Shura ya Maimamu yataka Mkataba wa Bandari Uboreshwe na haki itendeke kwa Makumi ya Masheikh walioko Jela nchi nzima

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,139
50,117
Bismillahir Rahmanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA
BARAZA LA IDD ADH-HA, ALKHAMISI TAREHE 29.06.2023 -1444.
“HAKI NA UKWELI VITHAMINIWE”

FALSAFA YA IBADA YA HIJJA
Awali ya yote tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema kwa kutupa fadhila nyingi. Tunamuomba Azidi kuturehemu kwa namna mbalimbali.

Aidha kwa furaha kubwa tunawapongeza Waislamu waliojipanga wakajitahidi wakaenda katika mji mtakatifu wa Makka kufanya ibada ya Hijja mwaka huu.

Juzi walikua Arafa mahala ambapo huwakutanisha mamilioni ya Waislamu kutoka kila kona ya dunia.

Dunia imejifunza kwa kuakisi mkutano kama huo mjini New Yorke Marekani ambapo mataifa mbalimbali hukuta katika kikao cha Umoja wa Mataifa UN.

Jana walichinja wanya katika kitongoji cha Jamarat kwa lengo la kushukuru na kuwafariji maskini kwa chakula chenye thamani siku ya sikukuu.

Mafundisho ya Hijja ni mengi mno na yenye faida kubwa katika maisha ya mwanadamu.

Mwisho tunajipongeza Watanzania tuliopo hapa nchini ambao tuliungana na wenzetu siku walipokutana Arafa na siku walipochinja kwaajili ya kuwafariji watu wenye kipato kidogo na maskini kabisa.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe maisha yalio bora hapa duniani na kesho akhera.

HAKI ZA BINADAMU TANZANIA
Hili ni tatizo kubwa linalo wakabili raia hasa Waislamu nchini Tanzania. Waislamu wamekuwa wakikandamizwa kama Waislamu kiasi cha kutungwa sheria zinazoashiria kuwahukumu kabla kutenda kosa.

Kwa sheria hizo hasa ile inayoitwa ya kupambana na ugaidi, wamekua wakiwekwa jela miaka mingi bila ya kuhukumiwa na wengine wakihukumiwa na kufungwa jela mpaka miaka 50. Hivi jana mjini Morogoro Waislamu 21, wamehukumiwa miaka 15, 20 na 30, baada ya kukaa jela kwa zaidi ya miaka 10.

Wengine 10, huko mkoani Tanga wamehukumiwa kunyongwa mpaka kufa.

Baadhi ya wale walioko katika gereza la Arusha wamekatwa viungo na vyombo vya dola na wengine wamepoteza maisha wakiwa mikononi mwa vyombo hivyo.

Tufupishe kwa kusema Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayopoteza sifa ya utu na haki kwa raia wake.

UCHUMI TANZANIA
Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961. Katika hatua za kuasisi misingi ya uchumi wake moja ilikuwa ni kutaifisha asasi zote kuu za uchumi za sekta binafsi na kuzifanya mali ya serikali.

Viwanda, Mashirika ya Uchumi, Mashamba makubwa na miradi mingine vikamilikiwa na serikali.

Asasi hizo ambazo zilikuwa zikiingiza mapato makubwa kwa wenyewe, vilevile zikichangia pato la serikali na kutoa huduma mbalimbali za kutosheleza mahitaji ya jamii, zilitarajiwa kuendelea na hali hiyo chini ya mmiliki mpya serikali.

Hata hivyo mashirika hayo baada ya kumilikiwa na serikali yalipoteza uwezo wa mapato, huduma bora, na kuwa tegemezi kwa serikali. Mashirika mapya yaliyoanzishwa na serikali nayo hayakuweza kutoa faida na wala huduma stahiki kwa umma.

Yapo mashirika mengi kama vile MUTEX (kiwanda cha nguo cha Musoma), toka yalipoundwa mpaka yalipokufa au kutoka mikononi mwa serikali (kwa zaidi ya miaka 20), hayakuingiza senti hata moja ya faida katika kapu lao wala kutoa gawio kwa serikali. Huduma kwa jamii pia ilikuwa sawa na hakuna.

Taarifa za ukaguzi wa hesabu za mashirika ya umma za Tanzania Audit Corporation, zilionesha ni takriban mashirika 10 tu, kati ya zaidi ya 400, ndio yaliyokuwa na ahweni kidogo na yaliosalia yalikuwa yakiendeshwa kwa hasara kubwa. Kwa muda wote huo serikali ilikuwa ikiyapa fedha (ruzuku), mashirika hayo kila mwaka na yao yakizalisha hasara.

Baadhi ya mashirika hayo likiwemo la chama tawala CCM (SUKITA), serikali iliyadhamini kwa kupewa mikopo ya mashirika ya fedha ya kimataifa na hatimaye madeni hayo yalibebwa na serikali baada ya mashirika hayo kushindwa kuyalipa. Mashirika hayo yalishindwa kurejesha gharama zao na kuingiza faida kwao na kutoa gawio kwa serikali.

Katika miaka ya 1980, mpaka 85, taarifa za viwanda, mashirika na kampuni mbalimbali za serikali kufungwa na mamia ya wafanyakazi kupewa likizo bila ya malipo, zilisikika kila kukicha Tanzania. Hata viwanda na kampuni ambazo zilikuwa hazina mpinzani wa kibiashara hazikufanya vizuri badala yake ziliingiza hasara kubwa na hatimaye kufa kabisa. Moja ya vinda hivyo ni kile cha kutengeneza matairi ya gari (General Tire). Si kwamba havikuingiza pato kwa serikali bali pia vilishindwa kutoa huduma inayoeleweka.

Aidha wakati Watanzania wakiendelea kung’ang’ania kuendesha mashirika hayo kwa hasara chini ya mfumo wa “mali yetu tuendeshe wenyewe”, mataifa ya jirani kama Kenya yalikua na mashirika kama hayo. Mashirika yao yalikuwa yakiendeshwa na sekta binafsi (kama Tanganyika ya zamani), na yalikua yakitoa faida kubwa kwa wamiliki wake, yakilipa kodi ya kutosha kwa serikali na huduma bora kwa umma.

Wakati Tanzania madukani hamna chochote zaidi ya chumvi, waya za kusugulia masufuria, majani ya chai na unga wa mhogo wenye wadudu, Kenya bidhaa zote zilikuwa zimefurika madukani na mahitaji yote ya kibinadamu kwa ujumla yalipatikana.

Tabia ya Watanzania ya kung’ang’ania kumiliki au kuendesha jambo hata kama hawaliwezi, halina faida kwao, linawaumiza, ilijengwa wakati huo.

Katika mjadala uliopo wa tuwape Kampuni ya DP World ya Dubai waendeshe Bandari ya Dar es Salaam au tusiwape, yupo kiongezi wa dini amesema tusiwape bali tuwajengee uwezo watu wetu. Bilashaka historia fupi ya uchumi wa Tanzania tuliyoitoa hapo nyuma inaweza kutusaidi katika hoja hiyo.

SERA YA UWEKEZAJI
Serikali ya awamu ya pili ilipoingia madarakani ilijaribu kufufua baadhi ya mashirika hayo lakini mafanikiao yalikuwa hafifu. Shirika la fedha duniani IMF, lilishauri serikali kutoyapa fedha (ruzuku) mashirika hayo kwa sababu hayana faida kwa taifa na hayakopesheki.

Katika muktadha huo serikali ilifanya marekebisho ya baadhi ya sheria na kutunga sheria ya ubinafsishaji inayokwenda pamoja na uwekezaji.

Serikali ya awamu ya tatu ilipoingia madarakani ilitekeleza sera hiyo mpya kwa kubinafsisha mashirika, viwanda, mabenki, mashamba, majumba, na migodi. (Haikuwa jambo la kujivunia lakini lipi bora kati ya uzalendo wa maendeleo na uzalendo wa kujiletea umaskini. Tunakiri pia katika utekelezaji kulikua na umakini mdogo na kasoro kadhaa).

Moja ya mashirika yaliyobinafsishwa ni Kiwanda cha Sukari Moshi TPC. Kiwanda hiki kama vingine kilikuwa kinaendeshwa kwa hasara kubwa kama tulivyosema huko nyuma. Wakati wa awamu ya tatu kikabinafsishwa kwa kuwapa wawekezaji Kampuni ya Wazungu ya ALTEO kutoka Mauritius. Wazungu hawa wamepewa hisa ya asilimia 75 na serikali imebaki na asilimia 25 tu. Faida yake leo hii tunaiona tunapata takriban shilingi bilioni 25, kwa mwaka na ajira zimeongezeka.

