Wacha nimpe darasa kidogo Mzee Jakaya Kikwete

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
207
453
Na Mwl John Pambalu

Nimeshangazwa sana na kauli ya mzee Kikwete aliyoitoa jana huko mkoani Mara siku moja baada ya tamko la Baraza la maaskofu Katoliki katika kile alichodai kuwa si sawa kuchanganya dini na siasa.

Kikwete ambaye marehemu Askofu Getrude Lwakatare alikuwa mbunge kupitia chama chake CCM na hakuwahi kuitoa kauli kama hiyo anayoitoa sasa. Kikwete ambaye Askofu Gwajima anayezunguka kuhubiri nchi nzima huku akitumia madhabahu kumnadi Rais Samia, wabunge na madiwani kwenye madhabahu na Kikwete alichagua kunyamaza. Kikwete ambaye Sheikh Mkuu wa Dar es laam Sheikh Walid Alhad aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Malezi wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Dar es laam, Kikwete alichagua kukaa kimya. Nini kinamtoa pangoni sasa?

Kwanza, upo uwezekano kuwa yumo kwenye scandal ya bandari kupewa waarabu so anatetea mkate wake wa kila siku.

Pili, anaona CCM chama chake kinaenda kuanguka kwa kukosa ushawishi kiasi kwamba sasa wanaogopa nguvu ya maaskofu katika ku speedup anguko la CCM kutokana na uovu wao.

Tatu: Unafiki.

Sasa wacha nimpe Darasa.

Mzee JK akimuona askofu ajue huyo askofu ameshirikishwa Ukuhani, Unabii na Ufalme wa Kristu. Leo nitazungumzia unabii tu na nitatolea mifano ya manabii wawili, Nabii Samweli na Nabii Nathani.

Zamani Mungu aliwatumia manabii kuwapaka watu mafuta ili wawe wafalme rejea 1 Samweli 9:17 "Huyu ndiye mtu niliyekwambia habari zake! Yeye ndiye atakayewatawala watu wangu". Hapa Nabii samweli anaambiwa amsimike mfalme Sauli kuwa nabii wa Israeli. Hii hata nchini kwetu huwa tunafanya, wakati wa kumuapisha Rais viongozi wa dini wanaalikwa ili washuhudie ama kushiriki kumsimika Rais mteule.

Hata katika kumkataa mfalme Mungu hutumia manabii Rajea 1 Samweli 16:1-7 "BWANA akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israel?". Samweli aliyetumika kumsimka Sauli kuwa nabii, Samweli yuleyule anatumiwa tena kuambiwa kuwa Mungu amemkataa Sauli.

Nafikiri unaweza ona namna dini na siasa zilivyokuwa zikihusika tangu Mwanzo katika kuwaweka na kuwaondoa wafalme.

Wakati fulani mfalme Daud alimchungulia mke wa mwanajeshi wake akioga yule mwanajeshi alikuwa akiitwa Huria. Akamtamani akalala na yule mwanamke, mwanamke akapata mimba, Daud akaagiza mumewe arejeshwe kutoka jeshini ili amlishe, amnyweshe na amuache akalale na mkewe ili ionekane ile mimba ni yake (Deception)

Mwanajeshi akarudi kweli akala na kunywa ila kwa kuwa alikuwa akijua miiko ukiwa vitani huruhusiwi kulala na mkeo hakwenda kulala na mkewe. Mfalme akakasirika akaagiza apelekwe kwenye mapambano makali vitani ili apigwe afe. Kweli akauawa vitani, mfalme Daud akamchukua mke wa yule jamaa.

Mungu akakasirika akamtuma nabii Nathani aende kumuonya mfalme Daud Rejea 2 Samweli 12:1-25 Mfalme Daudi akalia akatubu akisema, “Nimetenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu.” Mungu akamsamehe akaendelea kutawala Israel.

Nataka kusema nini?

