Nini hatima ya Wakristo walio Zanzibar kwenye sherehe za Pasaka baada ya zuio la kula mchana wakati huu wa Ramadhan?

sonofobia

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
384
2,525
Taifa la Mungu wakati tukijiandaa kusherekea Pasaka siku ya jumapili. Wakirsto waliopo Zanzibar wapo kwenye mtihani mkubwa.

Zanzibar kwa sasa ukila mchana unakamatwa na polisi na kuwekwa ndani.

Je itakuwaje kwenye siku ya Pasaka ambayo inatakiwa waumini wachinje na kula na kusherekea pamoja?

Wameambiwa watu wasile hadharani je kwenye hadhara ni wapi? Ukipika pilau lako unawekwa ndani?

Tumeshuudia watu wamekamatwa sababu wanasafirisha chakula walichoagiza kwa siri kutumia bodaboda hawakuwa wakila barabarani, je sasa hadharani ni wapi?

Ukiwa nyumba za kupanga za kushea huduma je hutakiwi kupika?
Watanzania wenzetu wapo kwenye mtihani mkubwa sana kipindi hiki na kosa lao ni moja tu kutokuwa waamini wa islamic religion. Tuwaombee maana hawana mtetezi huko.
 
Najua mnaoliza maswali Kama haya hampo Zanzibar,
Punguzeni chokochoko kwani Ramadan Zanzibar si tukio jipya na katazo la Kula hadharani si jipya.
M/Mungu awape moyo wa uvumilivu na wa kushinda matamanio ili msiwasumbue wasiokuwa na imani kama ya kwenu. Umefunga ila hutaki kuona msosi kisa mate yatakutoka, utakuwa hujafunga kwa imani bali kwa kufuata mkumbo.
 
Taifa la Mungu wakati tukijiandaa kusherekea Pasaka siku ya jumapili. Wakirsto waliopo Zanzibar wapo kwenye mtihani mkubwa.

Zanzibar kwa sasa ukila mchana unakamatwa na polisi na kuwekwa ndani.

Je itakuwaje kwenye siku ya Pasaka ambayo inatakiwa waumini wachinje na kula na kusherekea pamoja?

Wameambiwa watu wasile hadharani je kwenye hadhara ni wapi? Ukipika pilau lako unawekwa ndani?

Tumeshuudia watu wamekamatwa sababu wanasafirisha chakula walichoagiza kwa siri kutumia bodaboda hawakuwa wakila barabarani, je sasa hadharani ni wapi?

Ukiwa nyumba za kupanga za kushea huduma je hutakiwi kupika?
Watanzania wenzetu wapo kwenye mtihani mkubwa sana kipindi hiki na kosa lao ni moja tu kutokuwa waamini wa islamic religion. Tuwaombee maana hawana mtetezi huko.
kwa siku ya pasaka watakula na hapatakuwa na tofauti
 
Back
Top Bottom