Wakili Mwabukusi: Rais Samia atusikie, Mkataba wa Bandari haulindi uhai wa Nchi yetu

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,318
24,217

WAKILI MWABUKUSI: Rais Samia atusikie, Mkataba wa Bandari haulindi uhai wa Nchi yetu

Katika mahojiano leo na wakili Mwabukusi anaangazia mambo zaidi kamati ya bunge, uwakilishi wa muswada wa mkataba bungeni na jinsi muda finyu waliopewa wabunge kuujadili ...
.

Wabunge Halima Mdee, Aida Kenani pamoja na Luhaga Mpina ambaye hakupata nafasi bungeni kuwakilisha hoja hivyo kuwakilisha maoni nje ya bunge kwa maandishi watambuliwe kwa kupewa maua yao hayo bila kumsahau dada yetu mpendwa wa taifa Mange Kimambi amesema wakili msomi Boniface Mwabukusi

Aliyevujisha mkataba ni mzalendo halisi na hii inatia moyo kuwa bado kuna Wazalendo wachache ndani ya serikali... na huyu atambuliwe wajibu wake mkubwa kulinda maslahi ya taifa

Serikali inawajibika kwetu umma yaani wananchi hivyo viongozi wote serikalini watambue mamlaka zote tulizowapa ni zili zilizotamkwa katika katiba kama hawawezi waache nyadhifa zao waende nyumbani ...

Advocacy tunayofanya ni kazi ya kuelimisha wananchi na ndiyo wajibu wetu kwani waziri Mbawara katika hadhira tofauti tofauti anasema mkataba huu ni makubaliano na akifika mbele ya viongozi wa dini n.k wanasema mkataba ...

Viongozi waache propaganda kwa kwenda sehemu mbalimbali Tanzania kupotosha wananchi kuwa marekebisho yatafanywa... hata wakienda mpaka kilele cha mlima Kilimanjaro haitasaidia kuzimisha kelele za wananchi ...

Linalotakiwa ni bunge hili hili lirudi haraka ili kwa kikao cha kingine liupitie tena maana ni hitajito la kikatiba wakati kunapotokea hali kama hii tunayoiona badala ya kujaribu kuutetea mkataba huu mbovu ...

Bunge halina uwezo wa kuita watu kuwahoji hata pale walipowatisha kwa kuwaita kina Paschal Mayalla, Dr. Reginald Mengi na wengine ni batili. Kwa bunge haliwezi kuwa prosecutor na mahakama

Kumtishia balozi Dr. Wilbrod Peter Slaa ambaye ni Whistle blower bona-fide kuwa aitwe bungeni ahojiwe kuhusu press conference zake za kuhusu sakata la DP World, hili ni kinyume cha katiba na batili maana bunge halina mamlaka hayo....

Hata mimi Boniface Mwabukusi nikiitwa Dodoma siwezi kutishwa na sitakwenda maana ni wito batili na haramu wala kukidhi sheria na katiba yetu kwa kuwa bunge halina mamlaka hayo

Mikataba ya kunyonya Mali ya asili yetu haikubaliki ni mikataba pekee ambayo ina manufaa kwa taifa na muwekezaji ndiyo tunayoiafiki siyo mkataba mbovu kama huu ...

Tunawashukuru wananchi kwa kupaza sauti katika suala hili ..... maana sasa Bunge halitaweza tena kututia vitanzi kama hivi vya DP World, Loliondo, Madini n.k bila wananchi kuhusishwa kimamilifu na siyo kuburuzwa ....

Kuna masharti yasiyo general policy ndani ya mkataba .... reciprocacy hakuna, huu mkataba una mlinda mwekezaji badala ya kumpa haki ya kudai fidia pale anapodhulumiwa...

