Ramadhan Special Thread
Kuwa Na Rafiki Mwanamme (Boyfriend) Inajuzu?
Maswali: Maasi


Kuwa Na Rafiki Mwanamme (Boyfriend) Inajuzu?



Alhidaaya.com

Swali:



Assalam alaikum warahmatullahi wabarakatuh, nataka kuuliza kama kuwa na boy frend inaitikiwa katika dini ya islam,na nataka niwe na dalili ayat ama hadith.


wahadha assalam alaikum,kazi ndjema



Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Tunamshukuru dada yetu kuuliza Swali muhimu kama hili ambalo linahitajika kujibiwa na kuelimisha ndugu zetu makatazo hayo ambayo sasa imekuwa kama ni jambo la kawaida katika jamii zetu na hali sio kutokana na mafunzo ya dini yetu.



Ayaah na dalili za kukataza jambo hili zipo nyingi zikiwa zinazoashiria makatazo moja kwa moja (directly) na nyinginezo zenye uhusiano na makatazo haya. Kuwa na boyfriend bila shaka kutasababisha yatendeke maasi baina ya mwanamke na mwanamume kwani shaytwaan huwa pamoja nao akiwachochea kuingia katika kumuasi Mola wao:



عن عمر رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم : ((ما خلا رجل بامرأة إلا كان الشيطان ثالثهما)) الترمذي


Kutoka kwa 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Hachanganyiki mwanamume na mwanamke ila shaytwaan huwa ni watatu wao)) [At-Tirmidhiy]





Ndio maana pia Nabiy ((Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya kukaa faraagha mwanamke na mwanamume:

قال صلىالله عليه سلم : ((لا يخلوّنّ أحدكم بامرأةإلا مع ذى محرم)) متفق عليه



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hawi faraagha mmoja wenu pamoja na mwanamke ila awepo Mahram wake)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]



Matokeo yake ni shaytwaan kuwafikisha kuingia katika maasi ya zinaa na ndio maana sheria ya Kiislamu haikuruhusu jambo hilo au kufunga uchumba inavyojulikana engagement. Bali inatakiwa kufunga ndoa moja kwa moja baada ya kuwafikiana pande zote. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

((وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَأُوتُواْ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّمُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلاَ مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ وَمَنيَكْفُرْ بِالإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَالْخَاسِرِين))



Na wanawake walioimarisha sitara (wasiozini) miongoni mwa Waumini wanawake na wanawake walioimarisha sitara miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu; mtakapowapa mahari yao mkijistahi bila ya kuwa maasherati wala kuchukua hawara. Na yeyote atakayekanusha iymaan; basi kwa yakini imeporomoka ‘amali yake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika. [Al-Maaidah: 5].



Hizo ni mila za kikafiri ambazo zinapasa tuepukano nazo na ambazo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametuonya:



((وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُم))

((Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao)) [Al-Baqarah: 120].



Msichana wa Kiislamu unapokabiliwa na mvulana kutaka kufanya urafiki ujiepushe kabisa bali umshauri kwanza awasiliane na wazazi wako na baada ya kumjua kuwa ni mtu mwenye dini na tabia nzuri basi wazazi wasichelewa kukuozesha nawe uridhike kwani hivyo ndivyo ipasavyo na tulivyopewa mafunzo kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) :


((إِذَا خَطَبَ إِلَيْكُمْمَنْ تَرْضَوْنَ دِينَهُ وَخُلُقَهُ فَزَوِّجُوهُ إِلَّا تَفْعَلُوا تَكُنْ فِتْنَةٌفِي الْأَرْضِ وَفَسَادٌ عَرِيضٌ)) رواهالترمذي وقال الألباني : حسن


((Atakapoposa kwenu yule mtakaeridhika na dini yake, na tabia yake, basi muozesheni, kwani kutokufanya hivyo itakuwa fitna katika ardhi (duniani) na ufisadi mpana (mkubwa) )) [At-Tirmidhiy kasimulia na Shaykh Albaaniy amesema ni Hadiyth Hasan].



Tunatumai dada yetu na wengine wote wataridhika na mafunzo ya dini yetu ili wabakie wote katika usalama, stara na Ridhaa ya Mola wetu.


Na Allaah Anajua zaidi
 
Naam ndugu zangu katika Imani kikubwa nakuomba kwa ajili ya Allah pata hamasa ya kusoma mambo ya dini upate kuokoteza hili na lile,na elimu inakufikia hapa hapa jf kupitia uzi huu

Pamoja na kwamba kusudio la uzi huu lilikuwa kwa Ramadhani tu,lkn nikaona kutakuwa kuna faida gani ikiwa hatuto tumia uzi huu ambao unatuunganisha waislamu kupata faida zaidi katika Uislamu wetu

Ndio nikajitolea kwa ajili ya Allah na kwa wengine mtakao niunga mkono tufanye lile alilo tuagiza Allah subhaanahu wa Taala pale alipo sema "NA WAWEP0 MIONGONI MWENU WATAKAO AMRISHA MEMA NA KUKATAZA MABAYA"

Na

Vile vile tumeitwa Umma bora kwa sababu ya kuamrishana mema na kukatazana mabaya

Kwahiyo pitia nyuzi zako uzipendazo lkn ukiikuta hii thread basi ichungulie huenda ukaokota chochote chenye kukufaa hapa duniani na kesho akhera

Asalaam alaikum warahmatullah wabarakutuh

Baadae inshaallah
 
MASWALI NA MAJIBU


Swalaah Katika Kanisa Inafaa?
Maswali: Hukmu Za Swalah
Swalah Katika Kanisa Inafaa?



www.alhidaaya.com





SWALI:



Assallam Aleikum

Mimi ni mkazi wa hapa England jina …..swali langu ni kuhusu tatizo la msikititi hapa tunapoishi. Sisi tunasali kwenye kanisa ambayo tumeikodi hapa tunapoishi. Ni swala ya ijumaa na ramadhani taraawiyh. Je inaturuhusu sisi kuswali mahala hapo, ndani hapana sanamu lakini nje kuna Msalaba. Mahali penyewe hapauzwi haramu na kila ijumaa ya mwisho wa mwezi watu huja ku donate damu na pia masherehe mengine tofouti hufanyika. Naomba unijibu kwa mifano ya maswahaba na muhimu zaidi kwenye quraan na hadith, ili niweze kuwaeleza wenzangu





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Nimepatiwa vitu vitano ambavyo hakupatiwa mwengine kabla yangu: ((Ardhi yote imefanywa kwangu (na Ummah wangu) kuwa ni Msikiti na twahaarah, hivyo yeyote katika Ummah wangu anaweza kuswali popote Swalah inapomuingilia...”)) [Al-Bukhariy na Muslim kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ]



Hii Hadiyth ni ya kijumla kabisa katika utendaji kazi wake na hii ni kuwa Swalah kama nguzo muhimu sana ya Kiislamu haina udhuru isipokuwa zile ambazo zinajulikana na kila mmoja na hasa zinapatikana kwa kina dada kama kuwa katika ada ya mwezi, au kutokwa na damu ya uzazi baada ya kuzaa, n.k. Sasa hapa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anatuelekeza kuwa ardhi yote ni tohara na Msikiti hivyo unaweza kuswali popote isipokuwa unapoona najisi iliyo ya dhahiri kabisa.



Hivyo, kanisa liko katika ardhi na ndio pia tunapata athari ya Swahaba mtukufu kama ‘Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye ana kauli mashuhuri pale alipokwenda Baytil Maqdis ili kuchukua funguo za mji huo kutoka kwa kasisi Sophronius. Wakati wa moja wapo wa Swalah ulifika akiwa ndani ya kanisa, na yule kasisi mwenyeji wake akamwambia waweza kuswali hapa ndani lakini akakataa kufanya hivyo kwa kumwambia: “Sio kuwa nimekataa kwa sababu ni haramu lakini sitaki Waislamu watakaokuja baadae kutaka kulifanya hili kanisa kuwa Msikiti kwa sababu mimi nimeswali ndani yake”.



Kwa hali yenu ilivyo ikiwa mutaweza kupata sehemu nyengine ya kukodisha itakuwa bora zaidi na tunaamini kuwa zipo nyingi kwa jinsi tunavyofahamu hali ya Uingereza na kupatikana kwa nyumba nyingi za council za kukodisha kama wanavyofanya wenzenu wa miji mingine wanapofanya Mihadhara yao na shughuli za ndoa na pia Swalah za 'Iyd n.k.



Hamjafikia udhuru wa kuswali kanisani kwa hali yoyote, na bora zaidi muepukane na jambo hilo ingawa kuna baadhi ya Maulamaa wanaonelea kuwa hakuna tatizo iwapo patakuwa humo ndani hakuna masanamu na mapicha au kumezikwa watukufu wao.



Tunaona kwenye hadiyth maarufu ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) iliyopokewa na bi 'Aishah (Radhwiya Allaahu 'anha) kuwa: Aliporudi mmoja wa wake zake (Ummu Salamah) kutoka Habashah (Ethiopia) na kumsifia uzuri wa makanisa waliyokuta kule, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimjibu: (('Hao ni watu ambao, anapokufa mmoja wa watu wema wao, basi hujenga nyumba za kuabudia juu ya kaburi lake na kuweka picha na masanamu ndani yake. Hao ni viumbe viovu kabisa mbele ya Allaah [Al Bukhaariy na Muslim]



Kwa hiyo tunaona kwenye hadiyth hiyo kuwa wana tabia ya kuzika watukufu wao ndani ya majumba yao ya ibada na kama ilivyo sheria, ni haramu kuswali penye kaburi au kulielekea kama hadiyth zinavyoonyesha. Huenda kwa wakati huu si wote wanaozika watukufu wao ndani ya makanisa/mahekalu yao, lakini ni vizuri kuwa na tahadhari.

Na kama hamtopata sehemu kabisa ya kuswalia ikasababisha msipate kuswali Swalah ya Ijumaa na ni hapo tu mlipopata, basi munaweza kuswali humo ingawa ni Makuruhu. Na misalaba ilioko nje kama mnaweza kuondosha ni vizuri pia na kama haiwezekani basi si kikwazo, ila muhakikishe ndani hakuna masanamu wala mapicha.



Jaribuni kule ndani mutoe misalaba na mapicha yalioko ndani kisha muendelee na ‘Ibadah zenu, na kama itashindikana kutoa basi baadhi ya 'Ulamaa wanasema mnaweza kuyafunika kwa nguo au chochote, na haswa yale ambayo mkiswali mnayaelekea. Kwani Malaika haingii sehemu yenye masanamu/picha

Inasemwa katika vitabu vya historia kuwa:



Abuu Muwsaa al-Ash'ariy na 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz waliswali kanisani.
Ash-Sh'abiy, 'Ata, na Ibn Siriyn hawakuona tatizo lolote kwamtu kuswali kanisani, hasa ikiwa yuko hapo ndani na wakati wa Swalah umefika.
Al-Bukhariy amesema: "Ibn 'Abbaas alikuwa akiswali makanisani isipokuwa yale ambayo yana masanamu".
Waislamu wa Najran walimuandikia 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) ) kumwambia ya kwamba hawana sehemu iliyo safi na nzuri zaidi kuliko kanisa. 'Umar aliwajibu: Linyunyizieni maji na majani na kisha muswali ndani yake".
Kwa mujibu wa Hanafi na Shafi'i, haipendezi kiujumla kuswali katika sehemu hizo.
Imaam Ahmad kuwa haitofaa kuswaliwa humo kama kuna masanamu/mapicha.
Na Imaam Maalik kakataza kabisa hata kwa udhuru.
Pia inajulikana kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuzunguka Al Ka'abah hadi yalipovunjwa masanamu yote.
Imaam Muhammad bin 'Abdil-Wahhaab anasema katika kitabu cha Tawhiyd "aifai kuswali katika maeneo yenye kufanyiwa ibada za kishirikina".


Na kama tunavyojua, hawa wakristo wanamshirikisha Allaah kwa utatu wao; kuwa na mungu baba, mungu mwana, na roho mtakatifu.



Mwisho, kwa hoja hizo hapo juu, tunawanasihi ndugu zetu mjitahidi kadiri muwezavyo kutafuta maeneo mengine na mjiepusha na shub-ha hiyo, na kama tulivyosema na tujuavyo kuwa Uingereza maeneo ni mengi na yanakodishwa kwa gharama nafuu zinazomudiwa kwa hali ya kipato cha huko, kwa hiyo msuitafute njia za rahisi rahisi na mkato kwa sababu labda mmepata rai ya mwanachuoni mmoja au baadhi ya watu. Daima mfuate Hadiyth isemayo:

((Acha chenye kukutia mashaka na fuata kisichokutia mashaka)) [Imenukuliwa na An-Nasaaiy na at-Tirmidhiy ambaye amesema ni Hadith Hasan Sahiyh kutoka kwa Abuu Muhammad al-Hasan bin 'Aliy (Radhiya Allaahu 'anhu)]



Na Allaah Anajua zaidi
 
Kufanya Haja Ndogo (Kukojoa) Wima Imethibiti Katika Sunnah?



Alhidaaya.com







SWALI:



Assalam Alykum Warahmatullah Wabarakatuh. Swali langu ni kwamba Niliskia kuna Hadith ya Aisha radhiya Allahu anha kwamba amesema sijapato kumwona Nabii Swalla Allaahu alyhi wasallam akikojoa wima, na niliwahi kusikia kuwa imethibiti katika hadith kuwa Nabii Swalla Allaahu alyhi wa sallam alionekana akikojoa wima. Naomba kujua nifuate ipi. Jazaakum Allaahu Khayrah





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.







Hakika katika mas-ala haya zipo Hadiyth tano kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) – tatu sahihi na mbili dhaifu. Moja ni kukataa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikojoa kwa kusimama, ya pili ni kuonyesha kuwa alikojoa kwa kusimama na ya tatu akiwa ameketi. Na katika hizo Hadiyth dhaifu ni kukataza kwake kukojoa kwa kusimama na ya pili ni kukemea kwake Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa kukojoa kwa kusimama ni katika kukengeuka. Hapa twazitaja zote kwa faida ya kila mmoja wetu:





1-Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) aliyesema: “Yeyote anayekuhadithieni kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikojoa kwa kusimama msimsadiki. Alikuwa hakojoi ila kwa kuketi.” [Ahmad, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]





2- Hadiyth ya Hudhayfah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikwenda kwenye jaa la taka la watu, akakojoa kwa kusimama. Mimi nikaondoka, akasema: “Njoo.” Nikarudi mpaka nikasimama kwenye mabega yake, akatawadha na kupangusa juu ya viatu vyake. [Al-Bukhaariy, Muslim, Ahmad, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah]





3-Hadiyth ya ‘Abdur-Rahman bin Hasnah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliyesema: Alitoka kwetu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa mkononi mwake ana ngao ya ngozi, akaiweka, kisha akaketi nyuma yake akakojoa kuielekea… [Ahmad, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah]





Na zifuatazo ni Hadiyth mbili zilizo dhaifu:



1-Imepokewa na Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuwa ‘Umar (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniona nikikojoa kwa kusimama. Akaniambia: Ee ‘Umar! Usikojoe kwa kusimama. Akasema: Sikukojoa tena kwa kusimama baada ya hapo. [Ibn Maajah, Al-Bayhaqiy na al-Haakim lakini ni Hadiyth iliyo dhaifu]





2-Imepokewa na Buraydah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Vitu vitatu ni katika kukengeuka: Mtu kukojoa kwa kusimama, kupangusa mgongo wake kabla ya kuondoka katika Swalaah na kupuliza katika sijdah yake.” [Ameinukuu al-Bukhaariy katika Taariykh yake, al-Bazzaar, na akaikanusha al-Bukhaariy na at-Tirmidhiy. Na hii imethubutu kuwa ni kauli ya Ibn Mas‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu)]





Kutokana na Hadiyth hizo, ‘Ulamaa wametofautiana kuhusu kukojoa wima. Kwa ajili hiyo zikapatikana kauli tatu.



1. Inachukiza pasi na udhuru wowote: Hii ni kauli ya ‘Aaishah, Ibn Mas‘uwd, ‘Umar (katika riwaayah yake moja) Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu ‘anhum); Ash-Sha‘biy, Ibn ‘Uyaynah, Abu Haniyfah na ash-Shaafi‘iy.





2. Inajuzu daima dawamu: Hii ni kauli ya ‘Umar (katika riwaayah yake ya pili), ‘Aliy, Zayd bin Thaabit, Ibn ‘Umar, Sahl bin Sa‘d, Anas, Abu Hurayrah, Hudhayfah (Radhwiya Allaahu ‘anhum); ni kauli ya Ahmad bin Hanbal.





3. Ikiwa ni katika sehemu ambayo hairudishi (hauruki) mkojo kwake inajuzu na ikiwa unarudi basi haifai: Hii ni kauli ya Maalik, na Ibn al-Mundhir akaiona ni sahihi.





Baada ya hayo yaliyo juu, tunafupisha maneno kwa kusema kuwa hakuna uharaam wowote wa kukojoa kwa kusimama ikiwa mkojo hautarudi au kumrukia mwenye kukojoa ila ni bora kukojoa kwa kuketi. Imaam an-Nawawiy akizungumzia mas-ala haya amesema: “Kukojoa kwa kuketi inapendeza zaidi kwa rai yangu, lakini kufanya hivyo kwa kusimama wima kunaruhusiwa. Matendo yote mawili yamepatikana kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).”.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Bid'ah - Uzushi


Kupangusa Uso Baada Ya Kusoma Du’aa Inafaa?



Alhidaaya.com





SWALI:



Assalam aleikum

ningependa munifahamishe kuhusu mtu kufuta uso wake akimaliza dua wakati anaposema Amin, je kuna hadith yoyote ama kithibitisho kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alikuwa akifanya hivyo? Jaza yenu iko kwa Allaah subhanahuu wa Ta'aalaa kwa kazi munayo fanya, Shukran





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho



Kupangusa uso baada ya kuomba du’aa si kitendo cha Sunnah, na Hadiyth nyingi zilizopokelewa kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aailihi wa sallam) alipokuwa akiomba du’aa zake hakuwa akipangusa uso wake baada ya du’aa. Na hata katika Khutbah ya Ijumaa au Swalaah ya Istisqaa haikuthibiti kwamba alipangusa mikono yake usoni. Hadiyth moja au mbili zilizosimuliwa kuhusu kitendo hiki zimechambuliwa kuwa ni Hadiyth dhaifu, na 'ulaamaa wamekubaliana kwamba kitendo hiki hakipo katika Shari’ah.



