Polisi Tanzania: Hatutegemei kuona sherehe za Pasaka wakati Nchi bado ipo kwenye maombolezo

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
5,716
2,000
Jeshi la Polisi waachieni ndugu zetu wakiritu washerekee sherehe zao bila ya bugudha, Magu kashatangulia kilichobaki tusonge mbele acheni siasa
 

Asherymdudu

Member
Jul 13, 2018
19
75
Jeshi la Polisi nchini limesema halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za Pasaka kama za kipindi cha nyuma katika kipindi hiki ambacho nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
 

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,024
2,000
Ingekuwa nchi nyingine, kuna watu wangepoteza kazi kwa kutoa amri kama hizi. Ila kwa kuwa ni ndugu zangu Watanzania, hili litapita na litatekelezwa.
 

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
30,076
2,000
Acheni haya mambo, Yesu ni mkuu kuliko binadamu. Kufufuka kwa Yesu kristo ni sherehe kubwa sana katika imani ya Ukristo.
Sherehe za pasaka/XMass au zote za kikatoliki zinasherehekewa kiroho kwa kufurahia kufufuka kwa Yesu mioyoni mwa waamini. Husherehekewa kwa kufanya toba na kuadhimishwa misa takatifu.

Wenye uwezo hukaa na familia na jamaa kula na kunywa. Natuamaini Polisi haijakataza hayo. Ukisherehekea pasaka kinyume na hapo kama kwenda kunywa vilevi au mengine ya mwili basi utaishia kujichumia dhambi bure. Maana Kristo atakua kafufuka mwilini mwako na sio rohoni mwako.....Mkatoliki mkamirifu hawezi kupinga juu ya hilo
Wewe ulitaka kuiadhimisha vipi???
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
35,116
2,000
Tanzania ina viongozi wajinga sana!Huwezi kuingilia masuala ya imani za watu!!They are very stupidy!Ina maana Magufuli ni mkubwa na ni mkuu kuliko Yesu ambae anatarajia kufufuka siku ya Pasaka?!
Wonders shall never cease!!!
 

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
7,339
2,000
cha msingi hawajakataza bia
IMG_20201025_221424[1].jpg
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
40,105
2,000
Jeshi la Polisi nchini limesema halitegemei kuona sherehe na shamrashamra za Pasaka kama za kipindi cha nyuma katika kipindi hiki ambacho nchi bado ipo kwenye maombolezo ya kuondokewa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Aiseee mbona kazi ipo....yaani watu wasisherekee kufufuka kwa kristo?
 

Murashani GALACTICO

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
712
1,000
Mbona nyerere day bua zinauzwa kuanzia saa 3 asubuhi......
Vita hii sio ya wakristo vs serikali. Hii ni vita ya M/MUNGU vs SERIKALI.
Tamko kutoka TEC linasubiriwa kwa dakika hizi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom