Ramadhan Special Thread
Nimekwenda Nje Ya Ndoa, Nimjulishe Mume Wangu?
Maswali: Zinaa-Liwati
SWALI:



Kwaza kabisa ningependa kumskuru mwenyeezi mungu kwa kuwajaalia kufungua website hii. Kwani ni moja ya misaada kwa waislam waliopotea kuwakumbusha kurudi kwa mola wao. Mimi msichana ambae nimeolewa kwa muda wa miaka kumi ilio pita. Baada ya kuolewa nikaja urope na mume wangu. baada ya kipindi mume wangu aka badilika akawa hanijali yuko bize na shughuli zake za kibiashara. Hata kwa tendo la ndoa akawa hanijali mpaka kunakipindi ikawa ina fikia mwezi mzima hatukutani.Kitendo hicho kiliniumiza na ibilisi akaningia nikajikuta nimeenda nje ya ndoa. Kitendo ambacho nakijutia mpaka hivi sasa baada ya kutubu kwa mola wangu. Je mwenyeezi mungu atanisamehe mtu kamam mimi? Natatizo jengine kubwa zaidi ni Kwamba baada ya kwenda nje ya ndoa nilipata uja uzito nikaogopa zambi ya kutoa mimba ni kama ya kuua, Na mume wangu hajui kitu hicho. Kitu hichi kinaniuma sana na haswa baada ya kurudi kwa mola wa wangu na kutubu nakujaribu kumpa mume wangu mawaidha ili atulie tujenge ndoa yetu japokuwa ilichukua muda lakini mweyeezi mungu muweza alinijaalia na kusikia dua yangu na mume wangu tunasikilizana. Najitahidi kumuomba mwenyezi anipe uamuzi uliomwema kwani maisha yangu yote sijawahi kudanganya na wala kufanya kitu kibaya kama hichi. Mpaka sasa ninachofikiria ni kumuambia mume wangu ukweli lakini naogopa kuharibu ndoa yetu kwani nampenda mume wangu nanina penda kuishi nae. Na sipendi kitendo cha kuswali na kumuomba mwenyezi mungu anisamehe huku bado kuna uongo ndani yake. Kwani kutubu na kuendelea kumuaaswi mweyezi mungu kwa kuficha ukweli si kutubu, Naninamuomba mwenyezi mungu kila wakati azisikilize dua zangu japokuwa nimerejea kwa muumba wangu lakini bado sina raha kwani sijui mwenyezi mungu ananiangalia kwa jicho gani mtu kama mimi na sijui kama mwenyezi mungu anaweza kumsamehe mtu kama huyo. Ndugu zanguni naomba msaada au ushauri bora kutoka kwenu kupata jibu la swali la mitihani migumu iliyo nikabili. Namuomba Allaah aweze kujaalia kupata jibu au ushauri mzuri kutoka kwenu ndugu zangu waislam. Shukran na Mwenyezi mungu atawazidishia.





JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Tunashukuru dada yetu kwa swali lako zito na linalosikitisha.



Wamesema Wanachuoni: “Toba (tawbah) ni wajibu kwa kila dhambi. Ikiwa dhambi alilolifanya mja ni baina mja na Allaah aliyetukuka haliingiliani na haki ya binadamu, litakuwa na sharti tatu:



Ya kwanza: Kuacha maasiya.

Ya pili: Kujuta kwa kufanya hayo maasiya.

Ya tatu: Kuazimia kutorudia tena kosa lile milele. Likikosekana sharti moja katika hizi tatu basi toba haitosihi”.



Na ikiwa dhambi lililofanywa lina mafunagamano na mwanadamu sharti za kupata toba zinakuwa ni nne: “Sharti hizi tatu zilizotajwa hapa juu na ya nne ni kuirudishia haki ya yule mtu, ikiwa ni mali au kitu chengine chochote umrudishie. Ni wajibu kwa Muislamu kutubu (kuomba msamaha) kwa madhambi yote. Ikiwa atatubia baadhi ya dhambi husihi toba yake kwa dhambi ile na zinabaki zile zilizobakia. Zimedhihiri dalili katika Kitabu na Sunnah na Ijmaa’ ya Ummah katika uwajibu wa toba.



Ni hakika isiyopingika kuwa Uislamu umeacha wazi mlango wa toba kwa dhambi lililofanywa ikiwa aliyefanya ataweza kutekeleza masharti ya kusamehewa. Hakuna dhambi ambayo haisamehewi na Allaah Aliyetukuka, kwani Anasema:



“Sema: Enyi waja Wangu waliojidhulumu nafsi zao, msikate tamaa na rahmah ya Allaah. Hakika Allaah Husameheme dhambi zote” [39: 53].



Linalotakiwa ni kama alivyosema Allaah Aliyetukuka:

“Na tubuni nyote kwa Allaah, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa” [24: 31].



Mafanikio yetu hapa duniani na kesho Aakhirah ni kufanya hilo alilosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), kurudi na kutubia Kwake.



Ili toba kukubaliwa tunatakiwa tuwe wakweli na wenye ikhlaasw na niyyah safi katika hilo. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:



“Enyi mlioamini! Tubuni kwa Allaah tawbah iliyo ya kweli” [66: 8]



Muislamu anapotubia kweli kweli basi natija yake ni kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):



“Na wale wasiomwomba mungu mwengine pamoja na Allaah, wala hawaui nafsi Aliyoiharimisha Allaah isipokuwa kwa haki, wala hawazini - na atakayefanya hayo atapata madhara, Atazidishiwa adhabu Siku ya Qiyaamah, na atadumu humo kwa kufedheheka. Isipokuwa atakayetubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Allaah Atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Allaah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. Na aliyetubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kweli kweli kwa Allaah” [25: 68 – 71].



Katika haya yote dada yetu uko sawa kabisa kwani kulingana na maelezo yako ni kwamba umeacha maasiya hayo ya zinaa, umejuta kwa kufanya zinaa na umeazimia kutorudia tena kosa hilo.



Ama huyo mtoto, hatohusishwa na huyo mwanamme aliyezini na we, bali mtoto atahesabika kuwa ni mtoto wa mume wako japo umezaa nje ya ndoa. Na dalili ni kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:

“Mtoto atahusishwa na mume (mwenye kitanda cha ndoa) na mzinifu hastahiki chochote.” [Al-Bukhaariy na Muslim]



Hivyo, mumeo ndiye mwenye kuhusishwa na huyo mtoto na hilo halitofutika hadi mume amkatae huyo mtoto kuwa si wake kishariy’ah kwa njia ya Li’aan (taratibu za kishariy’ah za mtu kumkana mtoto kuwa si wake). Hilo ni kwa sababu misingi ya asli ya kishariy’ah, mtoto anahesabika ni wa yule mwenye kitanda (akikusudiwa mume halali wa mke wa ndoa) kama ilivyotangulia Hadiyth hapo juu.



Wanachuoni wa Baraza La Kudumu La Utoaji Fatwa Na Tafiti Za Kielimu waliulizwa:

“Kuna mwanamke aliyeolewa ambaye amefanya zinaa hali ya kuwa yuko kwenye ndoa (kaolewa). Akapata mimba na akazaa mtoto. Je, mtoto huyo ataishi na nani? Je, ataishi na mume kama inavyoeleza Hadiyth ((Mtoto ni wa (mwenye) kitanda (mume) na mzinifu hapati chochote)) au sivyo? Na ikiwa ataishi na mume wa mama yake, je (huyo mume) atamfanya kama mtoto wa kupanga na kumfanya ni kama mtoto wake pamoja na kupata haki zote anazostahiki, au atakuwa chini tu ya uangalizi wake? Na ikiwa (mtoto) atahusishwa kuwa ni wa mzinifu, je, (huyo mzinifu aliyezaa na mwanamke aliyeko kwenye ndoa) atakuwa na haki za kumfanya huyo mtoto kuwa wake halisi, au ataishi naye tu kama mtoto asiye halali?”



Wakajibu (Kamati ya Kudumu Ya Utoaji Fatwa):

“Ikiwa mwanamke huyo aliyeolewa, kafanya zinaa na akapata mimba kisha akazaa, basi huyo mtoto atakuwa ni wa (mwenye) kitanda (mume), kwa mujibu wa Hadiyth sahihi. Na ikiwa mwenye kitanda ataamua kukataa kuwa mtoto si wake kwa kufanya Li’aan, basi anaweza kufanya hivyo kwa Qaadhwi, na akishafanya hivyo, basi mtoto atakuwa si wa yeyote yule kwa mujibu wa makubaliano ya Wanachuoni wa Kiislamu ‘Ijmaa’’.

Lakini mtu akitaka kumfanya huyo mtoto kuwa ni wa kupanga, hilo halitohalalisha mtoto kuwa wake kihalali.

Na Allaah ni Mwenye Kuleta Tawfiyq.



[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah, mj. 20, uk. 339]



Na Allaah Anajua zaidi
 
Anaishi Na Kuzini Na Mtu Asiyemuoa Lakini Anaswali, Je, Swalah Zake Zinakubaliwa?
Maswali: Zinaa-Liwati
SWALI:



Je mtu aliezini akiswali swala yake inakubaliwa? Mfano mtu anaishi na mtu ambaye hajamuoa lakini anajitahidi kusali swala tano je hukumu inakuwaje?



JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuishi na kuzini na mwanamume. Hakika hili ni swali ambalo halifai kabisa kuulizwa na Muislamu. Hata hivyo, huenda katika kuuliza huku kukaleta faraja na kumtoa mtu katika maasiya ambayo yanampeleka mwanaadamu Motoni.



Ifahamike kuwa zinaa ni kitendo cha madhambi na tena ni miongoni mwa madhambi makubwa katika Dini yetu. Hata hivyo, dhambi hilo halikuvui wewe kutoswali na kutekeleza Ibaadah nyingine. Kutofanya Ibaadah hizo kunamaanisha kuwa unachuma madhambi zaidi. Hata hivyo, kufanya kwako zinaa inamaanisha kuwa Swalah yako haitekelezwi inavyotakiwa. Kwani ikiwa itafanyika katika njia ya sawa sawa itakuepusha na machafu na maovu:



“Soma uliyofunuliwa katika Kitabu, na usimamishe Swalah. Hakika Swalah inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Allaah ndilo jambo kubwa kabisa. Na Allaah Anayajua mnayoyatenda.” (29: 45).



Machafu yanayokusudiwa hapa ni zinaa na uchafu mwengineo. Allaah Aliyetukuka Amewaamuru Waislamu wasithbutu hata kuwa karibu na zinaa kwani ni njia chafu kabisa:



“Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya” (17: 32). Hivyo, ili Swalah iwe ina athari katika maisha yako inatakiwa uwe mbali na mambo ya madhambi na maasiya yakiwemo zinaa. Ni ajabu mtu atakuwa haoni hasikii mpaka azini ilhali anaweza kuolewa kisheria na mwanamume na akapata starehe hizo anazozipata kwa njia ya madhambi na maasiya.



Ikiwa kweli unajitahidi kuswali Swalah tano kwa nini pia hujitahidi katika kuacha zinaa. Kutekeleza Swalah tano huwa unapata thawabu na kuzini unapata madhambi. Kama vile ukiacha kuswali unapata madhambi na ukiacha kuzini unapata thawabu. Ndugu yetu fanya juhudi uwe ni mwenye kuacha zinaa. Hata tukisema ya kwamba utakuwa ni mwenye kupatiwa thawabu kwa Swalah unazoswali, thawabu hizi zitafutwa kabisa na madhambi unayofanya. Ndio Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati mmoja aliwauliza Maswahaba zake:



“Je, mwamjua muflis?” Wakajibu: “Ni yule asiye na dirham wala dinaar”. Akawaambia: “Ama kwa ummah wangu ni yule atakayekuja Siku ya Qiyaamah na amali ya Swalah, Zakaah, Funga na kadhalika lakini amemtusi huyu, akala mali ya huyu, akampiga huyu. Hivyo, thawabu zake zitachukuliwa na kupewa aliowadhulumu. Na pindi thawabu zake zitakapomalizika, atabandikwa madhambi ya aliowadhulumu” (al-Bukhaariy na Muslim).



Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewausia Waislamu kwa kuwaambia:




“Mcheni Allaah popote mlipo, na fuatishaneni baya kwa zuri. Zuri litafuta baya” (at-Tirmidhiy).



Na fahamu kuwa hakuna lisilowezekana, ukifanya juhudi kuacha ovu hilo Allaah Aliyetukuka Atakusaidia.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Ikiwa Mume Na Mke Wamekubaliana Kuingiliana Kinyume Na Maumbile, Je, Kuna Ubaya?
Maswali: Zinaa-Liwati
SWALI:



Assalam alaykum warahmatullahi wabarakatu tunashukuru sana kwa jinsi mnavyojitahidi kutujibia maswali yetu kadiri mnavyo weza na ALLAH subhanahu wataala inshaallah atakulipeni ujira ulio bora zaidi. Suala langu ni, nini hukmu ya mume kumtamkia mkewe unyumba lakini kinyume cha maumbile na nini athari zake na jee kama watakuwa wamekubaliana wote wawili kufanya tendo hilo kuna athari zozote na jee ALLAH subhanahu wataala atakuwa radhi kwa hilo?



Inshaallah tunategemea majibu yaliokuwa hayana mushkel ndani yake kwani ni suala linlowaumiza vichwa sana waislamu. ASANTE.



JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Shukrani zetu kwa swali lako. Hakika swali hilo ni katika maswali ya kushangaza kabisa, na Muislam kufikiria mambo kama hayo ni kuonyesha jinsi gani baadhi ya Waislam walivyo mbali kabisa na mafundisho ya Dini yao.




Inatakiwa tufahamu kuwa makubaliano yoyote yanayokwenda kinyume na maagizo ya Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huwa haifai kabisa kwa Muislamu kuyatekeleza.




Hakuna utiifu wala kukubali jambo linalopingana na sheria au jambo lolote lile la shari. Kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu hilo ni,

"Hakika utiifu ni katika wema". Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy, na Abu Daawuud.

Na pia,

"Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba". Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, An-Nasaaiy na Ahmad.




Ama tendo la ndoa ni lazima litekelezwe kwa mujibu wa tulivyofundishwa na Uislamu. Allaah Aliyetukuka Anatuambia:



"Wakishatwaharika basi waendeeeni katika pale Alipokuamrisheni Allaah. Hakika Allaah Huwapenda wanaotubu na Huwapenda wanaojitakasa. Wake zenu ni konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo" (2: 222-223).




Na kuziendea konde zenu mpendavyo, si sehemu ya nyuma, bali ni sehemu ambayo inapatikana uzazi na ndio ikafananishwa na konde/ shamba kwa sababu shamba hulimwa na kuota mazao ambayo kwayo hupatikana mavuno.

Kwa hivyo, ni ubaya sana kwa mwanamume kumwendea mkewe kwa nyuma na athari yake ni kubwa kwani inampatia shida sana mwanamke wakati wa kuzaa na matatizo mengine. Pia inaleta madhara ya kiafya, inakwenda kinyume na maadili matukufu na hii ni tabia mbaya sana.




Ama katika Dini yetu, hili ni jambo lililokatazwa kwa Aayah tuliyoitaja hapo juu na Hadiyth zifuatazo:

1. "Allaah Hatomtazama mwanamume mwenye kumuingilia mkewe kwa nyuma" (an-Nasaaiy na Ibn Hibbaan kwa Isnadi nzuri).

2. "Amelaaniwa mwenye kumjia mwanamke kwa nyuma" (Ahmad, Abu Daawuud na Ibn 'Adiy).

3. "Mwenye kumuingilia mwenye hedhi au mwanamke kwa nyuma au kumuendea mchawi na kumuamini kwa anayosema basi amekufuru kwa aliyoteremshiwa Muhammad" (Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah, na Isnadi yake ni Sahihi).

4. "Twaawuus amesema: 'Ibn 'Abbaas aliulizwa kuhusu mtu anaye muingilia mkewe kwa nyuma'. Akasema: 'Huyu ananiuliza kuhusu ukafiri'" (an-Nasaa'iy).




Ingia katika viungo vifuatavyo upate dalili zaidi za kuharamishwa tendo hilo ovu kabisa:




Kuharamishwa Liwati





Mume Wangu Ananitaka Njia Isiyo Ya Halali



Je Nitakuwa Nimeachika Ikiwa Mume Ananiingilia Kwa Njia Isiyo Ya Halali?



Mwenye Kufanya Maasi Ya Liwati Anaweza Kurudi Kwa Allah Kutubia?



Mume Anamuingilia Njia Isiyo Ya Halali Kwa Nguvu, Anaogopa Kudai Talaka Asije Kuzini



Mume Mwenye Tabia Chafu Ya Liwati Anafaa Kuwa Imaam? Je, Inafaa Kumuozesha Mke?




Kwa hivyo ikawa mmekubaliana katika hilo mufahamu mnafanya makosa makubwa mbele ya Allaah Aliyetukuka. Kwa hiyo, mnatakiwa mrudi katika njia ya sawa ambayo haina ujongo wa aina yoyote, na kama mlikuwa mnafanya hivyo, basi mtubie haraka sana na msije kurudia kamwe tendo hilo chafu.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kuharamishwa Liwati
08-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kuharamishwa Liwati




Imekatazwa mwanamume kumuingilia mkewe kwa nyuma. Hii inafahamika kutokana na Aayah iliyotajwa hapo juu (kwa vile 'konde zenu' inakusuduwa ni sehemu inayotoa mazao tu). Na kutokana na usimulizi ulioelezewa hapo juu. Vile vile kuna Hadiyth nyingine kuhusu maudhui kama zifuatazo:


Kwanza:



عن أم سلمة قالت: لما قدم المهاجرون المدينة على الأنصار تزوّجوا من نسائهم، وكان المهاجرون يجبون وكانت الأنصار لا تجبي، فأراد رجل من المهاجرين امرأته على ذلك، فأبت عليه حتى تسأل رسول الله صلى الله عليه وسلم، قالت: فأتته فاستحيت أن تسأله، فسألته أم سلمة فنزلت ((نساؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنّى شِئْتُم)) وقال: «لا إلاّ في صَمَّامٍ واحِدٍ»

Imetoka kwa Ummu Salamah رضي الله عنها kwamba: Muhaajiriyn walipokuja Madiynah kwa Ma-Answaar waliwaoa wanawake wao. Wanawake wa Muhaajiriyn walikuwa wakilala kifudifudi (wakati wa kujimai na waume zao) na wanawake Ma-Answaar hawakuwa wakifanya hivyo. Mwanamume mmoja Muhaajir alitaka mkewe afanye hivyo akakataa. Akaenda kwa Mtume lakini aliona hayaa kumuuliza swali hilo, kwa hiyo Ummu Salamah alimuulizia kisha Aayah ikateremshwa inayosema: ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo)). Mtume akasema: ((Hapana! (Sio kila njia upendayo) bali isipokuwa ni pale penye tundu)) (la mbele) [1]




Pili:

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: جاء عُمَر بن الخطاب إلىٰ رسول الله فقال: يا رسول الله، هلكتُ! قال: ((وما الذي أهلكك؟)) قال: حَوَّلْتُ رَحْلِي الليلة، فلم يردَّ عليه شيئاً، فأُوْحِيَ إلىٰ رسول الله هذه الآيةُ: ((نساؤكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنىٰ شئتم)) يقول: ((أَقْبِلْ، وأَدْبِرْ، واتقي: الدُّبر، والحَيضة))

Imetoka kwa Ibn 'Abbaas رضي الله عنهما ambaye amesema: Alikuja 'Umar ibnul-Khatwtwaab kwa Mjumbe wa Allaah akasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, Nimeangamia! Akasema: ((Nini kilichokuangamiza?)) Akasema: Nimepindua kipando changu usiku. Lakini (Mtume) hakumjibu kitu.

Akateremshiwa Aayah hii ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo)) Akasema: ((Kwa (mtindo) wa mbele, nyuma lakini chunga kumuingilia (sehemu ya maumbile ya nyuma) na akiwa katika hedhi))[2]




Tatu:

عن خُزَيْمَةَ بنِ ثابتٍ أَنَّ رجلاً سَأَلَ النبيَّ عن إتيانِ النساءِ في أَدْبَارِهِنَّ أو إتيانِ الرجلِ امْرَأَتَهُ في دُبُرِهَا، فقالَ النبيُّ: «حلالٌ»، فلمَّا وَلَّى الرجلُ دعاهُ أَوْ أَمَرَ بِهِ فدُعِيَ فقالَ: «كيفَ قلتَ، في أيِ الخُرْبَتَيْنِ أَوْ فِي أَيِّ الخُرْزَتَيْنِ أو في أيِّ الخُصْفَتَيْنِ أَمِنْ دُبُرهَا في قُبُلِهَا فَنَعَمْ، أَمَّا مِنْ دُبُرِهَا في دُبُرِهَا فَلاَ، إنَّ اللَّهَ لا يَسْتَحْيِي من الحقِّ، لا تَأْتُوا النساءَ في أَدْبَارِهِنَّ»

Imetoka kwa Khuzaymah ibn Thaabit رضي الله عنه "Mtu mmoja alimuuliza Mtume kuhusu kuwaingilia wanawake kwa nyuma au mwanamume kumuendea mkewe kwa nyuma yake. Akasema Mtume kuwa ni ((Halaal)). Alipoondoka Mtume alimwita au aliamrisha aitwe, akasema: ((Ulisema nini? Njia gani kati ya tundu mbili umemaanisha? Ikiwa ulimaanisha kutoka kwa nyuma na kumuingilia mbele (sehemu yake ya siri ya mbele) basi sawa. Lakini ikiwa umemaanisha nyuma katika sehemu yake ya siri ya nyuma basi hapana! Hakika Allaah Haoni hayaa katika haki. Msiwaingilie wake zenu katika njia zao za nyuma))[3]


Nne:

((لا يَنْظُرُ اللَّهُ إلى رَجُلٍ أَتَى امْرَأَةً في دُبُرِهَا))

((Allaah Hatomtazama mwanamume anayemuingilia mwanamke kwa nyuma))[4]




Tano:

(( مَلْعُون مَنْ ياَتِي النِّسَاءَ فِي مَحَاشِهِنَّ)) ( يعني : أدبارهن)



((Amelaaniwa anayewaendea wanawake katika njia zao za nyuma))[5]


Sita:

((مَنْ أَتى حَائِضاً أَوِ امْرَأَةً فِي دُبُرِها أَوْ كَاهِناً فَصَدَقَهُ بِمَا يَقُولُ فقدْ كَفَرَ بمَا أُنْزِلَ عَلَى مُحَمَّدٍ))

((Atakayemuingilia mwenye hedhi au mwanamke kwa nyuma au atakayemuendea kahini (mtabiri) akamuamini anayomwambia atakuwa amekufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammad))[6]






[1] Ahmad, At-Tirmidhiy na wengineo ikiwa ni Swahiyh

[2] An-Nasaaiy katika “‘Ishratun-Nisaa” ikiwa ni isnaad hasan, At- Tirmidhiy na wengineo

[3] Ash-Shaafi'iy, Al-Bayhaaqiy na wengineo ikiwa ni Swahiyh

[4] An-Nasaaiy ikiwa ni isnaad hasan, na imetiliwa nguvu katika "Al-Ishrah", At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan

[5] Abu Daawuud, Ahmad na wengineo ikiwa ni isnaad hasan na imetiliwa nguvu

[6] Abu Daawuud, At-Tirimidhiy na wengineo: Swahiyh
 
Tunaendelea na darsa la SWALA YA RASULLULLAH



032-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kurukuu, Sifa Na Ulazima Wa Kutulia Katika Rukuu


KURUKUU




Baada ya kumaliza kisomo chake (صلى الله عليه وآله وسلم), alikuwa akinyamaza kinyamazo kidogo([1]

), kisha huinua mikono yake(

[2]

) kwa namna zilizotangulia kuelezwa katika 'Takbiyr Ya Kufungulia, akaleta Takbiyr(

[3]

) na akarukuu.(

[4]

).




Na pia alimuamrisha mambo mawili hayo aliyeswali vibaya kwa kumwambia: ((Hakika Swalah ya mmoja wenu haitotimia mpaka akamilishe wudhuu vizuri kama Allaah Alivyoamrisha… kisha alete Takbiyr, amsifu na kumtukuza Yeye, na asome kiasi kinachosahilika tu kwake katika Qur-aan miongoni mwa Aliyofunzwa na Allaah (kwa kiasi cha wepesi) na uwezo wake, kisha alete Takbiyr na arukuu [na aweke mikono yake miwili juu ya magoti yake mawili] mpaka viungo vyake vitulie na vipumzike…))(

[5]

).










SIFA YA RUKUU




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akiweka viganja vyake juu ya magoti yake(

[6]

) na alikuwa akiwaamrisha kufanya hivyo(

[7]

) kama alivyomuamrisha mtu aliyeswali vibaya, kama ilivyoelezwa nyuma.




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiimakinisha mikono yake barabara na magoti yake (kama kwamba akiyashikilia](

[8]

), na alikuwa akivichanua vidole vyake(

[9]

), na alimuamrisha aliyeswali vibaya kama hivyo, kwa kumwambia: ((Utakaporukuu, weka viganja vya mikono yako juu ya magoti yako, na kisha vichanue vidole vyako, kisha bakia (hivyo) hadi kila kiungo kitue mahali pake))(

[10]

).




Alikuwa akijitawanya (sio kujigandamiza mkao mmoja) na akitenganisha viwiko vya mikono na ubavu wake.(

[11]

)




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anaporukuu, hutandaza mgongo wake na kuusawazisha(

[12]

) kiasi kwamba kama ungelimwagiwa maji, basi yangelitua (

[13]

). Na pia alimwambia aliyeswali vibaya: ((Utakaporukuu, weka viwiko vyako juu ya magoti yako, na tawanya mgongo wako na makinisha madhubuti rukuu yako)).(

[14]

)




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) hainamishi kichwa chake wala hakinyanyui (zaidi ya mgongo wake),(

[15]

) bali kilikuwa baina yake.(

[16]

)







ULAZIMA WA KUTULIA KATIKA RUKUU




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akitulia kwenye rukuu yake, na alimuamrisha awe hivyo aliyeswali vibaya, kama ilivyotajwa katika mlango wa rukuu.




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Kamilisheni rukuu na sujudu, kwani naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, hakika mimi nakuoneni nyuma yangu(

[17]

) mnaporukuu na mnaposujudu)).(

[18]

)




Alimuona mtu anaswali bila ya kukamilisha rukuu yake sawa sawa, akidonoa katika sujuud yake, akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Lau atakufa mtu huyu katika hali yake hii, basi atakuwa amekufa katika Mila isiyokuwa ya Muhammad, [anadonoa katika Swalah yake kama adonoavyo kunguru damu]. Mfano wa yule asiyekamilisha rukuu yake na akadonoa katika sujudu yake, ni kama mfano wa mwenye njaa anayekula tende moja au tende mbili, ambazo hazitomfaidisha kitu chochote))(

[19]

)




Abu Hurayrah (رضي الله عنه) alisema: "Rafiki yangu mpenzi (صلى الله عليه وآله وسلم) amenikataza kudonoa katika Swalah yangu mdonowo wa jogoo na kugeuka geuka kama ageukavyo mbweha, na kuchuchumaa kama achuchumaavyo tumbili"(

[20]

).




Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisema: ((Mwizi muovu kabisa miongoni mwa wevi ni yule anayeiba katika Swalah yake)). Wakasema: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Vipi anaiba katika Swalah yake"? Akasema: ((Hatimizi rukuu yake na sujuud yake))(

[21]

)




Mara moja, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiswali, na alitupa jicho kwa mtu ambaye hakusawazisha uti wa mgongo wake katika rukuu na sujuud. Alipomaliza alisema: ((Enyi Waislamu! Hakika hakuna Swalah kwa yule asiyesawazisha uti wake wa mgongo katika rukuu na sujuud)).(

[22]

)




Akasema katika Hadiyth nyingine: ((Swalah ya mtu haihesabiwi hadi asawazishe mgongo wake katika rukuu na sujuud)).(

[23]

)







[1]

Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.


[2]

Al-Bukhaariy na Muslim. Huku kuinua mikono ni jambo lililothibiti kutoka kwake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa njia ya mutawaatir (Iliyopokelewa na idadi kubwa -ya watu- yenye kuwa muhali katika kawaida kukubaliana kusema uongo) kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Na vile vile imethibiti kutoka kwake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa njia hiyo hiyo ya mutawaatir, kuinua mikono wakati wa kunyanyuka -wakati wa kuitadili - kutoka kwenye rukuu mpaka alingane sawa hali ya kusimama. Na hivi ndivyo walivyokwenda Maimaamu watatu; Maalik, Ash-Shaafi'iy na Ahmad, na wengineo katika kundi kubwa la Maulamaa wa Hadiyth na Maulamaa wa Fiqh. Na ndio mwenendo alioshikamana nao Imaam Maalik (رحمه الله) hadi kufa kwake kama ilivyoripotiwa na Ibn 'Asaakir (15/78/2). Baadhi ya Mahanafi wamechagua kufanya hivyo. Miongoni mwao ni 'Iyswaam bin Yuusuf Abu 'Aswmah Al-Balkhiy (aliyefariki 210) ambaye ni mwanafunzi wa Imaam Abu Yuusuf (رحمه الله), kama ilivyoelezewa katika utangulizi. 'Abdullaah bin Ahmad ameripoti kutoka kwa baba yake katika Masaail yake (Uk. 60).