Na hata Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akimaliza Swalaah zake na kutoa salaam, hakuwa kamwe akipangusa uso wake kama ilivyo ada ya Waislamu wengi hivi leo wanavyofanya na hawajui kwanini wanafanya hivyo na hata ukimuuliza mtu anashindwa kukupa jibu, na wengine wanajibu kuwa wamejikuta wakikuwa na kuona ikifanywa hivyo na wao wanafanya. Muislamu anapaswa kufanya matendo yake yote ya ‘Ibaadah kwa dalili na si kwa kubahatisha au kuiga bila dalili.



Na Allaah Anajua zaidi
 
CHEMSHA BONGO NAMBA 2

1] Ni ipi sura ya mwisho kushuka katika Qur'an ?

2] Mtume swallallahu alaih wasallam katajwa mara ngapi katika qur'an?


3] Khalifa gani aliamrisha msahafu uandikwe?


4] Khalifa gani aliagiza msahafu uandikwe kwa lahaja moja ya ki quraish?


5] Qur'an ilikusanywa yote kwa sababu gani?


6] Je qur'an iliposhushwa ilikuwa na harakaat zake (fatha,dhwamma,sakinah,kasra)?


7] Je qur'an ilishuka na lahaja ngapi?
 
029-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Za 'Iyd Mbili - Sifa Ya Swalah Ya Mtume


9- SWALAH ZA 'IYD MBILI



"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akisoma (mara nyingine) katika Rakaa ya kwanza



سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى



((Litakase jina la Mola wako Aliye juu kabisa)) [Al-A'laa 87: 19], na katika Rakaa ya pili:



هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ



((Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?)) [88: 26] [1]. Na mara nyingine "alikuwa akisoma katika hizo Rakaa mbili:



ق وَالْقُرْآنِ الْمَجِيدِ



((Qaaf, Naapa kwa Qur-aan Tukufu))[Qaaf 50: 45], na



اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ



((Saa imekaribia na mwezi umepasuka)) [Al-Qamar 54: 55][2].







[1] Muslim na Abu Daawuud.

[2] Muslim na Abu Daawuud.
 
030-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Ya Janaazah


10- SWALAH YA JANAAZAH



"Sunnah ni kusoma Suratul Faatihah[1] [na sura nyingineyo][2]. Pia "Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akikaa kimya kwa muda baada ya Takbiyr ya kwanza"[3]





KUSOMA KISOMO VILIVYO NA KUITENGENEZA SAUTI UNAPOSOMA



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma - kama Alivyoamrishwa na Allaah - Qur-aan vilivyo – kama inavyotakiwa kusomwa, mtu anatakiwa achunge hukumu za kuisoma-, bila ya kwenda mbio wala kuharakiza, bali kisomo cha "Uchambuzi/ufafanuzi chenye kupelekea kubaini herufi baada ya herufi"[4] (sana) hadi "alikuwa akisoma Surah mpaka inakuwa ndefu mno kulinganisha na Surah iliyo refu na hiyo anayoisoma (kwa kadiri inavyowezekana).[5]



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Itasemwa kwa mwenye kusoma Qur-aan (siku ya Qiyaamah): Soma na upande; soma (pole pole kwa mahadhi) kama ulivyokuwa ukisoma duniani; makaazi yako kwenye Aayah ya mwisho usomayo))[6]



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) "akirefusha kisomo chake (kwenye herufi za kurefushwa), alikuwa akirefusha Bismi Llaahi, na akirefusha Ar-Rahmaan na akirefusha Ar-Rahiym"[7] na katika "nadhiyd" [Qaaf 50: 10][8] na mfano wa (kama) hizo.



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisimama mwisho wa kila Aayah kama ilivyoelezwa kabla.



Mara nyingine "alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma kwa sauti ya kuvutia ya kutetema[9] kama alviyofanya siku ya kufunguliwa kwa Makkah hali ya kuwa yuko juu ya ngamia wake, anasoma Suratul-Fat-h [48: 29] [kwa suatinyororo][10] na 'Abdullaah bin Mughaffal amesimulia hii sauti ya kuvutia : aaa"[11]



Alikuwa akiamrisha kuipamba sauti katika kusoma Qur-aan, alikuwa akisema: ((Ipambeni Qur-aan kwa sauti zenu (kwani sauti nzuri huzidisha kuipamba Qur-aan))[12]



Na alikuwa akisema: ((Hakika mwenye sauti bora miongoni mwa watu katika kusoma Qur-aan ni yule ambaye mnapomsikia akiisoma, mtamdhania ni mwenye kumkhofu Allaah))[13]



Alikuwa pia akiamrisha kusoma Qur-aan kwa sauti ya kupendeza, alikuwa akisema: ((Jifunzeni kitabu cha Allaah, dumisheni kuisoma, ithibitisheni (kuhifadhi), na isomeni kwa (sauti ya) kughani, kwani Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, inakimbia haraka kuliko ngamia anavyochopoka katika kamba))[14]





Alikuwa pia akisema: ((Sio miongoni mwetu mwenye kuisoma Qur-aan bila ya kughani [kupendezesha sauti]))[15]



Na akisema:

((Allaah Hakuwahi kusikiliza kitu chochote zaidi ya jinsi ya kusikiliza [katika riwaaya nyingine: ((Kama Anavyomsikiliza))] Mtume (kwa shauku) ((kwa sauti ya kupendeza))], na [katika riwaaya nyingine: anavyosoma Qur-aan kwa sauti nzuri[16] ((ananyanyua sauti kwako))[17]



Alimuambia Abu Muusa Al-Ash'ariyy (رضي الله عنه) ((Lau ungeliniona nilipokuwa nasikiliza kisomo chako usiku wa jana, kwa Hakika umepewa mzumari[18] katika mizumari ya aila ya Daawuud!)) Hivyo Abu Muusa akasema: "Lau ningelijua kuwa uko, ningelizidi kuitengeneza na kuipendesha sauti yangu kwa ajili yako"[19]






[1] Hii ni kauli ya Imaam Ash-Shaafi'y, Ahmad na Is-haaq, na pia ni rai ya baadhi ya watafiti wa Mahanafi waliokuja baadaye. Ama kuhusu kusoma Surah baada yake, huu ni mtazamo wa baadhi ya Ma-Shaafi'y na ni mtazamo Swahiyh.

[2] Al-Bukhaariy, Abu Daawuud, An-Nassaiy na Ibn Al-Jaaruud. Na wala hii ziada sio ya pekee (haina mwenzake) (kitu kimoja hakina mwenzake hapa sio ajabu) kama At-Tuwayjiriy anavyodai.

[3] An-Nasaaiy na At-Twahaawiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[4] Ibn Al-Mubaarak katika Az-Zuhd (162/1 kutoka Al-Kawaakib 575), Abu Daawuud na Ahmad kwa isnaad Swahiyh.

[5] Muslim na Maalik.

[6] Abu Daawuud na At-Tirmidhiy ambaye amesema Swahiyh.

[7] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[8] Al-Bukhaariy katika Af'aal al 'Ibaad kwa isnaad Swahiyh.

[9] Inatokana na neon Tarjiy', Ibn Hajar ameeleza: kuwa ni sauti ya kutetema na asli yake ni at tardiyd, watarjiy’ sauti: ni kuikariri kutoka kwenye halq. Al-Manaawiy kasema, "Inakuja aghlabu kwa kuwa na hisia ya shangwe na furaha ambayo alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)siku ya Ushindi wa Makkah".

[10] Al-Bukhaariy na Muslim.

[11] Al-Bukhaariy na Muslim. Ibn Hajar amesema katika maelezo kuhusu "aaa (آآآ) "hii ni hamzah ikiwa na fat-haa, ikifuatia na alif ya kimya, ikifuatia na hamzah nyingine". Shaykh 'Aliy Al-Qaariy amenukuu kama hiyo kutokana na wengine na akasema: "Ni dhahiri kuwa hizi ni Alif tatu zenye kuvutwa (ndefu)"

[12] Al-Bukhaariy ta'aliyq (kiambatisho), Abu Daawauud, Ad-Daarimiy, Al-Haakim na Tamaam Ar-Raazi kwa isnaad mbili Swahiyh.

[13] Hadiyth ni Swahiyh, imesimuliwa na Ibn Al-Mubaarak katika Az-Zuhd (162/1 kutoka Al-Kawaakib 575), Ad-Daarimiy, Ibn Naswr, At-Twabaraaniy, Abu Nu'aym katika Akhbaar Aswbahaan na Adh-Dwhiyaa katika Al-Mukhtaarah.

[14] Ad-Daarimiy na Ahmad kwa isnaad Swahiyh.

TANBIHI: Hadiyth ya kwanza imegeuzwa na msimulizi mmoja, hivyo ameisimulia: ((Pambeni sauti zenu kwa (kwenye) Qur-aan)). Haya ni makosa katika usimulizi na ufahamu, na yeyote mwenye kusema ni Swahiyh basi huyo amezama zaidi katika makosa, kwani inapingana na Simulizi Swahiyh zilizofafanuliwa katika mlango huu. Bali ni mfano bora katika Hadiyth Maqluub (iliyogeuzwa) na maelezo zaidi ya hii (tanbihi) yamo katika Silisilatul-Ahaadiyth Ad-Dhwa'iyfah (Namba 5328).

