NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania

Verified Member
Sep 13, 2014
93
150
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
 
kahtaan

JF-Expert Member
Jul 11, 2009
17,512
2,000
sijawahi kuona Bank yenye wafanyakazi wachache kama hii.
kila branch ukiingia foleni mpk brbrn.
ongezeni staff acheni ubahili au wateja wataendelea kuwakimbia kila siku.
 
Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
1,178
2,000
Mimi mwenyewe nimeshawauliza kuhusu suala la uthibitisho wa mkopo wangu kuisha tangu August mwaka jana lakini wananiyumbisha tu.

Wananiambia niende makao makuu ya benki yao wakati sikukopa hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
NMB ni bank ya kijinga sana,wana matangazo meeengi ya kuvutia, mazuri lakini huduma zao za kipumbav. Nilipoteza kadi nikaenda kireport na maelezo juu. Nikaambie nisubiri ntapigiwa simu kwenda kuchukua. Mpaka leo kimya niliamua kusamee mana bank zipo nyingi. Nimeenda Equity kadi nikapata muda huo huo na ndio nayo tumia kwa sasa.

Wamefungua thread hapa wamekimbia,sa sijui ni akili gani,au wanajua watu wote tuko fb na huko insta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
3,271
2,000
NMB Please tupeni Mikopo Watumishi wa Umma tuliobakisha miaka Michache ya kustaafu. Nina miaka minne nistaafu nimeenda kuomba kukopa nimekataliwa eti hamruhusu aliyebakisha miaka 1-4 ya kustaafu. Siyo poa hata kidogo kwa sababu sera hii inabagua wakopaji ikizingatiwa kuwa mshahara wangu na mafao ya Kikotoo itapitia kwenu. Au mnadhani waliobakisha muda mfupi wa Utumishi wanakaribia kufa? Benki nyingine wanatoa bila sharti hili na mambo yanakwenda sawa. Kustaafu siyo ''Death Sentence'' wala ''Poverty Sentence''. Tupeni mikopo tuendeleze kujiandaa kwetu kustaafu.
 
Kete Ngumu

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
5,799
2,000
Kuna dada alikuwa Clock Tower nmb Arusha miaka kadhaa iliyopita kitengo cha mikopo ni kikwazo kwa maendeleo ya bank na kwa afya ya mkopaji, yani usipo mpatia rushwa mkopo hautoki, utazungushwa kama daktari asiyeona ugonjwa.
Huyu dada alikuwa sababu kubwa ya kachana na mikopo yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
james marco

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
208
250
*kwanza kabisa habari yenu wakuu
Aseee nimekereka sana na hawa NMB baada ya kuanza kufuatilia ATM card yangu iliyopotea toka january 7 nikapeleka taarifa kwenye tawivlao moja hapa DODOMA. Walinambia njoo baada ya wiki mbili week mbili zilipobisha nikaenda naaambiwa maombi hayajatumwa wakanambia njoo baada ya week mbili.baada ya hapo tukawa tumefunga chuo nikawa nimeondoka nimerud hivi mwezi wa tatu tarehe kumi na nane wananiambia kuwa card ilitengenezwa ikatumwa SENGEREMA ambako nilifungulia account yangu nikawauliza mbona niliombea hapa hiyo card wakanambia njoo baada ya siku tatu itakua ishafika hapa(hapo sikua mwenyew nilikutana na jamaa mwingine nae alikua na miezi minne anafuatilia anakuja kuambiwa card yake ipo KIGAMBONI ) sasa jana nimerud ikiwa ni takribani week baada ya kuambiwa nirudi, nilichokutana nacho naambiwa card bado haijafika nikamwuuliza huyo mzee ambae ndio yupo kama customer care kua mbona imekua mda sana sasa ananijibu "SASA MIMI NIFANYEJE" Ilibidi nimrudishie hilo hilo swali #kwa hyo unaniuliza mimi ufanyeje sio# akanirudishia form yangu na kunambia hana card kudadeki nilimaindi nikaona nitaharibu2 nikasepa ila NMB punguzeni usumbufu mbona CRDB ilikua week mbili tu jamanii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nusuhela

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
4,720
2,000
Hivi bado mnaitumia NMB?

Top Bottom