Nimeshangaa sana huyu Mzee leo.

Yani amejificha wee, mwisho wa siku amekuja mbele mwenyewe.
 
Waliua Magufuli wakajua wameshaichukua nchi..wakaanza kuitafuna wao na familia zao na rafiki zao.

Mara wanajiongezea madau kwenye dili za serikali, mara wanajipa maeneo..wakajua hakuna wa kusema maana waliwapa wapinzani asali..kina mbowe, kina zitto na wenzao.

Kuibuka kwa kanisa na kuamua kutetea mali za watanzania kindakindaki kumewashtua. Wameshaona safari yao sasa inaanza kuwa ngumu maana kuna uwezekano huu mnyororo wa kanisa ukaibua na masuala mengine ambayo wao walishaona hayataibuliwa hasirani.

Wanaona wazi safari yao ya kutawala nchi imeanza kuzongwa na miiba.

Kuna wengine wanaweza ona kanisa ni threat ila kwa mtawala wa haki inaweza kuwa mahali bora pa kushikilia.
 
"Napenda kuchukua nafasi hii kukumbushana kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa. Tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, na kama kuna viongozi wa dini wanataka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa, na kama kuna viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufa yao ya kisiasa, nawaombeni ndugu zangu tuwanyanyapae.

"Siku ikifika ambapo uwanachama wa chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha siasa kinachofuata ndio mwisho wa nchi yetu, mtakuwa na vyama vya siasa vya wakristu, waislamu, walokole nk. Kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, kiserikali, utawala kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari, halkadhalika watu kuyatazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za vyama vyao si jambo lenye afya kwa taifa letu.

"Yote mawili yataathiri umoja na kutishia amani, usalama na utulivu tunaoufaidi hivi sasa. Mfano Zanzibar walifika mahali waisilamu wanamuona shehe ambaye ni mfuasi wa chama ambacho sio chake sio shehe sawa sawa, kwahiyo wakienda kusali kama shehe ni msuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha, halafu anaingia shehe wa waislamu na wafuasi wake.

"Nawaambia vitu halisi na ndio maana nilipokuwa Rais nilishughulika sana pale na kupata muafaka, niliahidi kwenye hotuba yangu ya kwanza ya Bunge 2005 Dec 30, kwamba nitafanya kila ninaloweza tujenge muafaka Zanzibar, haukuwa rahisi. Mkutano ule tuliufanyia Butiama NEC, ilikuwa moja ya kikao kigumu kwelikweli, lakini nikasema pamoja na ugumu wote lazima hapa tuvuke. Tukafika mahali nilipoona mambo yamekuwa makali, nikasema twendeni kwanza tukale, tulipokuwa tunakula ndio tukawa tunaweka mikakati ya namna gani tunalimaliza hili jambo. Tukajipanga nani ataanza kuzungumza, tukakubaliana kwamba tutakwenda Zanzibar kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na ndio imetusaidia Zanzibar tuna mazingira ya utulivu mpaka sasa, tungekwenda na utaratibu ule ule wa zamani tusingefika.

"…Tukianza kuchanganya dini na siasa tukageuza mimbari za dini na madhabahu kuwa sehemu ya kuhubiri kwishilia mbali nchi yetu. Lakini baba wa taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa. Nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni ya jicho letu. Tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo wa aina hii iwe kwa siri au kwa Dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya."


Kikwete ameyasema hayo leo 20/8/2023 katika ufunguzi wa jengo Kanisa la Kiadventisti Wasabato Mara.
Aanza na kina Prof Asad na amshauri Sa100 arudishe hiyo bandari na haya hatoyaona. Wanayaset weyewe kisha wanainuka kujifanya hawayajui
 
Wakati watawala wanavunja amani ya nchi kwa vitisho na kuanza kuwashughulikia wakosoaji wa mkataba wa kipuuzi unaoipeleka nchi yetu kwenye utumwa wa milenia, mzee ulikuwa kimya wala haukutoa neno lolote.

Wakati Shura ya Maimamu walipotoa tamko la kuwasomea Itikaf waislam watakaojitokea kwenye mikutano ya kukosoa mkataba huu wa ajabu ulikaa kimya kabisaa.

Wakati viongozi walipotoa vitisho vya kuwashughulikia wanaoupinga mkataba uliona vyema ukakaa kimya

Sasa umeibuka kwa sababu ya hoja nzito zilizotolewa na wasomi naam weledi wanaojua kujenga hoja ikajengeka. Wameleta hoja mezani na badala ya kuzidadavua hoja hata kuwajibu unakuja na KARIPIO kwamba wanachanganya siasa na dini.

Fahamu kwamba kwenye lile andiko hakuna mahala walipoichanganya dini na siasa bali walisimama kuueleza ukweli ambao serikali na wewe mnatumia gharama kubwa sana kuupindisha.

Hebu onesha weledi maana kila tunapokuangalia usoni unaonekana umepaniki.

Mzee, endelea kukaa kimya maana huko tuendako zama zimeisha na mfalme mpya atawekwa na Mungu, huna la kufanya kuzuia
Ajiuluze kwanini makanisa katoliki pale DRC yanaweza kuishauri serikali jambo na likatekekezwa
 
Huku anawafuata kila uchao lakini kwenye DP-WORLD anajitenga nao!
JamiiForums-1424352711.jpg
JamiiForums2073748713.jpg
 
Binafsi sina shida na huu mkataba ila kwanini zanzibar hawapo katika hii agreement wakati sisi wote ni tanzania!! Hapo ndio ninapopatwa na wasiwasi.
 
Waraka wa TEC ni Zaid ya Tamko la USA 😅😅 vibaraka wote wa DP world watatoka shimoni mana wameshaona taa nyekundu chezea Wakatoliki wewe ...wasabato wenyewe wanawajua Wakatoliki vyemaaa
Wasengerema tu hakuna watakachofanya na muarabu anachukua bandari
 
Back
Top Bottom