zetu na kutenda mema. Sala na dua si kwa dharura tu, bali ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Ajali kama hizi zinatufundisha kuwa dunia si ya kudumu, na kwamba tunapaswa kuishi kwa moyo mnyenyekevu, tukimuomba msamaha Allah na kutenda mema kabla ya ajali ya maisha kutupata.
 
Maswali: Qur-aan


Anataka Tafsiri Na Ufafanuzi Wa Suwratun Nisaa

Aayah Ya 15 - (Wafanyao Machafu)



Alhidaaya.com







SWALI:



Assalam aleykum warahmatuLLahi wabarakaatuh. Shukrani sana ndugu zetu katika imani, inshALLAH Mola awalipe kheri kwa jitihada zenu za kututatulia yenye kututatiza katika dini yetu hii tukufu, namuomba ALLAH awalipe kheri hapa duniani pamoja na akhera nyinyi na sisi pia, amiin. Ammma ba'ad. Suali langu ni kwamba naomba ufafanuzi wa aya ya 15 suratul NNISAA (surat 4 verse 15), ningeomba tafsiri yake na ufafanuzi wake walau kidogo Biidhni LLAHI ta'ala. Shukran







JIBU:





AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani kwa swali lako kuhusu tafsiyr ya Suwrah An-Nisaa 4: 15. Kabla ya kutoa maelezo tungependa kukuekea tafsiyr yake hapa chini, nayo ni kama hivi:



وَاللَّاتِي يَأْتِينَ الْفَاحِشَةَ مِن نِّسَائِكُمْ فَاسْتَشْهِدُوا عَلَيْهِنَّ أَرْبَعَةً مِّنكُمْ ۖ فَإِن شَهِدُوا فَأَمْسِكُوهُنَّ فِي الْبُيُوتِ حَتَّىٰ يَتَوَفَّاهُنَّ الْمَوْتُ أَوْ يَجْعَلَ اللَّـهُ لَهُنَّ سَبِيلًا ﴿١٥﴾



Na wale wanaofanya uchafu miongoni mwa wanawake wenu, basi washuhudisheni mashahidi wanne kati yenu. Na wakishuhudia basi wazuieni majumbani mpaka mauti yawafishe au Allaah Awajaalie njia (nyingine)”.



Aayah hii imefungamana na Aayah inayofuatia ya 16.





Maelezo yake ni kuwa: “Hizi ni Aayah zinazotaja kutiwa adabu wale,



(a) Wanawake wanaofanya machafu wao kwa wao, yaani kusagana na



(b) Wanaume wanaofanya machafu, yaani ya liwati na



(c) Wanawake wanaofanya machafu na wanaume.



Yote haya ni mabaya kabisa; na zaidi ni yale ya wanaume kwa wanaume, na baadaye wanawake kwa wanawake.



Maoni ya wanachuoni wa Tafsiyr wengi ni kuwa Aayah mbili hizi ni juu ya wazinifu. Hukmu zilotajwa zilinasikhiwa (zilifutwa) na kubadilishwa na zile Aayah 2-3 Suwrah An-Nuwr:



الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ ۖ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَائِفَةٌ مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢﴾

Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamme mpigeni kila mmoja katika wawili hao mijeledi mia. Na wala isiwashikeni huruma kwa ajili yao katika hukmu ya Allaah mkiwa nyinyi mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na washuhudie adhabu yao kundi la Waumini.



الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ﴿٣﴾

Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina; na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina. Na imeharamishwa hivyo kwa Waumini. [Suwrah An-Nuwr: 2-3]





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Qur-aan


Kumfanyia Mtoto Sherehe Anapomaliza Kusoma Au Kuhifadhi Qur-aan



Alhidaaya.com





SWALI:





Assalaam aleykum .nimeambiwa na ustaadh kwamba ni lazima nimfanyie mwanangu sherehe ya kumaliza juzuu.je kuna ulazima au umuhimu wa kufanya hili jambo?

Shukran!





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hakuna dalili ya jambo hilo. Ustaadh aliyelazimisha jambo hilo ingelikuwa vyema kama angelikupa dalili kutoka katika Qur-aan au Sunnah kwani ‘amali zetu za Dini zote zinatokana na nyanzo hizo mbili. Na kwa vile hakuna dalili ya jambo hilo, basi linabakiwa jambo hilo kuwa ni la kuzushwa lisilokuwa la kweli na inapasa kujiepusha nalo.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Qur-aan


Kushika Na Kusoma Qur-aan Katika Hedhi, Nifaas Na Janaba



Alhidaaya.com







SWALI:



Jee mtu anapokua na hedhi, nifasi au Janaba anaweza kusoma Qur-an bila ya kuishika, na nini sheria yake katika hayo??



JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Suala la mwenye Hedhi kusoma Qur-aan ni suala ambalo 'ulamaa wametofautiana hukmu yake lakini ni suala lisilo na makatazo yaliyothibiti kishari'ah katika Hadiyth Sahihi. Na waliopinga mwanamke kusoma wametoa zaidi dalili ya Hadiyth inayosema: (("Hasomi mwenye janaba au mwenye hedhi chochote katika Qur-aan")) Imesimuliwa na Abu Dawud, At Tirmidhy na Ibn Maajah. Lakini Hadiyth hii ni DHAIFU kwa mujibu wa wanachuoni wa Hadiyth na wengineo akiwemo Imam Al-Bukhaariy, Ahmad bin Hanbali, Al-Bayhaqiy, Ibn Taymiyah, Ash-Shawkaaniy, Al-Albaaniy na wengineo.



Na pia waliopinga pamoja na wengi miongoni mwao kukubali kuwa mwanamke anaweza kusoma kimoyomoyo, au hata kwa sauti kwa mujibu wa wengine, lakini wamepinga kuishika hiyo Qur-aan na wametoa hoja ya kuwa mwanamke katika hali hiyo si msafi kuweza kushika Qur-aan kwa kutoa ushahidi wa aya isemayo:



لاَ يَمَسُّهُ إِلاَّ الْمُطَهَّرُونَ

Haigusi isipokuwa waliotakaswa kabisa. [Al-Waaqi'ah: 79]



Lakini pamoja na baadhi ya Maulamaa kusema kuwa aya hiyo imekusudiwa watu wote, ila kauli iliyo sahihi ya wafasiri, ni kuwa makusudio ya 'Al Mutwahharuun' katika aya hiyo ni Malaika na si wanaadam na isiyoguswa hapo si hii Misaahafu yetu tuliyonayo, bali ni Allawhul Mahfuwdh na aya za nyuma yake za 77 na 78 zinaonyesha kuwa ni Qur-aan tukufu katika Kitabu kilichohifadhiwa ambacho kiko mbinguni zinathibitisha hilo.



إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ ﴿٧٧﴾فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ ﴿٧٨﴾

Hakika hii bila shaka ni Qur-aan tukufu. Katika Kitabu kilichohifadhiwa. [Al-Waqi'ah 77-78]



Na 'ulamaa na wema waliopita wanasema kuwa waliotakaswa ni Malaika na si wanaadam. Tazama pia tafsiri ya Ibn Kathiyr.



Kwa hiyo, maadam aayah hiyo haiwakusudii wanaadam, na Hadiyth iliyotajwa mbeleni ya makatazo ya kusoma Qur-aan mwenye hedhi si sahihi, basi suala hili labaki kuwa lafaa hadi pawepo makatazo yaliyothibiti.



Na hoja nyingine ya kuonyesha kuwa jambo hilo halina makatazo, ni Hadiyth ((iliyosimuliwa na Jaabir bin 'Abdillaah kuwa katika tarehe nane ya mwezi wa Dhul Hijjah siku ijulikanayo kuwa ni ya 'Tarwiyah' walipokuwa wakielekea Minaa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), wakaleta talbiya ya Hijjah, kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaenda kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) akamkuta analia, akamuuliza: ''una nini?'' akajibu ('Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anha)) ''Nimepatwa na hedhi na watu wamehirimia na wamefanya twawaaf nami sijafanya vyote hivyo! Na watu wanaelekea kuhiji hivi sasa!!'' Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: "Hili ni jambo Aliloliandika Allaah kwa wanawake (wanaadam), basi nenda kaoge halafu kahirimie kisha Hiji na fanya yale anayofanya Mwenye kuhiji isipokuwa usitufu na kuswali". 'Aaishah akafanya matendo yote ya Hajj isipokuwa kufanya Twawaaf na Swalah.))



Hadiyth hii ya Jaabir inatuonyesha kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimruhusu kufanya yote afanyayo mwenye kuhiji kwenda Minaa kulala, kwenda 'Arafah, kutupa mawe na hata kwenda 'Swafaa wal Marwaa' ambako hapo kunasomwa aya isemayo:



إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٥٨﴾

Hakika Asw-Swafaa na Al-Marwah ni katika alama za Allaah. Basi yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah basi hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo. Na atakayejitolea kufanya khayr basi hakika Allaah ni Mwenye kupokea shukurani, Mjuzi wa yote. [Al-Baqarah: 158]



Kwa hiyo hapa tunaona kuwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) aliruhusiwa na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kufanya hata hayo ya Swafaa wal Marwaa ya kusoma Qur-aan, kwa kauli ya ((Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) "Fanya yote afanyayo mwenye kuhiji isipokuwa Twawaaf na Swalah")). Na ndio moja ya hoja ya 'Ulamaa wanaoona kuwa hakatazwi mwenye hedhi kusoma Qur-aan.



