Ramadhan Special Thread
IMG_20250320_170217.jpg
 
Tunapokuta mijadala ya hovyo hapa Jf yenye malengo ya kuitakana na kumdhalilisha Uislamu na Mtume wake (ﷺ) ni bora kuiepuka na tusipende kujingiza isipokuwa kukiwa na haja ya kutoa ubainifu Fulani au haja ya dharura na umuhimu kuwepo.

Na lingine la kuchunga tusiwe watu wa kwanza kuwachokoza na kuwatukana watu wa Dini nyingine humu jukwaani , Hilo ni jambo baya sana kwani litapelekea na wao kuanza kutakana dini yetu na wewe kuwa chanzo Cha hayo.

Ukiona umekutana na mtu wa jazba , mihemko, matusi , kejeli , dhihaka nk huyo mpuuze usihangaike kubishana nae Wala kurudishiana majibu , kwani Hilo kitu hakina afya na dini yetu imetukataza vikali.

Kingine tusiwe wavivu na wachoyo wa kutoa nasaha au kurekebishana unapoona ndugu yako kakoseq au anaenda kinyume na misingi ya dini , kwenye Hilo muhimu kutumia lugha nzuri ya hekima na kuzingatia faragha katika mambo yanayolazimu hivyo.


Brown and Blue Classic Islamic Hadith Quote Instagram Post_20250320_175119_0000.png
 
Tunapokuta mijadala ya hovyo hapa Jf yenye malengo ya kuitakana na kumdhalilisha Uislamu na Mtume wake (ﷺ) ni bora kuiepuka na tusipende kujingiza isipokuwa kukiwa na haja ya kutoa ubainifu Fulani au haja ya dharura na umuhimu kuwepo.

Na lingine la kuchunga tusiwe watu wa kwanza kuwachokoza na kuwatukana watu wa Dini nyingine humu jukwaani , Hilo ni jambo baya sana kwani litapelekea na wao kuanza kutakana dini yetu na wewe kuwa chanzo Cha hayo.

Ukiona umekutana na mtu wa jazba , mihemko, matusi , kejeli , dhihaka nk huyo mpuuze usihangaike kubishana nae Wala kurudishiana majibu , kwani Hilo kitu hakina afya na dini yetu imetukataza vikali.

Kingine tusiwe wavivu na wachoyo wa kutoa nasaha au kurekebishana unapoona ndugu yako kakoseq au anaenda kinyume na misingi ya dini , kwenye Hilo muhimu kutumia lugha nzuri ya hekima na kuzingatia faragha katika mambo yanayolazimu hivyo.


View attachment 3277610
Hili maalim limenigusa mno,unajua wenzetu upande wa pili hupenda sana kutuchokoza na kutudhihaki na wanafurahi vile tunavyo hamaki na kutokwa na povu,katu tusiwape hiyo starehe

Tuwadharau tu na kuwaacha kama walivyo,maana saa nyingine kunyamaza ni jibu na ni bora zaidi,mimi siku hizi hunikuti tena najadili na watu kama hao,labda ntajadili kama mtu anataka mjadala wa hekima na busara na kuelimishana

Kwahiyo ni sahihi kabisa tujiweke mbali na watu ambao nia yao sio nzuri kwetu sisi
 
MUHIMU

Kuna bisahara za kidunia na biashara za akhera biashara za kidunia ni kwa ajili kuimarisha maisha yetu ya hapa duniani ili tuweze kutekeleza majukumu yetu vyema na biashara za akhera ni kwa ajili ya kuimarisha maisha yetu ya kudumu na biashara zote hizo zina misimu yake wafanya biashara kunufaika na biashara zao

Mola wetu mlezi amesema :
{ إِنَّ ٱللَّهَ ٱشۡتَرَىٰ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِینَ أَنفُسَهُمۡ وَأَمۡوَ ٰ⁠لَهُم بِأَنَّ لَهُمُ ٱلۡجَنَّةَۚ
hakika ya Allah amenunua kwa waumini nafsi zao na mali zao kwakua wao watapata pepo ( kwa kutoa nafsi zao na mali zao kwa ajili yake )

