Ramadhan Special Thread
Wasio waislamu huwa wanatucheka ndoa ya kiislamu mahari rahisi na bla bla kibao,hawajui ni kwanini imefanywa hivyo?

Wao hawana mambo halali na haramu ndio maana hawatuelewi

Tena Nabii swallallahu alaih wasallam anasema hakika ndoa yenye mahari ndogo ndio yenye baraka

Kwahiyo unaweza ona madhara ya kuzaa nje ya ndoa ni makubwa sana,ndio maana ndoa imerahisishwa ili tusiwe na ugumu wa kufunga ndoa na kuishi katika njia anayo ridhia Allah

Tumche Allah
 
Maswali: Zinaa-Liwati
SWALI:




Assalam alaykum warahmatullahi wabarakat ama baada ya salam nakutakieni ramadhan maqbul. Kwa muislam alielawitiwa kwa kutezwa nguvu ni kweli hatoonana na MTUME (SAW). Na jee ni ipi hukumu yake.




JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta'ala) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Mtume. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea au kivivu. Pia hiyo ni ibada, na ibada inatakiwa ifanywe kwa namna iliyofundishwa na haifai kugeuza, kuongeza au kupunguza. Hali kadhalika Maswahaba walikuwa wakiandikiana barua na hakuna aliyekuwa akikatisha Salaam, wala kufupisha kumswalia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kufupisha kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwenye barua zao. Tuige na tufuate nyendo zao tusalimike.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu kulawitiwa kwa nguvu.

Hakika ni kuwa si kweli kuwa mwenye kutenzwa kwa nguvu kufanya liwati au dhambi jingine lolote kuwa hatopata radhi za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Amesema yafuatayo kuhusu kutenzwa nguvu:




“Anayemkataa Allaah baada ya kuamini kwake - isipokuwa aliyelazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani” (16: 106).







Ama Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuwa kalamu imenyanyuliwa kwa mtoto mpaka abaleghe, aliyelala mpaka aamke na aliyelazimishwa.




Kwa hivyo, aliyeliwatiwa kwa nguvu bila kutaka hatokuwa na makosa wala madhambi bali madhambi yatakuwa kwa aliyetenda hicho kitendo.







Kuhusu hokum ya uliwati pata maelezo katika viungo vifuatavyo:







08 Kuharamishwa Liwati







Mwenye Kufanya Maasi Ya Liwati Anaweza Kurudi Kwa Allah Kutubia?




Mume Wangu Ananitaka Njia Isiyo Ya Halali










Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Zinaa-Liwati
SWALI:

Asalamu aleikum warahmatullahi wabarakatu.

kwanza kabisa mimi nimeolewa nina miaka 16, lakini kwenye ndoa yangu nina matatizo na mume wangu na ni kuhusu ya kwamba huwa ana tabia ya kutaka kuniingilia sehemu ambayo haijahalalishwa kidini na ni haraam na kila ninapojaribu kumueleza hayo anaapa na kusema kuwa hatorudia lakini hakuna faida ana rudia haya daima sasa sijui nifanyeje. Naomba munipe nasiha itakayo nifaa mpaka Kesho Akhera.

Asalamu aleiykum.




JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), ahli zake, Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka siku ya Mwisho.

Haya ni baadhi ya matatizo ambayo dada zetu wanakumbana nayo katika unyumba. Hili tatizo hutokea kwa sababu ya malezi kwa mwanamme au mwanamke na pia kutofundishwa wajibu wa kisheria kwa wote wawili. Hivyo mume mara nyingi anakuwa hajui wajibu wake na haki yake katika ndoa na vile vile mwanamke. Hii hupelekea mmoja wao kuangukia katika haramu au kutotekeleza wajibu wake. Mara nyingi haya matatizo hutokea kwa sababu wazazi hawakuchunguza kwa kina kabla harusi.

Kumuingilia mwanamke kwa njia ya nyuma ni haramu, bali amuingilie katika njia iliyohalalishwa kama ilivyo katika kauli ya Allaah سبحانه وتعالى:

((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ وَقَدِّمُواْ لأَنفُسِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَاعْلَمُواْ أَنَّكُم مُّلاَقُوهُ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ))


((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Allaah , na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana Naye. Na wape bishara njema Waumini)) [2:223]

Kama tunavyoona katika hiyo aayah, Mwenyeezi Mungu katolea mfano shamba akionyesha kuwa ni mahali panapolimwa, na penye kulimwa panawezwa kulimwa kwa njia nyingi ingawa lengo ni kutatarajiwa kutoa mazao, na makusudio hapa kwa mwanamke, ni pahali anapoingiliwa mwanamke ambapo ni sehemu anayozaliwa mtoto. Kwa hiyo mtu kapewa ruhusa ya kumuingilia mkewe kwa mitindo mbalimbali lakini kwa sharti pawe sehemu ya mbele ambayo ndiyo inayotoa mazao ambayo ni mtoto. Na kumuingia mke kwa njia ya nyuma kunakwenda kinyume na fitrah (asili ya maumbile ya binaadamu). Vile vile mwanamke atakuwa amedhulumika kwa kupata sehemu yake ya kustarehe na mumewe na sehemu ya nyuma ni sehemu inayotoa uchafu na pia kitendo ni kitendo ambacho kimeharamishwa na Mola Mtukufu.

Kwa jinsi kitendo hichi kilivyokuwa ni kiovu kabisa, tunaona dalili ya kuharamishwa kwake kutoka katika Qur-aan na pia kuna dalili nyingi katika Hadiyth zifuatazo za Mtume صلى الله عليه وآله وسلم za kuharamishwa ambazo zina MAONYO MAKALI kabisa. Hivyo inampasa Muislamu ajiepushe kabisa nacho kitendo hicho ili aepukane na laana, adhabu na ghadhabu za Allaah سبحانه وتعالى :

Hadiyth ya kwanza: Haramu kitendo hiki:

عن خزيمة بن ثابت رضيَ اللَّهُ عنهُ انه قال: قالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((إِتْيَانُ النسَاءِ فِي أَدْبَارِهِنَّ حَرَامٌ)) الألباني في السلسلة الصحيحة

Imetoka kwa Khuzaymah bin Thaabit رضيَ اللَّهُ ambaye amesema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((Kuwaingilia wanawake kwa nyuma ni haraam)) [Shaykh Al-Abaaniy katika Silsilatus-Swahiyhah]

Hadiyth ya pili: Allaah سبحانه وتعالى Hatomtazama anayefanya kitendo hiki:

عن ابنِ عَبَّاس رضي الله عنهما قال: قال رسول الله)) لا يَنْظُرُ اللَّهُ إلى رَجُلٍ أَتَى امْرَأَةً في دُبُرِهَا))

صحيح ابن حبان
Imetoka kwa ibn 'Abbaas رضي الله عنهما ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((Allah Hatomtazama mwanamume anayemuingilia mwanamke kwa nyuma)) [Swahiyh Ibn Hibbaan]

Hadiyth ya Tatu: Amelaaniwa anayefanya kitendo hiki:

قال النبي صلى الله عليه وسلم : (( ملعون من يأتي النساء في محاشِّهن: أي أدبارهن (( رواه ابن عدي وصححه الألباني في آداب الزفاف

((Amelaaniwa anayewaingilia wanawake kwa njia ya nyuma)) [Imepokelewa na ibn 'Udayy na amesema ni sahiyh Shaykh Al-Albaaniy katika Adaabuz-zafaaf]



Hadiyth ya nne: Amekufuru anayefanya kitendo hiki:

عن أبي هريرة رضي الله عنه ((من أتى حائضا أو امرأة في دبرها أو كاهنا فصدقه بما يقول فقد كفر بما أنزل على محمد)) صحيح ابن ماجه و قال الألباني إسناده صحيح

Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه : ((Atakayemuendea (atakayemuingilia) mwenye hedhi au mwanamke nyuma au atakayemuendea mtabiri akamuamini anayomuambia, atakuwa amekufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammad)) [Sahiyh ibn Maajah na kasema Shaykh Al-Albaaniy kuwa isnaad yake ni Sahiyh]



Hadiyth ya tano:

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: جاء عُمَر بن الخطاب إلىٰ رسول الله فقال: يا رسول الله، هلكتُ! قال: (( وما الذي أهلكك؟)) قال: حَوَّلْتُ رَحْلِي الليلة، فلم يردَّ عليه شيئاً، فأُوْحِيَ إلىٰ رسول الله هذه الآيةُ: {نساؤكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنىٰ شئتم} يقول: أَقْبِلْ، وأَدْبِرْ، واتقي: الدُّبر، والحَيضة سنن النسائي الكبرى

