I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,727
- 10,023
Jeshi la Polisi nchini limesema halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za Pasaka kama za kipindi cha nyuma katika kipindi hiki ambacho nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
====
Ndugu wanahabari, kama mnavyojua bado taifa letu lipo katika siku 21 za maombolezo kutokana na kifo cha alikuwa Rais wwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Kutokana na tukio hilo kubwa la majonzi napenda kuwajulisha kwamba nchi yetu bado ipo shwari pamoja na kwamba kuna matukio machache ya kijinai yaliyotokea na ajali za barabarani zilizotokea ambazo kwa pamoja zinaendelea kushughulikiwa na baadhi ya watuhimiwa waliohusika katika matukio hayo wameshakamatwa.
Ndugu wanahabari, kufuatana na kalenda, kila ifikapo wakati huu waumini wa madhehebu ya Kikristo huungana kwa pamoja katika kusherehekea sikukuu za Pasaka...
Tuna imani, kama kila mwananchi atazingatia na kufuata Sheria na kujiepusha na vitendo vya kiuhalifu, ibada za Pasaka zitamalizika salama tukizingatia kuwa bado tupo katika kipindi cha maombolezo na hatutegemei zile sherehe na shamrashamra tulizozoea kipindi cha miaka ya nyuma kuwepo katika kipindi hiki.