
RAMADHWAAN NI MWEZI WA DU'AA.
ALLAAH (Subhaanahu wa Ta’aalaa) ANATAJA KUHUSU KUOMBA DU AA BAADA YA KUTUFARIDHISHA SWAWM:
وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ ۖ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴿١٨٦﴾
186. Na watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu (kwa ujuzi); Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi, wapate kuongoka. [Al-Baqarah:186]
Zinaendelea Aayah za kuhusu Swawm baada yake.

. -KUOMBA MAGHFIRAH NA TAWBAH:
Omba maghfira na tawbah kabla ya alfajiri. Kufanya hivi utakuwa miongoni mwa waja wema Anaowasifu Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
وَبِالأَ سْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ
Na kabla ya Alfajiri wakiomba maghfirah [Adh-Dhaariyaat: 18]
Vile vile Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Huteremka nyakati hizo kuweko katika mbingu ya kwanza:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ يَقُولُ: مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ)) البخاري و مسلم
Imetoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Allaah Tabaaraka wa Ta’aalaa Huteremka kila siku katika mbingu ya dunia inapobakia thuluthi ya mwisho ya usiku na Husema: Nani ananiomba Nimtakabalie? Nani ana shida Nimtekelezee? Nani ananiomba maghfirah Nimghufurie?)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]

. -KUUNGA UNDUGU NA JAMAA:
Jambo muhimu kulitekeleza siku zote. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametahadharisha kwa anayekata mawasiliano na ndugu au jamaa:
((الرَّحِمُ مُعَلَّقَةٌ بِالْعَرْشِ تَقُولُ: مَنْ وَصَلَنِي وَصَلَهُ اللَّهُ، وَمَنْ قَطَعَنِي قَطَعَهُ اللَّهُ)) رواه البخاري ومسلم
((Fuko la uzazi linaning'inia katika 'Arshi linasema: “Atakayeniunga, Allaah Atamuunga, na atakayenitenga Naye Allaah Atamtenga [Atamkatia]”)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