Mifano ipo mingi tutosheke na kwamba nchi yetu ina sera ya uwekezaji na wageni wamepewa miradi mikubwa mikubwa ikiwemo migodi ya dhahabu, almasi na mingine kama hiyo.

Aidha yale wanayoyafanya tunayaona kwa mfano Wazungu pale walipowekeza katika migodi yenye thamani kubwa, hawachukui madini tu balia wanachukua na vifusi vya mchanga wa ardhi hiyo na kupeleka katika mataifa yao. Ni kweli ni wajibu wetu kuzuwia kila linaloonekana kinyume na maslahi ya taifa lakini hatuwezi kusema tumewauzia nchi wazungu kwa sababu mikataba haisemi hivyo.

UWEKEZAJI BANDARINI
Tumeona hapo nyuma Tanzania ilitunga sheria na kufungua mlango kwa wawekezaji wa nje. Pia tumesema yapo mashirika mengi ya kigeni yaliyopewa dhamana ya miradi mikubwa ya kitaifa ikiwemo migodi mikubwa.

Katika muktadha huo ndio mwaka huu pamekua na mchakato wa uwekezaji katika sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam.

Baada ya serikali kukamilisha hatua zake za ndani ilipeleke mswada husika bungeni ili wawakilishi wa wananchi waujadili. Mswada huo ulikuwa na sehemu mbili kubwa. Kwanza ulitambulisha kampuni ya DP World ya Dubai kwamba ndiyo mbia anayetarajiwa kuendesha sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam. Pili ni sehemu ya rasimu ya mkataba unaotarajiwa kufungwa kati ya kampuni hiyo na serikali (Inter Government Agreement - IGA).

Wabunge wengi walijadili kwa namna tofauti lakini hatimaye wengi wao waliunga mkono makubaliano hayo ya awali (IGA). Kwa hali hiyo sehemu ya awali ya mkataba imepitishwa na bunge.

BAADA YA BUNGE KUPITISHA IGA
Wananchi walioona mjadala wa bunge waliona kama tulivyoeleza kwa ufupi hapo nyuma.

Kwa wale ambao hawakuona moja kwa moja bungeni, walipata taarifa ya jambo hilo kupitia wasemaji mbalimbaliu katika vyombo vya habari. Na hawa waliopata taarifa kwa njia hio ndio wengi zaidi.

Wasemaji hao walikua wamefanya mapitio ya mchakato wa zabuni na mkataba na hatimaye kwa uelewa wao waliona mambo kadhaa yakiwemo sita:

1. Mkataba una mapungufu ambayo hayawezi kurekebishika.

2. Mchakato wa zabuni umefanywa kwa kificho na makampuni mengine
hayakupewa fursa kama waliyopewa DP World.

3. Mchakato unatia mashaka kwa sababu baadhi ya viongozi akiwemo Rais,
Waziri wa Uchukuzi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, wanatoka upande wa pili
wa Muunga wa Tanzania (Zanzibar).

4. Mchakato huo haukuwa na nia njema kwa Tanganyika ndio maana
haukuhusisha bandari za Zanzibar wanakotoka viongozi hao.

5. Kupitia mkataba huo upo uwezekano wa bandari kutumiwa na magaidi kuingiza silaha na kuhatarisha amani ya taifa.

6. Baadhi yao walihitimisha kwa kusema kwa hali hiyo, bandari imeuzwa na wauzaji hawakua na nia njema kwa Tanganyika.

Hoja hizi zilipata nafasi kubwa katika vyombo vya habari na kupelekea baadhi ya jamii kujadili uwekezaji wa bandari ya Dar es Salaam kwa mwelekeo huo.

HALI ILIOPO SASA
Wabunge wengi wamefurahia kurejeshewa uhuru wao wa kujadili na kupitisha mambo muhimu ya taifa kwa niaba ya watu wao. Raia pia mtaani wamefurahia kutoa maoni kisha wakabaki salama.

Hata hivyo katika suala hili (mtaani) Watanzania wamekosa muundo mzuri unao wawezesha kujadili kama wamoja, kutafakari kwa kina na hatimaye kuona maslahi makubwa au hatari kwa taifa lao. Kwa upungufu huo watu wamegawika katika makundi makubwa matatu:

• Wako wanaosema mkataba wa serikali na DP World haufai kabisa uondolewe.

• Wako wanaosema mkataba huo ni mzuri upite kama ulivyo.
• Na wako wanaosema Mkataba unamapungufu yanayorekebishika.

Hiyo ndio taswira tuliyoiona katika jamii ingawa inabadilika kama tutakavyoona huko mbele.

MTAZAMO WETU
Kwa hakika hoja za Uarabu, Uislamu na Ukristo zilizotolewa katika suala hil, ni hoja binafsi ambazo hazina mashiko katika suala la uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam. Pia Uzanzibari, Utanganyika na Ugaidi ni hoja binafsi.

Mwka 1992, Serikali ya Tanzania iliingia mkataba na Kanisa uitwao, Memorandum of Understanding between Christian Council of Tanzania and Tanzania Episcopal Conference and the United Republic of Tanzania (MoU).

Kwa mujibu wa makubaliano hayo Serikali ya Tanzania inatao fedha (mabilion), kwaajili ya kuendeleza miradi mikubwa ya Afya na Elimu ya Makanisa. Ingawa fedha hizo ni za Watanzania wote lakini serikali haikuwahusisha Waislamu katika mjadala na wala haina mpango wa kufanya mkataba kama huo na raia Waislamu Tanzania. Kubwa zaidi mkataba huo ni wa milele hauna ukomo.

Pamoja na kwamba suala la MoU kati ya serikali na makanisa ni mkataba, na uwekezaji wa DP World na serikali ni mkataba, lakini abadan hatuwezi kuhusisha suala hilo na suala la Bandari. Kwa hoja au dhana tu (Interpretation), au kulinganiasha. Tukifanya hivyo tutakuwa tumeliingiza jambo mahala si pake.

Tofauti za uhakika katika suala la bandari ni tofauti za mtazamo wa kiuchumi zaidi na si vinginevyo.

Kwamfano ukisema bandari ikiendeshwa na Waarabu upo uwezekano wa magaidi kupenya itakuwa ni sawa na kusema, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam unatumika kuingiza magaidi kwa kuwa unaendeshwa na Wazungu wa “Swissport” jambo ambalo si kweli.

Aidha katika uchunguzi wetu kadiri mjadala unavyokomaa watu wanaelekea katika hatua nzuri. Hivi karibuni tumesoma waraka wa Wakili Msomi Boniface A. Mwambukusi ulio sheheni mambo mengi na katika aya za mwishoni amesema:

“Uboreshaji wa (Inter Government Agreement) IGA”.
1. Ukomo wa mawanda ya mradi na utekelezwaji wa shughuli zote zilizokubaliwa katika mradi husika.

2. Kuweka kifungu cha kuongoza uvunjaji wa Mkataba.

3. Kuondoa vifungu vinavyoashiria umilele.

4. Kuondoa vifungu ambavyo moja kwa moja au kwa matokeo yake vinaondoa
haki ya nchi ya umiliki wa rasilimali (Sovereignty), haki ya nchi kufanya ushindani na fursa ya nchi kuruhusu wawekezaji wengine katika eneo la uwekezaji wa bandari.

5. Kuhakikisha uzingatiwaji wa sheria zingine za nchi na kuhakikisha kwamba mkataba huu hauwi juu ya katiba ya nchi, sheria za ardhi na sheria zinazolinda rasilimali asili za nchi.

Mawazo ya uboresha wa mkataba kama hayo sasa yanatolewa na wengi yakiwemo yale ya kuundwa kampuni ya uendeshaji yenye umiliki wa asilimia 50-50, kati ya DP World na kampuni ya umma itakayokuwa na hisa nyingi zaidi. Mengine yanasema:

1. Suala la muda wa mkataba utakaoingiwa kwa ajili ya uwekezaji liwe wazi pamoja na vipindi vya kufanya marejeo (Contracts reviews).

2. Suala la aina ya uwekezaji liwe wazi kwamba itakuwa Concession Agreement- CA. (Yaani uwekezaji usiwe ni kukodisha bandari au kubinafsisha bali iwe Ubia). CA hii iwe na muda maalum kwa mfano miaka 25, na kila miaka 5, kuwe na mapitio ya kuona kama malengo yamefikiwa.

