Ramadhan Special Thread
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



068-Anayechelea Kudhurika Kwa Maji Baridi, Je Anaweza Kutayammamu Akiwa Na Janaba?



Alhidaaya.com





Anayejihofia kufa kutokana na maji baridi, inajuzu kwake kutayammamu kwa vile anakuwa katika ngazi ya mgonjwa. Huu ni mwelekeo wa Jamhuri ya Maulamaa. [Al-Mabswutw (1/122), Al-Majmu’u (2/330), Al-Istidhkaar (3/173), Al-Mughniy (1/163), Al-Muhalla (2/134) na Majmu’u Al-Fataawaa (21/399)].



Hoja yao katika hili ni:



1- Neno Lake Allaah Mtukufu:

((ولا تقتلوا أنفسكم إن الله كان بكم رحيما))

((Wala msiziue nafsi zenu, hakika Allaah ni Mrehemevu mno kwenu)). [An-Nisaa (4:29)].



2- Ni yaliyopokelewa toka kwa ‘Amri bin Al-‘Aas kwamba wakati alipopelekwa katika vita vya Dhaatu As-Salaasil alisema: “Niliota katika usiku wa baridi kali, nikahofia kufa kama nitaoga. Nikatayammamu, kisha nikaswali na wenzangu Swalaah ya Alfajiri. Tulipowasili kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'Alayhi wa Aalihii wa Sallam), wao walimweleza hilo, akasema:

((Ee ‘Amri! Hivi umeswali na wenzako ukiwa na janaba?))

Nikamwambia: “Nililikumbuka Neno la Allaah Mtukufu:

((ولا تقتلوا أنفسكم إن الله كان بكم رحيما))

nikatayammamu kisha nikaswali. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'Alayhi wa Aalihii wa Sallam) akacheka, na hakusema neno)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (334), Ahmad (3/203), Ad-Daara Qutwniy (1/178), Al-Haakim (1/177) na Al-Bayhaqiy (1/225). Sanad na matni yake zimetiwa doa. Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (1/182) amesema ni Swahiyh].



Hadiyth hii ina mvutano, na lenye nguvu ni kuwa ni dhwa’iyf. Lakini pamoja na hivyo, kaida za kisharia zinaitolea ushahidi. Vile vile mwelekeo huu unaungwa mkono na Neno Lake Allaah Mtukufu:

((ما يريد الله ليجعل عليكم من حرج))

((Hataki Allaah kuwafanyieni uzito)). [Al-Maaidah (5:6)].



Na hii ni baada ya kutaja tayammumi. Kana kwamba Ameashiria kuwa tayammumi inaruhusika panapokuwepo uzito wa kutumia maji. Na hakuna shaka kuwa ubaridi mkali wa maji ni katika uzito huo. Lakini inatakikana kutanabahisha kuwa kutayammumi hakuruhusiwi – katika hali hii – ila baada ya kushindwa kupasha maji moto. Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



069-Je Anaweza Kutayammamu Mtu Ambaye Wakati Umekuwa Mfinyu Kwake Na Wakati Wa Swalaah Utampita Kama Atatumia Maji?



Alhidaaya.com





Kuna kauli mbili za Maulamaa katika suala hili:



Ya kwanza:



Haijuzu kutayammamu hata kama wakati utampita. Limesemwa hili na Mashaafi’iy, Mahanbali na Abuu Yuusuf. [Al-Mughniy (1/166), Al-Majmu’u (2/280), Al-Istidhkaar (3/171) na Tamaam Al-Minnah (uk.132)]



Dalili zao ni:



1- Neno Lake Allaah Mtukufu:

((إذا قمتم إلى الصلاة فاغسلوا وجوهكم.... فلم تجدوا ماء فتيمموا))

((Mnaposimama kuswali, basi osheni nyuso zenu….na hamkupata maji, basi tayammamuni)). [Al-Maaidah (5:6)].



Wanasema: “Hapa kukosa maji kumefanywa kuwa ni sharti ya kuhalalika kutayammamu”.



2- Hadiyth ya Abuu Hurayrah ikiwa Marfu’u:

((لا يقبل الله صلاة أحدكم إذا أحدث حتى يتوضأ))

((Allaah Hakubali Swalaah ya mmoja wenu anapokuwa na hadathi mpaka atawadhe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (6954) na Muslim (526)].



3- Hadiyth ya Ibn ‘Umar ikiwa Marfu’u:

((لا تقبل الصلاة بغير طهور ولا صدقة من غلول))

((Swalaah haikubaliwi bila ya wudhuu, wala swadaqah ya mali haramu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (524), At-Tirmidhiy (1) na Ibn Maajah (272)].



Hapa mtu kaamuriwa kutumia maji. Ikiwa ataiwahi Swalaah, basi vizuri, na kama itampita kwa kuzembea kwake, basi hayo amejitakia mwenyewe.



Ya pili:



Anaweza kutayammamu na kuswali kabla wakati haujampita.

Wamelisema hili Ahlu Rra’ayi (Abuu Haniyfah na wenzake), Al-Awzaa’iy, Maalik, Ibn Hazm. Shaykh wa Uislamu amelikhitari hili. [Al-Mughniy (1/166), Al-Muhalla (2/117), Majmu’u Al-Fataawaa (21/439,456) na Al-Awsatw (2/30)].



Mahanafi wameliwekea hili sharti ya kuwa ni lazima liwe kwa Swalaah ambayo haina badala yake kama Swalaah ya maiti. [Al-Mughniy (1/166), Al-Muhalla (2/117), Majmu’u Al-Fataawaa (21/439,456) na Al-Awsatw (2/30)].



Hoja zao ni:



1- Hadiyth ya Abu Juhaym Al-Answaariy, amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'Alayhi wa Aalihii wa Sallam) alikuja akitokea upande wa kisima cha Jamal. Mtu mmoja alikutana naye akamsalimia. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'Alayhi wa Aalihii wa Sallam) hakuitikia mpaka alipokwenda ukutani, akapukusa uso na mikono yake. Kisha akamjibu salamu”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (337) na Muslim (800)].

Wamesema: “Na hii ni asili katika kujuzu kutayammamu kwa ajili ya kuhofia kupitwa na faradhi”.



2- Ibn ‘Abdul Barri amesema katika Al-Istidhkaar (3/171):

“Kila ambaye hakuyapata maji na akachelea kupitwa na Swalaah, anaweza kutayammamu kama ni mgonjwa au msafiri kwa matni. Na kama ni mkazi na mzima, basi ni kwa maana. Na Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi".



3- Shaykh wa Uislamu amesema:

“Kauli sahihi zaidi ya Maulamaa ni kuwa atatayammamu kwa kila lile analolichelea kupitwa nalo kama Swalaah ya maiti, Swalaah za idi mbili na kadhalika. Swalaah kwa kutayammamu ni bora zaidi kuliko kuiacha ipite..”



