Je, wezi wa mtandaoni hawaliogopi Jeshi la Polisi Tanzania?

Bigymeech

Member
Mar 29, 2023
25
93
Habari wana JF

Kwa mujibu wa sheria utapeli mtandaoni ni miongoni mwa makosa ya jinai yanayodhughulikiwa na JESHI LA POLISI TANZANIA kupitia kitengo cha uchunguzi wa makosa ya mtandaoni.

Kwasasa kumekuwa na akaunt nyingi mtandaoni za kitapeli hasa Instagram na Facebook zikijitangaza zinatoa mikopo mtandaoni kwa haraka na kwa riba nafuu. Mfano wa akaunt hizo ni Kama TALA TANZANIA COMPANY LIMITED yenye namba 0749254263, ULTIMATE FINANCE yenye namba +255 652 889 729. MO DEWJI yenye namba 0695534781 na zingine nyingi. Namba hizi zote za simu zimesajiliwa na wameziweka wazi kwenye akaunt zao za Instagram kwaajili ya kuwasiliana nao Kama utahitaji mkopo.

Wananchi wengi wamekuwa wakitapeliwa kwani unapo omba mkopo matapeli hao huwa wanakutaka ujaze fomu ya kuomba mkopo kisha utume kiasi flani cha fedha Kama akiba ya mkopo kutokana na kiasi cha mkopo unachohitaji. Mara zote mtu akishatuma tu kiasi hicho(AKIBA YA MKOPO) basi hapo hapo matapeli hao huwa wanablock namba ya mtu huyo au kutopokea sim yake tena. Unapo rudi kwenye mtandao wako wa simu na kuripoti Kama muamala ulotuma umekosea namba nakuomba urudishiwe, basi hela hiyo huwa tayari ishatolewa haraka kwa wakala.

Uki ingia social media hususan Instagram kwenye akaunt za hawa matapeli, upande wa comments utakuta wananchi wengi wanalalamika kutapeliwa huku na wengine wakiwa wame tag akaunt ya POLISI TANZANIA lakini matapeli hawa bila uwoga bado wanaendelea kuwaibia wananchi kwa namba hizohizo. Je, hawa matapeli hawaliogopi JESHI LA POLISI TANZANIA?

Wananchi wengi wanapata ujasiri wa kutuma hela kwenye hizo namba kwakuwa wanaamini tapeli hawezi kuanika namba yake waziwazi katika social media kwani wengi wa wananchi wanaamini kwakuwa namba za simu zinasajiliwa kwa kitambulisho cha NIDA tu, ni rahisi mtu huyo kukamatwa Kama atakuwa anajishughulisha na uhalifu Kwani kitambulisho cha NIDA huwa kinatoa taarifa zote za mtu husiku. Je, matapeli wa mtandaoni hawaliogopi JESHI LA POLISI TANZANIA?

Unapo omba mkopo matapeli hawa huwa wanakutumia fomu ya kujaza taarifa zako, na moja ya kipengele katika hiyo fomu huwa wanakutaka ujaze taarifa za kitambulisho chako na utume picha ya kitambulisho, mtu bila kuwaza mbali kwakuwa yupo kwenye kipindi cha matatizo na anahitaji fedha kutatua matatizo yake anaweza kutuma taarifa ya kitambulisho chake cha NIDA na kufanya hivyo tayari matapeli hao watakuwa washapata taarifa za kitambulisho cha mtu huyo na baadae wanaweza kwenda kuzitumia vibaya mbele ya safari kama kusajilia namba zingine za simu kwaajili ya kuendeleza utapeli. Je, Matapeli wa mtandaoni hawaliogopi JESHI LA POLISI TANZANIA?

Kupitia mitambo ya JESHI LA POLISI TANZANIA, tunatambua namba ikiwa hewani huwa ni rahisi kuifatilia mpaka kumfikia mtumiaji wa namba hiyo. je matapeli hawa hawajui Kama wanaweza kunaswa na JESHI LA POLISI TANZANIA muda wowote? Au nikwamba hawaliogopi JESHI LA POLISI TANZANIA?
 
Kuongopa njeshi ya mutizedi inatengemeana na njisi vile muakili yako kulivyo

Kama Mutu Tu Haamini Yesu ni Bwana wa mabwana Je ako na akili ya kukwepa ku victimee katika mu crimee ya utapeli?
 
Polisi wetu kwenye masuala ya technolojia ni weupe balaa,fikiria wakati wenzetu wakifanya upelelezi wa kisayansi na technolojia huku kwetu Bado mtu atang'olewa kucha au kuminywa pumbu ili atoe taarifa.
 
Spam ya ulaya ni kubwa sana though police forces zao zimejipanga. Inahitaji operation maalum kufatilia issue hizo. Haswa kama ripoti inatolewa. Ila unakuta wabongo. Baada ya ulichoandika ukakifungulie RB. Unaishia storry za vijiweni na jf..peleka polisi hata oysterbay. Pelekeni kwa idadi unayoongea lazma polisi watoke maofisini wakapambane. Wapeni grounds
 
Mambo sikuizi ni digital sio mpaka uache kazi zako uende mpaka kituo cha polisi kutoa taarifa ya uhalifu au utapeli, kupitia mtandao una uwezo wa kutoa taarifa polisi na polisi wakafanyia kazi Kama tu ulaya wanavyofanya.JESHI LA POLISI TANZANIA Lina akaunt Instagram Kama nilivyosema hapo juu ukiingia kwa baadhi ya hizi akaunt za hawa matapeli wananchi wengi wameitag akaunt ya polisi Tanzania Kama kuipa taarifa wafatilie hao matapeli na kuwatia nguvuni lakini cha ajabu matapeli bado wapo wanaendelea na utapeli kwa namba hizohizo.
 