Imetoka kwa Ibn 'Abbaas رضي الله عنهما ambaye amesema: Alikuja 'Umar ibnul-Khatwaab kwa Mjumbe wa Allah akasema: Ewe Mjumbe wa Allah, Nimeangamia! Akasema: ((Nini kilichokuangamiza?)) Akasema: Nimepindua kipando changu usiku (nimemuingilia mke wangu sehemu ya mbele lakini kwa kumgeuza) Lakini hakumjibu kitu. Akateremshiwa Aayah hii ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo)) Anasema: (unaweza kumuingilia) kwa mbele na kwa kumgeuza na chunga kumuingilia nyuma na wenye hedhi. [Sunnan An-Nasaail-Kubraa]



Hadiyth ya sita

عن أم سلمة قالت: لما قدم المهاجرون المدينة على الأنصار تزوّجوا من نسائهم، وكان المهاجرون يجبون وكانت الأنصار لا تجبي، فأراد رجل من المهاجرين امرأته على ذلك، فأبت عليه حتى تسأل رسول الله صلى الله عليه وسلم، قالت: فأتته فاستحيت أن تسأله، فسألته أم سلمة فنزلت: {نساؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنّى شِئْتُمْ} وقال: «لا إلاّ في صَمَّامٍ واحِدٍ» . : مسند الإمام أحمد

Imetoka kwa Ummu Salamah رضي الله عنها kwamba: Muhaajiriyn walipokuja Madiynah kwa Maanswaar waliwaoa wanawake wao. Wanawake Wa Muhaajiriyn walikuwa wakilala kifudifudi (wakati wa kujimai na waume zao) na wanawake wa Maanswaar hawakuwa wakifanya hivyo. Mwanamume mmoja Muhaajir alitaka mkewe afanye hivyo akakataa. Akaenda kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم lakini aliona haya kumuuliza swali hilo, kwa hiyo Ummu Salamah alimuulizia kisha Aayah ikateremshwa inayosema ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo)) Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: ((Hapana! (Sio kila sehemu upendayo) bali ni mbele tu. [Musnad ya Imaam Ahmad]

Nasaha zetu kwa dada yetu ni kama zifuatazo:-

1. Endelea kumcha Allaah سبحانه وتعالى bila kuyumba yumba.

2. Kuwa na istiqaamah na usimkubalie mumeo kukuingiza katika tendo hilo la haramu.

3. Mfanyie Da‘wah mumeo kwa hekima na mawaidha mazuri huenda akabadilika kutokana na tabia hiyo yake mbovu na mjulishe kuhusu Aayah yenye makatazo hayo katika Qur-aan na Hadiyth

4. Ikiwa imeshindikana kumrekebisha basi itisha kikao baina ya wazazi wako na wazazi wa mume. Na ikishindikana kabisa, bora udai talaka yako uepukane na haraam hiyo.



Tanbihi:

Mume kumuingilia mke kwa nyuma haina maana kwamba mke ameachika (Talaka) moja kwa moja kama wanavyofahamu wengi, bali ana haki mke kudai talaka lakini hakuna dalili kwamba hukumu ya talaka iwe imepita katika kitendo hiki.

Tunakuombea kwa Allaah Akupatie moyo wa kukataa maovu na Akupatie uimara katika kudumu na mazuri. Tunamuomba Allah Amuepushe mumeo na tabia mbaya hiyo na Amrudishe katika njia ya haki. Tunakuombea muafaka katika kutatua tatizo hilo.

Na Allah Anajua zaidi.
 
Naam,kwa kuongezea tu,jimai au tendo la ndoa limeruhusiwa kuliendea kwa mikao na staili mbali mbali,kwahiyo wale ambao mnaona haya mambo ya kizungu mnafeli sana

Ndio maana ikasemwa hao ni kama konde zenu ziendeeni mpendavyo

Tanbihi:

Kunyonyana sehemu za siri hapo ndio kwenye uzungu na haifai

...............

Darsa ya Swala ya Mtume itafuata baadae

Inshaallah
 
Assalaam alaikum ndugu zangu katika Imani kama nilivyosema awali darsa linafuatia,,,lkn kabla ya hapo tupate kidogo

NASAHA ZA IJUMAA

Ndugu zangu katika Uislamu hakuna KATAA NDOA,kama wewe kwa kukurupuka na kufuata mkumbo basi ikukae akilini mwako kwamba hatuna Kataa Ndoa

Nabii swallallahu alaih wasallam anasema mila yake ni kuoa,na asiyefuata mila yake basi amemkhalifu Mtume,sasa kama Mjumbe wa Allah ndio kigezo chetu katika mfumo mzima wa maisha yetu,je hiyo kataa yako ndoa umeitoa wapi???

Enzi za Nabii swallallahu alaih wasallam kuna masahaba walitaka kuwa wacha mungu kwa kutotaka kuoa,yaani wao washikamane na ibada tu

Nabii swallallahu alaih wasallam, aliwaambia yeye ni mcha mungu zaidi kuliko wao lakini anaoa kama kawaida

Haya hao hawakutaka kuoa kwa ajili wajikite zaidi katika mambo ya kheri na bado wakaambiwa waoe,je wewe mwenzangu ambaye kutwa kuchwa tunazini,halafu hatutaki kuoa,hivi tunajitambua kweli?

Kuoa ni lazima kwa yule ambaye hawezi kuzuia matamanio yake ili aepukand na machafu,lau kwa mtu ambaye anaweza zuia matamanio yake kwake sio lazima

Sasa swali la msingi kwako,je kukataa kwako Ndoa,unaweza kuzuia matamanio yako usizini?

Kama huwezi kuzuia basi salama yako ni kuoa na kuepuka uchafu wa uzinifu

Allah hakukataza tu zinaa ila amesema tusikaribie zinaa,yani wacha lile tendo lenyewe ya kuzini,lkn usikaribie kwa maana epuka mazingira yote ambayo yatakupelekea kuendea kwenye zinaa

Acha kuchati chati na mwanamke maana huko ni kuikaribia zinaa,acha mazoea kumkonyeza mwanamke au matani matani ya kimapenzi,hayo yote ni kukaribia zinaa

Kwahiyo ili ujue jinsi hii dhambi ilivyo kubwa mbele ya Allah,tumekatazwa kuikaribia wachia mbali kukamilisha tendo lenyewe

Sasa iweje mtoto wa kiislamu bila aibu nawe unapaza sauti na kuwa mmoja wa KATAA NDOA?

Wengine hawana dini na wengine hawamwamini Allah ndio maana wanapaza sauti bila woga na haya juu ya jambo hilo

Tumche Allah

Ijumaa Mubarak!
 
Naam tunaendelea na darsa nambari 22



022-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Alivyokuwa Akisoma (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Mbalimbali. 1 - Swalah Ya Alfajiri


ALIYOKUWA AKISOMA (صلى الله عليه وآله وسلم) KATIKA SWALAH (MBALI MBALI)



Kuhusu Surah gani na Aayah gani aliyokuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiisoma katika Swalah, hilo linatofautiana kwa kutofautika kwa Swalah tano na Swalah nyenginezo. Basi chukua maelezo ya upambanuzi wake kwa kuanzia na Swalah ya kwanza katika Swalah tano:





1- SWALAH YA ALFAJIRI



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Surah([1]) ndefu za mufasswal([2]) hivyo alikuwa (wakati mwengine) akisoma Al-Waaqi'ah (56: 96) na mfano wake katika Rakaa mbili.([3])



Alisoma kutoka Surat-Twuur (52: 49) katika Hijjatul-Wadaa’ (Hijjah ya Kuaga).([4])



Mara nyingine, alikuwa akisoma Surat Qaaf [50: 45] na mfano wake [katika Rakaa ya mwanzo].([5])



Mara nyingine alikuwa akisoma Surah fupi za mufasswal kama:



((إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ))



((Jua litakapokunjwa)) [At-Takwiyr 81: 29)).([6])



Na mara moja alisoma:

((إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا))





((Itakapotetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!)). [Az-Zilzalah 99: 8)



katika Rakaa zote mbili, jambo lililomfanya msimulizi kusema: "Sielewi kama Mjumbe wa Allaah alisahau au aliisoma kwa makusudi.([7])



Alisoma mara moja akiwa safarini:



((قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ))





((Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko)). [Al-Falaq 113: 5]



na



((قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ))





((Sema: Najikinga kwa Mola wa wana Aadam)). [An-Naas 114: 6][8]



Akasema kumwambia 'Uqbah bin 'Aamir (رضي الله عنه): ((Soma Al-Mu'awwidhatayn([9])katika Swalah zako, kwani hakuna mwenye kutafuta kinga kama hiyo))([10]).



Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma zaidi ya hivo, kwani alikuwa akisoma Aayah sitini (60) au zaidi([11]). Baadhi ya wasimulizi wake wamesema: " Sielewi kama ilikuwa katika moja ya Rakaa mbili au katika zote mbili."



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Surat Ar-Ruum [30: 60]([12]) na mara nyingine akisoma Surat Yaasiyn [36: 83)([13]).



Mara moja aliswali Swalah ya Alfajiri Makkah, akaanza kusoma Suratul-Mu-minuun [23: 118] hadi alipofikia kutajwa Muusa na Haaruun au kutajwa 'Iysa([14]) -Msimulizi mmoja hakuwa na hakika- alianza kukohoa hivyo akarukuu([15]).



Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwaswalisha katika Swalah ya Alfajiri kwa kusoma Suratu Asw-Swaaffaat [77: 182]([16])



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiiswali Swalah ya Alfajiri siku ya Ijumaa kwa kusoma Surat As-Sajdah [32: 30] (katika Rakaah ya mwanzo na Rakaa ya pili) Surat Ad-Dahr [76: 31].([17])



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akirefusha Rakaa ya kwanza na kufupisha Rakaa ya pili.([18])





KISOMO KATIKA SUNNAH YA ALFAJIRI



Kisomo chake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Rakaa mbili za Sunnah ya Alfajiri, kilikuwa chepesi mno([19]) hadi 'Aaishah رضي الله عنها) ) alikuwa akijiuliza kwa kusema: "Je, amesoma ndani yake Kifungulio cha Kitabu (Suratul Faatihah)?"([20]).



Mara nyingine alikuwa akisoma baada ya al-Faatihah katika Rakaa ya mwanzo ya hizo mbili Aayah hii:



((قُولُواْ آمَنَّا بِاللّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْنَا ...))



((Semeni nyinyi: Tumemwamini Allaah na yale tuliyoteremshiwa sisi…)). [Al-Baqarah 2:136) mpaka mwisho wa Aayah.





(katika Rakaa ya kwanza,) na katika ya pili alikuwa akisoma Aayah:





((قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْاْ إِلَى كَلَمَةٍ سَوَاء بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ ...))



((Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi…)) [Al-'Imraan 3: 64] ([21]) mpaka mwisho wa Aayah.



Mara nyingine husoma badala ya Aayah ya pili:



((فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَى مِنْهُمُ الْكُفْرَ))



(('Iysaa alipo hisi kuwa kati yao pana ukafiri)) [Al-'Imraan 3:52]([22]) mpaka mwisho wa Aayah.



Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Suratul-Kaafiruun [109 -6] katika Rakaa ya kwanza, na Suratul-Ikhlaasw [112-4] katika Rakaa ya pili.([23])



Pia alikuwa akisema: ((Hizi ni jozi bora kabisa za Surah (hizi)).([24])



Alimsikia mtu akisoma Surah ya mwanzo - Suratul-Kaafiruun - katika Rakaa ya kwanza, akasema: ((Huyu mja amemwamini Mola wake)). Kisha mtu huyo akasoma Surah ya pili - Suratul-Ikhlaasw - katika Rakaa nyengine, akasema: ((Huyu mja amemwelewa Mola wake)).([25])




[1] An-Nasaaiy na Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[2] Sehemu ya saba ya mwisho ya Qur-aan, kuanzia Surah Qaaf (Namba 50) kama ilivyo rai yenye nguvu kabisa kama ilivyotangulia.

[3] Ahmad, Ibn Khuzaymah (1/69/1) na Al-Haakim ambaye amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahaby amekubaliana naye.

[4] Al-Bukhaariy na Muslim.

[5] Muslim na At-Tirmidhiy. Imetolewa pamoja na inayofuatia katika Al-Irwaa (345).

[6] Muslim na Abu Daawuud.

[7] Abu Daawuud na Al Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh. Kinachodhihiri ni kuwa yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) alifanya hivyo kwa makusudi ili kuthibitisha kujuzu kwake.

[8] Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah (1/76/1), Ibn Bushraan katika Al-Amaaliy na Ibn Abi Shaybah (12/176/1). Al-Haakim amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahaby amekubaliana naye.

[9] Surah mbili za kujikinga; yaani Surah mbili za mwisho katika Qur-aan, zote zinaanzia na Qul-A'udhu…. (Sema najikinga….).

[10] Abu Daawuud na Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[11] Al-Bukhaariy na Muslim.

[12] An-Nassaaiy, Ahmad na Al-Bazzaar kwa isnaad nzuri.

[13] Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[14] Muusa ametajwa katika Aayah ya 45: ((ثُمَّ أَرْسَلْنَا مُوسَى وَأَخَاهُ هَارُونَ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ)) na 'Iysa ametajwa katika Aayah ya 50: ((وَجَعَلْنَا ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ آيَةً وَآوَيْنَاهُمَا إِلَى رَبْوَةٍ ذَاتِ قَرَارٍ وَمَعِينٍ))

[15] Muslim na Al-Bukhaariy katika Ta'aliyqan, nayo ni Hadiyth inayoondoshwa mwanzo wa isnaad yake msimulizi mmoja au zaidi kwa mfululizo kama ilivyoelezwa nyuma. Imetolewa katika Al-Irwaa (397).

[16] Ahmad na Abu Ya'laa katika Musnad zao, na Al-Maqdisiy katika Al-Mukhtaarah.

[17] Al-Bukhaariy na Muslim.

[18] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[19] Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[20] Al-Bukhaariy na Muslim.

[21] Muslim, Ibn Khuzaymah na Al-Haakim.

[22] Muslim na Abu Daawuud.

[23] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[24] Ibn Maajah na Ibn Khuzaymah.

[25] Atw-Twahaawiy, Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake na Ibn Bushraan. Ibn Hajar amesema kuwa ni nzuri katika Al-Ahaadiyth Al-'Aaliyaat (Namba, 16).
 
Msione mbona nimeruka darsa nambari 23,,,nimeona na 24 ziko sawa,,ni makosa ya kibinadamu



024-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Cha Aayaat Baada Ya Al-Faatihah Katika Rakaa Mbili Za Mwisho
KISOMO CHAKE (صلى الله عليه وآله وسلم) CHA AAYAAT BAADA YA AL-FAATIHAH KATIKA RAKAA MBILI ZA MWISHO



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akizifanya Rakaa mbili za mwisho fupi zaidi kulinganisha na Rakaa mbili za mwanzo kiasi cha nusu yake, kiasi cha Aayah kumi na tano,([1]) na pengine alifupisha katika Rakaa mbili za mwisho kwa kusoma al-Faatihah pekee.([2])



Alikuwa mara nyingine akiwasikilizisha Aayah.([3]) Na walikuwa wakisikia kutoka kwake mvumo wa kisomo chake:



سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى



((Litakase jina la Mola Aliye juu kabisa)) [Al-A'laa 87-19],

na



هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ



((Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?)) [Al-Ghaashiyah 88-26].([4])





Mara nyingine husoma:



((وَالسَّمَاء ذَاتِ الْبُرُوجِ))



((Naapa kwa mbingu yenye Buruji!)) [Al-Buruuj 85-22], na



((وَالسَّمَاء وَالطَّارِقِ))



((Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!)) [Atw-Twaariq 86-17], na Sura nyinginezo mfano wa hizi mbili.([5])



Mara nyingine alikuwa akisoma:



((وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَى))



((Naapa kwa usiku unapofunika!)) [Al-Layl 92-21], Na mfano wake.([6])




[1] Ahmad na Muslim. Katika Hadiyth hii, kuna dalili kwamba kusoma Surah zaidi ya Suratul-Faatihah katika Rakaa mbili za mwisho ni Sunnah, na Maswahaba wengi walifanya hivyo. Miongoni mwao ni Abu Bakr (رضي الله عنه). (Pia) na ni rai ya Imaam Ash-Shaafi'iy, na ni sawa tu kama itakuwa katika Adhuhuri au katika Swalah nyinginezo. Maulamaa waliofuatia, Abul-Hasanaat Al-Laknawiy katika ((At-Ta’aliyq Al-Mummajad ‘Alaa Muwattwa Muhammad)) (Uk. 102) (akasema:"Na baadhi ya wafuasi wetu wamekuja na rai ya ajabu, kwani waliwajibisha Sajdatus-Sahw (Sajda ya kusahau) kwa kusoma Surah katika Rakaa mbili za mwisho. Na kwa hakika wamejibiwa na wenye kutoa maelezo/ sharh ya Al-Maniyyah; Ibraahiym Al-Halabiy na Ibn Amiyr Haaj na wengineo, wamejibiwa majawabu mazuri mno. Bila shaka wale waliosema hivyo haikuwafikia Hadiyth iliyotaja hayo, na lau kama imewafikia wasingelisema hivyo"

[2] Al-Bukhaariy Na Muslim.

[3] Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1.67/2) na Adh-Dhiyaa Al-Maqdsiy katika Al-Mukhtaarah ikiwa na isnaad Swahiyh.

[4] Al-Bukhaariy katika Makala ya Tilaawah, na At-Tirmidhiy ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh.

[5] Muslim na At-Twayaalisiy.

[6] Al-Bukhaariy na Muslim.
 
Tusome Hadith

Leo tunamalizia hadith katika mlango wa kalimah ya Laa ilaha illallah,,,kesho tutaingia mlango wa Kuamini yasiyo onekana


Screenshot_20250418_204135_ReadEra.jpg
 
Chemsha Bongo No. 1

MAJIBU YAKE


Dhunun ni jina lingine la mtume gani?
- NI YUNUSI

Mtume gani aliomba dua maarufu-anlaa ilaaha ilaa anta subhanaka in kuntum minadhwalimini
- NI YUNUSI (baada ya kumezwa na samaki,aliomba dua hii akiwa ndani ya tumbo la samaki)

Mtume gani aliomba mtoto kwa Allah,akapewa mtoto anaitwa Yahya
-NI ZAKARIA


Ni mazingira au hali gani Muislamu atapaswa kutayamamu?
  • WAKATI UNAPO KOSA MAJI
  • WAKATI UNAPO SHINDWA KUTUMIA AMA KWA BARIDI AU UGONJWA

Nabii Mussa alifundishwa elimu ya ghaibu na mja wa Allaha,je anaitwa nani?
- DHULFIKIR (Inasemekana yupo hai mpaka leo)


Ni mja gani wa Allah alitembea Mashariki na Magharubi ya dunia,kisha akaujenga ukuta ambao Yajuju na Majuju wakashindwa kuukwea?
-DHUL CARNAIN (Huu ukuta upo mpaka leo,utakuja kuvunjwa na Allah siku ya Kiama)

Ni mitume watatu wamesifika kwa sifa ya Subira,je ni wapo hao?
  • ISMAIL
  • IDRISA
  • DHUL KIFLI
 
025-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Za Alasiri, Maghrib Na 'Ishaa


1- SWALAH YA ALASIRI



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma katika Rakaa mbili za mwanzo al-Faatihah na Surah mbili, hurefusha Rakaa ya kwanza kuliko ya pili([1]) na walikuwa wakidhani kuwa alikuwa akifanya hivyo ili watu waweze kuidiriki Rakaa ya mwanzo.([2])



Alikuwa akisoma kadiri ya Aayah kumi na tano katika kila Rakaa mbili za mwanzo, kiasi cha nusu ya kisomo alichokuwa akisoma katika Rakaa mbili za mwanzo za Swalah ya Adhuhuri, na alikuwa akizifupisha Rakaa mbili za mwisho kiasi cha nusu ya urefu wa Rakaa mbili za mwanzo.([3])



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma al-Faatihah katika Rakaa mbili za mwisho.([4]) Alikuwa akiwasikilizisha Aayaah (au zaidi) mara nyingine([5]), na alikuwa akisoma Surah tulizozitaja hapo nyuma katika Swalah ya Adhuhuri.







2- SWALAH YA MAGHRIB



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma katika Swalah hii – baadhi ya nyakati -Surah fupi za Mufasswal([6]), kiasi cha “wao wanapomaliza kuswali naye, huondoka mmoja wao, na hakika mtu (angeweza kuutupa na) kuona sehemu iliyoangukia mshale wake.”([7]).



Na (Mara moja), alipokuwa safarini alisoma:



((وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ))



((Naapa kwa tini na zaytuni!)) [At-Tiyn 95:8) katika Rakaa ya pili.([8])



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) mara nyingine akisoma Surah ndefu za Mufasswal na za wasitani, hivyo alikuwa akisoma:



الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّهِ



((Waliokufuru na wakazuilia njia ya Allaah)). [Muhammad 47: 1].([9])



Mara nyingine akisoma Suratu-Twuur [52: 49]([10])



Na mara nyingine akisoma Suratul-Mursalaat [77: 50] ambayo aliisoma katika Swalah (yake) ya mwisho aliyoiswali (صلى الله عليه وآله وسلم).([11])



Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma moja kati ya Surah mbili ndefu (atw-Twuwlayayn)([12]); [Al-A'araaf 7: 206] (katika Rakaa mbili).([13]) Na mara nyingine akisoma Al-anfaal [8: 75] katika Rakaa mbili.([14])







KISOMO KATIKA SUNNAH (BAADA YA SWALAH) YA MAGHARIBI



Ama katika Sunnah ya baada (al-ba’diyyah) ya Maghrib, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma:



((قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ))

((Sema: Enyi makafiri!)). [Al-Kaafiruun 109: 6], na





((قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ))

((Sema: Yeye Allaah ni wa Pekee)). [Al-Ikhlaasw 112: 4].([15])







3- SWALAH YA 'ISHAA



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Surah za kati na kati za Mufasswal katika Rakaa mbili za mwanzo([16]), hivyo alikuwa mara nyingine akisoma:





((وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا))

((Naapa kwa jua na mwangaza wake!)) [Ash-Shams 91: 15] na Surah nyingine zilizofanana na hiyo([17]).



Na mara nyingine alikuwa akisoma:



((إِذَا السَّمَاء انشَقَّتْ))



((Itapochanika mbingu)) [Al-Inshiqaaq 84: 25), na alikuwa akileta Sajdah humo([18]).



Pia mara moja alipokuwa safarini alisoma:



((وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ))

((Naapa kwa tini na zaytuni!)) [At-Tiyn 95:8) (katika Rakaa ya mwanzo).([19])





Alikataza (صلى الله عليه وآله وسلم) kurefusha kisomo katika 'Ishaa, katazo hili lilikuja wakati Mu'aadh bin Jabal alipowaswalisha watu wake Swalah ya 'Ishaa akaifanya ndefu, akajiondoa mtu mmoja katika Answaar na kuswali pekee. Mu'aadh akaelezwa habari ya mtu huyo akasema: "Hakika yeye ni mnafiki". Mtu yule ilipomfikilia taarifa, alikwenda kwa Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumweleza vile alivyosema Mu'aadh. Basi hapo Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)akamwambia Mu'aadh: ((Je, unataka kuwa mfitini ewe Mu'aadh? Utaposwalisha watu basi soma:





((وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا))

((Naapa kwa jua na mwangaza wake!)) [Ash-Shams 91: 15], na





سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى



((Litakase Jina la Mola wako Aliye juu kabisa)) [Al-A'laa 87: 19], na





((وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَى))



((Naapa kwa usiku unapofunika!)) [Al-Layl 92: 21] [Bila ya shaka huswali nyuma yako watu wazima, wagonjwa na wenye haja zao].[20])




[1] Al-Bukhaariy na Muslim.

[2] Abu Daawuud ikiwa na isnaad Swahiyh na Ibn Khuzaymah.

[3] Ahmad na Muslim.

[4] Al-Bukhaariy na Muslim.

[5] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[6] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[7] An-Nasaaiy na Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[8] Atw-Twayaalisy na Ahmad katika isnaad Swahiyh.

[9] Ibn Khuzaymah (1/166/2), Atw-Twabaraaniy na Al-Maqdisiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[10] Al-Bukhaariy na Muslim.

[11] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[12] At-twuulayayn ni Al-A'raaf [7] kwa makubaliano, na Al-an'aam [6] kutokana na kauli iliyo sahihi zaidi kama ilivyotajwa katika Fat-h al-Baariy.

[13] Al-Bukhaariy, Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah (1/68/1), Ahmad, Siraaj na Mukhlisw.

[14] Atw-Twabaraaniy katika Mu'jam Al-Kabiyr ikiwa na isnaad Swahiyh.

[15] Ahmad, Al-Maqdisiy, An-Nasaaiy, Ibn Naswr na Atw-Twabaraaniy.

[16] An-Nasaaiy na Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[17] Ahmad na At-Tirmidhy ambaye amekiri ni nzuri.

[18] Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaaiy.

[19] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[20] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni. Imetolewa pia katika Al-Irwaa (295).
 
026-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Ya Usiku - Sifa Ya Swalah Ya Mtume


1. SWALAH YA USIKU



Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)mara nyingine akifupisha ([1]) kisomo katika hiyo Swalah ya usiku, na mara nyingine hukirefusha, na wakati mwengine hukirefusha sana, mpaka ikampelekea 'Abdullaah bin Mas'uud kusema: "Usiku mmoja niliswali pamoja na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi aliendelea kusimama (kwa) muda mrefu sana mpaka nikawaza jambo baya. Pakaulizwa: "Uliwaza nini"? Akajibu: "Nilifikiria kukaa chini na kumuacha Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)!([2]).



Hudhayfah bin Al-Yamaan pia alisema:

"Usiku mmoja niliswali na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi alianza kusoma Suratul Al-Baqarah (2: 286). Nikasema (moyoni): "Atarukuu baada ya Aayah mia". Lakini aliendelea, nikawaza kuwa huenda ataimaliza Surah katika [rakaa mbili]. Lakini aliendelea na nikasema: "Atarukuu atakapoimaliza." Kisha akaanza kusoma Suratun-Nisaa (4: 176), akaisoma yote. Kisha akaanza kusoma Suratul-'Imraan (3: 200)([3]), akaisoma yote. Alikuwa akisoma polepole, anapopita kwenye Aayah zenye kumtukuza Allaah humtukuza, na anapopita kwenye Aayah zenye maombezi huomba, na anapopita kwenye Aayah za kujikinga hujikinga. Kisha akarukuu…" (Hadi mwisho wa) Hadiyth.([4])



Pia usiku mmoja alipokuwa akiumwa, alisoma Surah saba ndefu.([5])



Pia alikuwa akisoma moja ya Surah hizi saba ndefu katika kila rakaa.([6])



Haikupata kutokea kuwa yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) alisoma Qur-aan nzima katika usiku mmoja [abadani]([7]), na wala hakumkubalia hivyo 'Abdullaah bin 'Amru (رضي الله عنه) wakati alipomwambia: ((Soma Qur-aan nzima kila mwezi)). Akasema: Nikamwambia: "Ninao uwezo wa kufanya zaidi ya hivyo". Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Isome katika masiku ishirini)). Akasema: Nikamwambia: "Ninao uwezo wa kusoma zaidi". Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Basi isome katika siku saba na wala usipunguze zaidi ya hapo)).([8])



Kisha Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alimruhusu kuisoma Qur-aan nzima katika siku tano.([9])



Kisha Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alimruhusu kuisoma Qur-aan nzima katika siku tatu.([10])



Kisha Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akamkataza kuisoma Qur-aan nzima chini ya hivyo([11]) na akatoa sababu kwayo kwa kumwambia: ((Yeyote atakayesoma Qur-aan nzima chini ya siku tatu, hatoweza kuifahamu))([12]). Na katika riwaaya nyingine: ((Hawezi kufahamu mwenye kuisoma Qur-aan nzima chini ya siku tatu)).([13])



Kisha alimwambia: ((Kwa hakika kila mwenye kuabudu huwa ana muda wa shirrah([14]), na kila shauku ina kipindi cha kupunguka, aidha ielekee kwenye Sunnah au kwenye bid'ah. Hivyo basi mwenye kuwa upungufu wake umeelekea kwenye Sunnah, huyo basi amepata uongofu, na mwenye kuwa upungufu wake umeelekea kwenye kinyume cha hivyo, basi ameangamia))([15]).



Kwa sababu hii, akawa (صلى الله عليه وآله وسلم) hasomi Qur-aan nzima chini ya siku tatu.([16])



Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Atakayeswali katika usiku na akasoma Aayah mia mbili, basi huandikwa miongoni mwa watiifu wenye kumtakasia Allaah )).([17])



Pia alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Surat Bani Israaiyl (17: 111) na Surat Az-Zumar (49: 75) katika kila usiku([18]). Na alikuwa akisema: ((Atakayeswali katika usiku na akasoma Aayah mia, basi hatoandikwa miongoni mwa walioghafilika))([19]). Mara nyingine alikuwa akisoma katika kila Rakaa kiasi cha Aayah khamsiyn au zaidi([20]), na mara nyingine akisoma kiasi cha Suratul Al-Muzammil (73: 20).([21])



Na wala hakuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akiswali usiku mzima([22]), isipokuwa kwa nadra, kwani mara moja ‘Abdullaah bin Khabbaab bin al-Arat - ambaye alishuhudia vita vya Badr pamoja na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) – alimpeleleza Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) usiku mzima, na katika riwaaya nyingine: katika usiku alioupitisha kwa kuswali usiku mzima hadi ikawa pamoja na Afajiri. Alipoimaliza Swalah yake, Khabbaab alimwambia: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Kwa heshima zote za baba yangu, nakupa wewe na heshima zote za mama yangu!



"Usiku wa leo umeswali Swalah sikuwahi kukuona kuswali mfano wake".



Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Ndio, ilikuwa Swalah ya shauku na khofu, (na mimi kwa hakika) nilimuomba Mola Wangu عزوجل mambo matatu, Amenipa mawili, na Amenikatalia moja. Nilimuomba Mola wangu Asituangamize kwa kile Alichowaangamizia Ummah za kabla yetu [na katika riwaaya nyingine]: ((Asiuangamize Ummah wangu kwa njaa) Akanipa hilo, Nikamuomba Mola wangu عزوجل Asitusalitishe na adui asiye kuwa miongoni mwetu, Akanipa hilo, na nilimuomba Mola wangu Asituvurunge vurunge mpaka tukawa makundi yasiyopatana kwa mfarakano, (lakini) Amenikatalia hili)).([23])



Na usiku mmoja alisimama (صلى الله عليه وآله وسلم) (katika Swalah) akawa akikariri Aayah moja hadi alfajiri. Aayah yenyewe ni:



(( إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ))



((Ukiwaadhibu, basi hao ni waja Wako. Na Ukiwasamehe, basi Wewe Ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hikmah)). [Al-Maaidah 5: 121]



[kwayo karukuu nayo, na kwayo kasujuduia na kwayo kaomba], [Kulipopambazuka, Abu Dharr (رضي الله عنه) alimwambia: "Ewe Mjume wa Allaah! Hukusita kuisoma Aayah hii hadi kumepambazuka, umerukuu nayo, umesujudu nayo] [na umeomba nayo] [hali ya kuwa Allaah Amekufundisha Qur-aan nzima], [lau (ingelikuwa) mmoja wetu amefanya hivi, tungelimkemea]. [Akasema: ((Hakika nimemuomba Mola wangu عزوجل kuwashufaia Ummah wangu, Akanipa hilo, na Uombezi huo utapatikana Allaah Akipenda kwa yeyote asiyemshirikisha Allaah na kitu cho chote kile)).([24])



Mtu alimwambia: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Mimi ninaye jirani anayesimama kuswali usiku na hasomi isipokuwa:



((قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ))

((Sema: Yeye Allaah ni wa Pekee)) [Al-Ikhlaasw 112: 4],

(anaikariri) [haongezei nyingine] kama kwamba anaiona kuwa hadhi yake ni ndogo". Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, hakika hiyo ni sawa na thuluthi ya Qur-aan)).([25])




[1] An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[2] Al-Bukhaariy na Muslim.

[3] Hivi ndivyo ilivyopokelewa kutangulizwa Suratun-An-Nisaa (4) kabla ya Al-'Imraan (3), na hiyo ni dalili kwamba inaruhusiwa kusoma kwa kuacha kufuatilia mpangilio wa Msahafu wa 'Uthmaan katika kusoma. Umekwishapita mfano kama huu.

[4] Muslim na An-Nasaaiy.

[5] Abu Ya'laa na Al-Haakim ambae amesema kuwa ni Swahihy, na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye. Ibn Al-Athiyr amesema: “….Surah saba ndefu ni: Al-Baqarah (2), Al-'Imraan (3), An-Nisaa (4), Al-Maaidah (5), Al-An'aam (6), Al-A'raaf (7) na At-Tawbah (9)".