[15] Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amesema ni Swahiyh na Adh-Dhahaabiy amekubaliana naye.

[16] Amesema Al-Mundhiriy ‘taghannaa’ inamaanisha kuisoma kwa sauti ya kupendeza; Sufyaan bin 'Uyaynah na wengineo wamechukua rai kwamba ni kufanya istighnaa (yaani Qur-aan kumfanya mtu ajitenge na mapambo ya dunia) lakini hii imekanushwa.

[17] Al-Bukhaariy, Muslim, At-Twahaawiy na Ibn Mandah katika Tawhiyd (81/1)

[18] Maulamaa wamesema kuwa mizumari hapa inamaansiha: sauti nzuri, na asili ya az-zumar ni al-ghinaa: kuimba, na kwamba aila ya Daawuud inakusudiwa Daawuud mwenyewe, na aila fulani hutumika na humaanisha khaswa ya mtu mwenyewe. Daawuud (عليه السلام) alikuwa na sauti nzuri mno. Hii ameitaja An-Nawawy katika maelezo yake ya Swahiyh Muslim.

[19] 'Abdur-Razzaaq katika Al-Amaaliy (2/44/1), Al-Bukhaariy, Muslim, Ibn Naswr na Haakim.
 
Naam katika darsa nambar 30 tumeona Nabii swallallahu alaih wasallam anasema kwanza tusomapo qur'an kwanza tujitahidi kwa kuisoma kwa sauti nzuri,kwani sauti nzuri huzidisha uzuri wake,,wote mashahidi ukikutana na mtu anayesoma vizur wallah waeza pata hisia nzito huenda hata machozi yakakutoka


Pili tukithirishe kuisoma sana ili idhibiti vizuri vifuani kwetu,maana hakika inaponyoka haraka kuliko ngamia anavyoponyoka katika kamba yake,na hii ni kweli binafsi kuna sura nilizihifadhi leo nimeanza kuzihifadhi tena,kubwa sura ulizo zihifadhi jitahidi kuzisoma sana kwenye swala zako za sunna,hii itafanya zikae vizur kichwani kwako

Lakini tatu kama tulivyoona hapo awali,Allah anapenda ibada inayofanywa kwa uchache lkn yenye kudumu,basi walau azimia kila siku usikose kusoma qur'an japo kwa uchache,uzidi kujiwekea hazina yako itakayo kufaa siku ya kiama,na hakuna zikri bora mbele ya Allah kama kusoma maneno yake
 
031-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kumsahihisha Imaam Na Kujikinga Na Shaytwaan




KUMSAHIHISHA IMAAM




Ametoa (صلى الله عليه وآله وسلم)mfano katika kumsahihisha Imaam anapobabaika au anapochanganyikiwa na kisomo chake. Mara moja aliswali, akasoma ndani yake kisomo, akasahau. Alipomaliza alimwambia Ubayy: ((Uliswali na sisi?)). Alijibu: "Ndio". Akasema: ((Hivyo nini kilichokuzuia [kunisahihisha]?))([1]).










KUJIKINGA NA SHAYTWAAN NA KUTEMA MATE KIDOGO WAKATI WA SWALAH ILI KUONDOSHA WASIWASI




'Uthmaan bin Abil-Aasw (رضي الله عنه) alimwambia: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Shaytwaan ameingia baina yangu na baina ya Swalah yangu na kisomo changu, ananibabaisha katika kisomo changu!" Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Huyo ni Shaytwaan anayeitwa Khinzab, hivyo utakapomuhisi jikinge kwa Allaah naye, na tema mate kidogo([2]) upande wa kushoto kwako mara tatu)). Akasema: "Nikafanya hivyo, na Allaah Akamuondoshelea mbali nami".([3]).










[1] Abu Daawuud, Ibn Hibbaan, Atw-Twabaraaniy, Ibn 'Asaakir (2/296/2) na Adhw-Dhwiyaa katika Al-Mukhtaarah kwa isnaad Swahiyh.

[2] "At-Tafl" ni mpulizo ikiwa na mate kidogo, hivyo ni zaidi ya kupuliza. (An-Nihaayah).

[3] Muslim na Ahmad. An-Nawawiy (رحمه الله) amesema: "Hadiyth hii ina mapendekezo ya kujikinga na Shaytwaan anaposhawishi, pamoja na kutema mate upande wa kushoto mara tatu".
 
Adabu Za Kuchunga Katika Nyumba Ya Allaah (Misikiti)



Imefasiriwa Na: Abuu Nawwaaf



Alhidaaya.com





Bismillaahi Rahmaani Rahiim



Kila Muislamu anaujua utukufu wa nyumba za Allaah. Msikiti ulikuwa ni katika mambo ya mwanzo ambayo Rasuli Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliyasimamia mara alipofika Madiynah. Ni pahala ambapo Waislamu (wanaume) hukutana kila siku ili kuitekeleza nguzo ya pili ya Dini ya Kiislamu. Ni pahala ambapo elimu na busara vinatolewa na kugawanywa kutoka humo. Ni pahala ambapo Waislamu hupokea ujumbe wa wiki (khutbah za Ijumaa), kuhusiana na wajibu wao kwa Allaah, kwao wao wenyewe, kwa familia zao, na kwa viumbe wengine waliobakia.



Nyumba za Allaah zina sifa tulizotaja hapo juu na nyingine nyingi. Kwa msingi huo basi, tumeona ipo haja ya kujikumbusha, sisi wenyewe, na ndugu zetu wengine katika Uislam, juu ya baadhi ya adabu na kanuni zinazohusiana na kuhudhuria (kukaa) katika Msikiti (Masjid). Yafaa kuzingatia kuwa, hizi ni nyumba za Allaah, na pamoja na kuwa Yeye (Azza wa Jalla) yuko juu (kwamba hawezi kuishi ndani yake), kiuhalisia, zimejengwa kwa lengo maalumu la kumuabudia Yeye, na kwa hiyo, zinapaswa kuheshimiwa na kuadhimishwa na wale wanaohudhuria (katika Misikiti hiyo).



Kwa kuzingatia lengo hili, tumekusanya Makala hii fupi, inayohusiana na adabu za kuhudhuria nyumba za Allaah. Tunaomba na ni matarajio yetu kuwa kazi hii itainufaisha jamii ya Kiislamu na itabakia kuwa ukumbusho kwa wale ambao inawezekana wamesahau utukufu wa Msikiti.[1]





Faida Na Umuhimu Wa Msikiti (Nyumba Ya Allaah)



Nyumba za Allaah zina faida na Baraka ambazo hazipatikani katika jengo lingine lolote juu ya uso wa Dunia. Faida na Baraka hizi ni nyingi sana, na si tu kuwa zinapatikana kwa kuingia Msikitini, bali hata kabla ya mtu kuingia, kama ameweka niyyah ya kwenda Msikitini, anaanza kuchuma Baraka (hizo) punde tu anapotoka nyumbani kwake. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



“Atakayetoka (atakayekwenda) Msikitini, Allaah Atamuandalia sehemu (makazi) katika pepo, kila mara aendapo Msikitini.” [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].



Amesema pia:



“Yeyote mwenye kuchukua wudhuu nyumbani kwake, kisha akatoka kuelekea Msikitini kwa niyyah ya kutekeleza Swalah ya faradhi, hatua zake zitakuwa njia ya yeye kufutiwa madhambi. Hatua moja itafuta dhambi moja, ilhali hatua nyingine (itakuwa sababu ya yeye kuongezewa) thawabu.” [Swahiyh Muslim].



Pia ilitokea katika kipindi cha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kuwa:



“Mtu mmoja alikuwa akiishi mbali (na Msikiti), lakini alikuwa akijitahidi sana kuhudhuria Swalah za jamaa’ah katika Msikiti. Baadhi ya watu wakamshauri: “Kwa nini usinunue punda ili uwe unampanda (wakati wa kwenda Msikitini), hasa nyakati za usiku na (kunapokuwa na) joto kali? Akajibu: Sitaki kufanya hivyo. Ninatumai kuwa hatua zangu (ninazotembea) kuja Msikitini zinaandikwa (kama matendo mema), na pia hatua zangu wakati ninaporudi kwa familia yangu (baada ya Swalah) zinaandikwa (kama matendo mema). Baada ya kusikia haya, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Allaah Ameyaandika yote mawili kwa ajili yako.” [Swahiyh Muslim].



Ama kuhusiana na faida zinazopatikana baada ya kuingia Msikitini, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



“Malaika huendelea kumuombea mtu ambaye anabakia katika Msikiti alioswalia, muda wa kuwa hajatokwa na upepo(kutenguka wudhuu). Malaika husema: Ee Allaah msamehe (mja) huyu! Ee Allaah mrehemu (mja) huyu.” [Swahiyh Al-Bukhaariy].



Umuhimu wa Msikiti unajulikana pia kwa makafiri. Kama mtu atafuatilia kiundani historia ya vita baina ya Waislamu na wakatoliki, atagundua kuwa, hata mpaka leo hii, pindi makafiri wanapotaka kuvamia au kupigana na nchi ya Waislamu, moja ya maeneo ya mwanzo kushambuliwa (kuharibiwa) ni Msikiti. Hii ni kwa sababu makafiri wanautambua umuhimu wa Misikiti katika kuiunganisha na kuifundisha jamii ya kiislamu.





Kabla Ya Kuingia Msikitini





1. Muislamu anapaswa kutambua kuwa lengo kuu la Misikiti ni kwa ajili ya kuabudiwa Allaah (ndani yake). Kwa kuzingatia hili, inafaa kwa mtu kuweka niyyah sahihi kabla ya kuingia katika nyumba hii ya ‘ibaadah.



Allaah (Azza wa Jalla) amesema katika Qur-aan kuhusiana na Misikiti:





فِي بُيُوتٍ أَذِنَ اللَّـهُ أَن تُرْفَعَ وَيُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ يُسَبِّحُ لَهُ فِيهَا بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ



Katika nyumba ambazo Allaah Ameidhinisha litukuzwe na litajwe humo Jina Lake; wanamsabihi humo asubuhi na jioni. [An-Nuwr: 36].



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuhusiana na Misikiti:



"Kwa hakika nyumba za Allaah zimejengwa kwa ajili ya kumkumbuka (kumtaja) Allaah, kuswalia, na kusomea Qur-aan." [Swahiyh Muslim].





Kwa hiyo ni wajibu kwa Muislamu kutambua kuwa lengo la Misikiti si kwa ajili ya mikusanyiko ya kijamii na mazungumzo (yasiyohusiana na Msikiti), bali ni eneo lililoteuliwa na Allaah (Azza wa Jalla) kwa ajili ya kuabudiwa Yeye, kutajwa jina Lake, na kusomwa kitabu Chake. Mtu anyeingia Msikitini na akatoka, anatakiwa kujihisi ongezeko hasa la kiimani. Baada ya kuondoka Msikitini, kiwango chake cha imani na taqwa (Uchaji Allaah) kinatakiwa kuwa juu kuliko mwanzoni alipoingia Msikitini. Allaah (Azza wa Jalla) Amesema katika Kitabu Chake kitukufu:



إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ



Hakika Swalaah inazuia machafu na munkari. [Al-‘Ankabuwt: 45].



2. Ni lazima kwa mtu anayetaka kwenda Msikitini kuhakikisha kuwa hana (hatoi) harufu mbaya. Hii ni kutokana na kauli ya Allaah katika Qur-aan:



يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ



“Enyi wana-Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila Masjid (mnapokwenda Misikitini kwa ajili ya ‘ibaadah)” [Al-A‘raaf: 31].





Pia, maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



"Yeyote aliyekula vitunguu vyeupe (vitunguu thaumu) au vitunguu vya kawaida (vitunguu maji) asihudhurie Msikitini." [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].





Ushahidi tulioutoa hapo juu unatudhihirishia kuwa ni wajibu kwa Muislamu kuhakikisha kuwa hatowaudhi watu wengine kutokana na harufu (mbaya) ya mwili (wake) anapohudhuria Msikitini, na kwa hiyo, anapaswa kujitahidi kadiri awezavyo kujisafisha kabla ya kuhudhuria Swalah katika nyumba ya Allaah. Wanachuoni wa Kiislamu wanasisitiza juu ya katazo hilo tulilolitaja na kwamba linaenea zaidi pia kwa uvutaji sigara, kutokana na harufu mbaya ya sigara anayobaki nayo mvuta sigara mara tu amalizapo kuvuta sigara. Harufu hii (ya sigara), bila shaka, ina madhara na huwasumbua wanaoswali katika Msikiti, na pia huwasumbua (huwaumiza) Malaika. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:





“Kwa hakika Malaika huumia kwa kile ambacho huwaumiza bin Aadam.” [Swahiyh Muslim].





3. Wakati wa kwenda Msikitini, haifai kwa mtu kuharakisha na kukimbia, bali aende kwa mwendo wa kawaida. Hii ni kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



“Utakaposikia adhana (mwito wa Swalah) utembee kuelekea Msikitini katika hali ya utulivu, kwa amani, na usiharakishe. Utakachodiriki (katika Swalah), basi swali, na kile ambacho utakikosa, kimalizie.” [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].





Wakati Wa Kuingia Msikitini





Ukiingia Msikitini anapaswa kuzingatia taratibu (adabu) zifuatazo:





i. Kutanguliza Mguu Wa Kulia Kwanza



Swahaba maarufu wa Nabiy, Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema:



“Ni katika Sunnah, kuwa mtu anapoingia Msikitini basi atangulize mguu wake wa kulia, na (anapotoka), atoke kwa kutanguliza mguu wake wa kushoto.” [Mustadrak Al-Haakim].





Na imenukuliwa pia, kuwa ‘Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alikuwa na mtazamo huo huo. [Swahiyh Al-Bukhaariy].





ii. Du’aa (Ya Kusoma) Unapoingia Msikitini





Hii inapatikana katika Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



“Mmoja wenu anapoingia Msikitini, basi aseme: Allaahumma iftah liy ab-waaba rahmatik (Ee Rabb! Nifungulie milango ya Rahmah Zako).” [Swahiyh Muslim]



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema pia:



“Atakapoingia mmoja wenu Msikitini, aniswalie mimi, na kisha aseme: Allaahumma iftah liy abwaaba rahmatik (Ee Allaah, nifungulie mimi milango ya Rahmah Zako).” [Sunan Abi Daawuwd].





iii. Kuswali Rakaa 2 Kabla Ya Kukaa (Tahiyyatul Masjid)





Uthibitisho wa haya nimaneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):





“Mmoja wenu atakapoingia Msikitini, aswali rakaa mbili kabla ya kukaa.” [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].





iv. Kuswali Nyuma Ya Sutrah (Kizuizi)



Sutra ni kizuizi kinachomsaidia mtu anayeswali kutomruhusu mtu mwingine kupita mbele yake. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



“Mmoja wenu anaposwali, basi asimame nyuma ya sutrah na aswali karibu na hiyo sutrah. Hii ni kwa ajili ya kumzuia shaytwaan asimsumbue katika Swalah yake.” [Sunan Abi Daawuwd].







v. Mtu Ajitahidi Kadiri Awezavyo Kupata Nafasi Katika Safu Ya Kwanza[2]





Hii ni kutokana na maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



“Lau watu wangelijua malipo makubwa yapatikanayo kwa kuitikia mwito wa Swalah (adhana), na kuswali katika swafu ya kwanza, basi wangeshindania kupata nafasi katika swafu ya kwanza.” [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].



Amesema pia:



“Bora ya swafu kwa wanaume ni swafu ya kwanza.” [Swahiyh Muslim].



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipata kuwaona baadhi ya Swahaba zake wakiwa wamekaa (swafu) ya nyuma ya Msikiti punde tu, kabla ya kuanza kwa Swalah. Alipoona hivyo, alisema:



“Watajivuta na kujichelewesha (kuendea swafu ya kwanza) mpaka Allaah Atawachelewesha (kuingia peponi).”[3] [Swahiyh Muslim].





vi. Kurudia (Maneno) Baada Ya Muadhini



Hii ni kutokana na maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



“Utakapoisikia adhana, sema kama asemavyo Muadhini.” [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].





vii. Du’aa Baina Ya Adhana (Mwito Wa Swalah) Na Iqaamah



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameujulisha ummah wake nyakati tofauti ambazo du’aa zina uwezekano mkubwa wa kukubaliwa na Allaah. Moja ya nyakati hizo ni baina ya adhana na iqaamah. Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



“Du’aa inayoombwa baina ya adhana na iqaamah haitokataliwa.” [Musnad Imaam Ahmad].





viii. Kusoma Qur-aan Na Kumtaja Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)



Tumeshaonesha awali katika Makala hii, maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa:





“Kwa hakika nyumba za Allaah zimejengwa kwa ajili ya kumtaja Allaah, Swalah, na kusomwa Qur-aan (ndani yake).” [Swahiyh Muslim].





ix. Kujitahidi Kuhudhuria Mikusanyiko Ya Kielimu (Duruus Za Misikitini)





Haya ni kutokana na maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:



“Hakikusanyiki kikundi cha watu katika nyumba ya Allaah, wakisoma Kitabu Chake na kufundishana wenyewe kwa wenyewe isipokuwa utulivu hushuka juu yao, Malaika huwazunguka, Rahmah huwateremkia, na Allaah Huwataja katika mjumuiko Wake (mbele ya Malaika).” [Swahiyh Muslim].



Pia maelezo ya ujumla ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kuwa:



“Yeyote mwenye kuifuata njia (kwa ajili ya) kutafuta elimu, Allaah Atamfanyia wepesi njia yake kuelekea peponi.” [Swahiyh Muslim].



