Rais Samia azindua Vizimba na kugawa Boti za Kisasa, Eneo la Bismarck Rock Mwanza, leo Januari 30, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizindua Vizimba na kugawa Boti za Kisasa - Eneo la Bismarck Rock mkoani Mwanza, leo tarehe 30 Januari, 2024 katika ziara ya kikazi ya siku moja.

View: https://www.youtube.com/live/PbiNMKoRTzU?si=01tr_e35tIxB3CZs

View: https://www.youtube.com/watch?v=8cPBpnVq5Kg
9f20f148-7cfd-482b-a25b-47836583a007.jpg

MWa.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.
Mwaa.jpg

Baadhi ya Viongozi wa dini pamoja na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

MWA1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.

cdf3b280-2042-4cce-b77c-c683ed7e41b3.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Mwanza mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa Boti za Kisasa na vizimba kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

IMG-20240130-WA0019(1).jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kuhusu Boti za Kisasa na vizimba vya kufugia Samaki kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
IMG-20240130-WA0027.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. Wengine katika picha ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emanuel Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe pamoja na viongozi wengine.
IMG-20240130-WA0030.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi mfano wa funguo Wawakilishi wa vikundi vya Uvuvi kwa ajili ya ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
IMG-20240130-WA0018.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijiandaa kuzindua ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
IMG-20240130-WA0031.jpg
IMG-20240130-WA0028.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuzindua ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekeza jambo mara baada ya kuzindua Zoezi la ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
IMG-20240130-WA0022.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi mara baada ya kuzindua Zoezi la ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
IMG-20240130-WA0021.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kufika katika uwanja wa Nyamagana kwa ajili ya mkutano wa hadhara kuhusu ugawaji Boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
IMG-20240130-WA0024.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekeza jambo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akielezea kuhusu Samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika Ziwa Victoria mara baada ya uzinduzi wa Boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
IMG-20240130-WA0017.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akielezea kuhusu Samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika Ziwa Victoria mara baada ya uzinduzi wa boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
IMG-20240130-WA0025.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kuhusu Boti za Kisasa na vizimba vya kufugia Samaki kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
IMG-20240130-WA0015.jpg
IMG-20240130-WA0020.jpg
IMG-20240130-WA0014.jpg
IMG-20240130-WA0016.jpg
IMG-20240130-WA0013.jpg

Muonekano wa Boti za Kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua ugawaji wake kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla iliyofanyika Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. Boti na vizimba hivyo vimegaiwa kwa Wavuvi kwa mkopo usio na riba ili kuwawezesha kufanya Biashara ya Samaki kwa tija.
 
Haya majambazi yamebaki kugawa rushwa kwa kutumia kodi zetu. Rushwa juu ya Rushwa.

Utekaji kila mahali! yaani Nchi imebakia wananchi kujificha ili wasitekwe. Serikali ya kijambazi lazima iondoshwe!
 
RAIS SAMIA AIPA HEKO WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI, ARIDHISHWA NA KASI YA UTENDAJI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema serikali imedhamiria kuleta mageuzi makubwa katika Sekta ya Uvuvi, hivyo imeamua kutoa kipaumbele katika kukuza sekta hiyo kwa kuimarisha utendaji kazi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amebainisha hayo leo (30/01/2024) jijini Mwanza, wakati wa kukabidhi boti 55 na vizimba 222 kwa wanufaika kwenye Kanda ya Ziwa Victoria na kuitaka wizara kubuni mbinu zaidi za kuhakikisha inawezesha wanufaika wengi zaidi kupitia rasilimali za uvuvi.

Ameongeza kuwa kwa sasa wizara imekuwa ikifanya mambo mengi makubwa na yenye kuleta tija kwa wananchi ambapo katika Sekta ya Uvuvi wananchi wengi wamekuwa wakitegemea sekta hiyo kwa ajili ya kujipatia kipato.

Amewataka pia walionufaika wa boti za uvuvi na vizimba kuhakikisha wanatumia vyema zana hizo na kuzitunza pamoja na kuondokana na migogoro yoyote ambayo inaweza kujitokeza kwenye vikundi vyao kwa kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha mradi huo unaenda maeneo mengi zaidi hapa nchini.

Aidha, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 na 2023/2024 wizara hiyo ilipatiwa fedha Shilingi Bilioni 60 kila mwaka kwa miaka miwili mfululizo katika kukuza Sekta ya Uvuvi.

Pia Mhe. Ulega amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025 nia ya wizara ni kusambaza boti za uvuvi zisizopungua 500 kote nchini ili kuwezesha wanufaika wengi zaidi kwa kuwa Sekta ya Uvuvi inatoa ajira kwa zaidi ya watu Milioni 4.5.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw. Frank Nyabundege amesema Mwaka 2022 Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hasssan aliipatia benki hiyo Shilingi Bilioni 210 ambapo nia ya Mhe. Rais ni kuhakikisha benki hiyo inakua na kutatua changamoto mbalimbali kwa wakulima, wafugaji na wavuvi.

Amesema kupitia boti 55 zilizokabidhiwa kwa Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya shughuli za uvuvi zitanufaisha vijana zaidi ya 1,500 na kwamba mikopo ya boti na vizimba inatolewa bila riba hivyo TADB inatarajia kadri mikopo hiyo itakayovyokuwa inarudishwa itawanufaisha wengi zaidi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amesema wizara itahakikisha inaendeleza maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Sekta ya Uvuvi inazidi kutoa ajira zaidi kupitia zana mbalimbali zikiwemo boti na vizimba ambavyo amevigawa leo kwa wavuvi na wakuzaji viumbe maji kupitia mkopo usio na riba.