Kwahiyo polisi waigie instagram. Tanzania hii? Sio?
 
Kuongopa njeshi ya mutizedi inatengemeana na njisi vile muakili yako kulivyo

Kama Mutu Tu Haamini Yesu ni Bwana wa mabwana Je ako na akili ya kukwepa ku victimee katika mu crimee ya utapeli?
Nilijua tu utalazimisha mpaka yesu aingie apo ,wewe Yuda
 
Spam ya ulaya ni kubwa sana though police forces zao zimejipanga. Inahitaji operation maalum kufatilia issue hizo. Haswa kama ripoti inatolewa. Ila unakuta wabongo. Baada ya ulichoandika ukakifungulie RB. Unaishia storry za vijiweni na jf..peleka polisi hata oysterbay. Pelekeni kwa idadi unayoongea lazma polisi watoke maofisini wakapambane. Wapeni grounds
unaongelea police wa wapi ndugu,...nina matukio makubwa mawili yalionifanya niache kupeleka malalamiko polisi...kwa ufupi bora nikodi kikosi-kazi nikadili na muhalifu wangu kuliko kupeleka kesi polisi....
 
Ukichunguza sana utagundua.....

images - 2024-03-08T124734.413.jpeg
 
unaongelea police wa wapi ndugu,...nina matukio makubwa mawili yalionifanya niache kupeleka malalamiko polisi...kwa ufupi bora nikodi kikosi-kazi nikadili na muhalifu wangu kuliko kupeleka kesi polisi....
Na we sana unaongelea mifano hovyo mbona.
 
Habari wana JF

Kwa mujibu wa sheria utapeli mtandaoni ni miongoni mwa makosa ya jinai yanayodhughulikiwa na JESHI LA POLISI TANZANIA kupitia kitengo cha uchunguzi wa makosa ya mtandaoni.

Kwasasa kumekuwa na akaunt nyingi mtandaoni za kitapeli hasa Instagram na Facebook zikijitangaza zinatoa mikopo mtandaoni kwa haraka na kwa riba nafuu. Mfano wa akaunt hizo ni Kama TALA TANZANIA COMPANY LIMITED yenye namba 0749254263, ULTIMATE FINANCE yenye namba +255 652 889 729. MO DEWJI yenye namba 0695534781 na zingine nyingi. Namba hizi zote za simu zimesajiliwa na wameziweka wazi kwenye akaunt zao za Instagram kwaajili ya kuwasiliana nao Kama utahitaji mkopo.

Wananchi wengi wamekuwa wakitapeliwa kwani unapo omba mkopo matapeli hao huwa wanakutaka ujaze fomu ya kuomba mkopo kisha utume kiasi flani cha fedha Kama akiba ya mkopo kutokana na kiasi cha mkopo unachohitaji. Mara zote mtu akishatuma tu kiasi hicho(AKIBA YA MKOPO) basi hapo hapo matapeli hao huwa wanablock namba ya mtu huyo au kutopokea sim yake tena. Unapo rudi kwenye mtandao wako wa simu na kuripoti Kama muamala ulotuma umekosea namba nakuomba urudishiwe, basi hela hiyo huwa tayari ishatolewa haraka kwa wakala.

Uki ingia social media hususan Instagram kwenye akaunt za hawa matapeli, upande wa comments utakuta wananchi wengi wanalalamika kutapeliwa huku na wengine wakiwa wame tag akaunt ya POLISI TANZANIA lakini matapeli hawa bila uwoga bado wanaendelea kuwaibia wananchi kwa namba hizohizo. Je, hawa matapeli hawaliogopi JESHI LA POLISI TANZANIA?

Wananchi wengi wanapata ujasiri wa kutuma hela kwenye hizo namba kwakuwa wanaamini tapeli hawezi kuanika namba yake waziwazi katika social media kwani wengi wa wananchi wanaamini kwakuwa namba za simu zinasajiliwa kwa kitambulisho cha NIDA tu, ni rahisi mtu huyo kukamatwa Kama atakuwa anajishughulisha na uhalifu Kwani kitambulisho cha NIDA huwa kinatoa taarifa zote za mtu husiku. Je, matapeli wa mtandaoni hawaliogopi JESHI LA POLISI TANZANIA?

Unapo omba mkopo matapeli hawa huwa wanakutumia fomu ya kujaza taarifa zako, na moja ya kipengele katika hiyo fomu huwa wanakutaka ujaze taarifa za kitambulisho chako na utume picha ya kitambulisho, mtu bila kuwaza mbali kwakuwa yupo kwenye kipindi cha matatizo na anahitaji fedha kutatua matatizo yake anaweza kutuma taarifa ya kitambulisho chake cha NIDA na kufanya hivyo tayari matapeli hao watakuwa washapata taarifa za kitambulisho cha mtu huyo na baadae wanaweza kwenda kuzitumia vibaya mbele ya safari kama kusajilia namba zingine za simu kwaajili ya kuendeleza utapeli. Je, Matapeli wa mtandaoni hawaliogopi JESHI LA POLISI TANZANIA?

Kupitia mitambo ya JESHI LA POLISI TANZANIA, tunatambua namba ikiwa hewani huwa ni rahisi kuifatilia mpaka kumfikia mtumiaji wa namba hiyo. je matapeli hawa hawajui Kama wanaweza kunaswa na JESHI LA POLISI TANZANIA muda wowote? Au nikwamba hawaliogopi JESHI LA POLISI TANZANIA?
Jeshi haliko effecient enough ku deal na hawa watu. Kuna haja ya kuwa na active cyber response team itakayo kua ready for this types of situation
 
Back
Top Bottom