Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,253
- 26,162
Mwaka 2014Lini maaskofu wa TEC waliiba pesa za Escrow?
Mwaka 2014Lini maaskofu wa TEC waliiba pesa za Escrow?
Tumewachoka na sisi tusikilizwe bana sio wao tu kila siku nchi hii si yao peke yao,hawana jipya wapumzike.Wenye ugali wao wameibuka
Mwisho tuje kushtuka tuna Umoja ila nchi tushaiuza.....Ninaunga mkono hoja udini kwa namna yoyote ile kwenye siasa si mzuri bora ya sisi wapagani. nimesikia mashehe wakizungumza bandari kwa mlengo wa kidini, maaskofu,wachungaji nk wote pamoja na hoja zao nzuri kuhusu madhaifu ya makubaliano/mkataba bado inafungamanishwa na udini na kipindi fulani utanganyika/unzanzibari. Ni kweli mkataba una mapungufu tuujadili wenywe kama wenyewe na serikali ichukue hatua za maboresho ili tubaki na umoja wetu. Umoja kwanza bandari baadaye.
Ingependeza kama kauli hizo angeenda kuzitolea St. Joseph kuliko kwenda huko Rolya kijijini kwa wasabato.Alikuwa aliongea Leo huko Mara alikoalikwa kama mgeni Rasmi kwenye sherehe ya ufunguzi wa jengo la ibada la Kanisa.
My Take
Naunga mkono hoja,TEC na wachochezi wengine wakemewe na waonywe.
=====
"Tukianza kuchanganya dini na siasa, tukageuza...madhabahu ndio mahali pa kuhubiri siasa za vyama vya siasa, kwishiria mbali nchi yetu...lakini Baba wa Taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa, nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni za jicho letu tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo vya aina hii iwe kwa siri au kwa dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya" Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Jakaya Kikwete wakati akizindua kanisa la SDA Rorya mkoani Mara, leo Agosti 20, 2023.
View attachment 2722951
Alikuwa aliongea Leo huko Mara alikoalikwa kama mgeni Rasmi kwenye sherehe ya ufunguzi wa jengo la ibada la Kanisa.
My Take
Naunga mkono hoja,TEC na wachochezi wengine wakemewe na waonywe. ...
halafu wewe unajitambulisha kuwa ni msomi; tena msomi wa nini, sheria?Ndo nia yenu kumbe? Sasa sikiliza. Samia ndo Rais wako hadi 2030. Wafikishie salamu wenzako
Umeshukaje? Kwa hiyo nikubaliane na nyie kumsumbua Samia kwa nia zenu ovu?halafu wewe unajitambulisha kuwa ni msomi; tena msomi wa nini, sheria?
Nakumbuka uliwahi kujitambulisha mwenyewe huko siku za nyuma.
Sasa usomi wote umeshuka, hadi kufikia kwenye kiwango hiki, kweli?
Hutawasikia akiongelea Ufisadi na Nepotism kwa kuwa familia zao ni wafaifika wa huo mfumo."Napenda kuchukua nafasi hii kukumbushana kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa. Tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, na kama kuna viongozi wa dini wanataka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa, na kama kuna viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufa yao ya kisiasa, nawaombeni ndugu zangu tuwanyanyapae.
"Siku ikifika ambapo uwanachama wa chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha siasa kinachofuata ndio mwisho wa nchi yetu, mtakuwa na vyama vya siasa vya wakristu, waislamu, walokole nk. Kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, kiserikali, utawala kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari, halkadhalika watu kuyatazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za vyama vyao si jambo lenye afya kwa taifa letu.
"Yote mawili yataathiri umoja na kutishia amani, usalama na utulivu tunaoufaidi hivi sasa. Mfano Zanzibar walifika mahali waisilamu wanamuona shehe ambaye ni mfuasi wa chama ambacho sio chake sio shehe sawa sawa, kwahiyo wakienda kusali kama shehe ni msuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha, halafu anaingia shehe wa waislamu na wafuasi wake.