[Surah At-Tawbah: 111]

Mola wetu mlezi ametangaza biashara na waumin na bidhaa yake anayouza mbadala wa wanacho kitoa waja wake ni pepo

Mwezi huu ni msimu wa biashara ya akhera ili kuipata pepo na huu ndio msimu ambao mtume swalla Allah alaihi wasallam amesema maneno mengi kuuhusu katika hayo ni :
من حرم خيرها فقد حرم
Atakae nyimwa kheri zake hakika huyo amenyimwa

msimu huu ndio wa kuchuma kheri na atakaekosa kheri za msimu huu hakika huyo amekosa kheri katika maisha yake kwakua msimu huu malipo ni maradufu

Tunaelekea kumi la mwisho ambalo lina ubora zaidi ya masiku yote yaliopita lakini lina ashiria kumaliza kwa msimu je umejiandaa kulikabili ?

Je umefanya tathmin ya yale uliopanga kutenda katika ibada ndani ya msimu huu wa kuchuma kheri umefanikiwa kiasi gani ?

Ikiwa masiku yaliopita umefanya vizuri basi ongeza zaid ya ulichofanya , na ikiwa umezembea basi tengeneza hali yako sasa usamehewe uliyozembea awali

RAMADHAN MWEZI WA IBADA NA KUMI LA MWISHO NI KUMI LA ITIKAFU, TUKAKAE ITIKAFU

Abu fat'hiya khamis kiza
 
MWISHONI MWA RAMADHANI

KIpindi hiki watu wengi hughafirika sana hasa tunapokuwa katika kumi.la mwisho,jitihada kubwa tunaipeleka kununua nguo za sikukuu na matayarisho ya sikukuu,lakini tunasahau kwamba kipindi hiki ndio kipindi hasa cha kujipinda kwa ajili ya kufanya amali nyingi zaidi na kurekebisha pale ambapo tulipoteza kwa maana moja au nyingine

Sio vibaya kufanya matayarisho ya sikukuu lakini yaende sambamba na kufanya jitihada kubwa za kujipinda katika kumi hili la mwisho,siku zote matendo bora zaidi ni yale ya mwisho,na ndio maana siku zote huwa tunatakiwa kuomba tupate mwisho mwema

Ebu fanya tafakari,je umeswali swala za sunna za kutosha?

Je haukupitwa na swala za faradhi?

Je umesoma qur'an kiasi gani?

Je umemtaja Allah kiasi gani?

Umetoa sadaka mara ngapi?

Iwe umefanya hayo mara nyingi au mara chache basi kumi hili la mwisho linastahili juhudi kubwa zaidi

Tumche Allah
 
Fadhila Za Qiyaamul-Layl

(Kisimamo Cha Kuswali Usiku)



Alhidaaya.com





Muislamu anapaswa asikose Qiyaamul-Layl khasa katika mwezi wa Ramadhwaan kwa sababu ya Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ)) رواه البخاري 37 ومسلم 759

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Atakayesimama kuswali Ramadhwaan kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Al-Haafidh Ibn Rajab (Rahimahu Allaah) amesema: "Tambua kuwa Muumini anajumuisha katika mwezi wa Ramadhwaan jihaad mbili kwa ajili ya nafsi yake; jihaad ya mchana ya kufunga, na jihaad ya usiku kwa kusimama (kuswali), atakayejumuisha jihaad hizi mbili atapata ujira wake bila ya hesabu".



Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema: "Haimpasi Muislamu kuepukana na Swalaah ya Tarawiyh katika Ramadhwaan ili apate thawabu na ujira wake, na wala asiondoke mpaka Imaam amalize Swalaah ya Witr ili apate ujira kamili wa Qiyaamul-Layl".



Ili kuipata ladha ya Ramadhwaan na kuongeza utiifu, ni muhimu Muislamu ajumuike na Waislamu wenzie kuswali Tarawiyh asikilize Qur-aan inaposomwa katika Swalaah hizi kwa sababu itampatia utulivu wa moyo na pia atajichumia thawabu adhimu zinazopatikana katika kisimamo hiki kinachofuta madhambi kama ilivyotajwa katika Hadiyth iliyotangulia.