High level consultation kwa kutumia katiba yetu Ibara ya 27.1 ya raia kuwa na haki ya kulinda Mali inafanyika na si muda mrefu waTanzania watapewa mrejesho na watafahamishwa

Ibara ya 28 ya katiba hairuhusu mtu yeyote kumilikishwa eneo lolote bali inaruhusiwa kutumika kwa shughuli hivyo mwekezaji hatakiwi kumilikishwa bali kuendesha shughuli za kibiashara ...

Bungeni kulikuwa na tukio na siyo mjadala maana hakuna mwanasheria mkuu hakuoneshwa siku hiyo na mwanasheria mkuu ana kiti chake maalum bungeni lakini hakuwepo na badala yake spika wa bunge kuliteka bunge kinyume na uendeshaji wa bunge huku akiwadhalilisha, kuwa harass wabunge Halima Mdee, Aida Kenani na kulibadilisha bunge kuwa kama darasa la chekechea / kindergarten la a,e,i,o,u huku dhihaka za kutunzana noti, miluzi, kugonga meza kiasi cha bunge kuwa eneo mithili ya ngoma ya mchiriku wakati jambo muhimu la eneo la nchi linamilikishwa kwa taifa lingine geni milele

Ya fuatayo yarekebishwe katika mkataba huu wa DP World katika yafuatayo : Sheria za nchi zizingatiwe masuala ya umilikaji ardhi, umilikaji wa bandari, uvunjwaji wa mikataba, tusikatazwe kutwaa eneo pale usalama wa taifa unapotishiwa tofauti na mkataba huu unavyotukataza kitu ambacho ni kinyume na katiba, spika aache kuligeuza bunge kuwa kikaragosi cha serikali, maandamano yaratibiwe maana katiba inaruhusu

Ushauri kwa Mh. Samia Hassan, ni kuwa mimi nina mashaka rais amepotoshwa maana hata wataalamu kama mwanasheria mkuu hakuonekana ndani ya televisheni siku ya tarehe 10 June 2023 jumamosi mjini Dodoma. Pia namshauri mchakato wa haraka ufanyike Serikali iurudishe mkataba huu tena bungeni na utaratibu wote utumike kikamilifu na uwazi mkubwa kusuka upya mkataba huu tata.

Freeman A. Mbowe ameeleweka na watu wenye uwezo wa kufikiri ila kuna watu wanataka kupotosha ujumbe mzuri aliowakilisha

Ni nchi mbili tu yaani Palestina kule mashariki ya kati na Tanganyika hapa Afrika Mashariki nchi zao zimepotezwa .....

Rais amwelekeze waziri aliyemkasimisha madaraka (Delegata potestas non potest delegari) kujiuzulu maana alimuamini waziri hakutumia imani hiyo vizuri lakini sasa amemuingiza katika matatizi makubwa na pia mkataba huu urejeshwe bungeni tena maana paka akifungiwa chumbani katika kona paka huyu huweza kujigeuza Simba... pia Spika Tulia Ackson ajiuzuli nafasi yake mara moja ya uspika kwa kushindwa kulipa bunge na wabunge nafasi ya kuishauri serikali kwa uwazi hilo linawezekana maana Job Ndugai alijiuzulu kufuatia utata ... na kadhia hii ya bandari ni moto kuliko ya Job Ndugai spika aliyepita ..

Wazee wa taifa wajitokeze haraka kumshauri rais kwa heshima kuwa kuwa wajisahihishe kuurejesha mkataba huu tena bungeni ....

Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
 
Jambo la kumshukuru sana Mungu, kila mtanganyika mwenye kuitakia mema Tanganyika yake tunaongea lugha moja.

Ajabu sana, watanganyika waliotakiwa kutoa maoni yao kuhusu hili suala walitakiwa kufika Dodoma tarehe 5, ili kufikia tarehe 6 saa 7 mchana wawe tayari kwa kutoa maoni.

Wakili anashangaa, inawezekana vipi kwa mtanganyika anayeishi Kigoma, Sumbawanga, Kagera, Ukerewe, Arusha na kwingineko wote wafike Dsm kutoa maoni yao siku inayofuata?

