Ramadhan Special Thread
005-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kauli Za Maimaam Wanne Kuhusu Kushikamana Na Sunnah Na Kuacha Kufuatwa Rai Zao


KAULI ZA MAIMAAM WANNE KUHUSU KUSHIKAMANA NA SUNNAH NA KUACHA KUFUATA RAI ZAO



Itakuwa ni manufaa makubwa ikiwa tutazieleza baadhi ya kauli zao hapa, kwani labda hii itamuonya mtu au itawakumbusha wale ambao wanafuata rai za Maimaam au madhehebu maalum, bali wanaofuata kwa upofu wale Waalimu au Mashaykh na wale walio chini ya daraja ya hao Maimaam wanne wakubwa[1] wakishikilia madhehebu yao au rai zao kama kwamba zimeteremeshwa kutoka mbinguni! Na hali Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

((اتَّبِعُواْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلاَ تَتَّبِعُواْ مِن دُونِهِ أَوْلِيَاء))

((Fuateni mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake))[2]





WASEMAVYO MAIMAAM



1) ABU HANIYFAH (رحمه الله)

Wa kwanza wao ni Abu Haniyfah Nu'maan bin Thaabit.

Wafuasi wake wamesimulia kauli zake mbali mbali pamoja na maonyo tofauti ambayo yote lengo lake ni moja, nalo ni: Wajibu wa kuikubali Hadiyth na kuachilia mbali kufuata rai za Maimaam ambazo zinakhitilafiana nayo.

"Ikiwa Hadiyth imeonekana kuwa ni Swahiyh, basi hiyo ndiyo madhehebu yangu"[3]
"Hairuhusiwi[4] kwa mtu yeyote kukubali rai zetu ikiwa hawatojua wamezipata kutoka wapi"[5]
Katika usimulizi mwengine:"Imekatazwa[6] mtu ambaye hajui dalili zangu kutoa hukmu[7] kutokana na maneno yangu"

Usimulizi mwengine imeongezwa: "…Kwani sisi ni wanaadamu, tunasema jambo siku moja na kulirudisha (kulikataa) siku ya pili yake".

Na katika usimulizi mwengine: "Ole Ewe Ya'quub![8] Usiandike kila kitu unachosikia kutoka kwangu kwani huwa natoa rai moja leo na kesho huikataa. Au hutoa rai moja kesho na kuikataa keshokutwa".[9]

"Ninaposema jambo linalokhitilafiana na kitabu cha Allaah (سبحانه وتعالى) au yaliyosimuliwa na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi mpuuze kauli yangu".[10]




2) MAALIK BIN ANAS (رحمه الله)

Imaam Maalik bin Anas yeye amesema:

"Hakika mimi ni mwanaadamu: Ninafanya makosa (mara nyingine) na ninakuwa sahihi (mara nyingine). Kwa hiyo, tazameni rai zangu: zote ambazo zinakubaliana na Kitabu (Qur-aan) na Sunnah, zikubalini; na zote ambazo hazikubaliani na Kitabu (Qur-aan) na Sunnah, basi zipuuzeni". [11]


"Kila mmoja baada ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), atakuwa na kauli yake itakayokubaliwa na kukataliwa, isipokuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)" [12]


Ibn Wahb amesema: "Nilimsikia Maalik akiulizwa kuhusu takhliyl ya vidole vya miguu (kuvichanganua vidole ili kupitisha maji) wakati wa wudhuu. Akasema: "Watu si lazima kufanya hivyo". Sikumkaribia hadi zogo la watu lilipopunguka. Nilipomwambia: "Tunajua kuwa ni Sunnah kuhusu jambo hilo". Akasema: "Jambo gani hilo? Nikasema: "Layth bin Sa'd, Ibn Lahiy'a na 'Amr bin Al-Haarith wamesimulia kwetu kutoka kwa Mustawrid bin Shaddaad Al-Quraishiy ambaye amesema: "Nilimuona Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akisugua baina ya vidole vyake vya miguu kwa kidole chake kidogo". Akasema: "Hadiyth hii ni Hasan (njema); sikuwahi kuisikia abadan ila leo". Kisha baadaye nikamsikia akiulizwa kuhusu jambo hili hili, naye akaamrisha kufanya takhliyl ya vidole vya miguu"[13]




3) ASH-SHAAFI'IY (رحمه الله)

Ama kutoka kwa Imaam Ash-Shaafi'iy, kauli zake zilizonukuliwa ni nyingi na nzuri mno.[14] na wafuasi wake walikuwa ni bora kabisa katika kufuata.



"Sunnah za Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) zinamfikia na kumkwepa kila mmoja wetu. Kwa hiyo kila ninapotaja rai yangu au nikiunda sheria, na ikiwa ipo dalili kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), inayopinga rai yangu, basi rai iliyo sahihi ni aliyosema Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na hiyo ndio rai yangu"[15]


"Waislamu wamekubaliana pamoja kwamba ikiwa Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) imebainishwa dhahiri kwa yeyote, hairuhusiwi[16] kwake kuiacha kwa kufuata kauli ya mwengine yeyote[17]


"Ukiona katika maandishi yangu jambo ambalo ni tofauti na Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi zungumza kwa kurejea Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na acha niliyoyasema mimi". Katika usimulizi mwengine: "…basi ifuate (Sunnah) na usitazame tena pembeni kufuata kauli ya mwengine yeyote"[18]


Hadiyth ikipatikana kuwa ni Swahiyh, basi hiyo ndiyo madhehebu yangu"[19]


"Wewe (Imaam Ahmad)[20] ni mwenye elimu zaidi kuhusu Hadiyth kuliko mimi. Kwa hiyo Hadiyth ikiwa ni Swahiyh basi nijulishe, ikiwa ni kutoka Kufah, Basrah au Syria, ili nichukue rai ya Hadiyth madamu tu ni Swahiyh"[21]


"Katika kila jambo, ambako wenye kusimulia wakipata ripoti kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ambayo ni kinyume na niliyoyasema, basi narudisha kauli yangu nyuma, ikiwa wakati wa maisha yangu au hata baada ya kufa kwangu"[22]


"Ukinisikia nasema kitu, na kinyume chake ni Hadityh Swahiyh kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi tambua kuwa akili yangu imetoweka"[23]


"Kwa kila ninalosema, ikiwa upo usimulizi ulio Swahiyh, basi Hadiyth ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) inakuja mwanzo, kwa hiyo usifuate rai yangu"[24]


"Kila kauli kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ni rai yangu pia, japokuwa hujaisikia kutoka kwangu"[25]




4) AHMAD BIN HANBAL (رحمه الله)



Imaam Ahmad alikuwa wa mbele miongoni mwa Maimaam kukusanya Sunnah na kuzishikilia sana hadi alichukizwa kuona kinaandikwa kitabu kilichokusanya mambo yaliyogeuzwa na mambo yaliyotegemea rai zaidi[26] kwa hilo akasema:



Msifuate rai yangu, wala msifuate rai ya Maalik, au Ash-Shaafi'iy au ya Awzaa’iy, wala Ath-Thawriy, lakini chukueni kutoka kule walikotoa"[27]
Katika usimulizi mmoja: "Msiige dini yenu kutoka kwa mtu yeyote katika hawa, bali chochote kilichotoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake, chukueni, kisha kwa At-Taabi'iyn (Waliofuata) ambako mtu ana khiari".

Mara moja kasema: "Kufuata[28] ina maana kwamba mtu anafuata yaliyokuja kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake, ama baada ya At-Taabi'iyn (Waliofuata) anayo khiari" [29]

"Rai ya Awzaaiy, rai ya Maalik, rai ya Abu Haniyfah, zote ni rai, na ni sawa katika macho yangu. Lakini, dalili ni yale masimulizi kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake"[30]


"Yeyote atakayekanusha kauli ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) basi yumo katika ukingo wa kuangamia"[31]
Hizi ndizo kauli za wazi kabisa za Maimaam, Allaah (سبحانه وتعالى) Awe radhi nao, kuhusu kushikamana na Hadiyth na kukataza kufuata rai zao bila ya kuwa na dalili iliyo dhahiri kabisa.

Kwa hiyo, yeyote aliyeshikamana na lolote la Sunnah ambayo imeshuhudiwa kuwa ni Swahiyh hata kama imepinga kauli ya baadhi ya Maimaam, hatokuwa anapingana na madhehebu yao, wala hatopotoka katika njia zao, bali mtu huyo atakuwa anawafuata wote na atakuwa amekamata kile kilichoaminiwa zaidi akishika mkono ambao hautavunjika. Lakini hii haitakuwa hali ya yule anayeziweka kando Sunnah Swahiyh kwa sababu tu zimepingana na rai za Maimaam, bali mtu huyo atakuwa sio mtiifu kwao na amepingia kauli zao hizo za juu. Na tunaona Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

((فَلاَ وَرَبِّكَ لاَ يُؤْمِنُونَ حَتَّىَ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لاَ يَجِدُواْ فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُواْ تَسْلِيمًا))

((La! Naapa kwa Mola! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenyekee kabisa.))[32]

((فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ))

((Basi na watahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu iumizayo))[33]



Haafidhw Ibn Rajab Al-Hanbali (رحمه الله) amesema: "Kwa hivyo ni wajibu kwa mtu yeyote anayesikia amri ya Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) au kuijua, kuielezea kwa Ummah, kuwapa nasaha ya dhati na kuwaamrisha kufuata amri zake japo kama itakuwa ni kinyume na rai ya mtu mkubwa. Hii ni kwa sababu hukmu ya Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ina haki zaidi kuheshimiwa na kufuatwa kupita rai za mtu yeyote mkubwa aliyekwenda kinyume bila ya kujua na amri za Mtume katika jambo lolote. Ndio maana Maswahaba na waliofuatia walimpinga yeyote aliyekwenda kinyume na Sunnah Swahiyh, mara nyingine wakiwa wakali katika kuwapinga kwao[34], sio kutokana na kumchukia huyo mtu, bali alikuwa ni mpenzi wao na mwenye kuheshimiwa, lakini kwa sababu Mjumbe wa Allaah alikuwa mpenzi wao zaidi na amri zake zilikuwa juu ya amri za viumbe wengine. Hivyo inapokuwa amri ya Mtume na ya mtu mwengine zinapingana, amri ya Mtume huwa ndiyo ipasayo kutiliwa nguvu na kutekelezwa. Hakuna katika hili lingeliwazua wasimheshimu mtu waliyempinga kwa sababu wamejua kuwa atasamehewa[35] , bali aliyetajwa mwisho hatojali amri zake kupingwa itakapokuwa amri za Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) zimeonyesha dhahiri kuwa ni kinyume chake [36]

Vipi wachukiwe hayo ikiwa wamewajibisha wafuasi wa kama ilivyo, na kama tulivyoona, kuwa wameamrisha waziache kando rai zao zinazokwenda kinyume na za Sunnah. Bali Imaam ash-Shaafi'iy (رحمه الله) aliwaambia Maswahaba zake kuzihusisha kwake Sunnah zilizo Swahiyh pia, japo kama hakuzitekeleza au katekeleza zilizo kwenda kinyume nazo. Hivyo mhakiki Ibn Daqiyq alipokusanya pamoja katika mjalada mzito, mas-ala ambayo kila mmoja katika kauli za madhehebu ya Maimaam wanne kuwa yamekwenda kinyume na Hadiyth Swahiyh, kama alivyaondika mwanzoni mwake: "Imekatazwa kuhusisha majibu haya kwa Maimaam waliojitahidi na ni fardhi kwa wanasheria wanaofuata rai zao kujua hizi ili wasije kuzinukuu wakawazulia"[37]



Wafuasi Wa Maimaam Kuacha Rai Zao Ikiwa Zinapingana na Sunnah





Kutokana na yote tuliyotaja, wafuasi wa Maimaam, ((Fungu kubwa katika wa mwanzo Na wachache katika wa mwisho))[38] hawakubali rai za Imaam wao, bali wanazipuuza nyingi wanapotambua kuwa zinakenda kinyume na za Sunnah. Hata Maimaam wawili Muhammad Ibn Al-Hasan na Bu Yuusuf (رحمها الله) walikhitilafiana na Shekhe wao Abu Haniyfah 'Fiy Nahw thuluth al-madhhab'[39] kama vitabu vya masaail vinavyothibitisha. Imesemwa hivyo hivyo kuhusu Imaam Al-Muzaniy[40] na wafuasi wengineo wa Ash-Shaafi'iy na Maimaam wengine. Tungelianza kutoa mifano majadiliano yangeliendelea kuwa marefu na tungelitoka nje ya makusudio katika mas-ala utangulizi huu, hivyo tutajiwekea mipaka kwa mifano miwili:



1. Imaam Muhammad amesema katika Muwattwa yake[41] (Uk. 158). "Ama Abu Haniyfah hakuona kuwa kuna Swalah ya kuomba mvua, lakini kauli yetu ni kwamba Imaam anaswali Rakaa mbili na anaomba du'aa na anashika shuka yake…"



2. Tunaye 'Iswaam bin Yuusuf Al-Balkhiy mmoja wa wafuasi wa Imaam Muhammad[42] na mtumishi wa Imaam Abu Yuusuf[43] ambaye akitoa hukmu kinyume na Imaam Abu Haniyfah kwa sababu hakujua ushahidi wake na ushahidi mwingine ulijitokeza kwake wenyewe hivyo alikuwa akiutolea hukmu:[44] . Hivyo alinyanyua mikono katika rukuu (kwenye Swalah) na anaponyanyuka[45] kama ilivyo mutawaatir Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) bali Maimaam wake watatu (yaani Abu Haniyfah, Abu Yuusuf na Muhammad) wamesema vinginevyo na hawakumzuia kutekeleza Sunnah. Huu ni mfano ambao kila Muislamu inampasa kuwa nao kwani tumeshaona kutokana na ushahidi wa Maimaam wanne na wengineo huko juu.











[1] Hii ni aina ya taqliyd (kufuata kwa upofu [kiujinga]) ambayo Imaam At-Twahaawiy alihusisha aliposema: "Hafuati rai ila ni mtu mkaidi au mjinga" (kufuata kama kipofu)

[2] Al-A'raaf:3

[3] Ibnul-'Aabidiyn katika al-Haashiyah (1/63) na katika inshaa yake Rasm al-Mufti (1/4 kutoka Mkusanyiko wa Inshaa za Ibnul-'Aabidyin). Shaykh Swaalih Al-Fulaaniy katika al-Iyqaadhw al-Himaam (uk.62) na wengineo. Ibnul-'Aabidiyn amenukuu kutoka Sharh al-Hidaayah ya Ibn Al-Shahnah Al-Kabiyr, mwalimu wa Ibn Al-Himaam, kama ifuatavyo:

"Ikiwa Hadiyth iliyo kinyume na Madhehebu imeonekana kuwa ni Swahiyh basi mtu atende kwa kufuata hiyo Hadiyth na aifanye kuwa ni madhehebu yake. Kuifanyia kazi Hadiyth hakutombatilisha mtu kuwa sio mfuataji wa madhehebu ya Hanafi, kwani imeripotiwa kuwa Abu Haniyfah alisema: "Ikiwa Hadiyth imeonekana kuwa ni Swahiyh, basi hiyo ndiyo madhehebu yangu". Na hii imeelezewa na Imaam Ibn 'Abdil-Barr kutoka kwa Abu Haniyfah na kutoka kwa Maimaam wengine".

Hii ni sehemu ya ukamilifu wa elimu na uchaji Allaah wa Maimaam, kwani wameonyesha kwa kusema kwamba wao hawakuwa na maarifa (elimu) kamili ya Sunnah zote. Na Imaam Ash-Shaafi'iy amefafanua wazi wazi (tazama mbele). Hutokea wanapokwenda kinyume na Sunnah huwa ni kwa sababu hawakuitambua. Ndipo walipotuamrisha tushikilie Sunnah na tuizingatie kuwa ni sehemu ya madhehebu yao. Allaah Awashushie Rahma Yake kwao wote.

[4] Sio halaal

[5] Ibn 'Abdil-Barr katika Al-Intiqaa' fiy Fadhwaail Ath-Thalaathah Al-Aimmah Al-Fuqahaa (uk.145), Ibn Al-Qayyim katika 'I'laam Al-Muwaqi'iyn (2/ 309), Ibn 'Aabidiyn katika tanbihi zake kwenye Al-Bahr Ar-Raa'iq (6/ 293) na katika Rasm Al-Mufti (uk. 29, 32) na Sha'raaniy katika Al-Miyzaan (1/ 55) pamoja na usimulizi wa pili. Usimulizi wa mwisho ulikusanywa na 'Abbaas Ad-Dawriy katika At-Taariykh ya Ibn Ma'iyn (6/ 77/1) ikiwa na Isnaad Swahiyh kutoka kwa Zafar, mwanafunzi wa Imaam Abu Haniyfah. Usimulizi uliofanana upo kutoka kwa wafuasi wa Abu Haniyfah; Zafar, Abu Yuusuf na 'Aafiyah bin Yaziyd; taz. Al-Iyqaadhw (uk. 52). Ibn Al-Qayyim alithibitisha kwa nguvu usahihi wake kutoka kwa Abu Yuusuf katika I'laam Al-Muwaqi'yn (2/ 344). Nyongeza ya usimulizi wa pili unarejewa na mwandishi wa Al-Iyqaadhw (uk. 65) kwa Ibn 'Abdil-Barr, Ibn Al-Qayyim na wengineo.

Ikiwa hivi ndivyo wanavyosema kwa mtu asiyejua dalili zao, jibu lao litakuwa nini kwa yule anayetambua kuwa dalili zinapingana na kauli yao, lakini bado anatoa hukumu iliyopinga dalili? Kwa hiyo, fuata usemi huu, kwani pekee unatosheleza kuvunja ufuataji rai kwa ujinga. Ndio maana nilipomlaumu mmoja wa Mashaykh (Muqallid) wa madhehebu katika kutoa fatwa (hukm) kwa kutumia maneno ya Abu Haniyfah bila ya kujua dalili, aligoma kuamini kuwa hiyo ni kauli ya Abu Haniyfah!



[6] Haraam

[7] Fatwa

[8] Mwanafunzi mashuhuri wa Imaam Abu Haniyfah, Abu Yuusuf (رحمه الله)

[9] Hii ni kwa sababu Imaam kawaida hutoa rai yake kutokana na Qiyaas (analojia). Kisha tena hupata analojia iliyo na nguvu zaidi, au Hadiyth ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) humfikia. Kwa hiyo huikubali hiyo na kuipuuza rai yake ya nyuma. Maneno ya Sha'araaniy katika Al-Miyzaan (1/62) yamewekwa kwa mukhtasari kama ifuatavyo:

"Imani yetu na ya kila mtafiti wa Imaam Abu Haniyfah (رحمه الله) ni kwamba, aliishi hadi iliporikodiwa Sharia. Na safari za wahifadhi wa Hadiyth katika miji mbali mbali na mipakani kwa ajili ya kukusanya na kuzipata. Angeliipokea na kupuuza analojia zote ambazo alizozitumia, idadi za Qiyaas katika madhehebu yake zingelikuwa kidogo kama zilivyo katika madhehebu mengine. Lakini kwa vile dalili za Sharia zimetapakaa kwa Waliotangulia na waliowatangulia, na haizikukusanywa wakati wa maisha yake, ilihitajika kuwepo Qiyaas nyingi katika madhehebu yake kulingana na Maimaam wengine. Maulamaa wa baada ya hapo, kisha wakafanya safari kutafuta na kukusanya Hadiyth kutoka nchi mbali mbali na miji na wakaziandika. Hivyo baadhi ya Hadiyth za Sharia zimeelezea nyingine. Hii ni sababu ya kuweko idadi kubwa ya qiyaas katika madhehebu yake wakati kwenye madhehebu mengine ilikuwa ni idadi ndogo"

Abul-Hasanaat Al-Laknawiy amenukuu maneno yake kikamilifu katika An-Naafi' Al-Kabiyr (uk. 135) akiandika na kupanua tanbihi zake. Kwa hiyo yeyote anayependa kutafuta maelekezo yake afanye humo.

Kwa vile hii ni uthibitishaji kuwa kwa nini Abu Haniyfah mara nyingine alikhitilafiana na Hadiyth zilizokuwa Swahiyh bila ya kukusudia na ni sababu barabara ya kukubaliwa, kwani Allaah Haikalfishi nafsi kwa yale isiyoweza kubeba. Hairuhusiwi kumtukana kwa sababu hiyo kama walivyofanya watu wajinga. Bali ni wajibu kumheshimu, kwani yeye ni mmoja wa Maimaam wa Waislamu ambao wameihifadhi hii dini hadi ikafikishwa kwetu kutoka katika kila matawi yake. Na kwa vile yeye analipwa (Na Allaah سبحانه وتعالى) kwa hali yoyote ile; ikiwa kapata au amekosea kwa kutokusudia. Wala hairuhusiwi kwa wafuasi wake wapenzi kuendelea kushikilia kauli zake ambazo zinakhitilafiana na Hadiyth zilizo Swahiyh kwani kauli hizo sio madhehebu yake kama kauli zake hapo juu zilivyosema. Kwa hiyo hii ni mipaka miwili; ukweli na uongo katika yake. ((Na waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala Usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu)) [Al-Hashr 59:10]

[10] Al-Fulaaniy katika Al-Iyqaadhw Al-Himaam (uk.50), ikifuatilia kwa Imaam Muhammad na kisha kusema: "Hii haimhusu Mujtahid, (mwenye kujitahidi kwa elimu yake na kutoa hukmu) kwa vile hakujifunga katika rai zao, bali inamhusu Muqallid (mwenye kufuata).



[11] Ibn 'Abdil-Barr katika Jaami'ul Bayaan Al-'Ilm (2/32), Ibn Hazm akinukuu kutoka kwake katika Uswuul-Al-Ahkaam (6/149) na hali kadhaalika Al-Fulaaniy (uk. 72).



[12] Hii inajulikana sana miongoni mwa Maulamaa wa baadaye kuwa ni kauli ya Maalik. Ibn 'Abdil-Haadiy alikiri kuwa ni Swahiyh katika Irshaad As-Saalik (227/1); Ibn 'Abdil-Barr katika Jaami'ul-Bayaan Al-'Ilm (2/91) na Ibn Hazm katika Uswuul Al-Ahkaam (6/145, 179) alisimulia kama ni kauli ya Al-Hakam bin 'Utaybah na Mujaahid; Taqiyud-Diyn As-Subki alisimulia katika Al-Fataawa (1/148) kama ni kauli ya Ibn 'Abbaas akishangazwa kwa uzuri wake kisha akasema: "Haya maneno yameanzia kwa Ibn 'Abbaas na Mujaahid, na Maalik (رحمه الله) aliyachukua, na akawa mashuhuri kwayo". Inavyoelekea kwamba Imaam Ahmad kisha akachukua kauli hii kutoka kwao, kama Abu Daawuud alivyosema katika Masaail ya Imaam Ahmad (uk 276). "Nilimisikia Ahmad akisema: Kila mmoja anapokelewa na anakatiliwa katika rai zake, isipokuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)"



[13] Kutoka kwa Utangulizi wa Al-Jarh wat-Ta'diyl ya Ibn Abi Haatim (uk. 31-32)



[14] Ibn Hazm anasema katika Uswuul al-Ahkaam (6/118)

"Hakika, Mafuqahaa wote ambao rai zao zilikuwa zikifuatwa zilipingwa kwa taqliyd na waliwakataza wafuasi wao kufuata rai zao kijinga. Aliyekuwa mkali kabisa miongoni mwao ni Ash-Shaafi'iy (رحمه الله), kwani yeye alirudia kutilia mkazo zaidi kuliko yeyote mwengine kufuata usimulizi ulio Swahiyh na kukubali dalili yoyote iliyoamriwa. Vile vile alidhihirisha wazi na kujitenga kuwa hana hatia ikiwa atafuatwa yeye tu pekee na aliwatangazia hayo wale waliokuwa naye. Tunaomba hii imnufaishe mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) na thawabu zake ziwe za juu kabisa kwani alikuwa ni sababu ya mema mengi".

[15] Imesimuliwa na Al-Haakim ikiwa ina isnaad ya kuendelea hadi kwa Ash-Shaafi'iy kama ilivyo katika Taariykh Dimashq ya Ibn 'Asaakir (15/1/3), I'laam Al-Muwaqi'iyn (2/363,364) na Al-Iyqaadhw (uk. 100)

[16] Halaal

[17] Ibn al-Qayyim (2/361) na Al-Fulaaniy (uk. 68)

[18] Al-Haraawiy katika Dhamm Al-Kalaam (3/47/1) Al-Khatiyb katika Al-Ihtijaaj bi Ash-Shaafi'iy (8/2), Ibn 'Asaakir (15/9/10), An-Nawawiy katika Al-Majmuu' (1/ 63), Ibn al-Qayyim (2/ 361), na Fulaani (uk. 100) usimulizi wa pili ni kutoka Hilyah Al-Awliyaa ya Abu Nu'aym.



[19] An-Nawawiy katika Al-Majmuu' (1/ 63), Sha'raaniy (1/ 57), akitoa chanzo chake kama Al-Haakim na Al-Bayhaqiy na Al-Fulaaniy (uk. 107). Ash-Sha'raaniy kasema: "Ibn Hazm kasema: "Kwamba imeonekana ni Swahiyh naye au kwa Imaam mwengine". Kauli yake nyingine imethibitisha ufahamu huu.

An-Nawawiy amesema: "Wafuasi wetu walitenda kutokana na hili katika mambo ya tathwiyb (mwito wa Swalah baada ya adhana), shuruti za kutoka katika ihraam kwa ajili ya ugonjwa, na mambo mengine yaliyojulikana vyema katika vitabu vya madhehebu. Miongoni wafuasi wetu ambao wameripotiwa kuwa walitoa hukumu kutokana na chanzo cha Hadiyth (yaani kuliko kuchukua kauli ya Ash-Shaafi'iy) ni Abu Ya'quub Al-Buwiity na Abul-Qaasim Ad-Daarikiy. Wafuasi wa Muhaddithiyn (Wakusanyao Hadiyth), Imaam Abu Bakr Al-Bayhaqiy na wengineo walitenda kwa kufuata kauli hii. Wafuasi wengi wetu wa zamani, walipokumbana na jambo ambalo ilikuweko Hadiyth na madhehebu ya Ash-Shaafi'iy yalikuwa ni kinyume nalo, basi walitenda kwa kufuata Hadiyth na kutowa fatwa (hukmu) pia wakisema: "Madhehebu ya Ash-Shaafi'iy ni kila kinachokubaliana na Hadiyth". Shaykh Abu 'Amr (Ibn Asw-Swalaah) alisema: "Yeyote miongoni mwa Ash-Shaafi'iy akiona Hadiyth inayopinga madhehebu yake, alichukulia kama alitimiza shuruti za Ijtihaad kwa kawaida, au katika maudhui au jambo lile khaswa ambalo alikuwa huru kutenda kwa kufuata Hadiyth; kama sio. Lakini hata hivyo aliona vigumu kupingana na Hadiyth baada ya utafiti zaidi, hakuweza kupata uthibitishaji wa kukinaisha wa kupinga Hadiyth. Kwa hiyo, alibakia kutenda kwa kufuata Hadiyth ikiwa Imaam mwengine mwenye kujitegemea mbali na Ash-Shaafi'iy, basi alitenda kuifuata. Na hii huwa ni kithibitisho chake cha kuacha madhehebu ya Imaam wake katika jambo hilo". Alichosema (Abu 'Amr) ni Swahiyh na lililokubalika. Na Allaah Anajua zaidi.

Kuna uwezekano mwingine ambao Ibn As-Swalaah alisahau kutaja: Afanyeje mtu ikiwa hakumpata mtu yeyote ambaye alitenda kwa kufuata Hadiyth? Hii imejibiwa na Taqiyud-Diyn As-Subkiy katika makala yake 'Maana Ya Kauli ya Ash-Shaafi'iy: Ikiwa Hadiyth ikipatikana kuwa ni Swahiyh, basi ndio madhehebu yangu' (uk. 102, Mjalada 3). "Kwangu, lililo bora kabisa ni kufuata Hadiyth. Mtu na awaze kwamba yuko mbele ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kama vile ameisikia kutoka kwake, je, atakwenda demani (kufuata mweleko wa upepo) acheleweshe kutenda kwa kuifuata? Hapana! WaLLaahi, na kila mmoja anabeba jukumu kutokana na ufahamu wake".

Mjadala wake uliobakia umetolewa kuchambuliwa katika I'laam Al-Muwaqi'iyn (2/ 303, 370) na katika kitabu cha Al-Fulaaniy, (Kichwa cha habari kamili) Al-Iyqadhw Himam Uwl Al-Abswaar, Lil-iqtidaa Bisayyid Al-Muhaajiriyn Wal-Answaar, wa Tahdhiyrihim 'An Al-Ibitidaa' Ash-Shaai' fit-Quraa Wal-Amswaar, Min Taqlyid Al-Madhaahib Ma'a Al-Hamiyyat Wal-'Aswabiyyat Bayna Fuqahaa Al-A'swaar"

Kitabu hicho ni cha pekee katika maduhui hii, ambacho kila mpenda haki akisome kwa ufahamu na kutafakari.

[20] Akimwambia Imaam Ahmad bin Hanbal (رحمه الله)

[21] Imesimuliwa na Ibn Abi Haatim katika Aadaabu Ash-Shaafi'iy (uk. 94-5), Abu Nu'aym katika Hulya Al-Awliyaa (9/ 106), Al-Khatwiyb katika Al-Ihtijaaj Bish-Shaafi’iy (8/1) na kutoka kwake Ibn 'Asaakir (15/ 9/1), Ibn 'Abdil-Barr katika Al-Intiqaa' (uk. 75), Ibn Al-Jawziy katika Manaaqib Al-Imaam Ahmad (uk. 499) na Haraawiy (2/ 47/2) katika njia tatu kutoka kwa 'Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal kutoka kwa baba yake kwamba Ash-Shaafi'iy alimhusisha nayo katika I'laam (2/325) kama alivyofanya Al-Fulaaniy katika Al-Iyqaadhw (uk. 152) na kisha akasema: "Al-Bayhaqiy amesema: "Hii ndio maana yeye, yaani Ash-Shaafi'iy alitumia Hadiyth sana, kwa sababu alikusanya elimu kutoka kwa watu wa Hijaaz, Syria, Yemen na Iraq. Kwa hiyo alikubali yote aliyoona kuwa ni Swahiyh bila ya kutegemea au kuangalia yale yaliyokuwa nje ya madhehebu ya watu wa nchi yake, wakati ukweli ulipodhihirika kwake kutoka sehemu nyingine. Wengineo kabla yake, walijiwekea mipaka kwa waliyoyakuta katika madhehebu ya watu wa nchi yao bila ya kujaribu kuhakikisha usahihi wa yale yaliyokuwa kinyume nayo. Allaah Atusamehe sote"

[22] Abu Nu'aym (9/ 107), Harawiy (47/ 1), Ibn al-Qayyim katika I'laam Al-Muwaqqi'iyn (2/ 363) na Fulaani (uk. 104)

[23] Ibn Haatim katika Al-Adaab (Uk. 93), Abul-Qaasim Samarqandi katika Al-Amaal, kama katika uchaguzi kutoka kwa Abu Hafsw al-Mu'addab (234/ 1), Abu Nu'aym (9/ 106), na Ibn 'Asaakir (15/ 10/1) ikiwa ni sanad Swahiyh.



[24] Ibn Abi Haatim, Abu Nu'aym na Ibn 'Asaakir (15/ 9/2)

[25] Ibn Abi Haatim (uk. 93-4)

[26] Ibn Al-Jawziy katika Al-Manaaqib (uk. 192)

[27] Al-Fulaaniy (Uk. 113) na Ibn Al-Qayyim katika I'laam

[28] Ittibaa'

[29] Abu Daawuud katika Masaail ya Imam Ahmad (uk. 276-7)

[30] Ibn 'Abdil-Barr katika Jaami' Bayaan Al-'Ilm

[31] Ibn Al-Jawziy (uk. 182)



[32] An-Nisaa:4:65

[33] An-Nuur: 24:63

[34] Japokuwa ni dhidi ya baba zao na walimu wao, kama Atw-Twahaawiy katika Sharh Ma'aaniy Al-Aathaar (1/ 372) na Abu Ya'laa katika Musnad yake (3/ 1317) wamesimulia, ikiwa na isnaad ya watu walioaminika kutoka kwa Saalim bin 'Abdillaah bin 'Umar (رحمه الله) ambaye amesema:

"Nilikuwa nimekaa na Ibn 'Umar (رضي الله عنه) msikitini siku moja, alikuja mtu kutoka Syria na akamuuliza kuhusu kuendeleza 'Umrah pamoja na Hajj (Inayojulikana kama ni Hajj At-Tamaattu'). Ibn 'Umar akajibu: 'Ni vizuri na jambo jema'. Kisha mtu akasema: 'Lakini baba yako (yaani 'Umar bIn Al-Khattwaab) alikuwa akikataza' Basi Akasema,' Ole wako! Ikiwa baba yangu alikuwa akikataza kitu ambacho Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)alikuwa akifanya na kuamrisha, je, utakubali rai ya baba yangu au amri ya Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?' Akajibu: 'Amri ya Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)' Akasema: 'Basi nenda zako mbali na mimi' Ahmad (Namba 57000) amesimulia kama hivyo kama alivyosimulia At-Tirmidhiy (2/ 82) na amekiri kuwa ni Swahiyh.



[35] Bali atalipwa thawabu kwa sababu ya kauli ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Qaadhi akipitisha hukmu, akifanya juhudi (ijtihaad) na hukmu ikawa Swahiyh atapata thawabu mbili. Akifanya juhudi (ijtihaad) na akahukumu kimakosa, atapata thawabu moja)) [Imesimuliwa na Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

[36] Imenukuliwa katika tanbihi za 'Iyqaadhw al-Himam (Uk. 93)

[37] Fulaaniy (Uk. 99)

[38] Suratul Al-Waaqi'ah 56: 13-14

[39] Ibn 'Aabidiyn Katika 'al-Haashiyah (1/ 62) na Al-Laknawiy kaipa chanzo chake kutoka katika An-Naafi' al-Kabiyr (Uk. 93) ya Al-Ghazaaliy.

[40] Yeye mwenyewe amesema katika mwanzo wa 'Mukhtaswar Fiy Fiqhis-Shaafi'iy' (iliyochapishwa katika pembizo ya 'Al-Umm') "Kitabu hiki ni uchaguzi kutoka elimu ya Muhammad bin Idriys Ash-Shaafi'iy (رحمه الله) na kutokana na maana ya kauli zake kumsaidia yeyote anayekitaka akiwa anajua makatazo ya kufuata rai yake au ya yoyote mwengine ili mtu azingatie dini yake"

[41] Ambako ameelezea kumpinga Imaam wake katika masaail ishirini (Namba 42, 44, 103, 120, 158, 169, 172, 173, 228, 230, 240, 244, 274, 275, 284, 314, 331, 338, 355, 356 kutoka Ta'liyq Al-Mummajjid 'alaa Muwattwa' Muhammad (Tanbihi muhimu ya Muwattwa ya Muhammad)

[42] Ibn 'Aabidiyn amemtaja miongoni katika 'Al-Haashiyah' (1/ 74) na katika 'Rasm Al-Muftiy (1/17). Qurayshi amemtaja katika 'Al-Jawaahiyr Al-Madhwiyyah fiy Twabaqaat Al-Haniyfah' (uk. 347) na akasema: "Alikuwa ni msimulizi wa Hadiyth wa kutegemewa. Yeye na kaka yake Ibraahiym walikuwa Mashaykh wawili wa Al-Balakh katika zama zao".

[43] Al-Fawaaid Al-Bahiyyah Fiy Taraajim Al-Hanafiyyah (uk. 116)

[44] Al-Bahr Ar-Raaiq (6/ 93) na Rasm Al-Muftiy (1/ 28)

[45] Al-Fawaaid … (uk. 116) kisha muandishi akaongeza tanbihi yenye faida:

"Kutokana na hii inawezekana kutambulika ubatilifu wa usimulizi wa Makhuul kutoka kwa Abu Haniyfah: 'Kwamba mwenye kunyanyua mikono yake katika Swalah, Swalah yake itakuwa batili' ambayo Amiyr mwandishi wa al-Itqaaniy alivyohadaiwa kama ilivyotajwa kaitka historia yake. 'Iswaam Ibn Yuusuf, mfuasi wa Abu Yuusuf alikuwa akinyanyua mikono yake
 
006-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kuelekea Ka'abah Na Kusimama Kwenye Swalah


KUELEKEA QIBLAH





Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa anasimama kuswali Swalah zote za Fardhi na za Sunnah alikuwa anaelekea upande wa Ka'abah[1]



Naye Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliliamrisha hilo kwa kumwambia "mtu aliyeswali vibaya”[2]: ((Unaposimama kuswali, fanya wudhuu sawasawa, kisha elekea Qiblah na upige Takbiyr))[3].



"Wakati yuko safarini, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali Swalah za Sunnah na Swalah ya Witr na huku amepanda mnyama popote alipoelekea. (Mashariki au Magharibi)[4]





Hilo ni kwa Neno Lake Allaah Mtukufu:



فَأَيْنَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجْهُ ٱللَّهِ ...

((Basi kokote mnakoelekea, huko kuna wajihi wa Allaah))

[Al-Baqarah: 115]



Kauli hii inahusiana na Hadiyth hiyo[5] .



“Wakati mwengine alipokuwa anataka kuswali Swalah zisizo za fardhi juu ya ngamia wake, alikuwa akimwelekeza Qiblah, kisha akisema Takbiyr na akiswali kuelekea popote kule msafara unapoelekea.”[6].



"Alikuwa akifanya rukuu na sujuud huku amempanda mnyama kwa kuinamisha kichwa chake, na akiinamisha kichwa zaidi chini katika sujuud kuliko alivyoinamisha katika rukuu.”[7]



"Alipotaka kuswali Swalah za fardhi alikuwa akiteremka kutoka kwa mnyama na akielekea Qiblah.”[8]



Ama katika Swalah ya mtaharuki wa vita vilivyopamba moto, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliweka kwa ummah wake kanuni ya kuswali "wakiwa wamesimama na kutembea kwa miguu yao, au wakiwa wamepanda mnyama, wakielekea Qiblah au kutokuelekea”[9]. Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Wanapokutana majeshi Swalah ni Takbiyr na kuashiria kwa kichwa))[10]





Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) pia alikuwa akisema ((Kilichokuweko baina ya Mashariki na Magharibi ni Qiblah))[11]



Jaabir (رضي الله عنه) amesema,

"Mara moja tulikuwa na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) katika msafara au kikosi cha jeshi, na kulikuwa na mawingu, tukajaribu kutafuta Qiblah lakini tulikhtilafiana, kwa hiyo kila mmoja wetu akaswali kuelekea upande tofauti na kila mmoja wetu alichora mstari mbele yake ili kuweka alama mahali pake. Ilipofikia asubuhi, tukazitazama tukaona kwamba hatukuswali kuelekea Qiblah. Kwa hiyo tukamuelezea Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) lakini hakutuamrisha tuirudie (Swalah) na akasema:

((Swalah yenu imetosheleza)).[12]



Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali kuelekea Bayt Al-Maqdis (na Ka'abah ikiwa mbele yake) kabla ya kuteremshwa Aayah ifuatayo:



قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي ٱلسَّمَاء فَلَنُوَلّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا فَوَلّ وَجْهَكَ شَطْرَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ ...

((Kwa yakini tukiona unavyo geuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza kwenye Qiblah ukipendacho. Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu; na popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo…)) [Al-Baqarah, 2: 144]



Ilipoteremshwa Aayah hii alielekeza uso wake Ka'abah. Walikuwa watu katika msikiti wa Qubaa' wakiswali Swalah ya Alfajiri, alipokwenda mtu kuwaambia "Hakika Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameteremshiwa Aayah jana usiku na ameamrishwa kuelekeza uso wake Ka'bah. Basi jueni na elekeeni huko". Nyuso zao zilikuwa zimeelekea Shaam kwa hiyo wakageuka (na Imaam wao akageuza uso kuelekea Qiblah pamoja nao).[13]







KUSIMAMA KATIKA SWALAH





Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali kwa kusimama katika Swalah zote mbili za fardhi na za Sunnah kwa kufuata maamrisho ya Allaah



وَقُومُواْ لِلَّهِ قَـٰنِتِينَ

((…na simameni kwa ajili ya Allaah nanyi ni kuqunuti (kunyenyekea)) [Al-Baqarah, 2: 238]





Ama katika safari alikuwa akiswali Swalah za Sunnah na huku amempanda (mnyama).



Ameweka kanuni kwa ummah wake kuswali wakati wa khofu kubwa kwa kusimama juu ya mnyama. Na hili ni kwa Neno Lake Allaah Mtukufu:



حَـٰفِظُواْ عَلَى ٱلصَّلَوٰتِ وٱلصَّلَوٰةِ ٱلْوُسْطَىٰ وَقُومُواْ لِلَّهِ قَـٰنِتِينَ فَإنْ خِفْتُمْ فَرِجَالاً أَوْ رُكْبَانًا فَإِذَا أَمِنتُمْ فَٱذْكُرُواْ ٱللَّهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُواْ تَعْلَمُونَ



((Zilindeni Swalah, na khasa Swalah ya katikati,[14] na simameni kwa ajili ya Allaah nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea)))



((Ikiwa mnakhofu (Swalini) na hali mnakwenda kwa miguu au mmepanda. Na mtakapokuwa katika amani, basi mkumbukeni Allaah kama Alivyokufunzeni yale mliyokuwa hamyajui)) [Al-Baqarah, 2: 238-239]



Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali kwa kukaa wakati alipokuwa akiumwa hata akafariki[15]. Vile vile aliswali kwa kukaa kwa mara nyingine kabla ya hivyo wakati alipojeruhiwa, na watu waliokuwa nyuma yake waliswali kwa kusimama, akawaashiria wakae nao, wakakaa (na kuswali). Alipomaliza, akasema, Mlikuwa mnataka kufanya kama wanavyofanya wa-Fursi na Warumi wanavyofanya, wanawasimamia wafalme wao waliokuwa wanakaa. Kwa hiyo msifanye hivyo tena, kwani Imaam ni kwa ajili ya kumfuata, anapofanya rukuu fanyeni rukuu, anaposimama simameni, anaposwali kwa kukaa na nyinyi swalini kwa kukaa (nyote).[16]




[1] Jambo hili halina shaka yoyote kutokana na mlolongo wa umashuhuri wake (tawaatur). Kwa hiyo, halihitaji maelezo zaidi ingawa baadhi ya dalili zitafuata.



[2] Tazama Kiambatisho 3.



[3] Imekusanywa na Al-Bukhaariy, Muslim na Siraaj.



[4] Imekusanywa na Al-Bukhaariy, Muslim na Siraaj. Takhriyj yake imetolewa katika “Irwa'a Al-Ghaliyl” (289 na 588).



[5] Muslim. At-Tirmidhiy amekiri kuwa ni Hadiythi Swahiyh.



[6]Abu Daawuud na Ibn Hibbaan katika “Ath-Thiqaat” (1/12) na Adh-Dhiyaa katika “Al-Mukhtaarah” ikiwa na sanad hasan. Ibn As-Sukn amekiri kuwa ni Swahiyh na pia Ibn al-Mulaqqin katika “Khulaaswat Al-Badr Al-Muniyr” (22/1) na kabla yao, ‘Abdul-Haqq Al-Ishbiyli katika “Ahkaamuh” (Namba 1394 kwa uhakiki wangu). Ahmad ameitumia kama ni uthibitisho kama alivyoripoti Ibn Haani kutoka kwake katika “Masaailuh” (1/67).



[7] Ahmad na At-Tirmidhiy ambao wamekiri kuwa ni Swahiyh.



[8] Al-Bukhaariy na Muslim.



[9] Al-Bukhaariy na Muslim.



[10] Al-Bayhaqiy na Sanad inayoelekeana na mahitajio ya Al-Bukhaariy na Muslim.



[11] At-Tirmidhiy na Haakim wamekiri kuwa ni Swahiyh. Nimeitowa katika “Irwaa Al-Ghaliyl fiy takhriyj Ahaadiyth manaar As-Sabiyl” (292). Uchapisho wake Allaah (سبحانه وتعالى ) Ameufanya wepesi.



[12] Ad-Daara Qutniy, Al-Haakim, Al-Bayhaqiy, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na At-Twabaraaniy. Imetolewa katika “Al-Irwaa” (296).



[13] Al-Bukhaariy, Muslim, Ahmad, As-Siraaj, At-Twabaraaniy (3/108/2) na Ibn Sa'ad (1/243). Pia iko katika “Al-Irwaa” (290).



[14] Yaani Swalah ya 'Alasiri kutokana na usemi ulio Swahiyhi wa Maulamaa wengi. Miongoni mwao ni Abu Haniyfah na wanafunzi wake wawili. Kuna Hadiyth kuhusu kauli hii ambayo Ibn Kathiyr ameiweka katika Tafsiyr yake ya Qur-aan.



[15] At-Tirmidhiy ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh na Ahmad.



[16] Muslim na Al-Bukhaariy na imetolewa katika kitabu changu Irwaa' Al-Ghaliyl katika Hadiyth 394.
 
007-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Swalah Ya Mgonjwa Na Swalah Ya Kwenye Meli


SWALAH YA MGONJWA KATIKA HALI YA KUKAA




'Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه) alisema: "Nilikuwa naumwa ugonjwa wa bawasili (futuru), nikamuuliza Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) naye akasema:

((Swali kwa kusimama, ikiwa huwezi, swali kwa kukaa, ikiwa huwezi swali kwa kulala ubavu))”. [1]




'Imraan bin Huswayn pia amesema, "Nilimuuliza Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Swalah ya mtu anayeswali kwa kukaa, akasema:

((Anayeswali kwa kusimama ni bora, na anayeswali kwa kukaa, thawabu zake ni nusu ya anayeswali kwa kusimama, na anayeswali kwa kulala (na katika riwaya nyingine kwa kulala chali), basi atapata thawabu nusu ya yule mwenye kuswali kwa kukaa)).[2]




Makusudio hapa ni mtu mgonjwa, kwani Anas amesema: "Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka mbele ya watu waliokuwa wakiswali kwa kukaa kwa sababu ya ugonjwa, akasema:

((Hakika Swalah ya mwenye kukaa ni (sawa) na nusu ya Swalah ya mwenye kuswali kwa kusimama)).[3]




Siku moja Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alimtembelea mgonjwa na akamuona anaswali (huku ameegemea) juu ya mto. Akauchukua na akautupa (pembeni). Kisha mgonjwa akachukua kipande cha mti ili akiegemee katika Swalah yake. (Mtume) akakichukua akakitupa (pembeni) na akasema:

((Swali juu ya ardhi ukiweza, na kama huwezi, basi fanya harakaati kwa kichwa chako kwa kufanya sujuud iwe ya kuinama chini zaidi ya rukuu)).[4]










SWALAH YA KWENYE MELI (CHOMBO CHA BAHARINI)




Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu Swalah katika meli, akasema: ((Swali ukiwa umesimama ila ukiogopa kuzama)).[5]




Alipokuwa mzee mtu mzima, alijiwekea kiguzo katika sehemu ya kuswali ili kukiegemea.[6]












[1] Al-Bukhaariy, Abu Daawuud na Ahmad.




[2] Al-Bukhaariy, Abu Daawuud na Ahmad. Al-Khatwaabiy amesema: "Makusudio ya Hadiyth ya 'Imraan ni mgonjwa wa kukisiwa anayeweza kuchechemea na kusimama kwa tabu, na kwa hivyo, thawabu za mwenye kukaa zimefanywa nusu ya mwenye kusimama kwa ajili ya kumpa msukumo asimame ingawa inajuzu kwake kukaa.” Al-Haafidhw Ibn Hajr amesema katika Fat-h Al-Baariy (2/468): “Nayo ni makisio yenye kukubalika.”




[3] Ahmad na Ibn Maajah kwa sanad Swahiyh.




[4] At-Twabaraaniy, Al-Bazzaar, Ibn As-Samaak katika “Hadiythih” (2/67) na Al-Bayhaaqiy. Sanad yake ni Swahiyh kama nilivyoeleza katika Silisilah Al-Ahaadiyth As-Swahiyhah (323).




[5] Al -Bazzaar (68), Ad-Daaraqutniy na Abdul-Ghaaniy Al-Maqdisi katika “As-Sunan” (2/82). Na Al-Haakim amekiri kuwa ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy ameikubali.




[6] Abu Daawuud na Al-Haakim ambao wamekiri kuwa ni Swahiyh kama alivyokiri Adh-Dhahabiy. Nimeiweka katika “As-Swahiyhah” (319) na “Al-Irwaa” (383).
 
008-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kukaa Na Kusimama Katika Swalah Ya Usiku (Tahajjud)




KUKAA NA KUSIMAMA KATIKA SWALAH YA USIKU (TAHAJJUD)




Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa (mara) akiswali usiku mrefu akiwa amesimama na (mara nyingine) akiswali usiku mrefu kwa kukaa. Na alikuwa anaposoma kwa kusimama, hurukuu kwa kusimama, na anaposoma kwa kukaa, hurukuu kwa kukaa.[1]




Na wakati mwengine, alikuwa anaswali kwa kukaa, na husoma hivyo hivyo huku amekaa. Na inapobakia katika kisomo chake kiasi cha Aayah thalathini au arubaini hivi, husimama na kuzisoma kwa kusimama, halafu hurukuu na kusujudu. Kisha hufanya hivyo hivyo katika Raka'ah ya pili.[2]







Bali aliswali Asw-Swubha (Swalah ya Asubuhi)[3] kwa kukaa chini katika siku za mwisho za maisha yake alipokuwa katika umri mkubwa, na na hilo lilikuwa kabla ya kufariki kwake kwa mwaka mmoja.[4]




Vile vile alikuwa akikaa kwa kukunja miguu (mkao wa chuoni).[5]











[1] Muslim na Abu Daawuud.

[2] Al-Bukhaariy na Muslim.

[3] Ni Swalah ya Sunnah (usiku au jioni) imeitwa hivyo kutokana na yaliyokuwemo humo ya tasbiyh (Kumtukuza Allaah).

[4] Muslim na Ahmad.

[5] An-Nasaaiy, Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1/107/2), 'Abdul-Ghaaniy Al-Maqdisi katika Sunan yake (80/1) na al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh na adh-Dhahabiy amekubali.
 
009-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Swalah Kwa Kuvaa Viatu Na Swalah Juu Ya Minbar





SWALAH KWA KUVAA VIATU NA MAAMRISHO YA KUFANYA HIVYO




"Alikuwa akisimama (katika Swalah) bila ya viatu wakati mwingine na kuvaa viatu wakati mwingine"[1]




Ameruhusu kufanya hivyo kwa Ummah wake na kusema:

((Mmoja wenu anaposwali, basi avae viatu vyake au avivue baina ya miguu yake, na wala asimkere mtu kwa viatu hivyo)).[2]




Aliwasisitizia kuswali na viatu wakati mwingine, na kusema:

((Kuweni tofauti na Mayahudi, kwani wao hawaswali na viatu vyao wala na khufu [soksi za ngozi] zao)).[3]



Mara moja moja alikuwa anavivua wakati anaswali na kisha akiendelea na Swalah yake kama alivyosema Abu Sa'iyd Al-Khudriy:




"Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alituswalisha siku moja, na alipokuwa yumo katika Swalah, alivua viatu vyake na akaviweka upande wa kushoto kwake. Watu walipoona hivyo, nao pia wakavua viatu vyao. Alipomaliza kuswali alisema: ((Kwa nini mmevua viatu vyenu?)) Wakajibu: "Tumekuona wewe unavua viatu vyako na sisi pia ndio tukavua viatu vyetu". Akasema:

((Hakika Jibriyl alinijia na kunijulisha kwamba kulikuwa na uchafu)) au kasema (kulikuwa na) kitu cha madhara)). Katika riwaya nyingine ((uchafu/ Najsi)) katika viatu vyangu, kwa hiyo nikavivua. Kwa hivyo, mmoja wenu anapokuja msikitini, basi atazame viatu vyake. Akiona vina uchafu, au kasema kitu chenye madhara, na (katika riwaya nyingine) najsi, basi avifute kisha aswali navyo)).[4]




"Alipokuwa akivivua, alikuwa akiviweka upande wa kushoto kwake.”[5]




Na pia alikuwa akisema: ((Mmoja wenu anaposwali, asiweke viatu vyake upande wa kulia wala kushoto kwake, ambako vitakuwa katika upande wa kulia wa mwenzake, isipokuwa kama kutakuwa hakuna mtu upande wa kushoto, lakini aviweke baina ya miguu yake)).[6]










SWALAH KATIKA MINBAR




Mara moja Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali katika Minbar (na katika riwaya nyingine: iliyokuwa na daraja (vijingazi) tatu[7]). Hivyo (akasimama juu yake na akapiga Takbiyr (akasema 'Allaahu Akbar') na watu nyuma yake wakapiga Takbiyr wakati yuko juu ya Minbar), (kisha akarukuu juu ya Minbar), halafu akainuka na kushuka kinyume nyume mpaka akasujudu katika kitako cha Minbar. Kisha akarudi (na akafanya kama alivyofanya katika raka'ah ya mwanzo) mpaka akamaliza Swalah yake. Kisha akageuka kwa watu na kusema: ((Enyi watu! Nimefanya hivyo ili mnifuate na mjifunze Swalah yangu))[8].










[1] Abu Daawuud na Ibn Maajah. Ni Hadiyth yenye mapokezi mengi (Mutawaatir) kama alivyotaja atw-Twahaawiy.