Na amesema tena:

“Vile vile, kama hakuweza kuswali Swalaah ya Jamaa ya faradhi ila kwa kutayammamu, basi ataiswali kwa kutayammamu”.



Ninasema:



“Na huenda lililo wazi zaidi ni kuwa mtu atatayammamu ili aiwahi Swalaah, kwani tayammumi imewekwa kwa ajili ya kuuwahi wakati wa Swalaah na kuchelea kupitwa ili kuulinda wakati. Na Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



070-Anayeamka Usingizini Muda Wa Swalaah Ukawa Mfinyu, Je Atayammamu Ili Auwahi Wakati?



Alhidaaya.com





Kuna mielekeo miwili katika suala hili mfano wa ile ya suala lililotangulia: [Al Awsatw (2/30), Al Muhalla (2/117), na Majmuu Al-Fataawaa (22/35-36)]



Wa kwanza:



Atatayammamu na ataswali ndani ya wakati. Hili limesemwa na Maalik, Al-Awzaa’iy, Ath-Thawriy na Ibn Hazm.



Wa pili:



Ataoga na ataswali na hata baada ya kutoka wakati. Huu ni msimamo wa Jamhuri, na Shaykh wa Uislamu ameukhitari.



Msimamo huu ndio wenye nguvu zaidi, kwani wakati kwa mwenye kulala ni pale anapoamka.



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'Alayhi wa Aalihii wa Sallam) amesema:

((أما إنه ليس في نوم تفريط، إنما التفريط على من لم يصل الصلاة حتى يجئ وقت الصلاة الأخرى، فمن فعل ذلك فليصلها حين ينتبه بها))

((Ama hakika, hakuna uzembe usingizini, bali uzembe ni kwa yule ambaye hakuswali mpaka ukaingia wakati wa Swalaah nyingine. Mwenye kufanya hivyo, basi aiswali anapoikumbukia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (1532) na Abuu Daawuud (437).



Na imekuja katika Swahiyh Mbili katika Hadiyth Marfu’u iliyopokelewa na Abuu Hurayrah: “

((من نسي صلاة فليصلها إذا ذكرها لا كفارة لها إلا ذلك))

((Aliyeisahau Swalaah, basi aiswali anapoikumbuka, hakuna kafara yake ila hilo)).



Na katika tamshi la Muslim katika Hadiyth ya Anas:

((من نسي صلاة أو نام عنها فكفارتها أن يصليها إذا ذكرها))

((Aliyeisahau Swalaah, au akalala ikampita, basi kafara yake ni kuiswali anapoikumbuka))].



Ibn Taymiyah amesema (22/35):



“Na kama ni hivyo, kama ataamka kabla ya kuchomoza jua na hakuweza kuoga na kuswali ila baada ya kuchomoza, basi anakuwa ameiswali Swalaah katika wakati wake na wala hazingatiwi kuwa ameipitisha. Ni kinyume na yule aliyeamka mwanzoni mwa wakati. Huyu wakati wake ni kabla ya kuchomoza jua, atahadhari asiuache wakati wa Swalaah ukamtoka".
 
Naam ndugu zangu katika imani,wakati bado tunaendelea kusoma darsa la tohara ambalo ndio muhimu sana maana kama umefeli hapa basi hata ibada ya swala nayo utafeli

MOYO WA MWANADAMU NI KAMA SPONJI

Naam sponji ukiliweka katika maji basi litavyonza maji na ukilikamua litatoa maji,lau ukaliweka katika maziwa litavyonza maziwa na ukilikamua litatoa maziwa

Basi nyoyo zetu nazo ni hivyo,ukiwa na mapenzi sana na anasa na starehe basi hakika hayo mambo yatakuwa moyoni mwako siku zote na hata siku ya kufa huenda ukafia katika mazingira hayo

Na lau ukawa unapenda mambo ya kumkumbuka Allah,mambo ya kheri na ibaadati nyingine mbali mbali basi hayo yatakaa moyoni mwako na ndio yatakuwa maisha yako,na huenda hata roho yako ikatoka ukiwa katika mazingira hayo,Allah atujalie tuwe miongoni mwao

Je unapenda siku ya kufa neno lako la mwisho liwe la Tauwhid yani Laa ilaha illallah,basi kama ni hivyo kithirisha sana kumtaja Allah kwa wingi kwani linalokuwa moyoni mwako ndio linalotoka kinywani mwako


Binafsi nimezoe kila ninapojikwaa au kujigonga basi humsabihi Allah kwa kusema Subhanallah,na siku niliyopata ajali na wenzangu katika private car,tuligonga ukuta na kubiringita mara tatu kuelekea bondeni nakumbuka wakati inabiringita nikasema Subhanallah na ndio raundi ya tatu gari iliposimama na kwa matairi yake,lau ingeendelea kubiringita leo nisingekuwepo jf

Kwa neema ya Allah tulitoka na michubuko midogo tu hata bandeji hatukufunga

Kwahiyo nilichozea kusema ndio kilinitokea siku ya ajali,Allah atuhifadhi

Darsa litaendelea inshaallah
 
Naam ndugu zangu katika imani tutaendelea kupeana darsa katika mambo mbali mbali kwa kutaka radhi za Allah

Tutapitia pitia HADITH MBALI MBALI pia katika kitabu hiki

20250408_190249.jpg


Ili tupate Mafunzo Mbali Mbali kutoka kwa Rasul swallallahu alih wa wassallam

Allah atufanyie wepesi
 
Darsa ya Tohara itaendelea na huku tunaendelea na mambo mengine

TUTAANZA NA KALIMAH TAYYIBAH

"Hapana anayepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, Muhammad Swallallahu Alaih Wasallam ni Mjumbe wake

IMANI

Maana ya Imani kilugha ni kuamini maneno ya mtu kwa kuyasadikisha kwa ushahidi wake tu. Kidini ni kuyasadikisha yote aliyoyaeleza Rasulullah (swallallahu Alaih Wasallam) bila ya kuyaona na kuwa na uhakika nayo na kuwa na yakini nayo

Nitaacha aya za qur'an na moja kwa moja tunaenda kwenye hadith

Abu Huraira (radhiallahu anhu) amesimulia kuwa Rasulullah (s.a.w) amesema " imani ina matawi zaidi ya Sabiini. Lililo bora ni kutamka Lailaha illallahu (Hakuna anayepaswa kuabudiwa kwa haki ila Allah) na la chini kabisa ni kuondoa udhia njiani,na haya (kuona haya ) ni tawi la imani

Naam ndugu zangu kumbe hata kuondoa udhia njiani kama jiti,jiwe au miba nayo ni sehemu ya imani

Na kuona haya ni sehemu ya imani kwani hakika hayaa humzuia mtu kufanya maovu na inamkataza mtu kudharau haki za wengine
 
Abu Bakri (radhiallahu anhu) amesimulia kuwa Rasulullahi (s.a.w) amesema " Atakayeikubali kutoka kwangu kalima ambayo niliifikisha kwa ami yangu (Abu Talib wakati wa kufa kwake) na akaikataa (huyo Abu Talib) hii itakuwa ni sababu ya kuokoka kwake"

Naam leo kwa upande wa hadith tuishie hapa
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



071-Ni Sehemu Ipi Ya Ardhi Inayofaa Kutayamamia?