Watu wameitwa kuja kutoa maoni, ajabu mkataba wenyewe haujawekwa wazi, mtu anatakiwa kutoa maoni akiwa anajua nini anachozungumza, baada ya kupata muda wa kutosha kuuchambua mkataba, sasa unapowaficha mkataba, unataka wakazungumze kitu gani?!

Wakili anazidi kushangaa, kumbe bunge lilishaandaa Azimio la kupitisha mkataba, kabla hata bunge halijapitisha ule mkataba! huu ni ushetani kabisa.

Wakili anaendelea kusema, bunge badala ya kumshukuru Dr. Slaa kwa kuwa whistleblower, wao wanataka kumuita ili wamhoji, anadai bunge ni kinyago chetu tulichokichonga wenyewe, hakiwezi kututisha, zaidi anadai, yeye wakili akiitwa na bunge kutokana na haya maoni yake, hatakwenda. Cc Pascal Mayalla

Anadai bunge haliwezi kuwa mkamataji, muendesha mashtaka, na hakimu at the same time!.

Ana madini mengi sana.
 
PROFESA TIBAIJUKA ASTUKA NA KUFADHAISHWA NA UWEZO WA KUFIKIRI WA 'WANAWE' WAANDISHI VIJANA

Prof. Tibaijuka ashangaa maswali na hoja za waandishi wa habari katika sakata hili la mkataba wa DP World

Ni pale mwandishi alipouliza kuna tabu gani Kuwapa taarifa Dubai kila wakati wakati (Kifungu 4.2 cha mkataba) tunataka kufanya masuala ya sovereignty... profesa anashangaa waTanzania kutojipenda na kukubali kudharauliwa kutokana na maneno yalivyosukwa katika mambo makubwa na waandishi wanayachukulia kimasihara ... kuwa kuitwa kujieleza mbele ya Dubai ni suala la kishikaji / partnership wakati mkataba huu haupo hivyo Tanzania haina usemi katika mkataba huu mbovu ...

IBARA YA 4
SCOPE YA USHIRIKIANO NA UTEKELEZAJI WA VYOMBO

Upeo wa Mkataba huu ni kuwezesha utekelezaji wa maeneo ya ushirikiano yaliyowekwa katika Kiambatisho cha 1 kwa Mkataba huu.

Tanzania itajulisha Dubai fursa nyingine yoyote inayohusiana na bandari, maeneo huru na sekta za vifaa nchini Tanzania kuruhusu vyombo vya Dubai au Dubai kuelezea maslahi na kuwasilisha mapendekezo ya kuzingatiwa kwa heshima ya fursa zingine kama hizo....

N.B Ni tasfsiri isiyobeba legal language kikamilifu. Mkataba wa katika lugha ya Kiingereza ndiyo umebeba maana halisi kisheria. Tafsiri hii ya kiswahili imetiwa kusaidi kiduchu kuelewa yaliyo ktk mkataba na wajibu wa Tanzania ili mwananchi apate kapicha kadogo jinsi nchi ilivyobanwa
 
WAKILI MWABUKUSI: Rais Samia atusikie, Mkataba wa Bandari haulindi uhai wa Nchi yetu

Katika mahojiano leo na wakili Mwabukusi anaangazia mambo zaidi kamati ya bunge, uwakilishi wa muswada wa mkataba bungeni na jinsi muda finyu waliopewa wabunge kuujadili ...
.

Wabunge Halima Mdee, Aida Kenani pamoja na Luhanga Mpina aliyewakilisha maoni nje ya bunge kwa maandishi watambuliwe kwa kupewa maua yao hayo bila kumsahau dada yetu wa taifa amesema wakili msomi Boniface Mwabukusi

Aliyevujisha mkataba ni mzalendo halisi na hii inatia moyo kuwa bado kuna Wazalendo wachache ndani ya serikali... na huyu atambuliwe wajibu wake mkubwa kulinda maslahi ya taifa

Serikali inawajibika kwetu umma yaani wananchi hivyo viongozi wote serikalini watambue mamlaka zote tulizowapa ni zili zilizotamkwa katika katiba kama hawawezi waache nyadhifa zao waende nyumbani ...

