Mwaka 2013 nilikwenda kijijini ndani ndani uko kulikuwa na nyumba za udongo zilioezekwa nyasi lakini nililikuta kanisa la Roma likiwa na jengo kubwa la kanisa, hospital,shule ya msingi na sekondari na visima vya maji,kwa watu wote, Wakristo na Waislamu,Watanzania wote bila ubaguzi,usafiri pekee kutoka kijijini kwenda mjini ni lift ya Padre zaidi ya hapo utatembea kilomita kumi na nane ndio utakuta usafiri wa Lori au bus,huu ndio ukuu wa Kanisa la Roma,fuatana nami nikupe historia ya ushawishi wa kanisa la Roma duniani na Tanzania,tuanze na Roman Empire,yaani dola la Roma,dola la Roma lilikuwa milki kubwa lililoenea kwa karne kadhaa katika nchi zote zinazopakana na bahari ya Mediteranea,

Dola la Roma lilianza kwenye mji mkuu wa Roma na rasi ya Italia ikaendelea kuunganisha makabila na mataifa ya nchi nyingi kwenye mabara matatu ya Ulaya, Afrika na Asia,kuanzia karne ya 1 KK Watawala wa Dola wakaitwa makaisari:Kaisari wa kwanza alikuwa Augusto,nchi nyingi za sasa ziliwahi kuwa sehemu ya Dola la Roma kama vile Uingereza, Ufaransa,Hispania, Italia, Ugiriki na nchi za Balkani upande wa Ulaya, Moroko, Algeria,Tunisia, Libia na Misri upande wa Afrika, na Uturuki, Syria, Lebanon, Palestina, Jordan na hata Irak upande wa Asia,Upanuzi wa eneo la Roma kuanzia mwaka 510 KK hadi 480 BK;Dola la Roma lilipofikia kilele cha uenezi wake mwaka 117.

Katika kitabu chake Bw. Bergen kiitwacho Development and Religion in Tanzania,katika Ukurasa wake wa 98 mwandishi anasema "Catholic Missionaries came to East Africa to find not new churches, but new provinces of the Roman Church"kwa mujibu wa tafsiri yangu Wamishionari wa Kikatoliki hawakuja hapa Afrika ya Mashariki kwa minaajili ya kuasisi Makanisa mapya,bali walikuja kuunda majimbo mapya ya Kanisa la Roma,Ni kwamba,Tanzania (Tanganyika) ipo Afrika Mashariki, na kwa mujibu wa mwandishi Bergen,Tanzania nayo ni moja ya majimbo ya Kanisa la Roma,au kwa lugha nyepesi tuseme Tanzania ni koloni la Vatican! Je, ni kweli Tanzania (Tanganyika) ni Koloni la Vatican? Padri. Dk. Sivalon, naye katika kitabu chake Kanisa Katoliki na Siasa za Tanzania Bara (1953-1985) anaeleza bayana kuwa Mwalimu Julius Nyerere Rais wa Kwanza wa Tanzania alikuwa kiungo pekee kati ya Chama cha Mapinduzu (CCM),Serikali na Kanisa Katoliki,sijui mnanipata vizuri ndugu Watanzania!?

-Tanganyika kupewa Uhuru.

Baada ya mwarabu kufukuzwa na kina Karl Peters aka mkono wa damu na kwa kumlaghai Chifu Mangungo wa Msovelo kwa mkataba wa kilaghai uliotafsiriwa na Mkalimani Ramazan na baada ya "scramble and partition of Africa"Tanganyika ikawa chini ya Mjerumani,Wajerumani walikuwa na dini yao ya Kilutheri,ikumbukwe kuwa wakati wa ukoloni serikali ya kikoloni ilikuwa inatoa huduma zake za jamii hususani elimu kwa kuupendelea ukristo,kwa muislamu ili upate kusoma sharti ubatizwe na kuwa mkristo,waliobahatika kusoma bila kubatizwa ni watoto wa machifu,hivyo basi Waislamu waliotokana na Utawala wa Mwarabu walianza kupigania Uhuru Ili nao wapate Uhuru na kuabudu dini yao ya kiislamu,kwa hiyo Waislamu wengi walikuwa na vuguvugu la kuikomboa Tanganyika,kuelekea Tanganyika kupata Uhuru Muingereza akapewa Kuisimamia Tanganyika,