[6] Abu Daawuud na An-Nasaaiy kwa isnaad Swahiyh.

[7] Muslim na Abu Daawuud.

[8] Al-Bukhaariy na Muslim.

[9] An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy ambaye amesema kuwa ni Swahiyh.

[10] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[11] Ad-Daarimiy na Sa’iyd ibn Masnuur katika Sunan yake kwa isnaad Swahiyh.

[12] Ahmad kwa isnaad Swahiyh.

[13] Ad-Daarimiy na At-Tirmidhiy ambaye amesema kuwa ni Swahiyh.

[14] "Shirrah" ni msisimko, hamu, shauku, nguvu. Na Shirrah ya vijana mwanzo wake ni bidii, nguvu, hamasa na raghba. Imaam Atw-Twahaawiy amesema: "Ni bidii na hamasa katika vitendo ambavyo wanavitaka Waislamu kutokana na nafsi zao wenyewe katika ‘amali zao ambazo wanajikurubisha kwazo kwa Mola wao عزوجل. Na kwa hakika Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) anapenda zaidi kutoka kwao hivyo, na sio vile vitendo walivyovianza kutokana na shauku na hamasa ambayo hawana budi isipokuwa watakuwa na upungufu na kuachana navyo na kushikamana na kinyume chake. Kwa hiyo, aliwaamrisha waendelee kushikamana na vitendo vyema ambavyo wataweza kuviendeleza na kudumu navyo hadi watakapokutana na Mola waoعزوجل . Katika kulifafanua hili, imesimuliwa kutoka kwake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba amesema: ((Vitendo vipendezavyo kwa Allaah, ni vile vyenye kudumishwa japo kuwa ni vichache)).

Nasema: "Hadiyth hii ambayo ameitoa kwa njia ya kuonyesha kuwa msimulizi wake hajulikani (Majhuul) kama linavyomaanisha neno "imesimuliwa", ni Swahiyh na ni waliyowafikiana kwayo Al-Bukhaariy na Muslim kutokana na Hadiyth ya Mama wa Waumini 'Aaishah (رضي الله عنها).

[15] Ahmad na Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake.

[16] Ibn Sa'ad (1/376) na Abu-Ash-Shaykh katika Akhlaaq An-Nabiyy (صلى الله عليه وآله وسلم) (281).

[17] Ad-Daarimy na Al-Haakim ambaye amesema kuwa ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.

[18] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[19] Ahmad na Ibn Naswr kwa isnaad Swahiyh.

[20] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[21] Ahmad na Abu Daawuud kwa isnaad Swahiyh.

[22] Muslim na Abu Daawuud. Nimesema: "Kwa Hadiyth hii na nyingine, inaonyesha kuwa ni makruuh kukesha usiku mzima kila siku au aghlabu, kwani ni kinyume na mwenendo wake (صلى الله عليه وآله وسلم), na lau ingelikuwa kukesha usiku mzima ni bora, basi hilo lisingelimpita Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Na uongofu bora kabisa ni uongofu wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Na wala usidanganyike na yaliyosimuliwa kuhusu Abu Haniyfah kwamba yeye alikuwa akiswali Swalah ya al-Fajr kwa wudhuu wa 'Ishaa kwa miaka arubaini!! [Maelezo ya Mfasiri: Taz. Tabliygh An-Nisaab: Fadhila za Swalaah kilichoandikwa na Maulana Zakariyyah Kandhalvi kwa mifano ya dai kama hili]. Kwani usimulizi huu kutoka kwake, hauna msingi wo wote ule, bali 'Allaamah Al-Fairuuz ‘Abaadi amesema katika Ar-Radd 'alaa al-Mu'taridh (44/1): "Usimulizi huu ni miongoni mwa uongo uliowazi ambao haupaswi kuambatanishwa na Imaam, kwani hakuna fadhila yenye kutajwa katika kufanya hivyo. Na ilikuwa ni vyema kwa mfano wa Imaam kama huyu, kufanya yaliyo bora zaidi, na hakuna shaka yoyote ile kwamba kutawadha upya (Tajdiydul Wudhuu) kwa kila Swalah, ndilo linalopendeza zaidi, ndio ukamilifu na ndio bora zaidi. Hii kama itathibiti kuwa ilikuwa kweli kwamba yeye alikuwa akikesha usiku kwa miaka arubaini mfululizo! Jambo hili linaelekea kuwa kama jambo lisilowezekana, nalo ni katika simulizi za kale zilizozushwa na washabiki wajinga wavukao mipaka waliosema hivyo kuhusu Abu Haniyfah na wengineo, na yote ni uongo mtupu".

[23] An-Nasaaiy, Ahmad na Atw-Twabaraaniy (1/187/2). At-Tirmidhiy amesema ni Swahiyh.

[24] An-Nasaaiy, Ibn Khuzaymah (1/70/1), Ahmad, Ibn Naswr na Al-Haakim ambaye amesema ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.

[25] Ahmad na
 
028-Sifa Ya Swala Ya Mtume 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Ya Ijumaa - Sifa Ya Swalah Ya Mtume


8- SWALAH YA IJUMAA





Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akisoma mara nyingine katika Rakaa ya mwanzo Suratul-Jumu'aa [62: 11]:



يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ الْمَلِكِ الْقُدُّوسِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ﴿١﴾

((Vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi vinamtukuza Allaah, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikmah)),

na katika Rakaa ya pili:



إِذَا جَاءكَ الْمُنَافِقُونَ

((Wanapokujia wanaafiki)) [63: 11]([1]),



na mara nyingine - badala yake([2])- alikuwa akisoma:



هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ

((Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?)) [88: 26],

na mara nyingine akisoma:



سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى

((Litakase Jina la Mola wako Aliye juu kabisa)) [Al-A'laa 87: 19], katika Rakaa ya mwanzo na:





هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ

((Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?)) [88: 26],

katika Rakaa ya pili([3]).




[1] Muslim na Abu Daawuud. Imetolewa katika Al-Irwaa (345).

[2] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[3] Muslim na Abu Daawuud.
 
Amali anayoipenda sana Allah ni ile yenye kudumu kwa mujibu wa hadith kama tulivyo ona

Ni bora kuswali rakaa mbili tahajjud kwa muendellezo kuliko kuswali rakaa nyingi mara moja moja

Ni kheri kumtaja Allah (dhikri) mara chache kila siku kuliko kumtaja kwa wingi baadhi ya siku na siku nyingine humtaji kabisa
 
MASWALI NA MAJIBU



Maswali: Haki Za Mke Na Mume




SWALI:


baada ya salam ningependa kutanguliza shukrani za dhati kwa wale wanao shughulikia site hii na ningependa kujuwa je ni haki hii...ikiwa mume wangu anakaa online usiku bila ya kunijali kama mimi ndo mke wake wa ndoa na ninapo mwambia yeye anakuwa mkali na pia ananambia ninawasiwasi wa nini wakati yeye yumo ndani hatoki nje? lakini mimi ni mkewe wa ndoa na pia ninahitaji kupewa haki yangu na pia nahitaji heshima ya ndoa yangu na pia nahitaji kuenziwa sio mke tu ndani ya nyumba bila mapenzi wala imani wala huruma.kwani anapo fanya hivo mimi nahisi kama hanitaki tena au kapata mwengine...aAllaahu a'lam. na pia inanifanya hata nifikirie mambo mabaya kutokana bwana huyu hanipi haki yangu.

ustadh naomba uniwekee wazi juu ya hilo kutoka kwenye quran na hadith na pia ni nini nifanye na nimeshajaribu kusema nae mara nyingi tu na bila ya kunisikiliza? JazakAllaah khair..



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa dada yetu muuliza swali. Baina ya wanandoa kila mmoja ana haki na wajibu juu ya mwenziwe. Na katika haki ya mke kutoka kwa mume sio kupewa chakula, malazi na nguo tu bali pia kupatiwa haki ya unyumba. Kukosa kupewa haki hiyo ni sababu moja anayoruhusiwa mke kuomba talaka kwa mumewe.

Ni jambo la busara ulilofanya kwa kuzungumza na mumeo lakini bila ya mafanikio. Tunaomba ujaribu tena kuzungumza naye wakati unapoona ana makini na hali ya kuwa anaweza kukusikiliza. Usife moyo kwani kufa moyo si katika sifa ya Muislamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

"Enyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yuusuf na nduguye, wala msikate tamaa na faraji ya Allaah. Hakika hawakati tamaa na faraji ya Allaah isipokuwa watu makafiri" (12: 87).