3. Suala la kuvunjwa kwa Mkataba pale pande mbili zikishindana liwe wazi kwenye IGA.

4. Suala la eneo lipi bandari ya Dar es Salaam litaendeshwa na kampuni binafsi na bandari zipi zitakuwa sehemu ya uwekezaji huo liwe wazi kuondoa sintofahamu ya bandari zote za Tanzania kuwa chini ya DP World.

5. Suala la “exclusivity” ya kampuni binafsi itakayoendesha bandari kwamba nchi pia iwe na “exclusivity” dhidi ya kampuni hii kuwa na mikataba na bandari shindani na Tanzania. (Yaani kama ambavyo DP World imetaka serikali isiingie makubaliano na kampuni nyingine kuendesha bandari na wao wapewe sharti wasiwekeze kwa bandari shindani za jirani ya Tanzania).

Mapendekezo haya na mengine kama haya yanawatoa watanzania katika mawazo ya mapokeo waliyo yapata katika vyombo vya habari na kuwarejesha katika mjadala wenye maslahi kwa taifa.

MAPENDEKEZO YETU
Mjadala wetu ujikite kwenye kuongeza ufanisi wa bandari yetu ili kuongeza mapato ya serikali, na fedha za kigeni.

Wachumi wanatuambia bandari pekee inaweza kulipa mishahara ya watumishi wote wa Umma na kuhudumia (kulipa), deni la taifa ikiwa itatumika ipasavyo.

Moja ya tafiti inaonesha shehena kubwa ya mzigo, ikiwemo shaba na chuma ipo katika taifa la Congo DRC. Pia mataifa jirani kama Uganda na Rwanda yana shehena kubwa.

Shehena hizo kubwa na endelevu hukusanywa katika bandari kavu iliyopo Rwanda na kusafirishwa kupitia bandari ya Daban Afrika ya Kusini (ambayo iko mbali ukilinganisha na Dar es Salaam Tanzania).

Tunaelezwa mradi wa reli ya kisasa Tatanzania (SGR), ulilenga kunufaika na shehena hiyo kubwa na endelevu kutoka mataifa hayo ya magharibi.

Wawekezaji wa Bandari Kavu ya Rwanda inayokusanya shehena hiyo ni DP World ya Dubai. Kama tulivyosema huko nyuma, mjadala wetu ujikite zaidi kwenye kuongeza ufanisi wa bandari yetu ili kuongeza mapato ya serikali na fedha za kigeni.

Tuungane na Wanzania wanaosema tuboreshe mkataba wa bandari tusonge mbele kwa maslahi ya taifa letu.

SALAM ZA IDD
1. Tunawapongeza Watanzania kwa kuwezeshwa na Mwenyezi Mungu kudiriki Sikukuu tukufu ya Idd ya kuchinja mnyama mwaka huu.

La pili tunawapongeza kwa kujitokeza kujadili na kutoa maoni yao katika jambo muhimu la mkataa wa uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam. Katika Serikali ya Awamu ya Tano wananchi hawakujitokeza kujadili na kuhoji mambo muhimu kama hivisasa. Bila shaka ni kwa hofu ya kutokewa na yale yaliyowakuta akina Ben Saanane, Sheikh Khatbu Yunus, Simon Kanguye, Athumani Ali Kisinga na wengine wengi ambao walipotezwa baada ya kuhoji mambo muhimu kuhusu utawala.

Aidha tunawapongeza kwa kubadili mwelekeo na kuanza kujadili kiuchumi zaidi suala Bandari ya Dar es Salaam na uwekezaji wake.

2. Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita katika suala hili nyeti la mkataba wake na Kampuni ya DP World ya Dubai kwa kuupeleka mkataba huo bungeni ukajadiliwa na wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi.

Katika hili ili tusirudie makosa ya nyuma, tujikumbushe jinsi katiba ya nchi ilivyovunjwa mara kadhaa na serikali kwa kuingia mikataba mikubwa na wawekezaji hasa wazungu bila kuipeleka bungeni ikajadiliwe kama sheria inavyoagiza.

Baadhi ya mikataba ambayo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya hayati Dk. John Pombe Magufuli aliyoingia na wawekezaji bila kuipeleka bungeni:

Mkataba kati ya Tanzania na Barick Gold Corporation ya Canada.

Mikataba hii ni tisa iliyofungwa kati ya Tanzania na Barick (baada ya mgogoro wa kodi kati ya Tanzania na Kampuni ya Acacia ambayo baba yake ni Barick).