Taarifa za siri za CIA za miaka ya 1953 zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini kwamba baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka Tanganyika, mtu aliyepaswa kukabidhiwa nchi alikuwa ni kiongozi wa Wachaga Thomas Mariale,lakini katika nyaraka za shirika la Ujasusi la Uingereza la MI6 chini ya Fabian Society za mwaka 1944, zinaonyesha kwamba shirika hilo liliamini Chifu Kidaha alikuwa mtu sahihi wakukabidhiwa nchi baada ya Waingereza kuondoka.Nyaraka za shirika la Ujasusi la Kanisa Katoliki la Jeisuti za mwaka 1942 kupitia kwa Kasisi Arth Wills na Wash zinaonyesha kwamba wao waliamini Kambarage Burito Nyerere ndie alikuwa mtu sahihi wa kukabidhiwa nchi baada ya Uingereza kuondoka, tangu hapo walimbatiza pale Tabora na kumbadili jina na kuitwa Julius Kambarage Nyerere, hii ilikuja baada ya kifo cha Chifu Burito, awali kulikuwa na mwendo mrefu wa kumshawishi Chifu Burito akubali mtoto wake ajiunge nao lakini mzee yule alipinga, .

Hapa nadhani kuna factions(vigroup vya kisiasa)mbali mbali za wakoloni wakiingereza ambapo kila faction ilikuwa na mtu wake ambaye wangetaka awe Rais wa Tanganyika (baada ya kuona vugu vugu la uhuru kwenye nchi za Afrika haliwezi kuzuilika).Unaweza kuona kwamba Julius aliandaliwa na faction fulani (including yule padre wake) na Oscar aliandaliwa na faction fulani (including huyo askofu wake wa kianglikana). Pia kuna faction nyingine zilikua zinataka chifu huyu au yule awe Rais.Kidhehebu Muingereza aliwapendelea Anglicans kwanza, then Presbyterians, then Lutherans. Muingereza hakupenda wakatoliki. Walutheri alikuwa na wasi wasi nao kidogo kwamba wangependa wajerumani zaidi ya waingereza.

Moja wapo ya Dilemma ya waingereza kidini ni kwamba mjerumani alishakuja Tanganyika. Since ulutheri ndio ilikua dini ya watawala wa Ujerumani (Bismark na Kaiser), Wakoloni wa kijerumani walichagua maeneo mazuri sana ya TZ (Kilimanjaro, Usambara, Arusha, Mbeya, Iringa na Kagera) na kuyafanya maeneo ya walutheri. Of course wakatoliki wakijerumani walipewa pia sehemu ya maeneo hayo. Muingereza kuja akabidi aeneze uanglikana kwenye maeneo ambayo sio mazuri sana (Dodoma etc). Ingawa aliweka makanisa pia kwenye maeneo yale ya walutheri.

Baada ya Waingereza kuzidiwa na Jesuit Father's kupitia Padre Arth Wills wa kanisa la Roma ambao bila kupepesa walimtaka Julius Nyerere kuwa Kiongozi wa Tanganyika baada ya Uhuru baada ya kumfuatilia kwa miaka 20, Waingereza wakaamua kutumia Format ya double agent ‘rafiki’ wao namba moja (Julius) na ‘rafiki’ wao namba mbili (Oscar), ili rafiki yao namba moja asipofanya wanachotaka basi rafiki yao namba mbili anamuondoa huyo namba moja na kuwa kiongozi. Mara nyingi wanapenda rafiki yao namba moja awe boya na rafiki wao namba mbili ndo awe na madaraka ya kweli. Waingerea vile vile wameweza kuweka marais waislamu marafiki zao kwenye nchi za kiafrika e.g. magenerali wakiislamu wa Nigeria,saa nyingine wanaangalia maslahi yao na sio dini.