Alhidaaya.com





Maulamaa wana rai mbili kuhusu mchanga unaofaa kutayamamia:



Rai ya kwanza



Ni uso wowote wa ardhi ikiwa ni changarawe, mlima, mchanga au udongo. Huu ni mwelekeo wa Abuu Haniyfah, Abuu Yuusuf na Maalik. Umekhitariwa na Shaykh wa Uislamu. Pia Ibn Hazm amelikhitari hilo, lakini yeye kashurutisha kuwa endapo kama uso wa ardhi hauna udongo, basi uwe umeshikamana na ardhi. [Al-Istidhkaar (3/157), Al-Mabsuutw (1/108), Majmuu Al-Fataawaa (21/364) na Al-Muhallaa (2/158)].



Kati ya hoja zao ni:



1- Neno Lake Allaah Mtukufu:

((صعيدا زلقا))

((Ardhi tupu)) [Al-Kahf (18:40)]
Na Neno Lake Ta’alaa:

((صعيدا جرزا))

((Ardhi kame)) [Al-Kahf (18:8)]



Amesema katika “Al-Istidhkaar” (3/158): “Al-Juzur” ni ardhi ngumu isiyootesha kitu.



2- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((وجعلت لي الأرض مسجدا وطهورا))

((...na ardhi imefanywa kwangu kuwa sehemu ya kuswalia na kitwaharisho)). [Hadiyth Swahiyh: Imetangulia hivi karibuni].



3- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((يحشر الناس يوم القيامة على صعيد واحد))

((Watu watafufuliwa siku ya Qiyaamah juu ya ardhi moja)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (4712) na Muslim (472)].



4- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((جعلت الأرض كلها لي ولأمتي مسجدا وطهورا، فأينما أدركت رجلا من أمتي الصلاة فعنده مسجده وعنده طهوره))

((Ardhi yote imefanywa kwangu na kwa umati wangu kuwa sehemu ya kuswalia na kitwaharisho, na popote itakapomkuta Swalaah yeyote katika umma wangu, basi hapo ndipo sehemu yake ya kuswalia, na hapo ndipo kitwaharisho chake)). [Hadiyth Hasan: Imetangulia hivi karibuni].



5- Hadiyth ya Abuu Al-Juhaym kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipiga juu ya ukuta kwa mikono yake miwili, akatayamamu, kisha akamjibu mtu maamkizi. [Hadiyth Swahiyh: Imetangulia hivi karibuni].



6- Ni yale yaliyopokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba amesema:

“Uso mzuri zaidi wa ardhi ni konde na ardhi ya konde”. [Isnadi yake ni dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (1/161)].



Rai ya pili



Uso wa ardhi ni udongo na kisicho udongo hakifai kutayamamia.



Huu ni mwelekeo wa Ash-Shaafi’iy, Hanbali, Abuu Thawr na Ibn Al-Mundhir. [Al-Mughny (1/155), Al-Majmu’u (2/246), Al-Istidhkaar (3/159) na Al-Awsatw (2/43)].

Kati ya hoja zao ni:



1- Ni ziada iliyokuja katika Hadiyth isemayo:

((وجعلت تربتها لي طهورا))

))na umefanywa udongo wake kwangu ni kitwaharisho)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (522), Ibn Hibaan (1697), Ad-Daara Qutwniy (1/175) na Al-Bayhaqiy (1/213 – 230). Yeye amezungumzia kuhusu ziada, na la sahihi ni kuwa ziada hii ipo].



..katika Hadiyth ya

((جعلت لي الأرض مسجدا))

Wamesema: “Riwaya hii imehusishwa na riwaya isemayo:

((جعلت لي الأرض مسجدا وطهورا))

2- Ni Hadiyth iliyopokelewa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((أعطيت ما لم يعط أحد من الأنبياء : نصرت بالرعب، وأعطيت مفاتيخ الأرض، وسميت أحمد، وجعل لي التراب طهورا، وجعلت أمتي خير الأمم)).

((Nimepewa mambo ambayo hakupewa Nabii yeyote: Nimenusuriwa kwa kutiwa khofu maadui, nimepewa funguo za ardhi, nimeitwa Ahmad, nimefanyiwa udongo kuwa kitwaharisho, na umma wangu umefanywa umma bora zaidi)). [Hadiyth Munkar: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (1/98) na Al-Bayhaqiy (1/213)].



Ninasema:



“Yenye nguvu zaidi kwangu ni kauli ya kwanza. Ni kwamba inafaa kutayammamu kwa kila kile kinachoitwa ardhi, au kila kinachobeba chochote cha ardhini kama vumbi na mfano wake. Ama kauli ya pili, hebu tuitazame kwa pande mbili:



Kwanza: Hakuna chochote cha kuthibitisha katika dalili zao kama ulivyoona.

Pili: Wamelichukulia neno “at-turbah” katika Hadiyth kwa maana ya udongo. Na hapa hebu tuangalie. Abuu Hurayrah katika Hadiyth ya Muslim anasema:

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinishika mkono akaniambia:

((خلق الله – عز وجل – التربة يوم السبت، وخلق فيها الجبال يوم الأحد، وخلق الشجر يوم الإثنين ..))

((Allaahu ‘Azza wa Jalla Aliumba udongo (ardhi) siku ya Jumamosi, Akaumba humo milima siku ya Jumapili, na Akaumba miti siku ya Jumatatu…)).



Katika Kamusi ya “Lisaan Al-‘Arab”, mtunzi amesema:

"خلق الله التربة يوم السبت"

“Allaah Ameumba udongo Siku ya Jumamosi”, yaani ardhi.



Ninasema: Na maana hii iko wazi katika Hadiyth, Walillaahi Al-Hamd”.
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



072-Mwenye Kukosa Vitwaharisho Viwili (Maji Na Mchanga)



Alhidaaya.com





Kauli sahihi zaidi kati ya kauli mbili za Maulamaa kuhusiana na mtu aliyekosa vitwaharisho viwili (maji na mchanga) ni kuwa ataswali katika hali aliyonayo katika wakati wa Swalaah na wala hatoirejesha.