"Imesimuliwa kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir kwamba amesema kuhusiana na kunyanyua mikono miwili katika Swalah: "Anapata mema kumi kwa kila anapoinyanyua". Nikasema: Yana ushahidi - maneno ya ‘Uqbah - wenye nguvu kutokana na Hadiythul-Qudisy isemayo: ((…mwenye kutia nia ya kitendo chema na akakitekeleza, Allaah Atamuandikia mema kumi hadi mia saba)). Imesimuliwa na Ash-Shaykhaayn. Taz. Swahiyh At-Targhiyb Namba 16.


[3]

Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.


[4]

Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.


[5]

Abu Daawuud na An-Nasaaiy. Al-Haakim amesema ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.

[6]

Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.


[7]

Al-Bukhaariy na Muslim.


[8]

Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.


[9]

Al-Haakim ambaye amesema ni Swahiyh. Adh-Dhahabiy na Atw-Twayaalisy wamekubaliana naye. Imetolewa katika Swahiyh Abu Daawuud (809).


[10]

Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan katika Swahiyh zao.


[11]

At-Tirmidhiy ambaye amesema ni Swahiyh, na Ibn Khuzaymah.


[12]

Al-Bukhaariy na Al-Bayhaqiy kwa isnaad Swahiyh.


[13]

Atw -Twabaraaniy katika Mu'jam Al-Kabiyr na Mu'jam As-Swaghiyr, 'Abdullaah bin Ahmad katika Zawaaid Al-Musnad na Ibn Maajah.


[14]

Ahmad na Abu Daawuud kwa isnaad Swahiyh.


[15]

Abu Daawuud na Al-Bukhaariy katika Juzuu Al-Qaari'ah kwa isnaad Swahiyh. Na maana ya hakinyanyui, ni kuwa hakinyanyui kichwa chake mpaka kikawa juu zaidi ya mgongo wake, bali kinakuwa usawa wa mgongo.


[16]

Muslim na Abu 'Awaanah.


[17]

Nasema na kuona huku ni kuona kwa uhakika wake kimaumbile, na ni miongoni mwa miujiza yake (صلى الله عليه وآله وسلم), nako ni katika Swalah basi. Na hakuna dalili ya kuona kwa ujumla.


[18]

Al-Bukhaariy na Muslim.


[19]

Abu Ya'alaa katika Musnad yake (340/3491/1), Al-Aajuriy katika Al-Arba'iyn, Al-Bayhaqiy, Atw-Twabaraaniy (1/192/1), Adhw-Dhwiyaa katika Al-Muntaqaa (276/1), Ibn 'Asaakir (2/226/2, 414/1, 8/14/1, 76/2) kwa isnaad nzuri. Na Ibn Khuzaymah amesema ni Swahiyh (1/82/1). Ibn Batwtwah katika Al-Ibaanah (5/43/1) anao usimulizi Mursal -Hadiyth mwisho wa isnad yake ameangushwa Swahaba- unaounga mkono sehemu ya mwanzo ya Hadiyth ukitoa ziada katika Al-Ibaanah (5/43/1).


[20]

Atw-Twayaalisy, Ahmad na Ibn Abi Shaybah. Ni Hadiyth Hasan, kama nilivyoielezea katika tanbihi zangu kwenye Al-Ahkaam (1348) ya 'Abdul-Haqq Ishbiyliy (1348).


[21]

Ibn Abi Shaybah (1/89/2), Atw-Twabaraaniy na Al-Haakim ambaye amesema ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.


[22]

Ibn Abi Shaybah (1/89/1), Ibn Maajah na Ahmad kwa isnaad Swahiyh.


[23]

Abu 'Awaanah, Abu Daawuud na As-Sahmiy (61). Ad-Daaraqutwniy amesema ni Swahiyh.
 
033-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Adhkaar Za Rukuu


ADHKHAAR ZA RUKUU



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) katika nguzo hii akisoma namna mbali mbali za adhkaar na du'aa. Alikuwa akibadilisha katika kusoma kwake; mara nyingine husema hii na mara nyingine husema hii miongoni mwa zifuatazo:



1.

Sub-haana Rabbiyal ‘Adhiym



“Ametakasika Mola wangu Aliye Mtukufu, mara tatu”([1]). Na mara nyingine alikuwa akiikariri zaidi ya hivyo.([2])



Mara moja, katika Swalah ya usiku, aliikariri sana hadi rukuu yake ikawa inakaribiana na kisimamo chake, alichokuwa amesoma ndani yake Surah tatu katika Surah ndefu; Al-Baqarah, An-Nisaa na Al-'Imraan. Ndani yake (Swalah hii) kulijaa du'aa na kuomba Maghfirah, kama ilivvyotajwa katika '(Kisomo Katika) Swalah Ya Usiku (Tahajjud).





2.

Sub-haana Rabbiyal ‘Adhiym wabihamdihi



“Ametakasika Mola wangu Aliye Mtukufu Na Sifa Njema Zote Ni Zake, mara tatu”.([3])





3.

Subuuhun Qudduusun Rabbul Malaaikati war Ruuhi



“Mwingi wa kutakaswa Mtakatifu([4]), Mola wa Malaika na Jibriyl”.([5])





4.

Sub-haanaka Allaahumma wa Biham-dika Allaahumma gh-fir-liy



“Kutakasika ni Kwako, Ee Mola wangu, na sifa njema zote ni Zako, Ee Mola Nisamehe". Alikuwa akiileta kwa wingi hii katika rukuu yake na sujuud zake, alikuwa akitekeleza amri ya Qur-aan.”([6])





5.

Allaahumma laka Raka’tu, wabika Aamantu, walaka As-lamtu, [Anta Rabbiy] Khasha’a laka sam’iy, wabaswariy, wamukh-khiy, wa’adhwmiy, [wa ‘idhwaamiy] wa’aswabiy, [wamas-taqallat bihii Qadamiy Lillaahi Rabbil ‘Alamiyn]



“Ee Allaah! Kwako Wewe nimerukuu, na Wewe nimekuamini, na Kwako Wewe nimejisalimisha, (Wewe Mola wangu) umenyenyekea Kwako usikizi wangu, na uoni wangu, na ubongo wangu, na mfupa wangu, (katika riwaaya mifupa yangu) na hisia zangu, (na ambacho kimesimama juu ya miguu yangu([7]) kwa ajili ya Mola Wa viumbe vyote.”([8])





6.

Allaahumma laka Raka’tu, wabika Aamantu, walaka As-lamtu, wa’alayka tawakkaltu, Anta Rabbiy, Khasha’a laka sam’iy, wabaswariy, wadamiy, walahmiy, wa‘adhamiy, wa’aswabiy, Lillahi Rabbil ‘Alamiyn



“Ee Allaah! Kwako nimerukuu, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimejisalimisha, Kwako nimekutegemea, Wewe Mola wangu, umenyenyekea Kwako usikizi wangu, na uoni wangu, na damu yangu, na nyama yangu, na mfupa wangu, na ubongo wangu kwa ajili ya Mola Wa viumbe vyote”.([9])





7.

Subhaana dhil Jabaruuti wal Malakuuti wal Kibriyaau wal ‘Adhamati



“Ametakasika Mwenye Utawala, na Ufalme, na Ukubwa, na Utukufu”, Hii alikuwa akiisoma katika Swalah ya usiku.([10])




[1] Ahmad, Abu Daawuud, Ibn Maajah, Ad-Daaraqutwniy, Atw-Twahaawiy, Al-Bazzaar na Atw-Twabaraany katika Mu'jam Al-Kabiyr, kutokana na Maswahaba saba. Ndani yake kuna jibu kwa wale waliokataa ujio wa kutozidi mara tatu katika kuleta Tasbiiyhaat, kama Ibn Al-Qayyim na wengineo.

[2] Inapatikana hii kutokana na Ahaadityh zilizoweka wazi kwamba Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifanya kisimamo chake, na rukuu yake na sujuud zake sawa sawa kwa urefu, kama itakavyotajwa katika mlango ufuatao.

[3] Hadiyth Swahiyh. Imesimuliwa na Abu Daawuud, Ad-Daaraqutwniy, Ahmad, Atw-Twabaraaniy na Al-Bayhaqiy.

[4] Abu Is-haaq amesema: "Subuuh" ina maana ya Aliyetakasika na makosa yoyote, na "Qudduus" ina maana ya Mwenye Baraka au Aliyetwaharika". Ibn Saydah: "Subbuuh Qudduus" ni sifa za Allaah عزوجل kwa sababu Anatukuzwa na Kutakaswa". (Lisaanul-'Arab).

[5] Muslim na Abu 'Awaanah.

[6] Al-Bukhaariy na Muslim. Na maana ya “yata-awwalul Qur-aan” ni kuwa anatekeleza yale aliyoamrishwa ndani yake katika maneno Yake Allaah:

((فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا)).

((Zitakase sifa za Mola wako, na umwombe msamaha, hakika Yeye Ndiye Anayepokea tawbah)) [An-Naswr 110: 3]

[7] Ina maana niliyoyabeba, kutokana na neno "al-istiqlaal" lenye maana "al-irtifaa’". Ni ujumla (ta’miym) baada ya ukhusuusi (takh-swiys), kwa maana imekuja –niliyoyabeba- baada ya khusuus -kutaja kiungo kimoja kimoja- katika viungo vya mtu).

[8] Muslim, Abu 'Awaanah, Atw-Twahaawiy na Ad-Daaraqutwniy.

[9] An-Nasaaiy kwa isnaad Swahiyh.



[10]Abu Daawuud, An-Nasaaiy kwa isnaad Swahiyh.