[2] Abu Daawuud na Bazzaar (53, Az-Zawa'id), al-Haakim amekiri kuwa ni Swahiyh na adh-Dhahabiy amekubali.




[3] Abu Daawuud na Bazzaar.




[4] Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah na al-Haakim ambao wamekiri kuwa ni Swahiyh na adh-Dhahabiy na an-Nawawiy wamekubali. Ya kwanza imetolewa katika Irwaa.




[5] Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah na al-Haakim.




[6] Abu Daawuud, An-Nasaaiy na Ibn Khuzaymah (1/110/2) na kwa Sanadi iliyo Swahiyh.




[7] Hii ni Sunnah kuhusu Minbar, kwamba iwe na daraja tatu, na sio zaidi. Kuwa na zaidi ya daraja tatu ni bid'ah iliyoanzishwa na Bani Umayyah. Ni mara nyingi safu hukatika. Na kuliepuka hilo kwa kuiweka pembezoni mwa upande wa Magharibi wa Msikiti au wa Mihraab, ni bid'ah nyingine. Vile vile ni (bid’ah) kuipandisha katika ukuta wa kusini kama roshani ambako mtu hupanda kwa ngazi zilizoshikanishwa na ukuta! Na uongofu mbora kabisa ni uongofu wa Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم) ). Tazama Fat-h Al-Baariy (2/331).




[8] Al-Bukhaariy na Muslim. Riwaya nyingine ni yake Muslim na Ibn Sa'd (1/253). Imetolewa katika “Al-Irwaa” (545).
 
010-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Sutrah Na Yanayokata (Yanayotengua) Swalah










SUTRAH[1] NA KUWAJIBIKA KWAKE



"Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisimama karibu na sutrah, ili iweko (umbali wa) dhiraa tatu baina yake na ukuta”[2] na "baina ya sehemu ya sujuud na ukuta (kulikuweko) nafasi ya kuweza kupita kondoo”[3].




Alikuwa akisema,

((Msiswali isipokuwa mbele ya Sutrah, na msimuachie mtu kupita mbele yenu, lakini kama mtu akiendelea (kujaribu kupita) basi mzuwieni kwani yuko pamoja na rafiki)) (yaani Shaytwaan).[4]




Alikuwa akisema,

((Mmoja wenu akiswali mbele ya Sutrah, basi awe karibu yake ili Shaytwaan asiweze kuivunja Swalah yake)).[5]








Mara nyingine "Alikuwa anaswali mbele ya nguzo ya msikiti.”[6]




Alipokuwa anaswali (kwenye sehemu ya wazi ambako kulikuwa hakuna kitu cha kutumia kiwe Sutrah) alikuwa akiuchomeka mkuki ardhini mbele yake kisha akiswali kuuelekea na watu wakiwa nyuma yake.[7] Mara nyingine "alikuwa akiweka kipando chake (mnyama) kisha akiswali kukielekea kipando chake.[8] Lakini hii sio sawa na Swalah katika sehemu ya mapumziko ya ngamia[9] ambayo "ameikataza”[10] na mara nyingine "alikuwa akichukua tandiko lake (la ngamia) akiliweka kwa urefu kisha akiswali kuelekea nchani mwake.”[11]




Na alikuwa akisema,

((Mmoja wenu akiweka mbele yake kitu kama fimbo nchani (mwishoni) mwa tandiko la mnyama, basi aswali na asijali mtu yeyote atakayepita mbele yake)).[12]




Mara moja "Aliswali akiuelekea mti”[13] na wakati mwengine "Alikuwa akiswali mbele ya kitanda ambacho Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) alikuwa amelala (akiwa amejifunika shuka).”[14]




Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa haachii kitu chochote kupita baina ya Sutrah yake, kwa hiyo mara moja "alikuwa anaswali na kondoo alipokuja na kukimbia mbele yake alimkimbiza mpaka akalibonyeza tumbo lake katika ukuta (kisha akapita nyuma yake).”[15]







Vile vile mara moja "wakati anaswali Swalah ya fardhi, alikunja ngumi yake. Na alipomaliza (kuswali) watu walimwambia, "Ewe Mjumbe wa Allaah, kuna jambo limetokea wakati wa Swalah?" Akasema, ((Hapana isipokuwa Shaytwaan alitaka kupita mbele yangu, nikamkaba mpaka nikahisi ubaridi wa ulimi wake katika mkono wangu. Naapa kwa Allaah! Ingelikuwa sio ndugu yangu Sulaymaan kunitangulia[16]. Ningelimfunga (Shaytwaan) katika nguzo moja ya msikiti ili watoto wa Madiynah waweze kutembea mbele yake. (kwa hiyo yeyote atakayeweza kuzuwia kitu kumuingilia baina yake na Qiblah afanye hivyo).”[17]




Pia alikuwa akisema,




((Mmoja wenu anaposwali mbele ya kitu kama Sutrah baina yake na watu na mtu akitaka kupita mbele yake, basi amsukume kwa shingo yake)) (na amfukuze kadiri anavyoweza) (katika riwaya nyingine, ((amzuie mara mbili na akikataa (akishikilia kutaka kupita mbele) basi agombane naye kwani hakika huyo ni Shaytwaan)).[18]




Vile vile alikuwa akisema,

((Ikiwa mtu aliyepita mbele ya mtu mwenye kuswali amejua (kuwa ni dhambi) juu yake (kufanya hivyo), basi ingelikuwa ni bora kwake kusubiri arubaini kuliko kupita mbele)). Na nyongeza katika riwaya nyingine yasema, (Abu An-Nadr kasema, "Sikumbuki khaswa kama alisema ni siku arubaini, au miezi au miaka").[19]










YANAYOKATA (YANAYOVUNJA) SWALAH



Alikuwa akisema,

((Swalah ya mtu inavunjika (inakuwa baatwil) kunapokuwa hakuna kitu kama ncha ya tandiko (la mnyama) mbele yake (vitu vitatu) mwanamke (baleghe)[20] punda au mbwa mweusi)) Abu Dharr akasema, "Nilisema, Ewe Mjumbe wa Allaah, kwa nini mbwa mweusi na sio mwekundu?" Akasema, ((Mbwa mweusi ni Shaytwaan)).[21]








[1] Sutrah – "Kinga ya kuzuia" katika Swalah, inakusudia kitu cha kuwekwa mbele ya sehemu ya kusujudu kukinga ili asipite mtu au chochote mbele yake kama ilivyoelezewa katika somo hili.

[2] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[3] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[4] Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1/93/1) na Isnaad iliyothibitika.

[5] Abu Daawuud, Bazzaar (ukurasa 54 Zawaaid) na Al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahaabiy na An-Nawawiy wameikubali.

[6] Al-Bukhaariy. Sutrah ni lazima kuweko kwa Imaam au mtu anayeswali peke yake hata katika msikiti mkubwa. Ibn Haani amesema katika Masaa'il yake kutoka Imaam Ahmad (1/66) "Abu 'Abdillaah (Imaam Ahmad Ibn Hanbal) aliniona siku moja wakati naswali bila ya Sutrah mbele yangu na nilikuwa katika (Swalah ya) Jama'ah (kubwa) msikitini, kwa hiyo akaniambia, "Weka kitu kama Sutrah". Nikamchukua mtu kama Sutrah. Hii inaonyesha kwamba Imaam Ahmad hakutofautisha baina ya msikiti mkubwa au mdogo katika mas-ala ya Sutrah. Na hii hakika ni sahihi, lakini hili ni jambo ambali limedharauliwa na watu wengi pamoja na ma-Imaam wa misikiti katika kila nchi nliyotembea pamoja na nchi za Arabuni ambazo nimeweza kutembea katika mwezi wa Rajab wa mwaka huu (1410). Kwa hiyo ma-Ulamaa waambie watu na kuwanasihi jambo hili, na kuwafahamisha sheria yake na kwamba pia inahitajika kuweko katika misikiti miwili mitukufu.

[7] Al-Bukhaariy, Muslim na Ibn Maajah.

[8] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[9] Yaani ni sehemu yao ya kupiga magoti.

[10] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[11] Muslim, Ibn Khuzaymah (92/2) na Ahmad.

[12] Muslim na Abu Daawuud.

[13] An-Nasaaiy na Ahmad kwa Isnaad Swahiyh.

[14] Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Ya'laa (3/1107).

[15] Ibn Khuzaymah katika Swahihy yake (1/95/1) At-Twabaraaniy (3/140/3) na Al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy kaikubali.

[16] Inakusudiwa Du'aa ifuatayo ya Nabii Sulaymaan (عليه السلام) ambayo alijibiwa na Allaah (سبحانه وتعالى) kama ilivyo katika Qur-aan. ((Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji)) ((Basi Tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipo taka kufika)) ((Na tukayafanya mashaytwaan yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi)) ((Na wengine wafungwao kwa minyororo)) [Swaad, 38: 35-38].

[17] Ahmad, Daaraqutniy na At-Twabariy kwa Isnaad ya Swahiyh na iliyo na maana kama hii ni Hadiyth inayopatikana katika Al-Bukhaariy na Muslim na wengineo kutoka kwa mapokezi ya Maswahaba mbali mbali. Na mojawapo ya Hadiyth ambayo kundi la Maqadiyani hawaiamini kwani hawaamini (ulimwengu wa) majini ambao wametajwa katika Qur-aan na Sunnah. Desturi yao ni kukanusha maandishi yaliyo mashuhuri sana. Kama kutoka kwenye Qur-aan wanabadilisha maana yake mfano, maneno ya Subhaana Wa Ta’ala ((Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza)) [72:1] wanasema kwamba ina maana "kikundi cha binaadamu" na kulifanya neno la 'majini' kuwa inakaribia na maana ya 'binaadamu'. Kwa hiyo wanacheza na lugha na dini. Na kama kutoka katika Sunnah basi kama inawezeka kwao kubadilisha kwa tafsiyr ya uongo wanafanya hivyo, au sivyo wanaona ni wepesi kukiri kuwa ni uongo hata kama Maimaam wa Hadiyth wote na Ummah mzima kabla yao wamekubaliana na usahihi wake, (tunawaambia kuwa hilo wanalilikataa hapo) kuwa hapana, hiyo ni mutawaatir (imekuja kwa mapokei mengi haina shaka yoyote). Allaah Awahidi.




[18] Al-Bukhaariy na Muslim na riwaya zaidi ni kutoka kwa Ibn Khuzaymah (1/94/1).

[19] Al-Bukhaariy na Muslim.

[20] Ina maana baleghe, na maana ya 'inavunjika' ni kuwa 'haifai tena' (baatwil). Ama kuhusu Hadiyth "Hakuna kinachovunja Swalah" hiyo ni Hadiyth dhaifu na nimeionyesha katika Tamaam Al-Minnah (Ukurasa 306).

[21] Muslim, Abu Daawuud na Ibn Khuzaymah (1/95/2).
 
Naam hakika elimu ni tamu sana,hili la Sutrah kwakweli ni misikiti michache sana utakuta wamechonga vibao maalum vinavyotumika kama Sutrah

Lkn mingi ya misikiti hakuna kabisa,sasa ukiwa unaswali peke yako basi hakikisha mbele yako kuna kizuizi,inaweza kuwa chupa ya maji,nguo au chochote ambacho kitakuwa kama kizuizi chako

Hata ukiwa chumbani kwako,waeza swali karibu na ukuta au kama uko mbali basi weka chochote ambacho kitakuzuia na sheitwani

Kingine cha ziada imamu akiwa mbele yenu yeye ndio anakuwa Sutrah yenu,ndio maana baadhi ya misikiti unaweza kuta watu wanakatisha mbele ya safu za watu wanao swali,usijie kushangaa hii imekaaje maadamu imamu yupo mbele basi yeye ndie Sutrah
 
Pamoja na kuendelea na darsa nitakuwa naleta mambo mengine ambayo ni muhimu kupata elimu juu yake


Hadiyth Kuhusu Kuomba Du’aa Pamoja Baada Ya Swalaah Ni Swahiyh Au Dhaifu?



www.alhidaaya.com









SWALI:



Assalam alaikum



Ipo Hadithi ya mtume swalla Allaahu alayhi wa sallam, ambayo imesimuliwa na Abuu Umama Radhiya Allahu anhu amabyo ni hii hapa. Asema Mtume Swalla Allahu alayhi wasallama" halikusanyiki kundi la watu; wakaomba dua miongoni mwao na wengine wakaitikia aamiin; ila Allah atawajibu.” Amepokea Twabrani, Baihaqiy, Hakim kutoka kwa Habibi Ibn Salamatal Fihryyah; Allaah Awe radhi nao wote hao.



Hii ndio Hadithi ninayotaka kujuwa usahihi wake na kama ni Sahihi ukiunganisha na ya Abuu Umama itakuwa ni sahihi kuomba dua kwa pamoja baada ya swala ya fardhi? Kwani imethibiti dua ya pamoja na pia imethibiti dua baada ya swala. Yaani moja ya sehemu inayo kubalika dua ni baada ya swala ya faradh na kama alivyosema imamu Tirmidhy (Allah amrehemu) kuwa ni Hadiythi hasan. Je? Hadiythi hii inafaa kuwa ni hoja madhubuti kwamba kuomba dua baada ya swala ya fardh ni sunnah na imethibiti kwa mtume Swalla Allaahu alayhi wa sallam na ni muhimu sana kwa mtu kuomba dua baada ya swala ya fardhi kwani ni moja ya sehemu inayokubaliwa dua





Maelezo mengineyo ya muulizaji kuhusiana na swali lake:





Assalam alaikum,

Hadiythi ya Abuu Umama niloisema yazungumzia dua baada ya swala ni hii hapa kama alivyo inukuu Imamu Shaukani ktk Nailu L’autwar. Pia Hadiythi hii inapatikana ktk Riyadh swallihina Hadithi ya 1,500. Pia nime attach hadithi nilo andika kwa mkono, hii nimeikuta ktk vitabu hivi vya dua vidogovidogo, sijaiona ktk vitabu vya hadithi nimeikopi pamoja na muhtasari wa takhrij yake, sina hakika na usahihi wa Hadithi hii



1. Swali la kwanza, naomba mnifahamishwe usahihi wa Hadithi nilo andika kwa mkono (attachment number one) ama umadhubuti wake kama inafaa kufanyia kazi



2. Maelezo kwa ufupi: Hadithi ya Abuu Umama; Ibn Hajar ktk Fathu lbar juzu ya 11 ukurasa 153 (toleo la mwaka 2003) Kitabu da’awa (dua’u ba’ada swalat) ameinukuu na akaunganisha na Hadiythi ya Twabari kutoka kwa jaafar isemayo” dua baada ya swala ya fardh ni bora kuliko dua baada ya swala ya sunnat kama ilivyo kuwa ubora wa swala ya fardh kwa swala ya sunnat” pia akanukuu manenoya Watu wa Hanbal kuhusu kauli ya Ibn Lqaiym ktk kitabu chake cha Zadu l’ma’aad (alipo sema hakuna Hadithi Sahihi inayo thibitisha dua baada ya swala)



3. Swali la pili, Ikiwa Hadithi ya Abuu Umama na maelezo ya Ibn Hajar na Hadith ya Twabari ni sahihi Je kuomba dua baada ya swala ya Fardh ni Sunnat?



4. Swali la tatu, ikiwa Hadithi nilo andika kwa mkono (Swali la kwanza) ni sahihi ama ni madhubuti na inafaa kufanyia kazi, na kwa kuwa baada ya swala kuna kundi la watu, hivyo wakaamuwa miongoni mwao mmoja aombe dua na wengine waitikie wakaifanyia kazi Hadithi (kwani ni sababu ya kujibiwa dua kama hadithi inavyo jieleza) na kwa kuwa kuomba dua baada ya swala ni Sahihi ikiwa Swali la pili yaani Hadithi ya Abuu Umama ni madhubuti, Je, kuomba dua kwa pamoja baada ya swala (yaani kufanyia kazi Hadithi nilo andika kwa mkono na ya Abuu Umama kwa pamoja) itakuwa ni sunnat ama bid’a (ukizingatia sunnah inaweza kuwa Mtume Swalla Allaahu alaihi wa sallam amesema (sio lazima afanye), ama amefanya, amekubali jambo moja ktk ya haya matatu yaweza kuwa sunnat)



Wabillah taufi



JIBU:





AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



In Shaa Allaah tutajaribu kujibu nukta baada ya nukta kuhusu Hadiyth zilizotajwa hapo juu katika swali hilo.





Mwanzo tunatakiwa tufahamu kuwa du’aa ni jambo ambalo linahitajika kwa Muislamu. Na Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatufahamisha kuwa du’aa ni silaha ya Muumini. Kwa hiyo, baada ya kila ‘Ibaadah, Allaah ('Azza wa Jalla) Akatuwekea du’aa. Na ‘Ibaadah ya Swalaah si tofauti, kwani Allaah ('Azza wa Jalla) Anasema:



فَإِذَا قَضَيْتُمُ الصَّلَاةَ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمْ ۚ فَإِذَا اطْمَأْنَنتُمْ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۚ إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا ﴿١٠٣﴾

Mtakapomaliza Swalaah, mdhukuruni Allaah msimamapo, na mkaapo na mnapolala ubavuni mwenu Mtakapopata utulivu, simamisheni Swalaah (kama desturi), hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu. [An-Nisaa: 103]



Na Anasema pia Allaah (‘Azza wa Jalla):



فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ وَاذْكُرُوا اللَّـهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴿١٠﴾

Na inapomalizika Swalaah, tawanyikeni katika ardhi, na tafuteni katika fadhila za Allaah, na mdhukuruni Allaah sana ili mpate kufaulu. [Al-Jumu’ah: 10]





Hata hivyo, inatakiwa tuilete hiyo du’aa kwa njia ambayo tumefundishwa katika Shariy’ah sio tunavyotaka sisi.



Tukianza na Hadiyth ya Abuu Umaamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu). Nadhani itakuwa bora mwanzo tuanze na kuifasiri kwa ukamilifu wake ili ifahamike vizuri.