Pia tunaona kuna mgawanyiko wa makundi matatu kuhusu kusomwa Qur-aan na Mwenye Hedhi, Mwenye Nifaas na Mwenye Janaba;



Kundi la kwanza linasema wanaweza kusoma Qur-aan nalo ni Swahaba Mtukufu Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhu), Imaam Al-Bukhaariy, Ibn Mundhir na wengineo katika wema waliotangulia.



Kundi la pili ni la watu wa zama za Imaam Ahmad wanaojulikana Ahlul Hadiyth wao wanasema inajuzu kusoma lakini makruhu.



Kundi la tatu ni la ma-Imaam wa madhehebu ya ki- Shafi'i, Hanafi n.k. hayo yanapinga kabisa kusoma Qur-aan kwa watu wa hali hizo juu.



Kwa kufupisha, tunaona kwamba hakuna makatazo sahihi thabiti yenye kukataza mwanamke mwenye hedhi kusoma Qur-aan wala mwenye Nifaas na hata mwenye Janaba ingawa kwa maoni ya wengi miongoni mwa 'Ulamaa wanaonelea kuwa mwenye janaba inachukiza kwake kusoma kwa sababu hali yake inaweza kubadilika mara moja kwa kuoga janaba, yaani ni jambo ana khiyari nalo huyo mwenye janaba. Ila hali inakuwa tofauti kwa mwenye hedhi na nifaas kwa sababu wao hawana khiyari yoyote kwa hali hiyo iwapatayo ya kimaumbile.



Na mwanamke mwenye hedhi kushika Qur-aan, waliolikubali wamesema ni vizuri kushika kwa kitu glavu, au kuweka kizuizi chochote katika mkono. Lakini wanachuoni wote wamekubaliana ni rukhsa kushika Qur-aan ya Tafsiri na magazeti au vitabu vyovyote vyenye Qur-aan ndani yake isipokuwa Msahafu.







Na Allaah Anajua zaidi
 
Kusikiliza Qur-aan Huku Unafanya Kazi Zako



Alhidaaya.com





SWALI



Jee unaweza kusikiliza Qur-an kwa makini huku unafanya kazi zako jikoni kama kupika au kukosha vyombo ingawa akili yako yote iko katika kile kisomo?





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hii haina shaka kwani kusikiliza huko kwa makini ndiko kumesisitizwa zaidi. Na linalochukiza kwa baadhi ya ‘Ulamaa ni kuzungumza na huku Qur-aan inasomwa kwa ushahidi wa aya hii:



وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٢٠٤﴾

Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na bakieni kimya (mzingatie) ili mpate kurehemewa. [Al-A'araaf: 204]



Hata hivyo pamoja na baadhi ya wanachuoni kusema kuwa aayah hiyo makusudio ni popote, ila wanachuoni wengi na wafasiri kama Ibn Kathiyr katika tafsiri yake kasema: "Maana yake ni ukiwa ndani ya Swala ya Jamaa'ah, pindi Imamu anaposoma kwa sauti (swala za Alfajiri, Maghrib na 'Ishaa') kama ilivyopokewa na Imaam Muslim kwenye Sahiyh yake kutoka katika hadithi ya Abu Muwsaa Al-Ash'ariy aliyesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa Sallam) amesema: ((Imaam amewekwa ili afuatwe, kwa hivyo akisema: "Allaahu Akbar nanyi mfuateni kwa kusema kama yeye na akianza kusoma, nyinyi nyamazeni))



Vile vile akasema tena Ibn Kathiyr: Ibraahiym Ibn Muslim Al-Haajriy amepokea kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliyesema: Wao (Swahaba) walikuwa wakizungumza na hali ya kuwa wamo ndani ya swala, kwa hivyo ilipoteremshwa aya hii ... waliamrishwa wawe kimya.



Naye Imam At Twabariy kwenye tafsiri yake anasema kwamba Ibn Mas'uud amesema: Tulikuwa tukipeana salamu miongoni mwetu tukiwa ndani ya swala, kisha ikaja katika Qur-aan: Na isomwapo Qur-aan isikilizeni na nyamazeni.



Kwa hoja hizo inaonyesha aayah hiyo haihusiani na Qur-aan isomwayo maredioni na kwenye matelevisheni makompyuta au na watu nje ya swala, hata hivyo kwa kuyapa heshima maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni bora kunyamaza isomwapo au kuizima kama huwezi kusikiliza. Wa Allaahu A'alam



Nasiha Ya Kufuata Adabu Za Tilawa (Kusoma) Qur-aan;

Kwa hali yeyote ilivyo, ni bora kuipa heshima Qur-aan kwa kutimiza adabu za kusoma Qur-aan kwani ni maneno ya Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa na kuyatukuza ni wajibu. Nazo ni:



1) Kupiga mswaki

2) Kuwa na wudhuu

3) Kujifunika vizuri (mwanamke)

4) Kuelekea qibla

5) Kusoma kwa kutafakari

6) Kusoma kwa Tajwiid na kufuata sheria zake.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Back
Top Bottom