Ramadhan Special Thread
Asalaam Aleykum ndugu zangu wote katika imani,

Kuelekea mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhan, waislamu wote ninawaomba tukutane humu ili tuelimishane mawili matatu kuhusu mwezi huu.

Lengo kuu ni kuweza kufahamu yale yote aliyotufunza kipenzi chetu mtume Muhammad S.A.W kuhusu mwezi huu.

Vitu gani tukifanya vitaharibu swaumu zetu, vitu gani tukifanya vitaongeza thawabu zinazopatikana katika kufunga, ipi hukumu kwa wale wasiofunga na yapi malipo anayopewa mja ambaye anafunga swaumu kikamilifu.

Pia tuweze kujifunza neema zinazopatikana kwenye usiku wa lailatul qadr, usiku ambao umebarikiwa kuliko siku elfu moja.

Kwa haya machache ninapenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kwa muumba wa mbingu na ardhi ambaye si mwingine bali ni Allah S.W. T na kipenzi chake, Mtume Muhammad S.A.W.

Karibuni.
Duuu nyani kaona nini tena?

View: https://x.com/RadioGenoa/status/1915065377253466171
 
Screenshot_20250424_191850_Quran Swahili.jpg
 
Hizo hapo ni sifa za waumini walio fuzu,je unafiti hapo?

Kama haufiti unafanya juhudi gani uwe mmoja wapo?
 
Screenshot_20250424_194229_CamScanner.jpg


Hapo itakuwa ina maanisha makadirio ya kheri na shari,maana ikiwa ni makadirio ya mema na mabaya,itamaanisha kwamba mwanadamu amekadiriwa kufanya maovu na mema kitu ambacho sio sahihi

Kwasababu itamaanisha kuwa Allah kamafanya mtu awe muovu halafu itakuwaje kuwe na mizani ya uadilifu wakati mhusika alishakadiriwa toka awali awe muovu,sasa mizani ya amali zake ni ya nini wakati tayar ni wa motoni
 
NASAHA ZA IJUMAA

Assalaam alaikum warahmatullah wabarakatuh

Ndugu zangu alhamdulillah leo ni ijumaa ni siku bora kabisa kwetu Waislamu,kwani ni sikukuu kwetu sisi,kwahiyo hatuna budi kuifurahia,kikubwa tumswalie sana Nabii swallallahu alaih wasallam na kumtaja sana Allah subhaanahu wataala

Kwani Allah anasema ikiadhiniwa swala katika siku ya ijumaa,basi fanyeni haraka nendeni mkamtaje Allah,muache biashara na yote yenye kukushughulisheni,na kisha baada ya swala basii tawanyikeni katika ardhi na muendelee kumtaja sana Allah

Naam nasaha zangu ni juu ya hadith za Nabii swallallahu hapo juu,nataka tuzungumzie juu ya kuamini kadari kwamba kheri na shari hakika vyote vinatoka kwa Allah

Allah kabla ya kuumba mbingu na ardhi kipindi cha miaka hamsini elfu (50,000) alishaandika makadirio ya viumbe wote, je riziki yao itakuwaje,wataishi umri gani,watafia wapi,na mitihani ya kheri na shari kwa kila mmoja wetu, na anasema kalamu ikanyanyuliwa na wino ukakauka,kwa maana hakuna tena mwenye kubadilisha hatima yake


Ila inasemwa kwa kuomba dua basi Allah huweza kubadilisha baadhi ya hatima alizo tuwekea,ndio ile umeomba upate nyumba,lkn kumbe ulikadiria upate ajali ya gari,basi badala ya kupata nyumba ukajibiwa kwa kuepushwa na mtihani wa ajali

Sasa Nabii swallallahu alaih wasallam anasema kila jambo lina uhakika wake,na uhakika hasa wa imani ya mtu ni kuamini kwamba kheri na shari zinatoka kwa Allah,aamini lolote linalo mpata basi ni kadari ya Allah juu yake,ukifikia daraja hiyo basi wewe hakika imani yako ipo madhubuti sana

Na Allah anasema hata wakusanyike watu dunia nzima wa mwanzo na wa mwisho watake kukunufaisha wewe hawataweza ila utapata tu kile ulichoandikiwa (ulicho kadiriwa) na akaendelea Allah kusema hata watu dunia nzima wa mwanzo na wa mwisho watake au wapange kukudhuru basi hata hawata weza isipokuwa kwa lile dhara ambalo ulikwisha andikiwa likupate

Kwahiyo ndugu yangu katika imani hakuna mchawi au mwanga atakaye kudhuru pasina idhini ya Allah,kama uliandikiwa kupitia kwao upate mtihani basi utaupata na lau haikuwa hivyo hautadhurika

Na kuamini mambo ya kadari inakuwa kinga kwetu kutokana na hila za shetani,maana katika hali ya kawaida shetani huchochea fikra mbaya sana pale tunapopata mtihani,kama ni ajali tutaanza kusema hii sio ya kawaida hapa kuna namna,tukishaanza kusema hivyo hapo tayari shetani anatuchochea na kumuasi Allah,lkn tukiwa na imani madhubuti juu ya kadari tutasema tu 'INNA LILAH WAINA ILAIH RAJIUUN"

Tutambue kuwa ambalo lililokuwa likupate basi lisingekukosa na ambalo umelikosa basi lilikuwa lisikupate,kwahiyo haijilishi unapitia mitihani gani hapa duniani au umepata kheri gani tambua sio juhudi zako wala ujanja wako ila yote yanatoka kwa Allah

Na huo ndio ukweli na ndio imani ya muislamu wa kweli inatakiwa iwe hivyo katika maisha yake yote

Hii kadari ya kheri na shari ni mitihani ya Allah subhaanahu wa Taala, je ukipata kheri utaitumiaje na ukipata shari je utakufuru au utashukuru

Basi ndugu yangu muislamu kuwa na imani thabiti juu ya kadari ya Allah,na lolote litakalo kusibu basi rejea kwa Allah kwani ni yeye pekee wa kuombwa msaada na ndio yeye pekee atakaye tuondolea hiyo mitihani yake,kikubwa mja awe na subira,na akiwa na subira kwa yanayo mpata hakika analipwa ujia mkubwa sana

Subhaanaka allahumma wabihamdiki ashahadu anlaa ilaha ila anta astaghfiruka waatubu ilaik

Ijumaa Mubaraka!
 
Naam Darsa la Swala ya Nabii





038-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Wajibu Wa Kutulia Katika Sujuud Na Adhkaar Za Sujuud



WAJIBU WA KUTULIA KATIKA SUJUDU




Alikuwa ( (صلى الله عليه وآله وسلمakiamrisha kutimiza rukuu na sujuud, na akimlinganisha mtu asiyetimiza hivyo kuwa ni kama mtu mwenye njaa anakula tende moja au mbili ambazo hazimsaidii kitu cho chote. Pia akimuambia kuhusiana na asiyetimiza: ((Hakika yeye ni muovu kabisa miongoni mwa watu wezi)).