Kutokana na Hadiyth hiyo hapo juu, ni sawa kusema kuwa, ikiwa mtu ataondoka nyumbani kwake akiwa na niyyah ya kuswali (Swalah kwa) Jamaa’ah na pia akiwa na niyyah ya kutafuta elimu Msikitini, kwa kupenda Kwake Allaah, atapata malipo makubwa sana kutokana na ukweli kuwa amekusanya mambo (matendo) mawili makubwa Ayapendayo Allaah (Azza wa Jalla).





x. Ni Wajibu Kwa Misikiti Kuwa Misafi, Na Muumini Anatakiwa Ajitahidi Kadiri Awezavyo Kusaidia Hili





Hii ni kutokana na maneno ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) aliyesema kuwa, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliagiza kuwa Misikiti inapaswa kusafishwa na kufukizwa (manukato mazuri). [Musnad Imaam Ahmad].





Mambo Ya Kuepuka Wakati Wa Kutembelea Masjid (Misikiti)



Matendo ya Muumini wakati anapotembelea nyumba za Allaah yanatakiwa kuwa tofauti na matendo yake ya kawaida nje ya Misikiti. Hii ni kutokana na uelewa wake juu ya utukufu wa nyumba hizi (Misikiti). (Mja) Huzingatia mara zote kuwa, anatembelea sehemu ambayo imewekwa kwa ajili ya kumuabudu Allaah, na kwa hiyo, kila kinachofanyika ndani yake kinatakiwa kimuwezeshe mja kuwa karibu zaidi na Allaah.



Baada ya hayo, matendo yafuatayo yamekatazwa (ni haraam kufanyika Misikitini)





a. Kununua Na Kuuza Ndani Ya Msikiti[4]



Haya yametajwa katika kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



“Ukimuona mtu akinunua au akitafuta kununua ndani ya Msikiti, sema kumwambia: ‘(Namuomba) Allaah asiibariki biashara yako’.” [Swahiyh Muslim].





b. Kuongea Kwa Sauti Kubwa Au Kuongelea Masuala Yasiyo Na Umuhimu (Misikitini)[5]



Sa’iib bin Yaziyd amesema: “Nilikuwa nimesimama Msikitini siku moja niliposikia mtu akinishika. Nilipogeuka nikamuona kuwa alikuwa ni ‘Umar bin Al-Khatwaab. Alinielekeza nimpelekee watu wawili waliokuwa wamekaa Msikitini wakiongea kwa sauti kubwa. Nilipompelekea watu wale wawili, ‘Umar akawauliza: Mnatokea wapi? Wakajibu: Tunatokea Twaaif. ‘Umar akasema: Mngekuwa mnatokea katika mji huu, ningewapiga. Mlikuwa mnanyanyua sauti zenu (sana) katika Msikiti wa Nabiy!” [Swahiyh Al-Bukhaariy].



Sa’iyd bin Musayyib amesema:



“Pindi mtu anapokaa Msikitini, kwa hakika anakaa kwa ajili ya kumuabudu Rabb wake, kwa hiyo, aongee tu kwa lile ambalo ni jema.” [Tafsiyr Al-Qurtwubiy].



Yafaa pia kuwakumbusha wale ambao huenda na watoto katika nyumba za Allaah kuwa, wanawajibika kuwasimamia watoto wao na kuhakikisha kuwa tabia zao (watoto) haziwasumbui watu wengine wafanyao ‘ibaadah. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Kila mmoja wenu ni mchunga, na kila mmoja mmoja ataulizwa kuhusiana na wale walio chini ya uangalizi wake.” [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim]



Ingawa Hadiyth hii ina maana ya ujumla, bila shaka, inatumika pia kwa wale ambao wanakwenda na watoto katika nyumba za Allaah. Mzazi (Mlezi) anatakiwa kuwafundisha wale walio chini yake, tabia (taratibu) njema za kutembelea nyumba ya ‘ibaadah. Asimruhusu mtoto wake kukimbia kimbia ovyo Msikitini (hali itakayopelekea) kuwasumbua wengine wenye kujikurubisha kwa Allaah. Kama mtoto ni mdogo sana na hawezi kuzielewa taratibu hizi (za kukaa Msikitini), basi ni bora kumuacha nyumbani kuliko kuwabughudhi wengine walioko Msikitni.





c. Kusoma Qur-aan Kwa Sauti Kiasi Ambacho Inawasumbua Wengine Wanaofanya ‘Ibaadah



Abu Sa’iyd Al-Khudriyy ameripoti kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwasikia baadhi ya watu wakisoma Qur-aan kwa sauti kubwa (wakiwa) Msikitini, kwa hili akawaambia:



“Kila mmoja wenu anakusudia kumuomba Rabb wake, kwa hiyo msikwazane, wala msinyanyue sana sauti zenu mnaposoma (Qur-aan)” [Sunan Abi Daawuwd].



Katika Hadiyth hii kuna katazo la wazi kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya kuwabughudhi wengine Msikitini, sasa vipi kwa wale wanaowabughudhi wengine kwa mazungumzo yasiyo na maana (porojo), miziki kwenye simu zao za mkononi (rununu), vicheko na utani (mizaha), na kadhalika?! Hapana shaka kuwa kusoma Qur-aan ni moja katika matendo yenye kupendeza mbele ya Allaah, lakini pamoja hadhi yake kubwa katika Uislam, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mtu kuisoma kwa sauti ambayo itawabughudhi wengine wenye kufanya ‘ibaadah zao. Hii inatubainishia kuwa wale ambao huwabughudhi wengine kwa mambo (masuala) yenye hadhi ya chini ya Qur-aan watakuwa wamefanya makosa makubwa.[6]





d. Kupita Mbele Ya Mtu Anayeswali[7]





Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



“Lau mtu anayepita mbele ya mtu anayeswali angelijua uzito wa kosa lake hilo, ingelikuwa bora kwake kusubiri arobaini kabla ya kupita mbele ya mtu anayeswali.” [Swahiyh Al-Bukhaariy na Swahiyh Muslim].





Kutoka Msikitini



I. Du’aa Ya Kusoma Wakati Wa Kutoka Msikitini



Hii ni kutokana na maneno ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



“Mmoja wenu anapotoka Msikitini aniswalie mimi na aseme: Allaahumma inniy as-aluka min fadhwlik. Ee Allaah! Ninakuomba fadhila Zako.” [Swahiyh Muslim].





II. Kuwa Unatoka (Unaondoka) Katika Nyumba Ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)



Tumerejea mara kwa mara katika Makala haya kuwa mtu anayeingia Msikitini alenge zaidi kujikurubisha kwa Rabb wake. Muda wote wa kuwa kwake Msikitini anapaswa awe ameswali, kuomba du’aa, kumtaja Allaah, na ikiwezekana awe amesikiliza kitu katika elimu ya Dini ambacho kitamnufaisha katika maisha haya na yajayo (Aakhirah). Kwa hiyo, tabia yake wakati wa kutoka katika nyumba ya Allaah inatakiwa (inatarajiwa) kuwa bora zaidi na tofauti (yenye mfano mzuri). Watangu wetu wema (Salafus-Swaalih) wametujulisha kuwa ishara ya kuwa ‘ibaadah ya mtu imekubaliwa na Allaah ni kuwa matendo ya mja baada ya kutekeleza ‘ibaadah (inakuwa) ni bora na yenye kupendeza zaidi. Kama aliyefanya ‘ibaadah hajihisi kuongezeka iymaan (baada ya kutekeleza ‘ibaadah), inawezekana kuwa hazifanyi ‘ibaadah zake katika utaratibu unaokubalika (unaofaa) kishari’ah, kwa hiyo ajitathmini matendo yake kabla na wakati wa kuitenda (kuitekeleza) ‘ibaadah.





Kwa Kumalizia



Hizi ni adabu (taratibu) chache tu za kuchunga ambazo tumehisi kuna haja ya kujikumbusha, sisi wenyewe na ndugu zetu, kwani zinahusiana na (taratibu na adabu za) kuhudhuria katika nyumba za Allaah.



Allaah ni mjuzi zaidi. Swalah na Salaam za Allaah ziende juu ya Rasuli na Nabiy Wake wa mwisho, na juu ya familia yake na Swahaba zake.




[1] Hadiyth nyingi zilizopo katika Makala hii zimechukuliwa kutoka katika kitabu: Riyaadh Asw-Swaalihiyn cha Imaam An-Nawawiy.

[2] Hii ni kwa wanaume na wanawake kama kutakuwa na kizuizi (kitenganishi) chenye kutenganisha wanaume na wanawake. Kama hakuna kitenganishi, wanawake wanatakiwa waswali swafu za nyuma zaidi (ndiyo bora kwao).

[3] Hii imetajwa kama makameo kwa wale ambao mara nyingi hujivuta kuiendea swafu za kwanza.

[4] Hili linajuilisha pia uwekaji wa matangazo ya biashara (kutangaza bidhaa na huduma) katika Misikiti.

[5] Hili halihusishi kunyanyua sauti wakati wa khutbah na madarasani.

[6] Kwa hakika inatuhuzunisha sana kusikia baadhi ya mambo yanayotokea ikiwemo kupigana, kuzozana, n ahata kutishana kwa silaha, katika baadhi ya Nyumba za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)!! Hili kwa hakika ni kos ana ni uhaini mkubwa na wale ambao huyafanya haya wanapaswa kutubia kwa Rabb wao na kumuomba msamaha.



[7] Hili linamjuilisha Imaam (anayeongoza Swalah), au mtu anayeswali peke yake. Halimhusu mtu anayewali nyuma ya Imaam (Sutra ya Imaam inatosheleza).
 
