Kuhusika kwa Jeshi la Polisi vifo vya vijana wawili, tunataka uchunguzi huru

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya maafisa wa Jeshi la Polisi kuhusishwa na vifo vya vijana wawili ambao ni Bakari Ismail (21) na Shomari Kucheuka (22) waliokuwa wakiishi Vingunguti Dar es Salaam. Taarifa zinaeleza kuwa vijana hao walikamatwa kwa nguvu na Askari Polisi wakiwa nyumbani kwao mnamo Desemba 27, 2023.

Jambo la kusikitisha baada ya kukamatwa haikujulikana walipelekwa wapi kwa kuwa jitihada za ndugu na jamaa kufuatilia kwenye vituo vya Polisi takribani siku sita hazikufanikiwa kuwapata vijana hao. Vilevile, hawakuweza kuwapata kwenye hospitali hadi ilipofika tarehe 28 Desemba walipo taarifiwa kuwa miili ya vijana hao ipo Hospitali ya Amana iliyofikishwa na askari Polisi.

ACT Wazalendo tunaona kwamba zipo hoja zinazoonyesha kuhusika kwa Jeshi la Polisi kwenye mauaji haya. Mosi, kutajwa kwa Askari Polisi wakati wa ukamataji na baadaye tena kwenye kufikishwa miili ya vijana hao katika Hospitali ya Amana.

Pili, sio kawaida ya Jeshi la Polisi kuokota miili ya watu halafu ikaipeleka hospitali wakati tayari kuna taarifa ya watu walioulizia kuhusu ndugu zao. Tatu, hakuna taarifa za Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi ili kubaini nani aliyehusika na mauaji ya miili waliyoikota.

Kutokana na kujirudia kwa matukio na tuhuma za askari polisi kuhusishwa kwenye mauaji ni wazi taswira ya Jeshi la Polisi inaendelea kuchafuka na kushusha imani ya wananchi.

ACT Wazalendo tunarudia wito kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liunde Tume ya kuchunguza mauaji yote ya raia ili kujiridhisha na hatua zilizofanywa na Jeshi la Polisi.

Pili, kwa hatua za awali tunamtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchukua hatua ya kumfuatilia wanaotajwa kuhusika kwenye tukio hili la vijana.

Mwisho, tunaendelea kusisitiza mageuzi ya Jeshi la Polisi kutoka kuwa chombo cha mabavu na kuwa huduma ili liwe linatekeleza wajibu na majukumu yake kwa weledi na kufuata sheria.
Imetolewa na;

Wakili Bonifasia Aidan Mapunda
Waziri Kivuli wa Mambo ya ndani ya nchini
31 Desemba, 2023
 
ACT Wazalendo tunaona kwamba zipo hoja zinazoonyesha kuhusika kwa Jeshi la Polisi kwenye mauaji haya. Mosi, kutajwa kwa Askari Polisi wakati wa ukamataji na baadaye tena kwenye kufikishwa miili ya vijana hao katika Hospitali ya Amana. Pili, sio kawaida ya Jeshi la Polisi kuokota miili ya watu halafu ikaipeleka hospitali wakati tayari kuna taarifa ya watu walioulizia kuhusu ndugu zao. Tatu, hakuna taarifa za Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi ili kubaini nani aliyehusika na mauaji ya miili waliyoikota.

X: @BonifasiaMapunda

Hamumfahamu vyema Camillius Wambura.

Sisemi kaua bali nasema hamumjui vyema walah

Mwenye akili na afahamu
 
Dawa ya wezi/ majambazi ni risasi za kichwa!! Siyo watu wa kuonea huruma hata kidogo ukicheka nao wataendela kuumiza watu wengi sana!!

Wengi wenye hizo tabia wakipigwa za kichwa hata wanaoshirikiana nao au wenye hizo tabia au wanaotaka kufanya huo ujinga wataacha!!
 
Vibaka zilifika 40 zao. Hivyo wamevuna walichokuwa wamepanda na kukipalilia kwa muda mrefu.
 
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya maafisa wa Jeshi la Polisi kuhusishwa na vifo vya vijana wawili ambao ni Bakari Ismail (21) na Shomari Kucheuka (22) waliokuwa wakiishi Vingunguti Dar es Salaam. Taarifa zinaeleza kuwa vijana hao walikamatwa kwa nguvu na Askari Polisi wakiwa nyumbani kwao mnamo Desemba 27, 2023.

Jambo la kusikitisha baada ya kukamatwa haikujulikana walipelekwa wapi kwa kuwa jitihada za ndugu na jamaa kufuatilia kwenye vituo vya Polisi takribani siku sita hazikufanikiwa kuwapata vijana hao. Vilevile, hawakuweza kuwapata kwenye hospitali hadi ilipofika tarehe 28 Desemba walipo taarifiwa kuwa miili ya vijana hao ipo Hospitali ya Amana iliyofikishwa na askari Polisi.

ACT Wazalendo tunaona kwamba zipo hoja zinazoonyesha kuhusika kwa Jeshi la Polisi kwenye mauaji haya. Mosi, kutajwa kwa Askari Polisi wakati wa ukamataji na baadaye tena kwenye kufikishwa miili ya vijana hao katika Hospitali ya Amana. Pili, sio kawaida ya Jeshi la Polisi kuokota miili ya watu halafu ikaipeleka hospitali wakati tayari kuna taarifa ya watu walioulizia kuhusu ndugu zao. Tatu, hakuna taarifa za Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi ili kubaini nani aliyehusika na mauaji ya miili waliyoikota.

Kutokana na kujirudia kwa matukio na tuhuma za askari polisi kuhusishwa kwenye mauaji ni wazi taswira ya Jeshi la Polisi inaendelea kuchafuka na kushusha imani ya wananchi.

ACT Wazalendo tunarudia wito kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liunde Tume ya kuchunguza mauaji yote ya raia ili kujiridhisha na hatua zilizofanywa na Jeshi la Polisi.

Pili, kwa hatua za awali tunamtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchukua hatua ya kumfuatilia wanaotajwa kuhusika kwenye tukio hili la vijana.

Mwisho, tunaendelea kusisitiza mageuzi ya Jeshi la Polisi kutoka kuwa chombo cha mabavu na kuwa huduma ili liwe linatekeleza wajibu na majukumu yake kwa weledi na kufuata sheria.
Imetolewa na;

Wakili Bonifasia Aidan Mapunda
X: @BonifasiaMapunda
Waziri Kivuli wa Mambo ya ndani ya nchini
31 Desemba, 2023
Mnakurupuka na siasa uchwara za matukio.

Mmeanza lini kuwa watetezi wa Panya road?

Hebu nenda mwenyewe Vingunguti kawahoji wanazengo kama hujarudi hapa kufuta hizi pumba zako.

Vifo vya hao vijana vimepokewa Kwa furaha kubwa na wakazi wa eneo hili wanalipongeza Jeshi la Polisi Kwa kazi nzuri waliyoifanya.
 
Wanasiasa wanapenda kukurupuka
Hivi hao wanaijuwa vingunguti ilivyo
Hivi wanajuwa watu wa huko wamekutana na mikasa gani?

Ova
 
😂😂😂
Polisi inaweza ikakuchukua ikakuficha Kawe na ikaanza kukutafuta na ukitoa taarifa kwao wanaanza kukutafuta maeneo ya Mbagala. Nyinyi ACT fanyeni siasa masuala ya Polisi ni pasua kichwa.
 
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya maafisa wa Jeshi la Polisi kuhusishwa na vifo vya vijana wawili ambao ni Bakari Ismail (21) na Shomari Kucheuka (22) waliokuwa wakiishi Vingunguti Dar es Salaam. Taarifa zinaeleza kuwa vijana hao walikamatwa kwa nguvu na Askari Polisi wakiwa nyumbani kwao mnamo Desemba 27, 2023.

Jambo la kusikitisha baada ya kukamatwa haikujulikana walipelekwa wapi kwa kuwa jitihada za ndugu na jamaa kufuatilia kwenye vituo vya Polisi takribani siku sita hazikufanikiwa kuwapata vijana hao. Vilevile, hawakuweza kuwapata kwenye hospitali hadi ilipofika tarehe 28 Desemba walipo taarifiwa kuwa miili ya vijana hao ipo Hospitali ya Amana iliyofikishwa na askari Polisi.

ACT Wazalendo tunaona kwamba zipo hoja zinazoonyesha kuhusika kwa Jeshi la Polisi kwenye mauaji haya. Mosi, kutajwa kwa Askari Polisi wakati wa ukamataji na baadaye tena kwenye kufikishwa miili ya vijana hao katika Hospitali ya Amana.

Pili, sio kawaida ya Jeshi la Polisi kuokota miili ya watu halafu ikaipeleka hospitali wakati tayari kuna taarifa ya watu walioulizia kuhusu ndugu zao. Tatu, hakuna taarifa za Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi ili kubaini nani aliyehusika na mauaji ya miili waliyoikota.

Kutokana na kujirudia kwa matukio na tuhuma za askari polisi kuhusishwa kwenye mauaji ni wazi taswira ya Jeshi la Polisi inaendelea kuchafuka na kushusha imani ya wananchi.

ACT Wazalendo tunarudia wito kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liunde Tume ya kuchunguza mauaji yote ya raia ili kujiridhisha na hatua zilizofanywa na Jeshi la Polisi.

Pili, kwa hatua za awali tunamtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuchukua hatua ya kumfuatilia wanaotajwa kuhusika kwenye tukio hili la vijana.

Mwisho, tunaendelea kusisitiza mageuzi ya Jeshi la Polisi kutoka kuwa chombo cha mabavu na kuwa huduma ili liwe linatekeleza wajibu na majukumu yake kwa weledi na kufuata sheria.
Imetolewa na;

Wakili Bonifasia Aidan Mapunda
Waziri Kivuli wa Mambo ya ndani ya nchini
31 Desemba, 2023
Hilo ni muhimu maana tumeshaona polisi wakiuwa watu bila hatia.
 
Back
Top Bottom