Vilevile alikuwa ( (صلى الله عليه وآله وسلمakihukumu kubatilika kwa Swalah ya mtu asiyenyoosha mgongo wake sawa sawa katika rukuu na sujudu, kama ulivyotangulia uchambuzi wake katika rukuu, na akamuamrisha aliyeswali vibaya atulie katika sujuud, kama ilivyotangulia katika mlango wa kwanza.










ADKHAAR ZA SUJUDU




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema katika nguzo hii namna mbali mbali za adhkaar na du'aa zozote, mara hizi na mara nyingine hizi. Kati ya du'aa hizo ni hizi zifuatazo:




1.





Subhaana Rabbiyal ‘Alaa

Ametakasika Mola wangu Aliye juu. (mara tatu).( [1])







Mara nyingine aliikariri zaidi ya mara hizo.([2])







Mara moja aliikariri sana katika Swalah ya usiku hadi sujuud yake ilikuwa inakaribiana na kisimamo chake alichokuwa amesoma ndani yake Surah tatu katika Surah ndefu; Al-Baqarah, An-Nisaa na Al-'Imraan. Ndani yake (Swalah hii) kulijaa du'aa na kuomba maghfirah, kama ilivyotajwa kabla katika Swalah ya Usiku.







2-








Subhaana Rabbiyal ‘Alaa wabihamdihii

Ametakasika Mola wangu Aliye juu Na Sifa Njema Ni Zake. (mara tatu)([3]).







3-





Subuuhun Qudduusun Rabbul Malaaikati war Ruuh

Mwingi wa kutakaswa Mtakatifu, Mola wa Malaika na Jibriyl.([4])













4-








Sub-haanaka Allaahumma Rabbanaa wa Biham-dika Allaahumma gh-fir-liy

Kutakasika ni Kwako, Ewe Allaah! Mola wetu, na sifa njema zote ni Zako, Ewe Allaah! Nisamehe.

Alikuwa akiileta kwa wingi hii katika rukuu yake na sujuud zake, alikuwa akitekeleza amri ya Qur-aan.([5])







5-








Allaahumma laka Sajad-tu, wabika Aamantu, walaka As-lamtu, [Anta Rabbiy] Sajada wajhiy Li-lladhiy Khalaqahu waswawwarahu, [fa-ahsana swuwarahu] washaqqa sam’ahu wabaswarahu, [fa]tabaaraka Allaahu Ahsanul Khaaliqiyn.

Ee Allaah! Kwako nimesujudu, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimesilimu, (Nawe ni Mola Wangu) umesujudu uso wangu kumsujudia Yule Aliyeuumba na Akautia sura, na Akaupasua usikizi wake na uoni wake, [Basi] Ametukuka Allaah Mbora wa waumbaji.([6])







6-







Allaahumma gh-firliy dham-biy kullahu, wa diqqahu, wajillahu, wa awwalahu wa aakhirahu, wa’alaaniyyatahu wasi-rrahu.

Ee Allaah! Nisamehe dhambi zangu zote, ndogo na kubwa, za mwanzo na za mwisho, za dhahiri na za siri.([7])







7-














Sajada laka sawaadiy wakhayaaliy, wa aamana bika fuaadiy, abuu-u bini’matika ‘alayya, haadhay yadayy wamaa janaytu ‘alaa nafsiy.

Utu wangu na kivuli changu kimekusujudia, moyo wangu umekuamini, nakiri neema Zako kwangu, hii ni mikono yangu na yote niliyochuma dhidi yangu.([8])







8-











Subhaana dhil Jabaruuti wal Malakuuti wal Kibriyaau wal ‘Adhwamati

Ametakasika Mwenye Utawala, na Ufalme, na Ukubwa, na Utukufu([9]). Hii alikuwa akiisema katika Swalah ya usiku pamoja na zifuatazo:




9-








Sub-haanaka [Allaahumma] wabihamdika, La ilaaha illa Anta

Kutakasika ni Kwako, (Ee Allaah) na sifa njema ni Zako, hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe.([10])







10-








Allaahumma gh-firliy maa Asrartu, wamaa a’lantu

Ee Allaah! Nisamehe (dhambi) nilizofanya kwa siri, na (dhambi) nilizofanya dhahiri.([11])










11-











Allaahumma j-‘al fiy qal-biy nuura, [wafiy lisaaniy nuura], waj-‘al fiy sam’iy nuura, waj-‘al fiy baswariy nuura, waj-‘al min tahtiy nuura, waj-‘al min fawqiy nuura, wa’an yamiyniy nuura, wa’an yasaariy nuura, waj-‘al amaamiy nuura, waj-’al khalfiy nuura,[waj-‘al fiy nafsiy nuura], wa-a’dhim liy nuura.

Ee Allaah! Jaalia nuru katika moyo wangu, [na katika ulimi wangu nuru], na Jaalia katika masikio yangu nuru, na Jaalia katika uoni wangu nuru, na Jaalia chini yangu nuru, na Jaalia juu yangu nuru, na kulia kwangu nuru, na kushoto kwangu nuru, na Jaalia mbele yangu nuru, na Jaalia nyuma yangu nuru (na Jaalia katika nafsi yangu nuru), na Nifanyie kubwa nuru.([12])







12-








Allaahumma [Inniy] A’udhuu biridhwaaka min sakhatwika, [wa A’udhuu] bimu’aafatika min ‘uquubatika, wa’Audhuu Bika Minka, laa uhswiy thanaa-an ‘alayka Anta kamaa Ath-nayta ‘alaa Na-fsika

Ee Allaah! Hakika [mimi] najilinda kwa Radhi Zako kutokana na hasira Zako, na [najikinga] kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako, na najilinda Kwako Unihifadhi na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa Zako, Wewe ni kama Ulivyojisifu Mwenyewe.([13])
















[1] Ahmad, Abu Daawuud, Ibn Maajah, Ad-Daaraqutwniy, Atw-Twahaawiy, Al-Bazzaar na Atw-Twabaraaniy katika Mu'jam Al-Kabiyr kutoka kwa Maswahaba saba. Taz. Pia Tanbihi katika Adhkaar za Rukuu.

[2] Taz. Tanbihi katika Rukuu pia.

[3] Swahiyh, imesimuliwa na Abu Daawuud, Ad-Daaraqutwniy, Ahmad, At-Twabaraaniy na Al-Bayhaqiy.

[4] Muslim na Abu 'Awaanah.

[5] Al-Bukhaariy na Muslim.

[6] Muslim, Abu 'Awaanah, Atw-Twahaawiy na Ad-Daaraqutwniy.

[7] Muslim na Abu 'Awaanah.

[8] Ibn Naswr, Al-Bazzaar na Al-Haakim, aliyekiri kuwa ni Swahiyh lakini Adh-Dhahabiy hakukubali. Hata hivyo, inayo nguvu ambayo imetajwa katika toleo la muswada.

[9] Abu Daawuud na An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[10] Muslim, Abu 'Awaanah, An-Nasaaiy na Ibn Naswr.

[11] Ibn Abi Shaybah (62/112/1) na An-Nasaaiy; Al-Haakim amekiri ni Swahiyh na Adh-Dhahaby amekubali.

[12] Muslim, Abu 'Awaanah na Ibn Abi Shaybah (12/106/2, 112/1).