Huu ni mwelekeo wa Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Ibn Hazm. Ibn Taymiyyah ameukhitari mwelekeo huu. [Al-Mughniy (1/157), Al-Majmu’u (2/321), Al-Muhallaa (2/138) na Al-Fataawaa (21/467)]



Hoja yao ni Kauli Yake Allaah Mtukufu:

((فاتقوا الله مااستطعتم))

((Basi mcheni Allaah mwezavyo)) [At- Taghaabun ( 64:16]



Na Neno Lake Allaah Mtukufu:

((لا يكلف الله نفسا إلا وسعها))

((Allaah Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa uwezo wake)) [Al-Baqarah (2:286)]



Na kauli yake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((إذا أمرتكم بأمر فائتوا منه مااستطعتم))

((Nikiwaamuruni jambo, basi lifanyeni kwa uwezo wenu)) [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (7288) na Muslim (3199)].



Wamesema: “Huyu amefanya alichoweza katika Swalaah, na jambo la kujitwaharisha ambalo hakuliweza, limemwondokea. Na kwa hilo, anakuwa ametekeleza aliloamuriwa, na mwenye kutekeleza aliloamuriwa, basi hatolipa”.



Ninasema: “Na huenda mwelekeo huu unatiliwa nguvu na Hadiyth ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anha) aliyesema:

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma Asyad bin Al-Khudhayr – na hali mimi nasikia – kukitafuta kidani nilichokipoteza. Ukafika wakati wa Swalaah, nao wakaswali bila wudhuu. Kisha wakamjia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakamweleza hilo, na hapo ikateremshwa Aayah ya tayammum”[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (5882) na Muslim (795)].



Na ushahidi hapa ni kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwakubalia – wakati walipokosa maji – kuswali bila wudhuu na wala hakuwaamuru kurejesha Swalaah. Na endapo kama watakosa mchanga vile vile, basi hukmu ni hiyo hiyo. Na Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.



Na kwa upande mwengine, Abuu Haniyfah, Asw-haabur Ra-ay (Mahanafi), Maalik na Al-Awzaa’iy, wao wanaona kwamba hatoswali mtu mpaka apate maji ya kutawadhia au mchanga wa kutayamamia, hata kama wakati utatoka. [Al-Awsatw (2/45), Al-Istidhkaar (3/150) na Al-Muhallaa
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



073-Yanayohusiana Na Niya Ya Kutayammam



Alhidaaya.com






·

Niya ya kuondosha hadathi inatosheleza kuruhusika kuswali



Kauli za Maulamaa zilizo sahihi zaidi zinasema kwamba tayamumi inasimama mahala pa maji moja kwa moja. Yanayoruhusika kwa maji ndiyo yale yale yanayoruhusika kwa tayamumi, na utwahara wake huendelea kama unavyoendelea utwahara wa maji. Akitayamamu kwa ajili ya Swalaah ya Sunnah, anaweza pia kuswalia Swalaah ya faradhi na kinyume chake. Hii ndiyo kauli ya Maulamaa wengi kinyume na Maalik Allaah Amrehemu. [Al-Majmu’u (2/255), Al-Mughniy (1/158), Majmu’u Al-Fataawaa (12/436) na Al-Mabsuutw (1/117)]



Sheikh wa Uislamu anasema: [Majmu’u Al-Fataawaa (21/436)]

“Kauli hii ndio sahihi, na ndiyo iliyoashiriwa na Qur-aan, Sunnah na akili. Tunaona kwamba Allaah Ameifanya tayammum inatwaharisha kama Alivyoyafanya maji Akatuambia:

((فتيمموا صعيدا طيبا فامسحوا بوجوهكم وأيديكم منه ما يريد الله ليجعل عليكم من حرج ولكن يريد ليطهركم))

(( Basi ukusudieni mchanga mzuri, panguseni kwao nyuso zenu na mikono yenu. Allaah Hataki kuwafanyieni uzito lakini Anapenda kukutwaharisheni )). [Al-Maaidah (5:6) ]



Kwa hiyo, mwenye kusema kwamba mchanga hautwaharishi hadathi, basi amekhalifu Qur-aan na Sunnah. Na ikiwa unatwaharisha hadathi, haiwezekani hadathi ikaendelea kuwepo, kwani Allaah Amewatwaharisha Waislamu hadathi kwa tayamumi. Tayamumi inaondosha hadathi na inamtwaharisha mwenye hadathi, lakini uondoshaji huu ni wa muda mpaka pale atakapoweza kuyatumia maji. Tayamumi ni badali ya maji, nayo inabakia ni kitwaharisho madhali maji yamekuwa vigumu kupatikana”.



Ninasema: “Tayamumi imewekwa kisharia kwa ajili ya Swalaah, twawafu, kusoma Qur-aan, kugusa Msahafu na mengineyo yanayoruhusika mtu anapokuwa na wudhuu au baada ya kuoga madhali maji yamekuwa vigumu kupatikana. Mwenye kunuwiya kwa tayamumi yake kuondosha hadathi, ni halali kwake kufanya yale yote anayoruhusika anapokuwa na wudhuu na baada ya kuoga. Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi”.



Mwenye Kutayammamu Kwa Niya Ya Kuondosha Janaba, Je Itamtosheleza Na Wudhuu Pia?



Mwenye kutayamumi kwa niya ya kuondosha janaba, niya hiyo itamtosheleza na wudhuu pia kwa mujibu wa kauli sahihi ya Maulamaa kama Abuu Haniyfah na Ash Shaafi’iy. [Al-Mughniy (1/166)]



Na hii ni kwa mambo mawili:



1- Twahara ya viwili hivi ni moja. Inapoondoka moja, humwondosha mwenzake kama mkojo na kinyesi.



2- Tayamumi ni badali ya utumiaji maji, hivyo huchukua hukmu yake. Lenye nguvu zaidi ni kuwa kuoga, hutosheleza na wudhuu pia, na vile vile tayamumi.



Ama mwenye kutayamumi kwa niya ya kuondosha hadathi ndogo, je niya itatosheleza kuondosha janaba pia? Jibu hapa litaangaliwa; mwenye kuliangalia suala mtizamo wa sababu ya kwanza, jibu lake litakuwa ndiyo. Ama mwenye kuliangalia kwa mtizamo wa kuwa tayamumi ni badali ya maji, basi atazuia.



Maalik, Abuu Thawr, Mahanbali na Ibn Hazm, [Al-Mughniy (1/166) na Al-Muhallaa (2/138)]…..wao wanasema kwamba niya ya kimoja, haitoshelezi kingine kutokana na ujumuishi wa kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

(( إنما الأعمال بالنيات، وإنما لكل امرئ ما نوى))

((Hakika matendo ni kwa niya, na kila mtu ni kwa lile alilolinuwiya)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (namba moja)].
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



074-Namna Sahihi Ya Kutayammamu



Alhidaaya.com





Namna sahihi ya kutayamamu iliyokuja kwa njia sahihi toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni:



Atapiga mtu pigo moja kwenye mchanga kwa mikono miwili, kisha ataipuliza, halafu atajipukusa kwayo uso wake na vitanga vyake viwili.