Mkataba Huu ulisainiwa Januari 24, 2020 Ikulu. (Katika hatua za utekelezaji iliundwa kampuni ya pamoja ya Twiga ambayo serikali iliachiwa asilimia 16, tu ya hisa.

Hawa Barick wanaendesha migodi mikubwa ya dhahabu ya Buzwagi, North Mara na Bulyanhulu. Ni kampuni kubwa ya dhahabu duniani).

Rais Magufuli hakuona umuhimu wa mkataba huo mkubwa na nyeti kwenye rasilimali kubwa ya taifa kupelekwa kwa wawakilishi wa wananchi bungeni ukajadiliwe. (Tunaelezwa Tanzania ni nchi ya nne kwa uzalishaji wa dhahabu Afrika).

Mkataba kati ya Tanzania na ZL Nickel ya Uingereza

Mkataba huu ulisainiwa Januari 19, 2021, kati ya Tanzania na Kampuni ya ZL Nickel ili kuendeleza mradi wa madini ya Nickel kule Kabanga mkoani Kagera. (Nickel ni madini muhimu kwenye kutengeneza betri ya magari yanayotumia umeme). Kwakua mchakato wake haukupelekwa bungeni na ukafanywa kwa maslahi binafsi, ulisababisha mgogoro ulioigharim sana serikali.

Mradi huu ulikuwa chini ya makampuni mawili ya Barick (ya Canada) na Glencore (ya Uingereza), kabla ya Rais Magufuli kusitisha leseni zao na kuwapa ZL Nickel ya Uingereza.

Katika sintofahamu hiyo, ZL Nickel siku chache tu ilibadilisha jina na kuwa Kabanga Nickel ikiwa na mali za bilioni 16 tu, (sawa na dola za Marekani, milioni 8, wakati mradi umefanyiwa upembuzi yakinifu (Feasibility Study), kwa gharana kuwa ya pesa yetu Tanzania takriban dola milioni 250, (bilioni 500). Kwa hiyo ni sawa na kusema wamepewa bure, na huo pia ulikua mgogoro mkubwa.

Pamoja na ukubwa wa mradi na utata wote huo lakini mradi huo haukupelekwa bungeni kama sheria ya madini ya mwaka 2017, inavyoagiza.

Mkataba mwengine ni wa ujenzi wa bomba la mafuta kati ya Tanzania na Uganda wenye dhamana ya dola bilioni 3.55.

Mradi na mkataba huo chini ya Rais Magufuli na Rais Museveni wa Uganda, haukuwahi kupita bungeni toka mwanzo mpaka ulipokamilika.

Kwa ufupi Rais Magufuli aliingia mikataba mingi ikiwemo mikubwa ya sekta ya madini bila ya kuipeleka bungeni japo sheria ya madini ya 2017 ilimtaka aipeleke Bungeni.

Mifano hii mitatu inatosha kuonyesha ni kiasi gani bunge lilivyodharauliwa na Katiba ya Nchi kuvunjwa huko nyuma.

Ndio maana kwa hili la kulirejeshea uhai na heshma bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaipa kongole serikali kwa hilo.

3. Wananchi wamekuwa na mchango mwingi wa mapendekezo kuhusu Mkataba wa DP World na serikali. Vuguvugu lilikuwa kubwa na wengi walikuwa hawajui hatma ya mawazo yao.

Tarehe 19.06.2023, katika kongamano la kitaifa lililofanyika jijini Dar es Salaam kuhusu suala hilo, mbunge wa Jamhuri ya Muungano Profesa Kitila Mkumbo alifafanuzi kuhusu msimamo wa bunge.

Alisema bunge limejipanga kuzingatia mawazo ya wananchi katika rasimu na hatimaye mkataba halisi.

Wito wetu, tunalishauri bunge lisipuuze mawazo mapya ya wananchi, liyapokee na kuyafanyia kazi.

