NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri


NMB Tanzania

NMB Tanzania

Verified Member
Joined
Sep 13, 2014
Messages
92
Points
150
NMB Tanzania

NMB Tanzania

Verified Member
Joined Sep 13, 2014
92 150
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
 
Meeyah

Meeyah

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2016
Messages
14,433
Points
2,000
Meeyah

Meeyah

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2016
14,433 2,000
Una maanisha namba ya Siri au namba ya account yako ya NMB?
 
Saint anne

Saint anne

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2018
Messages
1,010
Points
2,000
Age
22
Saint anne

Saint anne

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2018
1,010 2,000
Jaribu Tena kurudi bank
Mimi Leo nimesaidiwa hili tatizo na ninaendelea kuitumia
Kuna form wamenipa nimejaza haijachukua hata dk 10 kutatua tatizo langu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BabaDesi

BabaDesi

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2007
Messages
2,948
Points
1,250
BabaDesi

BabaDesi

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2007
2,948 1,250
NMB ni vyema mkaja huku kujibu maswali na dukuduku za wateja, vinginevyo uzi huu hauna sababu ya kuwepo!

Sent using Jamii Forums mobile app
...hawa NMB sio kabisa. Kaka yangu mstaafu na ana matatizo ya kisukari, alikwenda pale tawi la Bank House meska jana kati ya mwezi wa saba na wa kumi na akamueleza mama aliyekuwa kwenye ofisi pale counter kwamba yeye alikuwa ni mstaafu anayesubiri pensheni yake na kitambulisho pekee alichokuwa nacho ni cha Ustaafu cha kampuni moja kubwa ya mawasiliano ya nchini.
akamueleza ukweli kwamba yeye hajapata kumiliki cheti cha mpiga kura hata siku moja na alikuwa akisubiri taratibu za kupatiwa kitambulisho cha taifa na aliisha jaza form zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Alichokuwa nacho kingine ni barua tu ya utsmbulisho kutoka serikali ya Mtaa.
Akamuomba mama yule amsaidie kufungua account ili pensheni yake iwe inapitia humo wakati akiendelra kusubiri kitambulisho chake cha taifa.
Bahati nzuri mama yule akawa mwelewa na kumuelekeza brother afungue account ya NMB KWIK.
Akafanikiwa kufungua account hiyo na mwezi December pensheni yake ikaanza kuingia na angalau krismas yake ikawa njema huku akiweza angalau kuwa na uhakika wa matibabu ya kisukari chake.
Mwana wa mbuzi kamba ni yake.
Mwezi uliofuata tu NMB wakaifunga account ya brothet na kumtaka awasilishe vitambulisho vyake ili account yake iweze kufunguliwa.
Kska akatoka huko aliko na kufika pale NMB House kuomba kufinguliwa account yake ili aweze kupata hicho kidogo cha kumsaidia matibabu yake.
Bahati mbaya sana kwake hakumkuta yule mama aliyekuwa amemsaidia kumfungulia acvount.
Aliyekuwepo hakutaka hata kusikiliza maelezo ya brother. Alichokuwa anataka ni kitambulisho cha mpiga kura, ama cha taifa, ama leseni, ama passport, basi. Barua ya utambulisho ya Serikali za Mitaa mamas hskutaka hata kuiangalia!
Ngoma imelala. Huu ni mwezi wa Tatu Pensheni inaingia kwenye acvount ya brother lakini hawezi kuichukua maana NMB walioahidi kumsaidia wameipiga Pini.
Sina haja ya kueleza kuwa miezi mitatu hii kisukari cha brother kinamsumbua maradufu.
Brother anasononeka kwamba kwa pensheni zao zimekuwa na mikutano mingi na kila mtu sasa amekuwa ni mtemi wa pensheni za wastaafu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
wasaa9

wasaa9

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2017
Messages
515
Points
250
wasaa9

wasaa9

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2017
515 250
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1.
Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
msaada...mm ni miongoni mwa wanachama wa benk ya nmb,naomba kufahamishwa kuhusu biashara ya kununua na kuuza fedha za kigeni katika benk ya NMB...natamani siku moja kama itawezekana nifanye biashara hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
namba force

namba force

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Messages
464
Points
250
namba force

namba force

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2017
464 250
Kuna wateja tulinunua hisa za UMOJA FUND kupitia Matawi ya NMB kupata gawio imekuwa shida sana na jamaa hawajulikani walipo tunaomba maelezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
suluta

suluta

Senior Member
Joined
Dec 22, 2016
Messages
108
Points
225
suluta

suluta

Senior Member
Joined Dec 22, 2016
108 225
Ni ipi Logic ya kusema mtu hawez kupata mkopo kwa kuwa hana barua ya confirmation? kwa nn hamuoni namna nyingine ya kubadili mfumo ili mkaendelea kufanya biashara. Kwa sababu kama lengo ni kukwepa Risks za watu kuachishwa kazi kwa kitothibitishwa kazini basi kwa nn Insurence policy yenu msiibafikishe. Yaani badala ya kusibiri mteja akatwe bima ya mkopo wakati anachukua nyie mnaweza ionheza kabisa awali na mnalipia kabisa huko ili ikitokea risks mnakuwa tayar covered?
 

Forum statistics

Threads 1,285,009
Members 494,369
Posts 30,847,189
Top