1. Kama Nabii Nathani (wa dini) alimuonya mfalme Daudi (wa siasa) dhambi iko wapi maaskofu kumkemea Rais Samia?

2. Kama Mfalme Daudi alijua makosa yake akanyenyekea na kutubu na kuacha njia yake mbaya, kwa nini Rais Samia asitazame nyuma na kuachana na mkataba ovu wa Bandari. Ili aendelee kutawala kwa amani bila pressure kutoka kwa umma wa anaowaongoza?

Nafikiri Rais bado anayo nafasi, asimsikilize Kikwete bali aangalie wapi kajikwaa, apige chini mkataba wa bandari, asimame tena asonge mbele akiwa na uhakika kuwa kama kuna mahali alifanya vibaya kwa hila, rushwa ama upendeleo Mwenyezi Mungu ni mwingi wa Rehema na Neema atamsamehe na kumuimarisha tena maana hatujakamilika huo ndiyo ubinadamu wetu.

La! akishupaza shingo maneno haya yatamuhusu. Arejee Daniel 5: 24-28 Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa. Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.

Wasalaam
John Pambalu
Pretoria - Afrika Kusuni
21.08.2023

Pia, soma
 
Kama Taifa tunayo bahati mbaya kuwa na viongozi wa kitaifa wanafiki na wameliumiza Taifa kwa kuwaambukiza wafuasu wao, hatuna kiongozi alienyooka anymore ambaye anaweza kuusema ukweli hata kama unakata maslahi yake nchi imekuwa ya kiunafiki ya level hatari kutokana na unafiki wa hawa watu wetu
 
Na Mwl John Pambalu

Nimeshangazwa sana na kauli ya mzee Kikwete aliyoitoa jana huko mkoani Mara siku moja baada ya tamko la Baraza la maaskofu Katoliki katika kile alichodai kuwa si sawa kuchanganya dini na siasa.

John Pambalu
Pretoria - Afrika Kusuni
21.08.2023
Mungu akubariki Pambalu. Ni mpuuzi na mjinga tu ndie anaeweza kusema siasa na dini havousiani!
 
Na Mwl John Pambalu

Nimeshangazwa sana na kauli ya mzee Kikwete aliyoitoa jana huko mkoani Mara siku moja baada ya tamko la Baraza la maaskofu Katoliki katika kile alichodai kuwa si sawa kuchanganya dini na siasa.

Kikwete ambaye marehemu Askofu Getruda Lwakatare alikuwa mbunge kupitia chama chake CCM na hakuwahi kuitoa
21.08.2023
Wewe ndo wa kumpa some Jakaya?

Vijana wa siku hizi bwana!!
 
JK kasahau kuwa chama chake kiliwaita viongozi wa dini kuwashirikisha suala la mkataba wa DP World? Mzee kajichanganya zaidi kutumia madhabahu kukemea dini kuchanganya na siasa yaani anakemea kitendo anachofanya yeye mwenyewe. Mbaya zaidi kutumia mimbari ya Wasabato kuwakabili Wakatoliki ilhali inajulikana wazi kuwa Wasabato hawawivi na Wakatoliki.
 
Na Mwl John Pambalu

Nimeshangazwa sana na kauli ya mzee Kikwete aliyoitoa jana huko mkoani Mara siku moja baada ya tamko la Baraza la maaskofu Katoliki katika kile alichodai kuwa si sawa kuchanganya dini na siasa.

1. Kama Nabii Nathani (wa dini) alimuonya mfalme Daudi (wa siasa) dhambi iko wapi maaskofu kumkemea Rais Samia?

21.08.2023
Kwa Rais Mstaafu @jmkikwete na mnaosema Baraza La Maaskofu wana chuki za kidini. Naombeni mnieleweshe:

Baraza hili la maakofu (TEC) mwaka 2018 lilipotoa waraka wa Pasaka wa kupinga mauaji na utekaji wa watu uliofanywa na Serikali ya Jiwe walikua na vhuki ya Kidini na 'Mkatoliki' Mwenzao Magufuli?

Mmesahau Askofu Severine Niwemuguzi alinyang’anywa Passport na kuambiwa sio raia kwa sababu ya kupinga uonevu wa
Jiwe, alikua na chuki na Mkatoliki mwenzake?

Wakati wa COVID Baraza La Maaskofu lilipotoa waraka wa kumpinga Magufuli kuwa COVID haipo na kutaka serikali iruhusu watu wapewe chanjo, walikua na chuki za kidini na Magufuli Mkristo mwenzao?

Walivyo kemea madudu ya uchaguzi wa 2020 walikuwa na chuki za kidini na Magufuli Mkristo mwenzao?

Kama kila wakati kukiwa na mjadala wa kitaifa wanatoa Waraka, na hamkuwai kuona shida, kwanini mnataka sasa wasitoe?

Kwahiyo wakitoa kwa Mkristo mwenzao sio chuki? Wakitoa sasa kwa Muislam ndio wana chuki?
 
Na Mwl John Pambalu

Nimeshangazwa sana na kauli ya mzee Kikwete aliyoitoa jana huko mkoani Mara siku moja baada ya tamko la Baraza la maaskofu Katoliki katika kile alichodai kuwa si sawa kuchanganya dini na siasa.

21.08.2023
Rais kazungukwa na wazandiki, waongo na wahuni wa kisiasa.

Maadam amewakumbatia basi wanamsaidia kuzama pamoja naye.

Sisi wananchi tupo wengi kuliko kikundi kidogo kinachoitafuna nchi.

Mungu anatuvusha salama
 
Na Mwl John Pambalu

Nimeshangazwa sana na kauli ya mzee Kikwete aliyoitoa jana huko mkoani Mara siku moja baada ya tamko la Baraza la maaskofu Katoliki katika kile alichodai kuwa si sawa kuchanganya dini na siasa.

Kikwete ambaye marehemu Askofu Getrude Lwakatare alikuwa mbunge kupitia chama chake CCM na hakuwahi kuitoa
21.08.2023
Na kawaida kabisa ukitaka kufanikiwa katika uongozi ,wasikilize wakuu wa dini.bila hivyo umekalia kuti kavu nakwambia!! Ogopa sana watu hawa.aidha wanamsikiliza Mungu au Yule mwingine.
 
JK kasahau kuwa chama chake kiliwaita viongozi wa dini kuwashirikisha suala la mkataba wa DP World? Mzee kajichanganya zaidi kutumia madhabahu kukemea dini kuchanganya na siasa yaani anakemea kitendo anachofanya yeye mwenyewe. Mbaya zaidi kutumia mimbari ya Wasabato kuwakabili Wakatoliki ilhali inajulikana wazi kuwa Wasabato hawawivi na Wakatoliki.
Amekata tawi alilolikalia
 
Na Mwl John Pambalu

Nimeshangazwa sana na kauli ya mzee Kikwete aliyoitoa jana huko mkoani Mara siku moja baada ya tamko la Baraza la maaskofu Katoliki katika kile alichodai kuwa si sawa kuchanganya dini na siasa.

Pretoria - Afrika Kusuni
21.08.2023
Kikwete anajua yote haya sema anataka kutufanya watz wote wajinga.

Issue ni kwamba .kuna mambo mengi sana kwenye ule mkataba hawana namna wanaanza kusingizia vitu vingine
 
Na Mwl John Pambalu

Nimeshangazwa sana na kauli ya mzee Kikwete aliyoitoa jana huko mkoani Mara siku moja baada ya tamko la Baraza la maaskofu Katoliki katika kile alichodai kuwa si sawa kuchanganya dini na siasa.

Pretoria - Afrika Kusuni
21.08.2023
Kwanza hakuna elimu uliompa zaidi yakuuliza maswali kikubwa tunaujua vizuri mchezo wanufaika wabandari ndiowapingao mkataba sabubu hawana wanaitwa kuuboresha hawana hoja wanaturudia sisi kupitia haswa kwa wenyekuungama nakusamehewa dhambi ilihaki iwebatili na batili iwehaki
 
Back
Top Bottom