4. Tunawatakia Watanzania na wengine kote duniani, Sikukuu njema ya Idd ya kuchinja (Adh-ha).

AMIRI SHAABAN IBRAHIM - 0748144720
 
Bismillahir Rahmanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

shurayamaimamutanzania@gmaili.com

“HAKI NA UKWELI VITHAMINIWE

*SALAM ZA IDD
*

"Kwa mujibu wa makubaliano hayo Serikali ya Tanzania inatao fedha (mabilion), kwaajili ya kuendeleza miradi mikubwa ya Afya na Elimu ya Makanisa. Ingawa fedha hizo ni za Watanzania wote lakini serikali haikuwahusisha Waislamu katika mjadala na wala haina mpango wa kufanya mkataba kama huo na raia Waislamu Tanzania. Kubwa zaidi mkataba huo ni wa milele hauna ukomo......."
Hi nchi buana ina mambo mengi watu wana duku duku zao
 
Wito wetu, tunalishauri bunge lisipuuze mawazo mapya ya wananchi, liyapokee na kuyafanyia kazi

Bandiko lingine zuri toka kwa mojawapo wa washikadau wenye ushawishi wa kuona nchi hii kiuchumi vipi tuende vizuri bila kuathirika na mikataba mibovu inayoibana taifa letu kuendelea kuwa masikini.

LIVE : SHURA YA MAIMAMU YATOA HADHARI UWEKEZAJI WA BANDARI , SHEIKH PONDA ATOA WARAKA
 
Wanaosema uboreshwe wanapoteza tu muda, hakuna kinachoboreshwa.
 
"Kwa mujibu wa makubaliano hayo Serikali ya Tanzania inatao fedha (mabilion), kwaajili ya kuendeleza miradi mikubwa ya Afya na Elimu ya Makanisa. Ingawa fedha hizo ni za Watanzania wote lakini serikali haikuwahusisha Waislamu katika mjadala na wala haina mpango wa kufanya mkataba kama huo na raia Waislamu Tanzania. Kubwa zaidi mkataba huo ni wa milele hauna ukomo......."
Hi nchi buana ina mambo mengi watu wana duku duku zao
Wanaotibiwa kwenye hizo Hospitali ni Wakristu peke yao? Hawa jamaa wana shida vichwani.
 
"Kwa mujibu wa makubaliano hayo Serikali ya Tanzania inatao fedha (mabilion), kwaajili ya kuendeleza miradi mikubwa ya Afya na Elimu ya Makanisa. Ingawa fedha hizo ni za Watanzania wote lakini serikali haikuwahusisha Waislamu katika mjadala na wala haina mpango wa kufanya mkataba kama huo na raia Waislamu Tanzania. Kubwa zaidi mkataba huo ni wa milele hauna ukomo......."
Hi nchi buana ina mambo mengi watu wana duku duku zao
Kwenye hili la serikali kutoa ruzuku kwa hospitali zinazomilikiwa na Kanisa, mbona siyo tatizo. Ifahamike kuwa wala halikuwa ombi la Kanisa kuwa na hiyo memorandum.

Hilo lilikuja pale Serikali ilipotaka hospitali za Kanisa zitumike kama hospitali za rufaa. Kwa hiyo kwenye hospitali hizo ambazo hazikuhitaji kuwa hospitali za rufaa, zikabebeshwa mzigo wa kubeba majukumu ya Serikali.

Na haikuwa maamuzi ya Kanisa, bali wataalam wa afya ndio waliopendekeza ni hospitali zipi zimefikia viwango vya kuwa hospitali za rufaa. Na ninaamini kama kungekuwa na hospitali yoyote inayoendeshwa na BAKWATA iliyokuwa imefikia viwango vilivyokuwa vinatakiwa, ingejumuishwa.

Tena hayo yalifanyika wakati Rais akiwa muislam. Na sahizi Rais ni muislam. Kama waislam wana duku duku kwenye hili, mbona wanaweza kuivunja hizo MoU, na hospitali zikarudi kwenye mfumo wake wa zamani. Tena hapo zamani, kabla ya Serikali kujiingiza humo, huduma zilikuwa bora zaidi, na hata msongamano wa wagonjwa haukuwa mkubwa kama ulivyo sasa.
 
Waraka huu wa ndugu zetu waislam, upo vizuri kabisa.

Kwenye suala la mkataba wa bandari, wapo watu ambao wameshindwa kuzijibu hoja za msingi za ubovu wa mkataba, ndiyo wanaokimbilia kusema kuwa eti DP inapigwa vita kwa sababu ya dini au Uarabu. Wanataka kusema ni Uislam ndio unaoagiza mkataba usiwe na ukomo, na sisi uwekezaji wetu tulioufanya usitambulike?

Waislam wa kweli ndiyo hawa, siyo akina Faizafox waliojaa chuki dhidi ya binadamu wengine.
 
Similar Discussions

19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom