Polisi Tanzania: Hatutegemei kuona sherehe za Pasaka wakati Nchi bado ipo kwenye maombolezo

King Mufasa

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
1,802
2,000
Jeshi la Polisi nchini limesema halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za Pasaka kama za kipindi cha nyuma katika kipindi hiki ambacho nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

====

Ndugu wanahabari, kama mnavyojua bado taifa letu lipo katika siku 21 za maombolezo kutokana na kifo cha alikuwa Rais wwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Kutokana na tukio hilo kubwa la majonzi napenda kuwajulisha kwamba nchi yetu bado ipo shwari pamoja na kwamba kuna matukio machache ya kijinai yaliyotokea na ajali za barabarani zilizotokea ambazo kwa pamoja zinaendelea kushughulikiwa na baadhi ya watuhimiwa waliohusika katika matukio hayo wameshakamatwa.

Ndugu wanahabari, kufuatana na kalenda, kila ifikapo wakati huu waumini wa madhehebu ya Kikristo huungana kwa pamoja katika kusherehekea sikukuu za Pasaka...

Tuna imani, kama kila mwananchi atazingatia na kufuata Sheria na kujiepusha na vitendo vya kiuhalifu, ibada za Pasaka zitamalizika salama tukizingatia kuwa bado tupo katika kipindi cha maombolezo na hatutegemei zile sherehe na shamrashamra tulizozoea kipindi cha miaka ya nyuma kuwepo katika kipindi hiki.


Pasaka.jpeg
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
157,738
2,000
Jeshi la Polisi nchini limesema halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za Pasaka kama za kipindi cha nyuma katika kipindi hiki ambacho nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Source: EATV news
kwani zile siku 21 zinaisha lini?
 

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
16,741
2,000
Hamnazo hawa jeshi la police Yani tusisherekee kufufuka kwa nwokozi wetu kisa watu ambao hawako duniani?
Jeshi kuweni serious acheni kuingilia Imani zetu
Kwa hili serikali isipokuwa makini itajikuta inatengeneza chuki hadi kwa ule upande ambao ulikua unaikubali serikali na team jiwe
 

gspain

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,690
2,000
Nchi hii tumeendekeza siasa mno. Kila kitu siasa hiyo ndio shida.
Ni hii katiba ya kipumbavu tuliyo nayo, hivi siku 21 watu wanaomboleza kipi labda cha maana? Tena ukute tunaye lazimishwa kumuomboleza kwa mujibu wa katiba alikuwa 'hopeless' enzi ya uhai wake.
 

laptop90

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
1,117
2,000
Dunia iko kwenye maombolezo ya mkombozi wao Yesu kristu, magufuli ni nani, mmekengeuka enyi polisi, futeni hyo kauli bila shuruti
Jeshi la Polisi nchini limesema halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za Pasaka kama za kipindi cha nyuma katika kipindi hiki ambacho nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Source: EATV news
 

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
3,316
2,000
Jeshi la Polisi nchini laimetoa taarifa na Maelekezo kuelekea sikukuu ya Psaka kuanzia Jumakuu hadi siku ya sikukuu yenyewe ambayo ni siku ya jumapili ambayo itakuwa tarehe 4/4/2021.

kamanda-misime.jpeg


Jeshi la Polisi limeomba ushirikiano kwa kamati za ulinzi la usalama katika nyumba za Ibada pia kwa raia wote ilii sikukuu iweze kwenda salama. Pia Jeshi la Polisi litoa ombi hili kwa vya moto.

 

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
7,829
2,000
Mungu na Magu nani zaidi.... masuala ya dini haendelee sherehe za serekali ndo zisimame.
Tusipangiane
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom