Freeman Mbowe: Tunazindua "Operation +255 Katiba Mpya Okoa Bandari Zetu" kuwaambia watanzania ubaya wa Mkataba wa DP World

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe atazungumza na watanzania kupitia mkutano na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni, juu ya maazimio ya Kamati Kuu ya Chama iliyoketi Julai 08, 2023 kuanzia saa 8:00 mchana huu.

Yote yanayojiri utayapata hapa.

F05xQQIWIAEpHZc.jpg


===

MKUTANO UMEANZA

Sisi ni taasisi, kama taasisi tunatoa maoni kulingana na maazimio ya wengi, tunatoa maoni ya pamoja, sio kwa utashi wa mtu mmoja mmoja.

Nikiwa Ujerumani nilitoa tamko la awali la kuonya juu ya mkataba huu. Baada ya hapo yalifata maneno mengi, mengine ya kubeza. Walioamua kufanya propaganda walisahau hoja ya msingi na kuanza kumshambulia Mbowe.

Nashukuru yote niliyozungumza, nikabezwa na kutukanwa, wenye akili walinielewa. Mkataba ule kwetu sisi ni kashfa ya taifa. Nawashukuru watanzania kwa makundi yote, wanasheria wa ndani na nje ya chama wameuchambua sana mkataba huu.

Mwenye macho haambiwi tazama, yote niliyotilia shaka yamedhihirika. Leo nitazungumza mambo 3, Kuhusu Mkataba, Maridhiano na Sakata la Ngorongoro (na hifadhi zingine za wanyama pori) lakini baada ya mashauriano tumeona tukizungumza yote tutaharibu maana yana uzito unaofanana.

Leo wengi wameongea na waandishi wa habari, tumesikia wamezungumza kwa zaidi ya masaa 8, bado tumeambiwa saivi Rais ana kikao cha uapisho. Tunawashukuru waandishi mliofika, tunatumaini taarifa zitafikia watanzania.

Ndugu zangu wana habari, ninazungumza moja kwa moja maazimio ya Kamati Kuu, wanasheria wakubwa wa nchi hii wameshajadili vifungu vyote.


===

MAAZIMIO YA KAMATI KUU
Kamati Kuu inalitaka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufutaazimio lake la kuridhia mkataba wa uendeshaji wa Bandari nchini kwasababu mkataba huo hauna maslahi yoyote kwa nchi yetu.

Kamati Kuu inaitaka Serikali kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria wote walioshiriki kuingiza nchi kwenye mkataba huu mbovu ambao haurekebishiki.

Kamati Kuu inaunga mkono jitahada mbalimbali zinachochukuliwa nawananchi mbalimbali nchini kupinga mkataba huo ikiwemo wale waliochukua hatua za kufungua kesi dhidi ya Serikali kwa ajili hiyo katika Mahakaka Kuu ya Tanzania.

Kamati Kuu imeazimia pia kwamba itashirikiana na wananchi kupitiamakundi mbalimbali bila kujali itikadi zao katika kupinga mkataba huu wauendeshaji wa Bandari nchini.

Kamati Kuu inawahimiza wananchi kwamba Mkataba wa Bandaripamoja na mikataba mingine ya siri ambayo ni mibovu na inayoliingiza taifa kwenye hasara kubwa ni chachu ya kuona haja ya kuendelea kutaka nchi yetu kuwa na Katiba Mpya ambayo itaweka utaratibu wa namna ya Bunge na vyombo vingine kupitia mikataba hiyo kwa maslahi ya Taifa.

Kamati Kuu imeazimia kwamba ikiwa Bunge na Serikali haitachukuahatua kuhusu malalamiko ya wananchi dhidi ya mkataba wa Bandari;Chama kitaanzishe na kuhamasisha umma kuchukua hatua kali dhidi yaserikali mpaka itakapousitisha mkataba huu.

Kamati Kuu imeridhika Mkataba hauna maslahi yoyote kwa nchi yetu na haukubaliki kwa CHADEMA na kwa mtu au taasisi yoyote inayoitakia nchini yetu mema. Kwa maneno ya mtaalamu maarufu wa sheria nchini kwetu, huu ni mkataba wa haki kwa upande mmoja (Dubai) na wajibu kwa upande mwingine (Tanzania).

Kamati Kuu imebaini kuwa kwa jinsi mkataba huu ulivyo, na kwa maoni ya CHADEMA na ya wataalamu mbali mbali walio huru, mkataba huuhaurekebishiki bila kuubadilisha wote, na bila makubaliano na Dubai. Chama cha Mawakili wa Tanganyika kimeonyesha katika uchambuzi wake kwamba mkataba huu unahitaji marekebisho katika vifungu vyake vyote muhimu.

Kamati Kuu imeridhika kuwa Mkataba huu ni kinyume cha Katiba ya nchi;kinyume cha sheria za nchi na kinyume cha sheria za kimataifa. Mkataba umepelekea Serikali hii ya CCM kuwasilisha muswada wa kubadilishasheria zinazohusu umiliki wa rasilimali asilia za nchi.

Kamati Kuu imebaini hakuna utafiti wowote wa kisayansi uliofanywa naserikali na ukawekwa kwa umma kuthibitisha ufanisi au uduni wa bandari zetu na ubora wa DPW ili kushawishi wananchi juu ya ufanisi utakaotokana na DPW. Kila jambo lilifanywa kisirisiri kienyeji na hakuna data zitokanazo na utafiti.

Kamati Kuu imejiridhisha kuwa Wananchi hawajui ASILI wala SHABAHA ya mkataba huu wa DPW na wao ndiyo wanaoathirika wakuu kwamaaamuzi haya ya serikali.