Assalaam alaikum ndugu zangu katika imani,naam sasa tutaanza kusoma Hadith zinazo husiana na Mambo Yasiyo Onekana



Screenshot_20250420_210035_ReadEra.jpg
 
MAJIBU YA CHEMSHA BONGO NAMBA 2

CHEMSHA BONGO NAMBA 2

1] Ni ipi sura ya mwisho kushuka katika Qur'an ?
- ANNASWR

2] Mtume swallallahu alaih wasallam katajwa mara ngapi katika qur'an?
- MARA 4


3] Khalifa gani aliamrisha msahafu uandikwe?
- ABUBAKARY SIDDIK

4] Khalifa gani aliagiza msahafu uandikwe kwa lahaja moja ya ki quraish?
- UTHAMNI IBN AFFAN


5] Qur'an ilikusanywa yote kwa sababu gani?
- WAISLAMU WENGI WALIKUWA WANAKUFA KWENYE VITA


6] Je qur'an iliposhushwa ilikuwa na harakaat zake (fatha,dhwamma,sakinah,kasra)?
- HAIKUSHUKA NA HARAKAAT YOYOTE

7] Je qur'an ilishuka na lahaja ngapi?
- SABA (7)
 
MASWALI NA MAJIBU


Maswali: Zinaa-Liwati
SWALI:




Mimi nina suala rafiki yangu kanituma nimuulizie suala lenyewe ni hili anasema yeye sasa hivi kashaolewa lakini katika utoto wake alifanya mambo mengi machafu ya kuwa na wanaume pamoja na kuzini nao, na na akawahi kuchukuwa mimba ya mwanamme wake mmoja kabla hajaolewa kwa bahati nzuri, akapata rizki ya mume na akaolewa lakini ile mimba alikuwa nayo bado baada ya wiki alikwenda kuitowa jee ndoa yake ina sihi ama vipi, hiyo mimba sio ya huyo mume alomuowa ni ya mtu mwengine lakini mumewe mpaka leo hajamwambia kuhusu kitu hicho, sasa kama nilivokwambia kuwa kashaolewa kakaaa na mumewe kwa muda kama wa mitano akakutana na bwana wake wa zamani kwa bahati mbaya akazini nae mara mbili, lakini mumewe hajui alikuwa ana wasi wasi mkubwa kuhusu suala hilo akamwambia kama kashawahi kumuendea kinyume ndani ya ndoa yake hamsamehe na tokea siku alomuendea kinyume si mke na mume wanazini tu na anaogopa kwa sababu mumewe anampenda mpaka leo jee ndoa anayo na afanye nini naomba jawabu





JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu zinaa kwa mwanamke aliyeolewa. Awali ya yote ni kuwa huyo rafiki yako amefanya madhambi kabla ya kuolewa na hata baada ya kuolewa. Kisha amemwendea kinyume mume ambaye anampenda sana kama ulivyoandika, ingawa hatudhani kuwa ni hivyo kwa sababu vipi ampende mumewe kisha amuendee kinyume?




Maasi hayo aliyoyafanya, inafaa yeye afanye yafuatayo ili apate kusamehewa na Allaah Aliyetukuka:




1. Kuacha maasiya.

2. Kujuta kwa kufanya kosa hilo.

3. Kuazimia kutorudia tena kosa hilo.

4. Na ikiwa kosa lenyewe linamhusu mwanaadamu ni lazima apate msamaha kutoka kwa aliyemfanyia.




Sharti moja likikosekana basi toba yake haikubaliwi. Kwa sababu hapa kosa alimfanyia mumewe inabidi apate msamaha kutoka kwake. Hata hivyo, suala hilo linakuwa ni shida kwani linaweza kutokea lolote endapo atataka kumweleza mumewe ukweli. Hivyo anachotakiwa kufanya ikiwa atachelea madhara kutoka kwa mumewe, inabidi awe ni mwenye kumtendea wema kila wakati ili Allaah Aliyetukuka Amtazame kwa jicho la huruma na kumsamehe.




Mwanzo inatakiwa mwanamke huyo apewe nasaha kuhusu aliyoyafanya na awe na nia ya kujirekebisha na kufanya mema kwa wingi sana kwani Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:




"Mche Allaah popote ulipo na fuatisha baya kwa zuri, nalo litafuta (hilo baya)" (at-Tirmidhiy).




Tunatumai kwa kufanya hivyo kwa ikhlaas na nia nzuri basi Allaah Aliyetukuka Atamsamehe na kumsaidia katika kubadili aliyo nayo.




Ama kuhusu ndoa yao ni sahihi wala mke hawi ameachwa kwa kufanya makosa kama hayo ya zinaa. Ndoa itakuwa ipo lakini mwanamke atakuwa amefanya madhambi makubwa na lau kutakuwa na sheria ya Kiislamu basi alikuwa auawe kwa kosa hilo. Tafadhali mpe majibu yafuatayo apate kuzingatia maasi makubwa hayo:




Nini Hukumu Ya Mwenye Kuzini Kwa Siri?




Kutoa Mimba - Hukmu Na Kafara Yake




Nimekwenda Nje Ya Ndoa, Nimjulishe Mume Wangu?










Na Allaah Anajua zaidi
 
Kutoa Mimba - Hukmu Na Kafara Yake
Maswali: Zinaa-Liwati


SWALI:

Asalama aleykum, kwaunza tu napenda unipatie jawabu
la suwala langu inshaalla kama utakavoweza suala nini hukumu ya mwanamke ambae katowa mimba kabla mimba hiyo haijapulizwa roho? na nini kafara yake?




JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho


Kutoa mimba ikiwa ni kabla ya kupuliziwa roho au baada ya kupuliziwa roho kisheria ni haraam. Wakati unaokubalika kutoa mimba ni pale tu itakapokuwa kuna dharura za kisheria ndipo panaweza kukubalika tena kwa masharti yake.


Dharura hizo, ni kama kumehakikishika kuwa kuna uwezekana wa mama kufariki kwa kuwa na kiumbe hicho, au kuendelea kwake kuwa na mimba hiyo kutamletea mauti. Na isitoshe kukubalika huko, bali kumetakiwa uthibitisho huo utolewe na daktari mwenye kuaminika kabisa. Na muhimu kwanza atafutwe daktari Muislamu mwenye kuaminika, ikishindikana, basi daktari yeyote ambaye ni muaminifu sana.


Ama kuitoa mimba tu kwa sababu ya kutotaka mtoto, au kukhofia riziki yake, au malezi yake, au kuchelea gharama za maisha kama kumsomesha, kumvisha, au kumlisha n.k. hayo yote hayaruhusiwi kisheria kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

“Wala msiwaue wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi Tunawaruzuku wao na nyinyi. Hakika kuwaua hao ni khatia kubwa” [Al-Israa: 31]

“Wala msiwaue watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi Tunakuruzukuni nyinyi na wao” [Al-An'aam: 151]



Ingawa kuna baadhi ya Maulamaa wanaonelea kuwa inafaa kutoa mimba katika siku za arobaini za mwanzo, lakini iliyo sahihi zaidi ni kutokufaa kutoa katika hali zote ila kwa dharura kubwa kabisa inayokubalika katika sheria.

Ama katika hatua ya pili ya siku arobaini nyingine ambayo ni 'alaqah (kipande cha damu), au hatua ya tatu ya siku arobaini nyingine ambayo inajulikana kama ni 'mudhwgah' (kipande cha nyama), haitoruhusiwa kutolewa hiyo mimba hadi jopo la madaktari wenye kuaminika wathibitishe kuwa kweli kuendelea kuwepo mimba hiyo kutasababisha mama kufariki au ikiwa kumeonekana na kujulikana kuwa kiumbe (kijusi) hicho kimeshakufa tumboni ndipo katika hali hiyo kutaruhusika kutolewa baada ya kila njia kutumika kuondosha hatari hiyo kufeli.

Baada ya hatua hiyo ya tatu, na kufika miezi minne (siku mia na ishirini, yaani arobaini tatu) ambapo ndio roho itakuwa ishapuliziwa hicho kiumbe, hapo patakuwa haparuhusiki kabisa na ni madhambi makubwa kabisa ila kwa dharura kuu kabisa kama ilivyotajwa hapo nyuma, na tena kuwe kumefanyika juhudi kubwa za kuokoa hali sababishi (chenye kusababisha) na kwa hali hiyo kutakuwa kumetumika maslahi ya 'unafuu kati ya madhara mawili'. Na unafuu hapo ni uhai wa mama ambao ndio bora zaidi na wa msingi zaidi kuliko wa huyo kiumbe. Kwa sababu mama tayari kamili na anaishi na kuwepo kwake bado kuna matumaini ya kupatikana vizazi vingine, pia ni mwenye majukumu na wajibu katika maisha, na msimamizi wa nyumba, mlezi, n.k., hali hicho kiumbe kilichopo tumboni, hakina uhakika wa kuishi hadi kitakapozaliwa na haijulikani kama kitakapozaliwa kitakuwa hai au la, na pia kisicho na majukumu yoyote kwa wakati huo. Kwa hali hiyo, kati ya kulinda na kuokoa hali moja kati ya mbili, basi kumuokoa na kumlinda mama ni bora zaidi kuliko kile kilichoko tumboni.

Hali hiyo uliyoieleza, inaonyesha hakukuwa na dharura hiyo, na hivyo huyo mwanamke katenda kitendo kiovu ambacho sheria haikikubali kabisa. Tendo hilo la dhambi, linahitaji toba kwa mtendaji; toba ya dhati kabisa.

Ama kafara ya kitendo hicho, wametofautiana Maulamaa wakati wake na hata aina ya kafara yenyewe. Baada ya kutazama pande zote, lililo lenye nguvu ni kuwa, kabla ya kupuliziwa roho kiumbe (kijusi), hakulazimiki kutoa kafara (fidia), pamoja na kuwa kuna wanaoona kuwa inapaswa kutolewa. Lakini aliyefanya kitendo hicho anatakiwa atubu toba ya kweli na azidishe kufanya 'amali nyingi za kheri na kutoa sadaka sana kulipa maovu yake, kwani mema hufuta maovu.


Ama baada ya kupuliziwa roho, hakuna tofauti kukubaliwa kwake kuwepo na kafara au kutolewa fidia 'Diyah' (blood money). Baadhi ya Maulamaa wamesema kuwa kunatolewa fidia ya pesa kwa wale wenye kuhusiana na kiumbe hicho kwa kiasi cha gramu 213 za dhahabu, na wanalipwa wale wanaomrithi kile kiumbe (yaani kaka, dada au babu, bibi n.k. kulingana na sheria ya Mirathi), hatopewa yule aliyeshiriki kukitoa (kukiua) japo anaweza kumrithi. Na ikiwa wanaomrithi wakasamehe basi hakuna malipo. Kisha anatakiwa aache huru mtumwa (ikiwa inawezekana hilo), ikiwa haiwezekani au hakuna hali hiyo, basi anatakiwa afunge miezi miwili mfululizo ambayo ni kafara kwa ajili kuua.

Kama Asemavyo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):

“Na haiwi Muumini kumuua Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuua Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipokuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hekima” [An-Nisaa: 92]

Hivyo, utaratibu wa kufanya kwa yule aliyetoa mimba baada ya siku mia na ishirini (miezi minne) yaani baada ya kupuliziwa roho, ni huu:

Kufanya toba ya kweli, na milango ya toba iko wazi hadi wakati karibu jua litakapochomoza upande wa magharibi (kabla halijachomoza), au wakati wa gharghar (roho itakapokuwa imefika kooni wakati wa kutolewa ‘mkoromo wa mauti’). Na masharti ya toba ni haya yafuatayo:
Kulipa fidia 'Diyah' (blood money);
Kafara kwa kukiua kiumbe, nayo ni kuacha huru mtumwa, au kufunga miezi miwili mfululizo.
Pia kutoa mimba kwa sababu imetokana na kitendo cha zinaa, ni jambo lisilokubalika kabisa. Kiumbe hakina makosa na tunajua kuwa habebi kiumbe madhambi ya mwengine. Allaah Anasema:

"Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine" [Al-An’aam: 164]

Na Amesema tena:

Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine.)) [Faatwir 35:18]

Pia tukitazama kisa cha mwanamke wa ki-Ghaamidy aliyezini na akaenda kwa Mtue kutaka apewe adhabu ya mzinifu, na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamtaka aende hadi atakapozaa, na kasha akamrudisha tena hadi amnyonyeshe huyo mtoto na kisha mtoto alipokuwa mkubwa ndipo akatekeleza adhabu kwake. (Swahiyh Muslim). Tukio hilo linatuonyesha kuwa mtoto japo wa kitendo cha zinaa hairuhusiwi kabisa kuuliwa anapokuwa tumboni.

Na tufahamu kuwa kila kiumbe kinachozaliwa kinakuwa ni Muislam, na huenda huyo mtoto wa tendo la zinaa akawa Muislam bora sana kuliko wengi. Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aallihi wa sallam) anasema: "Kila mtoto anazaliwa katika hali ya fitwrah (maumbile ya asli; Uislam)..." imepokewa na al-Bukhaariy

Vilevile mwanamke ambaye amebakwa, haruhusiwi kutoa mimba yake kwa kauli yenye nguvu, ingawa baadhi ya Maulamaa wanasema anaweza kutoa katika siku zile arobaini za mwanzo ikiwa kuwa kwake na hiyo mimba kutamsababishia madhara katika jamii yake au kwa watu wake ima kwa kumtenga, kumsusa au hata kumuua kwa kigezo cha ‘kulinda hadhi’ ya familia au ukoo. Lakini, pamoja na sababu hizo, utakuta hazitoshi kuhalalisha kutoa mimba kwani kufanya hivyo, ni kutenda dhambi nyingine na inajulikana kuwa hicho kilichopo tumboni hakihusiki kwa njia moja au nyingine na jarima ile ya kubakwa mwanamke huyo, na maadam haikuwa ridhaa ya mwanamke kufanywa hivyo na alijitahidi kupambana na mbakaji/wabakaji akazidiwa, ni wajibu wake kukihifadhi hicho kiumbe na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Atakilinda na kukijaalia kuwa ni chema na poza kwa mama yake. Na ikiwa mwanamke huyo hajaolewa, basi ni jambo jema kwa wanaume wa Kiislam kumsitiri na kumsaidia kumtoa katika mitihani hiyo iliyomkumba. Ama kama ana mume, basi mume wake ajitahidi japo ni vigumu sana, kusubiri na kukikubali kiumbe hicho ambacho hakina hatia yoyote ile. Na malipo makubwa yanawasubiri watu aina hiyo.

Wa Allaahu A’alam
 
Mwenye Kuzini Kwa Siri Nini Hukmu Yake?
Maswali: Zinaa-Liwati




SWALI:

Assalam aleykum, nawashukuru kwa kutuelimisha Allah (S.W.T) atawalipa Inshaalah je nini hukmu ya mtu aneyezini lakini ikawa anafanya siri.






JIBU:


Sifa zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), ahli zake, Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka siku ya Mwisho

Kwanza tunapenda na sisi kutoa shukurani kwa du'aa zenu nzuri mnazotuombea nyote mnaotuma maswali yenu pamoja na wengineo wanaoingia ALHIDAAYA kutafuta faida mbali mbali. Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atutakabalie hizo du'aa na Atuzidishie uwezo wa kuelemishana kwa kadiri Anavyotujaalia. Aamiyn

Hukumu ya zinaa ikiwa ni kwa siri au ni dhahiri adhabu yake ni mijeledi 100 ikiwa mwanamke au mwanamume hajaolewa na ikiwa ameoa au ameolewa basi adhabu yake ni kupigwa mawe mpaka kufa. Mara nyingi sisi kama wanadamu na hasa kama waislamu tunakosa hisia kwa kuona kuwa tukifanya dhambi kwa siri basi huwa hakuna dhambi wala adhabu.

Sisi kwa siri hiyo tunaweza kukwepa adhabu ya hapa duniani lakini tujue ya kwamba adhabu ya Akhera inaumiza zaidi. Allah Anasema:

((كَذَلِكَ الْعَذَابُ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ))

((Namna hivi inakuwa adhabu (Ya Mola duniani) Na adhabu Akhera ni kubwa zaidi, laiti wangalijua!)) [Al-Qalam:33]



Haya yetu ya kufanya madhambi kwa siri ni kukosa kwetu Ihsaan, kwani Mtume wa Allah amesema: “Ni kumuabudu Allah kama kwamba unamuona, kwani ikiwa humuoni basi Yeye Anakuona” (Muslim, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy na Abu Daawuud kutoka kwa ‘Umar ibn al-Khatwtwaab).

Na Mtume ametuusia kuwa tumche Allah popote pale tulipo na tukifanya baya basi tufuatishe kwa zuri, litafuta hilo baya

عن أبي ذَرٍّ جُنْدُب بِن جُنَادَة، وأبي عبد الرحمن مُعَاذ بِن جَبَلٍ رضي الله عنهما، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((اتَّقِ اللهَ حَيْثُما كنْتَ، وأَتْبِعِ السَّيئةَ الحسنةَ تَمْحُها، وخالقِ الناسَ بخُلُقٍ حسنٍ)). رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ، وَفِي بَعْضِ النُّسَخِ: حَسَنٌ صَحِيحٌ.

Kutoka kwa Abu Dharr Jundub Ibn Junaada na Abu 'Abdur- Rahmaan Mu'aAdh Ibn Jabal رضي الله عنهما ambao wamemsikia Mtume صلى الله عليه وسلم akisema: ((Mche Allaah popote pale ulipo na fuatisha kitendo kibaya kwa kitendo kizuri kitafuta (kitendo kibaya) na ishi na watu kwa uzuri)) [Imesimuliwa na At-Tirmidhi na kasema kuwa ni hadithi Hasan na katika maandiko mengine imesemwa kuwa ni Hasan Sahihi]

Hii ni nasaha mzuri hivyo tunawausia ndugu na dada zetu sote kwa pamoja tumche Allah kwani mafanikio yetu hapa duniani na kesho Akhera ni kuwa katika msimamo huo.

Ikiwa tumefanya jambo baya, la makosa hiyo ni katika udhaifu wetu, binadamu. Hivyo, tuombe toba na tufanye mambo mema. Na tunamuomba Allah Atuepushe kufanya madhambi kwa siri au dhahiri.



Na Allaah Anajua zaidi.
 
Back
Top Bottom