Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Rais Samia akihutubia wakati wa uapisho wa viongozi, akizungumzia kuhusu Wizara mpya ya Mipango na Uwekezaji ameonesha namna ya kuweza kuzitambua fursa mbalimbali na kuzifanyia kazi kama nchi ili zisipotee.
Akitolea mfano sakata la sasa la fursa ya uwekezaji kwenye bandari zetu amesema haya, nanukuu
Nataka niseme vizuri hili suala la fursa na watu wanavyozitumia. Ndugu zangu wakati sisi tunalumbana bandari yetu apewe nani, iende isiende, ikae, ivue, isivue, wenzetu kwa kuona malumbano yetu mmeona wame-jump wamekwenda kulekule, na lile jumba lililowekwa bendera ya Tanzania, limewekwa bendera ya jirani.
Sasa Tanzania tumeuza, wale jirani wamekimbilia kule kufanya nini?
Na siku ambayo Bunge letu hapa lilisema kwamba ni ruhusa bandari yetu iendeshwe na Serikali na sekta binafsi, siku ya pili wenzetu wakasema ninyi moja? Sisi zote zilizoko huku ziende private sector na wakakimbilia kwenda kule kwenda kuwahi nafasi. Kama wale wanalumbana, njooni huku.
Sasa muone jinsi fursa zinavyokuja na kukimbia haraka haraka na jinsi wengine wanavyoweza kuzitumia haraka haraka.
Nimesema tu nitoe mfano huo kuona changamoto na jinsi ya kupata fursa kuzitumia na kuzifanya zisiponyoke.