Kamati Kuu imebaini hakuna utafiti uliofanywa na serikali kuonyesha "faida" za kifedha wanazozungumza, wala hakuna ushahidi wa utafitiuliofanyika kuonyesha faida zisizo za kifedha zitokanazo na umiliki nauendeshaji wa bandari. Faida na hasara halisi hazipaswi kuwa za kinadharia bali ndizo zingekuwa sehemu ya vigezo vya kuamua taifa lifuate mbadala upi.

Kamati Kuu imebaini huwa hakuna utafiti wowote unaothibitisha kuwa Unyeti wa bandari kwa usalama wa taifa umezingatiwa kabla ya kuingia mkataba huu.

Kamati Kuu imejiridhisha kuwa hakuna ushahidi kwamba serikaliilifanya uchambuzi wa kiuchumi, kijamii, kisiasa au kiusalama kabla yakuamua na kusaini mkataba huu. Kama hayo yangefanyika, na yakawekwa wazi, mjadala juu ya bandari usingekuwa hivi ulivyo.

Kamati Kuu imejiridhisha pasipo shaka kuwa Serikali, Bunge nabaadaye CCM ilikurupuka na kujaribu kuficha mapungufu ya mkataba kwapropaganda na taarifa zisizo za kweli. Matokeo yake, sasa inagombana nawananchi, inawagawa wananchi, na inatumia nguvu na ushawishi haramu kuliko ushawishi wenye HOJA, UTAFITI NA USHAWISHI. Badala ya kujibu maswali, serikali inaibua maswali magumu zaidi.

Kamati Kuu imebaini mchakato wa kufikia makubaliano na DPW haukufuata kanuni za kisheria, kisiasa, kisayansi na hata kitaaluma. Na hata mfumo wa serikali kujibu HOJA za wananchi, haufuati kanuni zakisayansi na kitaaluma. Ndiyo maana unasikia wananchi wengine tayari wameanza kutishwa, makundi yanayotumika kutetea mkataba si makundi yenye dhamana wala utaalamu wa jambo husika.

Kamati Kuu imejiridhisha kuwa kwa kuwa hakuna utafiti, ushahidi walatathmini ya kina iliyofanywa na serikali juu ya jambo hili, na kwa kuwaserikali imekosa majibu yenye ushawishi kwa umma, na kwa kuwa chama tawala na serikali hawasikilizi maoni ya wananchi juu ya raslimali zao hizi, sisi Chadema kama serikali inayosubiri kuingia madarakani, tunatoa msimamo ufuatao.


===

MSIMAMO WA KAMATI KUU

Kwa sababu hizi zote na sababu nyingine nyingi, msimamo wa CHADEMA ni kwamba mkataba huu ufutwe wote. Aidha, CHADEMA itatumia njia mbali mbali, ndani na njeya nchi yetu, kuhakikisha kwamba mkataba huu unafutwa na rasilimali za nchi yetu na maslahi ya taifa letu yanalindwa.

Kamati Kuu imekubali kwa kauli moja kuwa mifumo yote ya Chama nchi nzima iongeze juhudi za kuufahamisha umma wa Watanzania, ubovu na hatari za Mkataba huu kwa nchi yetu.

Kamati Kuu sasa imeridhia Operation +255 Katiba Mpya inayoendelea nchi nzima, sasa iongezewe wajibu na kuwa Operation +255 Katiba Mpya Okoa Bandari zetu.

Kamati Kuu na Chama chetu kitaunga mkono uwekezaji wowote Mkubwa unaotokana na utafiti wa kisayansi,usiohatarisha usalama wa nchi yetu ikiwemo Utaifa wetu (sovereignity), wenye uwazi na tija kwa pande zote mbili na utakaolinda Uhuru na Haki zetu kama Taifa.

Mkataba huu unalenga kuwapa DP World umiliki wa bandari zote hadi zile za maziwa makuu ambayo Serikali haitaweza kusogeza hata tofali moja bila kibali chao.

Tunakwenda kuonana na wananchi kanda ya ziwa, kanda ya nyasa na mwambao wote wa Pwani.

Wajibu hoja wote wa Serikali hawatuambii mambo ya kitafiti, wanakazana kutuambia DPW ni kamouni kubwa, tajiri... hakuna anayekataa.

Hoja yetu watanzania na wanachadema sio Dubai, sisi tunawalaumu viongozi wetu waliotuingiza. Hoja yetu sio dubai, hoja yetu ni mkataba na hao watu, mkabata wa namna gani, mkataba huu unatudhalilisha kama taifa.

Tutaunga mkono uwekezaji wowote wenye utafiti na tija kwa taifa, usiohatarisha usalama na kutunyima hadhi yetu kama nchi.

Tunawaomba Kanda ya ziwa wajiandae kutupokea, kule tutaonesha sisi ni chama gani. Wote waliokwazika waone aibu kubeba kadi ya CCM. Tutakusanya kadi zote na vifaa vya CCM kutoka kwa wote waliokasirika na mkataba huu.

Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
 
Siku ya kwanza alisema walitumia single source kwa kuwa walikuwa wanajua uwezo wake, Leo kaja na jipya. Mkumbusheni Mbarawa asiwe msahaulifu

Saa100 kukaa kimya ni kusababisha uonekane 2025 hukubaliki.

Tokea nje ongea na watanganyika ndipo kura ziliko vinginevyo utakwenda kulima karafuu 2025.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe atazungumza na watanzania kupitia mkutano na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni, juu ya maazimio ya Kamati Kuu ya Chama iliyoketi Julai 08, 2023 kuanzia saa 8:00 mchana huu.

Yote yanayojiri utayapata hapa.

View attachment 2687669
We don't need anymore words about DPW because a lot of words are already spoken by several speakers. Now, we need actions because "Actions Speaks Louder Than Words".
 
Back
Top Bottom