[13] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo
 
039-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kukatazwa Kusoma Qur-aan Katika Sujuud, Kuirefusha, Na Fadhila Zake



KUKATAZWA KUSOMA QUR-AAN KATIKA SUJUUD




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akikataza kusoma Qur-aan katika rukuu na sujuud, na alikuwa akiamrisha kujitahidi na kuleta kwa wingi du'aa humo kama ilivyoelezewa kabla katika rukuu. Pia alikuwa akisema: ((Mja huwa karibu zaidi na Mola wake anaposujudu, hivyo leteni kwa wingi du'aa [humo])).([1])










KUREFUSHA SUJUUD




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akiirefusha sujuud yake kiasi cha kukaribiana na rukuu katika urefu, na mara nyingine aliifanya ndefu mno kwa kutokea jambo lisilotegemewa, kama alivyosimulia mmoja wa Maswahaba akisema:




Mjumbe wa Allaah Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alitutokea katika moja kati ya Swalah mbili za jioni (Adhuhuri na Alasiri) akiwa amembeba Hasan au Husayn. Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alitangulia mbele na akamuweka chini [karibu na mguu wake wa kulia], kisha akaleta Takbiyr ya Swalah, na kuanza kuswali, alisujudu –sajdah- kati ya sajdah za Swalah yake, sajdah aliyoirefusha akasema: Hivyo nikainua kichwa changu [baina ya watu] kumbe alikuweko mtoto juu ya mgongo wa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) hali ya kuwa amesujudu. (Kisha) nikarudi katika sajdah yangu [hii]. Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomaliza Swalah, watu wakasema: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Kwa hakika ulisujudu kati ya sajdah za Swalah yako, sajdah uliyoirefusha, mpaka tukadhania kuwa kuna jambo limetokea au ulikuwa unapokea wahyi". Akasema: ((Haikuwa lolote katika hayo, bali mwanangu alinipandia, nikachukia kumharakisha mpaka atapomaliza haja yake))([2]).




Katika Hadiyth nyingine, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akiswali, aliposujudu, Al-Hasan na Al-Husayn walimrukia mgongoni kwake. Watu walipojaribu kuwazuilia, aliwaashiria wawaachilie mbali. Alipomaliza Swalah, aliwaweka katika mapaja yake na akasema: ((Yeyote anayenipenda, basi na awapende na hawa wawili)).([3])













FADHILA ZA SUJUUD




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Hakuna yeyote katika Ummah wangu isipokuwa nitamtambua siku ya Qiyaamah)). Wakasema: "Vipi utawatambua ewe Mjumbe wa Allaah miongoni mwa umati mkubwa wa viumbe?" Akasema: ((Huoni kama ungeliingia katika boma ambako kuna farasi mweusi tii([4]) na farasi mwenye weupe katika kipaji chake na miguu([5]). Je, hutoweza kumtambua ni yupi baina yao?)). Wakasema: "Bila shaka". Akasema: ((Basi hakika Ummah wangu siku hiyo, watakuwa na weupe katika nyuso ([6]) kwa sababu ya sujuud, na wenye weupe katika mikono yao na miguu yao([7]) kwa sababu ya wudhuu)).([8])




Alikuwa akisema pia: ((Allaah Atakapotaka kumshushia Rahma Amtakaye katika watu wa motoni, Huwaamrisha Malaika wamtoe yeyote aliyekuwa akimuabudu Allaah, hivyo watawatoa, kwani wanawatambua kwa alama za sujuud. Kwa vile Allaah Ameuharamishia moto kuunguza alama za sujuud, hivyo watatoka kutoka motoni, kila binaadamu ataunguzwa na moto isipokuwa alama za sujuud)).([9])







[1] Muslim, Abu 'Awaanah na Al-Bayhaqiy. Imetolewa katika Al-Irwaa (456).

[2] An-Nasaaiy, Ibn 'Asaakir (4/257/1-2) na Al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali.

[3] Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake ikiwa na isnaad nzuri kutoka kwa Ibn Mas'uud (887) na Al-Bayhaqiy katika hali ya Mursal. Ibn Khuzaymah ameifasiri katika Mlango: "Dalili za kwamba kuashiria katika Swalah inavyofahamika katika Swalah haivunji wala kuharibu Swalah". Hichi ni kitendo kilichoharamishwa na Ahlul-Ra-y (watu wa rai). Hakuna Hadiyth katika Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo kuhusu jambo hili.

[4] Yaani rangi nyeusi safi isiyochanganywa na rangi nyingine yoyote. (An-Nihaayah)

[5] Weupe unakusudiwa sehemu ya farasi ambako minyororo na bangili zinavikwa pamoja na miguu ya chini lakini sio magoti.

[6] Yaani zinazong'ara usoni kutokana na nuru ya sujuud.

[7] Yaani sehemu zitakazong'ara kutokana na wudhuu: uso, mikono na miguu. Alama za kung'ara za wudhuu usoni, mikononi na miguuni za binaadamu kulinganisha na weupe wa uso farasi na miguu.

[8] Ahmad, ikiwa na isnaad Swahiyh. At-Tirmidhiy amesimulia baadhi yake na kakiri kuwa ni Swahiyh. Imetolewa katika Silsilatul-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah.

[9] Al-Bukhaariy na Muslim. Hadiyth inaonyesha kuwa wanaoswali lakini wana dhambi, hawatabakia motoni milele bali hata ambao wameacha Swalah kwa sababu ya uvivu hawatobakia motoni milele. Hii ni Swahiyh – taz. Asw-Swahiyhah (2054).
 
040-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kusujudu Juu Ya Ardhi Na Juu Ya Jamvi, Vikao Vyake Na Utulivu Ndani Yake



KUSUJUDU JUU YA ARDHI NA JUU YA JAMVI ([1])




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) sana akisujuud juu ya ardhi (tupu).([2])




Na Maswahaba zake walikuwa wakiswali pamoja naye katika joto kali, hivyo anapokuwa mmoja wao hawezi kumakinisha kipaji chake ardhini, hutandaza nguo yake na kusujudia juu yake.([3])




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((…. Imejaaliwa ardhi yote kuwa ni (sehemu ya kuswalia) Msikiti – mtu anaweza kuswali popote juu ya ardhi inapomkutia Swalah kama hapana najsi - na twahara –inatwaharisha: kuitumia kwa kujitwahirisha kutayammam- kwangu na kwa Ummah wangu. Hivyo basi Swalah inapomkutia mtu yeyote katika Ummah wangu, huwa anao Msikiti (mahali pa kuswali) na anayo twahara, (Ilikuwa) kabla yangu wakidhania kuwa ni jambo kubwa, kwani hakika walikuwa wakiswali makanisani na kaika masinagogi yao)).([4])




Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisujuud katika matope na maji. Na yalimtokea hayo katika asubuhi ya usiku wa ishirini na moja katika Ramadhaan, iliponyesha mvua, na paa la Msikiti lililojengwa na majani ya mtende liliezuliwa. Hivyo Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alisujuud katika matope na maji. Abu Sa'iyd Al-Khudriyy alisema: "Nimemuona kwa macho yangu, Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa na alama za matope na maji katika kipaji chake cha uso na pua".([5])




Pia mara nyingine alikuwa akiswali katika khumrah([6]), au mara nyingine katika zulia/ jamvi([7]), na mara aliswali juu yake na ilikuwa ishageuka nyeusi kutokana na utumiaji wa muda mrefu.([8])













KUINUKA KUTOKA KWENYE SUJUUD




Kisha, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akiinua kichwa chake kutoka kwenye sujuud huku akileta Takbiyr([9]) na alimuamrisha aliyeswali vibaya kufanya hivyo kwa kusema: ((Swalah ya mtu haikamiliki hadi …. Asujuud, hadi mifupa yake itue, kisha aseme 'Allaahu Akbar', na anyanyue kichwa chake mpaka atulizane hali ya kuwa amekaa (sawa sawa)).([10]) Pia, mara nyingine, alikuwa akinyanyua mikono yake pamoja na Takbiyr hii.([11])




Kisha alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiutandika mguu wake wa kushoto (ardhini) na kuukalia [hali ya kuwa ametulia]([12]), na alimuamrisha aliyeswali vibaya kwa kumwambia: ((Unaposujuud, jimakinishe kwa sujuud yako, na (kisha) unapoinuka, kalia paja lako la kushoto)).([13])




Alikuwa akiusimamisha mguu wake wa kulia([14]) na akielekeza vidole vya mguu wa kulia Qiblah.([15])









KIKAO BAINA YA SAJDAH MBILI (KIKAO CHA IFTIRAASH)([16])




Kisha alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiutandika mguu wake wa kushoto na kuukalia [hali ya kuwa ametulia]([17]), na alimuamrisha aliyeswali vibaya kwa kumwambia: ((Unaposujudu, jimakinishe kwa sujuud yako, na (kisha) unapoinuka, kalia paja lako la kushoto)).([18])




Alikuwa akiusimamisha mguu wake wa kulia juu([19]), na akielekeza vidole vya mguu wa kulia Qiblah.










AL-IQ-AA'U (KUSIMAMISHA MIGUU HUKU UMEKALIA VISIGINO) BAINA YA SAJDAH MBILI




Alikuwa mara nyingine akifanya 'iq-aau' (kupumzika kwa kukalia visigino vyote viwili na vidole vyake [vyote].([20])










WAJIBU WA KUTULIA BAINA YA SAJDAH MBILI




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akitulia mpaka kila mfupa unarudi mahali pake sawa sawa.([21]) Na alimuamrisha aliyeswali vibaya hivyo kwa kumuambia: ((Swalah ya mtu haitotimia hadi afanye hivyo)).([22])




Pia, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akikirefusha - hichi kikao baina ya Sajdah mbili- kiasi cha kukaribiana na urefu wa Sajdah yake([23]), na mara nyingine, alibakia katika (kikao hiki) mpaka mtu akasema: "Amesahau".([24])


[1] Al-Haswiyr – jamvi au mkeka uliotengenezwa kutokana na majani ya mtende au nyasi n.k.

[2] Hii ni kwa sababu Msikiti wake haukufunikwa na majamvi n.k. Hii ni dalili ya Hadiyth nyingi kama ifuatayo na ya Abu Sa'iyd itakayofuatia.

[3] Muslim na Abu 'Awaanah.

[4] Ahmad, Siraaj na Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[5] Al-Bukhaariy na Muslim.

[6] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni. "Khumrah" ni kipande cha jamvi, makumbi ya mtende, au nyenzo kama hizo za miti ambazo ni kubwa kiasi cha mtu kuweka uso wake katika Sajdah. Istilahi hiyo haitumiki kwa vipande vikubwa.

[7] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[8] Muslim na Abu 'Awaanah. Al-labisa kawaida ina maana 'kuvaa', lakini hapa imetumika kumaanisha 'kutumia', yaani kukalia n.k. Hivyo 'kuvaa' inajumuisha pia 'kuikalia'. Hii inaonyesha kwamba imekatazwa (haraam) kukalia hariri, kwa sababu ya kuharamishwa kuvaa kulikothibitishwa katika Swahiyh Al-Bukhaariy na Muslim na wengineo. Bali ni makatazo ya dhahiri kukalia hariri yamesimuliwa humo kwa hiyo asichanganywe mtu na kauli za Maulamaa wakubwa kuruhusu.

[9] Al-Bukhaariy na Muslim.

[10] Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali.

[11] Al-Bukhaariy katika Juzuu Raf' Al-Yadayn, Abu Daawuud ikiwa na isnaad Swahiyh, Muslim na Abu 'Awaanah. Imetolewa katika Al-Irwaa (316).




Kunyosha mikono hapa kwa kila Takbiyr imetajwa na Ahmad, kama ilivyo katika Al-Badaa'i ya Ibn Al-Qayyim (3/89). Athram (ibnul Athram) amenukuu kutoka kwake (Imaam Ahmad) alipoulizwa kuhusu kunyanyua mikono, alisema: "Kwa kila harakaat ya juu na chini". Athram kasema: "Nimemuona Abu 'Abdillaah (yaani Imaam Ahmad) akinyanyua mikono katika Swalah kwa kila harakaat ya chini au ya juu".




Hii pia ilikuwa ni rai ya Ibn Al-Mundhir na Abu 'Aliy wa Ash-Shaafi'iy, na pia rai ya Maalik na Ash-Shaafi'iy mwenyewe kama ilivyo katika Twarh At-Tathriyb. Kunyanyua mikono hapa pia kumesimuliwa kwa usahihi kutoka kwa Anas bin Maalik, Ibn 'Umar, Naafi', Atw-Twaawuus, Hasan al-Baswriy, Ibn Siyriin na Ayyuub As-Sikhtiyaaniy, katika Muswannaf Ibn Abi Shaybah (1/106) ikiwa na usimulizi Swahiyh kutoka kwao.




[12] Ahmad na Abu Daawuud ikiwa na isnaad nzuri.

[13] Al-Bukhaariy na Al-Bayhaqiy.

[14] An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[15] Muslim, Abu 'Awaanah, Abu Shaykh katika (Aliyopokea Abuz-Zubayr kutoka katika njia isiyo ya Jaabir) (Namba 104-6) na Al-Bayhaqiy.

[16] Ni kukalia tumbo la mguu wa kushoto na kuusimamisha unyayo wa mguu wa kulia.

[17] Ahmad na Abu Daawuud ikiwa na isnaad nzuri.

[18] Al-Bukhaariy na Al-Bayhaqiy.

[19] An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[20] Muslim, Abu 'Awaanah, Abu Shaykh katika (Aliyopokea Abuz-Zubayr kutoka katika njia isiyo ya Jaabir) (Namba 104-6) na Al-Bayhaqiy.

Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni. Ibn Al-Qayyim (رحمه الله) amesahau katika hili, hivyo baada ya kutaja "Iftiraash" ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) baina ya Sajdah mbili, amesema: "Hakuna aina nyingine ya kikao cha Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kilichohifadhiwa isipokuwa hiki". Vipi hii iwe sahihi na hali 'iq-'aau' imetufikia kutoka Hadiyth ya Ibn 'Abbaas katika Muslim, Abu Daawuud na At-Tirmidhiy ambaye amekiri ni Swahiyh na wengineo. (Taz. Silisilatul-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah 383), Hadiyth ya Ibn 'Umar ikiwa na isnaad nzuri kutoka kwa Al-Bayhaqiy na Ibn Hajar amekiri ni Swahiyh. Pia Abu Is-haaq Al-Harbiy amesimulia katika Ghariby al-Hadiyth (5/12/1) kutoka kwa Atw-Twaawuus, aliyemuona Ibn 'Umar na Ibn 'Abbaas wakifanya 'iq-'aa', sanad yake ni Swahiyh. Allaah Amteremshie Rahma Zake Imaam Maalik ambaye amesema: "Kila mmoja wetu anaweza kukosea na kukosolewa isipokuwa mwenye kaburi hili". Aliashiria kaburi la Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Sunnah hii imetekelezwa na Maswahaba mbali mbali, Salafus Swaalih na wengineo na nimeipambanua katika Al-Aswl.




Bila shaka, 'iq-'aa' hii ni tofauti na ile iliyokatazwa kama itakavyofuatia katika Tashahhud.




[21] Abu Daawuud na Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[22] Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubali.

[23] Al-Bukhaariy na Muslim.

[24] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni. Ibn Al-Qayyim amesema: "Sunnah hii imeachwa na watu baada ya zama za Maswahaba. Lakini anayefuata Sunnah na haangazi kwengine kunakoipinga, hana wasiwasi wa kupinga uongofu.
 
Anafanya Kazi Ya Ulinzi Hapati Kuswali Je, Anaweza Kuswali Huku Ameketi?
Maswali: Hukmu Za Swalah
SWALI:



Kwa uwezo wake ALLAH KARIM natumai mnaendelea vizuri na shughuli za kuwaelimisha waislam. Mimi nafanya kazi katika duka moja la kuuza germstone ikifika muda wa sala ya Adhuhuru naenda kuswali kwa kigezo kuwa natoka kwenda kwenye lunch, lakini muda wa laasiri ni ngumu kutoka kabisa naomba kuuliza je naweza kuswali nikiwa nimekaa kwenye kiti kwani hapa nilipo nipo kwenye mtihani. Nawatakia kila la kheri.



JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuswali ukiwa unaswali unapokuwa kazini.

Awali ya yote hukutueleza mwenye duka hilo ni nani – Muislamu au asiyekuwa Muislamu. Kwa hali zote, mwanzo unatakiwa ufanye bidii na juhudi ya kuzungumza na mwenye duka umuhimu wako kuswali wakati huo wa Alasiri. Unatakiwa uweke wazi kuwa Swalah ya Kiislamu haichukui muda mwingi na hata wanaweza kukupatia sehemu ya kufanyia ‘ibaadah hiyo.



Jambo hilo ni muhimu sana kwani ikiwa hukuwaelezea unaweza kuwa unaswali kwa kuketi wakati huo akaja mteja na ukashindwa kumfungilia ikawa ugomvi baina yako na mwenye duka. Ikiwa mwenye duka hakukubali kuhusu hizo dakika 5 zako kuswali, hata ukisema uswali kwa kukaa bado itakuwa tatizo kwako endapo atakuja mteja na hali wewe uko katika Swalah, sasa sijui umelitazama vipi hilo la kuswali kw akukaa ukaona lina tofautiana na la kuswali kwa kusimama katika mazingira uliyonayo?

Hata hivyo kwa dharura unaweza kuswali Swalah ya faradhi kwa kukaa, ama Swalah ya Sunnah haina tatizo kuiswali kwa kukaa.



Hata hivyo, jitahidi ulirekebishe hilo kwani huwezi kuswali hizo faradhi kwa kukaa siku zote kwani asli ni kuswali kwa kusimama na ndio ina daraja kubwa mara ya mbili ya anayeswali kwa kukaa.



Jitahidi uzungumze na wahusika kwa njia nzuri ya heshima na upole na inshaAllaah huenda wakaitikia maombi yako na kukupa wasaa wa kuifanya ‘Ibaadah hiyo kwa ukamilifu wake.



Tunakutakia kila la kheri uwe utafanikiwa kupatiwa ruhusa ili kusiwe na zogo wala kero kutoka kwa mwenye duka, na Allaah Atakulipa kwa juhudi zako hizo za kutaka kumtumikia Yeye vyema katika ‘Ibaadah zako




Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na faida ziada kuhusu mas-ala haya:







Kuswali Swalah Ya Safari Kwa Sababu Ya Udereva





Vipi Kukidhi Swalah Kama Shida Kuswali Kazini?



Hapati Kuswali Kwa Wakati, Kila Siku Anakidhi Swalah



Anaweza Kulipa Swalah Ya Magharibi Kila Siku Inayompita?







Na Allaah Anajua zaidi
 
Kuswali Swalah Ya Safari Kwa Sababu Ya Udereva
Maswali: Safari-Mgonjwa




SWALI:


Mimi nafanya kazi ya udereva hapa ulaya wa kuendesha basi la abiria wa town bus (DALADALA). Swala langu ni kwamba INAFAAA KWA mimi kuswali safari??? kwa sababu time nyingine ninakua sipati nafasi kwa sababu ukianza unakua unaenda kwa timu hadi unamaliza sasa time nyingine unachelewa hata timu ya kujinyoosha hamna yaani ukiingia kwenye usukani hadi 4 hrs later ndio unapata nafasi ya kutoka, au sipati maji ya kutia udhu au sehemu yenyewe inakua haisihi kuswali je inafaa kwa mimi kuswali safari?





JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani ndugu yetu kwa swali lako hilo kuhusu kuswali Swalah ya safari katika shughuli yako hiyo ya udereva. Hakika ni kuwa swali lako si kamili hivyo inakuwa ni vigumu kukujibu kikamilifu. Hata hivyo, tutajaribu kulitazama swali lako hilo katika kila upande.



Mwanzo hukutuambia uendeshaji wako wa daladala unakuwa kutoka wapi hadi sehemu gani. Je, kama ulivyosema katika suala lako ni uko mjini ambao wewe unaishi? Ikiwa jawabu ni ndio, basi itabidi ukamilishe Swalah kwani hutakuwa ni msafiri bali ni mkazi. Ikiwa safari yako inakupeleka mji mwengine basi hapo utakuwa umeingia katika wasafiri na unaweza kuswali kwa kuchanganya na kufupisha. Katika kuchanganya unaweza kuchelewesha Swalah au kuleta mbele, yaani unaweza kuswali Swalah za Adhuhuri na Alasiri wakati wa Adhuhuri au Alasiri.

Ama katika kadhia yako ikiwa uko mjini, basi unaweza baadhi ya nyakati kwa dharura hizo, kuunganisha Swalah mbili kwa pamoja, yaani Adhuhuri na Alasiri, au Magharibi na 'Ishaa lakini kwa kuziswali zote kamili na si kwa kuzifupisha. Ila usilifanye hilo kuwa ni ada ya kila siku.



Hakika wakati ni mtu kujipanga kwani hakuna uzito aina yoyote. Ikiwa una hima ya kweli unaweza hata kuzungumza na waajiri wako wakuweke ile zamu ya asubuhi ambayo itakupatia wewe fursa ya kuweza kutekeleza jukumu la Swalah kwa wakati wake. Inabidi uwaelezee waajiri umuhimu huo ili waweze kuelewa. Ikiwa wameelewa utapata afueni kubwa lakini usikae tu bila kujieleza ni lazima ufanye juhudi katika hilo.



Sijui hayo masaa 4 ambayo unasema unafanya mfululizo huwa ni namna gani? Je, unapoanza huwa hakuna hata ile nafasi ya kwenda chooni kujisaidia au kufika kituo na kubeba watu kwa dakika chache au ni vipi? Ikiwa zipo hizo nyakati basi hakutakuwa na shida yoyote kwani unaweza kutumia fursa hiyo.



Ama hakika kuswali si lazima maji yapatikane. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameifanya Swalah kuwa ni nguzo isiyokuwa na udhuru wa aina yoyote. Muislamu akikosa maji basi ameruhusiwa na sheria kutumia mchanga ili afanye tayamamu. Hivyo, ikiwa maji hakuna utatumia vumbi au mchanga kwa ajili ya kushika wudhuu na kisha kuswali.



Lakini tunayofahamu kama wewe ni dereva na unapoanza kazi zako unatokea nyumbani kwako, basi hatuoni kwanini unashindwa kuweka maji kwenye galoni na ukayachukua ndani ya daladala lako kwa ajili ya kutumia katika wudhuu? Hilo linawezekana kama ambavyo mnaweza kuweka maji ya akiba kwa ajili ya kujazia gari wakati yanapopungua! Tusitafute dharura ambazo si za msingi sana za kuifanya 'Ibaadah zetu ziwe ngumu. Na kwa hapo Ulaya ndio rahisi zaidi kwani kila pembe kuna sehemu zenye maji. Na ikiwa hakuna maji kabisa maeneo hayo, na akiba kwenye gari imekwisha kwa sababu moja au nyingine, basi rukhsa ya kutayamamu ipo hapo.



Ama sehemu kutosihi haipo katika Uislamu kwani ardhi yote imejaaliwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kuwa ni twahara. Kwa hiyo, Muislamu akifikiwa na wakati wa Swalah anaweza kuswali popote ila tu ikiwa ataona najisi ya dhahiri. Hivyo usitie wasiwasi kabisa kuhusu sehemu ya kuswalia.



Na pia kuna uwezekano wa kuchukua wudhuu katika maeneo vilivyopo vyoo huko kwenye vituo vya ma-bus au daladala kwa inavyojulikana, na hata humo mnapoanzia kuchukua daladala. La kufanya ni kuingia na kikombe chako cha kutumia na kutupa 'disposable cups' na kutumia kuwekea maji na kujisafisha nayo baada ya kujisadia, kisha ukaenda kuchukua wudhuu kwenye beseni (sink) zilizopo nje ya vyoo na ukifika sehemu ya miguu na ikiwa unachelea kuweka miguu yako kwenye hizo beseni kwa kuwa utawakera wengine ambao si Waislam, unaweza kupaka maji juu ya viatu vyako au soksi zako na ukaswali nazo, kwa sharti tu uhakikishe kuwa ulishanuia kufanya hivyo na kuchukua wudhuu wote na miguu kabla hujaamua kupangusa hivyo viatu au soksi baadaye (unaweza kuchukulia huo wudhuu kamili nyumbani kabla hujatoka, kisha baadaye utakuwa unapungusa tu juu ya viatu au soksi ukiwa uko kazini au njiani).

Soma Swali katika kifungo kifuatacho upate maelezo ya kuchukua wudhuu huo unaoitwa mashul-kufayn (kupangusa juu ya soksi/viatu):

Mtu Mgonjwa (Kilema) Afanye Wudhuu Vipi Na Aswali Vipi?

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akufanyie sahali suala lako hilo na Awafanye waajiri wenye kukupatia wakati muafaka wa kuweza kufanya kazi kwa njia nzuri na kuabudu kwa wakati wake. Na ukiwa na nia yote hayo yatakuwa mepesi kwa uwezo wa Allaah.

Na Allaah Anajua zaidi
 
Vipi Kukidhi Swalaah Kama Shida Kuswali Kazini?
Maswali: Hukmu Za Swalah




SWALI:
Asalam aleykum.

Samahani kama nilivyotuma haikuwa hivyo, mimi niliona nitume pamoja kwa kuwa yote yalikuwa yanahusu sala.

Mimi natoka nyumbani saa moja na nusu asubuhi baada ya kusali subhi, nakwenda kazini, narudi saa kumi na moja na nusu, swala ya dhuhuri na Asri zinanikuta kazini, je baada ya kufika nyumbani naweza kuzisali hizi ambazo sikuweza kuzisali kwa wakati wake? kwa sababu kazini sipati muda wa kusali na sehemu ya kusalia pia hakuna, sasa nifanyeje ili niweze kuzisali hizi sala ambazo zimenipita?

Mungu awabariki katika kazi hii ngumu



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaana wa Ta'aala) Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.

Kuswali kwa wakati wake ni jambo Aliloliamrisha Allaah (Subhaana wa Ta'aala) kama Anavyosema:

َ (( إِنَّ الصَّلاَةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا))

((Kwani hakika Swalah kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu))) [An-Nisaa:103]

Na ndio maana hata mtu anapokuwa katika hali ya ugonjwa anatakiwa aswali japo kwa kukaa au kwa kulala kwa jinsi ilivyo muhimu kutimiza Swalah kwa wakati wake.

Hivyo Muislamu inampasa afanye kila juhudi aweze kutimiza Swalah zake kwa kuswali kila kipindi cha Swalah kinapowadia hata kama yuko kazini au hata kama yumo safarini, mfano katika basi au treni na anakhofu kuwa atakapofika anakoelekea, wakati utakuwa umeshatoweka.

Bila shaka kazini utakuwa unao muda wa kupumzika, hivyo ni bora kuutumia kwa kutimiza ibada yako ya fardhi. Na kupata wakati kazini hatudhani kama ni shida kokote ulipo haswa ikiwa ni nchi za Kiislamu. Na hata nchi za kikafiri, inavyojulikana kuwa kuna haki za kupewa wakati wa kuswali na hata sehemu nyingine Waislam wanatengewa sehemu ya kuswalia. Ni juhudi ya mtu binafsi kuuliza, kuomba ili apewe haki yake. Na ikiwa hapatiwi haki yake hiyo basi hadi kuna uwezekano wa kupeleka malalamiko yake kwa vyama vya wafanyakazi makazini au kwa wanasheria (Lawyers). Mfano nchi za Amerika ya Kaskazini wako ndugu zetu wa Kiislamu wanaogombania haki kama hizo nao wanajulikana kama CAIRCAN. Kwa faida ya wanaoishi nchi hizo wanaweza kuingia katika kiungo kifuatacho kuweza kuwasiliana nao kwa matatizo yoyote yanayohusiana na dini yao:

Homepage - NCCM (CANADA)

Meilleur site de rencontre sérieux : comparatif et classement 2020 (USA)

Ikiwa umeshindwa baada ya juhudi zote kupata kuswali Swalah zako kwa wakati, basi utaweza kupata ruhusa ya kuunga Swalah ya Adhuhuri na Alasiri; ambazo zitakuwa ni Jam'u taqdiym (Kuswali Adhuhuri na Alasiri wakati wa Adhuhuri), au ukachelewesha Jam'u taakhiyr (Kuswali Adhuhuri na Alasiri wakati wa Alasiri). Zote utaziswali kikamilifu yaani Rakaa nne za Adhuhuri na Rakaa nne za Alasiri. Hii ni kutokana na dalili ya Hadiyth ifuatayo:

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال : صلَّى رسول الله صلى الله عليه وسلم الظهر والعصر جميعا بالمدينة في غير خوف ولا سفر ، قال أبو الزبير : فسألت سعيداً – أي : ابن جبير - لم فعل ذلك ؟ فقال : سألت ابن عباس كما سألتني فقال : أراد أن لا يحرج أحداً من أمَّته ( مسلم)

Imetoka kwa ibn 'Abbas (Radhiya Allahu 'anhumaa) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliswali (Swalah ya) Adhuhuri na Alasiri pamoja alipoikuwa Madiynah wakati hakukuwa na khofu wala hakuwa katika safari". Akasema Abu Az-Zubayr: "Nikamuuliza Sa'iyd (yaani ibn Jubayr) kwa nini alifanya hivyo?" Akasema: "Nilimuuliza ibn 'Abbaas swali hilo hilo na akasema: "Hakutaka mtu yeyote katika Ummah wake apate shida" [Muslim]

Lakini jaribu sana isiwe ni mazoea ya kila siku kufanya hivyo ujitahidi uwezavyo kuswali kila Swalah kwa wakati wake.

Na Allah Anajua zaidi
 
Anapitwa Na Swalaah Ya Magharibi Kila Siku
Maswali: Hukmu Za Swalah
SWALI:




A/Alaykum

Natumai hamjambo na mnaendelea vizuri na kazi zenu za kila siku Nashkuru kwa kutuwekea website hii ambayo inatuelimisha mambo mengi sana inshaallah M/Mungu atakujaalieni kila kheri Duniani na kesho Akhera Swali langu hivi?




Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu Daresalaam, muda wetu wa kuingia darasani ni saa 10 kamili jioni mpaka saa 2:00 usiku, kwa hiyo sala ya saa 10 na magharibi inanipita jee naweza kuzilipa kwa sala ya insha zote hizo?

Naomba nijibiwe





JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako hilo kuhusu kulipa Swalah. Hili ni swali ambalo linakaririwa sana kila wakati lakini jibu lake ni sahali sana. Hakika isiyopingika ni kuwa wengi wetu bado hatujakomaa kiimani na tuna udhaifu mkubwa kwa kushindwa hata kutimiza wajibu wa Allaah Aliyetukuka.

Allaah Aliyetukuka Anasema:




“Kwani hakika Swalah kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalumu” (4: 103).




Hivyo jibu ni kuwa haiwezekani kabisa kuwa kila siku wewe unalipa Swalah za Alasiri na Magharibi.


Licha wewe unasoma sehemu ambayo Waislamu ni wengi, wengine wanaosomea Chuo cha kikafiri katika nchi ya makafiri kusiko hata na kutambulika haki za Kiislam kama huko ulipo, na walikuwa wanaingia kuanzia saa tatu hadi Magharibi lakini hawakuwa wakikosa Swalah hizo kwa wakati wake.




Muhimu ni wewe kujipanga na kutoka kwa ajili ya Swalah pindi inapofika. Na kwa kuwa upo Dar es Salaam huenda ikawa Swalah ambayo utatoka darasani ni moja tu, Magharibi. Swalah ya Alasiri huwa inaingia mapema kwa maeneo ya pwani huenda ikawa inaingia kabla ya saa kumi. Unachotakiwa kufanya ni kupata nyakati za Swalah kwa eneo la Dar kwa mwaka mzima. Ukawa unatazama wakati wa kuingia Swalah, na ikiwa inaingia kabla ya saa kumi swali Swalah ya Alasiri kisha nenda darasani.




Na inapofika wakati wa Magharibi toka darasani pata mahali nje ya darasa na uswali Swalah yako kisha urudi darasani. Hutakosa mengi yaliyozungumzwa na mwalimu huyo katika somo hilo.




Ama ukiwa umebanwa sana unaweza baadhi ya siku ukaunganisha Magharibi na ‘Ishaa katika wakati wa ‘Ishaa ukiziswali zote kamili; yaani Magharibi rakaa tatu na ‘Ishaa rakaa nne.




Ingia katika kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:




Vipi Kukidhi Swalah Kama Shida Kuswali Kazini?




Hapati Kuswali Kwa Wakati, Kila Siku Anakidhi Swalah




Tunakuombea tawfiki ya kuweza kutekeleza ‘Ibaadah hiyo kwa wakati wake.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Anaswali Na Kuacha Lakini Anasoma Qur-aan Je, Anahukumiwa Vipi?
Maswali: Hukmu Za Swalah


SWALI:




Naomba munifafanulie, je ikiwa Muislam anaacha Sala mara kwa mara, mara atasalii mara hasali, lakini anapenda



sana kusoma Quraan takriban siku zote kila wakati anapopata nafasi. Je, ana malipo gani kwa mola mtu huyu?







JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola i wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako hilo zuri. Hakika ni kuwa kusoma Qur-aan kuna fadhila kubwa sana kwani Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusoma herufi kutoka kwa Kitabu cha Allaah atapata ujira mmoja, na ujira huu ni sawa na kumi mfano wake. Wala sisemi kuwa Alif Laam Miym ni herufi moja lakini Alif ni herufi na Laam ni herufi na Miym ni herufi” (At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh na ameipokea ad-Daarimiy nayo ni Sahihi). Qur-aan haifai kusomwa tu bali inatakiwa ifahamike na itiwe katika maisha kwa kufuata kimatendo. Hakika ni kuwa wenye kushikamana nayo wameokoka na wamefaulu na wenye kupuuza wamehiliki na wamepata hasara.


Ni ajabu kuwa Muislamu mfano wa huyu atapenda kuisoma Qur-aan lakini kukosa kuifuata. Tufahamu kuwa huyu Muislamu bado ana Imani hivyo ni juu yetu na yako kujaribu kumlingania ili arudi katika njia ya sawa na haki, Uislamu. Kusoma huko Qur-aan bila kuswali hakumnufaishi yeyote yule kwa chochote ila atubu na kujirekebisha.