Fadhila Nyenginezo Za Qiyaamul-Layl:



1-Qiyaamul-Layl ilikuwa ni amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Waumini wakatekeleza:





يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ﴿١﴾ قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا﴿٢﴾ نِّصْفَهُ أَوِ انقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا﴿٣﴾ أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ الْقُرْآنَ تَرْتِيلًا﴿٤﴾



Ee mwenye kujigubika! Simama na uonye. Na Rabb wako mtukuze. Na nguo zako toharisha. [Al-Muzzammil 1-4]



Na pia Amemuamrisha tena Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا ﴿٧٨﴾ وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ﴿٧٩﴾

Simamisha Swalaah jua linapopinduka hadi kiza cha usiku na Qur-aan ya (Swalaah ya) Alfajiri. Hakika Qur-aan ya Alfajiri ni yenye kushuhudiwa. Na katika usiku, amka uswali (tahajjud) kuisoma (Qur-aan); ni ziada ya Sunnah kwako Asaa Rabb wako Akakuinua cheo kinachosifika. [Al-Israa: 78-79]



Mujaahid amesema: "Qiyaam kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni naafilah (Sunnah ya ziada) kwa sababu ameshafutiwa madhambi yake yaliotangulia na ya mbele. Na kwa Ummah wa Kiislamu, Swalaah ya Qiyaamul-Layl huenda pia ikamfutia mtu madhambi yake atakayotenda". [Atw-Twabariy 17:525]



Anasema tena Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



فَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ﴿٣٩﴾وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَأَدْبَارَ السُّجُودِ﴿٤٠﴾



Subiri juu ya yale wanayoyasema, na sabbih kwa Himidi za Rabb wako kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa. Na katika usiku Msabbih na baada ya kusujudu. [Qaaf: 39-40]



Na:

وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا﴿٢٥﴾ وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا﴿٢٦﴾



Na lidhukuru Jina la Rabb wako asubuhi na jioni. Na katika usiku msujudie na uswali kwa ajili Yake usiku mrefu. [Al-Insaan: 25-26]



2-Qiyaamul-Layl ni njia mojawapo ya kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



Kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) sio kwa kutamka tu bali kwa kukiri moyoni na kwa matendo. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisimama usiku kuswali mpaka miguu yake ilikuwa ikivimba:



عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا: أَنَّ نَبِيَّ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُومُ مِنَ اللَّيْلِ حَتَّى تَتَفَطَّرَ قَدَمَاهُ، فَقَالَتْ عَائِشَةُ: لِمَ تَصْنَعُ هَذَا يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَقَدْ غَفَرَ اللَّهُ لَكَ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ؟ قَالَ: (أَفَلاَ أُحِبُّ أَنْ أَكُونَ عَبْدًا شَكُورًا) متفق عليه



Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisimama usiku hadi ikivimba miguu yake, nikamwambia: “Kwa nini unafanya hivi ee Rasuli wa Allaah na hali umefutiwa madhambi yako yaliyotangulia na yatakayofuatia?” Akasema: (Je, nisiwe mja mwenye kushukuru?) [Al-Bukhaariy na Muslim]



3-Qiyaamul-Layl ni Swalaah bora kabisa baada ya Swalaah ya fardhi kwa kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



(أَفْضَلُ الصَّلاةِ بَعْدَ الْفَرِيضَةِ صَلاةُ اللَّيْلِ) رواه مسلم.