Weka muda wa kujaribu kuokoa ndoa hiyo kwa mfano mwezi au na vikao vitatu naye.

Ikiwa hukufanikiwa, basi waeleze wazazi wake na wazazi wako au wawakilishi wenu muwe na kikao cha kujadili suala hilo kwa njia nzuri ya kutaka suluhu. Lau mtataka suluhu basi Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atawafanikishia na kuwaondolea tatizo hilo.

Ikiwa hukufanikiwa kwa njia hiyo ya pili pia, itabidi upeleke kesi yako kwa Qaadhi au Shaykh aliye karibu nanyi ili aingilie kati na kusuluhisha baina yenu. Kukiwa hapatopatikana ufumbuzi itabidi akuache au uombe talaka.

Twaomba msifike kote huko bali mpate suluhisho muafaka. Twawaombea kila la kheri.

Na Allaah Anajua zaidi
 
Mke Anayo Haki Kukataa Kufanya Kazi Za Nyumba?
Maswali: familia-Jamii


Mke Anayo Haki Kukataa Kufanya Kazi Za Nyumba?





Alhidaaya.com





Swali La Kwanza:



Naomba kuuliza swali kuhusu haki ya mke. Nimeolewa kwa kipindi cha miaka miwili na hutokezea matatizo mengi kuhusu ufanya kazi nyumbani kama kupika, kuosha kumpijia pasi mume n.k, je kama sikufanya hivo na mume anataka hayo kwa sababu yoyote ile je itakuwa nimekosea na kama sijakosea je hiyo imeandikwa wapi na nnaomba kama itakuwa vizuri kupata japo maandishi ya quran au hadith.



Asanteni.





Swali La Pili:



Naomba kuuliza swali. Mwanamkwe kumpikia mumewe na shughuli za nyumbani kwa ujumla ni wajibu wake au kufanya hivyo ni sehemu ya mapenzi kwa mumewe? Na



kama ni mapenzi ni nani anayestahili kufanya hayo? Allaah awape kila la kheri leo na kesho Aakhirah In shaa Allaah





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Japo dada yetu ameyagawa haya maswali na kuyafanya mawili lakini ni moja tu kwani yanafanana kabisa. Suala hili lina maoni tofauti baina ya wanazuoni mbalimbali.



Maswahabiyaat (Swahaba wa kike) [Radhwiya Allaahu ‘anhunna] walikuwa msitari wa mbele katika kuwahudumikia waume zao. Mfano mzuri ni Faatwimah binti ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliyekuwa akimhudumikia mumewe kwa kufanya kazi zote za nyumbani mpaka akamshitakia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa aliyokuwa akikumbana nayo mikononi mwake katika kusaga ngano na shayiri [Al-Bukhariy na Muslim].





Na Asmaa’ bint Abi Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: "Nilikuwa nikimhudumikia az-Zubayr bin al-‘Awwaam (mumewe - Radhwiya Allaahu ‘anhu) kazi zote za nyumbani. Az-Zubayr alikuwa na farasi niliyekuwa nikimtazama, nikimpatia nyasi na kumsimamia. Alikuwa akimlisha farasi wake na kumnywesha maji, kukanda na kubeba mbegu kichwani mwake kutoka sehemu iliyo na umbali wa maili mbili (kutoka nyumbani kwake)” [al-Bukhariy na Muslim].





Shaykh al-Islaam, Ibn Taymiyah anatuarifu: “Wanazuoni wamezozana (wametofautiana): Je, ni juu ya mke kumhudumikia mumewe kwa mfano kwa kutandika nyumba, kupika chakula, kinywaji, mkate na chakula cha wanyama pamoja na kuwatazama na mfano wake? Wapo wanaosema kuwa si wajibu wake lakini kauli hii ni dhaifu kama udhaifu kwa wanaosema: Si wajibu kuishi na kujamiiana, kwani huku si kuishi nao kwa wema. Panasemwa, na hii ndio kauli sahihi, wajibu wa kumhudumikia, kwani mume ni bwanake (Sayyid) katika Kitabu cha Allaah, naye ni mwenye kuwa na hamu na kunyenyekea kwake katika Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ni juu ya mwenye kunyenyekea (mfungwa) na mtumwa kuhudumu, kwani huo ndio wema. Kisha wapo wanaosema: Ni wajibu wake kuhudumikia kwa kazi nyepesi. Na wengine wanasema: Ni wajibu kuhudumu kwa wema, na hii ndiyo iliyo sahihi. Ni juu ya mke kumhudumikia mumewe kwa wema kwa mfano wao (wanandoa). Hiyo khidmah (huduma) inakuwa tofauti kwa kubadilika hali. Khidmah ya jangwani si kama ya kijijini, na ya kijijini si kama ya aliye dhaifu” (Al-Fataawaa, Mj, 34: uk. 90 -91).





Hivyo, rai ya wanazuoni wa Imaam Ahmad kama Abu Thawr, Abubakar ash-Shaybaaniy na Abu Ishaaq wanaosema ni wajibu wake. Hata hivyo, jamhuri ya wanazuoni wanasema si wajibu wa mke kumhudumikia mumewe na ni juu ya mume kumpatia mkewe msaidizi wa kumsaidia kazi zake.





Muhtasari wa maneno ni kuwa ‘Urf (ada na desturi) za watu ambazo haziendi kinyume na kanuni za Uislamu zinacheza duru kubwa na muhimu katika suala hili. ‘Urf kwa baadhi ya madhehebu ya Ahlus Sunnah ni chimbuko la sheria. Ndio tukaona kuwa Maswahabiyah (Radhiya Allaahu ‘anhunna) wakiwahudumikia waume zao kama mifano tuliyotoa ya Faatwimah binti ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Asmaa’ bint Abi Bakr (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakusema wanadhulumiwa. Katika sehemu ya Afrika Mashariki tunayoishi ni ‘Urf kwa mke kumhudumikia mumewe kwa kumpikia, kumpigia pasi na kumfanyia mambo mengineo. Mbali na kuwa kabla ya Nikaah mke ana haki kuweka masharti kama kumtaka mume amuwekee mfanyakazi wa nyumbani ili amsaidie. Au pia mume mwenyewe awe anamsaidia anaporudi kazini.





Hapana shaka kuwa wanandoa wanatakiwa wasaidiane kwa wema kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta‘aalaa) Anasema:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ

Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. Na Mcheni Allaah;.. [Al-Maaidah: 2].





Hivyo, mume anatakiwa amsaidie mkewe kama alivyokuwa akifanya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). ‘Aaishah amesema: Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwasaidia watu wake (wa nyumbani), yaani akiwahudumikia, lakini kipindi cha Swaalah kinapofika alikuwa anatoka kwenda kuswali [Al-Bukhaariy]. Ni juu ya mume kutazama hali ya mkewe na kutombebesha asiyoweza.





Mume anatakiwa atazame mazingira na hali ya mkewe kwani ameamuriwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta‘aalaa) pale Aliposema:

وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ

Na kaeni nao kwa wema.. [An-Nisaa: 19].





Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mcheni Allaah kuhusiana na wanawake kwani wao ni wasaidizi walio kwenu" [Muslim].





Na tena: "Mbora wenu ni mbora wenu kwa familia yake, nami ni mbora wenu kwa familia yangu" [at-Tirmidhiy, Ibn Maajah, ad-Daarimiy na atw-Twabaraaniy].





Kwa hiyo, mume akiwa na wasaa kwa kifedha ni vyema amwekee mkewe msaidizi wa kumsaidia kazi na mke naye anafaa pia asaidie katika baadhi ya kazi na nyumbani kama vile mume naye anafaa kufanya hivyo ili mapenzi yazidi baina yao.





Kwa maelezo zaidi ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:



43 Wajibu Wa Mwanamke Kumhudumia Mumewe





Na Allaah Anajua zaidi.
 
Muendelezo wa post namba hapo juu 2,932

Wajibu Wa Mwanamke Kumhudumia Mumewe


Ninasema: baadhi ya Hadiyth zilizotajwa zinaonyesha dhahiri wajibu wa mwanamke kumtii na kumhudumia mumewe madamu anao uwezo, na hakuna shaka kwamba jambo la kwanza linaloingia humu ni huduma za nyumba na yote yanayohusika humo kama kulea watoto na kadhalika. Maulamaa wamekhitilafiana katika mas-ala haya, kwa mfano Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema katika 'Al-Fataawa' (2/234-235),


"Maulamaa wamekhitilafiana katika mas-ala haya kama inampasa kumhudumia kama kushughulika na fenicha za nyumba na kutayarisha chakula na vinywaji, kusaga unga na kupika chakula kwa ajili ya watumwa wake na kuwalisha farasi na kadhalika. Kuna wengine wanaosema, Huduma hii sio lazima. Kauli hii ni dhaifu, kama ilivyo udhaifu wa kauli za wale wanaosema kuwa mume haimpasi kumtendea wema au kujimai naye. Kwa vile hii haitokuwa ni kumfanyia wema, kama ni rafiki katika safari…Ikiwa hatomsaidia maana yake ni kuwa hajamtendea wema.

Na inasemekana: Na hii ndio sawa, kwamba kumhudumia ni wajibu kwa vile mumewe ameitwa ni bwana wake katika kitabu cha Allaah سبحانه وتعالى katika Sunnah ya Mjumbe wa Allaah na mtumwa na mateka wanapaswa kuhudumiwa na kwa sababu hivyo ndivyo inavyojulikana sana.
Kisha kuna waliosema, Huduma nyepesi ya kawaida ni wajibu na wapo waliosema, ni wajibu kufanya wema na hili haswa ndio la sawa sawa.


Hivyo basi ni juu yake ahudumie katika mema ya kawaida ya mfano wake, hali hii inatofautiana na anuai za shughuli, kwa mfano mwanamke wa kibedui anatofautiana na mwanamke wa kijijini kwa anuai za shughuli na huduma anayotoa, kadhalika mwanamke mwenye nguvu atatofautiana na mwanamke dhaifu.

Nasema na hii ni Swahiyh Insha-Allaah, na ni usemi wa Maalik na Asbigh kama ilivyo katika 'Al-Fat-h' (9/418) na Abuu Bakar ibn Abu Shaybah na wengineo kama Al-Atwazijaariy wa Hanbali kama ilivyo katika 'Ikhtiyaaraat' (Ukurasa 145) na kundi la Maulamaa wa zamani na wa sasa kama ilivyo katika 'Az-Zaad' (4/46) na hatuoni dalili yoyote ya kufaa inayosema kuwa jambo hili halina uwajibu.

Na wengine wanasema: Kufunga ndoa kunahitaji starehe kufaidiana na sio kuhudumika rai hii imetupwa kwa sababu suala la starehe ni la wote.



Kama tunavyojua kuwa Allaah سبحانه وتعالى Amemuwajibisha zaidi mwanamume katika kumpatia mahitaji yake mke kama nguo, maskani na kumtimizia mahitajio yake. Kwa hiyo vile vile yeye mke pia anayo yaliyozidi kuwa wajibu kwake na hakuna zaidi ila ni kumhudumia. Khaswa kwa vile mume ndiye mwenye mamlaka ya mke, kwa hiyo ikiwa hatomhudumia, itabidi yeye mume amhudumie mke katika nyumba na hii itamfanya mke awe na mamlaka badala yake, jambo ambalo ni kinyume na Aayah ya Qur-aan kama ilivyo wazi. Kwa hiyo ni wajibu wa mke amhudumie mume.



Vile vile kuhudumu kwa mume kutaleta hali mbili zenye kugongana kwamba mume atazuilika kutafuta rizki na mahitajio mengine ambayo alipaswa kufanya na mwanamke atabakia nyumbani bila ya kufanya lolote.

Uharibifu/ufisadi huu upo dhahiri kabisa katika sheria ya Kiislamu, sheria ambayo imeweka usawa baina ya mume na mke katika haki mbali mbali, si hivyo tu bali pia umemfadhilisha mwanamume katika daraja na ndio maana Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakusikiliza malalamiko ya bintiye Faatwimah. Tunasoma malalamiko hayo katika Hadiyth ifuatayo,


“Faatwimah alikwenda kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kushitakia ugumu wa kazi za mikono nyumbani kwake, ingawaje hakumkuta babake Mtume صلى الله عليه وآله وسلم lakini alimuachia maagizo Ummul Muuminina ‘Aaishah. ‘Aliy anahadithia kuwa (baada ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kupata salamu zile) Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikwenda kwao na wakati huo walikuwa wameshapanda kitandani yeye na mkewe kulala, ‘Aliy anasema, ‘Tulitaka kusimama (baada ya kumuona Mtume صلى الله عليه وآله وسلم) lakini akatukataza na kutuambia, “Hapo hapo mlipo” Akakaa katikati yetu pale kitandani kiasi nikahisi ule ubaridi wa miguu yake tumboni mwangu. Akutuambia, “Je, nikujulisheni jambo zuri zaidi kuliko lile mliloomba?” Mnapoingia kitandani semeni "Subhaana-Llaah' mara thelathini na tatu, 'Alhamduli-Llaah' mara thelathini na tatu na 'Allaahu Akbar' mara thelathini na nne, kwani hiyo ni bora kuliko kuwa na mtumishi”[1]

Kwa hiyo mnaona kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakumwambia 'Aliy, kuwa hana haja ya kukuhudumia bali inambidi (Faatwimah) amhudumie mumewe. Na yeye Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakupendelea watu fulani katika kutoa sheria kama alivyotaja Ibn Al-Qayyim. Na anayetaka kujua zaidi kuhusu mas-ala haya basi asome kitabu chake cha thamani "Zaadul-Ma'aad' (4/45-46).

Majukumu ya mke kwa mumewe hayakatazi au kuzuia mume kumsaidia mke wake katika kazi zake. Hakuna kitu cha kudai mapendeleo ya usaidizi wa mume kwa mkewe ikiwa atapata wakati, bali hiyo ni mojawapo wa kutendeana wema baina ya mke na mume, na ndiyo mama wa waumini ‘Aaishah رضي الله عنها alisema: "Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akihudumia familia yake na Swalah ilipowadia alikuwa anakwenda kuswali"[2]


Na imenukuliwa katika 'Ash-Shamaa'il' (2/185) kutoka isnaad nyingine kwa maneno: "Mwanamume alikuwa akishughulikia nguo zake mwenyewe, akikamua kondoo maziwa, na akijihudumia mwenyewe". Na usimulizi wake ni Swahiyh na nyinginezo kidogo ni dhaifu. Lakini Ahmad na Abu Bakar Ash-Shaafi'y wamenukuu kwa isnaad iliyo na nguvu kama nilivyoonyesha katika 'Silsilatul-Ahaadiythis-Swahiyhah' (Namba 670) na kufuzu ni kutokana na tawfiki ya Allaah سبحانه وتعالى.

Huu ni mwisho wa yale Aliyoniwezesha Allaah سبحانه وتعالى kuandika kuhusu ‘Adabu za Ndoa na Sherehe za Harusi’ katika kitabu hiki.







سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك




Subhaanaka Allaahuumma Wa Bihamdika, Ash-Hadu An Laa Ilaaha Illa Anta, Astaghfiruka Wa Atuubu Ilayka.



[1] 'Aliy amesema: "Sikuiacha tena baada ya hapo". Ilisemwa: Hata usiku wa Siffiyn? Akasema: "Hata usiku wa Siffiyn" (imehadithiwa na Al-Bukhaariy 9/417-418)



[2] Imehadithiwa na Al-Bukhaariy (2/129 na 9/418), At-Tirmidhiy (3/314) ambaye amekiri ni Swahiyh, Al-Mukhlis katika 'Al-Mukhlisiyaat' (1/66) na Ibn Sa'ad (1/366)
 
Kama tulivyosoma hapo pamoja na mwanamke ni wajibu wake kumuhudumia mumewe kwa yale ambayo ni mepesi kwake, basi haimaanishi kwamba mume asimsaidie mkewe baadhi ya shughuli anapokuwa na wasaa

Kusaidiana ndio kuonyeshana mapenzi na huruma,siku moja moja unaweza kusaidia kazi za nyumbani na inakuwa safi,kwani Nabii swallallahu alaih wasallam alikuwa anafanya sana mambo hayo,tunaambiwa ilipofika mda wa swala huyo alienda kuswali

Kwahiyo wanaume tuache kasumba za kusema kazi za nyumbani eti huwezi kufanya,basi wewe utakuwa humfuati Rasullullahi ambaye ndie kiigizo chetu

Istoshe kufanya hivyo hakupunguzi hadhi yako na thamani yako

Alhamdulillah enzi za ndoa yangu kuna nyakati nilifua nguo zangu na za mke wangu,niliogesha wanangu,na kupika pia

Allah atuongoze inshaallah
 
Back
Top Bottom