Imepokewa kwa Abuu Umaamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema:

Aliulizwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Ni du’aa gani yenye kusikilizwa zaidi (inayokubaliwa)?” Akasema: “Sehemu ya mwisho ya usiku na baada ya kila Swalaah ya faradhi” [at-Tirmidhiy ambaye amesema ni Hasan].



Hivyo ndivyo ilivyonukuliwa na Imaam An-Nawawiy. Labda tuitazame msimamo wa Wanachuoni kuhusu Hadiyth hiyo.





Shaykh Muhammad Naaswirud-Diyn Al-Albaaniy ameiweka Hadiyth kuwa ni ya (1508), naye amesema Hadiyth hii ni Swahiyh. Hata hivyo, Shaykh Shu‘ayb Al-Arna’ut amesema Hadiyth hii ni dhaifu kwa sababu ya Isnadi yake lakini inatiliwa nguvu na Hadiyth nyingine ambayo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mja anakuwa karibu zaidi katika du’aa zake wakati wa usiku wa mwisho” [at-Tirmidhiy na an-Nasaa’iy, na Isnadi yake ni Swahiyh]



Hata hivyo, tukichukulia kuwa Hadiyth hii ni Swahiyh kabisa kama alivyosema Sh. Muhammad Naaswir ad-Diyn al-Albaaniy haimaanishi kuwa adhkaar na du’aa zinazoletwa baada ya Swalaah ni kwa pamoja. Zipo Hadiyth nyingi Swahiyh zinazotufundisha adhkaar na du’aa kwa mpangilo maalumu baada ya Swalaah ya faradhi. Na kufanya hivyo kunampatia mwenye kutekeleza ujira na thawabu nyingi. Kwa hiyo, ni muhimu kuhifadhi du’aa hizo na kuzileta kwa njia inayotakiwa na Shariy’ah. Pia tunatakiwa tulete baada ya Swalaah tu na kabla ya kuinuka latika sehemu aliyoswali Muislamu. Utaratibu wenyewe ni kama ufuatao:





1-Kusema



أَسْـتَغْفِرُ الله، أَسْـتَغْفِرُ الله، أَسْـتَغْفِرُ الله، اللّهُـمَّ أَنْـتَ السَّلامُ، وَمِـنْكَ السَّلام، تَبارَكْتَ يا ذا الجَـلالِ وَالإِكْـرام

[Muslim]





2-Kisha ni kusema:



لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْد، وهوَ على كلّ شَيءٍ قَدير، اللّهُـمَّ لا مانِعَ لِما أَعْطَـيْت، وَلا مُعْطِـيَ لِما مَنَـعْت، وَلا يَنْفَـعُ ذا الجَـدِّ مِنْـكَ الجَـد

[Al-Bukhaariy na Muslim].







3-Baada ya hapo:



لا إلهَ إلاّ اللّه وحدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ الملكُ ولهُ الحَمد، وهوَ على كلّ شيءٍ قدير، لا حَـوْلَ وَلا قـوَّةَ إِلاّ بِاللهِ، لا إلهَ إلاّ اللّـه، وَلا نَعْـبُـدُ إِلاّ إيّـاه، لَهُ النِّعْـمَةُ وَلَهُ الفَضْل وَلَهُ الثَّـناءُ الحَـسَن، لا إلهَ إلاّ اللّهُ مخْلِصـينَ لَـهُ الدِّينَ وَلَوْ كَـرِهَ الكـافِرون

[Muslim].







4-Kisha utaleta mara 33 kila moja ya:



سُـبْحانَ الله

الحَمْـدُ لله

واللهُ أكْـبَر

5-Kisha utasoma mara moja

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحْـدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ الملكُ ولهُ الحَمْد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَـدير

[Muslim]







6-Kusoma Ayaatul Kursiy



(2: 255) [An-Nasaa’iy, atw-Twabaraaniy na Ibn Sunniy]







7-Kusoma Suwratul Ikhlasw, al-Falaq na an-Naas ([Abu Daawuwd, at-Tirmidhiy na an-Nasaa’iy].





Shaykh Swaalih Fawzaan bin ‘Abdillaah al-Fawzaan katika kitabu chake: Al-Mulakhkhaswu al-Fiqhiyy amesema: “Na inapendeza kujihirisha Tahliyl, Tasbiyh, Tahmiyd na Takbiyr baada ya kila Swalaah lakini isiwe kwa sauti ya pamoja. Kila mmoja anasome peke yake. Baada ya kumaliza adhkaar hizi, kila mmoja anaomba kwa siri kile anachotaka. Hakika ni kuwa du’aa baada ya ‘Ibaadah na hizi adhkaar tukufu inaleta uwezekano mkubwa zaidi wa kujibiwa. Haifai kudhihirisha du’aa bali anaifanya kwa sauti ndogo, kwani kufanya hivyo ni karibu zaidi na ikhlaasw na unyenyekevu na mbali zaidi na riyaa. Ama kwa yale yanayofanywa na baadhi ya watu katika baadhi ya nchi kwa kuleta du’aa ya pamoja baada ya Swalaah kwa sauti kubwa au Imaam aombe na maamuma waitikie “Aamiyn”, hii ni bid‘ah inayochukiza kwani haijapokewa kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alikuwa anaposwalisha watu na baada ya kumaliza Swalaah akiomba kwa njia hii. Hakufanya hivyo katika Swalaah ya Alfajiri, wala Alasiri, wala Swalaah nyinginezo, wala hakupendeza hilo yeyote miongoni mwa Maimamu” [Mj. 1, uk. 154 – 160].





Ama tukija katika Fat-hul Baariy nimeipitia Hadiythi hizo ulizozitaja katika Mj. 11, uk. 159, chapa ya Daar as-Salaam, chapa ya tatu ya mwaka 1421 H/2001 M. Imaam al-Bukhaariy ana mlango wa 18: Baab ad-Du’aa’i ba‘da asw-Swalaah (Mlango wa Du’aa baada ya Swalaah). Imaam al-Bukhaariy ameweka Hadiyth mbili zilizoshereheshwa na Ibn Hajar, nazo ni kama zifuatazo:



1-Imepokewa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu): Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah! Hakika wametangulia wenye mali kwa daraja na neema za kuendelea. Akasema: “Itakuwaje hivyo?” Akasema: Wanaswali kama tunavyoswali, wanapigana Jihaad kama tunavyopigana, na wanatoa katika fadhila za mali zao, nasi hatuna cha kutoa. Akasema: “Je, niwajulishe jambo ambalo mkifanya mtawafikia waliokuwa kabla yenu na kuwashinda wanaokuja baada yenu, wala hatofikia yeyote kwa mlioleta ila atakayeleta mfano wake? Leteni Tasbiyh baada ya kila Swalaah mara kumi, Tahmiyd kumi na Takbiyr kumi”



2-Mughiyrah bin Shu‘bah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alimuandikia Mu‘aawiyah bin Abi Sufyaan (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema baada ya kila Swalaah baada ya salaam:



لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْد، وهوَ على كلّ شَيءٍ قَدير، اللّهُـمَّ لا مانِعَ لِما أَعْطَـيْت، وَلا مُعْطِـيَ لِما مَنَـعْت، وَلا يَنْفَـعُ ذا الجَـدِّ مِنْـكَ الجَـد



Kauli yake: “Mlango wa Du’aa baada ya Swalaah”, yaani baada ya Swalaah za faradhi. Hadiyth hizo mbili zilizo hapo juu zinatufahamisha kuwa ipo du’aa baada ya Swalaah, du’aa ambazo ni makhsusi kama alizotufundisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hata hivyo, hizo Hadiyth hazionyeshi kuwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba na Maswahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum) wakiitikia ”Aamiyn.”





Ama tukija katika Hadiyth ulizozitaja kwa mukhtasari ambazo amezitaja Ibn Hajr Al-Asqalaaniy, na pia kuna nyingine umeziacha zote hazina dalili ya kuomba du’aa kwa pamoja baada ya Swalaah. Na hivyo akamuusia Mu‘aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu ‘anhu) asiache kuomba du’aa baada ya Swalaah, du’aa maalumu [Abuu Daawuwd, an-Nasaa’iy, al-Haakim na Ibn Hibbaan].





Pia Hadiyth ya Abuu Bakrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwa kauli:



اللّهُـمَّ إِنّـي أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكُـفر، وَالفَـقْر، وَأَعـوذُبِكَ مِنْ عَذابِ القَـبْر،



“Ee Allaah! Najilinda Kwako kutokana na ukafiri, ufakiri na adhabu ya kaburi.” Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba kwayo baada ya kila Swalah [Ahmad, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy, na imesahihishwa na al-Haakim].



Na pia Hadiyth ya Sa‘d, Zayd bin al-Arqam, Swuhayb na Abuu Umaamah (Radhwiya Allaahu ‘anhum) zatuonyesha du’aa za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya Swalaah kwa njia ya siri ila kwa wakati mwengine alikuwa akinyanyua sauti ili wafuasi wake wapate kujifunza kwa njia sahali na rahisi.





Na maelezo yote hayo yanaweza kufupishwa kwa kauli ya Allaah (‘Azza wa Jalla):





وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ ﴿٢٠٥﴾

Na mdhukuru Rabb wako katika nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu na si kwa jahara katika kauli asubuhi na jioni; na wala usiwe miongoni mwa walioghafilika. [Al-A’raaf: 205]





Imaam ash-Shawkaaniy amesema kuieleza Aayah hii katika tafsiri yake Fat-hul Qadiyr kuwa, “Hiyo ni kuisikilizisha nafsi yake bila kutoa sauti, yaani kwa unyenyekevu na kwa khofu na kuzungumza kwa mazungumzo chini ya kujihirisha.”





Na Ibn Kathiyr naye amesema katika tafsiri yake, Tafsiyr Al-Qur-aanil ‘Adhwiym: “Mtaje Rabb wako kwa matumaini na khofu na kwa kimoyomoyo, si kwa jahara. Na hivi ndivyo Dhikru-Allaah inavyopendekezwa iwe, si kwa sauti ya juu wala kwa jahara.”



Na Aayah hii inafafanuliwa na Hadiyth iliyowazi kabisa kutoka kwa Abuu Muwsaa al-Ash‘ariy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alisema:



“Watu walinyanyua sauti zao katika du’aa wakati wa baadhi ya safari, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akawaambia: ‘Enyi watu! Jifanyieni wepesi katika nafsi zenu, kwani mnayemwomba si kiziwi wala si wa kughibu. Kwa hakika mnayemwomba ni Mwenye kusikia, wa karibu, yu karibu zaidi ya mmoja wenu kuliko shingo ya mnyama wake.” [al-Bukhaariy na Muslim].



Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Hukmu Za Swalah


SWALI:

Swala ni kitu cha lazima tulichoamrishwa na Allah, lakini wakati mwengine huwa unajisikia kama umechoka lakini ni lazima uswali kwa sababu unajuwa kama hujaswali utapata dhambi. Je, kama utaswali huku umekaa inakubalika Swalah hiyo?








JIBU:

Twamshukuru Allaah Ambaye pekee Anastahiki sifa na utukufu na Swalah na Salamu zimfikie kipenzi chetu, Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), familia yake, Maswahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Malipo.

Tunamshukuru ndugu yetu ambaye ana thiqah na sisi kwa kuuliza swali hili na tunaomba tawfiki ya Allaah katika kulijibu swali hili ili lipate kueleweka.

Mwanzo inatakiwa ieleweke kwa Swalah ni amali kubwa sana kwa Muislamu na fadhila zake ni nyingi na ndiyo amali ya kwanza itakayo hesabiwa Siku ya Qiyaama. Hivyo, tumetakiwa tudumu katika Swalah kama Alivyosema Aliyetukuka:

}}فَأَقِيمُواْ الصَّلاَةَ إِنَّ الصَّلاَةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا{{

{{“Na simamisheni Swalah hakika Swalah imekuwa kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalumu”}} (Q 4: 103).

Na ameifanya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nguzo ya pili katika nguzo za Uislamu tano (Imepokewa na Al-Bukhariy na Muslim kutoka kwa Ibn ‘Umar).

Swalah ina hekima kubwa kwa mwenye kuswali vilivyo, hivyo kumtengezea tabia na maadili mema na kumuondoshea mambo machafu.

Allaah Anasema:

}}وَأَقِمِ الصَّلَاةَ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَى عَنِ الْفَحْشَاء وَالْمُنكَرِ وَلَذِكْرُ اللَّهِ أَكْبَرُ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ{{

{{“Na simamisha Swalah hakika Swalah inakataza machafu na maovu”}} (29: 45).

Swalah ina ubora mkubwa sana kwa Muislamu na inatosha kuweka wazi ubora wa Swalah na ukubwa wa jambo lake.

((Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema: “Msingi wa mambo ni Uislamu, na nguzo yake ni Swalah na kilele cha nundu yake ni kupigana katika njia ya Allaah”)) (Imepokewa na at-Tirmidhiy).

Kwa ajili hii Allaah hakutuamru tuswali tu bali inatakiwa tusimamishe Swalah. Kuswali tu bila kutekeleza mambo ya msingi hakuna maana kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amesema:

}}وَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ{{

}}الَّذِينَ هُمْ عَن صَلاَتِهِمْ سَاهُون{{

}}الَّذِينَ هُمْ يُرَآؤُونَ{{

{{Ole wao wanaoswali. Ambao wanapuuza Swalah zao; Ambao wanajionyesha”}} (107: 4 – 6)

Hivyo tutahadhari sana tunaposwali tusiwe ni wenye kuipuuza au kufanya riyaa, na lau tutafanya hivyo itakuwa hatuna thawabu yoyote na tutakuwa na adhabu kali.

Kusimamisha Swalah ambayo imetajwa katika Aayah nyingi ni kutekeleza masharti ya kupasa kwake (mfano ni Uislamu, kuwa na akili timamu, kubaleghe, kuingia wakati na kuwa twahara). Na masharti ya kuswihi kwake ni kutwahirika, kusitiri tupu, na kuelekea Qiblah. Ili Swalah iwe itakubaliwa ni lazima nguzo zake zitekelezwe na hapa ndipo tunapokuja katika swali letu.

Je, nguzo za Swalah maana yake ni nini? Nguzo za Swalah ni yale mambo yanayofanywa ili kukubaliwa Swalah na lau moja ya nguzo itaachwa basi Swalah itakuwa haijakamilika. Miongoni mwa nguzo za Swalah ni kusimama kwa mwenye kuweza katika Swalah ya Faradhi. Swalah haitosihi kwa kukaa mwenye kuweza kusimama. Haya tunayapata kwa maneno ya Allaah Mtukufu:

}}حَافِظُواْ عَلَى الصَّلَوَاتِ والصَّلاَةِ الْوُسْطَى وَقُومُواْ لِلّهِ قَانِتِينَ{{

{{“Zihifadhini Swalah na hasa Swalah ya kati na kati na simameni kwa ajili ya Allah hali ya kuwa watiifu”}} (2: 238).

Na pia maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akimwambia Imran bin Huswayn (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye alikuwa na ugonjwa wa bawasili na akawa hawezi kuswali kwa kusimama,

((“Swali hali ya kuwa umesimama, ikiwa hutoweza kusimama basi swali katika hali ya kukaa, ikiwa hutoweza kukaa basi swali kwa kulala kwa ubavu”)) (Imepokewa kwa al-Bukhaariy, at-Tirmidhiy na Abu Dawud).

Kwa sababu Uislamu ni Dini ya kimaumbile ya mwanadamu haimkalifishi mtu jambo ambalo haliwezi. Allah anatuelezea:

}}لاَ يُكَلِّفُ اللّهُ نَفْسًا إِلاَّ وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ{{

{{“Allaah haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo. Faida ya iliyoyachuma ni yake, na hasara ya iliyoyachuma ni juu yake pia”}} (2: 286).

Ayah na Hadiyth tuliyoitaja juu ni dalili ya kuwa ni wajibu kuswali Swalah ya Faradhi kwa kusimama kwa yule mwenye kuweza. Ikiwa hataweza hilo katika Swalah ya Faradhi ataswali kwa ile hali anayoweza. Hivyo, ikiwa mtu ni mgonjwa au kiwete au ana matatizo mengine ambayo yanamfanya asiweze kusimama ataswali kwa kukaa au kulala ubavu kama Hadithi ilivyoeleza hapo juu. Na ikiwa hawezi kwa njia hizi basi hata kwa ishara, kwani swalah haina udhuru wa kuachwa isipokuwa kwa wanawake katika damu ya mwezi au ya uzazi, mtu ambaye ni mwendawazimu, au mtu ambaye yupo katika coma (amezirai kabisa).

Mtu anayeswali nyuma ya Imaam anafaa amfuate Imaam anavyoswali na ikiwa atashindwa kusimama, hivyo akiswali kwa kukaa na maamuma wataswali kwa kukaa.

((Wakati Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa mgonjwa aliswali kwa kukaa na akawaamuru wanaoswali nyuma yake pia kukaa)) (Imepokewa na al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Anas bin Maalik [Radhiya Allaahu 'anhu]).

((Imepokewa kwa Jaabir bin Abdillaah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipanda farasi Madinah. Farasi huyo alimwangusha kwenye mzizi wa mtende, hivyo mguu wake kuumia. Tulimzuru ili kujua hali yake na tukamkuta akiswali kwa kukaa katika chumba cha mama wa waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha). nasi tulisimama kuswali nyuma yake. Alinyamaza kimya. Tulimtembelea tena ili kumjulia hali tukamkuta anaswali Swalah ya faradhi kwa kukaa. Tulisimama nyuma yake naye akatuashiria tukae nyuma yake, nasi tukakaa. Alipomaliza Swalah alisema: “Imaam anaposwali kwa kukaa, nanyi swalini kwa kukaa na Imaam akiswali kwa kusimama swalini hivyo pia. Musiwe kama watu wa Fursi walipokuwa wakiamiliana na watemi (viongozi) wao (yaani watu walikuwa wanasimama nao walikuwa wanaketi))” (Abu Dawud).

Hadiyth hizi za kuonyesha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaagizia Masahaba wawe ni wenye kumfuata Imaam ni nyingi, hivyo Imaam akipiga takbiyr maamuma pia wafanye hivyo. Imaam akiswali kwa kukaa watu pia nao waswali kwa kukaa (al-Bukhaariy na Abu Dawud, Maalik).

Mtu anaweza kuswali Swalah ya Nafli kwa kukaa au kwa kusimama, kwani si wajibu kusimama kwayo. Hili limethibiti kutoka kwa

((Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alikuwa akiswali kwa kukaa na kusimama bila udhuru wowote)) (Imepokewa na Muslim kutoka kwa mama wa waumini ‘Aaishah na pia Abu Hurayrah [Radhiya Allaahu 'anhu]).

Watangu wema (Salafu Swaalih) pia walikuwa wakifuata mwendo huo, Yahya anasema, Maalik anasema alisikia kuwa Urwa ibn az-Zubayr na Said ibn al-Musayyab walikuwa wakiswali Swalah za Sunnah kwa kukaa.

Hivyo, ikiwa mtu ameshindwa kuswali kwa kusimama ataswali kwa njia ambayo anaiweza.

Na Allaah Anajua zaidi
 
Tunaendelea na darsa ya Swala ya Mtume s.a.w


011-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Swalah Kulielekea Kaburi, Nia, Takbiyr, Kunyanyua Mikono Na Kufunga Mikono Wa Kulia Juu Ya Kushoto








SWALAH KULIELEKEA KABURI



Alikuwa akikataza kuswali kwa kuyaelekea makaburi akisema:

((Msiswali kuelekea makaburi na msiyakalie)).[1]










NIA[2]




Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema:

((Vitendo vinategemea (vinalipwa kwa) nia na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokusudia)).[3]







TAKBIYR



Kisha Yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akianza Swalah kwa kusema:


‘Allaahu Akbar’.[4]




Alimuamrisha 'mtu aliyeswali vibaya' afanye kama ilivyotajwa na akamwambia: ((Hakika Swalah ya mtu haikamiliki hadi awe ametawadha kwa wudhuu uliyokamilisha viungo vya mwili kisha akasema Allaahu Akbar)).[5]




Pia alikuwa akisema:

((Ufunguo wa Swalah ni Twahara, inaharamishwa (inaanzwa) na Takbiyr na inahalalishwa (inamalizikia) na Tasliym)).[6]




Pia "alikuwa akipandisha sauti yake kutamka Takbiyr hadi walio nyuma yake walimsikia"[7]. Lakini "anapoumwa, Abu Bakr alikuwa akipandisha sauti yake kutamka Takbiyr kwa niaba ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم).[8 ]




Alikuwa akisema pia:

((Imamu anaposema: Allaahu Akbar, basi sema: Allaahu Akbar)).[9]







KUNYANYUA MIKONO



Alikuwa mara nyingine akinyanyua mikono pamoja na Takbiyr.[10] Mara nyingine baada ya Takbiyr[11] na mara nyingine kabla yake.[12]




Alikuwa akiinyanyua kwa kuvinyosha vidole vyake (sio kwa kuvitawanya wala kuvibana pamoja)[13] na "alikuwa akiiweka (mikono) sambamba na mabega yake"[14] ingawa kwa nadra, "alikuwa akiinyanyua hadi ifikie sawa na (ncha ya juu ya) masikio yake".[15]







KUWEKA (KUFUNGA) MKONO WA KULIA JUU YA MKONO WA KUSHOTO NA KUAMRISHWA KWAKE



"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto"[16] na alikuwa akisema:

((Sisi, Mitume, tumeamrishwa kukimbilia kufungulia Swawm, kuchelewa (kula) daku na kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto katika Swalah)).[17]




Vile vile: "alimpitia mtu aliyekuwa akiswali aliyeweka mkono wake wa kushoto juu ya mkono wa kulia, akamvuta kuondosha kisha akauweka wa kulia juu ya kushoto"[18]










[1] Muslim, Abu Daawuud na Ibn Khuzaymah.

[2] An-Nawawiy amesema katika Radhwah Atw-Twaalibiyn (1/224 iliyochapishwa na Maktab Al-Islaamiy): "Nia ni kusudio, kwa hiyo mtu anayetaka kuswali, hutia akilini tayari hiyo Swalah pamoja na yanayohusika nayo ya sifa zake, mfano kama ni Swalah ya kipindi kipi, je, ni Swalah ya faradhi n.k. ndipo huleta hivi vyote katika nia yake pamoja na Takbiyr ya mwanzo".

[3] Al-Bukhaariy na Muslim na wengineo. Imetolewa pia katika Al-Irwaa (Namba: 22).

[4] Muslim na Ibn Maajah. Hadiyth inaashiria kwamba hakuwa akianza (Swalah) kwa maneno ya baadhi ya watu: "Nawaytu Uswalliy… n.k" ambayo imekubalika kuwa ni bid'ah (uzushi). Bali wamekhitilafiana kama ni bid'ah njema au mbaya ambayo tunasema: Hakika bid'ah zote katika ibada ni upotofu, kutokana na kauli (صلى الله عليه وآله وسلم) ((…na kila bid'ah ni upotofu na kila upotofu ni motoni)). Lakini hapa sipo mahali pa maelezo marefu ya mas-ala haya.

[5] Atw-Twabaraaniy ikiwa na isnadi Swahiyh.

[6] Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na Al-Haakim ambao wamekiri usahihi wake na Adh-Dhahaabiy amekubali. Imetolewa katika Al-Irwaa (Namba: 301). Maana hasa ya 'inaharamishwa na Takbiyr', ni vitendo vyote ambayo Allaah Ameviharamisha wakati huo. 'na inahalalishwa na Tasliym' ni yote yaliyoruhusiwa nje ya Swalah. Kama vile Hadiyth ilivyothibitsha kuwa mlango wa Swalah umefungwa, hakuna mwenye kuabudu anaweza kufungua isipokuwa kwa Twahara, imethibitisha pia kuwa Swalah haiwezi kufunguliwa (kuanzishwa) isipokuwa kwa Takbiyr na haiwezi kumalizika bila ya Tasliym. Hii ni rai iliyokubalika kwa wengi wa Maulamaa.

[7] Ahmad, Al-Haakim ambao wamekiri kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana.

[8] Muslim na An-Nasaaiy.

[9] Ahmad na al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[10] Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy.

[11] Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy.

[12] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[13] Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah (1/62/2, 64/1), Tammaam Na Al-Haakim ambao wamekiri ni Swahiyh na Adh-Dhahaabiy amekubaliana.

[14] Al-Bukhaary na An-Nasaaiy.

[15] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[16] Muslim Na Abu Daawuud, pia imetolewa katika Al-Irwaa (352).

[17] Ibn Hibbaan na Adh-Dwiyaa ikiwa na isnaad Swahiyh.

[18] Ahmad Na Abu Daawuud ikiwa na isnaad Swahiyh.
 
012-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kuweka Mikono Juu Ya Kifua, Kutazama Mahali Pa Kusujudu, Na Khushuu (Unyenyekevu) Katika Swalah


KUWEKA MIKONO JUU YA KIFUA




"Alikuwa akiweka mkono wa kulia nyuma ya kitanga cha mkono wa kushoto, kiwiko na kigasha"[1] "na aliwaamrisha Maswahaba wake kufanya hivyo"[2] na (mara nyingine) "akiushika mkono wa kushoto kwa mkono wake wa kulia"[3]




"Alikuwa akiiweka juu ya kifua chake"[4]




Pia, alikuwa akikataza mtu kuweka mkono juu ya kiuno wakati wa Swalah na aliweka mkono wake juu ya kiuno (kuonyesha makosa hayo)[5] Na hii ndio swilb aliyokuwa akikataza.[6]










KUTAZAMA MAHALI PA KUSUJUDU NA KUSHUU (UNYENYEKEVU)




"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiinamisha kichwa chake wakati wa Swalah na kukongomeza (kuyaelekeza) macho yake katika ardhi[7]

"Alipoingia katika Kaabah, hakuacha jicho lake kutazama sehemu ya kusujudu hadi alipotoka nje"[8] na alisema: ((Haipasi kuweko na kitu chochote katika Nyumba kitakachomshawishi mwenye kuswali))"[9]




"Alikuwa akikataza kuinua macho kutazama mbinguni"[10] na alishikilia makatazo haya sana hadi alisema: ((Watu lazima waache kutazama juu mbinguni katika Swalah au macho yao hayatorudi kwao)) [na katika riwaaya nyingine] ((…au macho yao yatapofushwa))[11]




Katika Hadiyth nyingine: ((Mnaposwali msiangaze huku na kule kwani Allaah Huelekeza Uso Wake mbele ya uso wa mja Wake madamu mja hatoangaza kwengine)).[12] Akasema pia kuhusu kuangaza huku na kule: ((Ni kunyakuliwa ambako Shaytwaan hunyakuwa katika Swalah ya mja anaposwali))[13]




Akasema pia (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Allaah Haachi kuelekea kwa mja katika Swalah madamu tu mja haangazi huku na kule, anapogeuza uso wake mbali, Allaah Hugeuka mbali naye))[14] na "Akakataza mambo matatu; kudonoa kama jogoo, kuchutama kama mbawa na kuangaza kama fisi",[15] vile vile alikuwa akisema: ((Swalini Swalah ya kuaga (dunia) kama kwamba mnamuona Yeye (Allaah) na kama hamumuoni, hakika Yeye Anakuoneni))[16], na (akisema), ((Mtu yeyote anayefikwa na Swalah ya fardhi akatawadha vizuri, akakamilisha khushuu (unyenyekevu) zake, na rukuu zake, hakika itakuwa ni kafara ya dhambi alizotenda kabla ya Swalah hiyo madamu hajatenda dhambi kubwa, hali hiyo ni kwa mwaka wote))[17]




Mara moja yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali katika khamiysah[18] (na alipokuwa akiswali) alizitazama alama zake. Alipomaliza akasema: ((Ipelekeeni khamiysah hii yangu kwa Abu Jahm na nileteeni (badala yake) anbijaaniyyah[19] kwani imenipotezea umakini wangu katika Swalah)) [katika usimulizi mmoja] ((…kwani nimetazama alama zake wakati wa Swalah ilikaribia kunitia katika mtihani))[20]




Pia Mama wa Waumini 'Aaishah (رضي الله عنها) alikuwa na kitambaa cha picha kilichotandazwa mbele ya sahwah[21] ambayo Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali mbele yake, akasema: ((Iondoshelee mbali, [kwani picha zake hazikuacha kunishawishi katika Swalah]))[22]

Alikuwa akisema pia: ((Hakuna kuswali chakula kinapokuwa tayari, wala mtu anapotaka kukidhi haja kubwa na ndogo))[23]







[1] Abu Daawuud, An-Nasaaiy na Ibn Khuzaymah (1/54/2) ikiwa na isnaad Swahiyh na Ibn Hibbaan amekiri usahihi wake (485).

[2] Maalik, Al-Bukhaariy na Abu 'Awaanah.

[3] An-Nasaaiy na Ad-Daraqutwniy ikiwa na isnaad Swahiyh. Katika Hadiyth hii kuna ushahidi kwamba kuishikilia ni Sunnah na katika Hadiyth nyingine, kuwekea tu, hivyo yote ni Sunnah. Ama kuunga baina ya kuweka na kushikilia ambayo baadhi ya Mahanafi waliotangulia wameona ni vizuri, hivyo ni bid'ah; mfumo wake ni kama walivyotaja kuwa ni kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto, kushikilia kiwiko kwa kidole kidogo na cha gumba, na kuviweka bapa vidole vitatu vengine, kama ilivyoelezewa katika tanbihi za Ibn 'Aabidiyn kwenye Durr Al-Mukhtaar (1/454) kwa hiyo usibabaike na wasemayo.

[4] Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1/54/2) Ahmad na Abu Shaykh katika Taariykh Iswbahaan (Uk.125), At-Tirmidhiy amekiri moja ya isnaad ni hasan (njema) na maana yake inapatikana katika Al-Muwattwaa na Swahiyh Al-Bukhaariy ikichukuliwa kwa makini. Nimenukuu isnaad kamili ya Hadiyth hii katika kitabu changu Ahkaam al-Janaaiz (Uk. 118).




TANBIHI:

Kuiweka katika kifua ndivyo ilivyothibiti katika Sunnah, na kinyume chake ni aidha dhaifu au haina msingi. Na Imaam Is-haaq Ibn Raahawayh alifanya Sunnah hii kama alivyosema Al-Marwazy katika Masaail (Uk. 222). "Is-haaq alikuwa akiswali Witr pamoja na sisi … alikuwa akinyanyua mikono yake katika Qunuut na akileta Qunuut kabla ya kurukuu na kuweka mikono yake kifuani mwake au chini yake". Ni sawa na usemi wa Qaadhwiy 'Iyaadh Al-Maalikiy katika Mustahabbaat As-Swalah kitabu chake Al-I'laam (Uk. 15, chapa ya 3, Ar-Rabaatw) "Mkono wa kulia uwekwe juu ya mkono wa kushoto sehemu ya juu ya kifua". Na karibu na hii ni kama alivyohusisha 'Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal katika Masaail yake (Uk. 62): "Niliona wakati wa kuswali, baba yangu akiweka mikono yake mmoja juu ya mwenziwe juu ya kitovu (chini ya kifua kidogo)" Tazama Kiambatisho 4.






[5] Al-Bukhaariy na Muslim.

[6] Abu Daawuud, An-Nasaaiy na wengineo.

[7] Al-Bayhaaqiy na al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh kama alivyosema. Pia ina Hadiyth iliyotilia nguvu iliyoripotiwa na Maswahaba kumi: iliyosimuliwa na Ibn 'Asaakir' (17/202/2) Taz. Al-Irwaa (354).




TANBIHI:

Hadiyth hizi mbili zinaonyesha kwamba Sunnah ni kukaza macho yake mtu mahali pa kusujudu ardhini, hivyo kufunga macho katika Swalah kama wafanyavo baadhi ya watu ni ukosefu ya uchaji Mungu, kwani uongofu bora kabisa ni uongofu wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).




[8] Al-Bayhaaqiy na al-Haakim.

[9] Abu Daawuud na Ahmad ikiwa ni isnaad ya Swahiyh (Al-Irwaa 1771); iliyokusudiwa hapa 'Nyumba' ni Kaabah kama inavyoonyesha yaliyomo katika Hadiyth.

[10] Al-Bukhaary Abu Daawuud.

[11] Al-Bukhariy, Muslim na Siraaj.

[12] At-Tirmidhiy na al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh – (Swahiyh At-Targhiyb Namba: 353).



[13] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[14] Imesimuliwa na Abu Daawuud na wengineo. Ibn Khuzayma na Ibn Hibbaan wamekiri usahihi wake. Taz. Swahiyh At-Targhiyb (Namba 555).

[15] Ahmad na Abu Ya'laa. Taz Swahiyh At-Targhiyb (Na,ba 556)

[16] Al-Mukhlisw katika Ahaadityh Muntaqaa, At-Twabaraaniy, Ar-Ruuyaaniy, Adh-Dwiyaa katika Al-Mukhtaarah, Ibn Maajah, Ahamd na Ibn 'Asaakir. Al-Hayatamy amekiri ni Swahiyh kaitka Asnan Al-Matwaalib

[17] Muslim.

[18] Nguo ya sufi iliyo na alama.

[19] Nguo ya kukwaruza isiyo na alama.

[20] Al-Bukhaariy, Muslim na Maalik imetolewa katika Al-Irwaa (376)

[21] Chumba kidogo kilichobanwa kidogo katika ardhi kama chemba au kabati. (Nihaayah)

[22] Al-Bukhaariy, Muslim na Abu 'Awaanah. Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuamrisha kufutwa au kuchana picha bali aliziondosha kwa sababu. Na Allaah Anajua zaidi- hazikuwa ni picha zenye roho. Ushahidi wa hili ni kwamba yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) alichana picha nyinginezo kama ilivyothibiti katika usimulizi mwingi katika Al-Bukhaariy na Muslim na yeyote apendaye kutafiti zaidi atazame Fat-h Al-Baariy (10/321) na Ghaayah Al-maraam fiy Takhriyj Ahaadiyth Al-Halaal wal-Haraam (Namba: 131-145).

[23]Al-Bukhaariy na Muslim.
 
Amri bin Shuaib r.a amesimulia kuwa kwa hakika Rasulullah s.a.w amesema "Mwanzo wa kutengenea umma huu kulikuwa ni kutokana na Yakini na (imani madhubuti) na zuhd (kujitenga na raha za dunia)na mwanzo wa kuharibika kwa umma huu kutakuwa ni kutokana na ubahili na matumaini ya mda mrefu


Umar bin Khattab r.a amesimulia kuwa Rasullahi s.a.w amesema " Kama mungelikuwa mnamtegemea Allah inavyostahiki,basi mungeruzukiwa kama wanavyo ruzukiwa ndege. Wanatoka asubuhi matumbo yao yakiwa matupu na wanarudi jioni yameshajaa


Maiz r.a amesimulia kuwa aliulizwa Rasullahi s.a.w kuwa: "Ni amali gani zilizo bora zaidi (zenye fadhila) akasema "Kumuamini Allah peke yake,kisha jihadi,kisha hijja iliyokubaliwa. Amali hizi zinazidi nyingine zote kwa utukufu kama nafasi iliyo baina ya kuchomoza jua na kuzama kwake magharibi


Amr bin Abasah r.a aliuliza Imani ipi ni bora zaidi? Nabii s.a.w akajibu : "Hijra (kuhama) ,na akauliza tena : "Nini Hijra" akajibu "Kuyama Maovu


Sufyan bin Abdullah r.a amesema Nilisema "Ewe Rasullahi niambie jambo muhimu zaidi katika Uislamu,ambalo sitamuuliza baada yako jambo hilo mtu mwingine,na katika hadith ya Abu Usama "asie kuwa wewe"
Akasema "Sema namuamini Allah.kisha kuwa imara (kuwa na istiqaama)

Maelezo: Kwanza kumuamini Allah na sifa zake zote kisha kuzikubali amri zake zote na zile za Mjumbe wake. Imani hii na kutii huko kunapaswa kusiwe kwa kupita tu (kwa mda) lakini kunatakiwa kushikwe imara (daima)
 
Screenshot_20250415_154735_Quran Swahili.jpg


Aya hii katika Suratil Ambiyau / the prophets kwa ufupi kabisa inaeleza Kadar ya Allah

Kuwa kheri na shari ni mitihani ya Allah kwetu sisi,je tutakufuru au kushukuru
 
Salehe ibn Mismar na Jafar ibn Burqan (Rahimahumallahu) wamesimulia kuwa Nabii s.a.w alimuuliza Harith Ibn Malik: " Vipi hali yako ewe Harith Ibn Malik"?
Akajibu "Muumini ewe Rasullahi"
Akasema Rasulillahi " Muumini wa kweli"?
Akajibu "Muumini wa kweli"

Rasullullahi akasema "Kila kitu cha kweli kina udhibitisho wake,kwa hivyo ni nini uhakikisho wa Imani yako?
Akajibu " Nimejitenga na dunia na nikakesha usiku wangu ( katika kumuabudu Allah) na nikapitisha mchana wangu nikiwa mwenye kiu (nimefunga saumu). Na kama kwamba ninaiona Arshi ya Mola wangu wakati itakapo letwa,na kama kwamba ninawaona wakazi wa Jannah wakitembeleana baina yao humo. Na kama kwamba ninasikia makelele ya watu wa motoni". Kwa hayo akasema Rasullullahi swallallahu alaih wasallam: "Muumini ambaye moyo wake umeng'ara

(Musannaf Abdu Razaq)


Abdullah Ibn Amir Ibn Al'As r.a amesema kuwa Rasullullahi amesema: "Hakika Imani nyoyoni mwenu inachakaa kama inavyochakaa nguo na kuwa mbovu. Kwahivyo muombeni Allah,azifanye mpya Imani nyoyoni mwenu."