Haya ni madhehebu ya Mahanbali na Ibn Hazm. Na ndivyo walivyosema baadhi ya Masalafu, na Ibn Taymiyyah amelikhitari. [Al-Mughniy (1/159), Al-Muhallaa (1/146) na Al-Fataawaa (21/422)].



Dalili ya hili ni:



1-Hadiyth iliyoelezewa na ‘Ammaar bin Yaasir akisema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Ilikuwa inakutosha kufanya hivi”. Na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapiga ardhi kwa vitanga vyake, akavipuliza, kisha akapukusa kwavyo uso wake na viganja vyake”[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (338) na Muslim (798).



2-Hadiyth ya Abuu Hurayrah aliposema: “Ilipoteremka Aayah ya tayamumi, sikujua namna ya kutayamamu. Nikamwendea Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) lakini sikumkuta. Nikaondoka kumtafuta nikamwona nikamwelekea. Aliponiona alilijua lililonileta, akaenda haja ndogo, kisha akapiga mikono yake chini, akapukusa kwayo uso wake na viganja vyake”. [Isnadi yake ni laini. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abiy Shaybah (1/159). Hadiyth iliyotangulia inaitilia nguvu].



Na kwa upande mwingine, kundi jingine la Maulamaa linaona kwamba tayamumi ni mapigo mawili: Pigo moja la uso, na pigo jingine la mikono miwili mpaka kwenye viwiko viwili. Haya ni madhehebu ya Hanafiy, Maalik na Ash Shaafi’iy. Ath-Thawriy na Al-Layth wamesema hivi, nalo limepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar. Wengine ni Ash-Sha’abiy, Al-Hasan Al-Baswriy na wengineo. [Al-Mabsuwtw (1/106), Al-Istidhkaar (3/162) na Al-Majmu’u (2/242)].



Hoja zao ni:



1- Hadiyth ya Ibn ‘Umar kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:

((Tayamumi ni mapigo mawili: Pigo la uso, na pigo la mikono miwili hadi kwenye viwiko viwili)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Haakim (1/179) na Al-Bayhaqiy (1/207)].



2- Hadiyth ya Ibn ‘Umar kuhusiana na kisa cha mtu aliyepita kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa ameshughulika, akamsalimia. Ibn ‘Umar anasema: “Alipiga mikono yake miwili ukutani, akapangusa kwayo uso wake, kisha akapiga pigo jingine, akapukusa mikono yake miwili, kisha akaijibu salamu ya mtu yule”.[Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1/88) na Al-Bayhaqiy (1/207). Imaam Ahmad ameikataa].



3- Yaliyoelezewa na Abuu Juhaym aliposema: “Akasimama mbele ya ukuta, akaukwangua kwa fimbo aliyokuwa nayo, kisha akaweka mikono yake ukutani, halafu akapukusa uso wake na mikono yake, kisha akanijibu salamu”[Hadiyth Munkari: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ash Shaafi’iy katika musnadi yake (130) na Al-Bayhaqiy (1/205). Imekhalifiana na riwaya ya Swahiyh Mbili iliyotangulia].



4-Hadiyth ya ‘Ammaar isemayo kwamba alieleza kuwa walijipangusa kwa mchanga kwa ajili ya kuswali Salatul Fajr wakiwa pamoja na Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Wakaupiga mchanga kwa viganja vyao mara nyingine tena, wakajipangusa kwa mikono yao yote hadi kwenye mabega na makwapa kwa matumbo ya viganja vyao. [Hadiyth Mudhtwarib: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (1/84), Ibn Maajah (571), An Nasaaiy (1/168) na Al-Bayhaqiy (1/208)].



Ninasema: “Lenye nguvu ni kuwa tayamumi ni pigo moja tu kwa uso na mikono miwili hadi kwenye viwiko viwili kama tulivyotangulia kusema. Na hii ni kwa mambo mawili:



1-Dalili zote za wenye kukhalifiana na hilo ni dhwa’iyf. Hawana hata Hadiyth moja Marfu’u.



2-Hukmu ya tayamumi inafungamana na mikono miwili basi, dhiraa haiingii. Ni kama kuukata mkono wa mwizi. Hili linaashiriwa na kuhoji Ibn ‘Abbaas kuhusiana na kuainisha sehemu ya kukatwa mkono iliyoelezewa kwenye Aayah kwa mwizi kwa Neno Lake Allaah kuhusiana na tayamumi:

(( فامسحوا بوجوهكم وأيديكم منه))

((Basi pakeni nyuso zenu na mikono yenu kwa mchanga huo)). [Al-Maaidah (5:6)].



Na ukataji kwa mujibu wa Sunnah, ni viganja viwili.



Yanayotengua Tayammumi



Hadathi yoyote inayotengua wudhuu, hutengua tayamumi. Hili halina mvutano wowote kati ya Maulamaa. [Al-Muhallaa cha Ibn Hazm (2/122)].
 
Abu Huraira (r.a) amesimulia kuwa,Rasul (s.a.w) amesema: "ifanyeni mpya imani yenu". Pakasemwa , "ewe Rasul !
Ni vipi tutaifanya mpya imani yetu? Akasema "Tamkeni kwa wingi Laa ilaha illaillah

Jabir bin Abdullah (r.a) anasimulia : Nimemsikia Rasulullah (s.a.w) anasema "Dhikri (utajo wa Allah) bora ni Lailaaha illallahu na Dua (maombi) bora ni Alhamdulillah (kumsifu Allah)

Kalimah hii ni msingi wa dini yote. Bila kuiamini kalimah hii si imani wala amali (matendo) ambayo yatakubaliwa. Alhamdulillah ( kumsifu Allah) inasemwa kuwa ni Dua bora kwa sababu kumsifu Allah ambaye ni mkarimu kuliko wote,ni katika njia za kuomba msaada wake au fadhila zake
 
Abu Hurairah r.a amesimulia kuwa Rasul s.a.w amesema " Wakati mja anapo tamka Laa ilaaha illallahu kwa ikhlas,milango ya mbinguni inafunguliwa (ili ipande) mpaka inafika kwenye arshi ( kiti cha enzi cha Allah,na kwa hakika inakubaliwa)


Kuitamka kwa ikhlas maana yake ni kujiepusha na uongo na unafiki. Kujiepusha na madhambi makubwa kuna hakikisha kukubaliwa kwake kwa haraka,na hata kama itatamkwa bila ya kujiepusha na madhambi makubwa bado ni yenye faida na yenye ujira