Tukubali tukatae, Kanisa Katoliki lina upper hand kwenye siasa za dunia, si wengi wanajua kuwa kila rais katika Dunia hii lazima aungwe mkono na Vatican yaani Roma lazima itoe baraka zake,hapa Tanzania tumeona kila rais anapokuwa ni Mkristo ni lazima awe Mkatoliki!,Julius Nyerere alikuwa Mkatoliki, Benjamin Mkapa Mkatoliki na John Magufuli Mkatoliki,na atakaye mfuatia Mama Samia baada muda wake, ni lazima awe Mkatoliki!,hii ni indorsement toka Roma,kama hawakutaki utaondoka na kama wanakutaka utakaa,huu ni mfumo uliojichimbia mizizi toka enzi za Roman Empire,ni sawa na Marekani sasa na baada ya miaka mia ijayo,kuna nguvu itaendelea kuwa nazo,

Now,the winds of change is blowing across Tanzania,uprotestanti umepata nguvu tena Tanzania (especially wapentekoste na walutheri) wengine wametokea Kanisa Katoliki nadhani around 1/3 to 40% ya watanzania kwa sasa ni waprotestanti wa madhehebu mbali mbali,kuna dalili kwamba baada ya miaka 70 ya uhuru (2031) waprotestanti ndo wataiongoza Tanzania,lakini pia Waislamu wamepata nguvu, lakini tukumbuke Roman Katoliki lilipita katikati ya yote CIA waliomtaka Chifu Thomas Marealle na kati kati ya M16 waliomtaka Chifu Kidaha na wao wakahitimisha kumleta Julius Nyerere kama Kiongozi ajae wa Tanganyika baada ya vetting za miaka 20.

Nimalizie kwa kusema Julius Nyerere hakuwaangusha Roman Katoliki waliomchagua wala Watanzania tulionufaika nae,nadhani kutokana na political maneuverings alizopitia Julius Nyerere katika mazingira magumu na hatarishi anastahili kuwa mwenye heri wa kanisa lake la Roma,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliaminiwa na aka-deliver na kwenda extra miles kuifanya Tanzania kuwa Mama wa ukombozi katika bara la Afrika,nathubutu kusema bila ya yeye kanisa la Roma lingepata shida na Tanganyika ingepata shida,sijui kama leo tungekuwa na Tanzania.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Wakati wakihitaji amani utawasikia wakitaka viongozi wa dini wahubiri amani, wasaidie serikali kuhimiza amani, ila wanapokosolewa utawasikia dini isiingilie mambo ya serikali, nadhani yapasa kujua kwamba dini na watu ambao ndio serikali inawaongoza pia ndio hao hao ambao dini zinawaongoza. Inashangaza watu wanataka viongozi wa kidini wahubiri amani tu lakini wanapokemea maovu basi utasikia oh dini isichanganywe na siasa, lakini hao hao kutwa wapo sehemu za ibada,tuseme tu viongozi wasitake tu kusifiwa na viongozi wa dini ambao ni wawakilishi wa kiroho wa hao wananchi bali pia wasinyamazishwa pale wanapowasemea waumini wao, hatuwezi tukawaachia wabunge tu na viongozi kuwa wao ndio Alfa na Omega nao ni binadamu. Kama wabunge wanashindwa kuwasemea waliowachagua mnataka wananchi wasemewe na nani? na pia na wengine wasikike sio kila siku walewale nchi hii ni yetu sote, na hata mtu wa kawaida pia asikilizwe maoni yake. Tumewachoka kutusemea kila siku kwa manufaa yenu tu.
 
Ninaunga mkono hoja udini kwa namna yoyote ile kwenye siasa si mzuri bora ya sisi wapagani. nimesikia mashehe wakizungumza bandari kwa mlengo wa kidini, maaskofu,wachungaji nk wote pamoja na hoja zao nzuri kuhusu madhaifu ya makubaliano/mkataba bado inafungamanishwa na udini na kipindi fulani utanganyika/unzanzibari. Ni kweli mkataba una mapungufu tuujadili wenywe kama wenyewe na serikali ichukue hatua za maboresho ili tubaki na umoja wetu. Umoja kwanza bandari baadaye.
Mwisho tuje kushtuka tuna Umoja ila nchi tushaiuza.....
 
Alikuwa aliongea Leo huko Mara alikoalikwa kama mgeni Rasmi kwenye sherehe ya ufunguzi wa jengo la ibada la Kanisa.

My Take
Naunga mkono hoja,TEC na wachochezi wengine wakemewe na waonywe.

=====

"Tukianza kuchanganya dini na siasa, tukageuza...madhabahu ndio mahali pa kuhubiri siasa za vyama vya siasa, kwishiria mbali nchi yetu...lakini Baba wa Taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa, nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni za jicho letu tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo vya aina hii iwe kwa siri au kwa dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya" Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Jakaya Kikwete wakati akizindua kanisa la SDA Rorya mkoani Mara, leo Agosti 20, 2023.

View attachment 2722951
Ingependeza kama kauli hizo angeenda kuzitolea St. Joseph kuliko kwenda huko Rolya kijijini kwa wasabato.
 
Alikuwa aliongea Leo huko Mara alikoalikwa kama mgeni Rasmi kwenye sherehe ya ufunguzi wa jengo la ibada la Kanisa.

My Take
Naunga mkono hoja,TEC na wachochezi wengine wakemewe na waonywe. ...

Niamini kuwa hakuwa analenga Waraka wa TEC uliosomwa leo kwenye Makanisa yote nchini.

Uzito wa Waraka huo, na jinsi ulivyopokelewa, ni ujumbe tosha kwa Serikali kuchukua hatua iliyo sahihi kuhusu Mkataba wa uwekezaji bandari.

Ushauri
DP World, na Serikali ya Dubai, kama wana nia njema ya kutaka bandari zetu ziendelezwe, kufikia kiwango cha kimataifa, itoe teknojia kwa njia ya mkopo na si kwa njia ya kutaka kumiliki kupitia njia ya ulaghai ya kisingizio cha mkataba wa makabaliano.
 
Ndo nia yenu kumbe? Sasa sikiliza. Samia ndo Rais wako hadi 2030. Wafikishie salamu wenzako
halafu wewe unajitambulisha kuwa ni msomi; tena msomi wa nini, sheria?
Nakumbuka uliwahi kujitambulisha mwenyewe huko siku za nyuma.

Sasa usomi wote umeshuka, hadi kufikia kwenye kiwango hiki, kweli?
 
halafu wewe unajitambulisha kuwa ni msomi; tena msomi wa nini, sheria?
Nakumbuka uliwahi kujitambulisha mwenyewe huko siku za nyuma.

Sasa usomi wote umeshuka, hadi kufikia kwenye kiwango hiki, kweli?
Umeshukaje? Kwa hiyo nikubaliane na nyie kumsumbua Samia kwa nia zenu ovu?
 
"Napenda kuchukua nafasi hii kukumbushana kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa. Tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, na kama kuna viongozi wa dini wanataka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa, na kama kuna viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufa yao ya kisiasa, nawaombeni ndugu zangu tuwanyanyapae.

"Siku ikifika ambapo uwanachama wa chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha siasa kinachofuata ndio mwisho wa nchi yetu, mtakuwa na vyama vya siasa vya wakristu, waislamu, walokole nk. Kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, kiserikali, utawala kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari, halkadhalika watu kuyatazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za vyama vyao si jambo lenye afya kwa taifa letu.

"Yote mawili yataathiri umoja na kutishia amani, usalama na utulivu tunaoufaidi hivi sasa. Mfano Zanzibar walifika mahali waisilamu wanamuona shehe ambaye ni mfuasi wa chama ambacho sio chake sio shehe sawa sawa, kwahiyo wakienda kusali kama shehe ni msuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha, halafu anaingia shehe wa waislamu na wafuasi wake.