"Nawaambia vitu halisi na ndio maana nilipokuwa Rais nilishughulika sana pale na kupata muafaka, niliahidi kwenye hotuba yangu ya kwanza ya Bunge 2005 Dec 30, kwamba nitafanya kila ninaloweza tujenge muafaka Zanzibar, haukuwa rahisi. Mkutano ule tuliufanyia Butiama NEC, ilikuwa moja ya kikao kigumu kwelikweli, lakini nikasema pamoja na ugumu wote lazima hapa tuvuke. Tukafika mahali nilipoona mambo yamekuwa makali, nikasema twendeni kwanza tukale, tulipokuwa tunakula ndio tukawa tunaweka mikakati ya namna gani tunalimaliza hili jambo. Tukajipanga nani ataanza kuzungumza, tukakubaliana kwamba tutakwenda Zanzibar kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na ndio imetusaidia Zanzibar tuna mazingira ya utulivu mpaka sasa, tungekwenda na utaratibu ule ule wa zamani tusingefika.
"…Tukianza kuchanganya dini na siasa tukageuza mimbari za dini na madhabahu kuwa sehemu ya kuhubiri kwishilia mbali nchi yetu. Lakini baba wa taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa. Nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni ya jicho letu. Tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo wa aina hii iwe kwa siri au kwa Dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya."
Kikwete ameyasema hayo leo 20/8/2023 katika ufunguzi wa jengo Kanisa la Kiadventisti Wasabato Mara.
Kwa mara ya kwanza nimeamini CCM safari hii imekutana na mpini mgumu muno na isiposhtuka 2025 inaweza kuondolewa madarakani, kosa kubwa walilolifanya ni kuingiza vyombo vya ulimzi na usalama kwenye siasa wakiamini kwamba vitawalinda.
Waraka wa TEC unataka kuleta sura mpya ya siasa na utawala Tanzania.
Kitendo cha JK kutoka na kutoa hotuba Kali tena akiwa siriasi kuhusu kutenganisha dini na siasa kimenipa wasiwasi mkubwa juu ya kile kinachoendelea kwa sasa ndani ya serikali.
Kumbukeni huyu Rais mstaafu, kwahiyo anafahamu mambo mengi ambayo hata sisi watu wa kawaida hatufahamu.
Je hotuba hii ilikuwa ni kujibu Waraka wa TEC uliosomwa leo katika misa zote za kanisa katoliki?
Kuna kitu nyuma ya pazia juu ya DP world ambacho sisi kama raia hatukifahamu, haiwezekani TEC wachukua uamuzi huu, uwekezaji huu si wa kawaida inawezekana bado kuna vitu vingi hatuvifahamu kuhusu ili suala la bandari.
View: https://twitter.com/Jambotv_/status/1693233897662714215?t=UO0XpE-6d2yEkAmoQFCkig&s=19
Naona bado unaendelea tu na 'level' ile ile niliyokueleza hapo juu.Umeshukaje? Kwa hiyo nikubaliane na nyie kumsumbua Samia kwa nia zenu ovu?
I'm using my knowledge accordingly.Naona bado unaendelea tu na 'level' ile ile niliyokueleza hapo juu.
You're a learned person, please, use your knowledge accordingly. Partisanship has taken over your thinking ability!
you're losing sense of being.
Good to know!I'm using my knowledge accordingly.
CheersGood to know!
Ni rahisirahisi sana kwa watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri kama huyo bwana kuishia kusema maneno kama hayo aliyoyasema, lakini ukimuuliza aeleze tuhuma anazoziwasilisha hana uwezo wa kueleza chochote.Fahamu kwamba kwenye lile andiko hakuna mahala walipoichanganya dini na siasa bali walisimama kuueleza ukweli ambao serikali na wewe mnatumia gharama kubwa sana kuupindisha.