Abu Dhar r.a amesimulia kuwa. Nabii s.a.w amesema "Hakika mja yoyote atakaye tamka Lailaaha illaillahu na akafa na hali anaiamini,isipokuwa kwa hakika ataingia Jannah (peponi)
Nikauliza kama amezini na hata kama ameiba? Akasema "hata kama amezini na hataka kama ameiba" . Nikauliza tena "Hata kama amezina na hata kama ameiba"? Akarejea "hata kama amezini na hata kama ameiba" Nikauliza mara ya tatu: Hata kama amezini na hata kama ameiba,pamoja na kutoridhika kwako ewe Abu Dhar


Maelezo : Abu Dhar alishangaa kwamba pamoja na madhambi kama hayo,vipi mtu huyo ataingia Jannah,wakati uadilifu unataka aadhibiwe. Hapo Rasulllahi akasema katika hali ya kutia nguvu ili kuondoa mshangao wake kuwa,pamoja na kutoridhika kwa Abu Dhar,mtu huyo ataingia Jannah: amedokeza kuwa hata kama atakuwa amefanya madhambi,lakini kwa sababu yake,atatubia na kusamehewa madhambi yake, au Allah kwa rehma zake zisizo na mwisho,atamsamehe na kumuingiza Jannah bila ya kumuadhibu au baada ya adhabu,katika hali yoyote ile,mwishoni atampeleka Jannah


Abu Hurairah r.a amesimulia kuwa,Rasulullah s.a.w amesema: Anae tamka Lailaaha illallahu,iko siku moja itamnufaisha ijapokuwa kabla ya hapo atateseka (ataadhibiwa) kwa yale ambayo yatampata


Abdullah ibn Umar r.a amesimulia kuwa Rasulillah alisema " je nikujulisheni wasia wa Nuh (alaihi salaam) kwa mwanae. Wakasema "tujulishe " akasema : Nuh alimuisia mwanae kwa kusema " ewe mwanangu ninakuusia kufanya mambo mawili na nina kukataza mambo mawili: Ninakuhusia kutamka Laa ilaaha illallah! Kwani ikiwekwa kama itawekwa katika upande mmoja wa mzani na zikawekwa mbingu na ardhi upande mwingine,itazizidi. Na lau hizo mbingu na ardhi zingekuwa katika umbile la duara ingezilivunja ( hiyo kalimah) na ingelimfikia Allah Taala. Na ninakuhusia kutamka Subhaanallahi lladhim wabihamdih (ametuta Allah,mtukufu na sifa njema zote ni zake) kwani hii ndio ibada ya viumbe vyote,na kutokana nayo ndio wanagawiwa riziki zao (wanaruzukiwa)

Na nina kukataza mambo mawili,Shirki na Kibri kwani mambo hayo haya yana mtenganisha mtu na Allah
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



075-Masuala Mbalimbali Kuhusu Tayammumi



Alhidaaya.com






·

Je, inaswihi kuswali kwa tayamumi endapo maji yatapatikana kabla ya kuanza kuswali?



Ibn ‘Abdul Barri amesema: “Maulamaa wote wanakubaliana kwamba mwenye kutayamamu baada ya kukosa maji, kisha akayapata maji kabla hajaanza kuswali, basi tayamumi yake hubatilika, na hawezi kuswali kwa tayamumi hiyo, bali hurejea katika hali yake ya kabla ya kutayamamu”. [Al-Istidhkaar (3/167)]




·

Mtu ametayamamu akaanza kuswali, kisha maji yakapatikana kabla hajamaliza Swalaah yake, je ataikamilisha Swalaah au ataivunja?



Maulamaa wamehitilafiana katika suala hili kwa kauli mbili:



Ya kwanza: Atalazimika kuivunja Swalaah ili ayatumie maji, kisha aanze tena Swalaah upya.

Haya ni madhehebu ya Abuu Haniyfah na Ahmad. Hivyo hivyo kasema Ath-Thawriy na Ibn Hazm. [Al-Mabsuwtw (1/120), Al-Mughniy (1/167), Al-Istidhkaar (3/170), na Al-Muhallaa (2/126)].



Hoja zao ni:



1- Neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

(( الصعيد الطيب وضوء المسلم، وإن لم يجد الماء عشر سنين، فإذا وجدت الماء فأمسه جلدك))

((Mchanga safi ni wudhuu kwa Muislamu hata kama hakupata maji miaka kumi. Ukiyapata maji, basi yagusishe ngozi yako)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Wamekhitilafiana katika kuifanya Hadiyth Hasan. Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhy (124), Abuu Daawuud (329) na An-Nasaaiy (1/171). Tumeitaja katika mlango wa kuoga].



Wamesema: Hii ni kwa mwenye kuyapata maji.



2- Kwa vile ameweza kuyatumia maji, basi tayamumi yake hubatilika na kuwa kana kwamba yuko nje ya Swalaah.



3-Kwa vile tayamumi ni twahara ya dharura, hubatilika kwa kuondoka dharura. Ni kama twahara ya mwanamke mwenye damu ya istihaadhwah inapokatika damu yake.



Ya pili: Ataikamilisha Swalaah yake mpaka mwisho

Haya ni madhehebu ya Maalik na Ash Shaafi’iy, na riwaya ya pili toka kwa Ahmad lakini inasemekana kwamba aliachana nayo. Hivyo hivyo kasema Abuu Thawr, Daawuud na Ibn Al-Mundhir. [Al-Istidhkaar (3/169), Al-Majmu’u (2/357) na Al-Awsatw (2/65)].



Hoja zao ni:

1-Neno Lake Allaah Subhaanahu wa Taalaa:

(( ولا تبطلوا أعمالكم))

((Wala msizibatilishe amali zenu)). [Muhammad (47:33)].



Wanasema: Haijuzu kuivunja Swalaah kwa ajili ya hilo.



2-Twahara ina wakati wake, na Swalaah ina wakati wake. Na mtu baada ya kuingia kwenye Swalaah, anakuwa wakati huo haswali kwa ufaradhi wa twahara. Kwani yeye ametayamamu kama alivyoamrishwa, na kwa kupiga takbiyr, anakuwa ashatoka nje ya wigo wa faradhi ya twahara. Na hapo inakuwa haijuzu tena kuivunja twahara hiyo ambayo muda wake ushapita, au kuvunja rakaa ambazo ameshaziswali kama alivyofaradhishiwa. Na suala hili haliwezi kufanyika ila kwa dalili kutoka kwenye Qur-aan, au Sunnah, au Ijma’a.



Ninasema:

“Ninaloliona lenye nguvu zaidi ni kuwa mtu ataendelea kukamilisha Swalaah yake, kwa vile hakujathibiti lolote lenye kulazimisha kuikata Swalaah baada ya kuianza. Hii ni kama mfano wa mtu anayefunga Swaum ya kafara. Ikiwa ameanza Swaum yake kisha akapata mtumwa wa kumwacha huru, basi hatoivunja Swaum yake. Na Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi."




·

Ikiwa mtu ameswali kwa kutayamamu, kisha maji yakapatikana kabla ya wakati wa Swalaah kumalizika, je ataswali tena?