((Swalaah iliyo bora kabisa baada ya fardhi ni Swalaah ya usiku)) [Muslim]



4-Qiyaamul-Layl ni kufuata na kufufua Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)



Na pia Qiyaamul-Layl ilikuwa ni desturi ya Salaf na sababu kuu ya kumzidishia Muislamu iymaan yake na kumtakasa moyo kutokana na maovu mengi; uasi, unafiki, chuki, uhasidi n.k. Pia nyoyo hupata utulivu na huelekea kwa yanayomridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Hadiyth ifuatayo imethibiti:



عن بلال، أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: عليكُم بقيامِ اللَّيلِ ، فإنَّهُ دَأْبُ الصَّالِحينَ قبلَكُم ، و قُربةٌ إلى اللهِ تعالى ومَنهاةٌ عن الإثمِ و تَكفيرٌ للسِّيِّئاتِ ، ومَطردةٌ للدَّاءِ عن الجسَدِ



Amesimulia Bilaal (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Shikamaneni na Qiyaamul-Layl (kuswali usiku) kwani ni desturi za Swalihina (waja wema) kabla yenu, na kujikurubisha kwa Allaah, na inazuia madhambi, inafuta maovu na inaondosha maradhi mwilini.” [Ahmad na At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami (4079)]



‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa akipitia usiku akisikia kisomo cha Qiyaamul-Layl, akazimia siku moja yakapita masiku akiugua hadi akapona [Munswaf Ibn Abiy Shaybah]



Na yamemthibiti mengi kuhusiana na hali za Salaf kusimama kwao usiku kuswali.



5-Qiyaamul-Layl ni kujikurubisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



عن عَمْرُو بْنُ عَبَسَةَ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: ((أَقْرَبُ مَا يَكُونُ الرَّبُّ مِنَ العَبْدِ فِي جَوْفِ اللَّيْلِ الآخِرِ، فَإِنْ اسْتَطَعْتَ أَنْ تَكُونَ مِمَّنْ يَذْكُرُ اللَّهَ فِي تِلْكَ السَّاعَةِ فَكُنْ)) الترمذي هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ



Imepokelewa kutoka kwa 'Amru bin 'Abasah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba kamsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Wakati Allaah Anakuwa karibu kabisa na mja, ni wakati wa mwisho wa usiku, kwa hiyo ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomdhukuru Allaah katika saa hiyo basi uwe)) [At-Tirmidhy ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3579), Swahiyh Al-Jaami’ (1173)]







6-Qiyaamul-Layl ni kujikinga na maovu ya shaytwaan:





عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بن مسعود رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ: ذُكِرَ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلٌ، فَقِيلَ: مَا زَالَ نَائِمًا حَتَّى أَصْبَحَ، مَا قَامَ إِلَى الصَّلاَةِ، فَقَالَ: ((ذَاكَ رَجُلٌ بَالَ الشَّيْطَانُ فِي أُذُنِهِ)) روى البخاري (1144) ومسلم (774) والنسائي (1608) وابن حبان (2562)



Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’-uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba ilitajwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba kuna mtu alilala usiku wote hadi asubuhi bila kuswali, Akasema: ((Huyo ni mtu aliyekojolewa na Shaytwaan katika masikio yake)) [Al-Bukhaariy, Muslim, An-Nasaaiy, Ibn Hibbaan]



‘Ulamaa wamekhitilafiana kusudio la kauli: “mtu alilala usiku wote hadi asubuhi bila kuswali”. Wakataj wengine kuwa ni Swalaah ya fardhi na wengine wakaona ni Qiyaamul-Layl.







7-Wanaoswali Qiyaamul-Layl wameandaliwa Jannah:



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ ﴿١٦﴾ فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٧﴾



Mbavu zao zinatengana na vitanda, wanamuomba Rabb wao kwa khofu na matumaini, na katika yale Tuliyowaruzuku wanatoa. Basi nafsi yoyote haijui yaliyofichiwa katika yanayoburudisha macho. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [As-Sajdah: 16-17]







Aayah hizo tukufu zinambashiria Muumini Jannah pindi atakapojitahidi kuamka kuswali usiku pamoja na kutoa mali yake katika njia ya Allaah. Huko Jannah, kuna neema za kufurahisha zenye kudumu milele ambazo hajapatapo mtu kuona wala kusikia wala kuwaza kama ilivyotajwa katika Hadiyth Al-Qudsiy:



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ مَا لَا عَيْنٌ رَأَتْ وَلَا أُذُنٌ سَمِعَتْ وَلَا خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ)) قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ اقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: (( فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ)) البخاري، مسلم، الترمذي وابن ماجه



Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Amesema: Nimewatayarishia waja Wangu wema kile ambacho jicho lolote halijapata kuona na sikio lolote halijapata kusikia na wala haijapata kupita katika moyo wa binaadamu)) Akasema Abuu Hurayrah: Kwa hivyo, soma ukitaka:

فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ

Basi nafsi yoyote haijui yaliyofichiwa katika yanayoburudisha macho. [As-Sajdah:17] [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]





Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametaja pia kuhusu wanaoamka kuswali usiku:



إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ﴿١٥﴾ آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ﴿١٦﴾ كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ﴿١٧﴾ وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ﴿١٨﴾ وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ﴿١٩﴾



Hakika wenye taqwa watakuwa katika Jannaat na chemchem. Wakichukua yale Atakayowapa Rabb wao. Hakika wao walikuwa kabla ya hapo ni wahisani. Walikuwa kidogo tu katika usiku wakilala kwa raha. Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfirah. Na katika mali zao kuna haki maalum kwa mwenye kuomba na asiyeomba. [Adh-Dhaariyaat: 15-19]





Na pia Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):





عَنْ عَلِيٍّ قَالَ : قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((إِنَّ فِي الْجَنَّةِ غُرَفًا تُرَى ظُهُورُهَا مِنْ بُطُونِهَا، وَبُطُونُهَا مِنْ ظُهُورِهَا، فَقَامَ أَعْرَابِيٌّ فَقَالَ : لِمَنْ هِيَ يَا رَسُولَ اللَّهِ ؟ قَالَ : ((لِمَنْ أَطَابَ الْكَلامَ وَأَطْعَمَ الطَّعَامَ ، وَأَدَامَ الصِّيَامَ ، وَصَلَّى لِلَّهِ بِاللَّيْلِ وَالنَّاسُ نِيَامٌ )) وحسنه الألباني في صحيح الترمذي .



Imepokelewa kutoka kwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika katika Jannah kuna nyumba ambazo nje yake huonekana ndani na ndani yake huonekana nje)) Bedui mmoja akasimama na kusema: “Ee Rasuli wa Allaah kwa ajili ya nani hizo?”. Akasema: ((Kwa ajili ya wanaotamka maneno mazuri, wanaolisha watu chakula, wenye kudumisha swiyaam, na wenye kuswali usiku wakati watu wengine wamelala)) [At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (1984)]





8-Qiyaamul-Layl ni miongoni mwa sifa za waja wa Ar-Rahmaan:



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):





وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿٦٣﴾ وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا ﴿٦٤﴾



Na waja wa Ar-Rahmaan ni wale wanaotembea katika ardhi kwa unyenyekevu na upole, na majahili wanapowasemesha, wao husema: Salaam! Na wale wanaokesha usiku kwa ajili ya Rabb wao wakisujudu na kusimama. [Al-Furqaan: 63-64]





9-Wanaoswali Qiyaamul-Layl si sawa na watu wengine.



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):





لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾



Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah). [Aal-'Imraan: 113]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):





أَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاءَ اللَّيْلِ سَاجِدًا وَقَائِمًا يَحْذَرُ الْآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ ۗ قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٩﴾



Je, yule aliye mtiifu nyakati za usiku akisujudu, au akisimama (kuswali), anatahadhari na Aakhirah na anataraji rahmah ya Rabb wake (ni sawa na aliyekinyume chake?). Sema: Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua? Hakika wanakumbuka wenye akili tu. [Az-Zumar: 9]





10-Qiyaamul-Layl ni kughufuriwa madhambi.



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa wanaoswali thuluthi ya mwisho ya usiku:





الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ﴿١٧﴾



Wenye kusubiri na wasemao kweli, na watiifu, na watoaji mali katika njia ya Allaah na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri. [Aal-‘Imraan: 17]



Na katika Hadiyth Al-Qudsiy:





عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ، مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ، مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ)) البخاري و مسلم



Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Huteremka (kwa namna inavyolingana na utukufu Wake) kila siku katika mbingu ya dunia inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba du’aa Nimuitike? Nani Ananiomba jambo Nimpe? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy, Muslim]





11-Mwenye kuswali Qiyaamul-Layl hujaaliwa siha katika mwili wake.