FAIDA

Je, inakubalika kuchanganya baina ya hizi adhkaar (mbili au zaidi) katika rukuu moja au haikubaliki? Maulamaa wametofautiana katika hili. Ibn al Qayyim hakuwa na msimamo kuhusu hili katika Zaad Al-Ma'aad, na An-Nawawiy amechagua uwezekano wa mwanzo katika Al-Adhkaar, akisema: "Na lililo bora ni kuchanganya baina ya hizi adhkaar zote ikiwezekana. Na hivi ndio inavyotakikana iwe katika adhkaar za milango yote. Abu Atw-Twayyib Swiddiyq Hasan Khan katika Nuzuul Al-Abraar (84) hakukubaliana naye kwa kusema: "Alete adhkaar hizi mara hii, na alete adhkaar nyingine mara nyingine, wala sioni dalili ya kuchanganya. Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuwa akizichanganya kwa mpigo mmoja, lakini alikuwa mara akisema hii, na mara nyingine akisema nyingineyo. Na kufuata ni bora kuliko kuzusha". (Rai ya mwisho hii ni rai iliyo sahihi,) na hivi ndio haki Insha Allaah. Lakini imethibitika katika Sunnah kuirefusha nguzo hii na nyingine pia (kurukuu huku), kama itakavyokuja ufafanuzi wake, hadi iwe inakaribia urefu wa kisimamo. Hivyo, mwenye kuswali akipenda kumfuata Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Sunnah hii, basi hatoweza kufanya hivyo, isipokuwa kwa njia ya kuzichanganya tu (adhkaar) ambayo amekwenda/ameifuata An-Nawawiy, na Ibn Naswr ameipokea katika Qiyaamul-Layl (76) kutoka Ibn Jurayj kutokana na 'Atwaa, -haitowezekana- isipokuwa kwa njia ya kukariri iliyotaja katika baadhi ya hizi adhkaar. (moja ambayo inayo maandiko ya kukariri,) na hivi ndivyo karibu na Sunnah Na Allaah Anajua zaidi.
 
034-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kuirefusha Rukuu Na Kukatazwa Kusoma Qur-aan Katika Rukuu



KUIREFUSHA RUKUU




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akifanya rukuu yake, kisimamo chake baada ya rukuu, na sujuud yake na kikao baina sajda mbili, karibu sawa kwa urefu.([1])










KUKATAZWA KUSOMA QUR-AAN KATIKA RUKUU




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akikataza kusoma Qur-aan katika rukuu na sujuud.([2])




Alikuwa akisema: ((Hakika mimi nimekatazwa kusoma Qur-aan hali ya kuwa nimerukuu au nimesujudu. Hivyo basi katika rukuu mtukuzeni Mola (عزوجل), na (ama) katika sujuud, jitahidini kwa du'aa, kwani ni karibu kukubaliwa humo)).([3])










[1] Al-Bukhaariy na Muslim. Imetolewa katika Irwaa Al-Ghaliyl (331).

[2] Muslim na Abu 'Awaanah. Makatazo ni ya ujumla, hivyo inahusisha Swalah za Faradhi na Sunnah. Ziada ya Ibn 'Asaakir (17/299/1): "Ama Swalah za Sunnah, hakuna ubaya", ni (aidha) shaadhah au munkar. Ibn 'Asaakir ameashiria dosari humo, hivyo haijuzu kufanyiwa kazi.

[3] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.
 
Naam hakika elimu kubwa inapatikana katika darsa la swala ya Nabii swallallahu alaih wasallam

Inafahamika kuwa katika sujudi ndio sehemu ambayo mja huwa karibu sana na Allah,ndio maana inashauriwa kuleta dua sana baada ya kumaliza zile adhkar "subhaana rabbiyal aalaa

Ila kuna mkanganyiko wa lugha ya kutumia,wengine wanasema dua kwa lugha yoyote sawa,wengine wanasema haifai

Wengine wanasema kwenye swalaa za sunna ndio inafaa,basi ili mradi ni kipengele

Ili kuondoa sintofahamu basi ni bora usome dua zile mahsusi zinazo julikana au uombe kimoyomoyo

Inasemwa katika Uislamu "acha lenye kutia shaka na fanya lisilo na shaka"


Binafsi ukiacha zile dua zinazo julikana,huomba dua kwa kimoyomoyo kwa lugha ya kiswahilli

Darsa itaendelea......
 
CHEMSHA BONGO NAMBA 3

Qur'an ina juzuu ngapi?

Jumla ya ayah zilizopo katika qur'an ni ngapi?

Ipi ni sura fupi kuliko zote?

Nini maana ya qur'an?

Ni ayah zipi za mwanzo zilizo shushwa?

Zipo sura ngapi katika qur'an?

Kuna maneno mangapi ya sajdah katika qur'an?

Ni sura ipi ndefu kuliko zote?

Ni sura ipi isiyoanza na Bismillah?

Nilifanya test hii nikapata maksi 70, je wewe,jipime kwa nafsi yako yakija majibu utajua


Baadae inshaallah
 
Long image 04-22-2025 20.46.jpg
 
‘Amali Za Kuwatendea Wazazi Waliofariki Waendelee Kupokea Thawabu



Alhidaaya.com





‘Amali za mwana Aadam zinakatika baada ya kufariki kwake isipokuwa matatu kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



((إذا مات إبن آدم إنقطع عمله إلا من ثلاث: صدقة جارية أو علم ينتفع به أو ولدٌ صالح يدعوا له)) مسلم

((Anapokufa mja, hukatika amali zake zote isipokuwa mambo matatu, swadaqah inayoendelea, au elimu yenye kunufaikiwa, au mtoto mwema anayemuombea)) [Muslim]



Lakini Muislamu anaweza kuendelea kuwatendea wema wazazi wake wawili kwa ‘amali nyenginezo ambazo zimethibiti kuwa thawabu zake zinawafikia kama ifuatavyo:





1-Kuwaombea du’aa na kuwaombea maghfirah:



عن أبي أسيد مالك بن ربيعة رضي الله عنه قال: بينا نحن جلوس عند رسول الله صلى الله عليه وسلم إذا جاءه رجل من بني سلمة فقال يا رسول الله هل بقي من بر أبوي شيء أبرهما به بعد موتهما ؟ قال: ((نعم! الصلاة عليهما والاستغفار لهما وإنفاذ عهدهما من بعدهما وصلة الرحم التي لا توصل إلا بهما وإكرام صديقهما)) رواه ابن حبان في صحيحه أبو داود وابن ماجه

Kutoka kwa Abuu Asyad Maalik bin Rabiy’ah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Tulipokuwa tumekaa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja mtu kutoka [kabila la] Bani Salamah akasema: Ee Rasuli Allaah, je, kuna kilichobakia katika wema ninaoweza kuwafanyia wazazi wangu baada ya kifo chao? Akasema: ((Naam! Kuwaombea du’aa, kuwaombea maghfirah, kuwalipa deni zao, na kuunga ukoo ambao hauungiki ila kutokana nao, na kuwakirimu rafiki zao)) [Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake, Abu Daawuwd na Ibn Maajah]





Kuwaombea Maghfirah Ni Kupandishwa Kwao Daraja Ya Jannah (Peponi):



عن أبي هريرة رضي الله عنه ، قال : قال رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْه ِ وَ سَلَّمَ: ((إِنَّ الرَّجُلَ لَتُرْفَعُ دَرَجَتُهُ فِي الْجَنَّةِ فَيَقُولُ : أَنَّى هَذَا ؟ فَيُقَالُ :باسْتِغْفَارِ وَلَدِكَ لَكَ)) لإمام أحمد و في سنن ابن ماجة أيضاً بإسنادٍ صحيح

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mtu hupandishwa daraja yake Jannah (Peponi). Kisha huuliza: Kwa ajili ya nini? [huku kupandishwa kwangu daraja?] Huambiwa: Kwa ajili ya kuombewa maghfirah na mtoto wako)) [Ahmad, na katika Sunan Ibn Maajah ikiwa na isnaad Swahiyh]



Miongoni mwa du’aa za kuwaombea ni zilizotajwa katika kauli za Allaah ('Azza wa Jalla)



رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا ﴿٢٤﴾

Rabb wangu! Warehemu kama walivyonilea udogoni. [Al-Israa: 24]





رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾

Rabb wetu! Nighufurie na wazazi wangu wawili na Waumini Siku itakayosimama hesabu. [Ibraahiym: 41]



Katika Sunnah wanaposaliwa Swalaah ya Janaazah:



Maiti mwanamume:



اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُ وَارْحَمْـه، وَعافِهِ وَاعْفُ عَنْـه، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـه، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَه، وَاغْسِلْـهُ بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِ مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُ داراً خَـيْراً مِنْ دارِه، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـه، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِه، وَأَدْخِـلْهُ الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُ مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار

Eee Allaah, Mghufurie na Mrehemu, na Muafu na Msamehe na Mtukuze kushuka kwake (kaburini) na Mpanulie kuingia kwake, na Muoshe na maji na kwa theluji na barafu na Mtakase na makosa kama inavyotakaswa nguo nyeupe kutokana na uchafu, na Mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake, na mke bora kuliko mke wake, na Muingize Jannah (Peponi) na Mkinge na adhabu ya kaburi na adhabu ya moto.