Huyu hatorejesha tena Swalaah yake kwa mujibu wa kauli mbili sahihi za Maulamaa. Haya ni madhehebu ya Maalik, Ath-Thawriy, Al-Awzaaiy, Al-Mazniy, Atw-Twahaawiy na Ahmad katika moja ya riwaya mbili. Hivi hivi kasema Ibn Hazm. [Angalia Al-Majmu’u (2/353) na Al-Muhallaa (2/139)].



Lakini Abuu Haniyfah na Ash-Shaafi’iy, wao wanasema kwamba ni lazima ailipe upya Swalaah yake wakati anapoyapata maji. [Al-Majmu’u (2/353)].



Ibn Hazm amewajibu akisema: “Ama kauli ya Abuu Haniyfah na Ash-Shaafi’iy, ni wazi kwamba imedoda, kwa kuwa kumwamuru kwao mtu atayamamu na aswali, hakukosekani na; ima wao wamemwamuru kuswali Swalaah ambayo ni faradhi ya Allaah juu yake, au Swalaah ambayo Allaah Hakumfaradhishia, na hakuna la tatu hapo. Na ikiwa mwenye kuwafuata atasema: Wamemwamuru Swalaah ambayo ni faradhi juu yake, tutamwambia: Kwa nini basi aiswali tena baada ya wakati wake ikiwa alitekeleza faradhi yake? Na ikiwa atasema: Bali wamemwamuru Swalaah ambayo si faradhi juu yake, hapo atakuwa amekiri kwamba wao wamemlazimisha jambo lisilo lazima kwake, na hili ni kosa”.



Ninasema:

“Ndio. Si lazima kuswali tena. Lakini ni vizuri kuswali tena madhali muda upo na maji yamepatikana. Na hii ni kwa Hadiyth ya Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy aliyesema:

“Watu wawili walitoka kwenda safari. Ukawakuta wakati wa Swalaah na wao hawana maji. Wakatayamamu kwa mchanga kisha wakaswali. Halafu baadaye walipata maji kabla wakati haujatoka. Mmoja wao akatawadha na kuswali tena, lakini mwingine hakufanya. Halafu walikwenda kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakamweleza walilolifanya. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia yule ambaye hakuswali tena:

(( أصبت السنة وأجزأتك صلاتك))

((Umeipata Sunnah, na Swalaah yako imekutosheleza)).

Kisha akamwambia yule aliyetawadha na kuswali tena:

(( لك الأجر مرتين))

((Una ajri mara mbili)). [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (334) na An-Nasaaiy
 
Naam tumemaliza kipengele cha Kutayamamu

Tumeona ni namna gani Allah anatutakia yaliyo mepesi ili mradi tu tuitekeleze ibada yake

Kwahiyo hapa tunaona kwamba hakuna sababu ya mtu kukosa swala tena akiwa mwanaume maana hana udhuru maalumu kama mwanamke

Hata bahati mbaya ukiwa mahabusu hakuna maji wala mchanga,ila utatayamamu kwa kutumia ukuta maadamu tu ukuta huo uwe umebeba vitu vinavyotokana na ardhi,na kama ni ukuta wa matofali basi inafaa kwasababu hayo matofali yana asili ya mchanga ndani yake

Na tumeona unafuu ambao unaweza kutusaidia pale tunaposhindwa kutumia maji ima kwa baridi kali au ugonjwa,basi tutatayamamu

Tumeona kauli za wanazuoni juu ya je,ni pigo moja kutayamamu au mawili, na wametoa dalili zao,ni juu yako kufuata lile ambalo unaona linafaa

Binafsi nakubaliana au nafuata rai ya kupiga mapigo mawili

Allah anajua zaidi


Darsa litaendelea juu ya Hedhi na Nifasi,kesho inshallah
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



076-Hedhi Na Nifasi



Alhidaaya.com



Damu za kimaumbile zinazomtoka mwanamke zinagawanyika vigawanyo vitatu:



1- Damu ya hedhi



2- Damu ya nifasi



3- Damu ya istihaadhwah



Damu Ya Hedhi



[Majina mengineyo ya hedhi ni: الطمث – العراك – الضحك – الإكثار – الإعصار. (Al-Muhadh-dhab 1/341)]

Ni damu nyeusi, nzito na yenye harufu mbaya. Inamtoka mwanamke toka sehemu maalumu katika nyakati maalumu.



Hedhi ni jambo ambalo Allaah Amewaumbia wanawake wote kama Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyomwambia ‘Aaishah kama ilivyo katika Swahiyh Mbili:

(( إن هذا أمر كتبه الله على بنات آدم....))

((Hakika hili ni jambo, Allaah Amelihukumia kwa mabinti wa Aadam)).



Hawwaa (Amani iwe juu yake), yeye ndiye wa mwanzo kuipata. Imepokelewa kwa isnadi Swahiyh kwa Ibn 'Abbaas akisema:

“ Hawwaa alianza kupata damu ye hedhi baada ya kushushwa toka peponi”.



Damu ya hedhi haina mpaka wa uchache wala wingi, bali hilo linategemea maumbile ya mwanamke, kwa vile hakuna dalili yoyote sahihi toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inayobainisha uchache wake au wingi wake.



Shaykh wa Uislamu katika Kitabu cha Al-Fataawa (21/623) anasema:

“Ama wale wanaosema kwamba wingi wa hedhi ni siku kumi na tano na uchache wake ni siku moja kama Ash-Shaafi’iy na Ahmad, au wanaosema kuwa hedhi haina mpaka maalumu kama Maaliki, wao wanasema hayo tu, lakini halijathibiti lolote kuhusiana na hilo toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au Maswahaba zake. Na marejeo ya yote hayo yanasimamia juu ya maumbile ya mwanamke kama tulivyosema, na Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi.” [Jaami'u Ahkaamin Nisaa (1/179). Angalia Al-Muhalla (2/191) na Al-Mughniy (1/308)].
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



077-Kuanza Na Kumalizika Hedhi



Alhidaaya.com





[Jaami'u Ahkaamin Nisaa (1/200) na kurasa zinazofuatia]



1- Kuanza kwa hedhi kunajulikana kwa msukumo wa damu wakati wake, nayo ni damu nyeusi, nzito na yenye harufu mbaya.



2- Kumalizika kwake hujulikana kwa kukatika damu, kuwepo unjano na rangi yenye kumili weusi. Na hili linatokana na mambo mawili:



(a) Ukavu; nako ni kutoka kikiwa kikavu kilichoingizwa katika njia ya uzazi. Yaani ikiwa mwanamke ataingiza kitambaa au pamba katika utupu wake, basi hutoka kikiwa kikavu.



(b) Kuwepo maji meupe yanayotoka katika njia ya uzazi wakati wa kukatika damu ya hedhi.