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemsema:





((عليكُم بقيامِ اللَّيلِ ، فإنَّهُ دَأْبُ الصَّالِحينَ قبلَكُم ، و قُربةٌ إلى اللهِ تعالى ومَنهاةٌ عن الإثمِ و تَكفيرٌ للسِّيِّئاتِ ، ومَطردةٌ للدَّاءِ عن الجسَدِ))



((Shikamaneni na Qiyaamul-Layl (kuswali usiku) kwani ni desturi za waja wema kabla yenu, na kujikurubisha kwa Allaah Ta’aalaa, na inazuia madhambi, inafuta maovu na inaondosha maradhi mwilini)) [Ahmad na At-Tirmidhiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami (4079)]





12-Nyakati za Qiyaamul-Layl ni nyakati za kutakabaliwa du’aa:





عَنْ جَابِرٍ قَالَ : سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((إِنَّ فِي اللَّيْلِ لَسَاعَةً لَا يُوَافِقُهَا رَجُلٌ مُسْلِمٌ يَسْأَلُ اللَّهَ خَيْرًا مِنْ أَمْرِ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ إِلَّا أَعْطَاهُ إِيَّاهُ وَذَلِكَ كُلَّ لَيْلَةٍ)) مسلم



Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba kamsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika katika usiku kuna saa ambayo mja anapomuomba Allaah kheri katika mambo ya dunia au Aakhirah ila (Allaah) Humpa kheri hizo, na hivyo ni kila usiku)) [Muslim]







13-Kuswali Qiyaamul-Layl ni utukufu wa Muumini:



عنْ سهل بن سعد الساعدي عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم: ((أتاني جبريلُ ، فقال : يا مُحمَّدُ! عِشْ ما شِئتَ فإنَّك مَيِّتٌ، وأحْبِبْ من شِئتَ فإنَّكَ مُفارِقُه، واعمَل ما شِئتَ فإنَّك مَجْزِيٌّ بهِ، واعلَم أنَّ شرفَ المؤمنِ قيامُه باللَّيلِ، وعِزُّه استِغناؤُه عن النَّاسِ)) رواه الحاكم والبيهقي وحسنه المنذري والألباني



Imepokelewa kutoka kwa Sahl bin Sa’d As-Saa’idiy kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Amenijia Jibriyl akasema: Ee Muhammad ishi upendavyo bila shaka wewe utakuwa maiti, na mpende umtakaye bila shaka utafarikiana naye, na tenda unavyopenda lakini ujue utalipwa kwa vitendo hivyo, na tambua kwamba utukufu wa Muumin ni Qiyaamul-Layl, na heshima yake ni kujitosheleza na watu)) [Hadiyth imepokelewa pia kutoka kwa Jaabir na ‘Aliy Radhwiya Allaahu ‘anhumaa - Al-Haakim na Al-Bayhaqiy, na Al Mundhiriy na Al-Abaaniy wamesema ni Hadiyth Hasan – As-Silsilah Asw-Swahiyhah (831)]







14-Qiyaamul-Layl ni kupata husnul-khaatimah (mwisho mwema)





عبدالله بن عمرو عن النبي صلى الله عليه وسلم ((من قام بعشرِ آياتٍ لم يُكتبْ من الغافلينَ ، ومن قام بمئةِ آيةٍ كُتبَ من القانتينَ ومن قام بألفِ آيةٍ كُتبَ من المُقَنْطِرينَ)) صحيح أبي داود



Amesimulia ‘Abdullaah bin ‘Amr (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesimama usiku kuswali na akasoma Aayah kumi, hatoandikiwa kuwa miongoni mwa walioghafilika, na atakayesimama kuswali akasoma Aayah mia, ataandikiwa ni miongoni mwa watiifu, na atakayesimama kuswali akasoma Aayah elfu, ataandikwa miongoni mwa wenye mirundi (ya thawabu).’ [Abuu Daawuwd, Al-Albaaniy ameisahihisha: Swahiyh Abiy Daawuwd (1398), Swahiyh Al-Jaami’ (6439)]





