Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiri Tamasha la Utamaduni la Bulabo katika uwanja wa Redcross Ngomeni Kisesa mkoani Mwanza leo tarehe 13 Juni, 2023.



Akizungumza kwenye Tamasha hilo linaloashiria Mwanzo wa mavuno, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewashukuru kwa mwaliko huo wa kujumuika na machifu wenzie, yeye akiwa chifu Mkuu (Chifu Hangaya).

Ameungana na wakulima hao kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema na baraka zake kwa kuwezesha wakulima hao kupata mavuno ya kutosha kwenye nyakati hizi mbaya za mabadiliko ya Tabianchi. Ulimwengu kwa sasa unakabiliwa na upungufu wa chakula unaoweza kusababisha mfumuko wa bei kwenye chakula na matarajio ya ulimwengu ni kuwa mfumuko huu wa bei ungekuwa 5% lakini tofauti na ilivyotarajiwa dunua inakabiliwa na mfumuko wa bei unaofikia 10% na zaidi.

IMG_7597.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akitembelea Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza

Kuhusu Kilimo, Serikali imesema ilichukua baadhi ya hatua ikiwemo kuiongeza matumizi kwenye bajeti ya Wizara hii kwenye bajeti za kila mwaka ili wananchi walime zaidi, wavune zidi na wauze zaidi. Hii ni pamoja na kufanya usajili wa wakulima ili kufahamu idadi yao, kutoa ruzuku, kuongeza thamani ya mazao, ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula na kutenga fedha nyingi kwa ajili ya skimu za umwagiliaji badala ya kutegemea msimu mmoja wa mvua.

Pia, kwenye mwaka huu wa fedha, Serikali imetoa kibali cha kununua mazao ya nyongeza ili kuongeza akiba ya chakula kutoka tani laki 2 zilizopo sasa hadi laki 5 lakini pia watu wanapaswa kutunza chakula kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Kwa mujibu wa Sensa iliyopita, Vijana ndio kundi kubwa la watu waliopo kwenye nchi hii hivyo machifu hao wanapaswa kusimamania maadili ili vijana wasiharibiwe na maisha ya kisasa.

9913d22e-ee55-4f17-ba06-af1d99f591d1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akimsikiliza Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Renatus Nkwande kuhusu Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.

5f04ed91-d23c-4b1d-be1e-a0366acdd5ec.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu na akiwa amekaa kwenye kiti cha Kifalme cha Watemi wa Kisukuma katika Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Magu Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.

ca416a92-0555-456d-9238-0a7c04eb45a4.jpg

Mtoto Goziberti Bwele wa kikundi cha Ngoma za Asili ca Utandawazi Theater Group (Matwigachallo) kutoka Ukerewe akionesha umahiri wa kupiga ngoma kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kisukuma Bulabo lililofanyika katika viwanja vya Red Cross, Ngomeni Kisesa tarehe 13 Juni, 2023.

c4a155a7-b517-4496-a296-099ee2dffe08.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpongeza mtoto Goziberti Bwele (14) wa kikundi cha Ngoma za Asili cha Utandawazi Theater Group (Matwigachallo) kutoka Ukerewe kutokana na umahiri wake wa kupiga ngoma kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kisukuma Bulabo lililofanyika katika viwanja vya Red Cross, Ngomeni Kisesa tarehe 13 Juni, 2023. Tamasha la Bulabo huleta pamoja shughuli za Utamaduni na zile za dini.
c98610a4-8060-484e-86f1-92a5df2b97cb.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Machifu wakati alipohudhuria Tamasha la Utamaduni wa Kisukuma Bulabo lililofanyika Kisesa Mkoani Mwanza tarehe 13 Juni, 2023.
 
Mradi huu ulipitishwa kwenye Bunge la bajeti la mwaka jana 2022/2023, cha ajabu hadi leo hii pesa bado hazijatufikia walengwa. Rais asiondoke Mwanza kabla ya kuhakikisha mradi huu umezinduliwa na pesa zimelipwa kwa walengwa, ni aibu serikali ya CCM kufanya biashara kupitia mradi huu na kukwamisha utekelezaji wake kwa takribani mwaka mzima sasa..
CCM iache utapeli wa tamasha la BULABO, lipeni pesa za huu mradi uanze mara moja

Mikopo Vizimba.PNG
 
Hivi ndo kusema mama hasikii kelele za wananchi kuhusu hiyo bandari kupewa hao waarabu au ni vile kazoea watalilia mwishoe watanyamaza?
 
Kumbe wapiga-kura wanapoozwa kwa njia hiyo baada ya kukasirishwa na madudu ya mkataba wa bandari?
 
Back
Top Bottom