"Nawaambia vitu halisi na ndio maana nilipokuwa Rais nilishughulika sana pale na kupata muafaka, niliahidi kwenye hotuba yangu ya kwanza ya Bunge 2005 Dec 30, kwamba nitafanya kila ninaloweza tujenge muafaka Zanzibar, haukuwa rahisi. Mkutano ule tuliufanyia Butiama NEC, ilikuwa moja ya kikao kigumu kwelikweli, lakini nikasema pamoja na ugumu wote lazima hapa tuvuke. Tukafika mahali nilipoona mambo yamekuwa makali, nikasema twendeni kwanza tukale, tulipokuwa tunakula ndio tukawa tunaweka mikakati ya namna gani tunalimaliza hili jambo. Tukajipanga nani ataanza kuzungumza, tukakubaliana kwamba tutakwenda Zanzibar kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na ndio imetusaidia Zanzibar tuna mazingira ya utulivu mpaka sasa, tungekwenda na utaratibu ule ule wa zamani tusingefika.

"…Tukianza kuchanganya dini na siasa tukageuza mimbari za dini na madhabahu kuwa sehemu ya kuhubiri kwishilia mbali nchi yetu. Lakini baba wa taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa. Nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni ya jicho letu. Tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo wa aina hii iwe kwa siri au kwa Dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya."


Kikwete ameyasema hayo leo 20/8/2023 katika ufunguzi wa jengo Kanisa la Kiadventisti Wasabato Mara.
Hutawasikia akiongelea Ufisadi na Nepotism kwa kuwa familia zao ni wafaifika wa huo mfumo.
 
Kwa mara ya kwanza nimeamini CCM safari hii imekutana na mpini mgumu muno na isiposhtuka 2025 inaweza kuondolewa madarakani, kosa kubwa walilolifanya ni kuingiza vyombo vya ulimzi na usalama kwenye siasa wakiamini kwamba vitawalinda.

Waraka wa TEC unataka kuleta sura mpya ya siasa na utawala Tanzania.

Kitendo cha JK kutoka na kutoa hotuba Kali tena akiwa siriasi kuhusu kutenganisha dini na siasa kimenipa wasiwasi mkubwa juu ya kile kinachoendelea kwa sasa ndani ya serikali.

Kumbukeni huyu Rais mstaafu, kwahiyo anafahamu mambo mengi ambayo hata sisi watu wa kawaida hatufahamu.

Je hotuba hii ilikuwa ni kujibu Waraka wa TEC uliosomwa leo katika misa zote za kanisa katoliki?

Kuna kitu nyuma ya pazia juu ya DP world ambacho sisi kama raia hatukifahamu, haiwezekani TEC wachukua uamuzi huu, uwekezaji huu si wa kawaida inawezekana bado kuna vitu vingi hatuvifahamu kuhusu ili suala la bandari.




View: https://twitter.com/Jambotv_/status/1693233897662714215?t=UO0XpE-6d2yEkAmoQFCkig&s=19

baadhi ya wastaafu wanawashwawashwa
 
Umeshukaje? Kwa hiyo nikubaliane na nyie kumsumbua Samia kwa nia zenu ovu?
Naona bado unaendelea tu na 'level' ile ile niliyokueleza hapo juu.

You're a learned person, please, use your knowledge accordingly. Partisanship has taken over your thinking ability!

you're losing sense of being.
 
Naona bado unaendelea tu na 'level' ile ile niliyokueleza hapo juu.

You're a learned person, please, use your knowledge accordingly. Partisanship has taken over your thinking ability!

you're losing sense of being.
I'm using my knowledge accordingly.
 
Fahamu kwamba kwenye lile andiko hakuna mahala walipoichanganya dini na siasa bali walisimama kuueleza ukweli ambao serikali na wewe mnatumia gharama kubwa sana kuupindisha.
Ni rahisirahisi sana kwa watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri kama huyo bwana kuishia kusema maneno kama hayo aliyoyasema, lakini ukimuuliza aeleze tuhuma anazoziwasilisha hana uwezo wa kueleza chochote.
 
Kwanini wao wanaenda kwenye nyumba za ibada kuongelea siasa?

Yote yamesababishwa na wao wenyewe wasubirie kunyolewa
 
Back
Top Bottom