15-Nyuso za wanaoswali Qiyaamul-Layl hun’gaa kwa Nuru:



Hasan Al-Baswriy (Rahimahu Allaah) amesema:



"ما نعلم شيئًا أَشَدَّ من مكابدة اللَّيل ونفقة هذا المال" فقيل : ما بالُ المتهجِّدين من أحسن الناس وجوهًا ؟ قال : "لأنهم خلوا بالرحمن فألبسهم نورًا من نوره" إحياء علوم الدين

"Sijapata kuona ‘ibaadah iliyo nzito kama Swalaah katika kiza cha usiku na kutoa kwake mali". Akaulizwa: “Mbona wale Mutahajjudiyn (wanaoamka usiku kuswali) nyuso zao ni nzuri kabisa?” Akajibu: "Kwa sababu wamejiweka faragha na Ar-Rahmaan, basi Naye Akawavisha Nuru Yake". [Ihyaa ‘Uluwm Ad-Diyn]







Baadhi Ya Yatakayomwezesha Muislamu Qiyaamul-Layl



1-Kuwa na ikhlaasw katika ‘amali.



2-Kutafakari Hadiyth ya Al-Qudsiy kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anateremka thuluthi ya mwisho kuwakidhia Waislamu haja zao. Nani asiyekuwa na haja, nani asiyekuwa na madhambi ya kughufuriwa? Asiyejihimiza kuamka usiku ni kama kwamba hamhitaji Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amtakakbalie haja zake na Amghufurie dhambi zake!



3-Kutambua fadhila za Qiyaamul-Layl.



4-Kulala katika twahaarah, yaani kutia wudhuu kabla ya kulala.



5-Kusoma nyiradi za usiku na kumuomba sana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) tawfiyq ya kuamka usiku.



6-Kulala mapema



7-Kutokula sana mpaka mtu akashiba mno.



8-Kutokujitaabisha sana mchana khasa kwa mambo ya kidunia.



9-Usiache 'Qaylulah' (kulala kidogo mchana) kwa sababu ni Sunnah na inamsaidia mtu kumpa nguvu za kuamka usiku.



10-Kutokutenda maasi kwani yanamzuia mtu kutotimiza ‘ibaadah vizuri.



11-Kuutakasa moyo kutokana na maradhi ya moyo; uhasidi, chuki, uadui, ghiybah (kusengenya), an-namiymah (kufitinisha) na kila maovu.



12-Kutafakari mauti na kutokuwa na matumaini ya umri mrefu
 
UJUMBE KWA WATOA NASAHA NA WALINGANIZI

Amesema Sheikh Al-baaniy Allah amrehem :
الحق ثقيل، فلا تثقلوه أكثر
بسوء أخلاقكم
Haki ni nzito , basi musiipe uzito zaidi kwa ubaya wa tabia zenu
كنت أعتقد أن المشكلة في الأمة مشكلة عقيدة وتبين لي أنها عقيدة و أخلاق"
Nilikua nikiitakidi kuwa itikadi sahiih ndio tatizo la umma na nimebainika kuwa ni itikadi sahiih na tabia

سلسلة الهدى و النور الشريط ۹۰۰

Nimesema :

Tunaelezwa katika mambo yaliopeleka watu kuingia katika Uislam ni tabia za Mtume swallah Allah alaihi wasalam na maswahaba zake na sehem kubwa ya dini yetu imehimizwa tabia njema

Hata katika quraan aya zilizohimiza ibada na zilizohimiza Tabia njema na kukemea tabia mbaya ni nyingi zaidi kuliko za ibada

Wote tunayo haki ya kujipamba na tabia njema lakini kwa walioshika nafasi za kutoa nasaha na kulingania wana haki zaidi ya kujipamba na tabia njema kwakua kwa mienendo yao hunasibishwa dini pia , basi wasiifanye dini kuwa na ugumu zaidi

Abu fat'hiyyah khamis kiza
 
Back
Top Bottom