(Mustadrack Hakim)
 
013-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Du'aa Za Kufungulia Swalah




DU'AA ZA KUFUNGULIA




Kisha alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akianza kusoma kwake kwa aina nyingi za du'aa ambazo akimsifu na kumtukuza na kumuadhimisha Allaah (سبحانه وتعالى). Alimuamrisha "mtu aliyeswali vibaya" afanye hivyo akimwambia: ((Swalah ya mtu haikamiliki hadi atamke Takbiyr, amsifu Allaah (سبحانه وتعالى), amtukuze na amuadhimishe asome iliyo nyepesi katika Qur-aan…..))[1] .




Alikuwa akisoma du'aa zozote katika hizi zifuatazo:




1.









"Ee Allaah! Niweke mbali na madhambi yangu kama Ulivyoweka mbali baina ya Mashariki na Magharibi, Ee Allaah! Nitakase na madhambi yangu kama vile inavyotakaswa nguo nyeupe na uchafu, Ee Allaah! Nisafishe na madhambi yangu kwa theluji na kwa maji na kwa barafu"[2]

(Na alikuwa akisema katika swala za fardhi):

2.










“Nimeuelekeza uso wangu kwa yule Ambaye Ameumba mbingu na ardhi hali ya kumtakasia yeye dini yangu, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika Swalah yangu na kuchinja kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Allaah Bwana wa viumbe vyote, Hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa, nami na mimi ni wa kwanza waliojisalimisha.[3] Ee Allaah! Wewe ndiye Mfalme, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, Wewe ndiye Bwana wangu na mimi ni mtumwa (mja) Wako[4] Nimedhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nisamehe madhambi yangu yote, hakika hasamehe madhambi, ila Wewe. Na niongoze kwenye tabia nzuri, kwani haongozi kwenye tabia nzuri ila Wewe. Na Niepushe na tabia mbaya, kwani hakuna wa kuniepusha na tabia mbaya ila Wewe. Naitikia mwito Wako, na nina furaha kukutumikia.[5] Kheri zote ziko mikononi Mwako, na shari haitoki Kwako[6], Na ameongoka yule Uliyemuongoa, mimi nimepatikana kwa ajili Yako, hapana penye uokovu wala wa pa kukimbilia isipokuwa Kwako, umetakasika, na umetukuka, nakutaka msamaha na ninarejea Kwako (kwa kutubia).”




Alikuwa akisema hivyo katika Swalah za fardhi na za Sunnah[7]










3. Hii du’aa ni kama iliyo juu bila ya:













“Wewe Ni Mola wangu nami ni mja Wako…”




Hadi mwishoni pamoja na nyongeza ifuatayo:
















“Ee Allaah, Wewe Ni Mfalme, hapana apasaye kuabudiwa isipokuwa Wewe, Kutakasika ni Kwako na Sifa njema zote ni Zako”[8]







4- Kama na Namba 2 hadi,
















“…nami ni Muislamu wa mwanzo,




Na akiongeza,



















Ewe Allaah, niongoze kwenye tabia njema (nzuri) na vitendo vyema haongozi kwenye uzuri wake ila Wewe. Niepushe na tabia mbaya na vitendo vibaya hakuna mwenye uwezo wa kupesuha??? ubaya wake ila Wewe [9].







5-



















Kutakasika ni Kwako[10] Ee Allaah, na sifa njema zote ni Zako[11], na limetukuka Jina Lako[12], na Utukufu ni Wako[13], na hapana apasae kuabudiwa kwa haki, asiyekuwa Wewe[14]

Alisema (صلى الله عليه وآله وسلم) pia: ((Hakika maneno yanayopendwa kabisa na Allaah ni mja Wake anaposema: (سبحانك اللهم) Umetukuka Ewe Allaah…”[15]







6- Kama ilivyo juu kwa kuongeza katika Swalah za usiku:


















“Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah”




Mara tatu na













“Allaah ni Mkubwa”







Mara tatu







7-
















“Allaah Ni Mkubwa, Na sifa njema ni za Allaah kwa wingi, Ametakasika Allaah asubuhi na jioni.”
















Mmoja wa Maswahaba alifungua Swalah yake kwa du’aa hiyo, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: ((Imenipendeza hiyo (du'aa) kwani kwayo milango ya Pepo imefunguliwa))[16]







8-





















“Sifa njema ni za Allaah, sifa nyingi, nzuri, zenye Baraka”




Mtu mwengine alifungua Swalah yake kwa du’aa hiyo, kisha Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Nimewaona Malaika kumi na mbili wakishindana nani atakayeipeleka juu))[17]







9-







“Ee Allaah ni Zako sifa njema, Wewe ndiye nuru[18] ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na ni Zako sifa njema. Wewe ndiye Mwenye kuzisimamia[19] mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, [na ni Zako sifa njema, Wewe ni Mfalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake], na sifa njema ni Zako, Wewe ni Haqq, na ahadi Yako ni ya Haqq, na neno Lako ni Haqq, na kukutana Nawe ni Haqq, na Pepo ni Haqq, na Moto ni Haqq, na Sa’ah (Qiyaamah) ni Haqq, na Mitume ni Haqq, na Muhammad ni Haqq, Ee Mola Kwako nimeweka imani yangu, na Kwako nimetegemea, na Kwako ndio nakurejelea, nimepigana kwa ajili Yako, na kwa hukumu Zako ndio nazifuata zinihukumu, [Wewe ndiye Mola wetu na Kwako ndio tunaishia, nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza], [Na yote unayoyajua kutoka kwangu] Wewe ndiye mwenye kutanguliza na ndiye mwenye kuchelewesha, [Wewe ni Mola wangu] hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe[20];

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema hivi katika Swalah ya usiku alipokuwa akisoma du'aa ifuatayo[21]:




10-













“Ewe Mwenyezi Mungu Mola wa Jibiriyl na Mikaaiyl na Israafiyl, Muumba wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa mambo yaliojificha na yaliyowazi, Wewe unahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitofautiana, niongoze mimi kwenye haki katika yale waliyotafautiana kwa ruhusa Yako. Hakika Wewe unamuongoza umtakae kwenye njia iliyonyoka[22]”







11- Alikuwa akisema Takbiyr, Tahmiyd, Tasbiyh, Tahliyl na Istighfaar mara kumi kila moja na akisema:
















“Ee Allaah, nighufurie na niongoze na niruzuku [Na Nisamehe madhambi yangu]” mara kumi kisha akisema:
















“Ee Allaah, Najikinga Kwako na dhiki za Siku ya Hisabu”[23]




Mara kumi










12-













“Allaah ni Mkubwa [mara tatu] Mwenye Ufalme, Nguvu, Ufakhari na Utukufu”[24]










[1] Al-Bukhaariy, Muslim na Ibn Abi Shaybah (12/110/2) imetolewa katika Al-Irwaa (Namba 8)

[2] Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana.




[3] Imesimuliwa katika usimulizi mwingi, katika mwengine, 'Wa Anaa Minal-Muslimiyn’ (Mimi ni miongoni wa Waislamu). Inaweza kuwa ni kutokana na makosa ya usimulizi mmojawapo, na ushahidi mwingine unaelekeza hapo, kwa hiyo mwenye kuswali aseme: ‘Wa Anaa Awwalul-Muslimiyn’ (Nami ni Muislamu wa mwanzo). Hakuna makosa hivyo, kinyume na watu wanavyosema kwa uoni kwamba inamaanisha "Mimi ni Muislamu wa kwanza mwenye sifa hii, na watu wengine hawana sifa hii". Lakini sio hivyo, ibara hii inaashiria kushindana katika kutekeleza amri. Hii ni sawa na ((Sema: Ingelikuwa ar-Rahmaan ana mwana, basi mimi ningelikuwa wa kwanza kumuabudu)) [Az-Zukhruf, 43: 81] na kauli ya Muusa ('Alayhis-Salaam) ((na mimi ni wa kwanza wa Waumini)) [Al-A'raaf 7: 143].

[4] Al-Azhariy amesema kwamba, "Siabudu chochote kingine isipokuwa Wewe"

[5] Labbayk: Niko thabiti na daima niko katika utiifu Wako. Sa'dayk: Furaha kubwa kuwa katika amri Yako na kufuata kwa dhati dini Uliyoichagua.

[6] Yaani, Uovu haunasibishwi kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa sababu hakuna chochote kibaya katika vitendo Vyake, kwani vyote ni vyema vikianzia kutoka uadilifu, fadhila na hikma vyote ambayo ni kheri na havina shari ndani yake bila ya kuwa na shari ndani yake. Kwa sababu shari imekuwa shari kwa sababu hauwezi kurudia kwa Allaah. Ibn Al-Qayyim (Rahimahu-Allaah) amesema: "Yeye ni Muumba wa mema na maovu, lakini maovu yako katika baadhi ya viumbe Vyake, na sio katika kuumba Kwake na sio katika vitendo Vyake. Kwa ajili hiyo Ametakasika na dhulma ambayo asili yake ni kuweka kitu katika sehemu nyingine isiyopasa. Haweki kitu isipokuwa katika mahali panapostahiki ili yote yawe mema. Lakini uovu ni kuweka kitu mahali pasipostahiki. Kinapowekwa katika mahali panapostahiki, huwa si kiovu, kwa hiyo jua kuwa uovu hautoki Kwake. Lakini ikisemwa: Kwa nini Ameumba maovu? Nitasema: Ameumba, na vitendo Vyake ni vizuri sio viovu kwani kuumba na vitendo vinasimama na Allaah, haiwezekani uovu kufanywa au kuhusishwa na Allaah. Chochote kilichokuwa kiovu hakiwezi kurudishwa kwa Allaah, ama vitendo na Alivyoviumba vinaweza kuhusishwa Naye, na vinakuwa ni vyema". Majadiliano muhimu yaliyobakia na kimalizio chake kitapatikana katika kitabu chake Shifaa Al-'Aliyl fiy Massail al-Qadhwaa wal-Qadar wat-Ta'liyl – taz (uk. 178-206).

[7] Muslim, Abu 'Awaanah, Abu Daawuud, An-Nasaaiy, Ibn Hibbaan, Ahmad, Ash-Shaafi'iy na At-Twabaraaniy. Walioeleza kuwa ni Swalah za Sunnah wamekosea.

[8] An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[9] An-Nassaiy na Ad-Daaraqutwniy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[10] Nakutukuza ina maana kwamba nazingatia kuwa Umetakasika na kasoro yoyote. Na ‘Sifa njema’ maana yake ni kuwa tumezijua vizuri sifa Zako. Na ‘Kutakasika’ maana yake ni wingi wa kutakasika kwa jina Lako, kwa sababu kila la kheri linapatikana katika kulitaja jina Lako. ‘limetukuka Jina Lako’ maana yake ni kuwa limenyanyuka juu jina Lako (utukufu wako).

[11] Tumeshikamana katika kukusifu.

[12] Baraka za Jina Lako ni kubwa, kwani makubwa yaliyo mazuri hutokana na kukumbuka Jina Lako.

[13] Utukufu na Nguvu Zako.

[14] Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana. 'Uqayl amesema (Uk. 103) "Hii imesimuliwa kupitia njia mbalimbali kwa isnaad Swahiyh". Imetolewa katika Al-Irwaa (Namba 341) Imesimuliwa na Ibn Mandah katika At-Tawhiyd (123/2) kwa isnaad Swahiyh na An-Nasaaiy katika Al-Yawm wal-Laylah ikiwa ni mawquuf na marfuu' kama katika Jaami' Al-Masaaniyd ya Ibn Kathiyr (Mj. 3 Kifungu 2. Uk. 235/2)



[15] Abu Daawuud na Atw-Twahaawiy kwa isnaad Swahiyh.

[16] Muslim Na Abu Awaanah; At-Tirmidhiy kasema ni Swahiyh. Kadhalika Abu Na’iym ameisimulia katika ‘Akhbaar Aswbahaan’ (1/210) kutoka kwa Jubayr bin Mutw-am ambaye alimsikia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akiisoma kwenye Swalah ya Sunnah.

[17] Muslim na Abu 'Awaanah

[18] Wewe Ndiye Mwenye kuzipa mwanga na Kwayo ndio Wanaopata uongofu kutoka Kwako.

[19] Mwenye kuhifadhi na Mchungaji wao.

[20] Al-Bukhaariy na Muslim, Abu 'Awaanah, Abu Daawuud, Ibn Nasr na Ad-Daarimiy.

[21] Ingawa inapaswa kusomwa katika Swalah za fardhi pia, isipokuwa kwa Imaam kwa khofu ya kurefusha Swalah kwa Maamuma.

[22] Muslim na Abu 'Awaanah.

[23] Ahmad, Ibn Abi Shaybah (12/119/2), Abu Daawuud na At-Twabaraaniy katika Mu'jam al-Awswatw (62/2) ikiwa na isnaad moja Swahiyh na nyingine Hasan.

[24] At-Twayaalisiy na Abu Daawuud ikiwa na isnaad Swahiyh.
 
014-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Katika Swalah, Na Kusoma Aayah Moja Moja


KISOMO (TILAAWAH)




Kisha alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akijikinga kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kusema:





A’udhu bil Llaahi minash Shaytwaanir Rajiiymi Min Hamzihii Wa Nafkhihii Wa Nafathihi

“Najilindia na Allaah kutokana na Shaytwaan aliyefukuzwa, najilinda na (kutokana na) wazimu wake[1] na kiburi chake, na ushairi [kutabana] wake[2]

Mara nyingine huongeza kwa kusema,


A’udhu bil Llaahis Samiy’il ‘Aliymi Minash Shaytwaanir…

Najikinga kwa Allaah, Mwingi wa Kusikia, Mwenye Ujuzi, kutokana na Shaytwan…[3]

Kisha husoma,


Bismi-Llaahir Rahmaanir Rahiym

Kwa Jina la Allaah,Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.

Hakuwa akinyanyua au kupaza sauti[4]










KUSOMA AAYAH MOJA MOJA




Kisha alikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Suratul-Faatihah na akigawanya (kisomo chake,) kwa kuisoma Aayah moja moja; kama hivi:








BismiLlaahir Rahmaanir Rahiym

[Kisha hupumua/husimama, kisha husema:]


AlhamduliLlaahi Rabbil ‘Aalamiyn

[Kisha hupumua/husimama, kisha husema:]


Ar-Rahmaanir-Rahiym

[Kisha hupumua/husimama, kisha husema:]


Maaliki Yawmid Diyn

Kisomo chake kilikuwa kama hivyo, hadi mwisho wa Surah. Na hivyo hasa ndivyo ilivyokuwa kisomo chake chote, kila anaposoma huwa anasimama/anapumua mwisho wa Aayah na wala haiunganishi na Aayah inayofuatia[5].

mara nyingine alikuwa akiisoma bila ya kuivuta/bila ya kutia madda[6] (alisoma):


Malik Yawmid Diyn

Mfalme wa Siku Ya Qiyaamah




(badala ya


Maaliki Yawmid Diyn




Mwenye kumiliki Siku Ya Qiyaamah)












[1] Maneno matatu ya Kiarabu; hamz, nafkh na nafth yamefasiriwa na baadhi ya wapokezi kuwa hamz ni aina ya wazimu, na nafkh ni kiburi, na nafth ni ushairi; yametafsiriwa hivyo hivyo na msimulizi; tafsiyr zote tatu zimepokewa (zimerudiwa pia) marfuu’an kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa isnaad Swahiyh Mursal (Ni hadiyth katika isnaad yake hakutaja Swahaba, bali kataja Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)). Na kusudio la (kwa) 'ushairi' [kutabana] hapa ni mashairi yasiyokubalika/yasiyo na heshima/yenye kudharauliwa (ina maana kwa majaribio yasiyo na mafanikio) kwani Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika katika baadhi ya ushairi kuna (ni) hikma)) [Al-Bukhaariy)

[2] Abu Daawuud Ibn Maajah, Ad-Daaraqutwny na Al-Haakim ambaye pamoja na Ibn Hibban na Adh-Dhahaabiy wamesema ni Swahiyh. Imetolewa pamoja na inayofuatia katika Al-Irwaa Al-Ghaliyl (342)



[3] Abu Daawuud na At-Tirmidhiy kwa isnaad nzuri. Ahmad ameinukuu katika Massail ya Ibn Haaniy 1/50

[4] Al-Bukhaariy, Muslim, Abu 'Awaanah, At-Twahaawiy na Ahmad.




[5]Abu Daawuud na Sahmiy (64-65); Al-Haakim amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amakubaliana naye. Imetolewa katika Al-Irwaa (343). Na ameipokea Abu 'Amr Ad-Daaniy katika Al-Muktafaa (5/2) na kasema: Hadiyth hii ina njia nyingi na ndiyo tegemeo katika mlango huu, kisha akasema: (na) Kundi la Maimamu wengi waliotangulia na Maqurraa (wasomaji wa Qur-aan) waliopita walikuwa wakipendelea kusimama katika kila Aayah hata kama (Aayah nyingine) itakuwa imefungamana katika maana na Aayah ijayo") Nasema: Sunnah hii imepuuzwa na Maqurraa (wasomaji wa Qur-aan) wengi wa nyakati hizi, achilia mbali wengineo ambao si Maqurraa.

[6] Tamaam Ar-Raaziy katika Al-Fawaaid, Ibn Abu Daawuud katika Maswaahif (7/2), Abu Nu'aym katika Akhbaar Aswbahaan (1/104) na Al-Haakim ambaye amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahaby amekuliana naye, qiraa/kisomo hichi ‘Malik’ ni mutawaatir pia kama kilivyo kile qiraa cha kwanza ‘Maalik’.
 
Eti ndugu yangu Muislamu unaruhusu vipi kukosekana kwa maneno machache tu ya kutamkwa ndiyo kukufanye uingie Motoni

Maneno yenyewe,walii anasema "Nimekuoza" nawe unasema "Nimemuoa"

Huenda yakarudiwa mara mbili au mara tu

Hapo tayar umehalalisha ndoa,mosi umeepukana na machafu na pili umemridhisha Allah na tatu umeondoa uwezekano wa kuepushwa na Moto

Kwasababu Nabii swallallahu alaih wasallam anasema "mambo mawili ni sababu ya watu wengi kuingia motoni,mosi kilicho katikati ya midomo miwili (ulimi)na pili kilichopo katikati ya mapaja mawili (tupu)

Naongea haswa na hawa ambao mnakaa kinyumba mnapika na kupakua lkn kupitisha ndoa kwa maneno hayo tu ndio shida

Je,umeagana na Mola wako kuwa atakuacha kwa mda fulani ndio atachukua roho yako? Hadi ukawa na uhakika wa kuishi hivyo unavyo ishi kwakuwa una uwakika wa maisha marefu huko mbeleni?

Maana kama umeweza kuishi na mtu na mnapika na kupakua je,kipikigumu kwenu?

Mtume swallallahu alaih wasallam anasema miongoni mwa mambo yatawaangamiza umma huu ni "Ubakhili na matumaini ya kuishi mda mrefu"

Hasa hili la kuishi mda mrefu kwa mtazamo wangu ndio linatupa matumaini sana kwamba ngoja tuishi hivi hivi kwanza halafu tutafunga ndoa huko mbeleni

Hala hala ndugu yangu tambua hakika uhai ni dhaman ya Allah,mda wowote na sasa yoyote mimi na wewe ni marehemu watarajiwa

Tumche Allah
 
Kuna tofauti ya ndoa na sherehe au harusi,cha msingi ni ndoa na si sherehe,waeza funga ndoa kwanza kisha sherehe ikafuata baadae Allah akijalia

Wengi wenu mnahofia kuwa huna hela ya kufanya sherehe ndio maana hamfungi ndoa,sherehe ni ziada ila ndoa ndio ya msingi

Tena alhamdulillah waislamu hatuna mambo.mengi, toa mahari hata ya kuanzia lkn hakikisha unakuja kuimaliza huko mbeleni,hata watu watano tu mnamaliza swala la ndoa,awepo Walii wa mke,muoaji na mashahidi wawili shughuli imekwisha

Masheikh huwepo tu kuwapa muongozo taratibu za kufuata lkn muozeshaji haswa ni walii

Hata mkiwa nchi za mbali,mnawasiliana na walii wa mke hata akiwa mbali akitoa ruhusa ndoa inapita

Umeona haya yote ni kuifanya hii ibada iwe nyepesi na tuwe wasafi na kuepuka machafu

Tumche Allah
 
Darsa la Swala ya Nabii swallallahu alaihi wasallam inaendelea.....


015-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Ulazima Wa Kusoma Suratul Faatihah Na Fadhila Zake




ULAZIMA (UFARADHI) WA AL-FAATIHA NA FADHILA ZAKE




Alikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akitilia mkazo na kusisitiza kuhusiana na (Alisisitiza mno) umuhimu wa Surah hii, alikuwa akisema: ((Hakuna Swalah kwa asiyesoma [ndani yake] Ufunguo wa Kitabu))[1]




Na Katika usemi mwengine: ((Swalah haitimii mtu asiposoma ndani yake Ufunguo wa Kitabu))[2]




Na wakati mengine anasema: ((Mwenye kuswali Swalah yoyote ile bila ya kusoma ndani yake Ufunguo wa Kitabu basi hiyo Swalah ni khiddaaj[3], ni khiddaaj, ni khiddaaj, haikukamilika))[4]




Na anasema (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa:




Allaah (سبحانه وتعالى) Amesema: "Nimegawa Swalah[5] baina Yangu na mja Wangu (katika) sehemu mbili; nusu ya kwanza ni Yangu na nusu nyengine iliyobaki ni ya mja Wangu, na mja Wangu atapata alichokiomba" (Kisha) Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Someni: Mja anasema: "Al-hamdu Llillaahi Rabbil ‘Alaamiyn”, Allaah (سبحانه وتعالى) Husema "Mja Wangu amenisifu" Mja akisema: "Ar-Rahmaanir Rahiym”, Allaah Husema: "Mja Wangu amenitukuza" Mja akisema: "Maalik/Malik”,Allaah Husema: Mja Wangu Ameniadhimisha" Mja akisema: "Iyyaaka na’budu wa iyyaaka nasta’iyn”, [Husema]: "Hii ni baina Yangu na Mja Wangu, na Mja wangu atapata atachoomba". Mja akisema: "Ih-dinaas swiraattal mustaqiym, swiraattal Laadhiyna An’amta ‘alayhim ghayril maghdhuubi ‘alayhim wala-dhwaaliyn”, [Husema] Yote haya ni ya Mja Wangu na Mja Wangu atapata aliyoyaomba"[6]




Alikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Allaah Aliyetukuka hakuteremsha katika Tawraat wala katika Injiyl chochote kile chenye kufanana na Ummul Qur-aan -Mama wa Qur-aan-, nayo Ni Aayah Saba zisomwazo mara kwa mara[7] [Na Qur-aan Tukufu niliyopewa])[8]




Alimuamrisha (صلى الله عليه وآله وسلم) "Mtu aliyeswali vibaya" aisome hiyo Faatihatul Kitaabu katika Swalah yake"[9](Lakini) na kwa yule asiyeweza kuihifadhi alimuambia (aliyeisahau): Sema:





Subhaana Llaah, Wal-Hamdu Lillaah, wala ilaaha illa Llaahu, wa Allaahu Akbar, wala Hawla wala Quwwata ila bi Llaah




Ametakasika Allaah na sifa njema ni za Allaah na hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa na Hakuna uwezo wala nguvu ila za Allaah[10]







Na (Pia) alimuambia "aliyeswali kimakosa": ((Ikiwa umehifadhi cho chote kile katika Qur-aan basi isome, vyenginevyo msifu Allaah, kiri Ukubwa Wake, na kiri kwamba hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye))[11]












[1] Al-Bukhaairy, Muslim, Abu 'Awaanah na Al-Bayhaqiy. Imetolewa katika Al-Irwaa (302)

[2] Ad-Daaraqutwniy, ambae amesema kuwa ni Swahiyh, na Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake. Pia katika Al-Irwaa (302)

[3] Kwa maana kuwa ni kasoro, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alifasiri kwa kusema: haikutimilia

[4] Muslim na Abu 'Awaanah.

[5] Ina maana kuwa ni Suratul Faatihah, ni katika mifano ya kutaja kitu chote lakini kinachokusudiwa ni baadhi tu ya kitu hicho, kwa kusisitiza umuhimu/utukufu wake.

[6] Muslim, Abu 'Awaanah na Maalik, na inayo yenye kuipa nguvu –shaahid- kutokana na Hadiyth ya Jaabir iliyothibiti kwa As-Sahmiy katika Taariykh Jurjaan (144)

[7] Al-Baajiy amesema: "Anakusudia maneno ya سبحانه وتعالى: ((Na tumekupa Aayah saba zinazosomwa mara kwa mara, na Qur-aan Tukufu)) [Al-Hijr: 15:87]. Imeitwa 'saba', kwa sababu ni Aayah saba, na al-Mathaaniy (inayosomwa mara kwa mara') kwa sababu inarudiwa katika kila rakaa, na sababu ya kuitwa (Imeitwa) 'Qur-aan Tukufu' kubainisha jina hili kwa ajili yake khaswa, japokuwa kila sehemu ya Qur-aan ni Tukufu. Kama inavyosemwa kuhusiana na Ka'abah kuwa ni 'Nyumba ya Allaah' japokuwa kuwa nyumba zote ni Zake Allaah, lakini hivi ni kwa njia ya kuibainisha umahsusi na utukufu wake"

[8] An-Nassaiy na Al-Haakim ambae amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahaabiy amekubaliana nayo.

[9] Al-Bukhaariy katika makala yake 'Kusoma nyuma ya Imaam’ kwa isnaad Swahiyh.

[10] Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah (1/80/2), Al-Haakim, At-Twabaraaniy na Ibn Hibbaan ambae pamoja na Al-Haakim, wamesema ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana nayo. Imo katika Al-Irwaa (303)

[11] Abu Daawuud na At-Tirmidhiy ambae amesema ni nzuri; isnaad yake ni Swahiyh. (Swahiyh Abu Daawuud Namba. 807)
 
016-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kufutwa Kisomo Nyuma Ya Imaam Katika Swalah Za Sauti, Na Kuwajibika Katika Swalah Za Kimya
016-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kufutwa Kisomo Nyuma Ya Imaam Katika Swalah Za Sauti, Na Kuwajibika Katika Swalah Za Kimya




KUFUTWA KISOMO NYUMA YA IMAAM KATIKA SWALAH ZA JAHRIYYAH (SWALAH ZA KUNYANYUA SAUTI)




Alikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ameruhusu kwa wale waliokuwa ma-amuma kuisoma Suratul-Faatihah nyuma ya Imaam katika Swalah za jahriyyah, na mara moja alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم), "Akiswali Alfajiri na kisomo kikawa kigumu kwake. Alipomaliza alisema: ((Labda mnasoma nyuma ya Imaam wenu!)). Tukasema: "Ndio hadhdhan[1] Ewe Mjumbe wa Allaah". Akasema: ((Basi Msifanye hivyo isipokuwa [kwa kusoma mmoja wenu] Ufunguo wa Kitabu, kwani hakuna Swalah kwa asiyeisoma))[2]




Kisha aliwakataza kusoma katika Swalah za jahriyyah kabisa, na hilo lilitokea wakati,




"Alipomaliza Swalah ambayo alikuwa akisoma kwa sauti [katika usimulizi (mmoja) ilikuwa Swalah ya Alfajiri] basi akauliza: ((Je, kuna (yeyote) aliyekuwa akisoma pamoja nami hivi sasa?)) Mtu mmoja akajibu: "Ndio, mimi Ewe Mjumbe wa Allaah". Akasema: ((Mimi Nasema: sasa kwa nini naingiliwa kati katika kisomo changu][3] [Abu Hurayrah alisema]: (Hivyo) watu wakaacha kusoma pamoja na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kila anapokuwa anasoma kwa sauti baada ya kusikia hivyo kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) [wakawa wanaendelea kusoma kimya kimya kila anapokuwa Imaam haisomi kwa sauti][4]




Pia Akaufanya (صلى الله عليه وآله وسلم) ukimya katika kisomo cha Imaam kuwa ni sehemu katika kukamilisha kumfuata Imaam, kwa kusema: ((Kwa hakika amewekwa Imaam ili apatwe kufuatwa, hivyo anapoleta takbiyr, na nyinyi leteni takbiyr, na anaposoma kaeni kimya))[5] kama alivyofanya kumsikiliza Imaam kuwa kunatosheleza na kisomo nyuma yake, kwa kusema (aliposema): ((Mwenye kuwa na Imaam, basi kisomo cha Imaam huyo ni kisomo chake))[6]. Hii inahusu Swalah za jahriyyah.
















KUWAJIBIKA KUSOMA KATIKA SWALAH ZA SIRRIYYAH (SWALAH ZA KIMYA)




Ama katika Swalah za kimya kimya, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaachilia waendelea kusoma humo. Jaabir alisema: "Tulikuwa tukisoma katika (Swalah ya) Adhuhuri na 'Aswr nyuma ya Imaam katika Rakaa mbili za mwanzo Suratul-Faatihah na Surah nyingine, na katika mbili za mwisho Suratul-Faatihah[7]




Lakini, alichukizwa kwa tashwishi na kubabaishwa, kwa kisomo chao pale aliposwali Adhuhuri na Maswahaba akauliza: ((Nani katika nyinyi aliyesoma: "Sabbihisma Rabbikal A’laa" [Suratul-A'laa, 87:1])). Mtu mmoja akajibu: "ni mimi" [sikuwa na kusudio lo lote lile kwa kuisoma ila kheri] Akasema: ((Nilijua kuwa kuna mtu anavutana na mimi kwayo))[8]




Na Katika Hadiyth nyingine: "Walikuwa wakisoma nyuma ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), hivyo akasema: ((Mmenibabaisha katika kisomo changu))[9]




Akasema: ((Anayeswali huwa ananongo’na na Mola wake, basi aangalie cha kumnongo’neza, wala msisome Qur-aan pamoja wote kwa sauti))[10]




Pia alikuwa akisema: ((Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allaah atapata hasanah (jema) moja, na kila hasanah moja ni sawa na thawabu kumi, (wala) sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miym ni herufi moja)) [11]











[1] Hadhdhan: kusoma haraka haraka, kwa kukimbilia au kuharakiza.

[2] Al-Bukhaariy katika kijarida, Abu Daawuud na Ahmad. At-Tirmidhy na Ad-Daaraqutwniy wamesema ni nzuri.

[3] Amesema al-Khattabiy: maana yake ameingilia kisomo changu, pia yawezekana ikawa ushindani kwa maana ya kushirikiana na kubadilishana, na maana ya pili ndio iliyokusudiwa hapa kwa sababu ya kuacha Swahabah (رضي الله عنهم) kusoma moja kwa moja, na kama ingelikuwa kusudio ni maana ya kwanza, basi wesingeliacha kusoma, lakini inaonyesha kuwa ni kuingilia kati tu kama ilivyodhihiri.

[4] Maalik, Humaydy, Al-Bukhaariy katika kijarida chake, Abu Daawuud na Mahaamaliy (6/139/1) At-Tirmidhiy amesema ni nzuri, Abu Haatim Ar-Raaziy, Ibn Hibbaan na Ibn Qayyim wamesema kuwa ni Swahiyh, na hadiyth yenye kuipa nguvu –shaahid- katika Hadiyth ya ‘Umar ambayo mwisho wake: sasa kwa nini nashindaniwa Qur-aan?! Haimtoshelezeshi mmoja wenu kisoma cha Imaam wake?! Kwa hakika amewekwa Imaam ili apatwe kufuatwa, basi ataposoma kaeni kimya. Imepokewa na al-Bayhaaqiy katika kitabu ulazima wa kisomo katika Swalah, kama ilivyo katika al-Jaami’ al-Kabiyr (3/344/2)

[5] Ibn Abi Shaybah (1/97/1), Abu Daawuud, Muslim, Abu 'Awaanah na al-Ruwayaaniy katika musnad yake, (24/119/1). Imetolewa katika Al-Irwaa (332,394).

[6] Ibn Abi Shaybah (1/97/1), Ad-Daraaqutwniy, Ibn maajah, At-Twahaawiy na Ahmad kutoka njia mbali mbali, musnad na mursal. Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema kuwa ina nguvu kama katika Al-Furuu' ya Ibn 'Abdil-Haadiy (48/2). Al-Buswayriy amesema kuwa baadhi ya isnaad zake kuwa ni Swahiyh. Nimeijadili Hadiyth hii kwa kirefu na kuzitafiti njia zake (mbali mbali) za usimulizi katika maandishi kisha katika Al-Irwaa Al-Ghaliyl (Namba. 500)

[7] Ibn Maajah kwa isnaad Swahiyh. Imetolewa katika Al-Irwaa (506)

[8] Muslim, Abu 'Awaanah na Siraaj.

[9] Al-Bukhaariy katika makala yake, Ahmad na Siraaj kwa isnaad nzuri.

[10] Maalik na al-Bukhaariy katika Af'aal al-'Ibaad kwa isnaad Swahiyh.




TANBIHI:

Rai ya uthabiti wa kusoma nyuma ya Imaam katika Swalah za Sirriyah na sio za Jahriyyah, imetolewa na Imaam Ash-Shaafi'y mwanzo, na Muhammad mwanafunzi wa Abu Haniyfah katika usimulizi kutoka kwake ambao umependelewa (zaidi) na Shaykh 'Aliy al-Qaariy na baadhi ya Mashaykh (wengine) wa madhehebu. Pia (ulikuwa) ni msimamo wa Imaam Az-Zuhriy, Maalik, Ibn Al-Mubaarak, Ahmad bin Hanbal, na kundi la Muhaddithiyn na wengineo, na ni mapendeleo ya Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah.

[11] At-Trimidhiy na Ibn Maajah kwa isnaad Swahiyh. Imesimuliwa pia na Aajuriy katika Aadaab Hamalat al-Qur-aan. Ama Hadiyth: "Mwenye kusoma nyuma ya Imaam mdomo wake utajazwa moto" ni Hadiyth ya uzushi (mawdhwuu) na hii imelezewa katika Silsilat al-Ahaadiyth Adh-Dhwa'iyfah (Namba. 569) Taz. Kiambatisho 5.
 
Back
Top Bottom