Maiti mwanamke:



اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُا وَارْحَمْـها، وَعافِهاِ وَاعْفُ عَنْـها، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـها، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَها، وَاغْسِلْـهُا بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِا مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُا داراً خَـيْراً مِنْ دارِها، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـها، وَزَوْجَـاً خَـيْراً مِنْ زَوْجِها، وَأَدْخِـلْهُا الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُا مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار



Kuwaombea Wazazi Wawili:



اللهُـمِّ اغْفِـرْ لَهُما وَارْحَمْـهما، وَعافِهِما وَاعْفُ عَنْـهما، وَأَكْـرِمْ نُزُلَـهما، وَوَسِّـعْ مُدْخَـلَهما، وَاغْسِلْـهُما بِالْمـاءِ وَالثَّـلْجِ وَالْبَـرَدْ، وَنَقِّـهِما مِنَ الْخطـايا كَما يُنَقَّ الـثَّوْبُ الأَبْيَـضُ مِنَ الدَّنَـسْ، وَأَبْـدِلْهُما داراً خَـيْراً مِنْ دارِهما، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـهما، وأَزَوْاجَـاً خَـيْراً مِنْ اَزْوَاجِهِما وَأَدْخِـلْهُما الْجَـنَّة، وَأَعِـذْهُما مِنْ عَذابِ القَـبْر وَعَذابِ النّـار







2. Kuwalipia Deni La Swawm:



Kuwalipia deni la Swawm ikiwa ni la fardhi (Ramadhwaan) au Swawm ya nadhiri au ya kafara. Ama ikiwa amefariki kabla ya kumalizika Ramadhwaan na amewahi kufunga siku za nyuma, hakuna haja kumlipia:



عن ابن عباس رضي الله عنهما ، قال :جاء رجل إلى النبي صلى الله عليه و سلم فقال : يا رسول الله إن أمي ماتت، و عليها صوم شهر أفأقضيه عنها ؟ قال : (( لو كان على أمك دين أكنت قاضيه عنها ؟)) قال : نعم. قال: (( فدين الله أحق أن يُقضى)) البخاري و مسلم

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Ee Rasuli wa Allaah, Mama yangu amefariki naye ameacha deni la mwezi la Swawm, je nimlipie? Akasema: ((Je angelikuwa mama yako ana deni [la fedha] ungelimlipia?)) Akajibu: Ndio. Akasema ((Basi deni la Allaah lina haki zaidi ya kulipwa)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Na pia:



عن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قال رسول الله صلى الله عليه و سلّم: ((من مات و عليه صيامٌ صام عنه وليُّه)) البخاري و مسلم

Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Aliyefariki akiwa na [deni la] Swawm, walii wake amfungie)) [Al-Bukhaariy na Muslim]





3-Kuwafanyia Hajj Ikiwa Hawakufanya Au Kuwafanyia ‘Umrah:



عن ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما أَنَّ امْرَأَةً جَاءَتْ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ، فَقَالَتْ : إِنَّ أُمِّي نَذَرَتْ أَنْ تَحُجَّ ، فَمَاتَتْ قَبْلَ أَنْ تَحُجَّ ، أَفَأَحُجُّ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ ، حُجِّي عَنْهَا أَرَأَيْتِ لَوْ كَانَ عَلَى أُمِّكِ دَيْنٌ أَكُنْتِ قَاضِيَتَهُ ؟ )) قَالَتْ : نَعَمْ . فَقَالَ : ((اقْضُوا اللَّهَ الَّذِي لَهُ ، فَإِنَّ اللَّهَ أَحَقُّ بِالْوَفَاءِ )) رواه البخاري

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Alikuja mwanamke kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Nina mama ambaye aliweka nadhiri kuwa atahiji, akafariki kabla ya kuhiji, je nimhijie? Akasema: ((Ndio, mhijie je ingelikuwa mama yako ana deni ungelimlipia?)) Akasema: Ndio. Akasema: ((Mkidhieni Allaah (deni) Lake, kwani Allaah Ana Haki zaidi kutimiziwa)) [Al-Bukhaariy]



Pia:



عن عَبْد اللَّهِ بْن بُرَيْدَةَ عَنْ أَبِيهِ رَضِي اللَّه عَنْهما ، قَالَ : بَيْنَما أَنَا جَالِسٌ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ ، إِذْ أَتَتْهُ امْرَأَةٌ ، فَقَالَتْ: إِنِّي تَصَدَّقْتُ عَلَى أُمِّي بِجَارِيَةٍ ، وَ إِنَّهَا مَاتَتْ . فَقَالَ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : (( وَجَبَ أَجْرُكِ وَ رَدَّهَا عَلَيْكِ الْمِيرَاثُ)) قَالَتْ : يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّهُ كَانَ عَلَيْهَا صَوْمُ شَهْرٍ أفأصُومُ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((صُومِي عَنْهَا)) قَالَتْ : إِنَّهَا لَمْ تَحُجَّ قَطُّ ، أَفَأَحُجُّ عَنْهَا؟ قَالَ: ((حُجِّي عَنْهَا)) مسلم

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah kutoka kwa baba yake (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Nilipokuwa nimekaa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja mwanamke akasema: Nimemtolea mama yangu swadaqah ya kijakazi. Naye amefariki. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Umewajibika kupata ujira na mirathi itakurudia)). Akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, alikuwa ana deni la mwezi la Swawm, je nimfungie?” Akasema: ((Mfungie)). Akasema: “Yeye hakuwahi kuhiji, je nimhijie?” Akasema: ((Mhijie)) [Muslim]





4-Kuwatolea Swadaqah:



عن أمّ المؤمنين عَائِشَةَ رَضِي اللَّه عَنْهَا ، أَنَّ رَجُلاً قَالَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ أُمِّي افْتُلِتَتْ نَفْسُهَا ( أي ماتت فجأةً ) وَ أَظُنُّهَا لَوْ تَكَلَّمَتْ تَصَدَّقَتْ ، فَهَلْ لَهَا أَجْرٌ إِنْ تَصَدَّقْتُ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ)) البخاري

Kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Mtu mmoja alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Mama yangu imesokoteka nafsi yake [kwa maana amefariki ghafla] na nadhani kama alizungumza kutaka kutoa swadaqah. Je, atapata ujira nikimtolea swadaqah?” Akasema: ((Ndio)) [Al-Bukhaariy]



Pia



عن ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِي اللَّه عَنْهمَا ، أَنَّ سَعدَ بْنَ عُبَادَةَ رَضِي اللَّه عَنْهما تُوُفِّيَتْ أُمُّهُ وَ هُوَ غَائِبٌ عَنْهَا فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ أُمِّي تُوُفِّيَتْ وَ أَنَا غَائِبٌ عَنْهَا أَيَنْفَعُهَا شَيْءٌ إِنْ تَصَدَّقْتُ بِهِ عَنْهَا ؟ قَالَ: ((نَعَمْ )) قَالَ: فَإِنِّي أُشْهِدُكَ أَنَّ حَائِطِيَ الْمِخْرَافَ ( اسم لبستان كان له) صَدَقَة ٌ عَلَيْهَا .- البخاري

Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ambaye amesema: Sa’ad bin ‘Ubaadah (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) alifiwa na mama yake naye alikuwa hayupo akasema: “Ee Rasuli wa Allaah, Mama yangu amefariki nami sikuweko. Je, itamfaa lolote nikimtolea swadaqah?” Akasema: ((Ndio)) Akasema: “Basi nashuhudia kwako kwamba ukuta wangu wa al-Mikhraaf [jina la bustani yake] ni swadaqah kwa ajili yake.” [Al-Bukhaariy]



Pia,



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَجُلاً قَالَ لِلنَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَ سَلَّمَ : إِنَّ أَبِي مَاتَ ، وَ تَرَكَ مَالاً وَ لَمْ يُوصِ ، فَهَلْ يُكَفِّرُ عَنْهُ أَنْ أَتَصَدَّقَ عَنْهُ ؟ قَالَ : (( نَعَمْ)) روى مسلم و ابن ماجة و النسائي

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtu mmoja alimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Baba yangu amefariki na ameacha mali wala hakuiusia. Je, itakuwa kafara yake (atapata ujira na malipo) nikimtolea swadaqah kwayo?” Akasema: ((Ndio)) [Muslim, Ibn Maajah na an-Nasaaiy





5-Kuunga Ukoo Ambao Hauungiki Ila Kutokana Na Wao:



Dalili ni Hadiyth iliyotangulia katika nukta ya kwanza ambayo imetaja:

((na kuunga ukoo ambao hauungiki ila kutokana nao))



Ni kuwasiliana na ndugu, jamaa wenye uhusiano wa damu, wa karibu na wa mbali, mfano ‘ammu (kaka wa baba) ‘ammat (shangazi), khaal (kaka wa mama), khaalat (mama mdogo au mkubwa), watoto wao wote, bibi wa baba, bibi wa mama na wanaouhusiana wote kwa damu kwa kila upande.



Tutamube kwamba kuunga undugu wa uhusiano wa damu ni kitendo ambacho kimesisitizwa sana. Dalili zake zinapatikana katika Qur-aan na Sunnah kwamba mwenye kukataa kuunga undugu amelaaniwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), rizki yake itadhikika, umri wake utapunguka, Allaah ('Azza wa Jalla) Atamkatilia mbali na hatoingia Jannah (Peponi).







6-Kuwakirimu Rafiki Zao



عن عبد الله بن دينار عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما أن رجلا من الأعراب لقيه بطريق مكة فسلم عليه عبد الله بن عمر وحمله على حمار كان يركبه وأعطاه عمامة كانت على رأسه . قال ابن دينار : فقلنا أصلحك الله إنهم الأعراب وهم يرضون باليسير , فقال عبد الله بن عمر إن أبا هذا كان ودا لعمر بن الخطاب وإني سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: (( وإن أبر البر صلة الولد أهل ود أبيه )) مسلم

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Diynaar na kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba bedui mmoja alikutana naye njiani akielekea Makkah, akamsalimia ‘Abdullaah bin ‘Umar kisha akampakia juu ya punda aliyekuwa amempanda akavua kilemba chake na kumpa. Akasema Ibn Diynaar: Tukasema: “Allaah Akuwekee vizuri. Hao ni mabedui nao wanaridhika na kichache.” ‘Abdullaah bin ‘Umar akasema: “Baba yake huyu alikuwa mpenzi wa ‘Umar ibnul Khattwwaab [Baba yangu] nami nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Kitendo chema kabisa ni mtoto kumpenda (kuungana na) rafiki wa baba)) [Muslim]



Na pia:



عن أبي بردة قال: قدمت المدينة فأتاني عبد الله بن عمر فقال أتدري لم أتيتك ؟ قال قلت لا . قال سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((من أحب أن يصل أباه في قبره فليصل إخوان أبيه)) وأنه كان بين أبي عمر وبين أبيك إخاء وود فأحببت أن أصل ذاك - ابن حبان في صحيحه

Pia kutoka kwa Abuu Bardah ambaye amesema: Nilikuwa naelekea Madiynah akanijia ‘Abdullaah bin ‘Umar akasema: “Je, unajua kwa nini nimekujia?” Akasema: Nikasema: “Hapana!” Akasema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Anayependa kuungana na baba yake katika kaburi lake basi awasiliane na ndugu zake (rafiki zake) baba yake)) Na baina ya baba yangu ‘Umar na baba yako walikuwa na undugu wa mapenzi, basi nimependa kuwaunga.” [Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake]
 
Amana Katika Uislamu



www.alhidaaya.com





Baada ya kumhimidi na kumshukuru Allaah Aliyetukuka Ambaye Ametuneemesha na fursa hii ya kukutana ili kunasihiana na kukumbushana. Swalah na salamu zimfikiye hashimu, Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam), Maswahaba zake, ahli zake na Waumini wote mpaka Siku ya Qiyaamah.



Maudhui yetu ya leo ni muhimu sana katika zama zetu za leo na matatizo mengi tunakumbana nayo kwa sababu ya kukosekana. Hiyo ni maudhui ya amana.



Huenda mmoja wetu akauliza: Amana ina maana gani katika Dini yetu ya kweli? Suala hilo limejibiwa na Imaam al-Qurtwubiy (Allaah Amrehemu) pale aliposema: Amana inajumlisha shughuli zote za Kidini. Amana ndio faradhi ambazo kwayo Allaah Aliyetukuka Amewapatia waja Wake.

Na wametofautiana katika tafsili, hivyo kukawa na kauli nyingi. Baadhi yake ni:



Pakasemwa: Hiyo ni kuweka amana ya mali na nyengineyo.



Na pakasemwa: Katika kila faradhi, na iliyo nzito ni amana ya mali.



Na pakasemwa: Ni katika amana, kwa alichoaminiwa mwanamke kwa utupu wake, asiitumie katika uzinifu.



Na wakasema wengineo: Kuoga josho la janaba ni katika amana.



Na pakasemwa: Amana ni Swalah, pia Swawm na kuoga josho la janaba.



Na pakasemwa: Hana Imani asiye muaminifu.



Na pakasemwa: Hii ni amana ambayo Allaah Aliyetukuka Aliipatia mbingu, ardhi, majabali na viumbe katika dalili za Uungu Wake.



Na ametaja Ibn al-Jawziy amenukuu kutoka kwa baadhi ya Wafasiri wa Qur-aan kuhusu amana katika Qur-aani Tukufu imegawanyika sehemu tatu:





Ya kwanza: Ni Faradhi, na miongoni mwayo ni kauli ya Aliyetukuka:



﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَخُونُواْ اللّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُواْ أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ﴾ (الأنفال 27).



“Enyi walioamini! Msimfanyie khiyana Allaah na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua” (8: 27).





Ya pili: Kurudisha, na miongoni mwayo ni kauli ya Aliyetukuka:



﴿إِنَّ اللّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤدُّواْ الأَمَانَاتِ إِلَى أَهْلِهَا﴾ (النساء 58).



“Hakika Allaah Anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe” (4: 58).







Ya tatu: Ni utwahara na usafi, na miongoni ni kauli ya Aliyetukuka:



﴿إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ ﴾ (القصص 26).



“Hakika mbora wa kumuajiri ni mwenye nguvu na muaminifu” (28: 26).





Ndugu zangu katika Imani, jueni kuwa amana ni sifa miongoni mwa sifa za Manabii na Waumini wema kama Alivyotuambia Allaah Aliyetukuka katika Kitabu Chake.



Amesema Aliyetukuka kuhusu Nuwh (‘Alayhis Salaam):



﴿كَذَّبَتْ قَوْمُ نُوحٍ الْمُرْسَلِينَ. إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ. إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ. فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ﴾ (الشعراء 105 – 108).



“Kaumu ya Nuwh waliwakadhibisha Mitume. Alipowaambia ndugu yao, Nuwh: Je, Hamuwi wachaji? Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. Basi Mcheni Allaah, na nitiini mimi” (26: 105 – 108).



Na kuhusu Nabii Huwd (‘Alayhis Salaam) Anatuambia Aliyetukuka:



﴿كَذَّبَتْ عَادٌ الْمُرْسَلِينَ. إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ. إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ. فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ﴾ (الشعراء 123 – 126).



“Kaumu ya Huwd waliwakadhibisha Mitume. Alipowaambia ndugu yao, Huwd: Je, Hamuwi wachaji? Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. Basi Mcheni Allaah, na nitiini mimi” (26: 123 – 126).



Na kuhusu Muwsaa (‘Alayhis Salaam), Anasema Aliyetukuka:



﴿قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ الْقَوِيُّ الْأَمِينُ﴾ (القصص 26).



“Akasema mmoja katika wale wanawake: Ee baba yetu! Muajiri huyu. Hakika mbora wa kumuajiri ni mwenye nguvu na muaminifu” (28: 26).



Na kuhusu Yuwsuf (‘Alayhis Salaam), Anasema Aliyetukuka:



﴿وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ أَسْتَخْلِصْهُ لِنَفْسِي فَلَمَّا كَلَّمَهُ قَالَ إِنَّكَ الْيَوْمَ لَدَيْنَا مِكِينٌ أَمِينٌ﴾ (يوسف 54).



“Na mfalme akasema: “Nileteeni (Yuwsuf) nimteue mahsusi kwangu.” Basi aliposema naye, akasema: “Hakika wewe leo kwetu umetamakani kwa cheo na umekuwa muaminiwa.” (12: 54).



Ama Waumini watendao mema, Allaah Aliyetukuka Anatuambia:



﴿وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ﴾ (المؤمنون 8).



“Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao” (23: 8).





Allaah Aliyetukuka Ametuamuru kuwa waaminifu na kutekeleza amana kama Alivyotuambia:



﴿وَإِن كُنتُمْ عَلَى سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُواْ كَاتِبًا فَرِهَانٌ مَّقْبُوضَةٌ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللّهَ رَبَّهُ وَلاَ تَكْتُمُواْ الشَّهَادَةَ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ وَاللّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ﴾ (البقرة 283).



“Na mkiwa safarini na hamkumpata mwandishi, basi (mdai) akabidhiwe rahani. Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah, Rabb wake; na wala msifiche ushahidi; na mwenye kuuficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allaah kwa mnayoyatenda ni Mjuzi.” (2: 283).



Hapa tunapata kuwa hata katika safari ambapo hakuna shahidi, Muislamu anatakiwa awe muaminifu na asimkhini yeyote kwa chochote kile. Na shahidi naye ikiwa atakuwepo anafaa asifiche ushahidi kwani kuficha ni utovu wa amana. Na Muislamu anafaa afahamu kuwa yote anayofanya yanafahamika kwa Allaah Aliyetukuka, hivyo kufanya khiyana kutamweka mahali pabaya. Na Amesema Aliyetukuka:



﴿إِنَّ اللّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤدُّواْ الأَمَانَاتِ إِلَى أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَن تَحْكُمُواْ بِالْعَدْلِ إِنَّ اللّهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ إِنَّ اللّهَ كَانَ سَمِيعًا بَصِيرًا﴾ (النساء 58).



“Hakika Allaah Anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayo kuwaidhini Allaah ni mazuri sana. Hakika Allaah ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona” (4: 58).



Pia Mtume (صلى الله عليه وسلم) ametuamuru kutekeleza amana katika hali zote na hilo lilifahamika hata kwa wasikuwa Waislamu wa zama zake hata wa sasa pia. Imepokewa na ‘Ubaydullaah bin ‘Abdillaah kuwa ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) alimpasha habari:

أخبرني أبو سفيان أن هرقل قال له سألتك ماذا يأمركم؟ فزعمت أنه أمركم بالصلاة والصدق والعفاف والوفاء بالعهد وأداء الأمانة. قال: وهذه صفة نبي.



Alinieleza Abu Sufyaan (رضي الله عنه) kuwa Heraclius (Hiraql) alimwambia nilikuuliza (huyu Mtume) anawaamuru nini? Ukadai kuwa anawaamuru msimamishe Swalah, muwe wakweli, muwe safi (siozini), kutekeleza ahadi na amana. Akasema: Hizo ni sifa za Nabii (Al-Bukhaariy).



Enyi ndugu zangu watukufu, khiyana ya amana ni miongoni mwa alama za unafiki. Ametufahamisha hayo mkweli, mwenye kusadikiwa katika Hadith ya ‘Abdullaah bin ‘Amr bin al-‘Aasw (رضي الله عنهما) kuwa Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:



}أربع من كن فيه كان منافقا خالصا ومن كانت فيه خصلة منهن كانت فيه خصلة من النفاق حتى يدعها: إذا اؤتمن خان وإذا حدث كذب وإذا عاهد غدر وإذا خاصم فجر{ متفق عليه.



“Mtu yeyote akiwa na mambo manne atakuwa mnafiki hasa (kamili), na kama atakuwa na moja katika hayo manne atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aliache. Akiaminiwa hufanya hiyana; na akizungumza anaongopa; na apotoa ahadi huvunja na anapogombana anaiacha haki na kuwa jeuri” (Al-Bukhaariy na Muslim).



Na amesema Abu Hurayrah (رضي الله عنه):



بينما النبي صلى الله عليه وسلم في مجلس يحدث القوم جاءه أعرابي فقال: متى الساعة؟ فمضى رسول الله صلى الله عليه وسلم يحدث فقال بعض القوم سمع ما قال فكره ما قال وقال بعضهم بل لم يسمع حتى إذا قضى حديثه قال: }أين السائل عن الساعة؟{ قال: ها أنا يا رسول الله قال: }إذا ضيعت الأمانة فانتظر الساعة{ قال: كيف إضاعتها؟ قال: }إذا وسد الأمر إلى غير أهله فانتظر الساعة{



Alipokuwa Mtume (صلى الله عليه وسلم) alipokuwa anakhutubia kikao cha watu, mara akaja Mbedui na kuuliza: “Qiyaamah kitakuwa lini?” Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) akaendelea na mazungumzo yake. Hapo wakasema baadhi ya watu: “Amesikia alichoulizwa, lakini akachukia kukatizwa”. Na wengine wakasema: “Bali hajasikia”, mpaka alipomaliza mazungumzo yake, akasema: “Yuwapi muulizaji kuhusu Qiyaamah?” Akajibu: “Nipo hapa, ewe Mtume wa Allaah”. Akasema: “Inapopotezwa amana (kukawa na khiyana) basi ngojeeni Qiyaamah”. Akaulizwa: “Na itapotea vipi?” Akasema: “Pindi uongozi unapopatiwa watu wasiostahiki basi ngojeeni Qiyaamah” (Al-Bukhaariy).



Mvurugiko na machafuko mengi yanayotokea na yanayoendelea kutokea hivi sasa ni kwa sababu ya khiyana na kuchaguliwa kwa wasiofaa katika madaraka tofauti ya uongozi. Inabidi kama Waislamu tushikane barabara na muongozo wa Dini yetu Tukufu, miongoni mwayo ikiwa ni kutekeleza amana na kuwarudishia wanaostahiki.



Na kupotea kwa amana pia kumetabiriwa na Mtume (صلى الله عليه وسلم) kwa kiasi ambacho katika kijiji au mji hakutakuwa na waaminifu wenye kuchunga na kudhibiti amana ila wachache. Allaah Aliyetukuka Atujaalie tuwe wenye kuichunga amana.



Pia tufahamu kuwa yule mwenye sifa hiyo ya khiyana hatokuwa ni mwenye kutazamwa Siku ya Qiyaamah na Allaah Aliyetukuka. Kila mmoja ajiulize, Ikiwa Hutotazamwa na Allaah Aliyetukuka Utakuwa Wapi? Kila mmoja wetu atajijibu mwenyewe. Imepokewa na Abu Hurayrah (رضي الله عنه) kuwa Mtume (صلى الله عليه وسلم) amesema:



(قال الله ثلاثة أنا خصمهم يوم القيامة رجل أعطى بي ثم غدر ورجل باع حرا فأكل ثمنه ورجل استأجر أجيرا فاستوفى منه ولم يعطه أجره) رواه البخاري.



“Allaah Anasema: Nitakuwa dhidi ya (watu) watatu Siku Ya Qiyaamah; mtu anayefunga fungamano kwa jina langu kisha akafanya usaliti, na anayemuuza mtu huru (kama mtumwa) na kula thamani yake, na anayemuajiri mtu akafanyiwa kazi zake kwa ukamilifu lakini hamlipi ujira wake.”
 
CHEMSHA BONGO NAMBA 3
MAJIBU YAKE

Qur'an ina juzuu ngapi?
-30

Jumla ya ayah zilizopo katika qur'an ni ngapi?
-6236

Ipi ni sura fupi kuliko zote?
-al kawthar

Nini maana ya qur'an?
- kinachosomwa

Ni ayah zipi za mwanzo zilizo shushwa?
- aya tano za mwanzo za sura al alaq

96:1 - Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,96:2 - Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,96:3 - Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!96:4 - Ambaye amefundisha kwa kalamu.96:5 - Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.

Zipo sura ngapi katika qur'an?
- 114

Kuna maneno mangapi ya sajdah katika qur'an?
-15

Ni sura ipi ndefu kuliko zote?
- al baqara

Ni sura ipi isiyoanza na Bismillah?
- at'Tawabah

Kama ulipata maksi 70 basi umefaulu kwa mujibu wa wenye mtandao nilikotoa hiyo quiz
 
Fadhila Za Kumtembelea Mgonjwa




Alhidaaya.com







1. Kwanza Kabisa Ni Miongoni Mwa Haki Ya Muislamu Kwa Nduguye Muislamu



عن أبي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ خَمْسٌ: رَدُّ السَّلَامِ وَعِيَادَةُ الْمَرِيضِ وَاتِّبَاعُ الْجَنَائِزِ وَإِجَابَةُ الدَّعْوَةِ وَتَشْمِيتُ الْعَاطِسِ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nimesikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Haki ya Muislamu kwa nduguye Muislamu ni tano: Kujibu Salaam, kumtembelea mgonjwa, kulisindikiza jeneza, kuitikia mwito na kumuombea mwenye kupiga chafya)) [Al-Bukhaariy Muslim]





2. Siku Ya Qiyaamah Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atakuuliza



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يَقُولُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ: يَا ابْنَ آدَمَ مَرِضْتُ فَلَمْ تَعُدْنِي، قَالَ: يَا رَبِّ كَيْفَ أَعُودُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ: أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ عَبْدِي فُلَانًا مَرِضَ فَلَمْ تَعُدْهُ؟ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ لَوْ عُدْتَهُ لَوَجَدْتَنِي عِنْدَهُ؟ يَا ابْنَ آدَمَ، اسْتَطْعَمْتُكَ فَلَمْ تُطْعِمْنِي ، قَالَ: يَا رَبِّ وَكَيْفَ أُطْعِمُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ: أَمَا عَلِمْتَ أَنَّهُ اسْتَطْعَمَكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تُطْعِمْهُ؟ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ لَوْ أَطْعَمْتَهُ لَوَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟ يَا ابْنَ آدَمَ اسْتَسْقَيْتُكَ فَلَمْ تَسْقِنِي، قَالَ: يَا رَبِّ كَيْفَ أَسْقِيكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ اسْتَسْقَاكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تَسْقِهِ، أَمَا إِنَّكَ لَوْ سَقَيْتَهُ وَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟)) مسلم

Kutoka Kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: ((Hakika Allaah ‘Aliyetukuka na Jalali Atasema siku ya Qiyaamah: Ee mwana wa Aadam, Niliumwa na usije kunitembelea? Atasema: Ee Rabb (Mola), vipi nije kukutembelea nawe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Kwani ulijua kuwa mja wangu fulani alikuwa mgonjwa na hukwenda kumtembelea! Hukujua kuwa ungekwenda ungalinikuta Niko pamoja naye? Ee mwana wa Aadam, Nilikuomba chakula na hukunipa. Atasema: Ee Rabb, vipi nitakupa chakula na Wewe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Kwani hukujua kuwa mja wangu fulani alikuomba chakula na hukumpa? Hukujua kuwa ungalimpa chakula ungalikuta hayo (jazaa) kwangu mimi? Ee mwana wa Aadam, nilikuomba maji na hukunipa. Atasema: Ee Rabb, vipi nitakupa maji na Wewe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Mja wangu fulani alikuomba maji na hukumpa. Hukujua kwamba ungalimpa maji ungalikuta hayo (jazaa) Kwangu Mimi)) [Muslim]





3. Malaika Sabini Elfu Wanakuombea Rahmah



Kumtembelea mgonjwa kuna fadhila nyingi tukufu kama zilivyothibiti katika Hadiyth kadhaa mojawapo ni kwamba mwenye kumtembelea mgonjwa huswaliwa na Malaika elfu sabini. Hadiyth ya ‘Aliy bin Abiy Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu):



قَالَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِذَا عَادَ الرَّجُلُ أَخَاهُ المُسْلِمَ مَشَى فِي خِرَافَةِ الجَنَّةِ حَتَّى يَجْلِسَ فَإِذَا جَلَسَ غَمَرَتْهُ الرَّحْمَةُ، فَإِنْ كَانَ غُدْوَةً صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُوْنَ أَلْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُمْسِيَ، وَإِنْ كَانَ مَسَاءً صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُوْنَ أَلْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُصْبِحَ)).

Amesema (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam): ((Mtu anapomtembelea ndugu yake Muislamu mgonjwa, basi hutembelea katika bustani ya Jannah mpaka atakapoketi, na anapoketi hufunikwa na Rahmah ikiwa ni asubuhi wanamtakia Rahmah Malaika sabini elfu mpaka jioni. Na ikiwa ni jioni wanamtakia Rahmah Malaika sabini elfu mpaka asubuhi)) [Swahiyh Ibn Maajah (1/244), Swahiyh At-Tirmidhiy (1/286)]





4. Du’aa Kutakabaliwa



Juu ya hivyo ni fursa kwa Muislamu kuomba du’aa yake itakabaliwe. Aanze kwanza kumwombea mgonjwa du’aa zilizothibiti katika Sunnah kisha ajiombee nafsi yake:



عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ (رضي الله عنها) قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((إِذَا حَضَرْتُمْ الْمَرِيضَ أَوْ الْمَيِّتَ فَقُولُوا خَيْرًا فَإِنَّ الْملآئِكَةَ يُؤَمِّنُونَ عَلَى مَا تَقُولُونَ)) قَالَتْ: فَلَمَّا مَاتَ أَبُو سَلَمَةَ أَتَيْتُ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ أَبَا سَلَمَةَ قَدْ مَاتَ قَالَ: ((قُولِي: اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي وَلَهُ وَأَعْقِبْنِي مِنْهُ عُقْبَى حَسَنَةً)) قَالَتْ: فَقُلْتُ فَأَعْقَبَنِي اللَّهُ مَنْ هُوَ خَيْرٌ لِي مِنْهُ مُحَمَّدًا (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)

Imepokelewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mnapohudhuria mgonjwa au maiti basi semeni yaliyo mema kwani Malaika wanaitikia ‘Aamiyn’ msemayo)). Akasema: Alipofariki Abuu Salamah nilimwendea Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Abuu Salamah amefariki. Akasema: ((Sema: ‘Allaahumma-ghfir-liy wa lahu wa 'a-qibniy minhu ‘uqba hasanah’ [Ee Allaah, nighufurie pamoja naye na nilipie baada yake badali iliyo njema])). Akasema: Akanilipa Allaah aliye mbora zaidi kuliko yeye; (ambaye ni) Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam))). [Muslim, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]
 
Tumeona hapo fadhila hapo za kumtembelea mgonjwa,ndio maana Allah anasema wanao mcha yeye zaidi ni wale wanazuoni au wenye elimu ya dini

Maana ukijua fadhila na faida ya jambo fulani ndio utapupia kuifanya amali hiyo kwakuwa unajua Allah atakulipa

Kwahiyo naamini wale ambao hatukujua haya basi tuyafanye kwa kutaraji radhi za Allah

Na ni fursa ya kujiombea dua pia na ikakubaliwa
 
Back
Top Bottom