Advocacy tunayofanya ni kazi ya kuelimisha wananchi na ndiyo wajibu wetu kwani waziri Mbawara katika hadhira tofauti tofauti anasema mkataba huu ni makubaliano na akifika mbele ya viongozi wa dini n.k wanasema mkataba ...

Viongozi waache propaganda kwa kwenda sehemu mbalimbali Tanzania kupotosha wananchi kuwa marekebisho yatafanywa... hata wakienda mpaka kilele cha mlima Kilimanjaro haitasaidia kuzimisha kelele za wananchi ...

Linalotakiwa ni bunge hili hili lirudi haraka ili kwa kikao cha kingine liupitie tena maana ni hitajito la kikatiba wakati kunapotokea hali kama hii tunayoiona badala ya kujaribu kuutetea mkataba huu mbovu ...

Bunge halina uwezo wa kuita watu kuwahoji hata pale walipowatisha kwa kuwaita kina Paschal Mayalla, Dr. Reginald Mengi na wengine ni batili. Kwa bunge haliwezi kuwa prosecutor na mahakama

Kumtishia balozi Dr. Wilbrod Slaa ambaye ni Whistle blower bona-fide kuwa aitwe bungeni ahojiwe ni kinyume cha katiba na batili maana bunge halina mamlaka hayo....

Hata mimi Boniface Mwabukusi nikiitwa Dodoma siwezi kutishwa na sitakwenda maana ni wito batili na haramu wala kukidhi sheria na katiba yetu kwa kuwa bunge halina mamlaka hayo

Mikataba ya kunyonya Mali ya asili yetu haikubaliki ni mikataba pekee ambayo ina manufaa kwa taifa na muwekezaji ndiyo tunayoiafiki siyo mkataba mbovu kama huu ...

Tunawashukuru wananchi kwa kupaza sauti katika suala hili .....

Inafurahisha.
 
Wabunge Halima Mdee, Aida Kenani pamoja na Luhanga Mpina aliyewakilusha maoni nje ya bunge watambuliwe kwa kupewa maua yao
Leo, muda mfupi uliopita, Msigwa (Msemaji wa Serikali) Radio One allikuwa akieleza kuhusu mkataba wa ushirikiano na Dubai. Muda mwingi ametumia kusifu matarajio ya mapato badala ya ukakasi wa mkataba wenyewe. Nilijaribu kupiga simu kumwuliza swali ambalo hadi sasa sijapata jibu.

Wenye jibu wanijibu swali langu lifuatalo.

Kwa nini DPW haiingii ubia na TPA au kupitia TIC kuwekeza bandarini badala yake inatumia mgongo wa nchi yake?
 
WAKILI MWABUKUSI: Rais Samia atusikie, Mkataba wa Bandari haulindi uhai wa Nchi yetu

Katika mahojiano leo na wakili Mwabukusi anaangazia mambo zaidi kamati ya bunge, uwakilishi wa muswada wa mkataba bungeni na jinsi muda finyu waliopewa wabunge kuujadili ...
.

Wabunge Halima Mdee, Aida Kenani pamoja na Luhanga Mpina aliyewakilisha maoni nje ya bunge kwa maandishi watambuliwe kwa kupewa maua yao hayo bila kumsahau dada yetu wa taifa amesema wakili msomi Boniface Mwabukusi

Aliyevujisha mkataba ni mzalendo halisi na hii inatia moyo kuwa bado kuna Wazalendo wachache ndani ya serikali... na huyu atambuliwe wajibu wake mkubwa kulinda maslahi ya taifa

Serikali inawajibika kwetu umma yaani wananchi hivyo viongozi wote serikalini watambue mamlaka zote tulizowapa ni zili zilizotamkwa katika katiba kama hawawezi waache nyadhifa zao waende nyumbani ...

Advocacy tunayofanya ni kazi ya kuelimisha wananchi na ndiyo wajibu wetu kwani waziri Mbawara katika hadhira tofauti tofauti anasema mkataba huu ni makubaliano na akifika mbele ya viongozi wa dini n.k wanasema mkataba ...

Viongozi waache propaganda kwa kwenda sehemu mbalimbali Tanzania kupotosha wananchi kuwa marekebisho yatafanywa... hata wakienda mpaka kilele cha mlima Kilimanjaro haitasaidia kuzimisha kelele za wananchi ...

Linalotakiwa ni bunge hili hili lirudi haraka ili kwa kikao cha kingine liupitie tena maana ni hitajito la kikatiba wakati kunapotokea hali kama hii tunayoiona badala ya kujaribu kuutetea mkataba huu mbovu ...

Bunge halina uwezo wa kuita watu kuwahoji hata pale walipowatisha kwa kuwaita kina Paschal Mayalla, Dr. Reginald Mengi na wengine ni batili. Kwa bunge haliwezi kuwa prosecutor na mahakama

Kumtishia balozi Dr. Wilbrod Slaa ambaye ni Whistle blower bona-fide kuwa aitwe bungeni ahojiwe ni kinyume cha katiba na batili maana bunge halina mamlaka hayo....

Hata mimi Boniface Mwabukusi nikiitwa Dodoma siwezi kutishwa na sitakwenda maana ni wito batili na haramu wala kukidhi sheria na katiba yetu kwa kuwa bunge halina mamlaka hayo

Mikataba ya kunyonya Mali ya asili yetu haikubaliki ni mikataba pekee ambayo ina manufaa kwa taifa na muwekezaji ndiyo tunayoiafiki siyo mkataba mbovu kama huu ...

Tunawashukuru wananchi kwa kupaza sauti katika suala hili .....

Acheni kelele Mama aifungue Nchi, mnataka mubaki na bandari yenu mukipiga hela kila ripoti inayokuja wakati wanaoumia ni wananchi?

Maraisi kutoka Tanganyika wameongoza JMT wa Tanzania miaka 60 wameshindwa kufanya namna kumsaidia mtanzania na mifumuko ya bei za vyakula na kuondoa mdororo wa uchumi sasa amekuja Mama ameona kuna namna ya kufanya kuifungua Tanzania mnaleta vimaneno uchwara.

Nyi si muliwatukana sana waarabu na waislamu sasa ndio wanakuja kukufungulieni nchi yenu mupate ajira, bandari ya Dar es salaam itakuwa buzzy saa 24 watu watakuwa wanapiga kazi kuingizia nchi mapato mbali na majengo marefu zaidi ya kibiashara na ya kisasa hapo bandarini ambayo Dp world watakujengeeni kubadilisha sura ya nchi yenu sio hiyo bandari ya takataka na iliyokubuhu kwa uchafu.

Duniani hivyo ndivyo watu wanavyoishi, Mama anajua sana ni wakupongezwa kila saa na dakika.
 
Jambo la kumshukuru sana Mungu, kila mtanganyika mwenye kuitakia mema Tanganyika yake tunaongea lugha moja.

Ajabu sana, watanganyika waliotakiwa kutoa maoni yao kuhusu hili suala walitakiwa kufika Dodoma tarehe 5, ili kufikia tarehe 6 saa 7 mchana wawe tayari kwa kutoa maoni.

Wakili anashangaa, inawezekana vipi kwa mtanganyika anayeishi Kigoma, Sumbawanga, Kagera, Ukerewe, Arusha na kwingineko wote wafike Dsm kutoa maoni yao siku inayofuata?

Watu wameitwa kuja kutoa maoni, ajabu mkataba wenyewe haujawekwa wazi, mtu anatakiwa kutoa maoni akiwa anajua nini anachozungumza, baada ya kupata muda wa kutosha kuuchambua mkataba, sasa unapowaficha mkataba, unataka wakazungumze kitu gani?!