Imepokelewa na mwachwa huru wa ‘Aaishah akisema:

“Wanawake walikuwa wakimwendea na kitambaa chenye pamba yenye unjano utokanao na damu ya hedhi, kisha wanamuuliza kama wanaweza kuswali, naye huwajibu akisema: “Msifanye haraka mpaka mwone maji meupe”.



Hapa anamaanisha kwamba wametwaharika na hedhi. [Ni Hadiyth Hasan kwa nyingine. Imefanyiwa “ikhraaj” na Maalik (uk 59), Al-Bukhaariy akitoa maelezo (1/420 – Fat-h) na ‘Abdur-Raaziq (1/302) kwa Sanad Dhwa’iyf ingawa ina ushahidi kwa Ad-daaramiy (1/214), na Al-Bayhaqiy (1/337). Na Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi].
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



078-Nini Hukmu Ya Unjano Na Rangi Yenye Kumili Weusi Baada Ya Kutwaharika Na Hedhi?



Alhidaaya.com





Unjano na rangi yenye kumili weusi ni maji anayoyaona mwanamke mithili ya usaha. Maji haya yanakuwa si damu ya hedhi kama yatamtoka mwanamke baada ya kukatika damu au baada ya kukauka. Atazingatiwa yu twahara, ataswali, atafunga na mumewe atamwingilia.

Dalili ya hili ni Hadiyth ya Ummu 'Atwiyyah aliposema:

“Tulikuwa - baada ya kujitwaharisha - hatushughulishwi chochote na rangi yenye kumili weusi au unjano”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (307), An-Nasaaiy (1/186), Ibn Maajah (647) na wengineo. Al-Bukhaariy ameikhariji bila ziada (326)].



Faida



1- Damu inapokatika na mwanamke akawa twahara lakini maji ya kuogea yakakosekana, itambidi atayamamu na mumewe anaruhusika kumwingilia. Hili ndilo tamko la Maulamaa wengi. [Majmu’u Al-Fataawaa (1/625), Al-Muhallaa (2/171), Sharhu Muslim (1/593) na Jaami’u Ahkaamin Nisaa (1/152)]



2- Damu ikiendelea kutoka zaidi ya muda wake wa kawaida, nini atafanya?

Ikiwa kwa mfano damu yake kwa kawaida hutoka kwa muda wa siku sita kila mwezi, kisha ikazidi ikawa siku saba, au nane, au tisa, nini atafanya?



Tunasema: “Hali ya mwanamke huyu haiachani na moja ya mawili:




·

Ima atakuwa anaweza kupambanua na kutofautisha kati ya damu ya hedhi na damu nyingineyo.



Mwanamke huyu ataiangalia damu hii. Ikiwa rangi yake, harufu yake na maumbile yake yako sawa na damu ya hedhi, basi ataendelea kuacha Swalaah, Swaum na kuingiliwa kama alivyokuwa, kwa kuwa hakuna mpaka maalumu wa muda wa kutoka damu hii kama tulivyotangulia kusema. Na kama ataiona inatofautiana na damu ya hedhi, basi ataoga na kuswali.




·

Au atakuwa hawezi kupambanua na kutofautisha kati ya damu ya hedhi na nyingineyo (kuna baadhi ya wanawake wako hivi).



Huyu ataendelea kubakia bila kuswali, wala kufunga, wala kuingiliwa na mumewe mpaka atakapotwaharika, kwa kuwa hakuna mpaka wa upeo wa mwisho wa kutoka damu ya hedhi. [Jaami’u Ahkaamin Nisaa (1/215), na kitabu cha Fataawaal Mar-at cha Ibn ‘Uthaymiyn].



3- Ikiwa damu katika siku zake za mwezi inakuja siku mbili kwa mfano, kisha inakatika siku ya tatu, halafu inarudi tena siku ya nne na kadhalika.



Jibu sahihi la hali hii ni kuwa kukatika damu ndani ya masiku ya hedhi yanayojulikana, hakuzingatiwi bali huhesabiwa ni hedhi. Kinachozingatiwa ni kuonekana alama ya utwahara, nayo ni majimaji meupe ambayo akina mama wanayajua. [Fataawaal Mar-at, Jam’u Muhammad Al-Musnad (uk. 26)].



4- Je, mjamzito hupata hedhi? [Jaami’u Ahkaamin Nisaa (1/208)]



Maulamaa wana mielekeo miwili katika suala hili. Kundi la kwanza ambalo ni la wengi, wanasema kwamba mwanamke mjamzito haingii hedhini. Dalili yao ni Hadiyth ya Abuu Sa’iyd Al Khudriyyi (Radhwiya Allaahu Anhu) isemayo:

(( لا توطأ حامل حتى تضع ولا غير حامل حتى تحيض حيضة ))

((Mjamzito haingiliwi mpaka ajifungue, wala asiye mjamzito mpaka aingie hedhini)). [Hadiyth Hasan Lighayrih. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (2157), na Ahmad (3/62). Kuna Hadiyth nyingine kama hii kwa Ad Daar Qutwniy (3/257)].



Wanasema:”Linalothibitisha kwamba mwanamke hana kitu katika tumbo lake la uzazi, ni kutokwa na damu ya hedhi, na lau kama mjamzito anapata hedhi, basi hedhi hii haiwezi kuthibitisha kuwa hana kitu tumboni”.



Ama kundi la pili akiwemo Ash Shaafi’iy, wao wanasema kwamba mjamzito hupata damu ya hedhi.



Jibu sahihi kuhusiana na kauli yao hii ni kuwa asili na kaida kuu ya wingi ni kwamba mja mzito hapati hedhi. Lakini inaweza ikamtokezea mwanamke fulani katika hali isiyo ya kawaida akatokwa na damu wakati wa ujauzito. Damu hii itaangaliwa; ikiwa iko sawa na damu ya hedhi kwa rangi, harufu na maumbile, na ikamjia wakati uleule anaopata hedhi, basi itazingatiwa kuwa ni damu ya hedhi. Hapo ataacha Swalaah, Swaum na mumewe hatoruhusiwa kumwingilia. Lakini damu hii haitoingizwa katika hisabu ya eda, kwa kuwa Allaah Anasema:

(( وأولات الأحمال أجلهن أن يضعن حملهن))

(( Wenye mimba muda wao ni kuzaa mimba zao)). [At-Twalaaq (65:4)]



Ama ikiwa damu inayomtoka inatofautiana na sifa za damu ya hedhi na imekuja katika wakati usio wa hedhi, basi si damu ya hedhi na wala haibebi hukmu za hedhi. Itakuwa ni kama damu ya istihaadhwah.
 
Naam wote hatuwezi kuwa Masheikh ila jitahidi kutenga muda wako kusoma mambo kama haya ambayo ni muhimu kwa ibada zako

Ibada hazifanywi bila elimu


Darsa litaendelea inshallah
 
Back
Top Bottom