Swalah ina fadhila kubwa sana, hivyo kukosa kuswali ni kosa kubwa. Swalah ni amali ya kwanza itakayokaguliwa Siku ya Qiyaama na ndio ufunguo wa Pepo. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Faradhi ya mwanza atakayoulizwa Muislamu Siku ya Qiyaama kuwa kaitekeleza – na kaitekeleza vilivyo – ni Swalah. Ikiwa aliitekeleza vilivyo basi kunatarajiwa atafaulu. Ikiwa hakuitekeleza au kaitekeleza, lakini sivyo ndivyo, basi itatazamwa Swalah za Sunnah, na alizileta vilivyo … Ama ikiwa hana hata Sunnah au kaitekeleza sivyo ndivyo, basi keshapata khasara” (Ahmad, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaaiy na Ibn Maajah).

Amesema tena (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

“Funguo za kufungulia milango ya Peponi ni Swalah” (Muslim).


Ubaya wa kuacha Swalah ni mkubwa sana kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anasema:

“Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha Swalah, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kuta malipo ya ubaya” (19: 59).

Na pia: “Ni nini kilichokupelekeni Motoni? Waseme: Hatukuwa miongoni waliokuwa wakiswali” (74: 42 -43).

Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Kizuizi kilichoko baina ya mtu na ukafiri ni Swalah” (Muslim).

Pia: “Tofauti baina yetu Waislamu na wasio Waislamu ni Swalah” (Abu Daawuud, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah).


Hivyo, tumeona kuwa kukosa kuswali kunafanya amali za Muislamu zote kupomoka na kutokuwa na faida yoyote. Lakini mkosa akitubia na kufanya matendo mazuri malipo yake yatakuwa makubwa. Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anasema:


“Isipokuwa waliotubu, wakaamini, na wakatenda mema. Hao, basi, wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa chochote” (19: 60).



Tafadhali ingia katika kiungo kifuatacho usome makala muhimu kabisa zinazohusu Swalah, makatazo ya kuacha kuswali, adhabu zake n.k na tunakupa nasaha kuwa usiache kabisa kuswali kwani hatari ya kuacha kuswali ni kubwa mno kama utakavyosoma katika hizi makala.


Swalah


Na Allaah Anajua zaidi
 
Anaswali Swalaah Zote Mpaka Tahajjud, Ila Swalaah Za Asubuhi Zinampita
Maswali: Hukmu Za Swalah
SWALI:



Alhamdulilah namshukuru mola kwa kunipa afya na kidogo japo si sana elimu ya dini yetu, nasali na napanda sana mambo ya dua na kujisomea Qur'an kila mara. Ninasali alhamdulilah lakini tatizo langu ni sala ya subhi, yaani ni mtihani, kila njia najaribu nashindwa. Naomba msaada ila sala za tahajud na sunna za usiku naamka ila subhi labda mara 4 mpaka 5 kwa mwezi.



jazaka Allahu







JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.






Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuswali Tahajjud lakini kukosa Swalah ya Subhi.





Uislamu na sheria zake zimeipatia kipaumbele ‘Ibaadah za fardhi mwanzo kabla ya za Sunnah. Ikiwa utakuwa unafanya ya Sunnah na kushindwa ya fardhi basi itakuwa hujafanya lolote. Inavyotakikana ni kutanguliza ya Fardhi kwanza kisha Sunnah, na ni bora zifuatane zote kwa pamoja; yaani Fardhi na Sunnah uzitekeleze sambamba. Isiwe unafanya pia ya Fardhi ukawa umeridhika kabisa na ukaacha ya Sunnah.



Hadiyth hii ifuatayo inatuonyesha umuhimu mkubwa sana wa Swalah za Fardhi:

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) anatuelezea kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi aalihi wa sallam) amesema: Imepokelewa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye alisema kwamba: Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema ((Kitu cha kwanza kinachohesabiwa katika ‘amali za mja wa Allaah siku ya Qiyaamah ni Swalah zake. Zikiwa zimetimia, hapo tena atakuwa kaneemeka na kafuzu, na zikiwa zina kasoro atakuwa kaanguka na kala khasara. Ikiwa pana upungufu katika Swalah zake za fardhi Allaah ‘Azza wa Jallaَ Atasema: Angalia ikiwa mja Wangu ana Swalah zozote za Sunnah ambazo zinaweza kufidia zile zilizopungua, hapo tena ‘amali yake iliyobaki itaangaliwa hivyo hivyo)) [At-Tirmidhiy, Abu Daawuud, An-Nasaaiy, Ibn Maajah na Ahmad]

Nasaha yetu ni kuwa ujitahidi sana kuswali Swalah ya Subhi mwanzo. Na hilo linaweza kufikiwa kwa kufuata moja katika ya haya mambo:



1. Inuka kwa ajili ya Swalah ya Tahajjud nyakati zake za mwisho karibu sana na Subhi, ili ukimaliza Sunnah uswali Swalah ya Fardhi.



Punguza kuinuka kuswali Swalah ya usiku ili upate nafasi ya kulala vya kutosha na kuinuka kwa ajili ya Subhi.




Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:





Kutimiza Swalah Za Fardhi Kabla Za Sunnah







Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akupe hima na Akuwezeshe uswali Swalah zote – mwanzo za Fardhi na kisha ya Sunnah bila tatizo lolote.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Kutimiza Swalaah Za Fardhi Kabla Za Sunnah
Maswali: Hukmu Za Swalah





SWALI LA KWANZA

inafaa kuunga swala ya magharibi pamoja na ishaa kwa ajili ya tahajjud?



SWALI LA PILI

As salaam alaikum,ndugu zangu waislam alhidaaya,swali langu ninalopenda kuuliza ni kama ifuatavyo mimi naishi ktk nchi za ulaya magharibi,swala ya magharib huiswali usiku kutokana na kuzama kwa jua,je naweza kuswali na swala ya isha? Baada nikisha swalimaghrib?Nia na madhumuni niamke usiku ili niswali Tahjudd.Ambayo hii swala tumeambiwa tuswali usiku mwingi,kisha wakati huo nikimaliza swala yangu ya Tahjudd Alfajir nayo inakuwa imeingia.Je inawezekana kufanya hivyo?Wabilah taufiq.







JIBU:

Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Ibada ya Swalah, ni kati ya ibada zilizowekewa nyakati maaluum,

Anasema Allah, "Hakika ya Swalah kwa Waislam ni faradhi iliyowekewa nyakati makhsusi" (An-Nisaa: 102)

Na anasema Ibnu Mas'uud (radhiya Allahu 'anhu) nilimuuliza Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni jambo gani linalopendwa zaidi na Mwenyeezi Mungu? Akasema ni kuitekeleza ibada ya Swalah ndani ya wakati wake" Al-Bukhaariy Hadiyth Namba 527 na Muslim Namba 85.

Kwa maana hiyo unatakiwa uiswali kila Swalah katika wakati wake kama ulivyoainishiwa na Qur-aan na mafunzo sahihi ya Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ama sababu za kukusanya Swalah, kuiakhirisha, au kuiqadimisha, zimewekwa wazi katika vitabu vya fiqhi kama vile kuruhusiwa katika safari au wakati wa dhurufu fulani, lakini sio kwa kufanya ni kawaida ya Muislamu kwa ajili ya kufadhilisha Swalah ya Sunnah wakati ya fardhi ndio muhimu zaidi.

Na Allah Anajua zaidi
 
Back
Top Bottom