Wakili anazidi kushangaa, kumbe bunge lilishaandaa Azimio la kupitisha mkataba, kabla hata bunge halijapitisha ule mkataba! huu ni ushetani kabisa.

Wakili anaendelea kusema, bunge badala ya kumshukuru Dr. Slaa kwa kuwa whistleblower, wao wanataka kumuita ili wamhoji, anadai bunge ni kinyago chetu tulichokichonga wenyewe, hakiwezi kututisha, zaidi anadai, yeye wakili akiitwa na bunge kutokana na haya maoni yake, hatakwenda.

Anadai bunge haliwezi kuwa mkamataji, muendesha mashtaka, na hakimu at the same time!.

Ana madini mengi sana.
Mama naona kama ana kiburi,mbona kanyamaza kimya kama hayamuhusu vile, kwanini Mkuu wa nchi unanyamaza kimya kwenye suala nyeti kama hili na wakati kwenye nyaraka saini yake ipo?hii inamaanisha nini jamani!
Mzee Mkapa aliposhutumiwa na sera yake ya ubinafsishaji mashirika ya Umma na migodi,alitokeza kufafanua na Mzee Kikwete vilevile kwenye sakata la Richmond na IPTL Escrow Account alitoa ufafanuzi.
Kulikoni Rais Samia?
Kimbukeni ata sakata la mgomo Kariakoo,napo alikaa kimya kama hayupo na alimuhusu!
 
Acheni kelele Mama aifungue Nchi, mnataka mubaki na bandari yenu mukipiga hela kila ripoti inayokuja wakati wanaoumia ni wananchi?

Maraisi kutoka Tanganyika wameongoza JMT wa Tanzania miaka 60 wameshindwa kufanya namna kumsaidia mtanzania na mifumuko ya bei za vyakula na kuondoa mdororo wa uchumi sasa amekuja Mama ameona kuna namna ya kufanya kuifungua Tanzania mnaleta vimaneno uchwara.

Nyi si muliwatukana sana waarabu na waislamu sasa ndio wanakuja kukufungulieni nchi yenu mupate ajira, bandari ya Dar es salaam itakuwa buzzy saa 24 watu watakuwa wanapiga kazi kuingizia nchi mapato mbali na majengo marefu zaidi ya kibiashara na ya kisasa hapo bandarini ambayo Dp world watakujengeeni kubadilisha sura ya nchi yenu sio hiyo bandari ya takataka na iliyokubuhu kwa uchafu.

Duniani hivyo ndivyo watu wanavyoishi, Mama anajua sana ni wakupongezwa kila saa na dakika.
Wahi Mirembe Hospital kwa Uchunguzi wa Afya ya akili!
 
Delegata potestas non potest delegari

Mwabukusi waziri Profesa Mbarawa Mnyaa Makame alijitwisha majukumu zaidi ya yale aliyopewa na Mh. Rais Samia Suluhu Hassan anasema wakili msomi Boniface Mwabukusi hivyo hakuna namna lazima Profesa Mbarawa ajiuzulu kwa kukela fedheha kwa mkubwa wake

TOKA MAKTABA :

4 March 2019

KAZI ZA MKUU WA NCHI NI TOFAUTI NA ZA MKUU WA SERIKALI

Profesa Palamagamba Kabudi ameelezea kuwa kamwe akipewa jukumu na rais hawezi kwenda zaidi ya vile rais alivyomuamini Delegata potestas non potest delegari kwani kuna sheria moja inayosema madaraka yatumie vizuri usijifanye rais au kumpotosha boss wako

Prof. Palamagamba Kabudi ataja kazi za mkuu wa nchi ambazo haziwezi kukasimiwa kabisa yaani Delegatus non potest delegare.” kwa kilatini .....

Back
Top Bottom