Prof. Shemdoe ameongeza kuwa kupitia boti na vizimba vijana watapata fursa ya kujipatia ajira pamoja na kuongezea vipato kupitia ufugaji wa samaki na kwamba kupitia mradi huo jitihada mbalimbali zitaendelea kufanywa ili kufikia wanufaika wengi zaidi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makala amesema hafla ya kukabidihi boti 55 na vizimba 222 kwa mkoa huo, utakuza uvuvi endelevu kwa kuwa amekutana na wadau wa uvuvi ambapo tafiti zinaonesha samaki ndani ya Ziwa Victoria wamepungua kwa asilimia 30 na kuathiri baadhi ya viwanda vya kuchakata minofu ya samaki, kutokana na kukithiri kwa baadhi ya matukio ya uvuvi haramu na kwamba mkoa tayari umeweka mikakati mbalimbali kudhibiti vitendo hivyo.

Mhe. Makala ameongeza kuwa kitendo cha kuwakabidhi wavuvi boti kitasaidia kukuza uvuvi endelevu na kwamba elimu imekuwa ikiendelea kutolewa kwa wakazi wa mkoa huo kufuga samaki kwa njia ya vizimba ili kukuza soko la samaki.

Nao baadhi ya wanufaika wa boti na vizimba wameshukuru kwa kupatiwa zana hizo pamoja na vifaranga vya samaki na chakula cha samaki, wameiomba serikali kuwahakikishia mbegu bora za vifaranga vya samaki pamoja na chakula ili waweze kufuga kibiashara na kukuza kipato chao na hatimaye kuweza kurejesha mikopo.

Pia wamesema wamefurahia kupatiwa boti za kisasa na zenye injini za kupachika ambazo ni imara hivyo watahakikisha wanatumia vyema boti hizo ili waweze kurejesha mikopo na kuweza kukopa kwa awamu nyingine.
IMG-20240130-WA2096.jpg
IMG-20240130-WA2110.jpg
IMG-20240130-WA2108(1).jpg
 
Sijui nimekosea naona ujinga ujinga hapa

Hivi kweli rais ni wakwenda kufanya kazi kama hiyo karne ya leo.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizindua Vizimba na kugawa Boti za Kisasa - Eneo la Bismarck Rock mkoani Mwanza, leo tarehe 30 Januari, 2024 katika ziara ya kikazi ya siku moja.

View: https://www.youtube.com/live/PbiNMKoRTzU?si=01tr_e35tIxB3CZs

View: https://www.youtube.com/watch?v=8cPBpnVq5Kg
View attachment 2888865

View attachment 2888780
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.
View attachment 2888783
Baadhi ya Viongozi wa dini pamoja na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

View attachment 2888792
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.

View attachment 2888798
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Mwanza mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa Boti za Kisasa na vizimba kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

View attachment 2888771
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kuhusu Boti za Kisasa na vizimba vya kufugia Samaki kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
View attachment 2888767
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. Wengine katika picha ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emanuel Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe pamoja na viongozi wengine.
View attachment 2888768
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi mfano wa funguo Wawakilishi wa vikundi vya Uvuvi kwa ajili ya ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
View attachment 2888656
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijiandaa kuzindua ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
View attachment 2888796View attachment 2888799
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuzindua ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekeza jambo mara baada ya kuzindua Zoezi la ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
View attachment 2888654
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi mara baada ya kuzindua Zoezi la ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
View attachment 2888660
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kufika katika uwanja wa Nyamagana kwa ajili ya mkutano wa hadhara kuhusu ugawaji Boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
View attachment 2888659
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekeza jambo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akielezea kuhusu Samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika Ziwa Victoria mara baada ya uzinduzi wa Boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
View attachment 2888658
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akielezea kuhusu Samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika Ziwa Victoria mara baada ya uzinduzi wa boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
View attachment 2888662
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kuhusu Boti za Kisasa na vizimba vya kufugia Samaki kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
View attachment 2888663View attachment 2888664View attachment 2888665View attachment 2888666View attachment 2888667
Muonekano wa Boti za Kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua ugawaji wake kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla iliyofanyika Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. Boti na vizimba hivyo vimegaiwa kwa Wavuvi kwa mkopo usio na riba ili kuwawezesha kufanya Biashara ya Samaki kwa tija.

Huu uzi una taarifa nyingi Muhimu lakini Wadau wameususia kabisa.
Umepostiwa saa tano na dakika 40 jana mpaka leo saa nane na robo usiku unawasomaji kiduchu na wachangiaji wachache mno.

Hii ina aksi hali gani? Si ndio huko mwanza Mwenezi alikuwepo?
 
Katika dua ya ufunguzi wa mkutano wa kugawa Boti huko Mwanza Shehe wa mkoa amemwomba Allah aibariki CCM kwa jinsi inavyowaletea wananchi mambo mazuri mazuri

Shehe wa mkoa pia amemwomba Allah avibariki vyama vya upinzani Ili viendelee kuwa Washauri wazuri wa CCM Chama tawala

Mh Rais Dr Samia alikuwa mgeni rasmi kwenye Sikukuu hiyo

Source: TBC
 
Back
Top Bottom